Simulizi Yenye Funzo la Maisha: "SINA CHAGUO"

Simulizi Yenye Funzo la Maisha: "SINA CHAGUO"

TULIPOISHIA
Sikutishika na vitisho vyake, nilimwangalia kwa umakini kisha nikatabasamu baada ya kubaini kile nilichoshindwa kukibaini kwa wakati wote. Nikaichukua damu ile, nikainywa yote kwa mkupuo, kisha nikamuuliza kama kuna nyingine anipatie, “nimeipenda sana radha yake.” niliongea kwa furaha sana.''...

ENDELEA
(Kuna kizuri kibaya, Kuna kibaya kizuri.)

Lilichanua tabasamu la ajabu usoni mwake, akanikumbatia kwa nguvu huku akinipiga mabusu yasiyo na idadi usoni mwangu. Sikumzuia kufanya vile, nilimuacha mpaka alipoizoea furaha aliyokuwanayo ndipo tukaongea vizuri.

“Hatimaye umepona mgonjwa wangu” alianza maongezi kwa sentensi hii iliyofatiwa na maelezo marefu ya kweli na uhalisia ulioniacha mdomo wazi.

Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba, ugonjwa ulioniuguza kwa kipindi chote halikuwa tumbo wala kifua kama nilivyodhania, kiliuwa kichwa, yaani ugonjwa wa akili. Ajari iliyonipata iliuathiri ubongo wangu kwa kiasi kikubwa. Kile chuma kizito kilichonidondokea kichwani ndicho kiliupangua mfumo mzima wa ubongo wangu, nikaanza kuuishi ulimwengu wa vichaa na wendawazimu waliorukwa na akili. Sikuwahi kuzimia kama nilivyokuwa nikijidanganya, isipokuwa ubongo wangu ulishindwa kunasa kumbukumbu yoyote kila baada ya kupewa tiba ya tatizo langu. Akili yangu ilinitafsiri kinyume cha uhalisia wa taswira nyingi nilizoziona, nyeupe ikafanywa nyeusi, manjano ikawa kahawia na nyekundu ikafanywa nyeupe. Ndiyo maana nikamuona nesi wangu akinywa damu, hali ya kuwa yalikuwa maziwa mgando ya kawaida kabisa.

Ni kweli nilitafutiwa matabibu bingwa wa kunitibu, lakini walitibu kichwa wala si kifua. Walilazimika kutafuta vitu vichache ambavyo nilivitambua kwa uhalisia wake ambavyo vilitakiwa kutumika kama sehemu ya tiba yangu. Hawakupata vitu, ila watu wachache sana ambao bado nilikuwa nikiwatambua kwa uhalisia wao, watu hao ni wale marafiki zangu watatu, Salome, mwalimu, mama Eliza na Eliza mwenyewe. Kwamba nilishindwa kuwatambua hata wazazi wangu kwa kiwango kilichotakiwa ili wajumuishwe kwenye mchakato wa matibabu yangu. Mchakato wa matibabu yangu ulikuwa kuwatumia watu wachache niliowatambua kunitengenezea ulimwengu mdogo wa kimawazo ili niuishi uhalisia kupitia watu hao, ndiyo maana sikupewa muda wa kuwaza nje ya watu hao. Fikra za ulimwengu wangu ziliongozwa na kuelekezwa kuzunguka miongoni mwa watu hao tu ili kunitengenezea maisha halisi. Kwahiyo kitu halisi kwangu kilikuwa kile nilichokiona na kukisikia kwa watu hao tu, vingine vyote ni uongo na upotoshi wa ubongo wangu.

Mwanzo wa kupona kwangu lilikuwa ingizo la watu wapya katika ulimwengu wangu mdogo, mtu wa kwanza ni Rukundo au Pendo kama nilivyozoea kumuita. Huyu alikuwa mtu wa kwanza kabisa kufanikiwa kupenya na kuuingia ulimwengu wangu. Kila nilichokiona na kukisikia toka kwake kilikuwa halisi, nikakishika na kukikumbuka barabara kabisa mithili ya mtu mwenye akili timamu. Ndiyo maana alipendekezwa kuwa muuguzi wangu, kwasababu niliukumbuka vizuri sana uhalisia wake kila nilipomuona. Alikuwa nami katika kila hatua, akajitoa kwa hali na mali kuhakikisha ninauishi kwa usahihi ule ulimwengu wangu mdogo. Mtu wa pili kupenya na kuingia kwenye ulimwengu wangu alikuwa ni daktari Josefu, akafatiwa na baadhi ya matabibu, daktari Hamza na wengine wengi ambao ninawakumbuka mpaka sasa. Tatizo langu kubwa ilikuwa kutotambua uhalisia wa vitu vingi, nikavitambua vichache vilivyofanywa na wale watu wachache nilioutambua uhalisia wao. Ndiyo maana ningekula chakula kwa furaha baada ya kuambiwa kimetoka kwa yule nimjuaye. Matabibu walilazimika kuniongoza katika mzunguko wa ulimwengu mdogo wenye uhalisia, kuniepusha na ulimwengu mkubwa usio na uhalisia kwani ungezidi kuichanganya akili yangu, huenda ningekuwa kichaa kabisa.

“Nilifurahishwa na kila swali uliloniuliza kuhusu mtu au kitu cha nje ya ulimwengu niliokujengea maana liliashiria kuanza kulejea kwa kumbukumbu zako. Ila sikuyapenda yale maswali uliyoniuliza kuhusu warembo wako, ha! ha! ha! ha! ha!” Ndivyo Pendo alivyomalizia maelezo yake, kisha akanikumbatia kwa nguvu kama alivyofanya mwanzo. Awamu hii mwili wangu ulifunguka, viungo vya mwili wangu vikaingiwa na uwezo wa hisia, sasa nikalihisi vema joto tamu la mwili wake. Zilikuwa hisia za ajabu sana zilizoufanya mwili wangu kukakamaa sana, nikahisi kukaribishwa ndani ya ulimwengu huu wa watu wengi, ulimwengu wa raha.

“Nimekuwa hivi kwa muda gani sasa?” niliuliza wakati nikiendelea kuyashangaa mabadiliko ya mwili wangu, vinyweleo viliianza kusimama. “Miaka saba, nilikusubiria sana mpaka nikaanza kuhofia kama hutoirudia hali yako ya kawaida.” Alinijibu kwa sauti yake nyororo, sauti ya kubembeleza iliyosikika kama wimbo mtamu masikioni mwangu. Nilishangazwa sana na taarifa ile, nimewezaje kuishi ndani ya ulimwengu wangu mdogo kwa miaka yote saba? Mshangao huo haukuyazuia yale mabadiliko ya kasi niliyoyahisi mwilini mwangu. Mapigo ya moyo yalianza kudunda mbio, pumzi zikabadilika, nikaanza kuhema juujuu kama niliyeelekea kukata roho. “Usiwe na wasi wasi tena, ndiyo nimesharudi kwenye hali yangu ya kawaida.” Niliongea kwa sauti kavu ya kiume, yenye kitetemeshi, nikamwangalia Nesi wangu aliyekuwa bize kuyachochea mabadiliko yangu. Hakuridhishwa na kasi niliyokuwa nayo, akaanza kunibadilisha mwenyewe. Nilimshuhudia akiivua ile ngozi niliyovikwa ndani ya ulimwengu wangu mdogo, akaitoa yote kabisa.

Aliitupa pembeni kisha akanitazama kwa uso wake uliochanua tabasamu la haja, nikadhani sasa mchakato wa uponyaji umekamilika. “Kuna jambo moja nitalifanya japo halikujumuishwa kwenye majukumu yangu ya awali. Nataka nimuamushe.” Sikuweza kulipinga wazo lake, niliitikia kwa kugugumia mithili ya beberu lisilotaka kulikwaza jike lake. Hapo ndipo ukaanza mchakato mpya, akajitia uchizi wa kutamka maneno yasiyoeleweka akidai kwamba anamuamsha aliyelala kwa kipindi kilefu. Niliufurahia sana mchakato ule ulioleta raha ya ajabu kwetu sote, yeye aliufurahia utamu wa mchakato kwa kutoa miguno na vigeregere vingi vya kike; nikamuunga mkono kwa kumchombezea mahadhi ya sauti ya nne. Sauti nzito ambayo bila shaka aliifurahia sana. Mchakato ulitamatika kwa mafanikio makubwa sana, tukayaona kwa pamoja matalajio yetu. Ajabu akahitaji kurudia tena ajilidhishe zaidi uhakika wa kazi aliyoifanya. Tulirudia, tukarudia na karudia mpaka tukachoka wenyewe. “Kazi yangu imekamilika sasa, kesho nitakupeleka uuone ulimwengu mkubwa.” Aliongea kisha akajilaza kifuani mwangu.

Usika ulikuwa mrefu sana, uliosheheni matukio yaliyoichosha miili yetu. Labda nisiseme matukio, niliite tukio moja ambalo tulilifanya kwa kujirudiarudia, tena kwa kila namna tuliyoipenda mpaka pale tulipojihisi kuchoka ndipo tulikubaliana kulala. Nilikuwa wa kwanza kushtuka toka katika usingizi mzito ulioondoka na uchovu wangu wote, sasa nilijihisi kuwa mwepesi, wepesi wa ajabu ulioambatana na njaa tumboni. Nilijinyanyua kivivu nikaa kitako kumtazama yule aliyejilaza upande wangu wa kushoto, alikuwa kimya; kapitiwa na usingizi na kupotelea kusikojulikana. Niliuangalia kwa kina uso wa binti huyu ambaye nimeishinaye kwa muda mrefu sasa, nikagundua uzuri wa ajabu uliojificha ndani ya sura yake ya upole. “Ama kweli ni binti mrembo sana.” Nilijisemea kimoyomoyo, nikajishangaa kwa nini sikuuona uzuri wake mapema.
Niliulaumu sana ubongo wangu kwa kuupoteza ufahamu kwa kipindi kirefu, ukanipelekea kushindwa kuona na kuvitambua vitu vizuri vinavyonizunguka. Muda huo nilimuona akiutikisa mwili wake, nikazani ameamka kumbe alikuwa akijigeuza kuufaidi usingizi wake. Macho yangu yalitua juu ya miinuko miwili iliyojitengeneza ndani ya shuka, nikashuhudia namna ilivyovutia macho kutazama. Nilijiridhisha bila shaka yoyote kama Pendo ni msichana mzuri sana. Hisia za mapenzi zilipokolea, kiungo chenye hasira zaidi kilisimama kidete kwa ujasiri. Kikaanza kunishawishi nifanye juu chini nimuamushe aliyelala akione, huenda angekihurumia na kukitimizia hitaji lake. Nilikikemea kwa hasira, kikatulia kimya. Sikukubali kuongozwa na kiungo dhaifu namna ile wakati nina akili timamu.

Maajira ya saa mbili za asubuhi ndipo aliamka, bado alionekana kuwa na uchovu mwili, ikamlazimu kujimwagia maji ili kuuweka sawa mwili wake kabla ya kuingia jikoni kuandaa kifungua kinywa. Muda huu nilikuwa sebuleni, nimeketi mbele ya runinga kubwa iliyobandikwa ukutani; nikifatilia filamu kali ya mapigano. Niliuhisi ujio wa mtu aliyenyata kwa umakini mkubwa nyuma yangu. Hata hivyo sikujihangaisha naye maana nilijua amani inatawala sana ndani ya nyumba ile. Tulikuwa wawili tu, mimi na yeye, kwahiyo kama si mimi ni yeye na kama si yeye ni mimi. Alisogea mpaka pale nilipokaa, akatoa ukelele wa ghafla kunishtua lakini sikushtuka hata kidogo. Niligeuka kwa utulivu kumtazama; nikionesha kukasilishwa na tukio lile. Hilo likawa kosa langu kubwa kwa siku ile, alininunia wakati wote tulipokuwa tukipata kifunga kinywa. Akazila kuongea na mimi. Hakunijibu hata pale nilipomuuliza kuhusu safari ya kwenda ulimwengu mkubwa, akajitia ubize wa kuchezea simu yake. Japo mimi siyo bingwa wa mambo ya wanawake, ila niliikumbuka sentensi moja niliyowahi kuisoma ndani ya hadithi za mapenzi. Sifa ya mwanamke kudeka, adekezwe. Niliyaamini maneno hayo, nikajisogeza pale alipo nikaanza kumbembeleza nikimuomba msamaha kwa kutojali hisia zake.

Nilifanya hivyo kwa kitambo kidogo mpaka nikaanza kuchoshwa na kitendo kile cha kujitia uchizi na kuigiza utoto wa kubembeleza mtu mzima. Wakati nikielekea kuchoka ndipo niliyaona matunda ya kazi niliyoifanya, nililishuhudia tabasamu pana lilichanua usoni mwake. Nikamwangali kwa kina mpaka alipoanza kutoa kicheko chake cha chinichini kilichoambatana na machozi. Hakuwa amabadilika hata kidogo, ni yule yule nesi wangu, Pendo kiboko ya tabia yangu wa kutokujali hisia za wengine. Alinirukia, akanikumbatia kwa nguvu. Kile kicheko chake kikakoma, sasa akailejea ile sura yake ya kuvutia. Tulitazamana kwa kitambo kidogo kisha tukaulejea ulimwengu mdogo. Tulikuwa wawili tu, mimi na yeye. Tukakubaliana kuitumia siku hiyo kufanya kila kitakachoichosha na kuifurahisha miili yetu. Siku ile niliufaidi utamu wa mrembo yule kwa awamu ya pili, kila alichokifanya kiliukonga moyo wangu. Alipokea kwa ukarimu kile nilichompa, akashukuru kwa sauti yake tamu. Kisha akanitunuku kile alichojaaliwa na muumba wake.


ULIMWENGU MKUBWA

Kelele za ndelemo na vifijo zilipokoma, nilijua umefika wakati wangu. Wakati wa kufanya maamuzi ya maisha yangu. Nifanye uchaguzi wa aliye bora kwa maisha yangu yote. Nilikishikilia vizuri kipaza sauti, nikakipuliza kwa mbembwe, umati ukalipuka shangwe kubwa kuonesha utayali wa kuisikiliza sauti yangu ya sasa. Nilikohoa kidogo kusafisha koo langu, kisha nikaanza kuuhutubia ulimwengu mkubwa. Katikati ya miaka saba niliyoishi ndani ya ulimwengu mdogo, nimepitia mengi sana. Kila lililonipata limechangia kwa kiasi kikubwa kuniumba Mhanuzi mpya. Sasa umelejea utimamu wangu wa akili nikiwa ndani ya ulimwengu wenu mkubwa. Nimejifunza umuhimu wa kuishi vizuri na watu wanaonizunguka, umuhimu wa kujali na kuthamini hisia za wenzangu na umuhimu wa kuwa na watu upande wangu. Watakaonibeba wakati wa kuanguka, wanitie moyo wakati wa kukata tamaa. Watakaonifariji wakati wa misiba na wanizike nikifa na wawapokee wanangu, watakapowaendea kwa jina langu. Nimejifunza umuhimu wa uwepo wa Mungu ndani ya maisha yangu, anitiaye nguvu ya kuendelea na tumaini la kuyashinda magumu yote yanipatayo. Sijalikataa ombi lenu, nipo tayali kuchagua. Nitachagua kama mtakavyo, lakini naomba kwanza mnipe sababu za kutosha. Kwanini nichague hali ya kuwa kila mmoja alinifaa kwa wakati wake? Hamuoni kama kuchagua sasa ni kujitenga na msaada kwa siku zijazo?


ULIMWENGU MDOGO

Niliingia nyumbani kwa kuchelewa sana, nikawakuta wameketi sebuleni kwa utulivu; kila mmoja akijihangaisha na kile kilichoufurahisha moyo wake. Hawakuchukizwa na uchelewaji wangu kwa sababu walinijua vema. Niliwasalimu kwa heshima wakaniitikia, nikaongea busara iliyoeleweka na kila mmoja wao; wakaniachia faragha niliyoihitaji. Sasa nilisimama katikati ya sebule pana lenye uwazi wa kutosha, ulioniwezesha kuona kila kilichofanywa na wale walioyapambania maisha yangu. Mbele yangu nilimuona Eliza kitindamimba wa mzee Gelo. Yeye hakuwa mwingi wa maneno, bali vitendo; akiamini mkono mtupu haulambwi. Yuko bize kuweka bajeti ya matibabu yangu, akiwashawishi wazazi wake kutoa hela kuokoa maisha ya ampendaye. Akadiriki kutishia kutoa uhai wake kama hawatanihudumia mimi aliyenifanya kuwa mtalajiwa wake. Kulia kwangu amekaa Nesi wangu nimuitaye Pendo. Yupo makini kufatilia maendeleo ya afya yangu, akinihudumia kwa kila kitu kiasi cha kuutoa utu wake kwa ajili yangu. Anaimani na mimi, anapambana juu chini kuuweka sawa mwili na roho yangu, kisha ananionjesha utamu alionitunzia kwa wakati wote. Alinikaribisha kwake tuishi wote kama tulivyozoea kuisha. Kushoto kwangu namuona Salome asali halisi wa moyo wangu. Huyu ndiye dereva wa hisia zangu, zao la jitihada za mikono yangu. Hakunijua, mimi ndiye nilijitambulisha kwake; akanipokea. Niliuiba moyo wake; nikaufundisha kunipenda mimi tu, kisha nikautelekeza; akaumia sana. Baadae nilipourudia kwa nguvu, hakunikatalia. Aliurudisha kwangu kwa matumaini makubwa sana. Sasa yupo ndani, anasubiria kwa hamu jibu langu kama nitamtelekeza tena ama nitamkubali kama nilivyoahidi.
​
MWISHO​

**********************************************************************************************************************

KIPOFU MIMI

Hakika mimi sijui, Fungu jema kuchagua,
Uzuri siutambui, Ubaya kuung’amua,
Naepusha uadui, Kesho wakanibagua,
Penye mbili sichagui, mwisho zikaniumbua,


Hili laja hili lenda, Nashindwa lipi kupenda,
Saba nane au kenda, Nakosa lipi kutenda,
Uwe mchicha mlenda, Vinanitoa udenda,
Kuna kizuri kibaya, Kuna kibaya kizuri.​
 
JIONI YA JANA ILITAMATIKA SIMULIZI YA "SINA CHAGUO"
Kwa wale mliokuwa waoga wa kusoma mikihofia haitokamilika, basi njooni muanze sasa.@Benoit

Hongereni na ahsanteni sana kwa wote tuliokuwa pamoja kwa namna moja ama nyingine: hasa like, comments zenu.
@Shamuse_bey,
Matunzo 02,
mhanuzi wangu

babukijana​

Geranimo E K I A
realMamy@Psalm 103@realMamy@Mzigua_255

Mzigua_255[/HEADING][/HEADING]
[HEADING=3][HEADING=3]@Baba mtakatifu91 [/HEADING][/HEADING]
[HEADING=3][HEADING=3]@Sikio la muazini [/HEADING][/HEADING]
[HEADING=3][HEADING=3]@ephen
​

Mnachihanguuu​

Andromeda Galaxy​

Na wenginewe.🙏🙏🙏

Najivunia ninyi kwasababu UANDISHI Ndiyo Shauku, Uraibu, Hulka na kipaji changu ndiyo maana huwa nafurahishwa sana na maoni ya kila mdau juu ya kazi ya mikono yangu. Yawe hasi ama chanya, yote huniridhisha kwasababu yanao mchango wa moja kwa moja kwangu, na siku moja itakubali ile niitakayo.

Mwisho wa Simulizi hii unaanzisha mwanzo wa simulizi nyingine mpya iendayo kwa jina la, "MKASA WA JIRANI."
Simulizi hii itaanza Mwishoni mwa wiki hii. ✍️✍️✍️
 
Tupo nyuma yako mkuu unautunzi mzuri mwisho unafikilisha sana ukianza simulizi mpya nitag
 
JIONI YA JANA ILITAMATIKA SIMULIZI YA "SINA CHAGUO"
Kwa wale mliokuwa waoga wa kusoma mikihofia haitokamilika, basi njooni muanze sasa.@Benoit

Hongereni na ahsanteni sana kwa wote tuliokuwa pamoja kwa namna moja ama nyingine: hasa like, comments zenu.
@Shamuse_bey,
Matunzo 02,
mhanuzi wangu

babukijana​

Geranimo E K I A
realMamy@Psalm 103@realMamy@Mzigua_255

Mzigua_255[/HEADING][/HEADING][/HEADING]
[HEADING=3][HEADING=3][HEADING=3]@Baba mtakatifu91 [/HEADING][/HEADING][/HEADING]
[HEADING=3][HEADING=3][HEADING=3]@Sikio la muazini [/HEADING][/HEADING][/HEADING]
[HEADING=3][HEADING=3][HEADING=3]@ephen
​

Mnachihanguuu​

Andromeda Galaxy​

Na wenginewe.🙏🙏🙏

Najivunia ninyi kwasababu UANDISHI Ndiyo Shauku, Uraibu, Hulka na kipaji changu ndiyo maana huwa nafurahishwa sana na maoni ya kila mdau juu ya kazi ya mikono yangu. Yawe hasi ama chanya, yote huniridhisha kwasababu yanao mchango wa moja kwa moja kwangu, na siku moja itakubali ile niitakayo.

Mwisho wa Simulizi hii unaanzisha mwanzo wa simulizi nyingine mpya iendayo kwa jina la, "MKASA WA JIRANI."
Simulizi hii itaanza Mwishoni mwa wiki hii. ✍️✍️✍️
Safi sana Mkuu hapa umemaliza salama kabisa.
Tunasubiri next 👊
 
"...Nilifanya hivyo kwa kitambo kidogo mpaka nikaanza kuchoshwa na kitendo kile cha kujitia uchizi na kuigiza utoto wa kubembeleza mtu mzima. Wakati nikielekea kuchoka ndipo niliyaona matunda ya kazi niliyoifanya, nililishuhudia tabasamu pana lilichanua usoni mwake. Nikamwangali kwa kina mpaka alipoanza kutoa kicheko chake cha chinichini kilichoambatana na machozi. Hakuwa amabadilika hata kidogo, ni yule yule nesi wangu, Pendo kiboko ya tabia yangu wa kutokujali hisia za wengine. Alinirukia, akanikumbatia kwa nguvu. Kile kicheko chake kikakoma, sasa akailejea ile sura yake ya kuvutia. Tulitazamana kwa kitambo kidogo kisha tukaulejea ulimwengu mdogo. Tulikuwa wawili tu, mimi na yeye. Tukakubaliana kuitumia siku hiyo kufanya kila kitakachoichosha na kuifurahisha miili yetu..."

Hongera sana @JJ FORMAR
Nimeipenda sana Hii Simulizi, sema umezingua sana kuimalizia sehemu nzuri.
Huu mchezo ulitakiwa uendelee mpaka niuelewe vizuri, 🤣😂😂🤣🤣🤣😂
 
Hapa fasihi andishi imelala, nimeona mtindo changamano au rukia kwenye simulizi yako, hongera sana mtunzi kwa urumbi wa lugha, hapo tunasema kufaulu kwa mwandishi umeiachia hadhira ihitimishe, Mimi binafsi ningependa kijana umuoe Eliza maana kajitoa kuwashawishi wazazi wake wagharamie matibabu yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom