Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Kubwa unalopaswa kujua siku zote ni kuwa huwa hakuna siri ya watu wawili. Inaweza kudumu kwa muda mfupi au muda fulani lakini lazima itatoka. Sasa idadi yote hiyo ingewezekanaje kutunza siri hiyo. Hata mke mnayekula naye kiapo kanisani siku mkichokana atatoa yote ndio watu watajua kuwa una mikopo na watoto siyo wako ila ni wa rafiki yako kama tulivyoshuhudia juzi ya Muna na Peter kuhusu yule mtoto. Siri huwa ni mtu mmoja basi na wa pili atakuwa ni Mungu. Ndiyo maana huwa nashangaa wanaposema eti siri za serikali. Serikali ni kikundi cha utawala kilichopo kwa muda fulani hivyo hakiwezekani kukawa na siri hasa watunza siri ikiwa ni kwa watu wanaolipwa. Ndiyo maana naamini katika mtiririko huo huo waliomdhuru Lissu ni suala la muda tu tutawajua wote hata kama walirudi kwa msafara wa king'ora. Azori itajulikana tu. Kama makaburi ya halaiki ya miaka ya 40 iliyopita yanajulikana leo itakuwa hao waliompoteza Ben? It's just the matter of time. Time is a very good teacher - Time'll tell
CDM hoi?
 
umewai fanyiwa touchering na ant robbary wa police ni hatari ya kucheza na mamba kwenye maji

Hapana, lkn kwa hela aliyokuwa nayo Sharif alitakiwa atafute pro kupitia middle man Atoe mpunga ajitenge pembeni. Hapa nadhani mateso yalihusika sana.
 
Unajua kuna kitu kinanifikilisha.Iweje Sharifu mwenye Pesa atumwe Na chussa asiye Na Pesa za kumfanania??Na aogope Eti angetoka angemuua
Naomba tufafanulie hapo mkuu

Kabisa motive ya Sharifu kupanga kumuua Msuya haiko wazi kabisa. Sijashawishika na kwamba eti alitumwa na Chusa. Nadhani motive iko kwenye kuunganisha doti za aliyemuua dada wa msuya.

....kutokana na maelezo ya wadau hapa kama kweli mtuhumiwa wa mauaji ya dada wa msuya ni Mke wa Msuya, na kama kweli dada wa Msuya alikuwa mbele sana kusimamia hii kesi, na kama ni kweli inavyosemekana eti Msuya alitembea na mke wa Sharifu. Mwenyewe unaweza ku connect dot ukajua motive ya Sharifu itakuwa ni nini. Pengine wali team up na mke wa Msuya.
 
Bado siamin nahaya maigizo binafsi naona kuna zaid ya haya, kuuliwa kwa aneth(dada wamarehem) kifo chake lazima kitakua na mengi yanayo link nakifo cha kaka ake.

Kabisa! Naamini ile kesi ikichunguzwa vizuri kama hii kuna ukweli mzuri utagundulika na hapo ndo tutajua exactly nini ni nini. Nasubiri kwa hamu sana ile kesi ya dada.
 
Duuuh nimeamini Jeshi la Polisi wanafanya kazi, wanao beza hili jeshi hawajapata matatizo
Si kweli kuwa jeshi halifanyi kazi lipo poa sana tena makini kama litaachwa huru na c kuingiliwa jaribu kufuatilia kwa makini hata yanayofanyika ndani ya nchi likifanya nani hugundua?kama c kulalamika tu,police tanzania haishindwi kitu wako makini ni siasa tu ndo inaweza halibu sifa zake,ccm iwaache police wawe huru na c kuwatumia kwa maslahi yao.
 
hapa nawapa PONGEZI polisi, ila naomba kitu kimoja muboreshe, MNAPOKAMATA majambazi, msiishie kutuonyesha bunduki na RISASI, ni kosa la kimkakati, wenzenu nchi zilizoendelea tukio likitokea unakuta baada ya muda mfupi taarifa za mhalifu zinaonekana, urefu, rangi, asili, umri n.k, hii inaisaidia JAMII kuwa MAKINI na huyo mtu, lakini hata mhalifu anajirekebisha. MSIISHIE kuonyesha bunduki na visu tu
 
Ya ehe kweli kwangu inasomeka kama riwaya ;with all my respect kwa marehemu aliyekatishwa uhai wake,kwa familia yake na ndugu na marafiki wake walioondokewa na mpendwa wao,bado kwangu maelezo haya hayanipi direct link kati ya wahukumiwa na tukio,je murder weapon(s) zilikamatwa,any ballistic test report kuthibitisha kuwa zilitumika kwenye tukio?je wahukumiwa wamehusishwa vipi na crime scene? kama finger prints zao kupatikana kwenye eneo la tukio,alama za viatu walivyovaa kuoana na za kwenye crime scene(anything to put suspects at the crime scene) please kama kuna mwenye maelezo zaidi nitaelimika zaidi,na msimamo wangu siamini in death penaty maana haisaidii chochote kama kutufanya tuogope kutenda kosa kama hili na familia ya victims hawanufaiki chochote(long term jail inafaa zaidi).
 
Bongo movie wamekalia na stori za mke kumkimbia mme wake kisa maskini anaenda kwa boss/tajiri afu mwisho wake kila mtu anaujua...
mitaji midogo hawawezi cheza muvi wao wanacheza michezo ya kuigiza
 
Kabisa motive ya Sharifu kupanga kumuua Msuya haiko wazi kabisa. Sijashawishika na kwamba eti alitumwa na Chusa. Nadhani motive iko kwenye kuunganisha doti za aliyemuua dada wa msuya.

....kutokana na maelezo ya wadau hapa kama kweli mtuhumiwa wa mauaji ya dada wa msuya ni Mke wa Msuya, na kama kweli dada wa Msuya alikuwa mbele sana kusimamia hii kesi, na kama ni kweli inavyosemekana eti Msuya alitembea na mke wa Sharifu. Mwenyewe unaweza ku connect dot ukajua motive ya Sharifu itakuwa ni nini. Pengine wali team up na mke wa Msuya.
Mke wa msuya kuna kitu anajua, kina kipindi cha kiuchunguzi wa mambo ya mauji kama haya kwenye DSTV; UNUSUAL SUSPECTS , mhusika mkuu wa tukio anapatikana kwenye mazingira yasiyo ya kawaida kabisa .
 
Te
View attachment 817647Chusa
View attachment 817310Erasto Msuya View attachment 817311

Huyu mshatakiwa wa pili Swahibu Jumanne maarufu kama Mredi, alikuwa kama dalali wa kuwatafuta wakina Kahundwa na Ally Majeshi. Ambao ndio kimsingi walifyatua risasi zaidi ya 20 kwa Billionea Msuya, yeye kapona kwa sababu siku ya mauaji alikuwa anafunga ndoa huko Babati. Kwa hiyo alibi yake hapa ni ndoa.

Mshatakiwa wa 3 Mussa Mangu, pamoja na kutoa alibi ya kusafiri kwenda Singida kwa basi la Dar Express na kurudi kwa Lines, mahakama haikuona kama ni hoja ya msingi. Na kisha kumtia hatiani. Hii inaonyesha kuwa Jaji Magimbi katoa hukumu kwa kujiridhisha pasipo shaka kuhusu utetezi wa washtakiwa.

Sinema ilianzia katika gereza la Babati. Siku ambayo Shariff Mohamed alienda kumtembelea Chusa, ambaye kwa wakati huo alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji (katika mgodi wake).
Ndipo katika maongezi Chusa akamdokeza Shariff kuwa kuna jambo anaomba afanye. Na kwamba, hata kuwa kwake ndani ni njama za Msuya.

Vikao na mikakati yote iliratibiwa katika hotel ya Shamo Guest House. Hotel ya Shariff Mohamed, (mshtakiwa wa 1).
Ndipo mambo kadhaa yaliafikiwa.
1. Kumuingilia Chusa
2. Kusajili line za simu
3. Kununua pikipiki
4. Kutafuta shooter
N.k
Baada ya makubaliano hayo mchongo mzima ukaanza kusukwa. Na katika kusuka Chusa alimwambia Shariff (mshatakiwa wa 1), kwamba ukifika Arusha mjini mtafute Swahibu (mshatakiwa wa 2), ambaye leo kachomoka atakupa ramani yote na kinachotakiwa kufanyika. Ila wewe utafadhili zoezi zima.

Mredii kwa uzoefu wake akamtafuta Kuhundwa na Ally Majeshi. Ally Majeshi akatoa wazo kuwa Shariff atoe jiwe kisha akamuoneshe Msuya kuwa analiuza.
Shariff akakubali. Na mchongo ukawa ndio huo. Shariff akatoa jiwe lenye thamani ya zaidi ya 200 mil. Na kumpa Majeshi.

Majeshi alimpigia Msuya akamwambia anaitwa Ally anatokea Mererani kuna jiwe kapata. Hivyo anaomba waonane ili amwoneshe. Msuya akakubali na kumwambia wakutane mjini Arusha. Ilikuwa mida ya jioni saa 11, walikutana na Majeshi alimwonesha jiwe Msuya akalipenda akasema atatoa 140ml. Majeshi akakubali ila akamwambia hiyo biashara yuko na mdogo wake hivyo ni vyema mauziano yafanyike wakiwa wote wawili na mdogo wake.
Msuya akakubali. Kwa hiyo wanafanyaje. Majeshi akasema kesho kama anaweza wakutane njia panda KIA ili na mdogo wake pia awepo asione amemdhulumu. Msuya akakubali.

Huku maandalizi mengine yalikuwa yanaendelea. Line za simu zilisajiliwa Moshi mjini. Line 3 kwa kutumia jina la Kimasai nimelisahau kidogo nafikiri ni "Omolulu" line zote. Na aliyefanya kazi hiyo ni mshatakiwa wa tatu Mussa Mangi na aliyekuwa mshtakiwa wa 7 alichomoka na Ally.

Siku ya tukio asubuhi walikutana Shamo Hotel. Kisha wakakubaliana kuwa Kuhundwa atatumia bodaboda kutokea njia panda. Shariff alibaki njia panda na wengine.
Ally Majeshi alipakiwa na Msuya kutoka Arusha mjini. Kumbuka hapa anafuatwa mdogo wake Ally Majeshi ili mauziano yaweze kufanyika.

Walipofika njia panda wakakunja kuelekea alipo mdogo wake Ally Majeshi. Walipofika tayari Kuhundwa alikuwa kishafika eneo la tukio. Kisha Ally akashuka kama anaongea na Kuhundwa. Msuya kabla hajashuka Kuhundwa alifika na kufungua mlango kisha kuanza kumimina risasi. Kisha wakakamata boda na kuanza kuondoka. Shahidi pekee alikuwa kijana wa Kimasai wa miaka 18 aliyekuwa anachunga eneo hilo.

Mussa Mangu ambaye ni dereva wa Shariff Mohamed. Kuhundwa. Na Ally Majeshi, siku moja kabla walienda Namanga kununua Bunduki. Ambapo ilinunuliwa kwa 4 Mil. Na gari lililotumika kwenda ni la Shariff Mohamed aina ya VX.
Katika malipo ilikuwa imebaki kama millioni 10.

Walipofika njia panda. Wakaiweka pikipiki kwenye gari na kuelekea Arusha. Walipofika Arusha Shariff aliwamalizia hela yote 10 Mli. Iliyobaki. Hapo sasa maisha ya kawaida yaliendelea kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Ndipo wakaanza kukamatwa mmoja baada ya mwingine.


Kuhundwa alikamatwa Kaliua akiwa kwa mganga wa kienyeji. Polisi walioenda kumkamata walikaa kama siku 3 wakiwa wanatibiwa wote kumbe walikuwa kazini. Na Sadick pia madhani.

Ally alikamatwa Kigoma stand asubuhi saa 12. Alipofika Mwanza mnara ulisoma yuko Mwanza. Kisha akazima simu. Akaja kuiwasha akiwa anavuka Busisi. Mnara ukasoma tena. Wakasema huku anaelekea Geita au mikoa ya huko. Baada ya hapo mnara ukaja kusoma Kigoma. Ndipo polisi waliokuwa task force walifika Kigoma. Kwa siku mbili zote hawakufanikiwa kumkamata. Baada ya kukata tamaa wakiwa kwenye gari wanarudi, wakasema tupite stand kupata kifungua kinywa. Walipokuwa stand, moja wa askari akamuona mtu kama Ally. Alipojaribu kupiga ile namba Ally akapokea. Ndipo akamakamatwa.

Shariff Mohamed alikamatwa Arusha mjini. Baada ya kurudi kutoka safari. Saa 11 alfajiri alisikia watu wakigonga kengere ya getini. Alipochungulia katika CCTV camera akaona kuna polisi kisha akafungua geti na kukamatwa.

Chusa alikamatwa na kukaa ndani zaidi ya miezi 6 katika kesi hii ya Msuya. Kisha DPP akaonyesha nia ya kumuondoa Chusa katika hii kesi. Hoja kubwa ni yawezekana ni kwamba Chusa alikuwa gerezani by that time.

Wengine walikamatwa Mererani. Na wengine Arusha mjini. Chusa naye akakamatwa baada ya maelezo ya onyo "extra judicial statement" ya Shariff kueleza kuwa alipewa maelekezo ya kumuua Msuya na Chusa. Kwamba alipoenda kumtembelea Chusa gerezani Chusa alimuomba sana sana amsadie kumuua Msuya. Chusa alimwambia Msuya mtu mbaya sana, na amemdhulumu hela nyingi sana. Na kwamba hata kesi ya mauaji inayomkabili kwa sasa ni Msuya ndio alitengeneza.

Shariff anazidi kusema kwamba, kwa kuwa Chusa ni rafiki yake, na wanafanya naye biashara na ni rafiki mkubwa hakuweza kukataa ombi hilo. Ingawa alimuomba muda afikirie. Shariff anasema. Alipofikiria aliona kwamba Chusa akitoka anaweza kumuua yeye. Hivyo alikuwa hana jinsi zaidi ya kukubali hilo ombi la Chusa.

Ndipo idadi ya washatakiwa ikabaki 7. Moja akachomoka awali alipoonekana hana kesi ya kujibu. Wengine 6 ndio wamehukumiwa. 5 wamehukumiwa kunyongwa. Na 1 kachomoka ambaye ni Swahibu Jumanne maarufu kama Mredi. Ambaye yeye siku ya mauaji alikuwa Babati akifunga ndoa.

Three can keep a secret if two are DEAD.

MWISHO.

NB: Bongo Movie hizi ndo stori za filamu. Acheni mambo ya mvulana wa kimasikini kapendwa na msichana wa kitajiri.
Tengeneza script watu waanze kazi!
 
Back
Top Bottom