naona wazi sasa sinema la siasa la siasa linavyovutia watu na kuacha watu na matumaini na shida zisizotatulika.
Chadema wanashindwa kupigania mambo muhimu sasa kama bei duni za pamba, na minofu ya samaki mgomo wa madaktari, mgogoro wa walimu na selikali au uporwaji wa madini wanatuletea tena move ya maigizo ya dr slaa, myika na lema eti wanataka kuuawa!!
Lengo la muvu hii watu waache kujadili mambo nyeti wajadili utumbo huo. Mi sasa sioni harakati za chadema bali siasa uchwala. Sioni umoja tena wa chadema bungeni.
Wanasiasa mnakera, mnakera kweli. Wawaache wanaharakati wadili na mnyika kwa lipi.
Washabiki wa vyama fumbua macho chadema washakula chunguza uone.
Siamini kwenye miujiza au habari za kuhusu freemason na mikanda yao ya habari za "microchip".
Ila chadema inavyoenda nahisi sasa mbowe kawekewa microchip na sasa anaendeshwa na mtambo uliopo ikulu. Hakuna kitu sasa. Wakulima jipiganieni. Wavuvi jipiganieni, walimu jipiganiene. Chadema hakuna umoja tena wanaongea wanapata posho wanarara.
Siasa siasa siasa zinakera. A
waliopangwa kuwawa ndo hao wanaoongoza mijadala ya kudai maslahio ya watumishi wa umma. Wanatoa mapendekezo ili kufanikiwa hili,
1. Sheria za madini zirekebiswe, ili tuwe na win to win situation
2. Kupunguza kodi kwa walalahoi na kuzipandisha kwa mashirika, na makampuni yanayofurahia uhuru waliopewa na ccm. Hapa wapo vodacom, tigo, na wengine kibao.
3. Wanapendekeza mishahara na malupulupu kwa viongozi wa juu, wabunge mawaziri, makatibu vipunguzwe ili pesa itakayookolewa itumike kutatua kero za mda mrefu za elimu, afya na watumishi wa umma.
4. Kila siku ndio wanaosema, matumizi ya serikali ni makubwa, na wanaitaka serikali kubana matumizi yasiyo lazima, hasa kununua magari ya anasa, saffari za nje na mengine mengi. Kuthibitisha hilo, mnyika anatumia gari la milion 7-10 pekee, linamtosha na anatimiza matakwa ya wakazi wa ubungo vizuri, tena hadi kavuka mipaka ya ubungo, ni kiongozi wa kitaifa.
Sasa mauaji yaliyotajwa, si kwa kuwa ccm imeshikwa pabaya na hao walitajwa kupangiwa siku za kuishi? Kipi chadema imeenda pembeni?
Hata hivyo hujawahi kuwa na imani na chadema, kila siku wewe ni ccm