Singeli ni Muziki wa hovyo sana

Singeli ni Muziki wa hovyo sana

Sio lazima kila kitu kikufae wewe,kinachokufaa wewe mwingine kwake ni kero/upuuzi.
Dunia ni kama kapu Lenye Mazaga kibao,chukua kinachokufaa vingine Vina wenyewe.
Uzuri wa kitu sio universal,ni individual perception
Umeongea point sana we jamaa, mimi kapu langu siwezi kuwa na taarabu na singeli ni mambo ya hovyo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulikuwa kuna kigodoro mwali anachezwa.

He si nikawa narekodi video.

Kumbe masharti ya huko usiwe na pochi wala simu utaporwa.

Mtoto mmoja akanishtua "mama c ficha hiyo simu kwenye tight halafu tuwaombe wale wakusindikize ukaiache home ndo turudi hapa wanachora ramani wakuibie"

Kweli nikagundua wote hakuna mwenye simu wala kipochi..

Maajabu ya uswazi unaenda kwenye sherehe bila pochi wala simu unaogopa kuibiwa.
Me naendaga nakitorch hazichelewi kutokea fujo. 😂😂😂
 
Ni ujinga ujinga tu wala hakuna cha maana kinachoelimisha Jamii zaidi ya matusi na vijembe vya majungu tu, ndiyomaana hata Watu wanaoishi katika hizo Jamii hufanana akili na mitazamo finyu
Yani nikiweka redio mara pah nikasikia hizo nyimbo ni heri nizime redio nikae bila kusikiliza redio, ni heri ukimya kuliko hizo nyimbo matusiiii tu hakuna la maana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Democracy imeharibu sana maadili, hata hawa wana-bongo fleva nao ni ushenzi mtupu, hakuna mistari' video ya maadili wala elimu dunia.
Yani unawachia watoto waangakie mziki ukisikia wimbo fulani tu unapayuka badilisheni Chanel, hovyo kabisa, hivi basata wanazipitishaje hizi video [emoji329]?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom