Sina ujasiri wa kuacha kazi

Sina ujasiri wa kuacha kazi

How prepared are you after quitting your job? It's very interesting kusoma stories za namna hii, hasa kwa mtu kama wewe unayesema huna side hustle yoyote na unataka kuacha kazi.
Mkuu Hicho unachosema ndio woga wenyewe ambao umewakeep watu kwenye Ajira up to 60yrs tena na wengine bado waki retire wanaomba tena kazi au kufanya kazi za Mkataba, hii yoote imetokana na Hofu kwamba sasa niliacha mbona sijajipanga, mbona Sina chakufanya lakini cha ajabu anastafu bado Hana alichojipanga😅😅
 
Mume wangu aliniachia maamuzi nifanye mwenyewe.

Hata leo nikimuambia nimeacha hana neno ila naogopa tu.

Yeye ni muajiriwa na Mfanyabiashara pia, yeye hana mpango wa kuacha.
Ila naona ni vyema mwanaume ndo aache kazi asimamie biashara,ila siyo mwanamke.

Namaanisha kama wote wawili mume na mke ni waajiriwa,nk vyema mume ndo aache.
 
Mkuu Hicho unachosema ndio woga wenyewe ambao umewakeep watu kwenye Ajira up to 60yrs tena na wengine bado waki retire wanaomba tena kazi au kufanya kazi za Mkataba, hii yoote imetokana na Hofu kwamba sasa niliacha mbona sijajipanga, mbona Sina chakufanya lakini cha ajabu anastafu bado Hana alichojipanga😅😅
Mkuu angalau toa ABC ulivyo jiandaa kisaikolojia,maana kiukweli hizi kazi ni kama ulevi..hata kama unalipwa 300k kwa mwezi mtu unajikuta unakomaa tu.
 
Wengi tunatamani tufike hapo. Hongera .
Hayo malengo ulojiwekea kama yamekamilika , na hakuna inflation kubwa ya maisha, acha kazi kwa busara, wekaza muda zaidi kwenye vyanzo vingine huku ukifurahia Uhuru wako uloujenga baada ya muda mrefu.
 
Dadangu hakuna binadamu anayetosheka ni vile tuu sijui inakuaje

hao watoto unafànya kazi kwa ajili yao, wapambanie tuu

Huyo mume nae hapo ndo balaa siku mmepishana kiasi utawaza mengi

Usiache kazi dearest sis, we love you pambana familia ile,y
 
Habari wana JF.

Mtanisamehe kama nitaandika bila mpangilio, wengine hatuna utaalamu sana wa Lugha.

Wale watu wa dhihaka na kuona mtu akileta mada humu mnaona anajisifia plz, naomba mkae pembeni.

Nilijiekea dhamira na malengo nikifikisha 40 yrs nitaacha kazi sababu malengo yangu yatakua yametimia, ila Mungu ni Mkuu nimetimiza malengo yangu mwaka jana December nikiwa na 38 yrs.

Ila naogopa sana kuacha kazi, nimejikuta sina ujasiri kabisa.

Kwanini naacha kazi??
1. Sina passion na kazi hata kidogo, sipendi kuajiriwa.

2. Mshahara ninaopata kazini, naupata kwenye biashara tena zaidi pia niliweka FDR ambako nako kunanipa hela nzuri tu kila baada ya miezi 3. Hivyo, hata nikiyumba kibiashara nina uhakika wa kupata hela nzuri tu. Pia nina vitega uchumi vingine nisingependa kuviweka wazi ila vipo vinajiendesha vyenyewe mimi ni kupita tu kuangalia mara chache.

3. Kulea watoto wangu kwa ukaribu zaidi roho inaniuma kwa week napata siku mbili za kukaa full na watoto wangu.

4. Mume wangu anasafiri sana, hivyo nakosa muda wa kukaa nae pia anakua ananihitaji nimsindikize kwenye safari zake nashindwa. Natamani nipate muda zaidi nimlee pia Mume wangu

pamoja na yote hayo najikuta nakosa ujasiri kabisa, mlioacha kazi mliwezaje? Mlipata changamoto gani? Mlijutia? naomba ushauri.

Nimeona heri niombe ushauri huku sehemu ambayo sifahamiki.
Nakushauri acha Anza kuwa karibu na family Kwa kuwa tayari una vitega uchumi.
 
Me naona uache tu iyo kazi. Au badirisha taaluma. Mi mwenyewe nimeajiriwa ila kazi hainipelekeshi. Mwisho masaa 6 tu ofisini.
Hii kazi nzuri ingawa kazi zote za serikali ziko hivi, kazini saa 2 asubuhi, saa tisa upepo
 
Simara WENGI tumejiwekea malengo kama hayo ya kwako kufikia malengo fulani basi tupishe Ajira tufanye mambo mengine hasa tukiufikia Uhuru wa kifedha.

Kwa busara siku moja Njoo na Uzi wa Analysis angalau kidogo tu namna umeweza kufikia Uhuru wa kifedha ili nasisi tupite mlemle kwa maboresho zaidi.
 
Hofu yako inaweza kuwa ni mazoea tuu
Mazoea ya cycle ya wafanyakazi wenzio, au ile routine ya asubuhi
lakini utapata nafasi kubwa ya kulea watoto kimaadili na kuwafunza mengi kama mama
Kila la kheri
 
Ukiwa umeajiri na ukafungua biashara, basi biashara utaiendesha bila presha na itakimbiza hatari mpaka utaona kujiajiriwa ni kujichelewesha... Ila utakapoacha kazi basi biashara itaanza kulegalega..

Ila ukijipanga vizuri, kuajiriwa ni kujipotezea muda.. Kama umejipanga vema, fanya maamuzi sahihi
 
Back
Top Bottom