Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

duh "!!,kumbe nimefika mlipo ishia " .... leo nimejaribu kusoma hadithi ya nyemo " kwaajili yako Shunie ... huwaga simpi chapuo kiviiile " lakini kwa kuwa wewe ndio umeileta acha nikupe support "... huwenda nikapata mapya ya kujifunza toka kwake " ambayo huwa nayakosa kutokana na kumpuuzia kwangu ....


haya mwaga nondo hizo tayari umeshanipa arosto
 
SEHEMU YA 17

Safari ikaendelea zaidi, saa tano na robo usiku ndipo tukaingia An Nunud, kilometa mia saba kabla ya kuingia Darfur. Nikatoka garini na kukaa nje.

Kila abiria alichoka, nilibaki nikiongea na Majeed kwa kipindi kirefu zaidi huku nikitaka kufahamu mengi kuhusiana na Darfur.
“Kwa hiyo nitajua vipi kama tumeingia Darfur?” nilimuuliza Majeed.
“Utajua tu.”

“Nitajua tu. Kivipi?” nilimuuliza.
“Swali lako litajibika kirahisi sana,” Majeed aliniambia.
“Sijakuelewa.”

“Kimuonekano. Utakavyouona muonekano, utajua tu kwamba tutakuwa tumeanza kuingia Darfur,” Majeed aliniambia.

Sikutaka kuuliza maswali mengine zaidi, kiu yangu ilikuwa ni kuanza kuona dalili hizo ambazo niliambiwa kwamba ningejua tu kwamba tulikuwa tumeingia Darfur.

Ilipofika asubuhi tukaanza safari. Katika kipindi hiki kulikuwa kumebaki vituo viwili vikubwa, cha kwanza kilikuwa Nyala na cha pili kilikuwa Al Fashir.

Hiki kituo cha Al Fashir kilikuwa ndani ya Darfur ila huku pembeni pembeni kabisa katika upande wa Kusini mwa Mji wa Darfur.

Hapo ndipo ungekuwa mwisho wa safari yetu, japokuwa katika kipindi hicho nilitaka kuelekea katika sehemu iliyo na mapigano zaidi ya Al Junaynah, lakini Majeed aliniambia kwamba basi lisingeweza kufika huko.

“Kwa nini?” nilimuuliza.

“Huko ndipo kwenye mapigano yenyewe, huko hakuna amani hata kidogo,” Majeed aliniambia.

“Safi sana. Uko ndipo pazuri, na huko ndipo nilipotaka kwenda,” nilimwambia Majeed ambaye alionekana kushtuka zaidi.

Safari iliendelea, abiria wengi waliishia hapo Al Ubayyid. Kipindi cha nyuma ndani ya basi tulikuwa zaidi ya watu sitini lakini katika kipindi hicho tulikuwa tumebakia watu kumi na sita tu, wengine walikuwa wamekwishashuka.

Safari haikuishia hapo iliendelea zaidi na zaidi mpaka tukaingia Nyala, kituo cha mwisho kabla ya kuingia kituo cha Al Fashir, mwisho wa safari ya basi lile.
*
*

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 18

Safari ya kuelekea Al Fashir ikaanza. Hapa ningependa kuongea kitu kimoja kwa wale ambao waliweza kuongea mengi hata kabla safari ya kufika Darfur haikukamilika.

Darfur ndiyo mji mkubwa nchini Sudan na ndiyo maana mapigano yaliyokuwa yakiendelea huko yaliweza kuiathiri sana nchi hiyo.

Safari ya kuelekea katika mji mdogo wa Al Fashir ilikuwa ikiendelea. Hapa pia ningependa kuongea kitu kimoja ili kwa wale walioshangaa wasishangae tena.

Umbali wa kutoka Khatoum mpaka Darfur ilikuwa ni wa kilometa 8000 ila kilometa hizo ni mpaka pale ambapo unaingia katika Mji wa Nyala ambao upo Kusini mwa mji huo wa Darfur.

Umbali kutoka Khatoum mpaka hapo Nyala haukuwa ukipishana sana na umbali kutoka Nyala mpaka mwisho wa basi lile, Al Fashir.

Darfur ile ilikuwa kubwa sana, upana wake ulimshangaza kila mtu kiasi kwamba kuna wakati nchi ya Chad ikang’ang’ania kwamba Darfur ilikuwa ni sehemu ya nchi yao.

Darfur ilikuwa kubwa, eneo kubwa la Darfur lilikuwa jangwa kubwa, jangwa ambalo lilikuwa na joto kali katika kipindi cha mchana.

Umbali huo mkubwa ndio ukanifanya kupata majibu ya sababu ambayo ilimfanya dereva kuendesha gari kwa kasi kubwa zaidi ya magari ambayo yalikuwa yakisafiri katika ardhi ya Tanzania.

Nakumbuka nilikwishawahi kwenda Nairobi kwa kutumia mabasi ambayo yalikuwa yakikimbia sana, ila kwa mabasi yale ambayo yalikuwa yakisafiri kuelekea Darfur, mwendo wake ulikuwa ni mara mbili ya mabasi ya huku Tanzania.

Dereva alikanyaga mafuta hasa, muda mwingi nilikuwa na hofu lakini hakukuwa na mtu aliyehofu chochote kile, walionekana kuzoea.

Hapo ndipo ambapo safari ilionekana kuchosha sana, tulisafiri usiku na mchana na hatimaye kuingia Al Fashir, mji ambao basi lile lilikuwa limefikia mwisho.

Nikateremka na kumshukuru Mungu kwa kunifikisha salama katika ardhi ya Mji wa Al Fashir. Nilichokifanya ni kwenda kwenye kimgahawa kidogo na kupata chakula,
 
SEHEMU YA 19

Kumbuka kwamba hapo tayari tuliingia katika mji wa Darfur ila hatukuwa tumefika katika sehemu ile ambayo ilikuwa na mapigano makubwa.

Baada ya kukaa mahali hapo kwa muda wa masaa mawili, ndipo tukaanza safari ya kuelekea sehemu iliyo na mapigano makali, Al Junaynah.

Usafiri haukuwa wa basi tena, madereva wengi walikuwa wakiogopa kuelekea huko kwa hiyo tulichokifanya ni kutumia usafiri wa farasi ambao ndiyo ulikuwa usafiri uliokuwa ukitumika katika kipindi hicho sehemu hiyo.

Katika safari ya kuelekea Al Junaynah hatukuwa peke yetu, tulikuwa na watu zaidi ya kumi ambao nao walikuwa wakielekea huko.

Farasi walikuwa wakikimbia kwa kasi kubwa, na kwa kutumia farasi hao huku tukipumzika katika sehemu mbalimbali hasa nyakati za usiku na pale ambapo farasi walipochoka, tuliweza kutumia siku sita na ndipo tukaanza kuingia katika Mji wa Al Junaynah.

Mpaka hapo wala sikutaka kuuliza zaidi kama tulikuwa tumeingia katika mji huo au la, magari mengi ya Umoja wa Mataifa yalionekana machoni mwetu, mara kwa mara walikuwa wakitusimamisha na kutuuliza baadhi ya maswali na waliporidhika na majibu yetu, tulikuwa tukiendelea na safari kama kawaida.

Tukafika katika sehemu ambayo wala haikuwa ikieleweka kabisa, macho yangu yakatua katika vitu vyeupe ambavyo nikashikwa na shauku kubwa ya kutaka kuvijua ni vitu gani.

Nilichokifanya ni kuanza kuwaambia wenzangu kwamba ilikuwa ni lazima nijue vitu vile vilikuwa ni nini. Watu wote walikataa lakini nilipowalazimisha zaidi, wakakubaliana nami.

Nikateremka juu ya farasi pamoja na Majeed na kuanza kuelekea kule ambapo kulikuwa na mchanga mwingi. Sikuamini kile ambacho nilikuwa nikikiona mahali pale, yalikuwa ni mafuvu ya watu.

Kwanza nikapigwa na mshtuko sana, toka nizaliwe sikuwahi kuyaona mafuvu ya watu, wakati huo ndio ilikuwa mara ya kwanza.

Kuna vitu vingine huwa tunavipuuzia sana kila tunavyoviona kwenye televisheni, ila ukweli ni kwamba vinatisha kupita kawaida. Mafuvu ya watu yanatisha sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom