Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Ukitaka kujua Chusa alikua smart, alimsisitiza sana Shariff kuwa isichukuliwe hata sh. 100 ya Msuya baada ya kumuua,
Ni wazi kosa la kutokuchukua pesa na mawe ya Msuya baada ya kumuua imerahisisha sana polisi kuwapata watuhumiwa. Laiti wangechukua pesa na mawe ingeaminika ni majambazi tu wameuwa ili waibe mali za msuya.
Pia huyu Chussa anaonekana ni bandidu ndio maana jamaa akaogopa kumkatalia akijua atauliwa yeye.

Kuna urafiki mwingine ni mgumu kweli kweli.
 
Duuuh nimeamini Jeshi la Polisi wanafanya kazi, wanao beza hili jeshi hawajapata matatizo
Mkuu, jeshi linabezwa kwasababu wananchi wanajua kua lina uwezo wa kuwapata wauaji wa matukio mengi hasa haya ya karibuni ya kisiasa lakini halifanyi hivyo na badala yake picha inayojengeka katika jamii ni kwamba linatumika kisiasa.
 
Hapana siyo hivyo....

Soma haya maelezo ya ushahidi yaliyotolewa mahakamani na shahidi wa Jamhuri.....

Chilumba ambaye alikuwa kiongozi wa timu ya mawasiliano ya kimtandao (Cyber), alidai mahakamani jana kuwa timu yake ndiyo iliyobaini uwapo wa namba ya mwisho iliyowasiliana na marehemu.

Akiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavulla kutoa ushahidi wake, shahidi huyo alidai baada ya kufanikiwa kuondoa neno la siri katika simu za marehemu, walikuta SMS mbili.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, baada ya kufungua simu mojawapo ya marehemu, walikuta SMS hizo zikiwa zimetumwa kupitia namba ya mtandao wa Airtel siku moja kabla ya mauaji na siku ya mauaji.

“Ujumbe wa kwanza ulitumwa tarehe 6/8/2013 ukimjulisha (marehemu) kuwa ‘nina riziki’ na ujumbe wa tarehe 7/8/2013 saa nne au saa tano hivi ulisema niko Kia nakusubiri hapa,” alidai shahidi huyo na kuongeza:

“Tulianza kufuatilia ujumbe huo (wa tarehe 7/8.2013) ambao ndiyo ulikuwa wa mwisho kwenye simu ya marehemu na saa chache baadaye akauawa. Tuliandika barua Airtel kupata taarifa zake.”

Katika barua hiyo, shahidi huyo alidai waliiomba kampuni ya Airtel kuwapa taarifa mmiliki wa laini hiyo ya simu, ilikosajiliwa na kwa wakati huo ilikuwa ikisomeka eneo gani.

Alidai kuwa majibu ya Airtel yalionyesha kuwa laini hiyo ilikuwa imesajiliwa Arusha Agosti 3, 2013 kwa jina la Motii Mongululu lakini wakati huo haikuwa tena hewani.

“Walituambia baada ya kusajiliwa, laini hiyo ilifanya mawasiliano na namba nne tu na wakatuambia iliwahi kuchomekwa kwenye handset (simu) ambayo inatumia namba nyingine,” alidai na kuongeza:

“Tulifanikiwa kumkamata dada mmoja pale Arusha kituo kikuu cha mabasi anaitwa Hamisa (Kassim), ambaye ndiye mwenye hiyo namba, ambaye alikumbuka kusajili line kwa jina la Motii Mongululu.”

Hata hivyo, shahidi huyo alidai katika mahojiano, Hamisa aliwaeleza kuwa alisajili laini hiyo kwa maelekezo ya wakala mwenzake aliyemtaja kuwa ni Aneth Shija ambaye naye alikamatwa.

“Aneth alikiri ndiye aliyempa maelekezo Hamisa kusajili hiyo laini na nyingine mbili na kwamba, alizisajili kwa maelekezo ya mtu aliyemtaja kuwa ni Adam ambaye ni kijana wa kimasai,” alieleza.

Shahidi huyo alidai kupitia kwa Aneth walifanikiwa kupata namba ya Adam ambaye alikamatwa Mirerani, lakini naye akadai aliagizwa na mshtakiwa wa tatu, Mussa Mangu kusajili laini hizo.

Mkaguzi huyo wa polisi aliieleza mahakama kuwa baada ya Mangu kukamatwa na kuhojiwa, alikiri kusajili laini hizo za simu lakini naye akadai kuwa alitumwa na mshtakiwa wa kwanza, Sharifu.

“Alituambia maelekezo ya kusajili laini na kununua simu alipewa na bosi wake aliyemtaja kuwa ni Sharifu Mohamed. Alitueleza kuwa kwa ufahamu wake, yote yalikuwa ni maandalizi ya mauaji.

“Siku hiyo hiyo tulimkamata Sharifu nyumbani kwake na katika mahojiano ya awali alimtambua Mussa kama mfanyakazi wake na kukiri vitu vyote vilivyonunuliwa naye vilikuwa maelekezo yake,” alieleza.
Ahsante boss.
 
Ana alibi.Siku ya tukio alikua anafunga ndoa Singida.
Lakini ndiye aliyepokea laki 3 na kujaziwa mafuta na mshitakiwa wa kwanza akaahidi kumtafutia watu wa kazi kwa hiyo kweli siku ya tukio alikuwa harusini lakini alihusika kuratibu mauaji
 
Kumekucha!!!! Sasa kafanyeni kazi kwenye ALIBI zenu , mjadala utaendelea saa 7 mchana lunch time!!
Hivi hii neno ALIBI maana yake nn? Sijawahi kusikia likitamkwa hata kwenye kesi zingine za mauaji!!! Kesi hii police wameweka mbwembwe za Hatareeee!!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wadau naombeni jibu?
Alibi ni cover story, evidence inayokuonyesha ulikuwa sehemu Fulani Wakati wa tukio fulani ambayo ni sehemu mbili tofauti kiasi kwamba hauwezi kuwa maeneo yote kwa Wakati mmoja
 
Lakini ndiye aliyepokea laki 3 na kujaziwa mafuta na mshitakiwa wa kwanza akaahidi kumtafutia watu wa kazi kwa hiyo kweli siku ya tukio alikuwa harusini lakini alihusika kuratibu mauaji
Aisee, binafsi sijaifuatilia sana hii case.
Ila kama alitafuta watu tuu na hakuhusika na mission nyingine, ni rahisi kuchomoka.
 
View attachment 817647Chusa
View attachment 817310Erasto Msuya View attachment 817311

Huyu mshatakiwa wa pili Swahibu Jumanne maarufu kama Mredi, alikuwa kama dalali wa kuwatafuta wakina Kahundwa na Ally Majeshi. Ambao ndio kimsingi walifyatua risasi zaidi ya 20 kwa Billionea Msuya, yeye kapona kwa sababu siku ya mauaji alikuwa anafunga ndoa huko Babati. Kwa hiyo alibi yake hapa ni ndoa.

Mshatakiwa wa 3 Mussa Mangu, pamoja na kutoa alibi ya kusafiri kwenda Singida kwa basi la Dar Express na kurudi kwa Lines, mahakama haikuona kama ni hoja ya msingi. Na kisha kumtia hatiani. Hii inaonyesha kuwa Jaji Magimbi katoa hukumu kwa kujiridhisha pasipo shaka kuhusu utetezi wa washtakiwa.

Sinema ilianzia katika gereza la Babati. Siku ambayo Shariff Mohamed alienda kumtembelea Chusa, ambaye kwa wakati huo alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji (katika mgodi wake).
Ndipo katika maongezi Chusa akamdokeza Shariff kuwa kuna jambo anaomba afanye. Na kwamba, hata kuwa kwake ndani ni njama za Msuya.

Vikao na mikakati yote iliratibiwa katika hotel ya Shamo Guest House. Hotel ya Shariff Mohamed, (mshtakiwa wa 1).
Ndipo mambo kadhaa yaliafikiwa.
1. Kumuingilia Chusa
2. Kusajili line za simu
3. Kununua pikipiki
4. Kutafuta shooter
N.k
Baada ya makubaliano hayo mchongo mzima ukaanza kusukwa. Na katika kusuka Chusa alimwambia Shariff (mshatakiwa wa 1), kwamba ukifika Arusha mjini mtafute Swahibu (mshatakiwa wa 2), ambaye leo kachomoka atakupa ramani yote na kinachotakiwa kufanyika. Ila wewe utafadhili zoezi zima.

Mredii kwa uzoefu wake akamtafuta Kuhundwa na Ally Majeshi. Ally Majeshi akatoa wazo kuwa Shariff atoe jiwe kisha akamuoneshe Msuya kuwa analiuza.
Shariff akakubali. Na mchongo ukawa ndio huo. Shariff akatoa jiwe lenye thamani ya zaidi ya 200 mil. Na kumpa Majeshi.

Majeshi alimpigia Msuya akamwambia anaitwa Ally anatokea Mererani kuna jiwe kapata. Hivyo anaomba waonane ili amwoneshe. Msuya akakubali na kumwambia wakutane mjini Arusha. Ilikuwa mida ya jioni saa 11, walikutana na Majeshi alimwonesha jiwe Msuya akalipenda akasema atatoa 140ml. Majeshi akakubali ila akamwambia hiyo biashara yuko na mdogo wake hivyo ni vyema mauziano yafanyike wakiwa wote wawili na mdogo wake.
Msuya akakubali. Kwa hiyo wanafanyaje. Majeshi akasema kesho kama anaweza wakutane njia panda KIA ili na mdogo wake pia awepo asione amemdhulumu. Msuya akakubali.

Huku maandalizi mengine yalikuwa yanaendelea. Line za simu zilisajiliwa Moshi mjini. Line 3 kwa kutumia jina la Kimasai nimelisahau kidogo nafikiri ni "Omolulu" line zote. Na aliyefanya kazi hiyo ni mshatakiwa wa tatu Mussa Mangi na aliyekuwa mshtakiwa wa 7 alichomoka na Ally.

Siku ya tukio asubuhi walikutana Shamo Hotel. Kisha wakakubaliana kuwa Kuhundwa atatumia bodaboda kutokea njia panda. Shariff alibaki njia panda na wengine.
Ally Majeshi alipakiwa na Msuya kutoka Arusha mjini. Kumbuka hapa anafuatwa mdogo wake Ally Majeshi ili mauziano yaweze kufanyika.

Walipofika njia panda wakakunja kuelekea alipo mdogo wake Ally Majeshi. Walipofika tayari Kuhundwa alikuwa kishafika eneo la tukio. Kisha Ally akashuka kama anaongea na Kuhundwa. Msuya kabla hajashuka Kuhundwa alifika na kufungua mlango kisha kuanza kumimina risasi. Kisha wakakamata boda na kuanza kuondoka. Shahidi pekee alikuwa kijana wa Kimasai wa miaka 18 aliyekuwa anachunga eneo hilo.

Mussa Mangu ambaye ni dereva wa Shariff Mohamed. Kuhundwa. Na Ally Majeshi, siku moja kabla walienda Namanga kununua Bunduki. Ambapo ilinunuliwa kwa 4 Mil. Na gari lililotumika kwenda ni la Shariff Mohamed aina ya VX.
Katika malipo ilikuwa imebaki kama millioni 10.

Walipofika njia panda. Wakaiweka pikipiki kwenye gari na kuelekea Arusha. Walipofika Arusha Shariff aliwamalizia hela yote 10 Mli. Iliyobaki. Hapo sasa maisha ya kawaida yaliendelea kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Ndipo wakaanza kukamatwa mmoja baada ya mwingine.

Kuhundwa alikamatwa Kaliua akiwa kwa mganga wa kienyeji. Polisi walioenda kumkamata walikaa kama siku 3 wakiwa wanatibiwa wote kumbe walikuwa kazini. Na Sadick pia madhani.

Ally alikamatwa Kigoma stand asubuhi saa 12. Alipofika Mwanza mnara ulisoma yuko Mwanza. Kisha akazima simu. Akaja kuiwasha akiwa anavuka Busisi. Mnara ukasoma tena. Wakasema huku anaelekea Geita au mikoa ya huko. Baada ya hapo mnara ukaja kusoma Kigoma. Ndipo polisi waliokuwa task force walifika Kigoma. Kwa siku mbili zote hawakufanikiwa kumkamata. Baada ya kukata tamaa wakiwa kwenye gari wanarudi, wakasema tupite stand kupata kifungua kinywa. Walipokuwa stand, moja wa askari akamuona mtu kama Ally. Alipojaribu kupiga ile namba Ally akapokea. Ndipo akamakamatwa.

Shariff Mohamed alikamatwa Arusha mjini. Baada ya kurudi kutoka safari. Saa 11 alfajiri alisikia watu wakigonga kengere ya getini. Alipochungulia katika CCTV camera akaona kuna polisi kisha akafungua geti na kukamatwa.

Chusa alikamatwa na kukaa ndani zaidi ya miezi 6 katika kesi hii ya Msuya. Kisha DPP akaonyesha nia ya kumuondoa Chusa katika hii kesi. Hoja kubwa ni yawezekana ni kwamba Chusa alikuwa gerezani by that time.

Wengine walikamatwa Mererani. Na wengine Arusha mjini. Chusa naye akakamatwa baada ya maelezo ya onyo "extra judicial statement" ya Shariff kueleza kuwa alipewa maelekezo ya kumuua Msuya na Chusa. Kwamba alipoenda kumtembelea Chusa gerezani Chusa alimuomba sana sana amsadie kumuua Msuya. Chusa alimwambia Msuya mtu mbaya sana, na amemdhulumu hela nyingi sana. Na kwamba hata kesi ya mauaji inayomkabili kwa sasa ni Msuya ndio alitengeneza.

Shariff anazidi kusema kwamba, kwa kuwa Chusa ni rafiki yake, na wanafanya naye biashara na ni rafiki mkubwa hakuweza kukataa ombi hilo. Ingawa alimuomba muda afikirie. Shariff anasema. Alipofikiria aliona kwamba Chusa akitoka anaweza kumuua yeye. Hivyo alikuwa hana jinsi zaidi ya kukubali hilo ombi la Chusa.

Ndipo idadi ya washatakiwa ikabaki 7. Moja akachomoka awali alipoonekana hana kesi ya kujibu. Wengine 6 ndio wamehukumiwa. 5 wamehukumiwa kunyongwa. Na 1 kachomoka ambaye ni Swahibu Jumanne maarufu kama Mredi. Ambaye yeye siku ya mauaji alikuwa Babati akifunga ndoa.

Three can keep a secret if two are DEAD.

MWISHO.

NB: Bongo Movie hizi ndo stori za filamu. Acheni mambo ya mvulana wa kimasikini kapendwa na msichana wa kitajiri.
 
Alipofikiria aliona kwamba Chusa akitoka anaweza kumuua yeye. Hivyo alikuwa hana jinsi zaidi ya kukubali hilo ombi la Chusa.
Kwa hiyo anakiri kuwa Chusa ni muuaji alokubuhu.
 
Nitarudi kuusoma sahivi nina majukumu mengine
 
We nae unajifanya unajua kumbe hujui lolote.
Unajua chanzo cha Osama kukamatwa kilianzia wapi...
Unajua wali-trace vipi ile nyumba Abottabad alokua anakaa Osama pale Pakistan...
Kwa taarifa yako bila yule assistant wa Osama alokua anaenda sokoni kununua mahitaji asingekua anatumia simu mpaka leo hii Osama asingejulikana alipo.
Naona forex baada ya kukuharibia maisha yako umekuwa kichaa.

Sasa ulichoandika na nilichoandika kuna tofauti gani.

Hasira zako mpelekee ONTARIO sio mimi. Shubameet
 
Back
Top Bottom