Sina ujasiri wa kuacha kazi

Sina ujasiri wa kuacha kazi

Habari wana JF.

Mtanisamehe kama nitaandika bila mpangilio, wengine hatuna utaalamu sana wa Lugha.

Wale watu wa dhihaka na kuona mtu akileta mada humu mnaona anajisifia plz, naomba mkae pembeni.

Nilijiekea dhamira na malengo nikifikisha 40 yrs nitaacha kazi sababu malengo yangu yatakua yametimia, ila Mungu ni Mkuu nimetimiza malengo yangu mwaka jana December nikiwa na 38 yrs.

Ila naogopa sana kuacha kazi, nimejikuta sina ujasiri kabisa.

Kwanini naacha kazi??
1. Sina passion na kazi hata kidogo, sipendi kuajiriwa.

2. Mshahara ninaopata kazini, naupata kwenye biashara tena zaidi pia niliweka FDR ambako nako kunanipa hela nzuri tu kila baada ya miezi 3. Hivyo, hata nikiyumba kibiashara nina uhakika wa kupata hela nzuri tu. Pia nina vitega uchumi vingine nisingependa kuviweka wazi ila vipo vinajiendesha vyenyewe mimi ni kupita tu kuangalia mara chache.

3. Kulea watoto wangu kwa ukaribu zaidi roho inaniuma kwa week napata siku mbili za kukaa full na watoto wangu.

4. Mume wangu anasafiri sana, hivyo nakosa muda wa kukaa nae pia anakua ananihitaji nimsindikize kwenye safari zake nashindwa. Natamani nipate muda zaidi nimlee pia Mume wangu

pamoja na yote hayo najikuta nakosa ujasiri kabisa, mlioacha kazi mliwezaje? Mlipata changamoto gani? Mlijutia? naomba ushauri.

Nimeona heri niombe ushauri huku sehemu ambayo sifahamiki.
Kama upo stable financial kama ulivyosema unaweza kuacha tu na ukasimamia biashara zako kwa uhakika ila kama sivyo endelea na ajira ukiwa unaziwekea biashara misingi imara. Kazi (ajira) tunazifanya tukiwa tunalenga baadae tuje kujisimamia wenyewe sasa kama umeshafika uko, safi chukua maamuzi tu usijishauri sana. Nawasilisha
 
Hilo ndo tatizo apo kwenye kukubebwa na hyo status.......ni sawa na wale ndugu zetu wa kwenye system ata awe na mapesa gani bado wanawaza uchaguzi ujao.

Kwasababu wanaamini wakiwa uko ni mwendo wa mbeleko tu na status kuwa mimi mtu mzito.....

Ushauri, kaa na mumeo chini muongee vzuri, mmeo ndo anamaamuzi ya mwisho,

Najua unaogopa ukiacha kazi afu biashara nayo ikaja kuyumba jamii itakuonaje.....!! Ila mmeo ndo final say
Hongera sana. Mwenzio Bado napambana
 
Umesema unapata kipato zaidi ya mshahara kwenye biashara na vitega uchumi unavyo pia akiba si haba fanya maamuzi tu maisha mafupi sana Mkuu, wengi tuna ndoto kama zako kujitoa kwenye matrix ila angalia usije ukajikita kwenye biashara ukawa bize zaidi hata ya sasa lengo la kulea watoto na mume likafeli. Balance mzani
 
Tulia Kwa umakini fikisha miaka 45 hapo ata NSSF Yako utakuwa juu ndyo ufanye hayo maamuz
 
Back
Top Bottom