Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
157,400
Reaction score
465,170
Mtunzi Nyemo Chilongani SEHEMU YA 01

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2005, mwaka ambao nilimaliza kuchukua Diploma yangu ya Uandishi wa habari katika Chuo cha Uandishi cha DSJ (Dar es Salaam School of Journalism) kilichokuwa Mtaa wa Bungoni, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi hicho nilikuwa na furaha sana kwa sababu ndoto zangu ambazo nilijiwekea katika maisha yangu niliziona kuanza kutimia katika muda mchache ujao.

Katika kipindi chote ambacho nilikuwa katika chuo hicho nikipata elimu yangu, kichwani mwangu kulikuwa na ndoto nyingi, ndoto za kuwa mwandishi mkubwa ambaye ningekuja kuheshimika na jamii yote, mwandishi ambaye ningeweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta zote za uandishi nchini Tanzania.

Kila nilipokuwa nikimwangalia mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Charles Hilary, nikajiona nikizidi kupata nguvu zaidi za kusoma kwa sana, nilitamani sana kuwa kama yeye katika maisha yangu.

Nilikuwa na kiu sana ya kuwa mwandishi bora na kisha kutafuta nafasi ya kutangaza katika shirika lolote kubwa la Habari kama la BBC, CNN, Al Jazeera au shirika lolote ambalo lilikuwa likitambulika kimataifa.

Hapo ndipo ambapo nilipofikiria kitu kimoja ambacho nilitakiwa kufanya, kitu ambacho kingekuwa cha hatari sana katika maisha yangu.

Nakumbuka siku hiyo mara baada ya kutoka katika ‘field’ yangu niliyoifanyia katika kituo cha utangazaji cha Global TV, nikarudi nyumbani na kutulia chumbani kwangu.

Siku hiyo sikuonekana kuwa na furaha kabisa, kichwa changu kilikuwa kikifikiria ni kwa namna gani ningeweza kuwaambia wazazi wangu kuhusu kile nilichokuwa nikikifikiria kichwani mwangu.

Kiukweli nilihitaji sana ushirikiano kutoka kwa wazazi wangu, wao ndiyo walikuwa watu sahihi ambao kamwe wasingeweza kunishauri kitu kibaya.

Nilitulia chumbani kwangu kitandani, hakukuwa na siku ambayo niliwaona wazazi wangu wakichelewa kurudi nyumbani kama siku hiyo.

Muda wote macho yangu yalikuwa yakiangalia saa yangu ya mkononi, nilitamani sana waingie nyumbani hapo na kuwaambia kile nichokuwa nimepanga kuwaambia.


Screenshot_20181102-231642.jpeg
 
SEHEMU YA 02

Saa 2:23 usiku nikasikia muungurumo wa gari kutoka nje ya nyumba yetu, sikutaka kujiuliza zaidi, nikajua fika kwamba wazazi wangu walikuwa wakiingia ndani ya eneo la nyumba yetu.

Sikutaka kutoka wala kuonyesha kwamba nina presha, nikatulia chumbani mpaka pale walipoingia ndani na kuelekea chumbani kwao.
Baadaye walipotoka kwa ajili ya kula chakula cha usiku, nikaelekea mezani na kuanza kula pamoja nao.

Kwa wakati huo kichwa changu kilikuwa kikifikiria mengi, sikujua kama wangeweza kunielewa juu ya kile nilichotaka kuwaambia. Katika kipindi chote ambacho tulikuwa tukila, muonekano wangu ulionekana kuwa si wa kawaida, nilionekana kuwa na kitu moyoni mwangu.

“Thomas!” niliisikia sauti ya baba ikiniita, nikashtuka kutoka katika lindi la mawazo.
“Naam!” niliitikia huku nikionekana kushtuka.
“Unawaza nini?” aliniuliza baba huku akiacha kula.

“Siwazi kitu baba,” nilimwambia huku macho yangu yakionyesha dhahiri kwamba nilimdanganya.
“Hapana. Hauko kawaida leo. Hebu tueleze unawaza nini,” aliniambia.

Nilibaki kimya kwa muda, nikaanza kufikiria ni kitu gani nilichotakiwa kuwaambia. Nikaanza kujiuliza kama lilikuwa jambo sahihi kuwaambia kile nilichopanga kuwaambia ili wanishauri au nilitakiwa kukaa kimya na kuwashtukiza hapo baadaye.

“Kuna nini kipenzi,” mama aliingilia kwa kuniuliza swali. Nikayapeleka macho yangu usoni mwake.
“Nataka kuwa mwandishi mkubwa wa habari,” niliwaambia.

“Hilo tunalifahamu na umekuwa ukituambia kila siku. Nakumbuka huwa unatuambia kwamba unataka kuwa kama Charles Hilary, si ndiyo?” aliniambia baba na kuniuliza.

“Ndiyo. Natamani sana nifanye kazi katika mashirika makubwa ya habari duniani,” niliwaambia.

“Kila kitu kinaanza kwa hatua Thomas, huwezi kuwa mwandishi mkubwa wa habari na wakati haujapitia katika mashirika madogo.

Unakumbuka kuwa hata Charles Hilary kabla ya kujiunga na BBC alikuwa akifanya kazi ITV?” baba alisema na kuniuliza.
“Nakumbuka.”

“Basi hutakiwi kuwa na presha. Kuna siku utakuwa mwandishi mkubwa tu,” aliniambia.
 
SEHEMU YA 03

Nikabaki kimya kwa muda, baba aliniondoa katika kile nilichokuwa nimekifikiria kabla, alijitahidi kuniambia maneno mengi kwamba ningekuwa mwandishi mkubwa wa habari kama tu ningekuwa mvumilivu na kufanya kazi katika mashirika madogo, sikukubaliana na maneno yake kabisa.
“Kuna kitu nimekifikiria na ningehitaji ushauri wenu,” niliwaambia.
“Kitu gani?”

“Nataka nitengeneze makala yangu ihusuyo mambo fulani, na kama ikiwezekana basi nisafiri,” niliwaambia.
“Kuandaa makala yahitaji utulivu mkubwa sana.

Wewe unataka kusafiri kuelekea wapi kuiandika hiyo makala yako?” baba aliniuliza.
“Nataka kwenda Darfur, nchini Sudan,” niliwaambia.

Kila mmoja akashtuka, wote wakaacha kula na kuniangalia kwa macho yaliyoonyesha kutokuamini kile nilichokisema.

Wakanikazia macho zaidi, nilionekana kuongea kitu kilichowashtua mno. Nikamuona baba akiisogeza sahani yake mbele kuonyesha kwamba alikuwa ameshiba.
“Unasemaje?” aliniuliza huku akionekana kushtuka.

“Nataka kwenda Darfur,” nilimjibu.
Chakula hakikulika tena, kila mmoja alionekana kushiba, maneno niliyowaambia kwamba nilitaka kwenda nchini Sudan tena katika Mji wa Darfur yaliwashtua sana. Waliufahamu vilivyo mji huo na yale mauaji yaliyokuwa yakiendelea huko.

Hapa ningependa kuwaambia wale watu ambao hawakuwa wakiijua hii Darfur ambayo nilikuwa nimeizungumzia mahali hapo. Darfur ni mji mkubwa ambao unapatikana nchini Sudan. Mji huu ndiyo umekuwa na machafuko mengi ambayo yamepelekea nchi nzima kutokuwa na maelewano.

Watu walikuwa wakiishi kwa hofu huko, wakulima walihofia kuelekea mashambani mwao jambo ambalo lilipelekea nchi kuingia katika njaa kali.

Nchi hii ilionekana kama kuwa na laana kwani toka kipindi ambacho machafuko hayo yalianza, mvua nazo zilianza kunyesha kwa nadra sana.

Waandishi wa habari waliokuwa wakielekea katika mji huo wengi kuuawa kinyama kwa sababu wao wenyewe hawakutaka kufuatiliwa na maisha yao au kitu chochote kilichokuwa kikiendelea huko.
 
SEHEMU YA 04

Umoja wa Mataifa (UN) na Afrika (AU) ilijaribu kuingilia kati lakini hakukuonekana kuwa na mabadiliko kabisa, bado vita vya wenyewe kwa wenyewe viliendelea kama kawaida.

Katika mji huo huo ambao milio ya risasi ilionekana kuwa kama midundo ya muziki katika kumbi za usiku, mabomu ya mikono yalipoonekana kuwa kama mipira ya miguu, mji huo huo ndiyo ambao nilitamani kwenda kwa wakati huo.

Kiu yangu kubwa ilikuwa ni kuingia ndani ya nchi hiyo na kwenda katika Darfur ambapo ningetengeneza makala yangu nzuri na kuitangaza na hatimaye mashirika makubwa ya habari kunikubali na hivyo kuwa na haja ya kuniajiri na kuanza kazi pamoja nao.

Moyoni mwangu niliamini sana kwamba kama ningeweza kuelekea Darfur basi kila kitu kingekwenda kama kilivyotakiwa, kiu ya kuwa kama Charles Hilary ilinikaba kooni.

“Haiwezekani,” baba aliniambia.
“Kwa nini?”
“Ile si sehemu salama katika maisha ya binadamu.”

“Hata kama baba. Naomba mniruhusu nielekee huko, ninataka kupata kile ninachokitaka katika maisha yangu,” nilimwambia.
“Haiwezekani,” baba aliniambia kwa sauti kubwa iliyojaa ukali ambayo ilinifanya kubaki kimya.

Baba alionekana kukasirika sana, hapo hapo akanywa maji haraka haraka na kisha kuondoka mahali hapo na kueleka chumbani kwake.

Japokuwa sikuwa nimemaliza kula chakula, chakula kile kikaonekana kunikinai, sikuwa na hamu ya kukila tena. Mama nae akainuka, kwa jinsi nilivyokuwa nikimwangali, nae alionekana kukasirika, hakupenda nielekee Darfur, bado alikuwa akinihitaji.
“Nitakwenda tu, hata kama nitatoroka. Nitakwenda tu” Nilijisemea.

Japokuwa katika kipindi cha nyuma nilijifanya kutaka kuomba ushauri kutoka kwa wazazi wangu lakini moyo wangu ulikuwa umeweka msimamo mmoja tu kwamba ningekwenda tu nchini Sudan hata kama wangekataa kunipa nauli.

Moyo wangu ulikuwa umkwishaamua kwa wakati huo, nilichokuwa nikikitaka ni kuelekea nchini Sudan na kisha kuandika Makala ambayo niliamini ingenitangaza sana na hatimae kuajiriwa katika mashirika makubwa duniani.
 
SEHEMU YA 05

Nilibaki pale mezani kwa muda, mara nikaichukua simu yangu na kisha kumpigia simu mpenzi wangu niliyekuwa nae katika kipindi kile, Myra na kisha kumwambia kile ambacho nilikuwa nimekifikiria kukifanya kwa wakati ule.

Nilipompa taarifa Myra, nae alikuwa sawa na wazazi wangu, alikataa kata kata kunikubalia nielekee nchini Sudan.
“Hapana mpenzi” Myra aliniambia kwa sauti iliyojaa wasiwasi.

“Itanibidi nifanye hivyo Mage. Ni lazima niende Sudan. Haijalishi wewe hautaki au wazazi wangu hawataki, NI LAZIMA nilekee Sudan” Nilimwambia Myra.
Huo ndio uamuzi ambao nilikuwa nimeupanga.

Nikaanza kufikiria gharama ambazo zingenigharimu mpaka kukamilisha kila kitu, kitu cha kwanza kilikuwa kamera, nilihitaji kuwa na kamera ya video na ya picha. Pia nikahitaji kuwa na begi kubwa la mgongoni pamoja na kiasi fulani cha fedha ambacho kingeniwezesha kukitumia katika kipindi ambacho ningekwenda nchini Sudan.

Vitu hivyo havikuwa na shida sana, pia nilitakiwa kuwa na kitambulisho cha uandishi wa habari ambacho ningekionyesha kwa kila mtu ambaye angetaka kukiona hasa wale wafuasi wa upande wa pili ambao walikuwa kinyume na serikali ya Sudan.

Hapa ndipo nilipoamua kuwasiliana na rafiki yangu, Hamza Kimosa ambaye nilimwambia anitengenezee kitabulisho cha uandishi wa habari cha shirika la Aljazeera huku nikiwa nimemtumia picha ya itambulisho hicho ambayo niliipata kwenye mtandao.

“Ni LAZIMA niende Darfur hata kama hawataki. Hata kuwatoroka nitawatoroka tu” Nilijisemea katika kipindi ambacho nilikuwa nikielekea chumbani kwangu.
*
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom