Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Hapo kila mtu anajiuliza kma wewe,istoshe mbna hakuna mtu wa chusa kwenye group lote la mauaji,istoshe hakuna aliemtaja chusa hpo zaidi ya sharifu,kwahiyo wauaji hawamjui chusa
Aiseee naanza kuamini.Huenda Chussa hahusiki kabisa Na Ndo mana kapona.a
Na isitoshe Sharifu angeelezea Pesa alimpajepaje za kuwalipa wauaji??
Pia.Mbona nilisikia wana sema Sharifu aliwai tolewa (I mean aliachiliwa.VP akarudishwa tena?
 
Hatusapoti kuuana ila nyomi la mpango lilizidi..
Watu hata alibi walikua hawana wamekurupuka tu wamenda kufanya ujinga
Ishu ka hyo laini angekua mtu na elimu kdg asingesajili kizembe hivo
Kwanza ishu kama hii haikutakiwa kabisa kutumia simu
 
Hii case ilikamata watu wengi tu ila ambazo hawakuhusika wakaachiwa,kuna mmasai nyoka wa sharifu ndio hizo line ziliandikwa jina lake alipewa kibano mpka kuvunjwa mguu,hakua anajua chochote alivyoachiwa magereza hakuwahi kuonekana mererani karudi bush kwao tena alisilimu akiwa na sharifu.
Ila kwasasa amerudi kwenye imani yke hata mererani kapasahau
Ila upelelezi bongo bado, nguvu nyingi akili kudogo
 
Aiseee naanza kuamini.Huenda Chussa hahusiki kabisa Na Ndo mana kapona.a
Na isitoshe Sharifu angeelezea Pesa alimpajepaje za kuwalipa wauaji??
Pia.Mbona nilisikia wana sema Sharifu aliwai tolewa (I mean aliachiliwa.VP akarudishwa tena?
Sharifu hakuwahi kuachiwa maelezo yke yalinyooka hata hakupigwa
 
Issue ilipigwa kiimani sana yani aliamini watu wa imani yke mwanzo mwisho,dreva wake ndio alisajili line na kufuata bunduki namanga,jina la kwenye line ni mmasai nyoka wke sharifu hpo case hii inamrukaje,chusa alikua magereza kwa case ya mauaji mgodini kwake,
Kuhusu kuliwa mkewe ni maneno tu ua mtaani hii ilikua beef ya kibiashara
Chusa ilikuwaje akatoka jela
 
Bado siamin nahaya maigizo binafsi naona kuna zaid ya haya, kuuliwa kwa aneth(dada wamarehem) kifo chake lazima kitakua na mengi yanayo link nakifo cha kaka ake.
 
Hapana siyo hivyo....

Soma haya maelezo ya ushahidi yaliyotolewa mahakamani na shahidi wa Jamhuri.....


Chilumba ambaye alikuwa kiongozi wa timu ya mawasiliano ya kimtandao (Cyber), alidai mahakamani jana kuwa timu yake ndiyo iliyobaini uwapo wa namba ya mwisho iliyowasiliana na marehemu.

Akiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavulla kutoa ushahidi wake, shahidi huyo alidai baada ya kufanikiwa kuondoa neno la siri katika simu za marehemu, walikuta SMS mbili.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, baada ya kufungua simu mojawapo ya marehemu, walikuta SMS hizo zikiwa zimetumwa kupitia namba ya mtandao wa Airtel siku moja kabla ya mauaji na siku ya mauaji.

“Ujumbe wa kwanza ulitumwa tarehe 6/8/2013 ukimjulisha (marehemu) kuwa ‘nina riziki’ na ujumbe wa tarehe 7/8/2013 saa nne au saa tano hivi ulisema niko Kia nakusubiri hapa,” alidai shahidi huyo na kuongeza:

“Tulianza kufuatilia ujumbe huo (wa tarehe 7/8.2013) ambao ndiyo ulikuwa wa mwisho kwenye simu ya marehemu na saa chache baadaye akauawa. Tuliandika barua Airtel kupata taarifa zake.”

Katika barua hiyo, shahidi huyo alidai waliiomba kampuni ya Airtel kuwapa taarifa mmiliki wa laini hiyo ya simu, ilikosajiliwa na kwa wakati huo ilikuwa ikisomeka eneo gani.

Alidai kuwa majibu ya Airtel yalionyesha kuwa laini hiyo ilikuwa imesajiliwa Arusha Agosti 3, 2013 kwa jina la Motii Mongululu lakini wakati huo haikuwa tena hewani.

“Walituambia baada ya kusajiliwa, laini hiyo ilifanya mawasiliano na namba nne tu na wakatuambia iliwahi kuchomekwa kwenye handset (simu) ambayo inatumia namba nyingine,” alidai na kuongeza:

“Tulifanikiwa kumkamata dada mmoja pale Arusha kituo kikuu cha mabasi anaitwa Hamisa (Kassim), ambaye ndiye mwenye hiyo namba, ambaye alikumbuka kusajili line kwa jina la Motii Mongululu.”

Hata hivyo, shahidi huyo alidai katika mahojiano, Hamisa aliwaeleza kuwa alisajili laini hiyo kwa maelekezo ya wakala mwenzake aliyemtaja kuwa ni Aneth Shija ambaye naye alikamatwa.

“Aneth alikiri ndiye aliyempa maelekezo Hamisa kusajili hiyo laini na nyingine mbili na kwamba, alizisajili kwa maelekezo ya mtu aliyemtaja kuwa ni Adam ambaye ni kijana wa kimasai,” alieleza.

Shahidi huyo alidai kupitia kwa Aneth walifanikiwa kupata namba ya Adam ambaye alikamatwa Mirerani, lakini naye akadai aliagizwa na mshtakiwa wa tatu, Mussa Mangu kusajili laini hizo.

Mkaguzi huyo wa polisi aliieleza mahakama kuwa baada ya Mangu kukamatwa na kuhojiwa, alikiri kusajili laini hizo za simu lakini naye akadai kuwa alitumwa na mshtakiwa wa kwanza, Sharifu.

“Alituambia maelekezo ya kusajili laini na kununua simu alipewa na bosi wake aliyemtaja kuwa ni Sharifu Mohamed. Alitueleza kuwa kwa ufahamu wake, yote yalikuwa ni maandalizi ya mauaji.

“Siku hiyo hiyo tulimkamata Sharifu nyumbani kwake na katika mahojiano ya awali alimtambua Mussa kama mfanyakazi wake na kukiri vitu vyote vilivyonunuliwa naye vilikuwa maelekezo yake,” alieleza.
Salute!
 
Back
Top Bottom