Sehemu ya 90
Kufumba na kufumbua, tukajikuta tupo kitandani, tukiwa kama tulivyozaliwa. Dakika chache badaaye, tukawa tunaelea kwenye bahari kubwa ya huba.
Mambo yote hayo yalifanyika harakaharaka sana nyumbani kwao Lawalawa, mjini Tabora. Kuanzia siku hiyo niliishi na Lawalawa nyumbani kwao pale bila woga wowote.
Nilikuwa mario.
Hakuna nilichokuwa naogopa wala kujali, moyo wangu na mapenzi yangu yalikuwa kwa mwanamke huyo. Mara nyingi mke wangu Pili aliyekuwa mjini Kigoma kila aliponipigia simu niliishia kumdanganya kwamba aisone kimya niko bize na biashara.
Kuna wakati nilipoona simu za mke wangu zinanitia karaha, nikawa nazima simu. Wakati mwingine akawa akipiga simu sipokei. Kuna wakati nikawa namkatia simu. “Itabidi ubadilishe namba ya simu. Unaonaje?”siku moja Lawalawa alinishauri baada ya kero kuzidi.
“Uko sahihi, nitafanya kama utakavyo Lawalawa.”
Siku hiyo hiyo nilisajili laini nyingine, ile ya mwanzo nikaitupilia mbali. Mke wangu Pili, hakunipata tena.
Wiki ilipita. Kama mzaha maisha yangu na Lawalawa yaliendelea nyumbani kwao. Tuliishi vziuri mimi na yeye, ingawa gubu kubwa ilikuwa ni yule babu kizee.
Baba yake na Lawalawa, ambaye akama nilivyosimulia awali alikuwa mzee sana. Hakupenda kabisa mahusiano yetu. Mara kadhaa alikuwa akinilaani kwa kitendo cha kumtoa mtoto wake kwa mumewe wa ndoa na kuishi naye kwao nikiwa nalelewa.
“Mungu akulaani we’ ibilisi, umeharibu ndoa ya mwanangu, kama haitoshi unaendelea kumpotosha mwanangu.”
Mzee huyo aliniambia maneno hayo. Hata hivyo angenifanya nini?mtu mwenyewe alikwishajiishia anangojea siku zake chache zilizosalia ajifie.
Kwa hiyo maneno ya babu kizee huyo hayakunizuia mpumbavu mimi kuendelea kuishi na mwanaye ndani ya nyumba yake.
Siku moja Lawalawa aliniita na kuniambia jambo moja. Alisema:
“Nimewakumbuka wanangu Ajibu.” “Sasa?” nikamaka.
“Unaonaje nikienda kuwaona.” “Huko nchini Yemeni wanakoishi na baba yao?”