maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,144
- 15,144
Darasa la nne wamemaliza mitihani hivi karibuni.
Na wote tunafahamu jinsi hizi shule za siku hizi zinavyochukulia mitihani kama vita maana kipindi chote cha mwaka watoto hawapumziki kisa mtihani wa taifa na hubebeshwa madaftari yote na vitabu juu.
Mbaya zaidi watoto walianza kutoka jioni saa 12 mitihani ilipokaribia. Kiukweli watoto walichoka, sasa baada ya kumaliza mitihani yao juzi tukajua watapumzika na afya irejee lakini cha ajabu wameunga na sasa wanasoma kama kawaida masomo ya darasa la 5. Hivi Serikali mnavyotunga mitaala mnawaelewesha hawa wenye shule nini kinapaswa kufanyika?
Nakumbuka hata likizo ilibidi serikali iingilie kati baada ya wanaJF kuhoji shule kutofungwa kwa watoto wenye madarasa ya mitihani kuwaunganishia bila kupumzika.