Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

SEHEMU YA 14

Ni ndani ya dakika thelathini tu, tena nikiwa nimeongea maneno mengi ya ushawishi, Majeed akakubali kwenda pamoja nami Darfur huku nikiwa nimemhakikishia ulinzi mkubwa katika kipindi ambacho tungekuwa huko.

Tukakubaliana na kumuacha kwenda kujiandaa kwa ajili ya safari hiyo ya kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na mauaji ya kikatili.

Mimi ndiye nilikuwa mwandishi wa habari, na mimi ndiye nilijifanya kuwa mlinzi katika maisha yake bila kujua kwamba Darfur ilikuwa ni sehemu gani, ilikuwa na hatari kwa kiasi gani.

Akakubaliana nami, hakujali sana kuhusu fedha, kitu alichojua ni kwamba nilitoka katika Shirika la Habari la Aljazeera na ndiyo maana alijisikia fahari kukubali kutaka kufanya kazi pamoja nami, hakujua kwamba hata kile kitambulisho ambacho nilimuonyeshea kilikuwa cha bandia.

Alichojua ni kwamba alikuwa akifanya kazi na mwandishi wa habari kutoka Aljazeera kumbe ukweli ni kwamba alikuwa akifanya kazi na Mwananchi wa kawaida tu, yaani kama yeye.
***
Sudan ilikuwa nchi kubwa sana zaidi ya nilifikiria kabla.

Nilipomuuliza dada wa mapokezi katika hoteli ile, alinishangaa sana kwamba ilikuwaje nihitaji kuelekea Darfur na wakati mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yalikuwa yakiendelea huko?

Nilimtoa wasiwasi na kutaka kunipa maelekezo mengi kuhusu safari ya kwenda katika mji huo iana na kwenda katika mji huo ambao ulionekana kuwa tishio sana.

Dada yule akaanza kunielezea mambo mengi na hata umbali aliniambia kwamba kulikuwa na zaidi ya kilometa elfu nane kutoka katika jiji la Khatoum.

Umbali ule ukanishtua sana, sikutegemea kama kungekuwa na umbali wa namna ile. Hapo nilifikiria kupanda ndege, ila tatizo lililokuja ni kwamba hakukuwa na uwanja wowote wa ndege huko Darfur uliokuwa ukitumika katika kipindi hicho cha mapigano.
 
SEHEMU YA 15

Maneno ya dada yule yalinichosha kupita kawaida, ni mabasi tu ndio ambayo yalikuwa yakifanya safari ya kwenda huko kwa kutumia barabara ya lami ambayo ilikuwa ikiunganisha mpaka Kurdufan, kilometa mia tano kabla ya kuingia Darfur.

Niliporidhika na maelezo yake, nikarudi chumbani na kujiandaa na safari, asubuhi ya siku iliyofuata, safari ikaanza huku nikiwa pamoja na Majeed.
Ndani ya basi hatukuwa watu wengi, tulikuwa tumekaa katika viti vya nyuma kabisa.

Lugha ya Kiarabu ndio ambayo ilikuwa ikisikika ndani ya basi lile, sikuwa nikielewa kitu chochote kile lakini kila nilipotaka kuambiwa kile kilichokuwa kikiongelewa, Majeed alikuwa akiniambia.

Safari ilikuwa ni ya kuchosha sana, mizigo mingi ilikuwa imepakiwa ndani ya basi lile, kila basi lilipokuwa likisimama, hali ya hewa ilikuwa ikibadilika kabisa, ilikuwa ni ya joto kali sana.

Kichwa changu katika kipindi hicho kilikuwa kikifikiria kitu kimoja tu, kufika Darfur na kuanza kufanya kile ambacho kilikuwa kimenifanya kufika ndani ya nchi ile.

Dereva alikuwa akiendesha gari kwa kasi. Ndani ya gari hakukuwa na mtu yeyote aliyejali mwendo ule mkali, ni kama watu walionekana kutokuwa na habari, walikuwa wakiendelea kupiga stori kama kawaida. Ndani ya saa nane, tukawa tumefika Ad Duwaym, Kusini mwa Jiji la Khatoum.

Hapa kidogo ilikuwa ikinishangaza sana, Mji wa Darfur ulikuwa ukipatikana Magharibi mwa nchi ya Sudan, sasa ilikuwaje katika kipindi hicho tulikuwa tukielekea Kusini. Maswali hayo wala sikutaka kuyauliza, nilibaki nayo moyoni huku nikisubiri muda muafaka wa kuuliza utakapofika.

Kama ilivyokuwa Khatoum ndivyo ilivyokuwa hapo Ad Duwaym, kulikuwa na idadi kubwa ya watu huku magari mengi ya Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika yakiwa mahali hapo.

Hapo tukaruhusiwa kushuka na kuanza kununua vyakula. Hali ilikuwa ngumu sana kwangu, vyakula ambavyo vilipatikana hapo havikuwa sawa na mimi.
 
SEHEMU YA 16

Chakula ambacho nilihisi ningeweza kukila kilikuwa ni nyama ya ngamia tu, nyama tamu ambayo mara nyingi nilikuwa nikiila nchini Tanzania hasa katika kipindi cha Idd Al Hadji na El Fitri ambapo rafiki yangu, Ustadhi Maliki alipokuwa akituletea.

Baada ya nusu saa tukaingia ndani ya basi na kuendelea na safari yetu. Hakukuwa na safari ambayo ilikuwa inachosha kama ile.

Muda mwingi nilikuwa nikiiangalia saa yangu ya mkononi ambayo nilikuwa nimeiseti katika majira ya Sudan.

Safari iliendelea zaidi, sehemu kubwa ya nchi hiyo ilikuwa ni jangwa kubwa, tena jangwa lile ambalo lilikuwa na joto kali katika kipindi cha mchana.

Baada ya saa nane nyingine kupita, tukaingia katika Mji wa Kust na kuunganisha kuutafuta Mji wa Rabak ambapo hapo tungechukua barabara ya kuelekea Darfur.

Mchoko wa safari bado ulikuwa mkubwa mno, saa nne na robo usiku tukaingia Rabak ambapo hapo tulitakiwa kulala.

Usingizi haukupatikana hata kidogo, tulishinda usiku mzima tukipiga stori na Majeed ambaye hakuonekana kuwa na amani katika safari ile.

Bado niliendelea kumfariji na kumtoa hofu. Tulikula na kuendelea kupiga stori. Ilipofika saa kumi na mbili alfajiri, tukaanza tena safari ya kuelekea Darfur.

Hapo Rabak tuliwachukua abiria wengine waliokuwa wamefika na mabasi kutoka Sannar, Sanjar na Al Qadarif miji ambayo ilikuwa ikipatikana Mashariki mwa nchi ya Sudan.

Majeed ndiye ambaye alionekana kunichosha zaidi hasa mara baada ya kunitaarifu kwamba hata nusu ya safari tulikuwa hatujamaliza, tulisafiri kwa saa kumi na sita lakini cha ajabu eti hata nusu ya safari haikuwa imekwisha.

Safari ikaendelea zaidi, tayari nilionekana kukata tamaa ya kufika mapema, jua lilipochomoza mpaka kuwa la utosini ndipo tukafika Al Ubayyid. Hapo tukanunua chakula na kula tena.

Hali ya joto ilinisumbua, nilitamani kuvua shati langu lakini sikufanya hivyo kwa kutotaka kuonekana vibaya mbele za macho ya watu waliokuwa na asili ya Uarabu.
 
Usisahau kuni tag
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom