Simulizi yangu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi

1;> weka/chomeka flash yako kwenye kifaa unachotumia eidha kompyuta,laptop
2;> Fungua hiyo story yako
3;> Highlight story yako yote au kipande unachotaka kutuma.
4;> Fungua empty page kwenye window yako na upaste icho kipande cha story
5;> Hifadhi/save icho kipande kwa jina utalokumbuka.
6;> Chukua USB cable ile waya ya kuchajia simu chomeka kwenye simu yako.
7;> Hamisha kipande cha story yako uliyoipa jina hapo 5 kisha kitume kwenye simu yako kama unavotuma nyimbo au video.
8;> Fungua jf kwenye simu yako tafuta icho kipande ukipaste hapa.

Kama unatumia komputa kuingia JF ndio rahisi zaidi fuata hatua mpaka ya 4 halafu fungua jf na upaste story yako hapa.

Simpo laiki dhati
 
Waungwana habari ya leo fuatana nami kwenye simulizi yangu hii ambapo niliwahi kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi baada ya kukutana na changamoto mbalimbali za kimaisha.

Kiukweli ni vigumu kumjua yupi ni mganga wa kweli na yupi ni mganga feki ni kama vile ambavyo huwezi kumjua yupi ni mtumishi wa Mungu wa ukweli na yupi ni feki.Hali hiyo ilinifanya nihangaike kwa waganga mbalimbali ili kutatua changamoto zangu.

Wale ndugu zangu Walokole na Watakatifu wengine msiokuwa na dhambi mtanisamehe kwa hii simulizi.

Baada ya kumaliza masomo mwaka 2008 niliamua kurudi nyumbani kwetu Chunya na kujiajiri,sikupenda kuajiriwa kwa sababu kwetu Chunya marafiki zangu ambao nilisoma nao shule ya Msingi walikuwa wameishia darasa la saba walikuwa na pesa kushinda wasomi waliokuwa wameajiriwa na Serikali.

Hao marafiki zangu walikuwa machimboni kwa kuchimba au kununua dhahabu.Na Mimi nikajikita kwenye kuchimba lakini kabla ya hapo wakati nilipokuwa nasoma nilipokuwa napata nafasi nilikuwa naenda mgodini,ilikuwa rahisi kwenda machimboni kwa sababu kulikuwa na watu wengi niliokuwa nafahamiana nao.

Baada ya kuanza rasmi kuchimba madini niligundua machimboni kumetawaliwa na ushirikina wa hali ya juu,ndipo na mimi nikaanza kwenda kwa waganga wa kienyeji na kama ilivyo ada ukienda Roma ishi kama Waroma.Safari yangu ya kwenda kwa waganga ilianza kama ifuatavyo:

Mganga wa Ziwa Rukwa
Sikumbuki jina la kijiji ila kilikuwa karibu na ziwa Rukwa,nilienda kupitia Tunduma, naikumbuka barabara ilikuwa ya vumbi, milima, mabonde, miamba na yenye kona nyingi kali nilienda kwa kutumia fuso. Kijiji kilikuwa na Wafugaji wa Kisukuma wengi waliokuwa na mifugo mingi pamoja na wenyeji waliokuwa wakulima hodari wa mpunga kwenye bonde la ziwa Rukwa.

Niliipenda sana lugha ya Wenyeji kwani walikuwa wanaongea kama wanaimba au wanavuta maneno ,aina yao ya uongeaji ilinivutia sana.

Nilifika asubuhi na kumuona mganga,mganga mzee wa zaidi ya miaka sitini alikuwa hana vitu vingi vya kumtambulisha kama ni mganga wa kienyeji, nilimueleza sababu ya kwenda kwake akafanya uganga wake akaniambi usiku wa saa nane tutaenda kumalizia kufanyia uganga wake ziwani kwani huko ndiko kwenye mizimu yake, kutoka kwake hadi ziwa Rukwa kwa miguu ni saa mbili kwahiyo tulitoka kwake saa sita usiku ili tuweze kufika ziwani saa nane.

Tulitoka kwake watu wanne yaani mimi, mganga na watu wengine wawili, tulifika ziwani saa nane kasoro wakati tunaenda ilikuwa rahisi kwa sababu ilikuwa tunashuka tu kasheshe ilikuwa wakati wa kurudi kwani tulikuwa tunapandisha milima, usiku ule nilichoka sana.

Tulivyofika kwenye ufukwe wa ziwa mganga alituambia tugeuge tuangalie tulikotoka kisha alivua nguo zote akasisitiza tusimuangalie,wakati yeye anafanya uganga wake huku anaonge ongea maneno ambayo sikuyajua maana yake sisi wote watatu tulikuwa tunangalia pembeni.

Baada ya muda kidogo kukawa kimya, baada ya kama dakika tano nikasikia naitwa kwa kutajwa jina, sauti ilikuwa kubwa na yenye muungurumo, muda huo sehemu ile ya ziwa tulikuwa watu wanne tu sauti ile iliendelea kuniita lakini mtu aliyekuwa ananiita nilikuwa simuoni ila ilikuwa sauti ya mganga.

Sauti ilinitaka nielekee usawa wa ziwa, mimi kuogelea sijui ila sauti ilikuwa inanitaka niingie ziwani,wale jamaa wakaniambia kwa ukali niingie ziwani maana nilikuwa natembea kwa kusita sita, nilifika ziwani nikaingia kwenye maji nikawa naendelea kutembea kwenye maji kwa kusita sita sikuwa namuona mganga ila sauti nilikuwa naisikia ikiniambia niendelee kumfuta.

Niliendelea kutembea maji yalivyofika usawa wa magoti sauti ikanitaka nisimame nisiendelee kumfuata na mimi nikatii.
Itaendelea.

Sasa hivi najiandaa kwenda Mkwakwani kuwaona watani Yanga dhidi ya Coastal kwenye mechi yao itakayo chezwa saa kumi leo,nawatakia sare tu.

Nielekezeni jinsi ya kuipost hapa maana niliiandika yote imekamilika na ipo kwenye flash.
m
 
Story za vipande vipande hivi nikipita Kama hapa sirudi tena
 
Daraja la miti
Kama upo kweli Mkwawani njoo upande wa jukwaa kuu kulia, tafuta mtu aliyevaa t-shirt ya njano isiyo na maandishi na nimevaa kofia nyeupe, pembeni yangu yupo mwanamsimbazi na jezi yake.

Kama una smartphone nina OTG hapa nitakuwekea story yote kupitia simu yako alafu utapost mwenyewe.
 
Nimekuona
 
Upuuzi
 
1;> weka/chomeka flash yako kwenye kifaa unachotumia eidha kompyuta,laptop
2;> Fungua hiyo story yako
3;> Highlight story yako yote au kipande unachotaka kutuma.
4;> Fungua empty page kwenye window yako na upaste icho kipande cha story
5;> Hifadhi/save icho kipande kwa jina utalokumbuka.
6;> Chukua USB cable ile waya ya kuchajia simu chomeka kwenye simu yako.
7;> Hamisha kipande cha story yako uliyoipa jina hapo 5 kisha kitume kwenye simu yako kama unavotuma nyimbo au video.
8;> Fungua jf kwenye simu yako tafuta icho kipande ukipaste hapa.

Kama unatumia komputa kuingia JF ndio rahisi zaidi fuata hatua mpaka ya 4 halafu fungua jf na upaste story yako hapa.

Simpo laiki dhati
Hatua zoote hizo kwan akileta story yake humu mtamlipa?,jf pekee ndo watu hupanga maisha ya watu wengne
 
Back
Top Bottom