Huu sio mkanganyiko kuhusu Mtihani wa Mock Tanzania?

brokenagges

Member
Sep 29, 2022
44
28
Ninashindwa kujua ni ipi kanuni ama mwongozo wa mitihani ya mock Tanzania, ninauliza maana sina uhakika kwamba hiyo inampima mwanafunzi kwa kiwango kipi yaani ufauli ni upi? ama kufeli ni alama ipi?

Kwenye mtahani kama wa form 2 uliofanyika na matokeo yake kupatikana siyo siku nyingi ni alama zipi zenye kuhesabika kama ufaulj ambao unamwezesha mwanafunzi kuendelea na masomo ama kusitisha masomo kwa alama zipi kwa maana ya kwamba ame-feli/faulu?

Nauliza kwa sababu kunazo baadhi ya shule ambazo zinawaondoa shule wale wanafunzi waliopata div III na wakati huohuo zipo ambazo hata kwa waliopata div IV bado wanaendelea na masomo.

Kwangu mimi nikaona kama huu ni mkanganyiko ama ni kwamba huu mtihani hauna mwongozo kutoka wizara ya elimu? kiasi kwamba kila mmoja anajiamulia kufanya atakavyo? na kama ndivyo ilivyo basi ilikuwa haina haja mtihani huu kuwa ni wa taifa bali kila mmoja alitakiwa tu kujitungia mtihani kwa ajili ya wanafunzi wake na kuweka pass marks za kiwango anachohitaji yeye binafsi.

Ninapata ukakasi kwa hizi shule za namna hii na haşa ukizingatia kwamba shule hizi zimejiwekea pia masharti yake yenyewe ya kwamba ni wanafunzi wa namna gani wanawahitaji kujiunga na shule zao tangu pale wanapoingia kidato cha 1.

Ni kwamba pamoja na kwamba wanahitaji matokeo yako ya ufaulu wa la saba lakini pia bado watakupima kwa kutoa tena mtihani wao ambao utapaswa kufaulu kwa kiwango wanachohitaji wao na kwamba ukifanya vizuri mitihani yao basi unakuwa tayari una şifa ya kujiunga na shule yao na huko mbeleni ikatokea kwamba hiyo shule haina walimu wazuri wa kukuendeleza kwa muda wa miaka 2 hadi unapokuja kuja kufanya mtihani wa taifa wa form2 ikatokea ukafeli kwa sababu ya walimu ambao siyo wazuri wanaokuendeleza hapo shuleni na ambao hawana ujanja na utungwaji wa mitihani ya form2 ni kwamba watakuachisha masomo kısa ni kwamba huna akili.

Lakini wanasahau kwamba mtoto aliingia hiyo shule akiwa mwenye akili safi kabisa hivyo kama ni kurudi nyuma kielimu wa kulaumiwa siyo mtoto ila ni shule husika pamoja na waalimu wake ambao wamemfungia mtoto shuleni kwa muda wa miaka miwili bila kumwendeleza kwa mwendo ule ule aliokuwa akiendelezwa akiwa primary.

leo unamrudisha huyu mtoto badala ya kupanga mikakati ya kumfundisha unataka mzazi ampeleke wapi baada ya wewe kuiharibu ama kuififisha elimu yake?

Naomba serikali kupitia Wizara ya Elimu isimame na hili vizuri na kutoa kanuni na miongozo ambaoyo itakuwa ni wa kitaifa na siyo kila shule ijipangie kufanya vile inavyotaka.
 
Ungeandika point yako mkuu.

Naona kama umelalamika tu yani!!

by the way, Shule za umma zipo.
Ishi umo mkuu.
 
Nimeona waziri akipiga marufuku kufukuza waliofanya vibaya
hii mikwara Iko hivyo miaka yote mkuu.

Shule Ya Anwarite kule Moshi unasaini kabisa.
Asipofikisha pass mark hawasubiri hata muhula uishe.
 
Div 3 ya Form 2.
Hiyo ni automatic Div. 4 ya Form 4. au Div 3 ya mwisho kabisa.

Shule zinajaribu kuongeza ushindani.

Elimu ya binafsi ni Elimu Uria.
 
Ungeandika point yako mkuu.

Naona kama umelalamika tu yani!!

by the way, Shule za umma zipo.
Ishi umo mkuu.
Point yangu ni kwamba:
Ninauliza ni ufaulu wa namna gani utakaomwondoa mtoto shuleni form two kwamba hana şifa ya kuendelea na masomo? Na je ndani ya Tanzani kuna tofauti ya alama za ufaulu kati ya shule za umma ama zile za binafsi?
na kama alama za ufaulu ni tofauti ni kwa nini wanapewa mtihani unaofanana? na kama siyo tofauti pia ili kuwepo na maana ya huo mtihani (mock) kwa nini serikali kupitia wizara ya Elimu ama sijui baraza la mtihani lisitoe mwongozo wa jumla kwa watahiniwa wote wa binafsi na wa umma kwamba ni alama zipi akipata mwanafunzi atakuwa amepoteza şifa ya kuendelea na masomo??
 
Back
Top Bottom