Sina imani tena na Chadema

kwani jamani kuna m2 analazimishwa kuamini chama fulani? kuamini chama chochote ni m2 mwenyewe,kama huna imani na chadema kaunde chama chako then have faith with it usituzingue.
 
Nakubaliana nawewe kwamba madaktari ni watanzania lakini tatizo la watanzania hawa wapo tayari kuona watanzania wenzao wakipoteza uhai kwa ajili ya maslai yao

Hili swala la mgogoro wa madaktari kiongozi kuna mambo ya kusikitisha sana. Kuna mapungufu makubwa sana kwenye uongozi wetu na nadhani sababu kubwa ni kuendelea kufanya mambo kwa 'mazoea'. Miaka kama miwili nyuma nilishinda muhimbili, ukweli mortuary kulikuwa busy! Na nilijaribu kumuuliza dokta mmoja kuna namna madaktari wakakaa na kuangalia kwanini vifo ni vingi? jibu lilikuwa -vingi vinaepukika.

Sijui mawasiliano kati ya watawala na madakatri yalikuwaje huko nyuma lakini kwa mtazamo wangu kuna kasoro mahali, tena kasoro kubwa. Na matokeo yake madaktari wamejikuta wanafanya kazi ya kuwa 'eye witness' wa wagonjwa wanaopoteza maisha kwa mambo yanayoupukika. Lakini hebu tujuilize, hivi kweli taifa tumeshindwa kutatua huu mgogoro? Na inapotokea serikali inakuwa na mgogoro na watumishi wake nini njia bora ya kupata muafaka? Kama ipo kwanini hatujaitumia?
 

kwa ili la kuwaunga mkono madaktari wamaongea chadema wenyewe, njia ya kufuta makosa walitufanyia watanzaia wahali ya chini ni kutuomba radhi kwani wanaoiongoza chadema ni binadam na kukosea nijambo la kawaida kwa binadam.siyo kutaka kutuamisha kwenye ili kwa habari zao za kutaka kuuliwa. Izo mbinu chafu za ccm azifai kwa chama makini kama chadema
 
Waache kutoa visingizio kama wanataka kujimaliza wenyewe wasema tu .Uraisi utawamaliza 2015 sio mbali tusubiri tuone nafsi ya mtu itakufa kwa ahadi ya mwenyezi mungu na wala sio kwa kupenda binadamu
 

Shida iko wapi? William Mshumbusi si endelea na ccm?
Wengine tulishashituka zamani, hatudanganyiki tena kwa propaganda laini laini hizi!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu umeongea point sio wale wanaokalia kutukana baada ya kushindanisha oja. Ayo yote yametokana na ccm kwaiyo suluisho la tatizo ili na mengine mengi yanayoikabili nchi yetu nikuiondoa ccm madarakani sikuanza kutoana roho wenyewe kwa kunyimana matibabu uku viongozi wakiendelea kula raha. Kwani wao matibabu wanapata nje ya nchi, na swala la kuindoa ccm madarakani linawezekana kama chadema watajipanga vizuri, lakini si kwa njia ihi ya kushabiki mgomo wa madaktari
 
Reactions: FJM
Chadema wananchi wanaitaji kujua mtawafanyia nini sio siasa zenu za matukio.

Wananchi watakuwa na haki ya kuuliza maswali hayo baada ya kuiingiza CDM madarakan, hadi sasa nayeulizwa kafanya nini ni CCmi
 

Mara zote Chadema ilisema inaunga mkono madai ya madakatari kuhus uboreshwaji wa sekta ya afya mathalani wakati hivi sasa Hospiatalia kubwa ya Tumbi inayohudumia majeruhi wa ajali za barabarani husuana kipande kikubwa cha barabara kuu ya Morogoro, lakini hospiatali hiyo haina huduma ya X-ray inabidi wa wagonjwa wasafirishwe kwenda hospitali binafsi kama vile Bochi iliyoko Kimara Temboni ili kupata huduma hiyo. Madaktari walikuwa wakidai kuwa hospitali ya ngazi ya wilaya ipatiwe mtambo wa X-ray, hivyo serikali ingelazimikakununua mitambo 129 tu kwa kulingana na idadi ya wilya zilizopo. Mtambo wa kisasa kabisa wa X-ray unaghrimu Dola 140,000 tu sawa X Tshs 1570 =Milioni 219,800,000/=.

Hivyo Bilioni 27.5 zilizotumika kuadhimisha sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, miezi 6 tu iliyopita yaani tar 9 Desemba 2011 zingeweza kununua mitamboa ya X-ray Tshs 27,500,000,000/219,800,000= Mitambo ya Xray 125.

je kama kipi bora kusherehekea miaka 50 ya uhuru kwa wiliya kupatiwa mtamboa wa Xray au wanansiasa kufuja kiasi kikubwa cha fedha kiasi hiki? Fungua macho bro
 
Wewe si Chadema, sepa!, usalama wa mtu ni muhimu katika kuwa huru kufanya shughuli zake, wewe ungetishiwa usalama wako ungejisikiaje, au kwa vile sio wewe?!, kuwa mstaarabu, watu watafute namna ya kudeal na jambo moja ndio waendelee kupambana mengine kwa nguvu
 
Wewe si Chadema, sepa!, usalama wa mtu ni muhimu katika kuwa huru kufanya shughuli zake, wewe ungetishiwa usalama wako ungejisikiaje, au kwa vile sio wewe?!, kuwa mstaarabu, watu watafute namna ya kudeal na jambo moja ndio waendelee kupambana mengine vizuri
 
Wewe si Chadema, sepa!, usalama wa mtu ni muhimu katika kuwa huru kufanya shughuli zake, wewe ungetishiwa usalama wako ungejisikiaje, au kwa vile sio wewe?!, kuwa mstaarabu, watu watafute namna ya kudeal na jambo moja ndio waendelee kupambana mengine vizuri
 
Iwe Mushumbusi, huwezi kuwa na imani na chadema iwapo huna hata imani na wewe binafsi. Ushomile hadi unakosa imani kwa vwire wewe ni nshomile mwanangu.
 
Chadema wanashauri, wanapendekeza mengi mazuri but Serikali tawala, inayokusanya kodi za Wananchi na makusanyo mengine mbalimbali wanakuwa wabishi kutumia fedha zinazopatikana vizuri kwa manufaa ya nchi, huduma nyingi nchini ni mbovu, barabara ndio usiseme, hao maengineer utafikiri wanafunzi wanaojifunza kutengeneza hizo barabara, yaani mvua ikinyesha, barabara hazieleweki tena, wanapoteza hela kulipa watu wa aina hii, wanawapaga nini mpaka wanaendelea kufanya nao kazi, nani anawapitisha kupata that tender, mnabania hela za Wananchi ili mkajengee, au mnafikiri Chadema wawape hela pia, haiwezekani kihivyo, simple simple, nyie ndio hizo ofisi zenu zinakusanya kodi, tumieni mapato ya nchi vizuri, sio kuchakachua tu kila mara, mnaharibu nchi, haivutii kabisa bado miakayote hiyo ya Uhuru hata kuikaribia korea robo hamjaweza, hamjisikii aibu?!, Mi naona aibu, kwani Africa kunani hasa?!, ndio ubinafsi hautaki kupungua?!, viongozi wanaona rasilimali zilizopo kwenye nchi zao kama mali zao binafsi na wanachakachua bila aibu, wanajitafutia balaa kweli!
 
Mkuu wangu kazi ya Chadema sio kubadilisha sera za CCM..Chadema hawawezi kupigania bebi ya mazo wala mikataba ya madini isipokuwa wanaweza tu kushauri kwa kuonyesha mapungufu na CCM ndio wenye maamuzi ya kufuata ama kutofuata..

Kifupi labda nikwambie hivi Chadema ni sawa na mume alokataliwa.. Sasa ni kazi gani mume huyu anaweza kuingilia mapoensdzi yako na binti zaidi ya kuwashauri wananchi jinsi gani wanavyopokea abuse hizi. Na pia bado ni jukumu la wananchi wenyewe kufikiria kwamba wanaweza chagua chama kingine kama huyo binti anayekuwa abused. Ni jukumu pia la Chadema kuwaambia CCM abuse wanazozifanya sii haki wala uungwana isipokuwa ubora wa mwanamme ni kufanya kadhaa wakadhaa.. At the end of the day ni CCM anayekwenda na mwali chumbani.. Chadema hawezi kuingia hadi kitandani ankoo...Hiyo imani yako kwao ni kuwaonea maana unawataka wafanye kazi ya watu halafu ionekane wao ndio washenzi..
 
Watu wanazani kukipenda chama ni kwa kukisifia tu.

Tunapasa kukikosoa ili kisimamie hoja za wananchi.

Tunatumia akili kubwa sana kufikiria vitu vidogo. Sikatai chadema ndio chama bora kwa sasa. Ila mi si mwanasiasa.
Ni bora kwa msemo ufuatao

"Kwenye vipofu mwenye jicho mmoja Mfalme"
 
Yeyote anayezungumza au kanusha mwenzake bila hoja ni siasa siasa siasa tu. Mwisho 'TRUTH WILL OUT'.
 

aha ahaaahaa bado hujamalizia kuna madj, repa na majambazi pia!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…