Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha

SEHEMU YA 26

Bado kuna mambo mengi ambayo ningependa uyafahamu kuhusiana na hii Darfur ambayo huwa unaisikia tu katika vyombo mbalimbali vya habari.

Nchi hii ilifanana na Iran au nchi yoyote ambayo ilikuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kipindi kirefu.

Siku hiyo akili yangu ikawa kama imeonyeshwa kitu kingine, picha ambayo inaonekana katika upande wa pili katika maisha ya binadamu.

Maishani mwangu sijawahi kuishi kwa hofu hata kidogo lakini ndani ya Sudan, nilikuwa nikiishi kwa hofu sana kwani muda mwingi nilikuwa kama mtu aliyekuwa ameshika roho yake mkononi na muda wowote ule ingeweza kumtoka.

Maisha ya watu waliokuwa wakiishi hapo Zahor yalikuwa ni ya kuhuzunisha sana, moyoni niliumia kupita kawaida.

Japokuwa nchini Tanzania kuna sehemu ambazo watu wanasema zina njaa kali lakini nadhani kwa hapo Zahor mambo yalikuwa ni zaidi ya njaa kali.

Kama kuna wengine mmesahau subiri niwakumbushe kitu kimoja kwamba hapo nilipokuwa tayari nilikuwa nimeingia Darfur.

Yaani ilikuwa ni kama unataka kwenda Dar es Salaam halafu umefika Kimara na mapigano makubwa zaidi yalikuwa Posta (mjini), hiyo ndivyo ilivyokuwa hapo Zahor.

Zahor ilikuwa ni sehemu ya Darfur ila haikuwa sehemu ambayo mapigano yalikuwa makubwa kama ilivyokuwa Al Junaynah.

Mimi kama mimi nilikuwa nikitaka sana kwenda huko Al Junaynah, sehemu ambayo mapigano yalikuwa makali kabisa.

Kwa waandishi wengi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari kutoka katika mashirika makubwa ya habari duniani walikataa kwenda Al Junaynah kutokana na waandishi wengi wa habari kuuawa huko.

Maisha ya huko yalitisha kupita kawaida lakini mwisho wa siku nami nikatamani kuelekea huko bila kuogopa kitu chochote kile.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri ni kwamba niliondoka nyumbani huku kichwani mwangu nikifikiria kitu kimoja tu, kuwa na ndoto ya kuwa mwandishi mkubwa wa habari kutoka katika vyombo vya habari mbalimbali duniani.
 
SEHEMU YA 27

Watu walitaka kufahamu hali halisi iliyokuwa ikiendelea Darfur, dunia haikutaka kufichwa tena juu ya kile kilichokuwa kikiendelea na ndiyo maana nilikwenda huko.

Sikutaka kuishia hapo Zahor, nilitaka kusonga mbele huku nikitaka kuona kila kitu kama ambavyo nilitaka kurekodi makala yangu na kisha kuirusha hewani.

Hapo Zahor siku hiyo ilikuwa ni balaa, joto lilikuwa kali sana kitu ambacho kilitufanya kulala nje. Usiku sikupata usingizi, moyo wangu ulikuwa na shauku kubwa ya kutaka kufika huko Al Junaynah na kutaka kuona kile ambacho kilikuwa kikiendelea.

Kwa sababu nilikuwa nimefanya kazi ya kujitolea, katika kipindi hicho sikutakiwa kuhofia milio ya bunduki, sikutakiwa kuogopa kitu chochote kile, yaani hata kama kungekuwa na mtu ambaye angenifuata na kuniwekea mdomo wa bunduki mbele ya uso wangu, sikutakiwa kuogopa.

Naweza kusema kwamba usiku huo wala haukuwa wa amani. Nakumbuka vizuri ilipofika saa nne kama na robo hivi kwa mbali tukaanza kusikia sauti za watu. Kulikuwa na giza sana mahali pale hivyo hatukujua ni watu gani ambao walikuwa wakija kule tulipokuwa.

Sauti za farasi zikaanza kusikika, wenyeji wakafahamu ni watu gani ambao walikuwa wakija mahali hapo. Nikaanza kuwaona wakiinuka na kuanza kuelekea ndani.

Ni kweli nilijipa ujasiri mkubwa sana lakini katika kipindi hicho mambo nikayaona yakianza kubadilika. Tayari nilijua fika kwamba hatari iliingia na ndiyo maana wenyeji walikuwa wamekimbia mahali hapo.

Ndani ya sekunde thelathini, pale nje nilikuwa nimebaki na Majeed tu ambaye muda wote toka tulipokuwa hapo Zahor alikuwa akitetemeka kana kwamba alijua kwamba angekufa muda wowote ule.
“Tuondoke,” Majeed aliniambia.

Sikutaka kubaki, niliona kulikuwa na hatari, nikasimama na kuanza kuondoka nae kuelekea katika moja ya nyumba ambayo ilikuwa mahali hapo.

Tulipoifikia nyumba ile tukaanza kuusukuma mlango lakini haukufunguka hali iliyoonyesha ulifungwa kwa ndani.

Tukatoka na kuelekea katika mlango wa nyumba nyingine lakini napo kulikuwa vile vile.
 
SEHEMU YA 28

Tukachanganyikiwa, tukaona kulikuwa na hatari ambayo ingeweza kutokea mahali hapo.

Kwenye kuangalia huku na kule tukauona mlango wa nyumba moja ukiwa wazi kwani ulikuwa ukijibamiza bamiza sana, tukaanza kuufuata mlango wa nyumba ile.

Tulipoufikia, tukaingia ndani, kwa nje tulifikiri ni nyumba ambayo walikuwa wakiishi watu ndani ila tulipoingia tu, tukakutana na wanyama mbalimbali kama ng’ombe, mbuzi na ngamia wanne.

Tulikaa katika nyumba ile ambayo kwa hapa ningependa kuiita zizi ingawa ilikuwa kama nyumba ya kawaida.

Tulikaa mule kwa dakika kadhaa na ndipo tukaanza kusikia vishindo vya watu na farasi ambao walikuwa wakipita nje, tukabaki kimya kabisa.

Sijajua ni kwa nini watu wa pale Zahor walikuwa wakiwaogopa watu hao. Kichwani mwangu kulikuwa na maswali mawili ambayo niliona ni lazima niwaulize watu wa hapo Zahor kuhusiana na watu hao ambao walikuwa wamewakimbia.

Swali la kwanza nilitaka kujua sababu iliyowafanya kukimbia, na la pili lilikuwa ni kutaka kufahamu watu hao walikuwa akina nani.

Hayo ndio maswali mawili ambayo niliyapanga kuyauliza mara itakapofika asubuhi kwani niliamini kwamba nayo yangekuwa katika mchakato wa kukamilisha makala yangu ambayo nilipanga kuiandika katika kipindi hicho.

Hatukulala kabisa, usiku mzima tulikuwa macho na wala hatukuwa tukiongea kwa kudhania kwamba watu wale bado walikuwa nje ya eneo la nyumba zile.

Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, mwanga ukaanza kuonekana na kisha kutoka nje. Njaa ilinishika kwa sababu jana yake sikuwa nimekula chochote kile.

Nilikuwa nikifikiria namna ya kupata chakula lakini wala sikuona njia yoyote ya kuweza kupata chakula asubuhi hiyo.
“Nitakufa,” nilimwambia Majeed.
“Kwa nini?”

“Nasikia njaa sana. Yaani njaa imenikamata mpaka naona tumbo linauma,” nilimwambia Majeed ambaye alikuwa akiniangalia kwa macho ya kunionea huruma.
 
SEHEMU YA 28

Tukachanganyikiwa, tukaona kulikuwa na hatari ambayo ingeweza kutokea mahali hapo.

Kwenye kuangalia huku na kule tukauona mlango wa nyumba moja ukiwa wazi kwani ulikuwa ukijibamiza bamiza sana, tukaanza kuufuata mlango wa nyumba ile.

Tulipoufikia, tukaingia ndani, kwa nje tulifikiri ni nyumba ambayo walikuwa wakiishi watu ndani ila tulipoingia tu, tukakutana na wanyama mbalimbali kama ng’ombe, mbuzi na ngamia wanne.

Tulikaa katika nyumba ile ambayo kwa hapa ningependa kuiita zizi ingawa ilikuwa kama nyumba ya kawaida.

Tulikaa mule kwa dakika kadhaa na ndipo tukaanza kusikia vishindo vya watu na farasi ambao walikuwa wakipita nje, tukabaki kimya kabisa.

Sijajua ni kwa nini watu wa pale Zahor walikuwa wakiwaogopa watu hao. Kichwani mwangu kulikuwa na maswali mawili ambayo niliona ni lazima niwaulize watu wa hapo Zahor kuhusiana na watu hao ambao walikuwa wamewakimbia.

Swali la kwanza nilitaka kujua sababu iliyowafanya kukimbia, na la pili lilikuwa ni kutaka kufahamu watu hao walikuwa akina nani.

Hayo ndio maswali mawili ambayo niliyapanga kuyauliza mara itakapofika asubuhi kwani niliamini kwamba nayo yangekuwa katika mchakato wa kukamilisha makala yangu ambayo nilipanga kuiandika katika kipindi hicho.

Hatukulala kabisa, usiku mzima tulikuwa macho na wala hatukuwa tukiongea kwa kudhania kwamba watu wale bado walikuwa nje ya eneo la nyumba zile.

Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, mwanga ukaanza kuonekana na kisha kutoka nje. Njaa ilinishika kwa sababu jana yake sikuwa nimekula chochote kile.

Nilikuwa nikifikiria namna ya kupata chakula lakini wala sikuona njia yoyote ya kuweza kupata chakula asubuhi hiyo.
“Nitakufa,” nilimwambia Majeed.
“Kwa nini?”

“Nasikia njaa sana. Yaani njaa imenikamata mpaka naona tumbo linauma,” nilimwambia Majeed ambaye alikuwa akiniangalia kwa macho ya kunionea huruma.
nasubiri sehemu inayofuata kwa hamu
 
Hii story inawekwa kila siku sio kwa siku mara mbili ni mara moja tu

Halafu nilishasema toka mwanzo hii story inaweza kuwa na arosto
Sawa mrembo,nimeelewa. Naomba niweke kweny Tag list yako
 
SEHEMU YA 29

Tulikuwa tumekaa huku tukiwa hatufahamu ni kwa namna gani tungeweza kupata chakula mahali hapo. Baada ya dakika kama thelathini hivi, wenyeji wakatoka.

Kwanza kila mtu akatushangaa, walichofikiria tulikuwa tumeuawa na watu wale waliokuja usiku mara baada ya kutuacha mahali pale.
“Hawakutuona.

Tuliondoka na kuelekea katika nyumba ile,” niliwaambia huku nikinyooshea kidole ile nyumba ambayo kwangu ilionekana kuwa kama zizi.

“Siku nyingine mnapowasikia naomba msikae nje,” mzee yule ambaye alikuwa akifahamu lugha ya Kingereza aliniambia.

“Kwa nini? Kwani wale ni nani?” nilimuuliza maswali mawili mfululizo.
“Wale ni wafuasi wa waasi wa Darfur Liberation Front,” mzee yule alituambia.
“Na wamekuja kufanya nini hapa?” nilimuuliza.

“Huwa wanakuja huku kwa ajili ya kuhakikisha usalama,” mzee yule alituambia.

“Kuhakikisha usalama kivipi na wakati wao ni waasi?”

“Hawa huwa wanapigana na wanajeshi wa serikali pamoja na wale wa Umoja wa Afrika. Hawataki wanajeshi hao waingie ndani ya Darfur na ndio maana huwa wanazunguka zunguka,” mzee yule alituambia.

“Sasa kwa nini mlikimbia?”
“Huwa hawataki watu walale nje, wanataka watu wote wawe wanalala ndani kwa kuhofia kuchangamana na maadui zao.”

“Na kama wangetukuta nje ingekuwaje?”
“Wangewaua.”
“Kwa nini?”
“Sijui ila hiyo ndio sheria yao,” mzee yule alinijibu.

Hapo nikajihesabia kuwa kama mfu aliyekuwa akitembea, nikapata uhakika kwamba nilikuwa natembea huku roho yangu ikiwa mkononi mwangu kwa kuona kwamba kama ningejifanya kupuuzia mambo mengine basi ni mwili wangu tu ndio ungeweza kurudi nchini Tanzania au kuzikwa huko huko jangwani.
Maswali yaliyofuata mahali hapo ni kuulizia chakula.

Hakukuwa na chakula cha kueleweka hapo Zahor, walituletea tende tu ambazo tukaanza kuzila mpaka pale ambapo nilijiona kuwa na unafuu kidogo tumboni mwangu.
 
SEHEMU YA 30

Siku hiyo tulipanga kuondoka mahali hapo saa nne asubuhi kuendelea na safari yetu ya kuelekea Al Junaynah.

Kila mtu alitushangaa tulikuwa na moyo kiasi gani mpaka kudiriki kutaka kwenda Al Junaynah na wakati sehemu hiyo ilikuwa na vita vikali ambavyo vilikuwa vikiendelea?

Sikujali, dhumuni langu katika kipindi hicho lilikuwa ni kuelekea huko kwa ajili ya kuandika makala yangu kwa kina zaidi. Huku likiwa limebakia saa moja kabla ya kuanza safari yetu, kwa mbali tukaanza kuwaona watu ambao walikuwa wakija kule tulipokuwa huku wakiwa na farasi zaidi ya kumi.

Kwanza kila mtu akaogopa. Kwa hapa ngoja nikwambie kitu kimoja.

Hapo Zahor hakukuwa na amani hata kidogo, muda wote watu walikuwa wakiishi na mashaka kutokana na wanajeshi wa waasi ambao walikuwa wakifika mahali pale kila siku.

Hatukuwa na cha kufanya, tulichokifanya ni kuanza kuwasubiri ili kujua walikuwa wakihitaji kitu gani mahali pale.
“Tukimbie,” Majeed aliniambia huku akionekana kuwa na hofu.

“Tuelekee wapi?” nilimuuliza.
“Popote pale.” Hilo likaonekana kuwa suala gumu kukubalika moyoni mwangu. Ilikuwaje tukimbie na wakati watu wale walikuwa wamekaribia kabisa na mahali pale.

Nilichomwambia ni kwamba tulitakiwa tuendelee kubaki huku tukitaka kuona ni kitu gani ambacho kingeendelea.

Watu wale wakafika, kitu cha kwanza wakaanza kuangalia huku na kule, sisi tukabaki kimya huku tukionekana kuwa na hofu kupita kawaida.

Wakateremka kutoka migongoni mwa farasi wao na kuanza kutuangalia. Hofu...hofu...hofu ilikuwa imenishika sana, sikuamini kama siku hiyo ndio ambayo ningeweza kuonana na baadhi ya watu ambao waliifanya Darfur kuchafuka namna ile.

Machoni mwao, watu wale hawakuonekana kuwa chembe ya huruma, walikuwa watu waliokuwa makini katika kazi zao hasa za umwagaji wa damu. Mavazi yao yalikuwa yakiniogopesha zaidi, kwani yalikuwa na chembechembe za damu ambazo zilionekana kuganda.

“Wewe ni nani?” mwanaume ambaye alionekana kuwa kiongozi aliniuliza.
“Iqram Ibrahim, mwandishi wa habari kutoka Al Jazeera,” Nilimjibu mwanaume yule.
 
SEHEMU YA 31

“Lete kitambulisho chako,” mwanaume yule aliniambia na kwa haraka sana kufanya hivyo, nikamgawia kitambulisho changu.

Watu wote walikuwa kimya, bunduki ambazo nilikuwa nikiziangalia zilikuwa zikinitetemesha kupita kawaida. Moyo wangu ulikuwa na woga mkubwa sana, sikuamini kama mtu yule angeweza kuniacha hai katika kipindi hicho.

Macho yake yalikuwa yakikiangalia kitambulisho kile kwa makini zaidi. Hofu ikanizidi zaidi kwa kuona kwamba endapo angejua kwamba kile kitambulisho kilikuwa ni cha bandia basi angeweza kunipiga risasi pale pale.

“Una bahati,” mwanaume yule aliniambia huku akinirudishia kitambulisho kile.
“Ungekuwa mwandishi kutoka mashirika ya Ulaya au Marekani, ningekuua hapa hapa,” mwanaume yule aliniambia.

Kwa jinsi nilivyokuwa nikijisikia ilikuwa ni balaa, mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi sana, kasi ambayo sikuwahi kuyahisi yakidunda namba hiyo toka nizaliwe.

Muda wote nilikuwa kimya tu, jasho lilikuwa likinichirizika kupita kawaida. Baada ya kutulia kwa kipindi cha dakika kadhaa, nikajipa nguvu upya, nikajiona kama nilikuwa ninatakiwa kufanya kitu kimoja.

“Samahani mkuu,” nilimwambia mwanaume yule huku kila mwanajeshi akiwa amenielekezea bunduki kwa kuona kwamba inawezekana ningemdhuru kwa jinsi nilivyokuwa nimefuata.

“Kuna nini?” aliniuliza huku akionekana kukasirika japokuwa sikuwa nimemkasirisha.

“Nataka kwenda Junaynah,” nilimwambia kwa sauti ya ukakamavu iliyokuwa na woga kwa mbali.
“Kufanya nini?”
“Kukamilisha kazi yangu.”
“Kazi gani?”

“Ya uandishi wa habari,” nilimjibu.
Nahisi Mungu alikuwa upande wangu na alikuwa akinitetea sana. Kabla ya kuongea kitu chochote kile, mwanaume yule akawageukia wenzake na kuanza kuwaaangalia.

Akaamuru mwanaume mmoja anifuate na kuniamuru nipande juu ya farasi wa mtu huyo aliyemuita huku akianza kuongea nae kwa Kisudan, lugha ambayo wala sikuielewa kabisa.

“Huyu mtu atakupeleka mpaka Junaynah,” mwanaume yule aliniambia.
“Ila tupo wawili,” nilimwambia.
“Wawili?”
“Ndio.”
“Na nani?”

“Mtu wa kunishikia kamera,” nilimwambia mwanaume yule ambaye akaamuru mwanaume mwingine aje na farasi na kututaka tuondoke mahali hapo kwani kulikuwa na kazi ambayo alitaka kuifanya.
 
SEHEMU YA 32

Mimi na Majeed tukapanda katika farasi wale wa wale jamaa na kuondoka mahali hapo.

Sikuwa nikiyaamini macho yangu kwamba nilikuwa nimekutana na waasi na mwisho wa siku niliachwa huru. Sikujua ni kitu gani kilitokea nyuma kwani nikaanza kusikia milio ya risasi, wanawake wakaanza kulia kitu ambacho kiliniuma kupita kawaida kwa kuona kwamba watu wale walikuwa wamefanya mauaji ya kuwamiminia risasi baadhi ya watu waliokuwa mahali pale.

Safari ilikuwa inaendelea, safari ilikuwa ndefu sana, tulitumia siku mbili huku tukila mikate ya wanajeshi wale na kuanza kuingia hapo Al Junaynah, sehemu ambayo nilikuwa nikitaka kufika na kisha kufanya kazi yangu rasmi.

Hapa sijui nieseme nini, nadhani kweli hii sehemu ilistahili kukimbiwa na waandishi wa habari, nadhani mji wa Al Junaynah haukuwa mji wa amani hata kidogo, kwa muonekano wake tu ukanifanya nijute safari yangu ya kwenda Darfur….Oooh!

My God! Kwa nini niliamua kwenda Darfur na kuingia ndani ya mji wa Al Junaynah? Nilitamani nipate mbawa na kuruka kurudi nchini Tanzania au kama haiwezekani basi nipotee kama mchawi na kuibukia huko.

Picha ambazo zilikuwa zikionekana huko, kulikuwa na uhalali wa watu kukataa kwenda, nikajisikitikia mimi, nikamsikitia na Majeed pia, nilitamani kumuomba msamaha kwa ushawishi wangu uliomfanya kuelekea Al Junaynah, sehemu ile haikuonekana kuwa na amani kabisa, kama ni filamu, nadhani ilikuwa ni bora ya kuangalia filamu zile za kutisha kuliko yale ambayo nilianza kuyaona hapo Junaynah, mwili ulinisisimka kupita kawaida.

“Mungu nipe nguvu na uniondolee hofu moyoni mwangu” Nilisali kimoyo moyo, sala ambayo ilionyesha kwamba nilikata tamaa ya kuendelea kuishi kwani hali ilikuwa inatisha sana.
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 33

Damu zilitapakaa katika maeneo mbalimbali mahali hapo. Kuta za nyumba zilizojengwa katika eneo ambalo tulilokuwepo zilikuwa na damu nyingi, tena damu mbichi zilionyesha kwamba si muda mrefu watu waliuawa mahali hapo.

Hofu ikanishika moyoni, sikuamini kile nilichokuwa nakiangalia, wakati mwingine nilijiona kama nipo katika usingizi mzito ambao ulisababisha niwe na ndoto moja mbaya na ya kutisha sana.

Maganda ya risasi yalitapakaa katika barabara ambayo tulikuwa tukipita na farasi, mwili ulikuwa ukinitetemeka sana kwamba wakati mwingine nilijutia sababu iliyonifanya kuelekea katika nchi ile kwa ajili ya kutengeneza makala yangu.

Wanajeshi wa waasi walitapakaa kila kona huku wakiwataka watu kuendelea na kazi zao kama kawaida.

Nyuso zao zilionyesha hawakuwa na hofu hata kidogo, kwao, kila kitu kilionekana kitu cha kawaida sana. Tulikwenda na wale farasi mpaka tukafika katika eneo moja lililoanza kuniogopesha.

Ukiachilia mbali damu zilizotapakaa mahali hapo, kulikuwa na viungo vya binadamu barabarani kama mikono, miguu na wakati mwingine mpaka vichwa vya watu waliochinjwa.

Ile ilikuwa picha ya kutisha mno, nilichokifanya ni kuchukua kamera yangu na kuanza kupiga picha huku nikitetemeka kwa hofu na wakati mwingine nikihisi kutapika.

Hapa ningependa kuongea kitu kimoja na nieleweke kwa watu wote wanaosoma haya ninayoandika.
Unaposikia sehemu fulani kuna vita, sikia tu ni vita, muombe Mungu awaepushie na vita hivyo.

Hapo nilipokuwa nilianza kuwaona watu wengine kuwa wapumbavu, baadhi ya Watanzania ambao mara zote wamekuwa wakilalamika na kusema kwamba ilikuwa ni heri vita vya kidini, kisiasa au kikabila viingie nchini ili ijulikane nani bingwa.

Vita si mchezo, unaposikia mwenzako yupo vitani usiombee vikukute. Mambo yalikuwa yakitisha sana, ninakuhadithia haya huku nikitamani kile ambacho nilikuwa nikikiona machoni mwangu basi na wewe ukione.

Tulivyozidi kwenda mbele ndipo tukafika katika eneo moja ambalo lilikuwa na maiti nyingi zilizokuwa zimezagaa hovyo, katika eneo hili, kulikuwa na harufu mbaya na kali sana, harufu ambayo ilinishinda kuvumilia na kuanza kutapika.
 
SEHEMU YA 34

Hapo ndiyo ulikuwa mwisho wa safari yetu. Jamaa wale wakatuambia tushuke kutoka katika farasi wale na kutupeleka kwa baadhi ya wanajeshi wa waasi ambao walikuwa pembeni na kunitambulisha kwamba nilikuwa mwandishi wa habari kutoka katika kituo cha habari cha Kiarabu cha Al Jazeera.

Wakaniomba kitambulisho changu, nikawapa na kuanza kukiangalia.

Nilichogundua ni kwamba wanajeshi wa waasi hawakuwa wakiwapenda kabisa waandishi kutoka katika mashirika ya habari kutoka Uingereza, Marekani au nchi nyingine za Ulaya.

Waliponiona kwamba nilikuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Al Jazeera, wakaamua kuniacha na kunipa saa moja tu ya kufanya kazi mahali hapo.

Nikampa kamera Majeed na kuanza kutangaza kile kilichokuwa kikiendelea pale Darfur.

Sikutangaza kwa amani kwani macho ya wanajeshi wa kundi la waasi walikuwa wakiniangalia kwa mtazamo ambao ulinitia hofu kupita kawaida.

Majeed hakutofautiana na mimi, nae alikuwa akihofia uhai wake, mazingira ya mahali pale hayakuonekana kuwa ya amani kabisa.

Niliendelea na kipindi kile kwa muda wa saa moja, nilikuwa natangaza huku nikionekana kuumizwa na kile kilichokuwa kikionekana mahali pale.

Nilitangaza na kupiga picha huku nikiwaomba wale wanajeshi wa waasi nipige nao picha, wakakubaliana nami jambo lililonifurahisha sana.

Siku hiyo hiyo hatukutaka kubaki mahali hapo, harufu kali na uwepo wa maiti zile ulituogopesha kupita kawaida, hivyo tukaondoka na kurudi Zahor.

Mambo mengi niliyoyataka yakawa yamekamilika na hivyo nilitakiwa kurudi nchini Tanzania huku nikiwa salama kabisa.

Sikutaka kukaa sana Zahor, tukaunganisha safari mpaka baada ya siku nne kufika Al Fashir ambapo tukaunganisha mpaka Nyara. Kwa ujumla tuliendelea na safari ile na baada ya siku sita ndipo tukaingia Khartoum.

Mpaka kufikia hapo niliona mambo mengi na yaliyoniogopesha kupita kawaida.
Nilichokifanya kwa wakati huo ni kuonana na mwandishi mmoja wa habari wa BBC na kumuelezea kila kitu kilichotokea.
 
SEHEMU YA 35

Kwanza alifurahia na pia alihitaji nimuachie makala yangu jambo ambalo wala sikuwa na shaka nalo.

Sijui kwa sababu gani nilitokea kumwamini mwandishi yule aliyejitambulisha kwa jina la Michael Penn, mwandishi wa Shirika la Habari la BBC ambaye nae alikuwa amefika mahali hapo lakini aliogopa kuelekea Darfur kwa sababu ya kuhofia mauaji.

Penn akaniambia kwamba angefanya kila linalowezekana ili nikamilishe kile ambacho nilikuwa ninakitaka katika maisha yangu.

Akanitoa wasiwasi kwa kuongea nami kuhusu mambo mengi na ndio maana hata aliponiambia anataka kwenda na makala yangu nchini Uingereza, wala sikubisha hata kidogo kwa kujua kwamba ni lazima angekuwa ngazi ya mimi kuwa mwandishi mkubwa wa habari.

Baada ya siku moja kukaa hapo Khartoum ndipo nikaanza safari yangu ya kurudi nchini Tanzania huku nikiwa nimemuachia Majeed paundi milioni moja, huku nikimuahidi kuwa nae katika mambo mengi hasa masomo yake.

Ndani ya ndege nilikuwa nikifikiria namna ya kujitetea kwa wazazi wangu kwa uamuzi ambao nilikuwa nimeuchukua wa kutoroka na kuelekea nchini Sudan.

Sikuacha kumfikiria mpenzi wangu, Myra ambaye nafikiri katika kipindi hicho alikuwa na wasiwasi sana juu ya maisha yangu nchini Sudan.

Ndege ile ilichukua zaidi ya masaa sita angani na ndipo ilipotua nchini Tanzania na kisha kuanza kuelekea nyumbani.

Niliingia nyumbani saa kumi na moja jioni. Nakumbuka ile kukutana na mama tu, akaanza kunilalamikia kwa kile nilichokuwa nimefanya.

Wala sikujuta kwani kile nilichotaka kufanya nilikifanya. Mama hakuridhika, akampigia simu baba na kumwambia nilirudi, baba akaacha kazi zake na kuja nyumbani.

“Wewe ni mpumbavu sana,” baba aliniambiwa kwa sauti ya ukali.
“Naomba unisamehe baba.”
“Wewe ni mpumbavu mkubwa Thomas. Kwa nini utoroke nyumbani?” aliniuliza kwa ukali.
 
SEHEMU YA 36

Sikuwa na la kujitetea, nilijua nilifanya makosa kwa ule uamuzi ambao niliuchukua lakini katika kipindi hicho nilijiona kuwa shujaa, shujaa ambaye angeielezea dunia kwa kile kilichokuwa kimetokea.

Kwanza sikutaka kuwaambia juu ya kile kilichokuwa kimetokea kwani hawakuonekana kutaka kunisikiliza.
Siku hiyo nilishinda chumbani na baada ya muda kumpigia simu Myra ambaye alikuja nyumbani na kupitiliza mpaka chumbani kwangu.

Machozi yalikuwa yamejikusanya machoni mwake, hakuamini kuniona nikiwa hai kwa mara nyingine, akashindwa kuvumilia na kunikumbatia.

“Kwa nini ulitoroka?” Myra aliniuliza huku akiwa amenikumbatia.
“Sikuwa na jinsi,” nilimjibu huku nami nikimkumbatia.

Nikajiona kama mwanajeshi ambaye alikuwa amerudi kutoka vitani na ushindi mkubwa na hivyo Myra alitakiwa kunipa zawadi ya ushindi. Ndani ya dakika chache tukawa watupu.

Bado kumbukumbu zangu za Darfur ziliendelea kuwepo kichwani mwangu na hata nilipowaelezea wazazi wangu yale niliyokuwa nimeyaona kule, mama alibaki akilia huku baba aliyekuwa akijifanya mgumu machozi kuanza kumlenga.
Maisha ya Darfur yalikuwa mabaya, yalitisha kupita kawaida.

Machoni mwangu nikawa nimekwishawahi kuiona nchi ambayo ilikuwa ikiteseka kwa ajili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na ndio maana nakuwa na nguvu ya kusimama na kuwaambia kwamba vita ni hatari na kamwe usiombee vitokee nchini mwako.
Maiti za watoto na wanawake ambayo walikuwa wajawazito zilikuwa zikiendelea kujirudia kichwani mwangu.

Sikuweza kusahau kwani mambo yale niliyaona kwa macho yangu na si kuambiwa na mtu, ila yote kwa yote, vita vinatisha na ndio maana sikushtuka nilipoambiwa kwamba kulikuwa na mwanamke alimbeba mbwa mgongoni kwa kudhani alimbeba mwanae na kukimbia nae kwa zaidi ya kilometa kumi na kugundua alimbeba mbwa na si mtoto wake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda mwaka 1994.
“Kwa nini umemuamini tu kirahisi sana Thomas? Au kwa sababu ni Mzungu?”

Baba aliniuliza kuhusu Penn.
“Hapana. Nimemwamini kwa sababu ni mwandishi wa habari wa kimataifa,” nilimjibu.
“Hata kama. Sasa akikimbia nayo?”
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom