Marekani inapaswa kukutana na China njiani ili kutafuta jinsi ya kuelewana

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111464681707.jpg

Tarehe 15, Novemba kwa saa za Marekani, dunia nzima inaelekeza macho Philori Manor mjini San Francisco, ambapo Rais Xi Jinping wa China alialikwa na kuwa na mkutano wa saa nne na rais Joe Biden wa Marekani. Huu ni mkutano mwingine wa ana kwa ana kati ya wakuu wa nchi hizo mbili mwaka mmoja baada ya mkutano wao mjini Bali mwaka jana, ni kipindi muhimu cha kushughulikia uhusiano tata kati ya China na Marekani kwenye ngazi ya mkakati. Rais Xi Jinping alisema kwa uwazi wakati wa mkutano wao kuwa, "hakuna anayeweza kuhimili matokeo mabaya ya mgogoro na makabiliano kati ya China na Marekani."

Kusema kweli, katika mwaka mmoja uliopita, Marekani haikufuata makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa China na Marekani katika mkutano wao wa Bali, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutekeleza mkakati wa "vita baridi mpya" dhidi ya China, na kusababisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kudidimia sana. Lakini tangu mwezi Mei, kumekuwa na sauti zenye mantiki zaidi katika serikali ya Marekani na maoni ya wananchi wakisema kwamba mlango wa mazungumzo hauwezi kufungwa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bw. Antony Blinken, waziri wa fedha Bibi Jannet Yellen, waziri wa biashara Gina Raimondo na maafisa wengine wengi waandamizi wa serikali ya Marekani wameitembelea China, na kutuliza kiasi uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Hali hiyo iliweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa mkutano huo wa San Francisco.

Hivi sasa, dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya usalama, maendeleo, na usimamizi. Ikiwa uhusiano muhimu zaidi kati ya nchi hizo mbili duniani, iwapo China na Marekani zitafanikiwa kutafuta njia sahihi ya kuelewana sio tu kunahusu nchi hizi mbili pekee, bali pia kutaathiri mwelekeo wa siku zijazo wa dunia. Kuhusiana na suala hili, Rais Xi Jinping kwa mara nyingine tena alielezea mtazamo wa China katika mkutano wake na Biden kuwa, maadamu China na Marekani zinaweza kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana, zinaweza kudhibiti tofauti zao na kutafuta njia sahihi ya kuelewana kwa nchi mbili kubwa duniani. Kwa kweli, hii pia inaonyesha udhati na dhamira ya China ya kushughulikia vizuri uhusiano kati yake na Marekani.

Hata hivyo, suala kubwa zaidi linalozuia uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuboreshwa kwa sasa ni kama Marekani, ambayo imezoea kufanya maamuzi katika nyanja ya kimataifa, inaweza kutambua na kuheshimu ukweli kwamba China pia inachukua nafasi muhimu ya kuamua mchakato wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. China imejitolea kujenga uhusiano tulivu, mzuri na endelevu kati yake na Marekani, lakini hii haimaanishi kuwa inaweza kupuuza maslahi, kanuni na msingi wake. Wakati huo huo, Marekani pia inatakiwa kuacha makabiliano ya kiitikadi ambayo ni mtazamo uliopitwa na wakati wa Vita Baridi na kujenga upya tabia ya kushirikiana na China. Kwa kweli, China na Marekani zina maslahi makubwa ya pamoja katika nyanja nyingi, ikiwa ni pamoja na nyanja za jadi kama vile uchumi na biashara, na nyanja zinazoibuka kama vile mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo huko San Francisco unakuja kabla tu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi huko Dubai mwishoni mwa mwezi huu. Wachambuzi wanasema "diplomasia ya hali ya hewa" ya muongo mmoja uliopita imefuata mkondo kwamba wakati makundi makubwa zaidi ya kiuchumi duniani yanakaribia, mambo mazuri yatatokea. Iwapo China na Marekani zitashirikiana kwa mara nyingine tena katika kupunguza utoaji wa hewa chafuzi, zitahimiza maendeleo ya "Mkutano wa Dubai" na kutoa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano kati ya nchi kubwa katika kutatua matatizo makubwa yanayowakabili binadamu.

Mwaka kesho ni kumbukumbu ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani. Historia imetuambia kwamba maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani hayapatikani kwa urahisi. Hata hivyo, ni lazima ikubalike kwamba wakuu wa nchi hizo mbili wana nafasi ya kama "dira" ya kuweka kwa usahihi mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zao, na kufanya uhusiano wa nchi hizo urudi kwenye njia sahihi. Kama Rais Xi Jinping alivyomwambia Rais Biden wakati wa mkutano wao kuwa, "Sisi ni manahodha wa uhusiano kati ya China na Marekani na tunabeba majukumu mazito kwa watu, dunia na historia." Inaaminika kuwa baada ya mkutano huo, uhusiano kati ya China na Marekani unaweza angalau "kuacha kudidimia ", lakini pia haijulikani kama unaweza "kutulia na kuboreka", hali ambayo inahitaji juhudi za pamoja kutoka pande zote mbili.

Mji wa San Francisco umeshuhudia historia ndefu ya mawasiliano ya watu wa China na Marekani, pia umeshuhudia juhudi za China na Marekani za kujenga dunia bora. Inatarajiwa kwamba Marekani inaweza kutambua vya kutosha aliyosema rais Xi Jinping “Sayari ya Dunia ni kubwa ya kutosha nchi mbili kufanikiwa, na mafanikio ya nchi moja ni fursa kwa nyingine”, kukutana na China njiani baada ya mkutano wa San Francisco na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo. Jumuiya ya kimataifa imejaa matumaini makubwa juu ya hilo.
 
Xi Jinping alikuwa na mkutano na CEOs 20 wa makampuni makubwa ya Marekani kama Apple, Boeing, Nike, Qualcomm, FedEx, MasterCard n.k

Katikati ya hotuba wakasimama kumpa heshima kwa standing ovation

CEOs wameonyesha kukubaliana na speech ya Xi Jinping
 
Halafu kanajiabisha kenyewe, huwa anasema hivyo akitegemea Xi Jinping atamjibu kwa kejeli.

Xi Jinping hajawahi hata kumjibu kwa kejeki anasisitiza tu win-win cooperation

Xi ana busara sana
Biden anawapa kazi wenzake kuzisafisha kauli zake inshort ni kauli za kipuuzi katika diplomasia.
 
Xi Jinping alikuwa na mkutano na CEOs 20 wa makampuni makubwa ya Marekani kama Apple, Boeing, Nike, Qualcomm, FedEx, MasterCard n.k

Katikati ya hotuba wakasimama kumpa heshima kwa standing ovation

CEOs wameonyesha kukubaliana na speech ya Xi Jinping
Meza aliyo kaa Xi kwenye hiyo dinner ya China-US friends ilikuwa imejaa watu wazito balaa ni CEOs wazito kweli dunia haina fair kabisa🤡
 
Xi Jinping alikuwa na mkutano na CEOs 20 wa makampuni makubwa ya Marekani kama Apple, Boeing, Nike, Qualcomm, FedEx, MasterCard n.k

Katikati ya hotuba wakasimama kumpa heshima kwa standing ovation

CEOs wameonyesha kukubaliana na speech ya Xi Jinping
Huwa natamani sana miaka ya mbeleni nasi Tz tuna take headlines hivyo kama US na China just imagine mkutano ni wa APEC lakini meeting ya hawa Giant wawili US na China ndio headline kuliko hata summit inavyo zungumziwa.

Dunia ipo busy kufuatilia Xi-Biden wamekubaliana nini halafu hayo ya APEC summit ndio yanafuata kweli ukubwa raha na shida pia
 
Kabisa dunia ilitaka kujua Xi na Biden wamezungumza na kukubaliana nini masaa 2 waliyokaa kuzungumza pamoja

Ikimaanisha wanachokubaliana kinaenda kuathiri mataifa hayo 2, geopolitcal ya dunia na uchumi wa dunia either positively or negatively
 
Hata Musk kwenye huo mkutano alikuwepo sijui yeye alikaa wapi maana musk naye kichwa kibovu haaaaaah
Kuna muda alionekana akishake hands na Xi Jinping, halafu baadaye akaonekana wakati wa cocktail hour

20231117_003841.jpg

Alisikika akisema haya walipokuwa wanamkaribisha Xi kwenye gala dinner

"I look forward to meeting the president again... We are happy with our progress in China."
 
Kabisa dunia ilitaka kujua Xi na Biden wamezungumza na kukubaliana nini masaa 2 waliyokaa kuzungumza pamoja

Ikimaanisha wanachokubaliana kinaenda kuathiri mataifa hayo 2, geopolitcal ya dunia na uchumi wa dunia either positively or negatively
Kwa mwaka huu tu mikutano hii Putin-Xi( Russia- China, Moscow, Beijing ) Biden - Xi ( China - US, Bali & San Francisco ) imefuatiliwa kwa umakini sana kweli dunia imezunguka kwa hawa wakubwa watatu kwa sasa maamuzi yao yana athiri dunia pande zote kwa namna yoyote iwe positive au negative kama ulivyosema
 
Kuna muda alionekana akishake hands na Xi Jinping, halafu baadaye akaonekana wakati wa cocktail hour

View attachment 2816036

Alisikika akisema haya walipokuwa wanamkaribisha Xi kwenye gala dinner

"I look forward to meeting the president again... We are happy with our progress in China."
Huyu jamaa ni master sana harakati zake huwa zinanifurahisha ni mtu wa madili.

Huwa nashangaa tajiri anafunga safari toka US mpaka China na anakutana na Waziri mkuu wa China au rais kabisa sio kitu kidogo kukutana na Waziri mkuu/ Rais wa China kama wewe sio mzito.

Matajiri hawa wakubwa wadunia wanafanya mpaka meeting official ya viongozi wa ngazi za juu wa haya mataifa makubwa kweli hawa jamaa matajiri wana power sana sasa sisi tutaifa twetu tudogo si ndio mwendo wa kulaghaia tu.

Lile dili la Shanghai halilo saini musk na kupewa msamaha wa asilimia kadhaa wa kodi na kupewa hekari za kutosha kujenga kiwanda nikasema matajiri ni watu hatari sana 😄
 
Kama vile ambavyo Bill Gate alikutana na Xi Jinping mwaka huu, Xi akasema Bill Gate ni rafiki yake mkubwa na wa muda mrefu, hebu ona kauli kama hiyo

Musk tayari leo anasema anapanga ratiba ya kukutana na Xi wao kibinafsi siku za mbeleni, hebu imagine 🤔

Na Musk alipewa eneo la kujenga Tesla gigafactory mpya pale Shanghai

Ni wanasiasa tu wa Marekani wanajimwambafai ila hawa CEOs huwa wanawachora tu, wanajua umuhimu wa soko la China kwenye biashara zao.

Juzi kati tu hapo CEO wa Nike, John Donahoe alikuwa China akasema China ni soko kubwa na muhimu la bidhaa zao za Nike na akaikosoa sera ya Biden ya decoupling
 
Back
Top Bottom