Pole Sana, huwa iko hivyo siku zote ukitaka kuchukua maamuzi yatakayo badili uelekeo wa maisha yako, ni hofu Tu Inakuja hata haijulikani inatoka wapi..
Unajua katika suala lako Hilo jiangalie wewe kama wewe Kwanza, usifikirie mambo ya "itakuaje" au "kitatokea nini au watu watafikiriaje", siku zote kwenye Jambo kama lako hakuna siku itakayotokea utakuwa na huo ujasiri, usipochukua hatua mapema utabaki na wazi Hilo Hilo Hadi unakaribia kustaafu utabaki na zile "ningefanya Tu".
Ujasiri huwa hauji hivi hivi Bali hutengenezwa ndani yako Kwa kujivika utayari, ukishaacha Tu kazi baada ya miezi kadhaa Kila kitu utaona Kipo kawaida na maisha yataendelea...
Ukikaa chini na kutafakari na ukajiona kweli Niko tayari basi usisite, Fanya maamuzi hapo hapo, hakuna mtu yoyote Yule duniani ambaye amefanya maamuzi muhimu ya maisha Yake halafu kwenye huo mchakato wa kufanya maamuzi akajihisi comfortable lazima tu hofu na kukosa nguvu vinakuja but huwa tunakuwa wabishi na Ku move on, lazima uwe mbishi...
Sisi tuliokulia kwenye kujiajiri huwa tunaelewa Sana mambo yalivyo, sometimes kuna maamuzi makubwa ya biashara ambapo mambo yakienda vibaya basi unaanza moja, unafilisika but tunakomaa licha ya kuwa na hofu lakini tunakuwa wabishi tunasonga mbele....maamuzi mengi tumefanya Tukiwa hatuna uhakika but ni guts Tu.
Self belief ni muhimu Sana kuwa nayo, siku zote hakuna muda sahihi wa kufanya maamuzi kama hayo, lazima Tu utajawa na hofu...Na kinachokufanya hofu izidi kuwa kubwa ni kwamba Una Options, kama ungekuwa Huna option basi usingefikiri mara mbili ungejitosa moja Kwa moja kwenye biashara...