Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
116,407
Points
2,000

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
116,407 2,000
Sehemu ya 97

Simu sikuwa nayo, niliacha nyumbani tangu siku nilipoanguka bafuni, hivyo sikuweza hata kumpigia kujua amepatwa na nini. Siku hiyo ilipita, siku ya pili ikaingia nayo ikapita, Lawalawa sikumuona.

Siku ya tatu ilipotimu, nilimwomba mtu mmoja simu ili nimpigie mwanamke huyo kujua amepatwa na nini kiasi cha kuniacha hospitalini peke yangu.

Simu ilita kwa muda mfupi, ikapokelewa.
“Nani mwenzangu?” sauti ya Lawalawa ilisikika. “Mimi Ajibu. Mbona umeniacha mwenyewe mpenzi umepatwa na nini?” nilimuliza.

“Tena afadhali umenipigia Ajibu...” alisema. Akaendelea.
“Baba amefariki.”aliongea mara moja na kunyamaza, aliacha kauli hiyo iniingie akilini.

“Mungu wangu. Baba amefariki...Lini amefariki? kwa sababu gani!!” niliongea nikiwa nimechanganyikiwa kwa habari hiyo ingawa ukweli kutoka ndani kabisa ya moyo wangu taarifa hiyo niliifurahia.
Mzee huyo alikuwa akiniwekea kauzibe ndoa yangu na Lawalawa.
“Leo ni siku ya pili, amezikwa leo hii hii.”
“Eeeh!” nilimaka.

“Pole sana mpenzi, kwa nini hukunijulisha Lawalawa.” “Nikujulishe wewe kama nani kwangu?” Toba!! Kauli hiyo ilinivuruga na kunifanya nitamani kulala japokuwa ukweli ni kwamba wakati naongea naye nilikuwa nimelala. Hadi leo sijui ile hamu ya kutamani kulala ililenga kulala vipi.

“Lawalawa unasema!”
“Nikujulishe habari ya kifo cha baba yangu wewe kama nani? Wewe ni mume wangu? Ni mchumba wangu? ni mzazi mwenzangu? Wewe ni nani hadi nikujuze kila jambo langu? Ni kaka yangu wewe?”
Nilihisi niko angani naelea huku nikikaribia kujipigiza ardhini, maneno hayo yalikuwa ni mwiba mkali mno moyoni mwangu.

“Umepatwa na nini Lawalawa....”
“Ti, ti, ti, ti.” Simu ilikatwa.
Afanaleki!! Mate mepesi yalinijaa kinywani, dunia ilikuwa inanielemea kitandani pale. Lawalawa kapatwa na nini?

Nilipiga simu yake kwa mara nyingine. Alipokea mara moja akaniambia:
“Nakutumia ‘sms’ subiri kidogo.”
Simu ikakatwa tena. Nilisubiri kama dakika tano kisha nikapokea ujumbe kutoka kwakwe:

“Upumbavu wote ulionifanyia maishani nimeujua, sitaki kusika lolote kuhusu wewe, ukijaribu kunitafuta ama kunisogelea, nitakuvunja mguu mwingine, natamani ufe Ajibu, huna sifa ya kuwa mwanaume, sikupendi nakuchukia shetani wewe.”
 
Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
116,407
Points
2,000

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
116,407 2,000
Sehemu ya 98

Nilisoma ujumbe huo mara mbili mbili, machozi yakanibubujika. Kila kitu kilikwisha badilika ghafla tu, ushirikina na ushetani niliotegemea maishani, haukuwa na msaada wowote. “Kuna nini kaka?” Mwanaume aliyeniazima simu aliniuliza. Sikumjibu zaidi ya kumrudishia simu yake.

Lawalawa hakuwa tena mikononi mwangu, Sijui kama babu yake Felix Kisu ndiye ameniroga ama ni wale jamaa wawili walokuja kusoma dua ndio wamebadilisha yote haya? Ni nini hasa kilitokea? Sijui.

Je nirudi Unguja kwa mganga wangu? lakini nitaenda vipi na ufukara huu, kadhalika nitaishi kwa kutegemea uchawi hadi lini Ajibu mimi?
Sauti moja kichwani iliniuliza. Nililia kama mpumbavu kitandani pale.

Dunia ilinigeuka ghafla sana. **** KWA MSAADA wa Jeshi la Polisi, nilisafirishwa hadi kijijini kwetu Maji moto, nilirudi nikiwa nimepoteza mguu mmoja. Nilikatwa mguu kwa kile kilichodaiwa na madaktari eti, nilikuwa nina saratani ya mfupa.

Hili la kuwa na saratani hadi sasa siliamini, lakini nitafanya nini? Ushirikina sitaki tena.

Miaka karibu kumi na mbili iliyopita niliondoka nyumbani Maji moto nikiwa na miguu miwili, nikazifuata ndoto zangu nikiamini nitaishi maisha niyatakayo.
Sasa nimerudi nikiwa mwanaume dhalili, nisiye na mbele wala nyuma. Mambo mengi yalikuwa yamebadilika.

Baba yangu alikwisha fariki miaka mingi. Mama naye alikuwa mzee sana. Tangu niliporudi alilia, akalia na kulia na mimi wakati wote. Kitendo cha kuniona mwanaye ni kilema wa mguu ilikuwa ni mwiba mkali moyoni.

Uchungu wa mwana ajuaye mzazi japokuwa sijui kama baba ningemkuta hai kama angenipokea. Mke wangu Pili, naye nilisikia habari zake.

Taarifa zilisema kwamba, mwanamke huyo aliolewa na mwanaume mwingine wa kijiji cha tatu kutoka Maji moto miezi michache iliyopita. Na inasemekana hadi wakati huu alikuwa na mimba changa.
 
Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
116,407
Points
2,000

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
116,407 2,000
Sehemu ya 99

Wazazi kutotambua kipaji cha mtoto na kusimamia ndoto zake ipasavyo ni matokeo ya kuvurugikiwa maishani ni kama tu mtoto huyo ataamua kupuyanga peke yake kuzikimbilia ndoto zake. Soka la ushirikina lilinikutanisha na shetani, dunia yangu ya soka ikavurugika, maisha nayo yakanichapa. Hadi sasa ninaposimulia mkasa huu naishi kwa mateso kutokana na uchawi niliojihusisha nao maishani. ****

Nakushukuru kwa kuchukua muda wako kusoma mkasa huu wa kweli, ninapoweka kalamu chini naamini kuna mengi umejifunza kupitia simulizi hii ya kweli.

Mwisho..

Ahsante kwa muda wako.
 
Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
35,493
Points
2,000

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
35,493 2,000

Inasikitisha sana... Mwisho wa ubaya ni aibu...

Hivi hii imeisha kweli au umeamua kuirukisha?

Chapter Closed...

Cc: mahondaw
 
Englishlady

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Messages
1,187
Points
2,000

Englishlady

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2013
1,187 2,000
Sehemu ya 99

Wazazi kutotambua kipaji cha mtoto na kusimamia ndoto zake ipasavyo ni matokeo ya kuvurugikiwa maishani ni kama tu mtoto huyo ataamua kupuyanga peke yake kuzikimbilia ndoto zake. Soka la ushirikina lilinikutanisha na shetani, dunia yangu ya soka ikavurugika, maisha nayo yakanichapa. Hadi sasa ninaposimulia mkasa huu naishi kwa mateso kutokana na uchawi niliojihusisha nao maishani. ****

Nakushukuru kwa kuchukua muda wako kusoma mkasa huu wa kweli, ninapoweka kalamu chini naamini kuna mengi umejifunza kupitia simulizi hii ya kweli.

Mwisho..

Ahsante kwa muda wako.
Ni mkasa wa kweli ama hadithi.

Nzuri sana.
 
Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
35,493
Points
2,000

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
35,493 2,000
Hahahahaha imeisha bwana halafu mbona imeisha vizuri tu
Ajibu kaptwa na maswahiba ya kukatwa mguu, mzazi wake mmoja kufariki, mwingine kumkuta mzee...

Lawalawa kugundua michezo ya ushirikana ya Ajibu na kumkataa...

Aliyekua mke wa Ajibu kuolewa na mwanaume mwingine...

Hapo bado lawalawa hajafunzwa adabu na walimwengu au ulimwengu kisawa sawa... dunia imemuhurumia sana...

Cc: mahondaw
 
chiqutitta

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2015
Messages
540
Points
1,000

chiqutitta

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2015
540 1,000
Ajibu kaptwa na maswahiba ya kukatwa mguu, mzazi wake mmoja kufariki, mwingine kumkuta mzee...

Lawalawa kugundua michezo ya ushirikana ya Ajibu na kumkataa...

Aliyekua mke wa Ajibu kuolewa na mwanaume mwingine...

Hapo bado lawalawa hajafunzwa adabu na walimwengu au ulimwengu kisawa sawa... dunia imemuhurumia sana...

Cc: mahondaw
Ila Lawalawa hana kosa sana
 
Forum statistics

Threads 1,343,343
Members 515,022
Posts 32,781,535
Top