Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Ila naona hizi Mali za Msuya Ndo Tabu yote hii.Sasa Sijui Bora nini.
Huyo Dada narudia tena Hakustahili kuuawa vile(kuna MTU alisema walai(sio vizuri napo)angepigwa Hata shaba.Sasa Kumchinja vile??
Yoyote aliyehusika kumchinja yule Dada.Alaanike.!!!!!
Yule dada aliniuma sana. Mungu ampe raha ya milele.
 
Bado hakuna jibu kama huyo Chussa yuko lupango ama aliachiliwa based on ile kesi yake nyingine.
Kwa hiyo Sharrif atakua na bifu lingine na Chussa mpaka akamuunganisha kwenye kesi isiyomuhusu??
 
Kwa hiyo Sharrif atakua na bifu lingine na Chussa mpaka akamuunganisha kwenye kesi isiyomuhusu??
Inawezekana alijua Chusa hatatoka lupango maana ana kesi ya mauaji nadhani akaamua amchomekee na hiyo ili kufunika mambo mengine.
 
Kubwa unalopaswa kujua siku zote ni kuwa huwa hakuna siri ya watu wawili. Inaweza kudumu kwa muda mfupi au muda fulani lakini lazima itatoka. Sasa idadi yote hiyo ingewezekanaje kutunza siri hiyo. Hata mke mnayekula naye kiapo kanisani siku mkichokana atatoa yote ndio watu watajua kuwa una mikopo na watoto siyo wako ila ni wa rafiki yako kama tulivyoshuhudia juzi ya Muna na Peter kuhusu yule mtoto. Siri huwa ni mtu mmoja basi na wa pili atakuwa ni Mungu. Ndiyo maana huwa nashangaa wanaposema eti siri za serikali. Serikali ni kikundi cha utawala kilichopo kwa muda fulani hivyo hakiwezekani kukawa na siri hasa watunza siri ikiwa ni kwa watu wanaolipwa. Ndiyo maana naamini katika mtiririko huo huo waliomdhuru Lissu ni suala la muda tu tutawajua wote hata kama walirudi kwa msafara wa king'ora. Azori itajulikana tu. Kama makaburi ya halaiki ya miaka ya 40 iliyopita yanajulikana leo itakuwa hao waliompoteza Ben? It's just the matter of time. Time is a very good teacher - Time'll tell
Huo ndiyo uhalisia ndugu.
 
Endelea kujidanganya.


Osama alikuwa hatumii simu kabisa ila alipatiakana. Kaangalie operation Neptune osama alikuwa na zaidi ya miaka 10 anatumia barua kama njia ya mawasiliano ila sasa hivi imebaki history.

Tatizo yule mlinzi wake alikuwa anatumia simu kupigia ndugu zake dubai so wakalink nae na kuona anakaa wap na kuuhisi osama anakaa hapo hapo coz yule alikuwa mtu wake wa karibu so wakachunguza sana iyo nyumba na tabia za watu wa nyumba iyo nakumkamata osama bila ivyo osama mpaka leo angekuwepo
 
Last edited:
Tutashukuru sana kama watatupatia BEN SAANANE na walio mpira risasi TUNDU LIDU
 
Ya ehe kweli kwangu inasomeka kama riwaya ;with all my respect kwa marehemu aliyekatishwa uhai wake,kwa familia yake na ndugu na marafiki wake walioondokewa na mpendwa wao,bado kwangu maelezo haya hayanipi direct link kati ya wahukumiwa na tukio,je murder weapon(s) zilikamatwa,any ballistic test report kuthibitisha kuwa zilitumika kwenye tukio?je wahukumiwa wamehusishwa vipi na crime scene? kama finger prints zao kupatikana kwenye eneo la tukio,alama za viatu walivyovaa kuoana na za kwenye crime scene(anything to put suspects at the crime scene) please kama kuna mwenye maelezo zaidi nitaelimika zaidi,na msimamo wangu siamini in death penaty maana haisaidii chochote kama kutufanya tuogope kutenda kosa kama hili na familia ya victims hawanufaiki chochote(long term jail inafaa zaidi).
Watu kama wewe huwa siwaelewagiii.Simu walizotumia Ndo zimewaponza.Fatilia Uzi au mfate twenty 4seven anaujua mkasa wote.
Sasa u nataka MTU akiua aachiwe coz Marehemu hatarudi.
What a poor mind!!!!!
 
View attachment 817647Chusa
View attachment 817310Erasto Msuya View attachment 817311

Huyu mshatakiwa wa pili Swahibu Jumanne maarufu kama Mredi, alikuwa kama dalali wa kuwatafuta wakina Kahundwa na Ally Majeshi. Ambao ndio kimsingi walifyatua risasi zaidi ya 20 kwa Billionea Msuya, yeye kapona kwa sababu siku ya mauaji alikuwa anafunga ndoa huko Babati. Kwa hiyo alibi yake hapa ni ndoa.

Mshatakiwa wa 3 Mussa Mangu, pamoja na kutoa alibi ya kusafiri kwenda Singida kwa basi la Dar Express na kurudi kwa Lines, mahakama haikuona kama ni hoja ya msingi. Na kisha kumtia hatiani. Hii inaonyesha kuwa Jaji Magimbi katoa hukumu kwa kujiridhisha pasipo shaka kuhusu utetezi wa washtakiwa.

Sinema ilianzia katika gereza la Babati. Siku ambayo Shariff Mohamed alienda kumtembelea Chusa, ambaye kwa wakati huo alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji (katika mgodi wake).
Ndipo katika maongezi Chusa akamdokeza Shariff kuwa kuna jambo anaomba afanye. Na kwamba, hata kuwa kwake ndani ni njama za Msuya.

Vikao na mikakati yote iliratibiwa katika hotel ya Shamo Guest House. Hotel ya Shariff Mohamed, (mshtakiwa wa 1).
Ndipo mambo kadhaa yaliafikiwa.
1. Kumuingilia Chusa
2. Kusajili line za simu
3. Kununua pikipiki
4. Kutafuta shooter
N.k
Baada ya makubaliano hayo mchongo mzima ukaanza kusukwa. Na katika kusuka Chusa alimwambia Shariff (mshatakiwa wa 1), kwamba ukifika Arusha mjini mtafute Swahibu (mshatakiwa wa 2), ambaye leo kachomoka atakupa ramani yote na kinachotakiwa kufanyika. Ila wewe utafadhili zoezi zima.

Mredii kwa uzoefu wake akamtafuta Kuhundwa na Ally Majeshi. Ally Majeshi akatoa wazo kuwa Shariff atoe jiwe kisha akamuoneshe Msuya kuwa analiuza.
Shariff akakubali. Na mchongo ukawa ndio huo. Shariff akatoa jiwe lenye thamani ya zaidi ya 200 mil. Na kumpa Majeshi.

Majeshi alimpigia Msuya akamwambia anaitwa Ally anatokea Mererani kuna jiwe kapata. Hivyo anaomba waonane ili amwoneshe. Msuya akakubali na kumwambia wakutane mjini Arusha. Ilikuwa mida ya jioni saa 11, walikutana na Majeshi alimwonesha jiwe Msuya akalipenda akasema atatoa 140ml. Majeshi akakubali ila akamwambia hiyo biashara yuko na mdogo wake hivyo ni vyema mauziano yafanyike wakiwa wote wawili na mdogo wake.
Msuya akakubali. Kwa hiyo wanafanyaje. Majeshi akasema kesho kama anaweza wakutane njia panda KIA ili na mdogo wake pia awepo asione amemdhulumu. Msuya akakubali.

Huku maandalizi mengine yalikuwa yanaendelea. Line za simu zilisajiliwa Moshi mjini. Line 3 kwa kutumia jina la Kimasai nimelisahau kidogo nafikiri ni "Omolulu" line zote. Na aliyefanya kazi hiyo ni mshatakiwa wa tatu Mussa Mangi na aliyekuwa mshtakiwa wa 7 alichomoka na Ally.

Siku ya tukio asubuhi walikutana Shamo Hotel. Kisha wakakubaliana kuwa Kuhundwa atatumia bodaboda kutokea njia panda. Shariff alibaki njia panda na wengine.
Ally Majeshi alipakiwa na Msuya kutoka Arusha mjini. Kumbuka hapa anafuatwa mdogo wake Ally Majeshi ili mauziano yaweze kufanyika.

Walipofika njia panda wakakunja kuelekea alipo mdogo wake Ally Majeshi. Walipofika tayari Kuhundwa alikuwa kishafika eneo la tukio. Kisha Ally akashuka kama anaongea na Kuhundwa. Msuya kabla hajashuka Kuhundwa alifika na kufungua mlango kisha kuanza kumimina risasi. Kisha wakakamata boda na kuanza kuondoka. Shahidi pekee alikuwa kijana wa Kimasai wa miaka 18 aliyekuwa anachunga eneo hilo.

Mussa Mangu ambaye ni dereva wa Shariff Mohamed. Kuhundwa. Na Ally Majeshi, siku moja kabla walienda Namanga kununua Bunduki. Ambapo ilinunuliwa kwa 4 Mil. Na gari lililotumika kwenda ni la Shariff Mohamed aina ya VX.
Katika malipo ilikuwa imebaki kama millioni 10.

Walipofika njia panda. Wakaiweka pikipiki kwenye gari na kuelekea Arusha. Walipofika Arusha Shariff aliwamalizia hela yote 10 Mli. Iliyobaki. Hapo sasa maisha ya kawaida yaliendelea kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Ndipo wakaanza kukamatwa mmoja baada ya mwingine.


Kuhundwa alikamatwa Kaliua akiwa kwa mganga wa kienyeji. Polisi walioenda kumkamata walikaa kama siku 3 wakiwa wanatibiwa wote kumbe walikuwa kazini. Na Sadick pia madhani.

Ally alikamatwa Kigoma stand asubuhi saa 12. Alipofika Mwanza mnara ulisoma yuko Mwanza. Kisha akazima simu. Akaja kuiwasha akiwa anavuka Busisi. Mnara ukasoma tena. Wakasema huku anaelekea Geita au mikoa ya huko. Baada ya hapo mnara ukaja kusoma Kigoma. Ndipo polisi waliokuwa task force walifika Kigoma. Kwa siku mbili zote hawakufanikiwa kumkamata. Baada ya kukata tamaa wakiwa kwenye gari wanarudi, wakasema tupite stand kupata kifungua kinywa. Walipokuwa stand, moja wa askari akamuona mtu kama Ally. Alipojaribu kupiga ile namba Ally akapokea. Ndipo akamakamatwa.

Shariff Mohamed alikamatwa Arusha mjini. Baada ya kurudi kutoka safari. Saa 11 alfajiri alisikia watu wakigonga kengere ya getini. Alipochungulia katika CCTV camera akaona kuna polisi kisha akafungua geti na kukamatwa.

Chusa alikamatwa na kukaa ndani zaidi ya miezi 6 katika kesi hii ya Msuya. Kisha DPP akaonyesha nia ya kumuondoa Chusa katika hii kesi. Hoja kubwa ni yawezekana ni kwamba Chusa alikuwa gerezani by that time.

Wengine walikamatwa Mererani. Na wengine Arusha mjini. Chusa naye akakamatwa baada ya maelezo ya onyo "extra judicial statement" ya Shariff kueleza kuwa alipewa maelekezo ya kumuua Msuya na Chusa. Kwamba alipoenda kumtembelea Chusa gerezani Chusa alimuomba sana sana amsadie kumuua Msuya. Chusa alimwambia Msuya mtu mbaya sana, na amemdhulumu hela nyingi sana. Na kwamba hata kesi ya mauaji inayomkabili kwa sasa ni Msuya ndio alitengeneza.

Shariff anazidi kusema kwamba, kwa kuwa Chusa ni rafiki yake, na wanafanya naye biashara na ni rafiki mkubwa hakuweza kukataa ombi hilo. Ingawa alimuomba muda afikirie. Shariff anasema. Alipofikiria aliona kwamba Chusa akitoka anaweza kumuua yeye. Hivyo alikuwa hana jinsi zaidi ya kukubali hilo ombi la Chusa.

Ndipo idadi ya washatakiwa ikabaki 7. Moja akachomoka awali alipoonekana hana kesi ya kujibu. Wengine 6 ndio wamehukumiwa. 5 wamehukumiwa kunyongwa. Na 1 kachomoka ambaye ni Swahibu Jumanne maarufu kama Mredi. Ambaye yeye siku ya mauaji alikuwa Babati akifunga ndoa.

Three can keep a secret if two are DEAD.

MWISHO.

NB: Bongo Movie hizi ndo stori za filamu. Acheni mambo ya mvulana wa kimasikini kapendwa na msichana wa kitajiri.
Uvivu wangu katika kusoma; nimesoma tu hiyo Tanbihi nimeridhika napita zangu[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Itapendeza sana wote waliohusika wahukumiwe.Ila sI kwamba walichofanya polisi ni cha ajabu.Wenzetu huko majuu wanasolve crime ambazo ziko very complicated.Hilo group kubwa lazima kuwapata ni rahisi.
 
Stori imeanzia katikati, bado sijajua chanzo cha Msuya kuuwawa, yani kwanini walifikia hayo maamuzi.

Para ya 3, mwandishi ameeleza chanzo japo sio kwa uwazi sana ...

Sinema ilianzia katika gereza la Babati. Siku ambayo Shariff Mohamed alienda kumtembelea Chusa, ambaye kwa wakati huo alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji (katika mgodi wake).
Ndipo katika maongezi Chusa akamdokeza Shariff kuwa kuna jambo anaomba afanye. Na kwamba, hata kuwa kwake ndani ni njama za Msuya.
 
Inawezekana alijua Chusa hatatoka lupango maana ana kesi ya mauaji nadhani akaamua amchomekee na hiyo ili kufunika mambo mengine.
Sasa ndio kaenda kukutana naye huko maisha yao yote! Sijui itakuwaje huko. Ila Chusa (pichani) hata kwa sura tu anaonekana sio binadamu wa kawaida ...
chusa.jpg
 
Hii kesi imenikumbusha ile kesi ya aliekua Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe ambapo yeye, mshitakiwa wa pili Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, mshitakiwa wa tatu Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na WP Jane Andrew, CPL Emmanuel Mabula, D8289 PC Michael Sonza, D 2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisab, na Saad Alawi walituhumiwa kuwaua Wafanyabiashara Watatu wa Madini kutoka Mahenge, Morogoro na Dereva Teksi wa Manzese Ndg Juma Ndugu..

Katika kesi hii, wapo ambao walichomoka just because Bastola iliyotumika kuua wale wafanyabiashara ilikua ni moja tu ambae ni Koplo Saad Alawi aliekimbia, na hakukua na ushahidi wa bastola hiyo kushikwa na mtu zaidi ya mmoja either kwa pamoja au kwa kupokezana. Kwa hiyo yale mambo ya sijui kula njama au kushiriki hapa hayakuwepo, kilichotuhumiwa hapa ni "kuua" ambapo alilengwa alieshika bunduki ni nani.
 
.... Kwa hiyo yale mambo ya sijui kula njama au kushiriki hapa hayakuwepo, kilichotuhumiwa hapa ni "kuua" ambapo alilengwa alieshika bunduki ni nani.
Ha ha ha! Inawezekana mitaala ya sheria huko mavyuoni imebadalika siku hizi Mkuu! Kwamba hata "intention", "support" whether moral, financial, etc. ya kutenda kosa sio kosa tena siku hizi bali ile "actual doing" ndio kosa.
 
Back
Top Bottom