Mhhhhhh
Hongera kijana Sinkala kwa kuuvua ukapera na kupata Jiko umetuonyesha njia na sisi tutakufuata punde. Kila la kheri mkuu.
yaani ya kwako hata kama nikiwa wapi kama ukihabarisha mapema muhimu nihudhurie...lol naisubiria kwa hamu!....kila la kheri Sinkala.
Hahaha Nyamayao subili utaarifiwa tu hapa hapa tena manaake itakuwa bab kubwa....nitafunika mbona.
ndio mana nipo mkao wa kula luv....
Nasita kukupa hongera.....unatafuta kero kuowa mazee, uliza waliowa wakuambie ukweli....naona wengi tunasepa hicho kipengele....kwanini msiishi pamoja tu....na hata watoto mkazaa kuliko kujivalisha pingu?
Hongera basi kwa kuwa wengi wamekuambia ila I have warned you with your decision in the first place
Mas
Haya luv bado nipo kwenye mchakato wa kumpata manaake kufunga PINGU za maisha si mchezo kuna milima na mabonde itabidi nivuke.
Nasita kukupa hongera.....unatafuta kero kuowa mazee, uliza waliowa wakuambie ukweli....naona wengi tunasepa hicho kipengele....kwanini msiishi pamoja tu....na hata watoto mkazaa kuliko kujivalisha pingu?
Hongera basi kwa kuwa wengi wamekuambia ila I have warned you with your decision in the first place
Mas
Kwa wale mlio Dar na wale ambao mngependa kushirikiana na mwenzetu...
Kuna mwenzetu (Sinkala) anatarajia kufunga ndoa mwezi huu.
Kwa wale ambao wangependa kushirikiana katika kuiwakilisha JF ama kushirikiana na mwenzetu katika hali na mali tuwasiliane via PM ili niwape mwongozo wa huyu mwenzetu.
Aidha unaweza kuwasiliana na Maxence via +255713444649.
JF itatoa zawadi yake katika harusi hii. Ushirikiano wenu unakaribishwa sana.
Mkuu nifikishie salamu zangu kwa kijana Sinkala zenye kumtakia kila la heri. Huu ni uamuzi unaofanywa na watu wachache kwa hiyo big up! Asimsikilize mtu, moyo wake tu. Sisi twaweza kumpa uzoefu tu lakini yeye asonge mbele. Kama ningeweza, basi siku hiyo ningekuwepo ili nimuume sikio na kumwambia kuwa saa yake ya ukombozi ni saa hiyo hiyo anapoachana na maisha ya kutanga tanga kama ndege. Mwambie apige kwata na kusonga mbele. Asimtishe mtu ila asiende kufanya majibio. Afanye kweli (huyo mdogo wangu) ili aingie kwenye orodha ya wanaume (na baba) wachache tuliobaki kwenye hii dunia ya vichaa wa utandawazi!!