Waganga wa kienyeji walivyovunja undugu kwenye ukoo wetu

plus_ix

JF-Expert Member
Jul 10, 2022
559
1,387
Habarini wana JF natumaini tumeanza mwaka vyema kabisa

Bila kupoteza wakatai nataka niwaletee hiki kisa ambacho tumeishi nacho tukiwa wadogo mpaka hivi sasa tumekuwa tunazidi kueelewa ilikuwaje maana wakati wadogo tulikuwa hatuambiwi chochote.

Iko hivi familia ya mzee wangu walizaliwa watoto wa tano kutoka kwa mke mkubwa maana babu alikuwa na wake watatu na familia tatu ila izo nyingine sitozizungumzia ntaongelea familia ya mzee wangu baba ni mtoto wa kwanza kwenye hii familia anafatiwa na dada ake ambaye ni shangazi yetu pia na wadogo zake wawili huyu mdogo wake watatu ambaye ni bamdogo wangu ndo chanzo cha mkasa mzima japo yeye hahusiki moja kwa moja.

Ilianza bamdogo alipo taka kuoa ni mwanzoni mwa miaka ya 2000s familia ilikuw imemchagulia mke sasa yeye akumpenda yule mke akawaelekeza wazee wake wakamueelewa akasema tayari anamchumba wake ambaye yuko kijiji jirani basi mdaa ulipo fika alienda kumchukua na kumtambulisha kwa wazee kwamba huyu ndio mke wake siku tu ya kwanza mke wa bamdogo kufika vilizaliwa visirani na shangazi awakutokea kupendana kabisa ukiskia ugomvi wa mawifi sasa huyu mke wa bamdogo ambaye ni mamdogo wangu alikuwa mpweke sana maaana alionekana sio chaguo la familia kwa sababu kijiji anachotoka kinasifika kwa uchawi basi ikalazimika bamdogo haame kipindi iki mzee alikuwa anafanya biashara zake mkoa mwingine ko ikabidi amchukue bamdogo na mke wake wakae nae huku akimfundisha biashara maisha ya kaeendelea kawaida kabisa huku shangazi akigoma kuja kututembelea kwa sababu ya mamdogo akidai ni mwanga baada ya kipindi kifupi bamdogo aka master biashara na kuanza kujitegemea na kuondoka kwa mzee (kaka yake).

Basi visanga vilianza rasmi baada ya mamdogo kutopata mtoto na kila mimba aliyokuwa anashika inatoka/kuaribika aisee hili lilikuw tatizo kubwa mnoo kweny hukoo ki ujumla kwa upande wa familia ya mzee shangazi ndo alikuwa mkali akidai huyu mwanamke hafai ana mikosi na rahana za ukoo wao niliwaambia toka mwanzo amkutaka kunieelewa, amna jambo baya kuonekana hufai na unazidi kuthibitisha hufai bamdogo alihisi kuvurugwa lakini alishikilia msimamo wake na akumkatia tamaa mke wake bamdogo hiki kipindi alikuwa mtu wa mawazo sana alipoteza nuru alikonda ka mgonjwa kwa upande wa ma mdogo ndugu zake walimwambia amerogwa inabidi aende kwa mganga na akapewa maelekezo huku akirini mwake akiamini hivi vyote ni visa vya shangazi kwa kuwa hamtaki.

Mamdogo alinambia kwa uchungu sana huku akinambia mwanangu nimetafuta sana mtoto
Basi baada ya kupewa maeelekezo na ndugu zake mamdogo ilibid arudi kwao kwajiri ya kufanyiwa utalamu na mganga wa jadi ambaye anaaminika.

Mamdogo alieenda kwao na alikaa zaidi ya mwezi mmoja na akiwa anapewa dawa na huyo mganga na kufanyiwa matambiko ya ukoo wao alirud akiwa kakondaa sana hiki kipindi bamdogo na mzee ndo walieenda kumchukua alirudi na chale nyingi sana mgongoni kwa kifuani sehemu ya juu kidigo ya maziwa na sehemu nyingine huku akisema mganga kamwambia aliye mroga ila hatakiwi kusema kwa mtu yoyote ili jambo lilileta shida kidogo kwa kuwa wanafamilia walitaka kujua ukweli wote hapa ndo chuki zilizidi baada ya babu kujua mkwe wake kaeend kwa mganga.

Basi miezi kadhaa ikapita mamdogo alifanikiwa kushika mimba na miezi tisa ikapita hatimaye alijifungua mtoto wa kiume lakini mtoto alizaliwa na matatizo walivyodai wao akuwa baraka bali maumivu kipindi hiki nilimuona mtoto nilikuw mdogo pia ila nilimzid miaka kadha mtoto alizaliwa na ulemavu alikuwa awez kukaa wala kutambaa ni kulala tu hata mdaa wakufanya ivyo ulivyofika ilikuw shida sana furaha ya mamdogo kupata mtoto ilianza kupotea kabisa walitafuta njia mbali mbali za kumsaidia mtoto zilishindikana na mwisho wakarudi kwq waganga wa kienyeji..
 
Dah kisa cha kuhuzunisha na kusikitisha sana kwakweli
Ila waganga sio watu wazuri maana kuna muda wanaweza kua sababu ya matatizo familiani
Ila hapo kwa mtoto wakulala tu imenigusa zaidi sababu nipo na same mtoto wakulala tu asee kila kitu afanyiwe changamoto kubwa sana kwakweli ila watoto wote wanahitajia upendo ila wakiwa na matatizo kama hawa wanahitajia upendo zaidi nakushikamana kwa familia wazazi ndugu na jamaa kwa pamoja laa sivyo wanasimanzika sana kwahakika ila ndio kazi ya Mungu
Nilichogundua huyo mke wakaka ako hakupendwa na wifi zake hizo nyengine zimekuja kama sababu naunajua ukitaka kumuua umbwa mpe kwanza jina baya ili upate uhalali wakumtwanga
Hizo chuki ubaya wake hua zinaendelea vizazi na vizazi kutoka tena inawezekana ila ngumu sana sana sanaa
 
Baada ya kurudi kwa waganga wakienyeji walipewa dawq ya kila aina mamdogo ananisumulia qalipewa masharti magumu ambayo kuna mdaa walitakiwa wamuogeshe mtoto na dawa saa tisa usiku kwa jitihada nyingi walizo zifanyazilionekana ni kazi buru baada ya mtoto kufariki mamdogo alilia sana hiki kipindi nilimshuhudia na shangazi alivyofika kusalimia msiba alionekana yeye ndiyo mkosaji na msababishi wa matatizo yote haya mamdogo alilopoka kwa uchungu akimwambia shangazi wewe ndo umeniulia mwanangu staki kukuona hapa kimbembe kikarudi kutafuta mtoto kwa mara nyingine hapa mamdogo na bamdogo walifunga safari kwenda kwa mganga kwenye vijiji vya uko sumbawanga na huyu mganga alikuwa mtalamu kweli kweli kwa maelezo ya mamdogo alisema walivyofika mganga aliwataka waoge kwanza na aliwapa chumba cha kulala ilikuw majira ya saa tatu usiku hadi walivyofanya ivo mganga akawaambia shida yenu naijua nimeiona amna haja ya kunieeleza chochote pumzikeni nitawaamsha walipuumzika ilivyofika saa 9 usiku mganga aliwaamsha akawapeleka kwenye chumba kilichopo nyuma ya nyumba ilikuw ni chumba cha nyasi ambacho kina mlango wa kitamba cheusi na mle ndani kulikuwa na vigoda vinne na chungu kilikuw katikati mganga akasema naeenda kukuonyesha mchawi wako na jinsi alivyokuroga mganga alichanganya dawa zake nakutupia kwenye chungu na kumwambia mamdogo fumba macho usifumbue ata ukiona kitu cha kutisha mamdogo ananisimulia alimuona shangazi akimwekea dawa kweny maji ya kuoga na kusemea maneno na pia aliweka dawa nyingine chini ya godoro alilo lala mwisho mamdogo aliamini kuwa shangazi ndio mchawi wake na mganga aliwaambia warudi baada ya siku kadhaa awape dawa mamdogo akutaka kusikia lolote kuhusu shangazi alipelekea chuki kuzaliwa pia kwa babamdogo kwenda kwa dada yake na kuleta ugomvi wa kifamilia kwa mzee hakutaka kusimama na yoyote kwenye hili yeye akushiliki ata kutoa ushauri vita ilikuw kubwa sana ukoo ulilazimishwa kuamini mamdogo karogwa na shangazi licha yakukosa ushahidi mkubwa nakumbuka nilipewa onyo na babmdogo kuwa sitakiwi kwenda kwa shangazi na chochote atakachokupa usipokee basi tukiwa wadogo tulishindwq kua na majibu yq uhakika na kufanya yale tuliyoambiwa tukiaminishwa shangazi ni mchawi siku zilizidi kwenda na mamdogo alipewa dawa lakini amna kilichotokea bado alieendelea kutafuta mtoto mganga huyu akuwa suruhisho bali chanzo cha vita kwenye ukoo watoto washabgazi hatukurusiwq kucheza nao japo tulikuw tunacheza pamoja kwa uwizi mwisho mamdogo baada ya miaka kadhaa alijifungua mtoto wa kiume salama kabisa na mbaka sasa ana watoto wanne ambao kajifungua salama kabisa ila bado vita yake na shangazi haijaisha mbaka leo watoto washangazi awaruhusiwi kwenda kwa mamdogo na watoto wa mamdogo ivo ivo.
 
Dah kisa cha kuhuzunisha na kusikitisha sana kwakweli
Ila waganga sio watu wazuri maana kuna muda wanaweza kua sababu ya matatizo familiani
Ila hapo kwa mtoto wakulala tu imenigusa zaidi sababu nipo na same mtoto wakulala tu asee kila kitu afanyiwe changamoto kubwa sana kwakweli ila watoto wote wanahitajia upendo ila wakiwa na matatizo kama hawa wanahitajia upendo zaidi nakushikamana kwa familia wazazi ndugu na jamaa kwa pamoja laa sivyo wanasimanzika sana kwahakika ila ndio kazi ya Mungu
Nilichogundua huyo mke wakaka ako hakupendwa na wifi zake hizo nyengine zimekuja kama sababu naunajua ukitaka kumuua umbwa mpe kwanza jina baya ili upate uhalali wakumtwanga
Hizo chuki ubaya wake hua zinaendelea vizazi na vizazi kutoka tena inawezekana ila ngumu sana sana sanaa
Kweli kabisa na pole kwa changamoto na mwanao naamini mambo yata kaa saw
 
Kama ni ukweli kuna uchawi wacha ukoo usambaratike tu hakuna jinsi.

Inafaida gani kuzani ni ndugu kumbe ni mtesi?

Mtesi ni zaidi ya adui.

Adui akiwa ndugu wa karibu anakuwa mbaya zaidi sababu anaweza ku Access vitu vyote muhimu vya kukufunga ukafungika au kukuua, kuharibu ndoa, kufunga watu wasizae, watoto Shule wawe wasindikizaji, kuharibu kazi n.k.
 
Kama ni ukweli kuna uchawi wacha ukoo usambaratike tu hakuna jinsi.

Inafaida gani kuzani ni ndugu kumbe ni mtesi?

Mtesi ni zaidi ya adui.

Adui akiwa ndugu wa karibu anakuwa mbaya zaidi sababu anaweza ku Access vitu vyote muhimu vya kukufunga ukafungika au kukuua, kuharibu ndoa, kufunga watu wasizae, watoto Shule wawe wasindikizaji, kuharibu kazi n.k.

Unajuaje kama ndugu ni mchawi ?

Diagnosis ya uchawi inafanywa na mashine gani ? Ama kipimo gani ?
 
Kwanza fahamu kuwa kumfahamu adui yako na mtesi ni hatua moja nzuri sana.

Tena ukijua shukuru Mwenyezi Mungu maana itakupa kuishi nao kwa tahadhari ya hali ya juu na kujiwekea mipaka.

Mwenyezi Mungu akikubainishia adui na Watesi ujue anakupenda sana na kama unapitia mitihani mizigo jua unaenda kushinda muda si mrefu .
 
Natamani ungemuuliza Shangazi yako kuhusu tuhuma dhidi yake ili ku balance story..
 
Natamani ungemuuliza Shangazi yako kuhusu tuhuma dhidi yake ili ku balance story..



Chances kubwa atakataa kuwa mchawi.

Isipokuwa ni vizuri amuulize ktk majadiliano kuna namna atajichanganya mahala kisha atajua tu kuwa ni Mchawi au sio.

Nazani huwa wanaambiana kuwa kuhisiwa ukiulizwa kataa.

Actually ni tabia ya mtuhumiwa kukataa kufanya kosa kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa jinai.

Kwa hiyo hata akikataa haitoshi kumwamini.

Wanaogopa kukubali shauri wanaogopa kuuwawa maana Mchawi ni zaidi ya jambazi.

Ni mtu ambae Mwenyezi Mungu ameruhusu auwawe hasa akiwa mwanamke.
 
Kuna Mchawi ndugu wa mama Mdogo kwa mkubwa alistukiwa alipoulizwa akakataa,
Alokuwa anamhoji yuko makini sana akitaka kutoka kwenye mstari anamrejesha mwisho akasema labda alivyokuwa Mdogo ndipo alimroga na mama yake mzazi .

Imagine

Akamwambia Sasa ukitaka nikusitiri na nisikukate mapanga wala bastora nenda kaninasue, nenda kanifungue nakupa muda mfupi sana la sivyo ama żako nimechoka mateso ya miaka mingi.

Akaanza kumwelekeza kwa watu 3 akaaguliwe.
 
Muhimu ukimhoji usiwe kwenye panic mode.

Uwe na utulivu.

Uwe rohoni.

Mwambie nimejiridhisha vya kutosha kila ninapoenda kwa manabii, waganga, kwenye maono hata nimekaa nakukamata wewe tu , Kwanini isiwe watu wengine?

Lakini iwe ni kweli usemayo.
 
Kama ni ukweli kuna uchawi wacha ukoo usambaratike tu hakuna jinsi.

Inafaida gani kuzani ni ndugu kumbe ni mtesi?

Mtesi ni zaidi ya adui.

Adui akiwa ndugu wa karibu anakuwa mbaya zaidi sababu anaweza ku Access vitu vyote muhimu vya kukufunga ukafungika au kukuua, kuharibu ndoa, kufunga watu wasizae, watoto Shule wawe wasindikizaji, kuharibu kazi n.k.
Uchawi unathibitishwa na mchawi?
 
Back
Top Bottom