Hii kesi imenikumbusha ile kesi ya aliekua Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe ambapo yeye, mshitakiwa wa pili Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, mshitakiwa wa tatu Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na WP Jane Andrew, CPL Emmanuel Mabula, D8289 PC Michael Sonza, D 2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisab, na Saad Alawi walituhumiwa kuwaua Wafanyabiashara Watatu wa Madini kutoka Mahenge, Morogoro na Dereva Teksi wa Manzese Ndg Juma Ndugu..
Katika kesi hii, wapo ambao walichomoka just because Bastola iliyotumika kuua wale wafanyabiashara ilikua ni moja tu ambae ni Koplo Saad Alawi aliekimbia, na hakukua na ushahidi wa bastola hiyo kushikwa na mtu zaidi ya mmoja either kwa pamoja au kwa kupokezana. Kwa hiyo yale mambo ya sijui kula njama au kushiriki hapa hayakuwepo, kilichotuhumiwa hapa ni "kuua" ambapo alilengwa alieshika bunduki ni nani.