Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Sehemu ya 92

Siku moja jioni baada ya kutoka matembezini, niliporudi nyumbani, wakati nafika getini nilimkuta Lawalawa akinongoja kwa shauku.

“Kuna ugeni. Ugeni wa wasiwasi.” Lawalawa aliniambia.
“Ugeni gani huo wa wasiwasi?”
“We’ ingia ndani uone.”

Nilipita ndani, Lawalawa akanifuata kwa nyuma. Nilipofika koridoni. Nilishituka sana kwa watu nilokuwa wamekaa kwenye viti mbele yangu.

Alikuwa ni mke wangu Pili na mwingine alikuwa ni mzee mwenye baraghashia kichwani. Baada ya wao kuniona, Kila mmoja alishituka.

Nilitembea kuwafauta. “Karibuni jamani,” niliwakaribisha, ingawa sikujua kule kuwakaribisha kama kulitoka moyoni ama nilijisemea tu ili mradi.

Mpenzi wangu Lawalawa aliniletea kiti na kuketi mbele yao. Yeye alisimama kando kusikiliza mazungumzo yetu.

“Pili hujambo?”
“Sijambo, ”alinijibu bila kuniangalia usoni.
“Mzee shikamoo.” “Marhabaa!. Bila shaka wewe ndiye Ajibu?”

“Naam! mimi ndiye,”nilimjibu mzee yule aliyeonekana kujawa na shari usoni mwake. “Nimekungoja kwa muda mrefu hapa, naomba tuongee pembeni ili niondoke zangu.” Alisema yule mzee.

“Kwani hampo wote pamoja?” nilimuliza, nikimaanisha kwamba ujio wao hakuwa wa pamoja na mke wangu Pili. Ujio wenye ajenda ya pamoja. “Hata!...” mzee yule alinijibu. Uso wake uliendelea kuonyesha hakuhitaji maswali zaidi ya kunieleza kilichomleta.

Akaendelea kuniambia:
“Huyu bibi amenikuta, ndio maana nakwambia nimefika hapa muda mrefu, hebu nakuomba kijana, tuongee kando ili niwahi kuondoka, mimi mgeni hapa Tabora ujue.”

Alaa!!... Kweli huu ni ugeni wa wasiwasi, huyu mzee anatokea wapi? ana shida gani na mimi? Amejuaje kwamba mimi naishi kwenye mji huu? Nilijiuliza bila majibu.

Nilisimama tukasogea hatua chache.
“Nakusikiliza mzee.” Nilisema. “Naitwa mzee Mwakanjara Kisu ni babu yake na Felix Kisu....”

Alipojitambulisha tu hivyo tumbo likapata joto, kimoyomoyo nikasema kumekucha. Akaendelea.

“Nimekuja hapa kutaka jambo moja tu baba, sio kukuomba, laah! Kutaka.” Alisema, akaweka kituo huku akiniangalia usoni kwa makini sana.

“Nimekuja kutaka ukafukue uchawi ulifukia makaburini ili mwanangu awe huru na maradhi uliyomtupia, vinginevyo nakupa siku tatu kisha utaona. Umesikia?”
 
Sehemu ya 93

Yalikuwa ni maneno yaliyonifanya nihisi kizunguzungu. Nilibaki kimya huku nikikosa jibu la kumpa mzee huyo. Nilikuwa nimenywea, nimenyauka kama ua lililokosa maji nyikani.

“Umenialewa vizuri Ajibu?” aliniuliza.
“Umekuja kunitisha mzee?”
“Oooh!. Mimi naondoka, sintarudi tena hapa kama usipofuata matakwa yangu, utakayenitafuta ni wewe, kwaheri.” Alisema na kuondoka.

Nilibaki nimesimama nikimwangalia mzee huyo akitokomea gizani na kuishia zake.
Lawalawa alinijia pale nilipokuwa nimesimama na kuniuliza:
“Alikuwa anataka nini yule?”

“Sijui kakosea njia, simwelewi.”
“Yule mzee mwanga Ajibu, alifika hapa tangu mchana, dada wa kazi alimwona akitoa midawa fulani hivi akaimwaga uwani” Lawalawa alisema akionekana kuwa na wasiwasi sana.

Kwakweli maneno hayo yalizidi kunitisha. Kwa mwonekano mzee yule aliononeka alikuwa ‘konki’ kwenye mambo ya ulozi, ningewezea wapi mimi kupambana naye.
Niliogopa sana, hata hivyo nilificha hofu yangu mbele ya Lawalawa.

“Usijali, mpenzi kuwa na amani.” “Na yule mwanamke ni nani Ajibu?” Lawalawa aliniuliza tena, akimanisha mke wangu Pili.

“Yule ndiye mwanamke niliyekwambia siku zile.”
“Amekuja kufuata nini?”Lawalawa alizidi kuhoji. Uso wake ulianza kutengeneza wivu.

“Kama nilivyokwambia Lawalawa, huyo ni yule aliyekuwa mwanamke wangu, nilimwacha bila sababu nikaja kwako.

Nadhani ujio wake itakuwa kaja kulalamika na kunililia hapa. Ngoja nikamsikilize,” nilisema. Tukasogea kwenda kumsiliza mke wangu Pili.
Nilipofika nikaketi kwenye kiti. “Pili nambie, umejuaje naishi hapa.”

“Ajibu, hilo sio la msingi, lililo la msingi ni pesa ya mkopo uliyonidanganya nikupe ukaja kutumbua na hawala wako huku, nataka pesa ya watu.” Alisema. Uso wake ulijaa shali.

“Pesa gani?” Lawalawa akadakia.
Nikamsimulia kwa kifupi Lawalawa, wakati namweleza mke wangu Pili alikuwa akitokwa na machozi. “Kwa hiyo anadai shilingi laki tatu tu?” Lawalawa aliuliza kwa kiburi.

“Ndio.” “Nitampa laki nne kesho asubuhi, kuna jingine?”
“Eti Pili kuna jingine?” nikalisindikaza swali lile kwa mke wangu Pili.
 
Mambo yote muhimu alikuwa akisimamia mpenzi wangu huyo. Naweza kusema kipindi chote, nilikuwa ‘mario’ niliyeshindikana


😂😂😂😂😂 huko tuendako lazima balaa limpate
 
Mambo yote muhimu alikuwa akisimamia mpenzi wangu huyo. Naweza kusema kipindi chote, nilikuwa ‘mario’ niliyeshindikana


huko tuendako lazima balaa limpate
tena balaa zito,.
alafu ukute pili atamsamehe tu
 
Sehemu ya 94

Masikini Pili, aliishia kutokwa na machozi.
MWANAMKE huyo alisimama na kuondoka. Huruma ilinishika lakini sikuwa na la kufanya, sikuwa tayari kuliacha penzi la Lawalawa.

Siku hiyo ilikuwa na nuksi. Na niliweka nadhiri ya kurudi kwa mganga wangu wa Unguja baada ya kumalizana kabisa na mke wangu, Pili. Kitu nilichokiona bado ni kikwazo kwenye maisha yangu ni wale jamaa zake na Felix Kisu.

Asubuhi ya siku ya pili ilifika kwa kishindo. Mke wangu Pili, aliwasili nyumbani pale nilipokuwa nikishi na mpenzi wangu, alifika mapema sana. Alikuta bado mimi na mpenzi wangu Lawalawa tumelala.

Alikaribishwa kiti nje akingojea tuamke ili apewe pesa ambazo alizikopa kwenye vikoba akanipatia mpumbavu mimi nikazitumia kumtafuta mpenzi wangu Lawalawa ambaye nilikuwa nimepotezana naye kitambo.

Tulipoamka nusu saa badaye, tulimkuta mwanamke huyo anatungoja. Uso wake ulionekana kuwa na maumivu makali ya nafsi.

Alichokifanya mpenzi wangu Lawalawa, alimtumia pesa yake yote katika simu.
“Haya dada unaweza kuondoka, pesa zako ushalipwa,” Lawalawa alimfukuza Pili.

Pili alipandisha kamasi, akapangusa machozi mashavuni mwake. “Ajibu.” Aliniita, nilimwangalia usoni, macho makavu bila haya. “Sitakulaumu kwa hiki ulichonifanyia maishani, nashukuru angalau umenifundisha kuwa makini na machaguzi yangu katika maisha,” alisema.

Sikuzingatia maneno yake, wala sikuelewa alikuwa na maana gani. Aliondoka akiniacha nikiendelea na maisha yangu na Lawalawa wangu.

Kuanzia siku hiyo sikujua lolote kuhusu mke wangu. Sikujua kama alirudi Kigoma kuendelea na maisha yake, ama alikwenda nyumbani huko Maji moto mkoani Mara. Sikuvutika kujua kwa sababu sikumpenda.

Na kuhusu yule babu yake Felix Kisu, aliyenijia akinitaka nikafukue uchawi niliouzika kiasi cha kumfanya mjukuu wake kuteseka, naye sikujua habari zake. Sikujua habari zake kwasababu hapakuwa na lolote baya kama ambavyo alivyoniahidi.

Siku zilikwenda miezi ikakatika maisha yangu na Lawalawa yakizidi kuwa matamu, naye hakuwa na habari na watoto wake, achilia mbali mume wake. Akili yake yote ilikuwa kwangu.
“Unaonaje tukifunga ndoa?” nilimuuliza Lawalawa.

“Hata mimi nilikuwa na wazo hilo.”
“Sasa tunasuburi nini?”
 
Sehemu ya 95

“Acha nimshirikishe baba, unajua ndio mzazi niliyembakiza.”
“Baba yako hapendi kabisa uhusiano wetu, atakubali?”

“Hana jinsi, lazima akubaliane na ninachotaka.”
“Sawa. Utamwambia lini?”
“Leo hii hii.”

Siku hiyo Lawalawa alimwambia baba yake juu ya wazo hilo. Usiku ulipotimu, akanipa mrejesho juu ya maamuzi ya mzee wake huyo.

“Baba amegoma,” Alisema.
“nilijua tu. Kwa nini amegoma?”
“Hana sababu za msingi, anasema bado anamtambua mume wangu wa Yemen na siyo wewe.”
“Kwa hiyo?”
“Sijui nifanye nini.”

Tuliendelea kuishi kama wapenzi bila kujua hatma yetu ni nini. Pamoja na kugomewa kuoana mimi na Lawalawa, maisha yetu yaliendelea kuwa ya furaha siku zote, tukiishi kama wapenzi nilinenepeana nyumbani kwao Lawalawa.

Waswahili husema: Mwenda tezi na omo siku zote marejeo huwa ni ngamani. Katika nyakati hizo za raha na furaha, ghafla mambo yalibadilika. Mambo yalianza kubadilika kimzaha mzaha.

Ilikuwa kama mchezo wa kugiza.
Ni siku moja jioni, walikuja nyumbani watu wawili waliovalia kanzu na baraghashia, kwa kuwaangalia walikuwa ni kama mashekh.

Lawalawa aliniambia watu hao walikuja kufamfanyia dua baba yake ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali.

Wale watu waliingia ndani sebuleni. Mwenyeji wao akiwa ni baba yake Lawalawa ambaye alikuwa mzee sana. Ambaye tangu mwanzo nilisema hakuwa akinipenda hata kidogo.

Walimtaka Lawalawa awepo mahali pale wakati dua maalumu kwa ajili yake ikiwa inaendelea.

Lawalawa alijifunika khanga akasogea karibu. Mimi nilibakia nje. Nilitengwa. Huko ndani ubani ukachomwa kisha dua ikaanza kusomwa na wale mabwana wawili.

Dua ilisomwa kwa lugha ya Kiarabu kwa zaidi ya lisaa lizima. Kama nilivyosema, wakati wote mimi nilikuwa nje, sikujua kilichokuwa kikiendelea subuleni hapo.

Wale mabwana wawili walipondoka, nilikwenda ndani, nilipoingia sebuleni, sikumkuta Lawalawa, alikwepo baba yake ambaye aliniangalia kwa jicho baya.
Nilipitiliza hadi chumbani, nikamkuta mwanamke huyo amelala.

“Vipi, unaumwa?” nilimuuliza.
“Nahisi kuchoka sana baada ya dua ya mashekh wale.”

Nilianza kuwa na wasiwasi. Isije ikawa wale mabwana walikuja pale kuondoa uchawi niliomfanyia mwanamke huyo ili asinipende tena.
 
Sehemu ya 96

Kwa kweli nilikuwa mwanaume mpumbavu sana.

Siku hiyo tulilala vizuri, ingawa mara kwa mara usiku nilikuwa nikijiwa na ndoto za ajabu ajabu. Asubuhi kulipokucha, nilikwenda bafuni kuoga tayari kwa kuendelea na shughuli zangu za kila siku.

Wakati natoka bafuni, ile namaliza kushuka ngazi za bafuni, nikasikia sauti nzito ya mwanaume ikiniita ndani ya bafu, wakati nageuka kutizama, sijui nilikanyaga wapi, nikateleza na kupiga mweleka.

Nilianguka kidogo tu, ajabu nilipata maumivu makali sana ya kwenye goti, nilipotaka kusimama nikashindwa kabisa. mfupa wa mguu ulikuwa umevunjika.
Toba!!

****
Ni siku ya tatu nilikuwa nimelazwa kwenye hospitali ya Kitete ya mjini Tabora. Mguu wangu uliovunjika baada ya kuanguka bafuni ulikuwa umefungwa hogo.

Katika zile siku tatu zilikuwa ni siku za mateso makubwa, mguu ulikuwa unauma kana kwamba, kulikuwa na mtu anakwangua mfupa kwa kisu ndani kwa ndani.

Muda wote nilikuwa nalia kwa maumivu makali hadi madaktari wakashangaa.
“Itabidi afanyiwe kipimo cha X- ray upya, inawezekana kuna mahali kwenye mguu wake kuna tatizo.” Dokta aliamwambia Lawalawa aliyekuwa akiniuguza hospitalini hapo.

“Inawezekana kweli?”
“Kabisa.”
Mwanamke huyo hakuwa na tatizo, alilipia gharama za vipimo, muda mfupi badaye nikachukuliwa na kupelekwa maabara. Huko nikafanyiwa upya kipimo cha X- ray.

Majibu yalipotoka hayakutofautiana na yale ya awali, sehemu mfupa ulipovunjika ilikuwa ni palepale.

Sasa maumivu hayo yalitokana na nini?
Siku hiyo nililala nikiugulia maumivu makali. Pamoja na kuchomwa sindano za ganzi na maumivu, lakini wapi, niliendelea kuteseka usiku kucha.

Asubuhi ya siku ya pili, siku ya nne tangu nilazwe hospitali ya Kitete, tofauti na siku zingine hadi inatimu saa sita mchana, sikuwa nimemwona mpenzi wangu Lawalawa.

Kwa kuwa hapakuwa na mtu mwingine aliyekuwa akiniuguza zaidi ya Lawalawa, nilijikuta nakosa chakula. Kwa kudra zake Jalali. Kulikuwa na chakula cha msaada, siku hiyo kikanifaa. Hadi inatimu saa kumi jioni bado sikumwona Lawalawa.
 
Na mimi kam baharia wa nchi kavu niliezamia daslam ukubwan tena nikiwa na ndevu zangu ,,,hakuna mwanaume wa staili hii katika hii dunia (nieleweni mwanaume na sio mvulana au mwanamume).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom