Simulizi: Miss Tanzania

Simulizi: Miss Tanzania

MISS TANZANIA
SEHEMU YA 38
MTUNZI 😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Jeneza likashushwa garini na kuingizwa kanisani na kabla ya kuanza kwa ibada ikatolewa tena nafasi nyingine ya kutoa heshima za mwisho kwa wale ambao hawakuipata nafasi hiyo nyumbani.Zoezi hili lililazimika kusitishwa kutokana na idadi kubwa ya watu hivyo .Ibada ilichukua takribani saa moja halafu safari ya kuelekea makaburini kwa ajili ya kuhitimisha safari ya mwisho ya Vero ikaanza.Saa kumi za jioni waliwasili makaburini na ikafanyika ibada ya makaburini na taratibu mwili wa Vero ukashushwa kaburini.Lilikuwa ni tukio lililowafanya watu wengi wapoteze fahamu.Miongoni mwa watu waliopoteza fahamu alikuwa ni Loniki.Hii ilikuwa ni mara ya tatu katika siku hii kupoteza fahamu.Kifo hiki cha Vero kilikuwa kimemuumiza mno.
Familia na watu wa karibu wa marehemu wakatupa udongo kaburini na kisha likaanza zoezi la kulifunika kaburi.Baada ya zoezi lile lililofanywa na mafundi mahiri kukamilika ,yakawekwa mashada ya maua halafu Padre akalibariki kaburi na kisha watu wakatawanyika na kurejea msibani kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine.Safari ya Vero duniani ikafikia mwisho.

ENDELEA………………


“Andrew ninaondoka ,ninahitaji kuonana na Happy jioni hii” akasema Savanna muda mfupi tu baada ya kurejea nyumbani kwa akina Patrick wakitokea katika mazishi ya Vero
“Sawa Savanna.Tutaonana kesho.Patrick anafahamu kama baba yake anazikwa kesho?
“Sina hakika kama anafahamu ,lakini nitamfahamisha nitakapomtembelea kesho asubuhi.”
“Ukionana naye kesho mpe salamu zangu nyingi.Nitakwenda kumtembelea baada ya kumalizika kwa shughuli hizi za msiba wa mzee” akasema Andrew kisha Savanna akaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani kwa akina Happy.
“Kwa kweli hata mimi niliumia sana katika mazishi ya Vero.She was so pretty.Maskini Vero,amekufa na uzuri wake.Happy alistahili adhabu kwa kosa alilolifanya.Sielewi ni kwa nini Patrick ameamua kujitwisha yeye mzigo huu mzito ambao hakuustahili” akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea kwa akina Happy
“Hata hivyo nitamsaidia Patrick kwa kila namna nitakavyoweza na atashinda hii kesi.Ninayafanya haya yote kwa sababu ya upendo wangu kwake.Ninampenda sana Patrick.Toka tulipoamua kusitisha mahusiano yetu baada ya mimi kumpata George ,bado sijaweza kabisa kumtoa Patrick moyoni mwangu.Hii ni nafasi yangu ya kumrudisha tena Patrick kwangu.Nitashinda hii kesi na Patrick lazima awe wangu tena.Happy hastahili kuwa na Patrick tena.” Akaendelea kuwaza Savanna.
Jua tayari lilikwisha punguza nuru yake kuashiria kwamba muda wowote litazama kulipisha giza lichukue nafasi yake.Savanna akafika nyumbani kwa akina Happy akafunguliwa geti na kuingia ndani.Akapokewa na mtumishi wa ndani
“Happy nimemkuta? Akauliza Savanna
“Ndiyo umemkuta.Karibu ndani ngoja nikamuite” akasema Yule msichana na kuelekea chumbani kwa Happy akamtaarifu kwamba Savanna amekwisha fika.Happy akatoka chumbani kwake na kuelekea sebuleni
“Karibu sana Savanna.” Akasema Happy huku akitabasamu
“Nashukuru sana Happy.Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Namshukuru Mungu kwani ninazidi kupata nguvu kila siku”
“Nafurahi kusikia hivyo Happy.Ni jambo la faraja sana kuona hali yako inaboreka siku hadi siku” akasema Savanna.Kikapita kimya kifupi halafu Savanna akasema
“Happy ,nilisikia kwamba umelivua taji la Miss Tanzania..”
“Ndiyo Savanna.Niliamua kulivua taji lile ili kuendelea kulipa heshima yake kwa sababu kila neno baya lilikuwa linasemwa kwa kutanguliwa na miss Tanzania badala ya Happy.Nilifikiria na kuona haitakuwa busara kama taji la miss Tanzania likaendelea kuchafuliwa. Nikaona ni bora nilivue.”
“Pole Happy.Haya yalikuwa ni maamuzi magumu sana”
“Nimekwisha poa Savanna.Sikuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kulirudisha taji lile.” Akasema Happy
“Nimetoka katika mazishi ya Vero.Mimi na Andrew tuliiwakilisha familia ya Patrick katika mazishi.” Akasema Savanna.Happy hakujibu kitu akainama chini
“Happy nimepita mara moja kukuona kama ulivyokuwa umeomba.” Akasema Savanna ,Happy akainua kichwa.
“Samahani Savanna kwa kukusumbua.Ni kweli nilihitaji kuonana nawe kwa maongezi ya muhimu”
Akasema Happy
“Nakusikiliza Happy” akajibu Savanna.Happy akainama kidogo akafikiri na kusema
“Leo nimekwenda kuonana na Patrick gerezani.Tumeongea japo si kwa muda mrefu .Nilijaribu kumuuliza kuhusiana na maendeleo ya kesi na akanitoa wasi wasi na kusema kwamba mambo yote kuhusiana na kesi hii ameyaacha mikononi mwako.Amenihakikishia kwamba wewe ni wakili mahiri na kesi kama hii haiwezi kukusumbua hata kidogo.Kuna kitu aliniambia vile vile kilichonistua kidogo eti kwamba umekataa malipo yoyote na kwamba unaifanya kazi hii bure kabisa.Ni kweli?
Savanna akatabasamu kidogo na kusema
“Ni kweli Happy.Mimi ndiye ninayeisimamia kesi ya Patrick nikishirikiana na mawakili wazoefu toka katika kampuni yangu ya uwakili.Kuhusu malipo ni kweli kama alivyokwambia Patrick.Sihitaji kulipwa hata senti moja.Nimejitolea kuifanya kazi hii bure kwa sababu Patrick ni rafiki yangu mkubwa na wa siku nyingi.Kuna tatizo lolote katika suala hilo? Akauliza Savanna
“Hakuna tatizo Savanna.Nilihitaji tu kupata uhakika toka kwako kwa sababu haikuniingia akilini mtu kusitisha shughuli zake nyingine na kuisimamia kesi hii ngumu bila kuhitaji kulipwa hata shilingi moja.Labda naomba niwe wazi kwako Savanna kwamba moyo wangu hauna amani hata kidogo nikimuona Patrick gerezani.Ninataka kufanya kila linalowezekana ili Patrick ashinde kesi na atoke gerezani na ndiyo maana ninahitaji kuwa na uhakika kuhusiana na mtu anayeisimamia kesi yake.Kwa maana hiyo Savanna kama kuna kiasi chochote cha pesa ambacho ungependa kulipwa usisite kuniambia na nitakupatia.” Akasema Happy.Savanna akacheka kidogo halafu akamtazama Happy na kusema
“Happy mimi na wewe tumekutana na kufahamiana hivi karibuni baada ya kutokea tukio hili hata hivyo nadhani bado haujanifahamu vizuri.Mimi na Patrick tumekutana miaka mingi iliyopita,na tunafahamiana vyema. Sipendi kujisifu lakini mimi ni wakili mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia kesi kubwa na karibu katika kesi zote ambazo tumewahi kusimamia mimi na kampuni yangu hatujawahi kushindwa.Ni kutokana na umahiri huo katika sheria nimeweza kukusaidia hata wewe kuondokana na kesi hii inayomkabili Patrick ambayo ulistahili uibebe wewe.Patrick ananifahamu vizuri na ndiyo maana hakusita kuiweka hatima ya kesi yake mikononi mwangu.Kuhusu malipo bado narudia tena kwamba sihitaji chochote.Ninafanya kazi hii kwa moyo kumsaidia rafiki yangu na si kwa ajili ya kutengeneza fedha.Ninazo pesa za kutosha na hata nikikwambia unilipe kama unavyotaka ,can you afford to pay me 100 millions? Akauliza Savanna akionyesha wazi kukerwa na maneno yale ya Happy.Happy akainama chini.
“Can you pay me 100 milions Happy? Akauliza tena Savanna
“Savanna samahani kama nimekuudhi ,lakini halikuwa kusudio langu kufanya hivyo.Lengo langu nilitaka niwe na uhakika kuhusu utetezi wa Patrick.” Akasema Happy
“One more thing.Who are you Happy? Akauliza Savanna huku sauti yake ikionyesha kuanza kubadilika.Happy akakaa kimya
“You are not even a member of Patrick’s family,….!!” Akasema Savanna.
“Savanna samahani kama kwa kukuuliza vile nimekukera.Niliuliza kwa lengo zuri tu” akajibu Happy
“Happy nimeshangazwa sana na namna ulivyoonyesha wasi wasi kwangu.Umesahau kwamba mimi ndiye niliyesababisha wewe uwe huru mpaka wakati huu na Patrick awe gerezani.” Akasema Savanna halafu akakaa kimya akamtazama Happy
“Kesho asubuhi,nitakwenda kumtembelea Patrick na nitamwambia kwamba najitoa katika kesi hii kwa sababu umeonyesha kutokuniamini nadhani litakuwa jambo la busara kama utaitumia nafasi hiyo kumuweka wakili unayemtaka wewe ambaye atafanya kazi hii kwa malipo tofauti na mimi ambaye sihitaji hata senti moja” akasema Savanna
“Savanna nakuomba usifanye hivyo.Usimweleze chochote Patrick.Atazidi kuumia.Nakuomba sana Savanna usimwambie Patrick chochote.” Akasema Happy
“Happy ahsante sana.Mimi naondoka.Kumbe umenipotezea muda wangu mwingi kwa kuja kunieleza mambo kama haya.!!!! Akasema Savanna huku akiinuka na kutoka mle sebuleni.Happy alikuwa ameinamisha kichwa.
“Bastard !!!..” akasema Savanna kwa hasira baada ya kuingia katika gari lake.
“Sijawahi kudharauliwa hata siku moja kuhusiana na kazi yangu na sipendi mtu aidharau taaluma yangu.Sikuwa nimetaka kukasirika lakini Happy amenikasirisha sana.Yeye ni nani hata anifanyie mahojiano na kuhoji uwezo wangu? akawaza Savanna.
“I will destroy you Happy.nitahakikisha Patrick humpati tena” Akawaza Savanna.

* * *

Baada ya kurejea nyumbani toka katika mazishi ya Vero Loniki hakutaka tena kuongea wala konana na mtu yeyote .Akajifungia chumbani kwake.
“Siyo ndoto tena kama nilivyokuwa nadhani.Ni kweli Vero amekwenda na sintamuona tena.Nilimpenda kupita kiasi na hii ni sababu inayonifaya niumie kiasi hiki.Vero amekufa , amekwenda na uzuri wake.Sintampata tena ndugu kama yeye.Patrick ameniondolea furaha ya maisha yangu na kwa hili sintamsamehe hadi siku naingia kaburini na lazima nihakikishe nimemlipia kisasi mdogo wangu.Kitendo alichofanyiwa na Yule shetani si cha kibinadamu na hakivumiliki hata kidogo na ninaapa kwa miungu yote kwamba lazima yeye na wale wote walioshiriki kumuua ndugu yangu wanalipa.Damu ya Vero haiwezi kupotea bure.They must pay ..!!!!!” akasema kwa hasira Loniki huku akigonganisha mikono yake.Akainuka kitandani akaendea kabatini akachukua pakiti la sigara akachomoa moja na kuanza kuvuta huku akipuliza moshi mwingi hewani.
“Sarah naye lazima atanieleza ni kwa nini kila mara amekuwa mtetezi mkubwa wa Patrick. Hata amediriki kuwaalika watu wake msibani.Anaonekana hana uchungu wowote na kifo cha Vero.Lazima naye nipambane naye.Zile fedha zilizotoka kwa akina Patrick nazo lazima zirudi zilikotoka .Itakuwa ni dhihaka kubwa kuzikubali pesa zilizotoka kwa watu waliomuua ndugu yetu.Sintakubali kamwe fedha zile ziendelee kukaa mikononi mwetu.Kama hawatazirejesha zilikotoka nitazirejesha mimi.” Akawaza Loniki huku akiendelea kuvuta sigara kwa fujo.
“Sintarejea London hadi nihakikishe wale wote walioshiriki katika kumuua Vero wamelipa uovu wao.Lazima walipe.Siihitaji hiyo haki ya mahakama,nitaitafuta haki kwa namna ninayojua mimi mwenyewe.” Akawaza Loniki huku akiendelea kupuliza moshi mwingi wa sigara hewani. Akafungua mlango na kutoka mle chumbani akamtafuta shangazi yake
“Shangazi naomba simu yako kuna mtu nahitaji kuwasiliana naye” akasema Loniki na shangazi yake akampa simu Loniki akarejea chumbani kwake akuchukua kitabu ambacho huandika kumbu kumbu zake mbali mbali akautafuta ukurasa ambao ameandika namba mbali mbali za simu akazipata namba alizokuwa anazitafuta akaziandika katika simu na kupiga
“Hallow Linah,Loniki hapa naongea” akasema Loniki baada ya simu kupokelewa.
“wow ! Loniki.!!....ni wewe kweli? Siamini .Umekuja lini shoga yangu.Na mbona umerudi kimya kimya? Akauliza Linah
“ Linah ina maana hujasikia matatizo yaliyonipata?
“Matatizo !!!.Linah akashangaa
“ Ndiyo Linah.Ina maana huna taarifa zozote?
“Mbona unanistua Lonny? Mimi sina taarifa zozote kwa sababu nimerudi mchana wa leo toka Nairobi kuna mizigo yangu ilikwama pale kwa hiyo sifahamu chochote na wala sijajua kama umerudi.Nini kimetokea Lonny?
“Linah nilipatwa na msiba mzito”
“Msiba !!! Linah akastuka
“Pole sana Lonny.Nani kafariki?
“Vero amefariki dunia !
“Vero !? ..Vero huyu mdogo wako?
“Ndiyo.”
“Acha masihara Lonny.”
“Si masihara Linah.Ni kweli Vero amefariki dunia na ni kifo ambacho kimetangazwa sana na nchi nzima wanajua kama Vero amefariki dunia na jioni ya leo tumetoka kumzika katika makaburi ya Kinondoni.”
Kimya kifupi kikapita.Linah akavuta pumzi ndefu na kusema
“Loniki umenistua sana .Bado siamini kama uliyonieleza ni ya kweli”
“Sikudanganyi Linah.Ni kweli kabisa Vero amefariki dunia.Vero hatunaye tena.”
“Ouh my Gosh !!!”
“pole sana Lonny.Kwa kweli ni msiba mzito sana na wala sina taarifa zozote.Loniki nitajitahidi nifike hapo nyumbani kesho asubuhi kwa sababu kwa sasa niko mbali kidogo ”
“Nitashukuru sana kama ukifika Linah ninahitaji sana kukuona.Nina maongezi nawe ya muhimu sana”
“Usijali Lonny nitafika hiyo kesho bila kukosa.Mpe pole sana mama na Sarah”
“Ahsante sana Linah ,tutaonana hiyo kesho” akasema Loniki na kukata simu,akachukua sigara nyingine katika pakiti na kuiwasha akaendelea kuvuta
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 39
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kimya kifupi kikapita.Linah akavuta pumzi ndefu na kusema
“Loniki umenistua sana .Bado siamini kama uliyonieleza ni ya kweli”
“Sikudanganyi Linah.Ni kweli kabisa Vero amefariki dunia.Vero hatunaye tena.”
“Ouh my Gosh !!!”
“pole sana Lonny.Kwa kweli ni msiba mzito sana na wala sina taarifa zozote.Loniki nitajitahidi nifike hapo nyumbani kesho asubuhi kwa sababu kwa sasa niko mbali kidogo ”
“Nitashukuru sana kama ukifika Linah ninahitaji sana kukuona.Nina maongezi nawe ya muhimu sana”
“Usijali Lonny nitafika hiyo kesho bila kukosa.Mpe pole sana mama na Sarah”
“Ahsante sana Linah ,tutaonana hiyo kesho” akasema Loniki na kukata simu,akachukua sigara nyingine katika pakiti na kuiwasha akaendelea kuvuta

ENDELEA………..

Kumepambazuka Dare es salaam siku mpya imeanza.Pilika pilika katika jiji hili kubwa la kiuchumi nchini Tanzania ziliendelea kama kawaida.Saa tatu za asubuhi ilimkuta Savanna katika gereza la uwangwa kwa ajili ya kuonana na Patrick.Aliwahi sana kufika siku hii ya leo.Kutokana na kufahamika kwake hupewa nafasi ya kuongea na mteja wake katika chumba maalum tofauti na watu wengine ambao hukutana na mahabusu katika sehemu yenye uwazi.
Dakika nane toka aingie mle chumbani mlango ukafunguliwa na Patrick akaingia.
“Hallo Patrick “ akasema Savanna
“mambo vipi Savanna? Akajibu Patrick huku akitabasamu
“Mambo poa Patrick.Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Ahsante sana kwa msaada wako kwani ninapata huduma nzuri hapa gerezani tofauti na mahabusu wengine.Vipi wewe unaendeleaje?
“Mimi pia niko salama Patrick.Nafurahi kama unapatiwa huduma nzuri.Unajua mkuu wa gereza ni rafiki yangu sana na hata viongozi wengi wa gereza hili ninafahamiana nao kwa hiyo ninafurahi kama ombi langu kwao la kuwaomba wakupatie huduma nzuri linatekelezwa” akasema Savanna kikapita kimya kifupi
“Patrick.Unajisikiaje leo?
“Ninajisikia vizuri sana Savanna.Nipe habari za huko duniani” akasema Patrick na kumfanya Savanna acheke kidogo
“Jana tumemzika Veronika.Amezikwa katika makaburi ya Kinondoni.Watu walikuwa wengi mno.” Akasema Savanna halafu Patrick akainama chini.Baada ya sekunde kadhaa Savanna akasema
“Mimi na Andrew tulikuwakilisha wewe na familia nzima katika mazishi hayo ikiwa ni pamoja na kupeleka salamu za rambi rambi kwa niaba ya familia.Tulipewa nafasi ya kusema machache na Andrew akaongea machache.Alitoa salamu za pole kwa niaba yako.”
“Ndugu wa Vero mlifanikiwa kuonana nao?
“Tulionana na Sarah ambaye ndiye amekuwa akitupa ushirikiano mkubwa na alifika hadi nyumbani kwenu kumpa mama pole kwa msiba wa baba.Dada mkubwa wa Vero amekuwa mgumu sana na juzi aliwafukuza Andrew na wazee wengine walipokwenda kushiriki msiba” akasema Savanna
“Please forgive me Vero.I didn’t mean to cause your death” akasema Patrick huku ameinamisha kichwa.
“Patrick leo tunamzika baba .Nasikitika kwamba hutaweza kuhudhuria lakini usijali kwani nitakuwepo kukuwakilisha” akasema Savanna na kukaa kimya akamtazama Patrick.
“Nashukuru sana Savanna kwa taarifa.Hakuna mtu mwingine yeyote ambaye amekuja kunitembelea na kunipa taarifa kuhusiana na na kinachoendelea huko nyumbani.Bila wewe nisingefahamu chochote kuhusu mazishi ya Vero wala baba yangu.” Akasema Patrick kwa masikitiko.
“Patrick,familia yako wala ndugu zako hawajakutenga wala kukutelekeza.Wameshindwa kufika kukutazama kwa sababu wako katika majonzi makubwa hivi sasa.Baada ya kumaliza shughuli za msiba wa baba nina imani watakuwa wakifika hapa mara kwa mara kukujulia hali.” Akasema Savanna
“Anyway,I deserve to be treated this way” akasema Patrick
“Patrick we’re here for you.I’ll always be here for you.Anytime you need a friend,or a shoulder to cry on ,I’ll be here .Maumivu yako ni yangu na ndiyo maana ninakuahidi kufanya kila ninachoweza ili kuhakikisha kwamba unashinda kesi hii.Tafadhali usijihisi mpweke Patrick”
“Nashukuru sana Savanna.Toka nimepatwa na matatizo haya umekuwa ni mtu pekee ambaye uko nami kila siku.Wewe ndiye mfariji wangu .Sina cha kukulipa Savanna kwa wema huu wote ulionitendea.Mungu atakulipa.” Akasema Patrick
“Patrick ninayafanya haya yote kwa sababu wewe ni rafiki yangu na mtu wangu wa muhimu sana.Halafu kuna kitu nimekumbuka Patrick”
“Kitu gani Savanna?
“Jana nilikwenda kuonana na Happy baada ya kutoka katika mazishi ya Vero.Alinipigia simu na kunitaka nionane naye kuna jambo anataka kunieleza.Nilishangazwa sana na Happy kuonyesha wasi wasi wa mimi kuisimamia kesi yako.Anaonekana hana uhakika kama ninaweza kuisimamia kesi hii hadi mwisho.Anyway sitaki kuliongelea sana suala hili nilitaka tu ufahamu na umwambie kwamba awe mkimya na awe mfuatiliaji mzuri wa kesi na si mtoa maamuzi.” Akasema Savanna.Patrick akamtazama na kusema
“Savanna ,samahani sana kama kuna maneno yoyote aliyoyatamka Happy yakakuudhi kiasi hicho.Ni kweli jana alifika hapa na aliniuliza kuhusu mwenendo wa kesi nikamwambia kwamba mambo yote kuhusiana na kesi nimeyaacha mikononi mwako.Sikutegemea kama angekutafuta na kukuuliza kuhusu suala hili.Savanna wewe ni zaidi ya rafiki,naomba usimsikilize Happy kwa lolote.Tafadhali nakuomba usiache kunisaidia katika kesi hii.Without you I’m finished.I need you now more than ever” akasema Patrick.Savanna akaishika mikono ya Patrick.
“Patrick hakuna binadamu yeyote katika hii dunia ambaye anaweza kunizuia mimi nisikutetee katika hii kesi.I’ll get you out of here .I’ll make sure you are free.Believe me” akasema Savanna.
“Ninakuamini Savanna.” Akajibu Patrick.
“Ahsante sana Patrick.Kilichonileta hapa siku hii ya leo ni kukujulia hali na kukupa taarifa za kinachoendelea nyumbani.Nitakuja tena kesho” akasema Savanna.
“Savanna nakushukuru kwa kuja kunitembelea na kunipa taarifa za mazishi ya baba na Vero.Naomba usiache kuja kunitembelea kwani wewe ndiye mfariji wangu mkuu kwa sasa” akasema Patrick.
“Usijali Patrick,hapa ni kama nyumbani na nitakuwa nikija kila siku kujua maendeleo yako.Sintaacha kukutembelea hadi siku nitakayohakikisha kwamba umekuwa huru” akasema Savanna akaagana na Patrick na kuondoka
“Ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumrejesha Patrick katika mikono yangu lazima kuifuta taswira ya Happy katika akili ya Patrick.Lazima niichafue picha nzuri ya Happy kichwani mwa Patrick na hapo ndipo nitakapokuwa na uhakika kwamba ninaweza kumpata Patrick tena.Najua si rahisi lakini ninatakiwa kufanya kitu kimoja tu.I have to make him hate her” akawaza Savanna na kutabasamu.

* * * *

Saa mbili na dakika ishirini za asubuhi , gari moja dogo la kifahari likawasili nyumbani kwa akina Vero na akashuka mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa gauni refu jeusi na kichwani alijitanda mtandio mweusi na kuvaa miwani mikubwa myeusi kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua kwa haraka.Huyu alikuwa ni Linah rafiki mkubwa wa Loniki.Mara tu aliposhuka katika gari Loniki akatokea na kukumbatiana naye.Linah akashindwa kujizuia akaanza kuangua kilio kikubwa.na kumfanya Loniki naye aanze kulia.
Baada ya kulia kwa takribani dakika kumi,Loniki na Yule mwanadada ambaye ni rafiki yake kipenzi na wa siku nyingi wakanyamza kisha Linah akaitumia nafasi hiyo kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki waliokusanyika hapo nyumbani wakiendelea na matanga.Kisha toa mkono wa pole,Loniki na Linah wakaelekea bustanini.Loniki akamuacha Linah pale bustanini ,akarejea chumbani kwake na kuchukua chupa ya mvinyo pamoja na glasi mbili bila kusahau pakiti yake ya sigara .Akarejea bustanini alikomuacha Linah na kumimina mvinyo katika glasi ,akawasha sigara na kupuliza moshi mwingi hewani.
“Bado hujaacha kuvuta sigara Lonny? Akauliza Linah.Loniki akapuliza tena moshi mwingi hewani na kusema.
“Siwezi kuacha kuvuta sigara Linah.Nimeanza kuvuta sigara nikiwa shule ya msingi na siwezi kuacha sasa hivi.Vipi wewe huvuti tena?
“Hapana Lonny,niliacha kuvuta sigara muda mrefu .nilipatwa na tatizo la kifua nikashauriwa kuachana na sigara.” Akasema Linah halafu kikapita kimya kifupi.Loniki bado aliendelea kunywa mvinyo na kuvuta sigara
“Lonny pole sana shoga yangu kwa msiba huu mkubwa.Bado siamini kama ni kweli Vero amefariki dunia.Usiku kucha nilikuwa nikitafakari kuhusu suala hili kama ni kweli au ulikuwa unanitania.Hapa nilipo mwili unanitetemeka sana,nimestuka mno” akasema Linah
“Ni vigumu kuamini Linah lakini ukweli ni kwamba Vero hatunaye tena.Jana tumempumzisha katika nyumba yake ya milele.Hata mimi bado inaniwia ugumu kuamini kwamba sintamuona tena Vero.Tabasamu lake ,ukarimu na ucheshi wake hatutaviona tena.Inauma sana Linah.Inauma sana” akasema Loniki huku akilengwa na machozi.Akachukua glasi yake ya mvinyo na kupiga funda kubwa halafu akawasha sigara nyingine.Linah ambaye naye alikuwa anafuta machozi akamtazama shoga yake na kusema
“Lakini Lonny hebu nieleze kifo cha Vero kimesababishwa na nini? Alikuwa anaumwa? Nakumbuka mara ya mwisho kuonana naye ni wiki tatu zilizopita.Nilimuomba afike dukani kwangu ili kuchukua mchango wa harusi kwa sababu nilikuwa na safari ya kwenda Dubai.Alifika dukani kwangu nikaonana naye na kumpatia mchango na akaniahidi kuniletea kadi ya harusi.Taarifa za kifo chake cha ghafla zimenistua sana” akasema LInah
“Linah dunia hii imejaa watu makatili hakuna mfano.Wamemkatili uhai mdogo wangu.Vero hakupaswa kufa mapema namna hii.” Akasema Loniki
“Ina maana Vero ameuawa? Nani hao wamefanya kitendo hicho cha kinyama?
“Ilikuwa ni siku ya pili toka aliporejea nchini akitokea London alikokuja kufanya manunuzi ya harusi yake.Kwa mujibu wa maelezo niliyopewa ni kwamba aliporejea toka London alikwenda kumtembelea mchumba wake na kushinda huko na baadae jioni wakaelekea nyumbani kwa wazazi wa Patrick kulikokuwa na kikao.Baada ya kufika huko kikaoni Patrick akasimama na kuanza kueleza mambo ambayo ni upuuzi mtupu na baadae akatangaza kwamba ameuvunja uchumba kati yake na Vero.” Akasema Loniki
“What .!!!! Linah akashangaa
“Usistuke Linah.Dunia hii imejaa watu makatili mno.Baada ya tangazo hilo la kuuvunja uchumba,watu wengi walianguka na kupoteza fahamu.Kwa mujibu wa mashuhuda ,baada ya kitendo kile Vero alipotea na haikujulikana alikwenda wapi.Baba mzazi wa Patrick ambaye naye amefariki dunia jana alikimbizwa hospitali kwa shinikizo la damu.Wakiwa hospitali walikompeleka baba yao,Patrick na kahaba wake ambaye inasemekana ndiye chanzo cha kuachana na Vero walishangaa kumuona Vero ametokea ghafla akiwa na bastora.Ulitokea ugomvi na Patrick akataka kumnyang’anya Vero bastora na aliposhindwa akaamua kumsukuma Vero akajigonga ukutani na kupoteza maisha.Wamemuua mdogo wangu ,wamemfanyia ukatili mkubwa” akasema Loniki.Linah akavuta pumzi ndefu
“Pole sana Lonny .Kwa kweli ni jambo la kuhuzunisha sana.Siamini kama ni kweli Patrick amemfanyia hivi Vero.Ni kwa nini amefanya hivi?
“Ni kwa sababu alimpata mwanamke mrembo ambaye ni miss Tanzania,akamuona Vero hafai tena.”
“Yaani Patrick aliamua kumuacha Vero kwa sababu ya Miss Tanzania? Akauliza Linah
“Huu ni ukatili mkubwa na hauvumiliki hata kidogo.” Akasema Linah kwa hasira
“Ni ukatili mkubwa sana Linah.Vero amekufa na uzuri wake.Hakuwa hata na mchubuko.” Akasema Loniki
“Patrick yuko wapi? Amekwisha kamatwa? Akauliza Linah
“Anashikiliwa na jeshi la polisi.Tayari kesi yake imekwisha tajwa mahakamani.” Akajibu Loniki
“Afadhali kama amekamatwa.Haki itatendeka kwani siku hizi mahamaka zimeboreshwa na mashauri yanaharakishwa sana.lazima ahukumiwe kutokana na kosa alilolitenda.Anastahili kifungo kirefu gerezani au ikiwezekana hata kifo” akasema Linah
“No Linah.!!....mimi sihitaji hiyo haki ya mahakama.Sina huo muda wa kusubiri haki itendeke baada ya miaka miwili.Isitoshe siviamini vyombo vya kutoa haki.Ni watu wangapi wametenda makosa makubwa na hata mauaji lakini bado tunawaona mtaani? Hakuna awezaye kuufahamu uchungu nilinao moyoni mwangu” akasema Lonny
“Kwa hiyo umepanga kufanya nini Lonny?
“Ndiyo maana nimekuita Linah.Kuna mambo nataka unisaidie”
“Sema chochote Lonny.Mimi niko tayari kukusaidia.” Akasema Linah.Lonny akanywa funda moja la mvinyo na kusema
“Linah nataka kutafuta haki kwa namna ninayojua mimi mwenyewe.Nataka wale wote waliohusika kwa namna yoyote ile na kifo cha mdogo wangu Vero walipe uovu wao kabla mdogo wangu hajaoza kaburini.They all must pay” akasema Loniki halafu akatoa sigara nyingine na kuiwasha akavuta na kumgeukia Linah
“Linah wewe ni rafiki yangu mkubwa toka shule ya msingi na hadi leo hii umeendelea kuwa mshirika wangu wa karibu.Nina imani utakuwa nami katika hili ninalotaka kulifanya kwani naamini hata wewe ulimpenda Vero kama mdogo wako pia” akasema Loniki
“Lonny wewe ni zaidi ya rafiki.Niko nawe katika kila jambo.Vero alikuwa ni mdogo wetu sote na kifo chake kimeniumiza sana kama kilivyokuumiza wewe.Niambie umefikiria kufanya nini?
“kama nilivyokueleza Linah kwamba ninataka kuitafuta haki mimi mwenyewe.Nataka unisaidie kutafuta mtu ambaye ataifanya kazi ya kulipa kisasi kwa wale wote waliohusika na kifo cha Vero.Wa kwanza kushughulika naye ni huyu msichana miss Tanzania ambaye ndiye chanzo cha Patrick kumuacha mdogo wangu na ndipo nimgeukie Patrick.” Akasema Lonny
Linah akavuta pumzi ndefu,akachukua glasi ya mvinyo akanywa kidogo halafu akasema
“Unataka huyu Happy ashughulikiwe vipi?
“Ninataka kwanza ateseke sana kabla ya kumuondoa katika uso huu wa dunia.”
“Unaposema kumuondoa duniani unamaanisha kumuua ? akauliza Linah
“Exactly..!!!!!Ninataka baada ya kupatwa na mateso makali hatimaye auawe halafu Patrick afuate.wakisha uawa watu hawa ndipo roho yangu itakapotulia.Kwa vile wao pia waliutoa uhai wa Vero basi nao hawana budi kutolewa uhai wao.Je tuko pamoja katika hili? Akauliza Loniki
“Tuko pamoja Lonny.Siwezi kukuacha katika suala hili japokuwa si suala rahisi na linahitaji umakini mkubwa sana.”
“nalifahamu hilo Linah na ndiyo maana nimekuita ili tuongee na kuweka mikakati mizito.Nina hakika suala hili haliwezi kutushinda hata kidogo.Nimekwisha weka nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba hawa wote waliohusika na kifo cha Vero wanalipa. Damu ya mdogo wangu haiwezi kupotea bure.Lazima nimlipie kisasi” akasema Loniki
“Lonny utakuwepo hapa nchini kwa muda gani? Akuliza Linah
“Sintaondoka hapa hadi nitakapohakikisha kwamba Patrick na Happy wamelipa uovu wao”
“Basi itakuwa vyema kama utaendelea kuwepo nchini kwa muda mrefu zaidi”
“Ndiyo Linah nitakuwepo hapa nchini kwa muda mrefu tu.Ninachokihitaji ni mtu wa kuweza kuifanya kazi hii kwa umakini mkubwa na ufanisi.Ni kazi ambayo haihitaji aina yoyote ya makosa.Ninajua unafahamiana na watu wengi wa hapa mjini ambao wanaweza kuifanya kazi hii.”
“Usijali Lonny kuhusu hilo.Mimi nitalifanyia kazi hilo suala na ……………….” Kabla hajendelea zaidi mara akatokea shangazi yake Loniki.Mama huyu amekuwa rafiki mkubwa wa Loniki na amekuwa akimuunga mkono katika kila jambo ambalo Lonny analifanya.Hii imepelekea awe akipokea misaada mingi toka kwa Loniki.
“Loniki kikao cha ndugu kinataka kuanza,unaombwa uwe karibu..”
“Sawa shangazi.Ninakuja sasa hivi” akasema Loniki
“Linah twende katika kikao” akasema Loniki
“Hapana Lonny.Kikao hicho kinawahusu wanandugu pekee”
“Toka lini umeacha kuwa ndugu yangu Linah ?Twende tukahudhurie kikao halafu tutaendelea na maongezi yetu”akasema Loniki halafu wakainuka na kuelekea kikaoni.
Karibu ndugu wote walikuwa wamejikusanya kwa ajili ya kikao cha kuhitimisha shughuli za msiba na kutoa ruhusa kwa watu waliotoka mbali kuondoka.Ni mtu mmoja tu ambaye alikosekana katika kikao hiki.Ni sarah.Akatumwa mtu mmoja kwenda kumtafuta nyumba nzima lakini hakuwepo na hata gari lake halikuwepo.Shangazi yake akajaribu kumpigia simu lakini simu ilikuwa inaita bila kupokelewa.
“Simu yake inaita bila kupokelewa” akasema
“hakuna haja ya kumsubiri.Tuendeleeni na kikao” akaamuru Loniki na wote wakakubaliana naye kikao kikaanza
“Najua mahali alikoelekea Sarah.Huyu naye lazima nipambane naye.Ngoja kwanza tumalize msiba nitamfundisha adabu ” akawaza Loniki wakati kikao kikiendelea.
Sarah akiwa garini simu yake iliita akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni shangazi yake.Hakupokea akaiweka chini.
“Najua wananitafuta kwa ajili ya hicho kikao chao.Watanisamehe kwani sintahudhuria kikao hicho.Lazima nihudhurie mazishi ya baba yake Patrick.Nataka upendo na amani vidumishwe baina yatu na si kujenga chuki na hasama.Nawashangaa sana ndugu zangu kwa kumuunga mkono Loniki kwa kila atakachokisema hata kama hakina msingi wowote.Kwa sasa karibu wote wanamuunga mkono kuhusu kulipa kisasi wa Patrick .Nafikiri ni kwa sababu anaishi ulaya na misaada anayowatumia mara kwa mara imewafanya wamsikilize na kumfuata kwa kila jambo atakaloliongea na kumfanya awe ni mtu mwenye sauti katika familia na ukoo .Mimi sintakubaliana kwa namna yoyote ile na upuuzi ambao Loniki anaufanya.Vero alikuwa ni ndugu yetu sote na sote tumeguswa na kifo chake na hapo hapo yatupaswa tukumbuke kwamba hata yeye vero alikuwa na makosa tena makubwa ,na ndiyo chanzo cha haya yote yaliyotokea.Huu ni ukweli ambao hatupaswi kuona haya kuusema.Ninapenda kuona maisha yakiendelea kama awali na sipendi kuona familia zetu zikiingia katika mzozo mwingine.Patrick anashikiliwa na vyombo vya dola na vitafanya uchunguzi na endapo atathibitika kwamba ana makosa basi atapewa adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi” akawaza Sarah akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa akina Patrick kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Patrick
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 40
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mimi sintakubaliana kwa namna yoyote ile na upuuzi ambao Loniki anaufanya.Vero alikuwa ni ndugu yetu sote na sote tumeguswa na kifo chake na hapo hapo yatupaswa tukumbuke kwamba hata yeye vero alikuwa na makosa tena makubwa ,na ndiyo chanzo cha haya yote yaliyotokea.Huu ni ukweli ambao hatupaswi kuona haya kuusema.Ninapenda kuona maisha yakiendelea kama awali na sipendi kuona familia zetu zikiingia katika mzozo mwingine.Patrick anashikiliwa na vyombo vya dola na vitafanya uchunguzi na endapo atathibitika kwamba ana makosa basi atapewa adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi” akawaza Sarah akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa akina Patrick kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Patrick.

ENDELEA……………..

Msafara wa magari ukitokea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kuuchukua mwili wa baba mzazi wa Patrick ,uliwasili nyumbani kwa marehemu na kulifanya eneo lote ligubikwe na vilio.Wengi wa waombolezaji walikuwa wamevaa fulana zenye picha ya marehemu.Taratibu jeneza likashushwa toka ndani ya gari na kuingizwa ndani .
Taratibu zikafanyika na zoezi la kutoe heshima za mwisho likaanza.Watu walikuwa ni wengi sana na zoezi lilichukua muda mrefu tofauti na ilivyotazamiwa.Baada ya zoezi la kutoa heshima za mwisho kukamilika zikafuata salamu za rambi rambi toka sehemu mbali mbali,zoezi lililotanguliwa na kusomwa kwa wasifu wa marehemu.Salamu nyingi za rambi rambi zilitolewa.Toka serikalini ,watu binafsi,mashirika ya umma n,k.Wengi walionyesha kuguswa na msiba huu .Mzee huyu alikuwa ni kipenzi cha wengi na alikuwa na heshima ya kipekee katika jamii.
Salamu za rambi rambi zikamalizika na hivyo kutoa nafasi kwa ratiba nyingine kuendelea.Mwili wa marehemu ukapakiwa garini na kuelekea kanisani kwa ajili ya ibada.Kanisa lilifurika watu waliokuja kumsindikiza mzee huyu katika safari yake ya mwisho.Ibada iliyoongozwa na msaidizi wa askofu wa jimbo kuu la dare s salaam ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa mzee huyu ilimalizika na msafara ukaelekea makaburini kwa ajili ya mazishi.Watu walikuwa ni wengi sana
Hatimaye ilipotimu saa kumi za jioni safari ya mwisho ya baba yake Patrick ikahitimishwa pale ambapo jeneza lililobeba mwili wake liliposhushwa kaburini.Baada ya familia,ndugu na wawakilishi wa makundi mbali mbali kutupia mchanga katika kaburi,hatimaye zoezi la kufukia likaanza.
Askofu mkuu msaidizi akalibariki kaburi na huo ukawa mwisho wa shughuli nzima ya mazishi.Waombolezaji walitawanyika na wengine wakarejea nyumbani kwa marehemu ili kuendelea na ratiba nyingine.

* * * *

Saa kumi na mbili za jioni Sarah akawasili nyumbani kwao akitokea katika mazishi ya baba mzazi wa Patrick.Mara tu alipowasili akakutana na dada yake Loniki akiwa amesimama nje ya nyumba akiwa na rafiki yake Linah.
“Linah amekuja lini? Sijamuona kitambo kirefu.Mmmhhh !!! ninaanza kupatwa na wasi wasi.Loniki akikutana na Linah.Ninamfahamu Linah ,sifa yake si nzuri hata kidogo.Imewahi kusikika kwamba anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.Si mtu mzuri huyu hata kidogo na kwa namna anavyoonekana akiongea na Loniki ninahisi kuna jambo wanalipanga.Kwa jinsi ninavyomfahamu Loniki najua lazima atataka kumshirikisha Linah katika mipango yake ya kulipiza kisasi.” Akawaza Sarah halafu akashuka garini na kwenda kuwasalimu.
“Sarah …Pole sana jamani .Pole sana kwa msiba.Mimi sikuwa nafahamu chochote hadi Lonny aliponipigia simu na kunifahamisha .Nimeumizwa sana na kifo hiki cha ghafla cha vero” akasema Linah
“Ahsante Linah tumekwisha poa.Ni mapenzi ya Mungu.Habari za siku nyingi?
“Habari nzuri Sarah.Nimekuwa na safari nyingi hivi sasa ndiyo maana hatuonani .”akasema Linah.Loniki ambaye alikuwa amesimama pembeni akasema
“Sarah mbona hukuhudhuria kikao cha wana ndugu? Ulikuwa wapi?
Sarah akamtazama dada yake bila kumjibu kitu halafu akamgeukia Linah.
“Linah nashukuru sana kwa kufika kwako katika msiba huu.Nikipata wasaa nitafika dukani kwako kuangalia bidhaa mpya”
“Unakaribishwa sana Sarah tena kuna mzigo mpya umewasili.”
“Ok Linah nitafika” akasema Sarah halafu akaelekea ndani akawaacha Lonny na Linah wakiendelea na mazungumzo yao
“Kwa hiyo Linah naomba ulipe uzito unaostahili suala hili.Usijali kuhusu pesa.Ukisha wapata watu wanaoweza kuifanya kazi hii naomba unifahamishe mara moja .Yule hayawani anategemea kupandishwa tena kizimbani jumatano ijayo kwa hiyo sitaki mambo haya yachukue muda mrefu”
“Usijali Loniki.Nitajitahidi kuifanya hiyo kazi .kama nilivyokwambia awali kwamba suala hili ninalipa uzito mkubwa sana na ninakuhakikishia kwamba ndani ya muda mfupi nitakuwa nimewapata watu wanaoweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi” akasema Linah halafu wakaagana akaondoka.Baada ya kuachana na Linah,Loniki akaelekea moja kwa moja hadi katika chumba ambacho Sarah allikuwa amekaa na mama yake pamoja na akina mama kadhaa,akamuita Sarah na kumuomba wakaongee nje
“Ile ni tabia gani uliyoionyesha mbele ya Linah? Akauliza Loniki
“Tabia gani?
“Nilikuuliza ulikuwa wapi toka asubuhi,hukunijibu kitu na badala yake ukanitazama kwa dharau.”
“Sikuwa na jibu la kukupa kutokana na swali uliloniuliza.Mimi nina masuala yangu na shughuli zangu nyingi tu na anayepaswa kuniuliza swali kama lile ni mume wangu pekee na si mtu mwingine yeyote”
“Kwa maana hiyo hukuona umuhimu wa kuwepo katika kikao cha familia leo? Akauliza Loniki
“Kwani kukosekana kwangu kumeharibu kitu? Au kuwepo kwangu kungebadili kitu? Akasema sarah.Loniki akamuangalia kwa macho makali
“Kuwa makini Sarah na hayo majibu yako yaliyojaa dharau.Mimi ni dada yako na hupaswi kunijibu namna hiyo”
“Si dharau Loniki,ninakueleza ukweli kwa sababu toka umefika hapa umekuwa ndiye mwenye kutoa amri ya kufanyika kila unachopenda.Kwa taarifa yako Loniki ,mimi siko tayari kukunyenyekea eti kutokana na fedha zako au kwa sababu unaishi nje ya nchi.Nina maisha yangu mazuri tu na mume wangu na sihitaji kumsujudu mtu.Kama utaniheshimu nami nitakuheshimu pia lakini kama hutaniheshimu basi hata mimi sintakuheshimu” akasema Sarah.
Loniki akakunja uso na kumuangalia Sarah kwa hasira
“Nasikitika sana Sarah kwa namna ambavyo umeonyesha kutokuguswa na kifo cha mdogo wako.Nafahamu kabisa ulikuwa katika mazishi ya baba yake Patrick mtu ambaye alimuua mdogo wako kwa makusudi kabisa.Huna aibu hata kidogo” akafoka Loniki.
“Ni kweli nimetoka kumzika baba yake Patrick.Mimi sina roho ya kikatili kama uliyonayo wewe.Hakuna mtu anayepaswa kulaumiwa kwa kilichotokea.Hakuna mtu aliyetegemea mambo haya yangefika hapa yalipofika.nafahamu kwamba umedhamiria kulipiza kisasi kwa Patrick,nakuonya usifanye hivyo.Viachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.” Akasema Sarah
“ Stupid !!!!!.akasema loniki kwa ukali
“Sarah wewe ni mdogo sana na huna nafasi yoyote ya kunizuia kufanya chochote.Mimi ndiye niliyeguswa na kifo cha Vero,wewe huonyeshi kuguswa hata kidogo.Kwa maana hiyo ninakuhakikishia kwamba sintafumba macho hadi nihakikishe kwamba wale wote waliohusika katika kusababisha kifo cha Vero wamelipa.Hata wewe kama utaamua kuungana na mashetani hawa,nitapambana nawe vile vile.” Akasema Loniki kwa ukali na kuondoka kwa kasi akaelekea ndani.
“Siko tayari kumtukuza Loniki na kumuacha afanye kila anachotaka kukifanya.Japokuwa ni ndugu yangu lakini niko tayari kupambana naye endapo atafanya jambo lolote lisilokuwa zuri kwa Parick,familia yake au Happy” akasema Sarah huku naye akipiga hatua kuingia ndani

* * * *

Ni saa tano za usiku bado Loniki amekaa kitandani.Juu ya meza ndogo iliyo pembeni ya kitanda kulikuwa na chupa ya mvinyo.Chumba kilikuwa kimejaa moshi wa sigara kutokana na kuvuta sigara mfululizo.
“Sarah amenichefua sana siku ya leo.Ninasema nitamuonyesha kwamba mimi ni mkubwa kwake,kiumri ,kifedha na hata kiuwezo.majibu aliyonijibu jioni ya leo yalijaa dharau kubwa sana.Hapana sintakubali kudharauliwa na mtu kama sarah.lazima nim……………………..” akakatisha mawazo yake baada ya mtu kugonga mlango wa chumba chake..Akainuka na kwenda kuufungua.Alikuwa ni shangazi yake.
“Ouh Shangazi karibu “ akasema Loniki
“Ahsante Loniki.Linah amepiga simu na anahitaji kuongea nawe.” Loniki akachukua simu na kuufunga mlango kisha akampigia Linah
“Loniki kuna habari njema nataka kukupa” akasema Linah baada ya kupokea simu.
“Habari gani hizo Linah”
“Tayari nimempata mtu ambaye unamuhitaji kwa ile kazi”
“wow !!..hizo ni habari njema sana.Hebu nipe taarifa zaidi“ akasema Loniki kwa furaha
“Mtu huyo anaitwa Khumalo.Ni mtaalamu na ana uzoefu mkubwa na shughuli hizi.Ni mtu anayeaminika kwa uwezo wake wa kufanya kazi za namna hii.Tayari nimekwisha ongea naye na amenihakikishia kwamba yuko tayari kuifanya kazi hii.Amekataa kutaja kiwango cha pesa anachokihitaji hadi hapo atakapokutana nawe na akapata maelezo ya kina toka kwako.Amenihakikishia kwamba anao uwezo wa kumshughulikia hata mtu ambaye yuko gerezani kutokana na kuwa na mtandao mpana.Kwa hiyo ametaka siku ya kesho tukutane naye ili tuweze kuangalia namna tutakavyoweza kuutekeleza mpango wenyewe” akasema Linah
“Nashukuru sana Linah kwa msaada wako huu mkubwa.Kesho tutaonana muda gani na huyo khumalo?
“Njoo saa nne ofisini kwangu halafu yeye atatuelekeza mahala pa kumkuta.Yeye si mtu wa kuonekana hovyo hovyo”
“Ok Linah.Nitakuja dukani kwako hiyo kesho saa nne” akasema Loniki halafu akaagana na Linah.
“lazima Patrick na Happy walipe damu ya ndugu yangu.Nataka wao pia wapate maumivu kama ninayoyapata mimi hivi sasa.” Akawaza Loniki huku akiuma meno kwa hasira halafu akachukua glasi ya mvinyo akapiga funda kubwa.

* * * *

Ni saa sita na dakika kumi za usiku,siku mpya imekwisha anza.Bado Savanna yuko macho .Licha ya kuhisi macho mazito na kulemewa na usingizi lakini bado alikuwa ameinamia vitabu vyake vya sheria akiendelea kupitia mambo mbali mbali ya kisheria ambayo yangeweza kumsaidia katika kesi inayomkabili Patrick
Alizidi kulemewa na usingizi,taratibu akainuka na kuelekea jikoni akatengeneza kahawa na kurejea tena katika chumba chake cha kusomea akaendelea na kazi yake.Alipokaa tu ,simu yake ikaanza kuita.Akaichukua na kutazama mpigaji ,alikuwa ni George.Akakunja uso na kuitupa simu pembeni.
“Huyu mwanaume anatafuta kitu gani kwangu? Kwa nini hataki kuelewa kwamba mimi na yeye basi? Nimekwisha mweleza kwamba sihitaji mawasiliano yoyote naye lakini hataki kunisikia.? Akawaza Savanna.Simu ikaendelea kuita akaamua kuipokea.
“Hivi wewe ni mtu gani ambaye hutaki kuelewa? Nimekwisha kuambia kwamba sitaki mawasiliano yoyote na wewe.George naomba usinisumbue tafadhali.Stay away from me and my life” akasema Savanna kwa ukali
“Ouh Savanna yaani kutengana siku hizi chache umenichukia na hutaki hata nikusalimie? Nimeshindwa kulala bila kuisikia sauti yako.Hebu niambie mpenzi wangu unaendeleaje?” akasema George kwa sauti ya taratibu na kuzidi kuchukiza Savanna
“George tafadhali naomba usiendelee kunisumbua nina kazi nyingi za maana za kufanya.Naomba hii iwe ni mara yako ya mwisho kunipigia simu.” Akasema kwa ukali Savanna
“Oooh Savanna ,naomba tafadhali usikate simu.Najua una kazi nzito ya kufanya kwa ajili ya kumsaidia Patrick ambaye ndiye mwanaume pekee unayemuota usiku na mchana.Naomba ufahamu kwamba jitihada zote unazozifanya ili uwe na Patrick ni kazi bure.Hutaipata hiyo nafasi.Unaelewa ni kwa sababu gani huwezi kuipata hiyo nafasi. Ni kwa sababu Patrick hakupendi.He’s just using you.Pamoja na hayo naomba niweke wazi kwamba mimi ndiye mwanaume wako wa pekee na hutapata mwanaume mwingine zaidi yangu.Ninakupenda kuliko wanaume wote wa dunia hii na nitahakikisha ninakuwa nawe katika maisha yangu yote.Kwa maana hiyo nitahakikisha lengo lako la kutaka kuwa na Patrick halifanikiwi hata kidogo..Nitafany………..”
“Stupid !!!!!!!!!..” Savanna akasema na kukata simu kwa hasira.
“Huyu mwanaume ana akili zote kweli? Yeye ni nani wa kuweza kunizuia mimi nisitekeleze mipango yangu? Ni Mungu pekee ambaye anaweza kunizuia mimi kuwa na Patrick.Hakuna mwanadamu anayeweza kunizuia.Nitahakikisha Patrick anakuwa huru na anakuwa wangu .” akasema Savanna halafu akainamia vitabu vyake.

* * * *

Saa sita za mchana iliwakuta Linah na Loniki katika jumba la kifahari linalomilikiwa na Khumalo.Tayari mlinzi alikwisha pewa taarifa ya ujio wao hivyo akawaruhusu kuingia ndani bila matatizo.Muhudumu aliyekuwa amevaa suti nzuri nyeusi akawapokea na kuwaongoza hadi katika sebule moja kubwa yenye nakshi na samani za kupendeza sana
“Wow !! Inaonekana huyu jamaa ni mtu mwenye kujiweza sana” akanong’ona Loniki baada ya kuviona vitu mbali mbali vya thamani ndani ya sebule lile kubwa.Linah akatabasamu hakujibu kitu.Muhudumu akawakirimu kwa vinywaji wakati wakiendelea kumsubiri Khumalo.
Baada ya dakika zipatazo kumi toka wamefika ,kijana mmoja mwembamba ,mrefu aliyevaa suti iliyomkaa vyema akaingia mle sebuleni.Mara tu alipokutanisha macho yake na Linah,kijana yule akaachia tabasamu pana sana.Linah naye akatabasamu halafu akainuka pale sofani wakakumbatiana.
“Ouh Linah..I missed you so much” akasema Yule kijana
“Its been a long time khumalo.’ Akasema Linah.Loniki akatabasamu alipogundua kwamba Yule kijana ndiye Khumalo.
“Habari yako Linah” akasema khumalo akiwa bado ameushika mkono wa Linah.
“Habari yangu nzuri khumalo.Ni muda mrefu hatujaonana. Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Linah.Umepotea siku hizi,haupatikani kabisa.Nilipita China kama wiki tatu zilizopita,nikaonana na Frank akaniambia kwamba ulikuwepo pale na uliondoka jana yake kuelekea Port Elizabeth.Nilisikitika sana kukukosa”
“Ni kweli nilipita China nikaonana na Frank lakini sikukaa sana nilikuwa nawahi shughuli muhimu Port Elizabeth.Mambo yako yanakwendaje?
“Mambo yanakwenda vizuri sana Linah.Nimefurahi sana kukuona.Naona leo umeniletea mgeni” akasema Khumalo huku akimuangalia Loniki na kutabasamu
“yah ! Samahani kwa kutokutambulisha mapema.Huyu ndiye Yule rafiki yangu anaitwa Loniki.Kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Uingereza.Amekuja nyumbani mara moja kutokana na matatizo ya kifamilia.” Akasema Linah halafu akamgeukia Loniki
“Lonny,huyu ndiye Khumalo,rafiki yangu wa siku nyingi na ambaye atatusaidia katika ile kazi yetu”
“Karibu sana Loniki.Nimefurahi kukuona.Mimi ninaitwa Khumalo kama alivyokueleza Linah.Ninajishughulisha na biashara mbali mbali.Karibu sana na ujisikie nyumbani.” Akasema Khumalo huku akiinuka na kumfuata Loniki mahala alipoketi na kumpa mkono.
“Hata mimi nimefurahi sana kukuona Khumalo.” Akasema Loniki
“Linah alinieleza kwa ufupi kwamba una matatizo na unahitaji msaada.Nilitaka nionane nawe ili tuweze kuongea suala hili kwa kina.Nataka nipate picha kamili ya nini tatizo lako na nini unataka nikufanyie.” Akasema Khumalo huku akitoa sigara katika pakiti na kuiwasha.Loniki akarekebisha koo lake na kumsimulia Khumalo mkasa mzima uliohusiana na kifo cha Vero.Khumalo alikuwa kimya akimsikiliza kwa makini.Baada ya kumaliza kusimulia mkasa ule ,kimya kifupi kikatanda mle sebuleni.Khumalo akainuka na kuelekea katika friji akachukua mapande ya barafu na kurejea akiwa na chupa ya mvinyo mkononi.Akajimiminia mvinyo katika glasi na kupiga funda moja kisha akawasha sigara nyingine akavuta na kupuliza moshi hewani.
“pole sana Loniki.Nimeguswa sana na maelezo yako.Hata kama ningekuwa ni mimi ningefanya kama unavyotaka kufanya.Watu waliosababisha kifo cha mdogo wako hawastahili kuendelea kuwa hai.Mimi niko tayari kukusaidia kufanya hivyo unavyotaka lakini kabla hatujaenda huko nina ushauri mdogo.Nimekuelewa kwamba lengo lako ni kutaka wale wote waliosababisha kifo cha mdogo wako wapate mateso makali na hatimaye kuuawa.Hilo ni jambo lililo ndani ya uwezo wangu lakini kutokana na uzoefu wangu katika shughuli kama hizi ni kwamba kwa wakati huu ambao suala hili bado bichi,tukisema tumuue mmoja wapo kati ya Happy au Patrick basi inaweza ikawa mbaya kwa upande wako kwani itaonekana kabisa kwamba mauaji hayo yamefanyika kwa lengo la kulipa kisasi na familia yako inaweza ikahusishwa moja kwa moja na mauaji hayo na hii inaweza ikatuletea shida sisi sote.” Akasema Khumalo akanyamaza akamuangalia Loniki.
“kwa hiyo unashauri tufanye nini Khumalo” akauliza Linah
“Nionavyo mimi,tunachotakiwa kufanya kwanza ni kuvuruga kabisa mipango yote ya Patrick na Happy ya kuwa pamoja .Tutaanza kwanza kumshughulikia Happy.Tutamfanyia jambo ambalo litauvuruga kabisa uhusiano wake na Patrick na hata yeye mwenyewe anaweza aamue kujitoa uhai wake.Patrick anampenda Happy na endapo wakitengana Patrick atapata mateso makubwa mno.Nadhani ndivyo unavyohitaji Patrick na Happy wapate mateso makali.” Akasema Khumalo.
“Linaonekana ni wazi zuri lakini nahitaji ufafanuzi zaidi hasa namna utakavyomshughulikia Happy hadi yeye na Patrick watengane na ikiwezekana akaamua kujitoa uhai wake yeye mwenyewe” akasema Loniki.
Khumalo akachukua glasi yake ya mvinyo akanywa kidogo halafu akasema
“Tutamteka Happy.” Akanyamaza na kupuliza moshi mwingi hewani
“Nini kitafuata akishatekwa?
“Tutampeleka katika maficho yetu na halafu tutamfanyisha ngono na kundi la wanaume huku akipigwa picha na kurekodiwa katika filamu.Baada ya hapo tutachukua picha zile na kuzisambaza katika magazeti yote ya udaku na katika mitandao yote ya kijamii.Ninaamini baada ya hapo hakutakuwa tena na mahusiano kati ya Patrick na Happy.Happy tayari ana jina kubwa nchini na kwa kitendo cha picha zake za utupu kusambaa atadhalilika sana na nina hakika kama si kuikimbia nchi basi ataamua kujitoa uhai wake.Atateseka sana na hatakuwa na sehemu ya kupita kwani filamu zake tutazisambaza hadi vijijini.Mnaonaje kuhusu mpango huu? Akauliza Khumalo
Linah akatabasamu huku akimtazama Loniki na kusema
“That’s a perfect plan.Au unasemaje Lonny?
“hata mimi nakubaliana na mpango huo kwani lengo langu hasa ni watu hawa wapate mateso makubwa.Nina imani kama mpango huo utafanikiwa basi Happy atakuwa katika wakati mgumu sana.Atateseka sana kisaikolojia na kutokana na msongo wa mawazo ataona ni bora ajitoa uhai.Nadhani tukifanikiwa mpango huu kwa Happy tutakuwa tumemgusa kwa kiasi kikubwa na Patrick ambaye anampenda Happy.Wote wawili watapata mateso makali sana ya moyo na nina hakika hawatakuwa pamoja tena.Gharama nzima ya shughuli hii yote ni kiasi gani Khumalo? Akauliza Loniki.Khumalo akapuliza moshi mwingi hewani na kusema
“Kwa sababu ni wewe na umeletwa na swahiba wangu Linah basi utanipa shilingi million hamsini tu, pesa ambayo nitawapa vijana watakaonisaidia katika kuifanya hiyo kazi.Mimi sintapata chochote katika kazi hii.Nimeamua kukusaidia tu” akasema Khumalo.Loniki alistushwa sana na kiwango kile kikubwa alichokitaja Khumalo.Akainama na kufikiri.
“Ok Khumalo,pesa si tatizo.Ninachohitaji mimi ni mpango utekelezeke.Nitakupatia hizo millioni hamsini”
“Sawa Loniki.Kitu kingine ninachokihitaji toka kwako ni picha ya huyo Happy na maelezo yake kamili,mahala anapoishi au kama huna nipe picha yake na mahala anapoishi vijana wangu watamtafuta.”
“kwa sasa sina picha ya Happy lakini jumatano ijayo kesi ya Patrick itatajwa tena.Ingekuwa vyema kama ungehudhuria mahakamani wewe na vijana wako na mkamuona huyo mtu mwenyewe.”
“Hilo ni wazo zuri.Basi tutafika mahakamani siku hiyo na kumtambua huyo Happy na Patrick.” Akasema Khumalo halafu akaagana na akina Linah kwani kuna mahala alikuwa akiwahi.
“Linah umefahamiana vipi na Khumalo? Akauliza Loniki wakiwa njiani baada ya kuondoka nyumbani kwa Khumalo
“Khumalo nilifahamiana naye katika michakato yangu ya biashara.Toka wakati huo tumekuwa marafiki wakubwa sana.”
“Amenifurahisha sana kwa namna anavyojiamini na hata mpango wake ni mzuri.Ninachotaka ni Happy na Patrick waumie na endapo mpango huu utakamilika basi najua wataumia mno na ndoto yao ya kuwa pamoja itapotea” Akasema Lonny
“Khumalo ni mtu mwenye roho ya paka.Usoni anaonekana ni kijana mpole lakini awapo kazini sura yake hubadilika na kuwa ya shetani.Wewe utaona tu namna atakavyoifanya kazi hii uliyompa.”
“Nitafurahi sana sana kuona namna huyo kahaba Happy aliyevamia mapenzi ya watu atakavyodhalilika.Nataka aumie moyoni kama sisi tulivyoumia.Damu ya Vero haiwezi kupotea bure”
“Usijali Lonny.Kwa sasa unaweza kupumua baada ya kumkabishi Khumalo jukumu zima.” Akasema Linah
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 42
MTUNZI 😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Patrick amewahi kuwa na mahusiano na Savanna…?!!!.” Kila alipowaza jambo hili aliendelea kumuumia sana kichwa.
“Ninakubaliana na maneno ya George kwa sababu Patrick huwezi kumweleza chochote kuhusu Savanna akakuelewa.Anamuamini Savanna kupita kiasi.Vile vile hainiingii akilini hata kidogo katika ulimwengu wa sasa mtu akajitolea kuifanya kazi hii ngumu ya kisheria bila kulipwa chochote.Savanna amefanya hivi kwa sababu ana agenda yake ya siri.I’m so confused” akawaza Happy
“lakini pamoja na kuwa na agenda ya siri,Patrick ataendelea kuwa wangu peke yangu.Sintamruhusu Savanna amchukue Patrick toka katika mikono yangu.I’ve sacrificed a lot for Patrick and I wont loose him this time.Nitapambana naye” akawaza Happy

ENDELEA…………..

“Loniki,tayari nimekwisha wafahamu wahusika wakuu wanaotakiwa kushughulikiwa.Huyu mwanamke ,Happy ndiye nitakayeanza naye na siku ya kesho lazima nimpate” akasema Khumalo huku akipuliza moshi wa sigara hewani.Walikuwa katika ofisi ya Linah baada ya kutoka mahakamani.
“Nitashukuru sana kama zoezi hili litakwenda haraka kwani itanisaidia hata mimi kurejea haraka Uingereza.Nimeapa sintaondoka Tanzania hadi Patrick na Happy na wengine wote ambao wamesababaisha kifo cha Happy wawe tayari wamekwishalipa..Jioni ya leo nitakupatia kiasi cha shilingi million arobaini na zitakazobaki kumi nitakupatia baada ya kazi hii kukamilika.Kama kazi itakwenda vizuri basi ninaweza hata kukuongeza zaidi.Kwangu mimi pesa si tatizo hata kidogo.” Akasema Loniki.Khumalo akaaga na kuondoka zake kwa miadi ya kuonana jioni ili aweze kupatiwa mzigo wake wa shilingi millioni arobaini.
“Ninamuamini sana Khumalo.Anaongea taratibu lakini siku zote huwa anamaanisha anachokisema.Kama ameahidi kwamba kesho atampata Happy basi amini atafanya hivyo” akasema Linah baada ya Khumalo kuondoka
“Nitashukuru sana .Leo roho yangu imechafuka mno baada ya kumuona Patrick mahakamani tena akitabasamu kana kwamba hana hatia.Sitaki kuisubiri haki ya mahakama ambayo pengine isipatikane.Nitamlipia Vero kwa namna ninayojua mwenyewe.Natamani hata sasa hivi nisikie kamba Patrick na Happy wamefariki dunia.Sikufichi Linah ,moyo wangu utakuwa na amani pale tu Patrick na Happy watakapoacha kuivuta hewa hii safi na sintafumba macho mpaka nitakapohakikisha kwamba wameondoka duniani” akasema Loniki halafu akaagana na Linah kwa miadi ya kukutana jioni ili wamkabidhi Khumalo mzigo wake.
Baada ya kutoka ofisini kwa Linah,Loniki akarejea nyumbani na kumkuta mdogo wake Saraha tayari amekwisha fika na anaongea na mama yake.Loniki akasalimiana na mama yake bila kumsemesha lolote Sarah
“Mbona Sarah humsalimu? Mmekwisha onana? Akauliza mama yao
“Mama sijisikii hata kumpa salamu yangu huyu mwanao.Sioni kama anastahili salamu yangu.” Akasema Loniki kwa dharau
“Sihitaji salamu yako Lonny.” Akasema Sarah huku akitabasamu
“Sarah kwa nini unamjibu hivyo dada yako? Akafoka mama yao
“Mama kamwe sintakubali au kuvumilia dharau za Loniki.Siko tayari kumnyenyekea Loniki na kumsikiliza kwa kila anachokiongea kwa sababu tu anaishi Ulaya.” Akasema Sarah na kwa hasira akaelekea katika gari lake na kuondoka akiwaacha mama yake na Loniki wakishangaa
“Mama huyu mwanao amenichefua sana .Sikutegema kabisa kumuona akiwa hivi.Haonyeshi uchungu wowote ule wa kufiwa na mdogo wake na badala yake anadiriki hata kushirikiana na wauaji wa mdogo wake.Mama siko tayari kuvumilia upuuzi kama huu anaoufanya Sarah.Ngoja nimalize mambo yangu nitamfundisha adabu” akasema Loniki
“Hata mimi sijafurahishwa kabisa na tabia ya Sarah na hasa ya kuchangamana na familia ya Patrick,ambao wametupa mateso haya yote.Kwa uchungu nilionao sijui hata nifanye nini” akasema mama yake Loniki
“Usijali mama,haki lazima ipatikane.Lazima Patrick na wale wote waliosababisha kifo cha mdogo wangu walipe.Sintarejea Uingereza hadi nihakikishe kwamba wote walimuua mdogo wangu wamelipa”
“ Kwa kweli kwa uchungu ninaousikia hata mimi natamani sana waliomuua mwanangu nao walipe uovu wao.Walitenda kitendo cha kinyama sana.Wamemuua mwanangu bila kosa lolote..Ouh Vero ..!!!!” akashindwa kuendelea akaanza kulia.Loniki ambaye naye macho yake yalijaa machozi akamkumbatia mama yake
“Basi usilie mama Haki lazima ipatikane.” Akasema Loniki
“Ahsante mwanangu ,ila naomba wewe na Sarah msigombane kwani sina uwezo wa kuhimili maumivu mengine tena .”
“Hatutagombana mama .Tutarekebishana tu “akasema Loniki

* * * *

Saa kumi na moja za jioni Happy aliamka .Toka aliporejea akitokea mahakamani alikuwa amelala.Kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo aliamua kumeza vidonge vya usingizi na kulala kwa muda mrefu namna hiyo.Mambo aliyoambiwa na George yalimchanganya sana na alishindwa afanye nini.Kichwa kilikuwa kinamgonga kupita kiasi. Akainuka na kukaa kitandani.
“For the first time I feel dead.Kwa mambo aliyoniambia George ninajihisi kama mfu.Siamini kama Patrick na Savanna waliwahi kuwa wapenzi.Na ninavyohisi kuna kila dalili kwamba bado wanaendelea na mahusiano yao kwa siri kwani walikuwa na mahusiano hata kipindi kile ambacho Patrick alikuwa na Vero.Hii nina maana Patrick hakuwa mwaminifu kwa mchumba wake.Alimsaliti Vero. Na kama aliweza kumsaliti Vero hatashindwa kufanya hivyo hata kwangu.Ouh My God..why always me ? akawaza Happy halafu akaanza kuzunguka zunguka mle chumbani.
“Ninampenda Patrick na nimejitolea kila kitu kwa ajili yake.Lazima nipambane nihakikishe kwamba Savanna hapati nafasi hiyo anayoitaka.Siwezi kukubali ndoto zangu nyingi na za muda mrefu za kuwa na Patrick zipotee hivi hivi.Nilipendana na Patrick kabla hajakutana na Savanna kwa hiyo Patrick ni wangu peke yangu.I’ve made so many sacrifices just to be with him,so I cant let all that be for nothing,I must fight” akawaza Happy halafu akachukua simu na kumpigia Pendo akamuomba amtengenezee juisi ya embe.Baada ya kumaliza kuongea na Pendo akazitafuta namba za simu za Savanna akataka kumpigia lakini akasita .Akavuta pumzi ndefu na kutafakari kwa sekunde kadhaa na mwishowe akakakata shauri
“Lazima nimpigie.Siwezi kumpa Savanna nafasi ya kumpata Patrick.” Akawaza Happy halafu akabonyeza kitufe cha kupigia simu na simu ikaanza kuita.
“Hallow Happy.habari yako?” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Habari yangu nzuri Savanna.” Akajibu Happy
“Happy mbona sauti yako inaonyesha kama vile hauko sawa? Una tatizo lolote Happy? Akauliza Savanna
“Savanna we need to talk” akasema Happy na kumstua kidogo Savanna
“To talk?
“yes Savanna”
“Talk about what?
“About what I’ve discovered today”
“Ok Happy ngoja niegeshe gari hapa pembeni tuongee vizuri.Nitakupigia baada ya muda mfupi” akasema Savanna na kukata simu
“Leo lazima nimeueleze ukweli na utakuwa mwisho wake kuisimamia kesi ya Patrick.Niko tayari hata kukodisha mawakili kumi lakini si kuwa na wakili mmoja aliyevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni simba.”Akawaza Happy huku simu yake ikiwa mkononi akisubiri Savanna ampigie.Baada ya dakika tano simu yake ikaita.Alikuwa ni Savanna
“Happy tayari nimeegesha gari.Jambo gani unalotaka kunieleza?
“Savanna kuna jambo ambalo ninataka kulifahamu toka kwako.Wewe na Patrick mlifahamiana lini?
“Kwa nini unauliza hivyo Happy ?
“Just answer my question Savanna” akajibu Happy huku sauti yake ikionyesha kutokuwa na masihara.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita halafu Savanna akajibu
“Mimi na Patrick tulikutana miaka kadhaa iliyopita,sikumbuki ilikuwa katika mazingira gani”
“Mahusnao yenu baada ya kukutana yalikuwaje?
“Happy mbona unauliza maswali ya namna hiyo? Kuna matatizo gani?
“Savanna naomba unijibu maswali yangu” akasema Happy
“Patrick ni rafiki yangu wa muda mrefu.” Akajibu Savanna kwa ufupi
“Savanna usinidanganye.Tayari ninaufahamu ukweli halisi kuhusu wewe na Patrick.”
“Mimi na Patrick ..!!!!” Savanna akastuka
“Ndiyo.wewe na Patrick”
“Unafahamu ukweli gani kuhusu mimi na Patrick? Akauliza Savanna
“Ninafahamu kila kitu”
“Kila kitu gani Happy?
“Wewe na Patrick mliwahi kuwa wapenzi na bado mnaendelea na mahusiano yenu kwa siri na lengo la wewe kuamua kujitolea kumtetea Patrick mahakamani ni moja ya malengo yako ya kutaka kurudiana tena na Patrick “
“ouh My gosh …!!!!” Savanna akastuka
“Umezipata wapi hito taarifa? Akauliza Savanna
“Sina haja ya kukwambia nimezipata wapi .Ninachotaka kujua toka kwako je ni kweli ? akauliza Happy
“Happy nisikilize vizuri sana mdogo wangu.Tuko katika wakati mgumu wa kuhakikisha kwamba Patrick anashinda kesi kwa maana hiyo haya mambo unayoniuliza hayana msingi wowote kwa sasa.Naomba tuyaache hadi hapo tutakapomaliza haya mambo ya mahakamani na ndipo tutapata muda mzuri wa kuulizana maswali kama hayo” akasema Savanna
“Savanna mambo haya hayana umuhimu kwako lakini kwangu mimi ni muhimu sana.Tafadhali naomba unijibu” akasema Happy
“Happy kwa nini hutaki kunielewa? Nimekwisha kwambia siko tayari kukujibu maswali yako ya kipuuzi kwa muda huu” akasema Savanna kwa sauti ya ukali kidogo
“Savanna wewe ndiye hutaki kunielewa.Nimekuuliza swali rahisi sana Kwa nini hutaki kunipa jibu?
“Nenda kwa aliyekupa taarifa hizo yeye ndiye atakaye kuthibitishia kama ni kweli au si kweli.Mimi sina muda huo wa kupoteza.Tena Happy ninakuomba kama huna jambo la maana la kuongea nami,tafadhali naomba usinipigie simu.Nina mambo mengi ya kushughulikia kesi uliyoisababisha wewe mwenyewe” akasema Savanna
“Savanna hapo ulipo katika kidole chako unayo ile pete uliyopewa na Patrick? Akauliza Happy.Savanna akavuta pumzi ndefu na kusema
“Ninayo”
“kwa nini alikupa pete hiyo? Na kwa nini hujawahi kuivua kidoleni mwako? Kitu kingine ni kwa nini umekorofishana na mumeo George baada ya kuanza kujihusisha na kesi ya Patrick?” akauliza Happy.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa,Savanna akatamani kukata simu lakini akaamua andelee kuongea na Happy
“Happy unahitaji nini toka kwangu?
“Umekubaliana nami kwamba kila nilichokiongea hapa ni ukweli mtupu? Akasema Happy.Savanna akakasirika sana.
“Unahitaji kuujua ukweli,sasa ngoja nikwambie ukweli” akasema Savanna kwa hasira
“Ni kweli mimi na Patrick ni wapenzi.Unataka ukweli gani zaidi ya huo? akasema Savanna na kumpandisha hasira Happy
“Malaya mkubwa wewe.Siku zote hizi umekuwa ukijifanya ni mtu mwema kumbe una lako jambo.Nyoka mkubwa we” akafoka Happy
“Happy naomba usinitukane.Wewe ni binti mdogo sana wa kutukanana na mimi.Tena naomba iwe ni mara yako ya mwanzo na mwisho kuniita mimi Malaya.Una jeuri ya kuufungua mdomo wako na kunitukana sasa hivi wakati kwa uwezo wangu umekuwa huru?.Hivi sasa ulitakiwa uwe gerezani na mimi na Parick tungekuwa huru tunajinafasi kwa raha zetu.Happy narudia tena kukuonya kwamba kuwa makini na kauli zako.Mimi ni mtu mzuri sana lakini hubadilika na kuwa mbaya pale ninapokorofishwa.” Akasema Savanna kwa ukali
“Savanna naomba usinitishe.Kwa taarifa yako sikuogopi hata kid……………!!!!” Happy akastuka baada ya kumuona Pendo akiwa amesimama mlangoni akiwa na sura yenye mshangao na mkononi akiwa na glasi ya juisi.
“Kwa muda gani umekuwepo mlangoni? Happy akamuuliza Pendo
“Nimefika muda huu” akajibu Pendo
“Ok weka hiyo Juisi hapo mezani na uondoke” akasema Happy na pendo akatoka mle chumbani.
“Savanna,narudia tena kukwambia kwamba usitubutu tena kunitolea vitisho.Sikuogopi na huwezi kunifanya lolote.Nakuonya kuanzia sasa achana na hiyo kesi ya Patrick.Mimi nitagharamia kumtafuta wakili mpya wa kumtetea Patrick” akasema Happy na kumfanya Savanna acheke kwa dharau.
“Happy huna uwezo wa kuniamrisha mimi nisimtetee Patrick.Wewe ni mtu mdogo sana kwa Patrick.Kama huamini basi nenda kamweleze Patrick kwamba hutaki nijihusishe tena na kesi yake na usikie jibu atakalokupa na hapo ndipo utakapoamini kwamba wewe ni mtu mdogo sana kwake na huna nguvu wala uwezo wa kuamua chochote kuhusiana na maisha yake” akasema Savanna na kuzidi kumpandisha hasira Happy
“Savanna kama hutajitoa katika kesi hii hadi kesho ba………………..” Kabla Happy hajamaliza kusema alichotaka kukisema Savanna akamzuia.
“Utanifanya nini?
“Nitapambana nawe.Sintakubali unichukulie mpenzi wangu.Nitapambana nawe hadi mwisho.Patrick nimetoka naye mbali sana na sintaruhusu fisadi kama wewe kuyaingilia mapenzi yetu.” Akasema Happy kwa ukali
“Huna lolote la kunifanya Happy.Nakuonea huruma sana Happy hujui unachokiongea.Kuwa makini na kauli zako.Kama unajiona una uwezo wa kupambana na mimi nakuruhusu ujaribu..” akasema Savanna na kukata simu.Happy jasho lilikuwa linamtiririka.Mishipa ilikuwa imemtoka usoni kwa hasira alizokuwa nazo.
“Aaaaaggggghhhh..!!!!!!!!!!!!!!!!!!” akasema Happy kwa hasira na kuanza kutupa tupa vitu hovyo mle chumbani
“Savanna siwezi kukupa nafasi,nitapambana nawe kwa kila namna nitakayoweza.Siko tayari kumpoteza Patrick” akasema Happy kwa hasira huku machozi yakimtoka

* * * *

Zaidi ya dakika tano zimekwishakwenda tangu Savanna amalize kuongea na Happy simuni.Alikuwa ameegemea kiti chake akiwa na hasira kali.
“Bastard ..!!!!!!!” akasema Kwa ghadhabu huku akiipiga mikono yake katika usukani wa gari.
“Happy mbona anataka kukivuruga kichwa changu? Amefahamuje kama nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Patrick?Amefahamuje kama nilikorofishana na George sababu ikiwa ni Patrick?Ameitaja hadi pete hii aliyonipa Patrick” Akawaza Savanna halafu akainua mkono wake wa kushoto akaitazama pete ya dhahabu yenye kung’aa iliyokuwa na maandishi P&S,akatabasamu
“Ni kweli pete hii tulipeana na Patrick ishara ya kupendana hadi kifo.Patrick ni kila kitu kwangu na sintamuacha kamwe” akawaza Savanna halafu akaibusu ile pete
“Nimepata jibu.taarifa hizi zote atakuwa amepewa na George.Ni yeye pekee anayefahamu kila kitu kuhusiana na kinachoendelea kati yangu na Patrick.Aliahidi kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kamba mimi na Patrick hatuwi pamoja tena.Hata hivyo anajidanganya na hawezi kamwe kuizuia mipango yangu.Hata kama ikitokea bahati mbaya nikashindwa kufanikisha mipango yangu ya kuwa na Patrick tena,itakuwa vyema kama nitaishi maisha yangu yaliyobakia bila ya kuwa na mwenzi kuliko kuwa na mtu kama George.Nimekwisha mtoa katika akili yangu na juhudi zake zote za kutaka kuhakikisha kwamba anavuruga mipango yangu kwa matazamio ya kurudiana naye tena ,hazitazaa matunda.Tena ngoja nimuonye asijaribu kupambana na mimi” akawaza Savanna na kuzitafuta namba za George akapiga
“Hallow mpenzi wangu.habari yako.Missing you like crazy my angel…” akasema George mara tu alipopokea simu.Savanna akasonya kwa hasira
“Savanna my love usich………………” kabla hajaendelea Savanna akamkatisha
“Sikiliza George tena naomba unisikilize kwa makini.Sijakupigia simu kutaka kuusikiliza upuuzi wako.Ninataka kukueleza jambo moja tu.Hongera sana,juhudi zako nimeziona.Yote uliyomwambia Happy nimeyasikia.Pamoja na hayo naomba nikwambie kitu kimoja,stay away from me,far away from my life,forget that I exist.Naomba unifute kabisa katika akili yako na usitegemee kwamba siku moja mimi na wewe tutakuwa wapenzi .It’s over George.Huna nafasi tena kwangu.I don’t love you and I never loved you.Ni heri nikaolewa na shetani kuliko kuwa na mtu kama wewe” akasema Savanna
“Savanna..!!!” George akataka kutamka neno lakini Savanna akamzuia.
“Subiri nimalize George.” Akasema Savanna kwa ukali
“Ninakuonya George kwamba usijaribu kushindana na mimi .Kama unahitaji kunifahamu vizuri basi endelea kufuatilia maisha yangu.” Akafoka Savanna na kukata simu.
“Si George ,Happy wala mtu yeyote anayeweza kunizuia kuwa na Patrick.I’ll do everything ,I mean everything to be with Patrick again” akawaza Savanna na kuwasha gari akaendelea na safari yake
“Hii ni vita na inanibidi kupambana.Patrick ni mwanaume ninayempenda na nitahakikisha ninashinda vita hii ya kumgombania.Najua akili yake iko kwa Happy lakini nitafanya kila linalowezekana ili kuiharibu taswira ya Happy kichwani mwake.” Akawaza Savanna .
Mara tu alipomaliza kuongea na Savanna simuni,George akampigia simu Happy.Uso wake ulikuwa umejikunja kwa hasira.
“Hallo naongea na Happy ? akauliza George baada ya simu yake kupokelewa
“Ndiyo George.Happy hapa ninaongea’
“Happy umefanya nini? Kwa nini umemueleza Savanna yale mambo niliyokueleza? Tulikubaliana iwe ni siri yetu mimi na wewe.Kwa nini umekiuka makubaliano yetu? Akasema George kwa ukali
“George nimeshindwa kuvumilia.Patrick ni mtu wangu na nimeshindwa kuvumilia kuona kuna mtu mwingine akiwa katika jitihada za kutaka kumchukua.Nimeamua kumueleza ukweli Savanna ili aachane kabisa na mipango yake.” Akasema Happy
“Happy umekosea sana.Umefanya kosa kubwa sana.Umeharibu kila kitu.Umeniharibia kabisa mimi .Savanna ndiye mwanamke ninayempenda kuliko wote na kwa maneno uliyomwambia umezidi kumuweka mbali nami zaidi.Sikutegemea kama ungeweza kufanya jambo la kijinga kama hili…Unadhani kwa kumweleza ukweli Savanna utamzuia aachane na Patrick? Unajidanganya Happy umezidi kujiweka katika sehemu mbaya na usipoangalia hata huyo Patrick utabaki unamsikia tu.Kwa nini ukakurupuka bila kuuliza Happy???Nilikuona ni mtu mwenye akili kumbe ni mjinga kiasi hiki…..”
Happy hakumpa nafasi George ya kuendelea kuongea akakata simu.
“ Stupid !!!....” akasema kwa hasira
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 43
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“George nimeshindwa kuvumilia.Patrick ni mtu wangu na nimeshindwa kuvumilia kuona kuna mtu mwingine akiwa katika jitihada za kutaka kumchukua.Nimeamua kumueleza ukweli Savanna ili aachane kabisa na mipango yake.” Akasema Happy
“Happy umekosea sana.Umefanya kosa kubwa sana.Umeharibu kila kitu.Umeniharibia kabisa mimi .Savanna ndiye mwanamke ninayempenda kuliko wote na kwa maneno uliyomwambia umezidi kumuweka mbali nami zaidi.Sikutegemea kama ungeweza kufanya jambo la kijinga kama hili…Unadhani kwa kumweleza ukweli Savanna utamzuia aachane na Patrick? Unajidanganya Happy umezidi kujiweka katika sehemu mbaya na usipoangalia hata huyo Patrick utabaki unamsikia tu.Kwa nini ukakurupuka bila kuuliza Happy???Nilikuona ni mtu mwenye akili kumbe ni mjinga kiasi hiki…..”
Happy hakumpa nafasi George ya kuendelea kuongea akakata simu.
“ Stupid !!!....” akasema kwa hasira

ENDELEA…………………..

“Its gonna take a lot to drag me away from you.
There ‘s nothing that 100 men or more could ever do
Just like the rain down in Africa
Its gonna take some time but I know you’re worth fighting for
I’d fight for you
Eh ba bam ba eh eh ba bam baeh
I’d fight for you
Eh ba bam ba eh eh ba bam ba eh
I’ d fight for you
Let’s go
Friends are cool
But we both know
They don’t wanna see us together
Don’t wanna lose what I live for
I’m with willing to do whatever
Cause I don’t wanna see you cry
Give our love another chance
I bet we get it right this time
As long as youre prepared to fight,prepared to fight
I don’t wanna live another day
Without your body next to me
I’m not gonna let them break us down
Cause baby I know now,know now

If you got someone that’s worth fighting for .let no body hold you down.
Let me hear say whoa—oh – oh--oh
And if you you found someone that’s worth dying for
The one you cant live without
let me hear say whoa –oh—whoa

Wimbo huu ulioimbwa na Jason De Rulo ndio uliokuwa ukisika chumbani kwa Happy asubuhi hii..Kuonyesha ni namna gani wimbo ule ulivyokuwa umemgusa Happy alikuwa akiimba akienda sambamba na mashairi haya yenye ujumbe mzito.
Saa ya ukutani ilionyesha ni saa mbili na dakika kumi na nane za asubuhi.Happy bado alikuwa mbele ya kioo kikubwa cha meza yake iliyosheheni vipodozi vya kila aina.Siku hii ya leo alidamka mapema sana na aliutumia muda mrefu katika kujiandaa.Baada ya kuhakikisha kwamba amejipodoa vya kutosha akaenda katika kioo kikubwa cha kujitazamia mwili mzima ,akajitazama na kutabasamu
“Sipendi kujisifu lakini mimi ni mzuri.Yule Kunguru Savanna,hafikii hata robo ya uzuri wangu.” Akawaza Happy huku akiendelea kujitazama katika kioo.Siku hii ya leo alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi nyeupe iliyomkaa vyema aliyoiambatanisha na shati jeupe lenye nakshi za kuvutia.Chini alivaa viatu virefu vyeupe.Hakika kama ungefanikiwa kumuona Happy siku hii ya leo ungekubali kwamba alistahili kuwa mrembo wa Taifa.
Akiwa katika harakati za kutaka kutoka mle chumbani mara mlango wa chumba chake ukafunguliwa na akaingia mama yake.
“Wow ! mama .!Shikamoo.”
“Marahaba mwanangu ,unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri mama”.
“Happy una haraka sana?
“Ndiyo mama..kuna tatizo lolote?
“Kuna jambo nilitaka kuongea nawe”
“Mama kuna mahala ninawahi lakini nitarejea baada ya muda mfupi. Tutakuja kuongea nikirudi mama” akasema Happy na kuchukua mkoba wake mweupe na kutoka mle chumbani akaingia katika gari lake na kuondoka.Hakutaka kumueleza mtu yeyote alikokuwa anaelekea.
“Its gonna take a lot to drag me away from you.
There‘s nothing that 100 men or more could ever do
Just like the rain down in Africa
Its gonna take some time but I know you’re worth fighting for”
Mashairi ya wimbo huu alioupenda Happy yalimfanya atikise kichwa huku akifuatilizia na kuimba taratibu.Alikuwa akiutumia mkono wake wa kushoto kuendesha gari huku mkono wake wa kulia akiwa ameuegemeza dirishani.Alikuwa analivuka daraja la kigamboni kuelekea Uwangwa prison kuonana na Patrick
“Nimewahi sana leo.Natumai muda huu Savanna bado hajafika.Naomba Mungu iwe hivyo na mimi nifike kabla yake.Nataka atakapofika akute tayari nimekwisha ongea na Patrick na kuanzia leo asimame kuisimamia kesi ya Parick.Ni Patrick pekee mwenye uwezo wa kumsimamisha Savanna asiendelee kumtetea.Nina imani atakubaliana na hoja zangu kwa sababu mimi ndiye mwanamke pekee anayenipenda na nimejaa katika akili yake.Nitakuwa tayari kulipa kiasi chochote cha pesa kwa wakili mwingine ili aendelee kumtetea Patrick mahakamani na si Savanna.” Akawaza Happy huku gari likienda kwa kasi kubwa.
Saa nne kasoro dakika saba ilimkuta Happy katika gereza la Uwangwa.Alisalimiana na askari kadhaa waliokuwepo mapokezi.Tayari walikwisha anza kumfahamu hivyo alishughulikiwa haraka haraka kukamilisha taratibu za kuonana na mahabusu wake .Siku hii ya leo alimkuta askari mmoja aliyemsaidia na kumpeleka katika sehemu ya tofauti na ile iliyozoeleka ambayo hutumiwa na kila mtu ajaye kumuona mahabusu.Sehemu hii aliyopelekwa Happy ilikuwa nzuri na ilifaa hata kwa maongezi ya faragha.Baada ya dakika kama kumi hivi Patrick akaletwa na alipogonganisha macho yake na Happy akaachia tabasamu kubwa.
“Ouh my angel..!!!” akasema Patrick
“Patrick..!!!” akasema Happy kwa furaha huku akiinuka kitini na kumkumbatia.
“Mama una dakika thelathini za kuongea na mtu wako” akasema askari aliyekuwa ameambatana na Patrick
“Ahsante sana” akasema Happy kisha akakumbatiana na Patrick.
“Nimefurahi sana kukuona malaika wangu” akasema Patrick kwa furaha halafu akaipeleka mikono yake yote miwili kichwani kwa Happy wakaangaliana kwa sekunde kadhaa halafu wakapeana busu zito na kukumbatiana tena
“Ouh my angel,I was dying to see you” akasema Patrick huku akiketi kitini.
“Patrick my love,before coming here I felt like I was dead but now I feel alive “ akasema Happy
“Ouh Happy usihofu kitu malaika wangu.Mimi ni mzima ninaendelea vizuri sana.Nitashinda hii kesi na nitakuwa huru tena” akasema Patrick
Happy akatabasamu na kuufungua mfuko aliokuwa amekuja nao uliokuwa umesheheni vitu mbali mbali alivyokuwa amemchukulia mpenzi wake.
“Ahsante sana mpenzi wangu kwa kunijali” akasema Patrick.Happy hakujibu kitu akatabasamu.Kimya kifupi kikapita wakati Patrick akiendelea kunywa juisi aliyoletewa na Happy
“Jana ulifika mahakamani? Akauliza Patrick
“Ndiyo nilifika na nilikuwamo katika chumba cha mashtaka .Usingeweza kuniona kwa sababu nilikuwa nimekaa mwisho kabisa.Hata hivyo nilitoka wakati wanasheria wakivutana baada ya kugundua kwamba kuna watu walikuwa wakinitazama vibaya sana.Nahisi watakuwa ni ndugu zako au wa Vero.Sikutaka kuwakwaza ikanilazimu kutoka nje.” Akasema Happy
“Pole sana Happy.Najua kwa wakati huu baadhi ya ndugu zangu na familia nzima hawatakuangalia kwa jicho zuri wakiamini kwamba wewe ndiye chanzo cha haya yoye.Kaza moyo na usiwajali .Elekeza akili yako katika ndoto yetu ya kuwa pamoja.Kesi hii nitashinda na nitakuwa huru na ndoto yetu ya siku nyingi ya kuwa pamoja itatimia.Ninamuamini Savanna,ana uwezo na uzoefu mkubwa katika kusimamia kesi kama hizi na amenihakikishia kwamba lazima atashinda kesi hii” akasema Patrick .Happy aliposikia jina la Savanna likitajwa na kumwagiwa sifa akabadilika ghafla na kuinama chini.Patrick akaendelea kunywa juisi .
“Patrick..!!” akaita Happy
“Yes my angel “ akaitika Patrick.Happy akamtazama usoni kwa sekunde kadhaa na kusema
“Umefahamiana lini na Savanna?
“Savanna ni rafiki yangu wa muda mrefu.Tumefahamiana miaka mingi iliyopita”
“Ouh Okk.! “ akajibu Happy.Patrick akamuangalia Happy usoni na kugundua Hakuwa sawa.
“Happy kuna kitu gani kinakusumbua leo mpenzi wangu? Nakuona kama hauko sawa.Halafu kwa nini umeniuliza kuhusiana na Savanna?
“Usihofu Patrick.Mimi niko sawa kabisa na sina tatizo lolote.Nilihitaji tu kumfahamu Savanna vizuri”
“Happy whats going on? Akauliza Patrick.Happy akainama chini kwa sekunde kadhaa na kisha akainua kichwa na kusema
“Patrick I know you love me”
“Yes I I love you so much”
“As much as you love me you’ll never lie to me” akasema Happy na kuzidi kumshangaza Patrick
“Happy una tatizo gani leo? Akauliza Patrick
“Patrick wewe na Savanna mmewahi kuwa wapenzi? Akauliza Happy.Patrick aliyekuwa ameshika boksi la juisi akastuka na kuliweka mezani akamtazama Happy
“Happy are you ok today?
“I’m ok Patrick.Just answer my question” Patrick akaendelea kumtazama Happy halafu akasema
“Hapana .Mimi na Savanna ni marafiki na hatujawahi kuwa wapenzi”.
Patrick akavuta pumzi ndefu baada ya kumpa Happy jibu lile.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita wakabaki wanatazamana.
“Are you sure Patrick?
“Yes I’m sure.Happy kuna kitu gani kinakusumbua leo?
Happy akatoa kitambaa na kujifuta jasho.
“I know down deep in your heart you know exactly that you are lying to me.” Akasema Happy.Patrick akahisi kuchanganyikiwa.
“Happy nimekwambia ukweli mtupu na siwezi kukudanganya malaika wangu”
“Patrick muda niliopewa ni mdogo sana na si lengo langu kuanza kubishana nawe.Ninaomba tu ufahamu kwamba ninaufahamu ukweli wote kwamba wewe na Savanna mliwahi kuwa wapenzi wakati ukiwa na Veronika na mlitengana baada ya Savanna kumpata bwana aitwaye George.Is that true? Akasema Happy.Patrick midomo ilikuwa inamtetemeka.
“Unakumbuka tukiwa Arusha niliwahi kukuhoji kuhusu yale maneno P&S yaliyoko katika pete yako na ukaniambia kwamba hayana maana yoyote? Ukweli ni kwamba maneno yale yanamaanisha Patrick na Savan.Maneno haya yapo pia katika pete na mkufu wa Savanna.” Akasema Happy.Patrick jasho lilikuwa linamtoka
“Savanna bado anakupenda sana na kwa taarifa yako ana mpango wa kuitumia kesi hii kuwa chanzo cha wewe na yeye kurudiana na kuwa wapenzi tena na ndiyo maana amejitolea hata kuifanya kazi hii ya uwakili bure kabisa.Hii ni sababu iliyosababisha aachane na mumewe akiamini kwamba atarudiana na wewe”
Patrick jasho liliendelea kumtiririka.Happy akainuka ,akamfuta jasho kwa kitambaa chake.
“Happy mambo haya yote umeyatoa wapi? Nani aliy………………..” akataka kuuliza Patrick lakini Happy akamzuia
“Patrick hakuna haja ya kuanza kupoteza muda wa kuelezana mambo haya nimeyajua vipi.Kitu pekee ambacho unapaswa kukifahamu na kukizingatia ni kwamba wewe ndiye maisha yangu ,furaha yangu,pumzi yangu na kila kitu changu.Ninakupenda Patrick zaidi ya ninavyoweza kueleza.Usihofu kuhusu haya niliyokueleza,nilitaka tu ufahamu kwamba ulifanya kosa kuwa na mahusiano ya siri wakati ukiwa na Veronika.Sina hakika kama unaweza ukanifanyia mimi jambo kama hilo kwa sababu endapo nikigundua kwamba una mahusiano nje ya uhusiano wetu ,Patrick I swer I‘m gonna kill you and kill myself.You are mine alone.Anyway tuachane na hayo ni mambo yaliyopita na hayana nafasi kwa sasa.Ila kuna jambo moja ninaloliomba toka kwako”
“Jambo gani hilo Happy?
“I want Savanna out of this case.”
Patrick alihisi kama kuishiwa nguvu ,akabaki anamtazama Happy asijue aseme nini.
“Happy…..!!” Patrick akataka kusema kitu lakini Happy akamzuia
“Patrick you are my angel,my everything.Uko hapa ndani kwa sababu yangu,kwa sababu ya upendo wako kwangu.Patrick hicho ni kitu pekee ninachokuomba mpenzi wangu.Nataka Savanna aachane kabisa na kesi hii .Mimi niko tayari kumtafuta wakili mwingine mahiri ambaye ataendelea kukutetea mahakamani lakini si Savanna.Siko tayari kukupoteza Patrick.” akasema Happy.Patrick akainama akatafakari na kusema
“Happy napenda nichukue nafasi hii kwanza kukuomba msamaha kwanza kwa kusema uongo pale uliponiuliza kama niliwahi kuwa na mahusiano na Savanna.Ni kweli niliwahi kuwa na mahusiano na Savanna lakini tulisitisha mahusiano yetu pale yeye alipompata George.Toka wakati huo tumeendelea kuwa marafiki wa kawaida.Tumekuwa tukisaidiana katika mambo mengi na ndiyo maana hata katika kesi hii Savanna ananisimamia kama rafiki na mtu wake wa karibu na si kama mpenzi wake.Savanna ni mwanasheria aliyebobea na mzoefu katika kesi kubwa kama hizi.Amekuwa akisimamamia kesi kubwa kubwa na hajawahi kushindwa.Tafadhali nakuomba uniamini Happy kwamba hakuna kinachoendelea kati yangu na Savanna kwa sasa zaidi ya urafiki wa kawaida.Nakuomba Savanna uniamini kwamba ni Savanna pekee ambaye anaweza kuniweka huru.Naomba tusimuondoe katika kesi hii” akasema Patrick kwa sauti ndogo
“Patrick nakuelewa na sina tatizo na uwezo wa Savanna..Najua unamuamini sana na ni wakili mzoefu na mbobezi wa sheria.Ninachotaka kukiepuka mimi ni kupigana vita ya pili kati yangu na Savanna.Wewe ni mwanaume wangu wa pekee na niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yako na ndiyo maana nimeamua kuachana na kila kitu kwa ajili yako kwa hiyo atakapotokea mwanamke ambaye atatishia usalama wa penzi langu nawe lazima nipambane naye.Sitaki kupambana na Savanna na ndiyo maana ninataka umuondoe katika kesi hii.Mimi niko tayari kulipa gharama za wakili hata zaidi ya mmoja.Najua Savanna anakupenda na yeye atafanya kila linalowezekana ili aweze kunitenganisha nawe.tafadhali Patrick naomba unikubalie jambo hili moja tu.” Akasema Happy
“ Happy nimekuelewa unachokisema na mimi niko radhi kufanya chochote kile kwa ajili yako na ndiyo maana niko hapa gerezani muda huu.Pamoja na yote uliyonieleza bado sijaona sababu ya msingi yakumuondoa Savanna katika kesi yangu.Naomba Happy muache Savanna aendelee kunisimamia mahakamani”
“Patrick umejitolea kuibeba adhabu yangu kwa sababu ya upendo wako mkubwa kwangu.Sina cha kuweza kukulipa kulingana na thamani ya upendo wako kwangu.Please Patrick allow me to do at least one thing for you.Allow me to hire another lawyer for you to replace Savanna.” Happy akaendelea kusisitiza
“Happy najitahidi sana kupingana na nafsi yangu kuhusiana na suala hilo unalolitaka.Najitahidi kutaka kukubaliana nawe lakini bado moyo wangu unakataa kabisa.Najua una lengo zuri la kutaka kunisaidia lakini sina hakika kama uamuzi wa kumuondoa Savanna ni uamuzi unaofaa kwa sasa.Nahitaji kutoka humu gerezani,nahitaji kushinda kesi ili niwezi kuitimiza ndoto yangu ya kuwa nawe na hilo litawezekana tu kama Savanna ataendelea kuisimamia kesi hii.Endapo tutaamua vinginevyo basi ndoto zangu zote za kuwa nawe zitapotea kwa sababu nitapotelea gerezani”
“Patrick huwezi kupotelea gerezani.I give you my word.Nitamtafuta wakili mahiri kabisa na hata zaidi ya mmoja kama itahitajika.” Happy akaendelea kuusimamia msimamo wake bila kutetereka.Patrick akainama akafikiri kidogo na kusema
“Happy hilo ni jambo lisilowezekana hata kidogo.” Happy machozi yakamlenga
“You are still in love with her,right? Akauliza Happy
“Si hivyo unavyofikiri Happy “
“Nijibu Patrick.Bado unampenda Savanna? Kwa sababu yake hauko tayari hata kunisikiliza mimi mpenzi wako” akasema Happy huku machozi yakimtoka na mara mlango ukafunguliwa na wote wakapigwa na butwaa baada ya kumuona mtu aliyesimama mlangoni.Alikuwa ni Savanna.Nyuma yake alikuwepo Andrew ,rafiki mkubwa wa Patrick ,Alois kaka wa Patrick aliyeongozana na mke wake na pamoja nao alikuwepo mama yake Patrick.
Happy akahisi mwili wote unamtetemeka.Akakosa neno la kusema.Savanna akawaongoza watu aliokuja nao wakaingia mle chumbani.Mama yake Patrick nusura aanguke kwa mstuko baada ya kuingia mle chumbani na kugonganisha macho yake na Happy
“Wewe ..!!!” akasema kwa sauti yenye mshangao.Hakuwa ametegemea kama angekutana na Happy mahala pale.Happy alikuwa anatetemeka kwa woga namna alivyokuwa anaangaliwa kwa jicho la chuki.
“Shikam…….” Happy akataka kumsalimu mama yake Patrick lakini kabla hajamaliza salamu yake akazuiwa.
“Haraka sana toka nje” akasema kwa ukali mama yake Patrick.
“Mama ..!!! Patrick akataka kusema jambo lakini naye akazuiwa
Kwa Haraka Happy akauchukua mkoba wake uliokuwa kitini .Machozi yalikuwa yanamtoka akaanza kupiga hatua kuondoka.
“Na iwe ni mara ya mwanzo na ya mwisho kufika hapa.Sitaki kukuona tena karibu na mwanangu shetani wewe.Kila mara unapokaa karibu na mwanangu lazima jambo baya limfike.Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati.” Akasema kwa ukali mama yake Patrick
“Basi mama imetosha.Usiongee sana utasababisha matatizo mengine” akasema Alois
“Na wewe Patrick naomba ukae mbali kabisa na huyu mwanamke.Sitaki kuona ukiwa karibu naye.Yeye ndiye chanzo cha haya matatizo yote” Akaendelea kufoka mama yake Patrick.
“Patrick nimekuletea wageni” akasema Savanna baada ya hali kutulia mle chumbani
Patrick akasalimiana na mama yake pamoja na ndugu zake.Waliongea mambo mengi na kumpa moyo kuhusiana na kesi inayomkabili.Baada ya maongezi yao yaliyochukua zaidi ya nusu saa wakaaga na kuondoka.Ni Savanna pekee aliyebaki.
“Patrick unajisikiaje leo kwa kuonana tena na ndugu zako na hasa mama? Akauliza Savanna
“Nimefurahi sana kuonana nao tena,nimefarijika sana.Ahsante Savanna kwa kuwaleta.Pamoja na ujio wao lakini bado kichwa changu hakiko sawa” akasema Patrick.Savanna akamuangalia kwa makini na kusema
“Its because of her,right? Amekwambia nini Happy?
Patrick akafikiri kidogo na kusema
“Tayari anafahamu kwamba mimi na wewe tuliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.”
“Hata mimi alinipigia simu jana na kunieleza kuhusu suala hilo na sikuweza kukataa kwa sababu alikwisha elezwa kila kitu na George.Happy alinitukana sana na kusema kwamba atahakikisha ninaondolewa katika kesi yako.Nadhani hilo ni jambo mojawapo lililomleta kwako asubuhi hii.She wanted me out,right?
“Ni kweli Savanna.Happy alinitaka nikuondoe katika kesi yangu na nitafute mawakili wengine”
“wewe umemjibu nini?
“Siwezi kufanya jambo la kipuuzi kama hilo.” Akasema Patrick
“Kwa nini hujamsikiliza mpenzi wako Patrick.Kwa nini hujamtimizia alichokuomba? Akauliza Savanna
“kwa sababu nakuamini Savanna.Umejitolea kunitetea na ninaamini kwamba nitashinda kesi.Hakuna mtu anayeweza kunishauri nikutoe katika kesi hii.”
Savanna akatabasamu baada ya kauli ile ya Patrick.
“Nilikwambia Happy,mipango yako kamwe haitaweza kufanikiwa.Nilikuonya kwamba Patrick hawezi akakusikiliza .Na huu ni mwanzo tu.Ulitaka mapambano na mimi na sasa utaiona nguvu yangu “ akawaza Savanna
“So is that true? akauliza Patrick
“Is what true?
“kwamba umeachana na George.
“Yah..its true.” Savanna akajibu
“Samahani Patrick kwa kutokufahamisha kuhusu jambo hili kwa sababu halikuwa na umuhimu wowote”
“Sababu gani iliyopelekea mkaachana? Akauliza Patrick
“George alinitaka niachane na kesi yako.Aliogopa kwamba kesi hii ingeweza kutuweka karibu muda mwingi kwa hiyo akahofu kwamba pengine tunaweza kujikuta tukirejesha mahusiano yetu ya zamani.Sikuwa tayari kuachana na kesi yako kama alivyotaka George kwa hiyo tukaachana.Patrick niko tayari hata kutengana na dunia nzima lakini si kukuacha katika kipindi hiki kigumu.Hakuna mtu yeyote chini ya jua zaidi yako wewe mwenyewe anayeweza kunizuia nisikutetee.” Akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna kwa kunithamini namna hii.Sina kitu cha kukulipa kwa wema wako huu mkubwa.Tafadhali fanya kila linalowezekana ili uweze kuniondoa katika kesi hii”
“Patrick usihofu.Nitafanya kila linalowezekana na kukuweka huru.naomba uniamini.I’ll fight till you get free.I give you my word” akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu
“Ahsante sana Savanna” akasema Patrick
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 44
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“George alinitaka niachane na kesi yako.Aliogopa kwamba kesi hii ingeweza kutuweka karibu muda mwingi kwa hiyo akahofu kwamba pengine tunaweza kujikuta tukirejesha mahusiano yetu ya zamani.Sikuwa tayari kuachana na kesi yako kama alivyotaka George kwa hiyo tukaachana.Patrick niko tayari hata kutengana na dunia nzima lakini si kukuacha katika kipindi hiki kigumu.Hakuna mtu yeyote chini ya jua zaidi yako wewe mwenyewe anayeweza kunizuia nisikutetee.” Akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna kwa kunithamini namna hii.Sina kitu cha kukulipa kwa wema wako huu mkubwa.Tafadhali fanya kila linalowezekana ili uweze kuniondoa katika kesi hii”
“Patrick usihofu.Nitafanya kila linalowezekana na kukuweka huru.naomba uniamini.I’ll fight till you get free.I give you my word” akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu
“Ahsante sana Savanna” akasema Patrick

ENDELEA……….

Ilimchukua Happy zaidi ya dakika kumi kutulia na kuwasha gari.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka. Kitambaa chake cha mkononi kilikuwa kimeloa machozi.Hatimaye akawasha gari na kuondoka maeneo yale ya mahakamani.
“Na iwe ni mara ya mwanzo na ya mwisho kufika hapa.Sitaki kukuona tena karibu na mwanangu shetani wewe.Kila mara unapokaa karibu na mwanangu lazima jambo baya limfike.Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati”
Maneno haya ya mama yake Patrick,yalikuwa yanajirudia kichwani kwa Happy na kumfanya aangushe machozi huku akiendesha gari.
“Kwa mara ya kwanza ninajuta ni kwa nini nilionana tena na Patrick.Nadhani ingekuwa vyema kama Patrick asingejitokeza tena katika maisha yangu.Nilikuwa na maisha yangu mazuri na yenye furaha na Mike.Sikutegema hata siku moja kama siku moja ningekuja kuwa na wakati mgumu namna hii.Toka nilipoonana na Patrick maisha yangu yamebadilika ghafla.Ndoto zangu zote za maisha nilizokuwa nazo zimepotea.Mateso na maumivu ya moyo hayaishi.Nimekuwa ni mtu wa kulia kila siku.maisha yangu yamepoteza mwelekeo” akawaza Happy huku akipunguza mwendo wa gari na kufuta machozi
“Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati.”
Maneno ya mama yake Patrick yakazidi kujirudia kichwani mwa Happy
“Inawezekana ni kweli nina laana na ndiyo maana mambo yangu hayafanikiwa.lakini ni kwa nini hunikuta nikiwa na Patrick pekee? Miaka hii yote niliyokuwa na Mike sijawahi kuangusha hata chozi”.Happy akajiuliza na kushindwa kupata jibu.Sura ya mama yake Patrick akimtazama kwa macho makali yaliyojaa chuki ikamjia kichwani.
“Kila nikiikumbuka sura ya Yule mama mwili unatetemeka.Macho yake yalionyesha dhahiri ni namna gani anavyonichukia.Nimeogopa sana na sijui nitawezaje tena kuonana na Patrick .Kwa sasa itanibidi nijitahidi kwa kila namna nitakavyoweza kuikwepa familia ya Patrick kwani kwao mimi ni adui wao namba moja” Happy alikuwa amezama katika mawazo mazito.Alikuwa analivuka daraja la Kigamboni.
Wakati akiendelea na safari yake huku kichwa chake kikiwa kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo,mita kama mia moja hivi nyuma yake gari mbili zilikuwa zinakuja kwa kasi.Gari zile zilionekana kana kwamba zilikuwa zinafukuzana.Happy aliziangalia kupitia kioo cha pembeni lakini hakuzitilia maanani.Gari zile zikafika usawa wa gari la Happy na zote mbili zikawa kama zinataka kupishana kwa wakati mmoja.Gari lililotaka kupitwa likasogea karibu sana na gari la Happy kitendo kilichomstua na kabla hajafanya chochote gari lake likakwaruzwa ubavuni.Happy akataharuki na kufunga breki ya ghafla .Kwa bahati nzuri hakuwa katika mwendo mkali.Gari lililomkwaruza ubavuni nalo likasimama mbele yake.Happy akashuka kwa hasira na kutazama gari lake lilivyokwaruzwa.Kwa hasira akaelekea katika gari lililomkwaruza ambalo lilisimama mita chache toka aliposimamisha gari lake.Milango ya gari lile ikafunguliwa na wakashuka watu watatu mwanadada mmoja na wanaume wawili.
“You people don’t you know how to drive?? !!....” akafoka Happy
“Samahani sana dada.Hatukutegemea kama tungeweza kukukwaruza.Nilikuwa najaribu kumkwepa Yule jamaa” akasema mmoja wa wale jamaa huku akimuelekezea jamaa mmoja aliyevaa suruali nyeusi na fulana nyeupe aliyekuwa akiwaelekea
“Nasema hivi,sitaki kesi wala mjadala wowote.Nahitaji gari langu likatengenezwe.” Akaendelea kufoka Happy
“Usihofu madam,wenye makosa ni sisi na tunaomba tugharamie matengenezo ya gari lako na hata kukupatia gari lingine la kutembelea wakati gari lako linatengezwa mahala lilipokwaruzwa”
“Nimesema sihitaji kitu chochote ninachotaka ni gari langu litengenezwe haraka sana” akaendelea kufoka Happy Muda huo huo jamaa mmoja mnene akiongozana na vijana wawili akafika eneo la tukio”
“Dada samahani sana kwa tatizo lililotokea,naomba tusipoteze wakati,tuelekee gereji gari lako likatengenezwe” akasema yula jamaa mnene.Happy akaanza kupiga hatua kurejea katika gari lake lakini Yule jamaa akamzuia
“Hapana panda gari hili” Happy akageuka kwa hasira .Hakuamini macho yake kwa alichokiona.Alikuwa anatazamana na midomo miwili ya bastora.Kijasho kikamtoka,mwili mzima ukamtetemeka.
“Taratibu bila ubishi ingia ndani ya gari hili.Usitulazimishe tutumie nguvu” akaamuru Yule jamaa.Huku akitetemeka Happy akajikaza na kuuliza
“What’s going on here? What’s the meaning of this?
“Get in the car ,now !! akafoka Yule jamaa mnene.Bado miguu ya Happy ilikuwa mizito sana kunyanyuka.Hakuamini kilichotokea aliona ni kama njozi.
Kwa haraka mwanadada aliyekuwa ameongozana na watu wale akamfuata Happy na kumnong’oneza kitu sikioni halafu akamshika mkono na kumuingiza katika gari lile aliloamriwa kupanda.Haraka haraka wakarejea katika magari yao na kijana mmoja akaenda katika gari la Happy.Magari yakawashwa na kuondoka eneo lile.Kitendo kile hakikuchukua zaidi ya dakika kumi.

* * * *

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuwaona watu wale waliokuwamo garini.Hakuwafahamu na wala hakufahamu lengo la wao kumtaka aongozane nao.Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda kwa kasi ya ajabu na jasho jingi lilimtiririka na kuloanisha shati lake jepesi.
“Mungu wangu mambo gani haya yananitokea tena ? Watu hawa ni akina nani na wanataka nini kwangu? Happy akawaza huku machozi yakimtoka.
“Jamani mnanipeleka wapi? Naombeni msinidhuru tafadhali.Nitawapa kiasi chochote cha pesa mtakachokihitaji” Akalia Happy
“Shut up !!! akafoka jamaa aliyekuwa amekaa pembeni yake.Happy alikuwa amewekwa kati kati ,mikononi alifungwa pingu.Gari lilikuwa linakwenda kwa kasi kubwa na kabla ya kulimaliza daraja la kigamboni jamaa mmoja aliyekuwa amekaa mbele pembeni ya dereva akapokea simu na kuongea kwa takribani dakika mbili halafu akawageukia wale waliokuwa wamekaa kiti cha nyuma ,akawafanyia ishara Fulani na kwa haraka wale jamaa wakamfunga Happy kitamba cheusi usoni na hakuweza kuona chochote tena.Bado aliendelea kulia akiomba aachiwe huru lakini hakuna mtu hata mmoja aliyemjali na kumsikiliza.gari lilianza kukata mitaa ya jiji .Happy hakuweza kutambua ni wapi walikokuwa wanaelekea .
Katika gari iliyokuwa imetangulia mbele,kijana mmoja mwembamba mrefu alikuwa anatabasamu kwa furaha wakati akiongea na simu.Alipomaliza kuzungumza na simu akamgeukia dereva wake
“Sasa ngoja nimpigie simu Loniki nimtaarifu kwamba mtu wake tayari tumekwisha mtia mikononi.” Akasema na kuzitafuta namba za simu la Loniki na kumpigia
“Hallow Khumalo” akasema Loniki baada ya kupokea simu
“Hallo Loniki ,habari yako.Uko wapi mida hii?
“Kwa sasa niko saluni natengeneza kucha”
“Lonny nimekupigia simu kukutaarifu kwamba Happy tayari tumemtia mikononi mwetu na hivi sasa tunaelekea mahala kazi itakapofanyikia.Nitakutaarifu baadae ni wapi tumempeleka ili ushuhudie namna atakavyofanyiwa”
“Wow !! that’s wonderful.Thats good news” akasema Loniki kwa furaha
“One more thing lonny,hatutakiwi kumuweka mafichoni kwa muda mrefu sana.Kila kitu kinatakiwa kifanyike usiku wa leo na halafu tumuache huru.Ukumbuke vile vile kuja na kiasi cha pesa kilichobakia.Jambo la mwisho vijana wanataka uwaongeze shilingi million ishirini ili waweze kuendelea kutoa ushirikiano katika kazi iliyobaki.Kwa kweli vijana wamefanya kazi kubwa na ya kitaalamu sana kiasi kwamba tumemchukua Happy bila ya rabsha wala mtu yeyote kugundua kwa maana hiyo basi vijana wanahitaji motisha ili waendelee kuwa na ari ya kazi.”
“Twenty million more …!!!!???. Loniki akastuka
“yes Lonny vijana wanataka uwaongeze kiasi hicho”
“Khumalo hatukupatana hivyo na wala hatukukubaliana kuongeza kiasi chochote cha pesa zaidi ya kile cha million hamsini tulichopatana.Hizo million ishirini unazozisema nitazipata wapi sasa hivi? Its a lot of money” akasema Loniki
“Sikiliza Lonny.tusiendelee kubishana kuhusu suala hilo.Ulitupa kazi ya kufanya tumekwisha ifanya tayari lakini kutokana na ugumu wa kazi yenyewe vijana wanataka uwaongeze kiasi hicho cha pesa ili kazi yako ikamilike.Najua hauko tayari kuona kazi hii kubwa ikiharibika,kwa hiyo jitahidi upate kiasi hicho cha pesa na tutakapoonana jioni ya leo utukabidhi.”
“Khumalo that’s unfair” akasema Loniki
“Lonny find that money.Mpaka jioni ya leo kama hutakuwa umezipata ,nitamuachia Happy” akasema Khumalo na kukata simu.Uso wake ukapambwa na tabasamu kubwa.Bado akiwa na simu yake mkononi akazitafuta namba za Linah na kumpigia
“Hallow Linah” akasema Khumalo
“Khumalo vipi maendeleo?
“Kila kitu kinakwenda vizuri.Tayari Happy tunaye na kwa sasa tunampeleka mafichoni.Nimempigia simu Lonny na kumwambia kwamba aongeze milioni ishirini na kama akishindwa kuzipata fedha hizo hadi jioni ya leo basi nitamuachia Happy.Nina uhakika atakupigia simu , na kama akifanya hivyo na wewe endelea kumsisititiza ili aweze kuzitafuta hizo fedha.”
“Good job Khumalo.Its time now to make easy money.Kama nilivyokwambia kwamba Lonny ana pesa na nina hakika mpaka jioni ya leo atakuwa amezipata hizo fedha.Hakukuwa na tatizo lolote wakati wa kumkamata Happy?
“Hapana Linah.Tulimchukua kirahisi mno na ni tukio ambalo lilichukua chini ya dakika kumi na hakuna nguvu iliyotumika zaidi ya gari lake kupata mikwaruzo kidogo”
“Vizuri sana khumalo.Nitakuja jioni na Lonny”
“Sawa Linah .Nitamtuma kijana ambaye atakuja kuwachukua jioni na kuwaleta mahala tutakapompeleka Happy”
“Ok Khumalo.Lakini naomba msimuumize Happy.Namuonea huruma sana huyo binti hana kosa lolote”
“Usijali kuhusu hilo.Hakuna mtu atakayempiga hata kofi moja.Atapatiwa kila kitu na hata mimi mwenywe sijisikii vizuri kwa kitendo hiki lakini kwa kuwa kazi hii ina hela nzuri imenilazimu kuifanya tu.See you later Linah.” Akasema Khumalo na kukata simu
“hahahaaaaa..!!! thats why I love Dar es salaam.Its easy to make money in here” akasema Khumalo nakuendelea kucheka halafu akatoa sigara yake akaiwasha na kuvuta.


* * * *

Mara tu alipomaliza kuongea na Khumalo simuni ,Loniki alihisi kuchanganyikiwa.Haraka haraka akapanda gari na kurejea nyumbani.Alipofika nyumbani akamvuta pembeni mama yake aliyekuwa amekaa na kundi la akina mama waliokuja kumpa pole.
“ Loniki vipi,mbona uko hivyo? Akauliza mama yake
“Mama nina shida”
“Shida gani Lonny?
“Mama nina shida ya pesa”
“Pesa !! mama yake akaonyesha mshangao.Hakuwahi kumsikia hata siku moja Loniki akiwa na shida ya pesa
“Unahitaji kiasi gani cha pesa? Akauliza mama yake
“Nahitaji million ishirini”
“Millioni shirini !!!! mama yake akastuka
“Ndiyo mama”
“Pesa zote hizo za nini Loniki?
“Nina shida nazo kubwa na ya haraka kwa leo.Nimeongea na mume wangu na ameniahidi kunitumia pesa hizo kesho toka London.Kama una kiasi hicho cha pesa naomba uniazime na kesho nitakurejeshea.”
Mama yake akabaki anamuangalia loniki kwa mshangao.
“Mama mbona unanitazama hivyo?
“Nimestushwa na kiasi hicho kikubwa cha pesa.lakini hebu niambie Loniki unataka kuzipeleka wapi fedha zote hizo?
“Mama nina shida nazo sana kwa leo.” Akasema Loniki.Mama yake akafikiri kidogo na kusema
“Kwa sasa bado sijajua nina kiasi gani cha pesa ndani kwani Vero ndiye aliyekuwa meneja wangu.Twende ndani nikaangalie nina kiasi gani “ akasema mama yake na wakaelekea chumbani kwake ,akafungua kabati na kutoa vitita vya pesa wakaanza kuhesabu.
“Millioni kumi na tatu” akasema mama yake wakatazamana
“Bado million saba” akasema Loniki
“Tutatoa wapi hizo zilizobaki? Akauliza mama yake
“Mimi sijui mama.Jaribu kufanya maarifa.” Akasema Loniki
“Jaribu kuongea na mdogo wako Sarah anaweza akakupatia kiasi hicho cha pesa”
“Hapana mama siwezi kufanya hivyo.Tena ninaomba usimweleze chochote kile kuhusiana na pesa hizi.Kama unataka kuazima kwa Sarah,azima kama wewe na asifahamu kama unanipa mimi.” Akasema Lonny.mama yake akachukua simu na kumpigia Sarah.
“Hallow mama” akasema sarah
“Sarah nina shida kidogo mwanangu”
“Shida gani mama?
“Nina shida ya pesa “
Sarah akacheka kidogo aliposikia mama yake anashida ya pesa.
“Mbona unacheka Sarah?
“Ni mara yangu ya kwanza kukusikia ukisema una shida ya pesa”
“Kweli Sarah nina shida ya pesa lakini nitakurejeshea kesho”
“Unahitaji shilingi ngapi mama?
“nahitaji million saba”
“Millioni Saba? !!!!..Sarah akastuka
“Ndiyo sarah.Ninahitaji pesa hizo kwa haraka.Kama unazo naomba uniazime na kesho nitakurejeshea.”
Sarah akavuta pumzi ndefu na kimya kifupi kikapita
“Sarah unaweza ukanisaidia kiasi hicho cha pesa?
“Mama unataka kutumia kwa kazi gani fedha zote hizo?
“Nina mizigo yangu imekwama nataka nikaikomboe.Kesho nitakwenda benki na kukurejeshea pesa zako”
Sarah akafikiri kidogo na kusema
“mama naomba unipe masaa mawili,nitakuletea fedha hizo nyumbani”
“Ahsante sana Sarah” akajibu mama yake na kukata simu
“Sarah atatupatia fedha hizo.Lakini hakikisha kwamba kesho tumepata fedha za kumrudishia ndugu yako”
“Usijali mama kesho nitatumiwa fedha na tutazirejesha fedha za Sarah,ila nakuomba sana Sarah asifahamu lolote kama fedha hizo unanipa mimi.”
“Usihofu Loniki sintamwambia kitu”
“Haya ahsante mama.Niko chumbani kwangu” akasema Loniki na kuinuka akaelekea chumbani kwake.
Baada ya kuingia chumbani kwake akampigia simu Linah na kumuomba amfahamishe Khumalo kwamba tayari amekwisha pata kiasi cha pesa alichokuwa anakihitaji na atampelekea jioni ya siku hiyo kama alivyokuwa ameagiza

* * * *

Bado kitambaa kilikuwa machoni kwa Happy na hakuweza kuona chochote.Hakutambua walikuwa wapi lakini alichojua ni kwamba alikuwa wamefika mahala fulani na gari likasimama.Milango ya gari ikafunguliwa na wale watu wakashuka na kumshusha naye pia.Hakujua alikokuwa anaelekea lakini alihisi kama vile alikuwa anashushwa ngazi.Mara wakafika mahala wakasimama na watu wale wakajadili jambo halafu akasikia milango inafungwa na kitambaa kikatolewa machoni.Happy akajikuta katika chumba kikubwa chenye samani za kuvutia.Kulikuwa na kitanda kikubwa kizuri chenye nakshi,kilichotandikwa mashuka mazuri,.Kulikuwa pia na kabati kubwa la nguo na meza kubwa iliyosheheni vipodozi.Kulikuwa vile vile na runinga kubwa na sofa nzuri za kupendeza..hali ya hewa ilikuwa ni ya ubaridi uliotokana na kiyoyozi.
Happy alikitazama chumba kile halafu akageuza shingo yake na kumgeukia mwanadada aliyesimama mbele yake.
“Mmenileta wapi? Mnataka nini toka kwangu? Nani kawatuma mnilete huku? Happy akauliza maswali mfululizo.Mwanadada yule akatabasamu na kusema
“Usihofu Happy.Hapa uko salama na hakuna tatizo lolote.Jisikie huru na wala usiogope chochote.”
“mnataka nini kwangu? Nani kawatuma mnikamate na kuja kunifungia humu? Niambieni mnataka kiasi gani cha pesa? Familia yangu itatoa” akasema Happy huku machozi yakimtoka
“Relax Happy.Huna haja ya kutoa machozi.Sisi hatuna haja na pesa zako na wala hatujakuleta hapa kukudhuru au kuitaka familia yako itupe pesa” akasema Yule mwanadada
“Kama hamna shida na pesa,kwa nini basi mmeniteka nyara?
“Tumekuleta hapa ,kuna mtu anataka kuongea na wewe”
“Mtu anataka kuongea na mimi? Thats crazy.!!!! Kwa nini mtu huyo asinitafute nikaongea naye hadi awatumie ninyi mniteke na kunileta hapa?
“Happy darling,why don’t you take some rest first? Tumekuandalia kitanda kizuri.Feel at home.Anything you need let me know” akasema Yule mwanadada halafu akainuka sofani na kuufungua mlango mmoja
“Kuna bafu hapa.Ingia uoge ujisikie vizuri.Katika kabati kuna nguo nzuri utabadilisha baada ya kuoga”
“Nimesema sitaki kitu chochote,nataka mniache huru niende zangu.” Akasema Happy kwa ukali
“Huna haja ya kukasirika Happy.Mara tu mtu anayetaka kuongea nawe akifika tutakuacha huru.By the way ninaitwa Rosa” akasema Yule mwanadada.Happy akamtazama kwa hasira halafu akajitupa kitandani
“Mambo gani haya yananitokea mimi? Mbona mikosi inaniandama namna hii? Kabla ya suala moja kumalizika linaibuka lingine.why always me?” akawaza Happy huku machozi yakimtoka
“Watu hawa walionileta hapa ni akina nani ? Huyo mtu anayetaka kuongea na mimi ni nani? Anataka nini kwangu? Ouh Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja mnene akaingia akiwa na sinia la chakula.Happy akamkumbuka alikuwa ni mmoja wa watu waliomteka.Taratibu mtu yule akamsogelea Happy pale kitandani
“How do you feel Happy? Akasema Yule jamaa huku akiliweka sinia lile juu ya meza ndogo
“what do you want from me? Who are you people? Akauliza Happy kwa ukali
“Usihofu Happy.Sisi si watu wabaya na wala hatuna lengo baya nawe.Just relax and eat”
“Sintakula chochote hadi huyo mtu aliyewatuma mniteke na kunileta hapa aje anieleze sababu ya kunileta na kunifungia humu.”Yule jamaa akamtazama Happy usoni halafu akatoka nje.
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 45
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Watu hawa walionileta hapa ni akina nani ? Huyo mtu anayetaka kuongea na mimi ni nani? Anataka nini kwangu? Ouh Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja mnene akaingia akiwa na sinia la chakula.Happy akamkumbuka alikuwa ni mmoja wa watu waliomteka.Taratibu mtu yule akamsogelea Happy pale kitandani
“How do you feel Happy? Akasema Yule jamaa huku akiliweka sinia lile juu ya meza ndogo
“what do you want from me? Who are you people? Akauliza Happy kwa ukali
“Usihofu Happy.Sisi si watu wabaya na wala hatuna lengo baya nawe.Just relax and eat”
“Sintakula chochote hadi huyo mtu aliyewatuma mniteke na kunileta hapa aje anieleze sababu ya kunileta na kunifungia humu.”Yule jamaa akamtazama Happy usoni halafu akatoka nje.

ENDELEA…………..

Sarah aliwasili nyumbani kwako baada ya masaa mawili kama alivyokuwa ameahidi.Katika mkoba wake kulikuwa na kiasi cha shilingi millioni saba alizokuwa ameomba mama yake.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mama yake kumuomba msaada wa kiasi kikubwa cha pesa kwa hiyo alifanya kila aliloweza hadi akazipata fedha hizo.
Baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea sehemu alikokuwa mama yake halafu wakaelekea chumbani akamkabidhi fedha zile
“Mama mzigo huu hapa.Nimelazimika kuzichukua katika akaunti ya mume wangu kwa hiyo kama ulivyoahidi kuzirejesha kesho naomba iwe hivyo” akasema Sarah
“Ahsante sana Sarah.Kesho nitakurejeshea fedha zote”
“Sawa mama,lakini mbona hujaniambia fedha hizo ni kwa ajili ya nini? Umepatwa na tatizo gani?
“Usijali sarah.Ni suala la kawaida katika biashasra zangu” akasema mama yake.Sarah hakutaka maongezi mengi akatoka mle chumbani lakini wakati akitoka akagongana na Loniki ambaye naye alikuwa anaelekea chumbani kwa mama yake.Sarah akapatwa na wasi wasi.
“Whats going on here? kuna kitu gani kinaendelea kati ya mama na Loniki.? Sarah akajiuliza maswali lakini hakutaka kuwafuatilia akaendelea na shughuli zake.Baada ya kama dakika ishirini toka Loniki aingie mle chumbani mwa mama yake mlango ukafunguliwa na wote wawili wakatoka.Sarah akamfuata mama yake
“mama kitu gani kinaendelea kati yako na Loniki?Mna mipango gani ya siri?
“Hakuna kitu chochte kibaya Sara.Kuna masuala Fulani yanayohusiana na biashara zangu ambayo Loniki anakwenda kuyashughulikia.”
“Ni masuala gani hayo mama? Naomba unieleze.”
“Ni masuala yangu ya kibiashara. Mbona maswali yanakuwa mengi Sarah?
“mama nina haki ya kufahamu tatizo lako kama mwanao.Kinachonishangaza ni kwamba miaka hii yote Loniki hakuwepo na tuliokuwa tukikusaidia katika masuala yako mbali mbali ya kibiashara ni mimi na Vero sasa iweje leo uniache mimi na umtumie Lonny?
“Sarah si kila kitu kuhusiana na biashara zangu unapaswa kukifahamu.” Akasema mama yake
“Mama nimetoa pesa zangu nyingi katika tatizo hilo kwa hiyo nina haki ya kujua zinakwenda wapi”
“Sarah inatosha sasa.Nimechoshwa na maswali yako.Umenipa pesa subiri kesho nitakurejeshea pesa zako” Akasema kwa ukali mama yake na kuanza kuondoka lakini Sarah akamuita
“Samahani mama kama nimekuudhi lakini nimekuuliza kwa nia njema tu ya kutaka kufahamu kama una tatizo lolote.Siku zote nimekuwa rafiki yako na hujawahi hata siku moja kunificha tatizo linalokusumbua.Vile vile hata siku moja hujawahi kuniomba pesa na ninafahamu unazo pesa za kutosha toka katika miradi yako .Kitendo hicho kimenistua sana na ndiyo maana nahitaji kufahamu endapo kuna matatizo katika biashara ili kwa pamoja tuone namna ya kuweza kuyaondoa”
“Sarah ahsante sana kwa msaada wako.Kwa sasa tatizo lenyewe limekwisha na endapo nitahitaji msaada zaidi nitakueleza.” Akasema mama yake na kuondoka.Hakutaka tena maongezi na Sarah
“lazima nifahamu Lonny anazipeleka wapi zile pesa.Sina hakika kama mama ana shida ya pesa.Biashara zake zinamuingizia mamilioni ya pesa na hawezi kuwa na shida na millioni saba.Lazima kuna kitu kinaendelea hapa ambacho mama hataki kukiweka wazi.Hata macho yake yanaonyesha kabisa kuna jambo analificha.Taa ya tahadhali inaanza kuwaka kichwani,inaonekana Lonny ameanza kutekeleza mpango wake wa kulipiza kisasi.” Akawaza Sarah

* * * *

Saa kumina mbili za jioni gari aina ya Toyota Surf lenye rangi nyeusi likawasili katika jumba moja la kifahari lenye rangi nyeupe lilizungukwa na miti na maua mazuri
Linah na Loniki wakashuka katika ile gari .Wakiongozwa na kijana aliyetumwa kwenda kuwachukua wakaingia ndani ya jumba lile kubwa la kifahari.Walikaribishwa katika sebule kubwa na nzuri sana na baada ya dakika tano akajitokeza Khumalo.
“Karibuni sana” akasema khumalo huku akiwapa mikono
“Hii ni moja ya makazi yangu pia na mara nyingi hupenda kuja kupumzika huku.Ni watu wachache sana wanaopafahamu mahala hapa? Akasema Khumalo huku akitabasamu na kupuliza moshi wa sigara hewani
“Hongera ,umejitahidi sana Khumalo” akasema Linah
“Ahsante sana” akajibu Khumalo halafu kikapita kimya kifupi ,Khumalo akasema
“Miss Tanzania tuko naye hapa na anaendelea vizuri”
“Kazi nzuri sana Khumalo.Hakukuwa na rabsha zozote wakati wa kumchukua? Akauliza Loniki
“Hapana Loniki.Hakukuwa na tatizo lolote.Tukio hilo limefanywa kitaalamu sana.Natumai umekuja na ule mzigo kamili kama tulivyoongea” akasema Khumalo
“Ndiyo Khumalo.Nimekuja kamili” akasema Loniki na kuufungua mkoba wake akatoa mabunda ya noti akayaweka mezani.
“million thelathini.” Akasema Loniki.Khumalo akayashika mabunda yake akatabasamu
“Mtu wangu yuko wapi? Akauliza Loniki
“Usihofu Loniki.Utamuona tu” akasema Khumalo halafu akayakusanya mabunda yale ya noti akaondoka nayo na baada ya dakika tano akarejea na kuwaomba Linah na Loniki wamfuate.Waliongozana hadi katika chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na mitambo mingi.Kilionekana ni kama studio.Kulikuwa na kompyuta nyingi na runinga kubwa ukutani.
“Nipatie namba nane” Khumalo akamwambia kijana aliyekuwamo mle ndani na baada ya sekunde kadhaa kupitia ile runinga kubwa Happy akaonekana akiwa amekaa kitandani.Loniki akasonya na kukunja uso kwa hasira
“Unaweza kuniruhusu nikaonana naye ana kwa ana?
“Hapana Lonny.Hutakiwi kuonana naye ana kwa ana.si vizuri kwa usalama wetu.Nadhani tusiendelee kupoteza muda ni wakati wa kuianza kazi sasa”.Akasema Khumalo,Loniki akatikisa kichwa kuitikia lakini ilionyesha dhahiri kamba alikubali kwa shingo upande.Lengo lake lilikuwa ni kuonana ana kwa ana na Happy
“Ninyi mtashuhudia kila kinachoendelea kupitia hii runinga ambayo imeunganishwa na kamera zilizoko katika chumba alimo Happy.Mtashuhudia kila kitu” akasema Khumalo halafu akatoka mle chumbani.Bado Loniki aliendelea kumtazama Happy kwa hasira

Mlango wa chumba alimowekwa Happy ukafunguliwa na Khumalo akaingia.Happy ambaye alikuwa amejiinamia akainua uso wake baada ya kusikia mlango unafunguliwa.Akakutana na sura iliyomstua na kumfanya aismame
“Its you ..!!!” akasema Happy kwa mshangao
“Hallo Happy..!! akasema Khumalo huku akitabasamu.
“Kumbe ni wewe !!!.Nakukumbuka sana.Ulikuwepo mahakamani juzi na ulikuwa unaniangalia kwa jicho baya.Who are you? ..Happy akasema kwa hasira
Khumalo akatabasamu na kuizima sigara aliyokuwa anaivuta
“Calm down my love.Huna haja ya kuhamaki namna hiyo.Unajisikiaje Happy? Mbona hujala chakula? Akasema Khumalo na kuketi sofani.Happy bado aliendelea kumuangalia kwa hasira
“Niambie ni kwa nini umewatuma watu wako waniteke na kunifungia humu? Unataka nini toka kwangu?
“Happy naomba ukae,kuwa na amani na wala usiwe na hasira.Nimekuleta hapa nina maongezi nawe mafupi lakini ya muhimu sana.Baada ya kumaliza maongezi nawe nitakuruhusu uende zako” akasema Khumalo kwa upole
“Unataka kuongea nami nini na kwa nini usinitafute katika njia za kawaida hadi uniteke nyara? Akauliza Happy
“Happy ni saa moja za jioni sasa na nina imani familia yako tayari imeanza kuwa na wasi wasi juu yako kwa hiyo naomba tusipotee muda .Nisikilize kile kilichonifanya nikulete hapa halafu nitakuacha uende zako” akasema Khumalo na kauli ile ikamfanya Happy atulie.
“Naitwa Job.Mimi ni mfanya biashara wa kimataifa.Nafikiri ni mara yako ya pili kuniona.Baada ya kujitambulisha kwako ,napenda nichukue nafasi hii kukuomba samahani kwa usumbufu wote ulioupata.Nafahamu ulikuwa na shughuli zako nyingi tu na zote zimevurugika kwa kukuleta hapa.Kuna mtu ambaye alitaka uwepo hapa kwa sababu anazojua yeye mwenyewe lakini kwa bahati mbaya hutaweza kumuona mtu huyo kwani jukumu zima la kuongea nawe amenikabidhi mimi.” Akasema Khumalo na kukaa kimya akamuangalia Happy
“ Ni nani huyo aliyekutuma unikamate? Ni Savanna? Akauliza Happy kwa hasira.Khumalo hakujibu kitu akamuangalia Happy kwa makini usoni na kusema
“Happy nafahanmu uko katika wakati mgumu hivi sasa kutokana na mfululizo wa matukio lakini kuna swali moja tu ninalotaka kukuuliza.” Khumalo akatulia halafu kwa sauti ndogo akauliza
“Do you love Patrick?
Happy akamtazama Khumalo kwa mshangao na kusema
“yes I do love him”
“How much do you love him?
“More than my life” akajibu Happy kwa ufupi
“Good.Nafurahi kusikia hivyo” akasema Khumalo
“Jibu lako ninanifanya niamini kwamba uko radhi kufanya jambo lolote kwa ajili yake?
Happy akamuangalia Khumalo machoni halafu akasema
“Ndiyo .”
“nafurahi sana kusikia hivyo.Ni watu wachache sana ambao wanaweza kuyatoa maisha yao kwa ajili ya wale wawapendao.” Akasema Khumalo akakaa kimya kwa muda halafu akasema
“Patrick alikuwa na mpenzi wake aitwaye Veronika.walipendana sana na walikuwa katika hatua za mwishoni ili wafunge pingu za maisha na kuishi maisha yenye raha,lakini ulipojitokeza wewe mipango yao yote ikavurugika. Patrick alibadilika na kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa yake na Vero.Watu wengi sana waliumia.Vero alipatwa na uchungu mwingi na hatimaye alifariki dunia.Ni pigo kubwa kwa ndugu zake,rafiki zake na wale wote waliompenda.Matukio haya yote yaliyotokea yanadhihirisha wazi ni namna gani wewe na Patrick mnavyopendana.Ninadiriki kusema kwamba wewe na Patrick mmeumbwa ili muwe pamoja.Penzi lenu ni zito na la kweli na hakuna wa kuwatenganisha katika hii dunia” akasema Khumalo .Happy bado aliendelea kumshangaa asielewe alikuwa anamaanisha nini kwa maneno yale.Kumalo akaendelea
“Awali ulinihakikishia kwamba uko tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya Patrick.Vizuri sana Happy.Nitapenda nilitibitishe hilo siku ya leo” akasema Khumalo
“Sijakuelewa unamaanisha nini.Naona unaongea maneno mengi sana na sikuelewi unahitaji nini toka kwangu.Kama unahitaji pesa niambie unahitaji kiasi gani nikupatie ili niondoke zangu” akasema Happy
“Happy naomba unisikilize tena unisikilize kwa makini sana.Hatuna haja na pesa zako ,mtu aliyetutuma tukulete hapa ametupa pesa nyingi sana ,a lot of money .Kwa hiyo hatuna shida na senti yako hata moja.” Akasema Khumalo
“Hivi tunavyoongea “ akaendelea Khumalo
“Kuna mtu ambaye ni mfanyakazi wa idara ya magereza anayefanya kazi katika gereza alimo Patrick,yuko tayari na chakula chenye sumu ambacho anasubiri kumpa Patrick na baada ya dakika kumi tu atakuwa amekufa.Anachosubiri ni maelekezo yangu tu.Just one call and Patrick dies” akasema Khumalo
“whaaattt…!!!!!!!!!!.Happy akastuka na kusimama akamuangalia Khumalo kwa hasira
“Najua umestuka sana kusikia kwamba Patrick yuko hatarini kuuawa.Najua Patrick ndiye mwanaume wa maisha yako na endapo atafariki basi ndoto zako zote za kuwa na maisha yenye furaha pamoja naye zitayeyuka.Maisha yako yataharibika na juhudi zako zote ulizozifanya katika kulijenga penzi lako na Patrick zitakuwa ni kazi bure.Maisha ya Patrick ,mwanaume umpendaye yako mikononi mwako hivi sasa.Wewe ndiye utakayeamua hatima ya maisha yake kwa sasa endapo aendelee kuishi au afariki dunia kwa sumu.” Akasema Khumalo.Happy akatetetemeka .Khumalo hakuonyesha kama anafanya masihara
“Please Job,don’t ever hurt Patrick.Hakuna anayefahamu umuhimu wake kwangu.Patrick ndiye maisha yangu,ndiye furaha yangu,ndiye kila kitu kwangu.Siwezi kuishi bila yeye.Tafadhali naomba msimfanye jambo lolote la kumdhuru.Nambieni mtu aliyewatuma amewapa shilingi ngapi? Nitawapa mara mbili yake” akasema Happy huku akilia
“Happy sisi kwa maelekezo tuliyopewa na mtu aliyetutuma tukulete hapa ,hatutamgusa Patrick na wewe utaachiwa huru endapo utakubali kufanya anavyotaka yeye.”
“Huyo mtu anataka nini toka kwangu? Nimemkosea nini? Naomba niongee naye mimi mwenyewe anieleze nilichomkosea” akasema Happy
“Hapana Happy.Huwezi kuongea naye.You’ll talk to me” akasema Khumalo
“Ok Niambie unataka nini? Huyo mtu wenu anataka nini toka kwangu kama malipo ya kutomdhuru Patrick?
“Ni kitu kidogo sana ambacho kiko ndani ya uwezo wako.Kabla sijakwambia nini unatakiwa kufanya hebu kwanza angali picha hizi namna mtu aliyekula sumu hii tunayotaka kumpa Patrick anavyokufa” akasema Khumalo na kwenda katika runinga akachomeka kifaa kidogo cha kuhifadhi kumbu kumbu na kukiwasha.Picha zikaanza kuonekana
“Ukimaliza kuangalia kama utakuwa tayari kumuokoa Patrick utabonyeza kitufe hiki chekundu.Hii ni kengele ambayo itaniashiria kwamba uko tayari na mimi nitakuja mara moja.You have twenty minutes to decide” akasema Khumalo na kutoka.Happy akabaki peke yake mle chumbani akitazama picha zile za kutisha

* * * *

Baada ya kutoka katika chumba alichokuwamo Happy ,chumba ambacho kilijengwa chini ya ardhi,Khumalo akapanda moja kwa moja hadi katika chumba walimo Linah na Loniki walikokuwa wakifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea kule chini kupitia runinga kubwa.
“Nimemuacha aangalie picha zile na nina hakika baada ya kumaliza kuzitazama lazima ataniita.Anampenda Patrick sana na hawezi kukubali Patrick adhurike.” Akasema Khumalo
“Bado roho yangu haina amani kabisa Khumalo.Nilichokuwa nakitaka ni kuona mida hii Happy akiwa katika mateso makali sana.” Akasema Loniki
“Relax Lonny.Hii ni mbinu ya kumfanya Happy akubali kufanya mapenzi yeye mwenywe kwa hiari yake na vijana wetu na ili filamu zitakapotoka isionekane kwamba kuna nguvu ilitumika.Ninakuhakikishia Lonny ,kama lengo lako ni kutaka Happy ateseke basi ndani ya muda mfupi ujao atapata mateso makali sana na kwa namna jina lale litakavyochafuka nina hakika lazima atachukua jukumu la kujimaliza .Filamu hiyo tutaisambaza katika mitandao ya ngono duniani,katika mitandano ya kijamii,katika simu na kila sehemu ambayo tutaweza kuitumia kumchafua Happy.Atateseka kwa maisha yake yote yaliyobaki hapa duniani.” Akasema Khumalo
Lonny bado aliendelea kumtazama Happy kwa hasira kupitia runinga ile.
“Usisahau vile vile kwamba picha zitakazopigwa ,Happy akifanya mapenzi na vijana wetu atafikishiwa pia Patrick gerezani.I swear to you Lonny,kwa namna Patrick anavyompenda Happy I’m sure he will drop dead” akasema Khumalo huku akicheka
“Kwa mtu mwenye jina kubwa kama la Happy kuingia katika kashfa kubwa ya ngono ni habari ambayo haitaweza kufutika kwa urahisi katika vinywa vya watanzania.Ni historia ambayo itadumu kwa vizazi hadi vizazi na atakayeteseka si Happy pekee bali hata familia yake ka ujumla na zaidi sana Patrick” Akasema Khumalo huku akipuliza moshi mwingi hewani
“Damn you Happy !!.Laiti ningekuwa na uwezo wa kufika katika chumba ulimo ,ningekuua mimi mwenyewe kwa mikono yangu.Natamani hata niutafune moyo wako.Wewe ni sababu ya mdogo wangu kufariki dunia.I swear I’ll make your life a living hell before you die” akawaza Lonny huku akiendelea kumtazama Happy kwa hasira kupitia Runinga


* * * *

Familia yote ya mzee Kibaho ilikwisha rejea nyumbani na walikuwa wanajiandaa kupata mlo wa usiku.Ni Happy pekee ambaye hakuwa ameonekana .Toka amerejea nyumbani,mzee Kibaho hakuwa ameonana na mwanae kipenzi Happy.
“Happy ameshindaje? Yuko wapi? Akauliza mzee Kibaho
“Bado hajarejea toka alipoondoka asubuhi.” Akajibu mama yake Happy
“Toka alipoondoka asubuhi?? Akashangaa mzee Kibaho
“Ndiyo.Aliondoka hapa nyumbani asubuhi na alisema kwamba hatakawia kurudi lakini nashangaa mpaka mida hii hajarajea”
“Alikuaga anakwenda wapi?
“Hakusema anakwenda wapi lakini ilionekana alikuwa na haraka na mahala alikokuwa anakwenda”
Mzee Kibaho akainuka na kwenda chumbani kwa Happy kuhakikisha kama ni kweli Happy hayupo.Akarudi sebuleni na kuchukua simu yake akapiga namba za simu za Happy lakini simu haikuwa inapatikana.
“Si kawaida ya Happy kuzima simu.” Akasema kwa wasi wasi mzee Kibaho huku akijaribu tena na tena kupiga simu ya Happy lakini jibu likawa ni lile lile namba anayopiga haipatikani.
“Margreth,Happy hakukueleza mahala anakoelekea leo? Akauliza mzee Kibaho baada ya Margreth kuingia pale sebuleni
“Hapana baba .Jana nilichelewa sana kurudi na sikuweza kuonana naye na leo asubuhi nimeondoka mapema mno na yeye akiwa bado amelala.Nilimtafuta katika simu yake mchana lakini simu yake haikuwa ikipatikana”
Mzee Kibaho akamuita Pendo mfanyakazi wa ndani
“Pendo wewe ndiye uliyekuwa na Happy jana mahakamani.Kuna jambo lolote alikueleza kuhusu mahala alikokusudia kwenda leo?
“Hapana baba hakunieleza chochote.Ninachokumbuka ni kwamba kabla hatujaondoka pale mahakamani alitokea kijana mmoja akaongea kitu na dada halafu tukaondoka naye hadi katika baa Fulani wao wakashuka mimi nikabaki ndani ya gari.Walikuwa na maongezi muhimu lakini sikujua walikuwa wanaongea nini.Baada ya muda mfupi dada akarejea garini kwa kasi akauinamia usukani akaanza kulia.Nilimuuliza alikuwa analia nini lakini hakunijibu kitu,akawasha gari tukaondoka.Jioni mida ya saa kumi na moja akanipigia simu akaniomba nimtengenezee juisi ya maembe.Nilipompelekea chumbani kwake nilimkuta akiongea na simu na kuna mtu alikuwa kama anajibizana naye.Walikuwa ni kama wanazozana.Nakumbuka nilimsikia akitaja jina la Savanna katika maongezi yao”
“ Savanna !!..akastuka mzee Kibaho
“Ninayo namba ya simu ya Savanna ngoja tumpigie pengine anaweza kufahamu mahala alipo Happy” akasema Margreth
“Nipe niongee naye” akasema mzee Kibaho
“hallo Margreth” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Hallow Savanna.Mimi ni mzee Kibaho baba yake na Happy”
“Ouh shikamoo mzee.”
“marahaba Savanna.Samahani kwa kukusumbua usiku huu.Tumekuwa na wasi wasi kuhusu Happy.Hajaonekana toka alipoondoka nyumbani asubuhi ya leo na hata katika simu hapatikani.Umeonana naye kwa siku ya leo?
“Ndiyo baba.Happy nilionana naye asubuhi .Tulikutana gerezani alikuja kumtembelea Patrick.Mimi nilimkuta tayari amekwisha fika na inaonekana aliwahi mapema sana.Hatukupata wasaa wa kuongea zaidi ya kusalimiana kwa sababu nilikuwa nimeongozana na familia ya Patrick.” Akasema Savanna.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu
“Ahsante sana Savanna,.Endapo ikitokea ukawasiliana naye basi tutaarifu mara moja”
“Sawa baba nitafanya hivyo.” Akajibu Savanna na kukata simu
“Kwa mujibu wa maelezo ya Savanna,Happy alikwenda gerezani asubuhi ya leo kuonana na Patrick.” Akasema mzee Kibaho baada ya kumaliza kuongea na Savanna simuni
“Atakuwa ameelekea wapi? Akauliza mama yake
“Alipoondoka asubuhi alinihakikishia kamba hatakawia kurudi.Na hata mavazi yake hayakuonyesha kama alikuwa na safari ya kuelekea mbali.Alivaa mavazi ya kawaida”
“Kama ni hivyo atakuwa wapi? Akauliza Magreth na kisha wakaanza kupiga simu kwa watu mbalimbali kumuulizia Happy lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa amemuona Happy
“Msiwe na wasi wasi.Happy ni mtu mzima na anafahamu kitu anachokifanya.Inawezekana amepatwa na dharura kama mnavyofahamu kwa siku za hivi karibuni amakuwa na mambo mengi .Tuendeleeni kumsubiri na nina hakika atarejea muda si mrefu” mzee Kibaho akawapa moyo familia yake lakini hata yeye alikuwa na wasi wasi mwingi moyoni kutokana na mfululizo wa matukio yaliyomuandama binti yake
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 46
MTUNZI 😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Msiwe na wasi wasi.Happy ni mtu mzima na anafahamu kitu anachokifanya.Inawezekana amepatwa na dharura kama mnavyofahamu kwa siku za hivi karibuni amakuwa na mambo mengi .Tuendeleeni kumsubiri na nina hakika atarejea muda si mrefu” mzee Kibaho akawapa moyo familia yake lakini hata yeye alikuwa na wasi wasi mwingi moyoni kutokana na mfululizo wa matukio yaliyomuandama binti yake

ENDELEA……………….

Mlio wa kengele ukasikika katika chumba walichokuwamo akina Khumalo.
“kazi imeanza.” Akasema Khumalo na kuondoka kuelekea katika chumba alichokuwamo Happy
“Hallo Happy” akasema Khumalo
“Stop it..Please stop it” akalia Happy huku akiyafunika macho yake kwa viganja vya mikono ili asiendelee kuzitazama picha zile za kutisha
“Umeona Happy? Umeona namna sumu hii inavyowatesa watu kabla hawajafa?
“ Please Job ,dont do that to Patrick.I beg you don’t hurt Patrick” akalia Happy
“Kwa hiyo umeamua nini? Uko tayari kufanya kile tunachotaka kwa ajili ya kuokoa uhai wa Patrick? Akauliza Khumalo
“I’m ready.Please don’t hurt Patrick.I’m ready to do anything to save him”
“Vizuri sana.Watu kama wewe ni wachache sana.Hata mimi namuonea wivu Patrick kwani amempata mwanamke anayempenda kwa dhati.”
“Tafadhali sema mnataka niwafanyie nini? Akasema Happy huku akifuta machozi.Khumalo akainuka pale sofani alipokuwa amekaa akamsogelea Happy
“Stop crying Happy.Usilie tena.” Akasema Khumalo halafu akanyamaza kidogo akamtazama Happy usoni na kusema
“ Aliyenituma nikulete hapa alitoa sharti moja tu ambalo ukilitekeleza utaokoa maisha ya Patrick na wewe utakuwa huru.Anao vijana wake wawili wanaokupenda sana na anataka ufanye nao mapenzi.”
“ What !!!!????...Happy akastuka na kumtazama Khumalo kama ameona mzuka
“Hilo ndilo sharti pekee alilolitoa mtu aliyekuleta hapa.Ni juu yako kukubali au kukataa.Kama hautakuwa tayari sisi tutakuacha uende zako lakini nakuhakikishia kwamba wakati wewe ukitoka ndani ya jumba hili,mtu umpendaye kuliko wote duniani atakuwa atakuwa tayari amelala usingizi wa milele.” Akasema Khumalo na kuzidi kumtisha Happy.
“ Ni nani huyo shetani ambaye amenileta hapa? Ni nani huyo asiyekuwa na hata chembe ya ubinadamu? Nimemkosea kitu gani hadi aamue kunitenda namna hii ? akasema Happy huku akilia kwa uchungu
“Happy ni juu yako kuamua .Kilio na matusi kamwe havitakusaidia na muda wetu unazidi kwenda.Ninakupa tena dakika kumi nyingine za kuamua “ akasema Khumalo na kupiga hatua kutoka mle chumbani
“Ouh My God !!!! akalia Happy.Alihisi kuchanganyikiwa
“whats happening to me? Ni kweli nina laana? Kwa nini ninaandamwa na mikosi kama hii kila siku? Huyu mtu aliyenileta hapa ni nani na kwa nini atake kunidhalilisha namna hii? Happy akazidi kulia
“Huyu mtu aliyenileta hapa lengo lake ni moja tu ,kunidhalilisha. Nini kitatokea kama nitakataa kufanya anavyotaka? Je ni kweli Patrick yuko katika hatari ya kuuawa? Sina hakika kama suala hili ni la kweli.Huyu mtu lengo lake ni kuudhalilisha utu wangu.Ninaanza kuhisi mtu huyu atakuwa ni Savanna kwani ndiye mtu niliyelumbana naye jana na tukatoleana vitisho.Pengine ameamua kunionyesha uwezo wake kwa kuniteka na kunileta hapa ili nidhalilike.Siwezi kukubali hata kidogo kuwapa nafasi ya kuuchezea mwili wangu.Ni bora waniue kuliko kuwapa nafasi ya kunichezea.” Akawaza Happy lakini mara akastuka
“What if its true and Patrick is going to die? Inawezekana pengine watu hawa wakawa wanasema kweli ..Am I ready to let Patrick die? I’m confused..!!! Happy akahisi kuchanganyikiwa
“Patrick amejitolea mengi kwa ajili yangu na hata hivi sasa anasota gerezani kwa ajili yangu.Kwa nini na mimi nishindwe kusimama imara kuutetea uhai wake? Kwa maana hiyo itanilazimu kukubaliana na matakwa yao ya kufanya mapenzi na watu wawili? Ouh Jamani akili yangu naona haifanyi kazi tena.Sijui nifanye nini” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa Khumalo akaingia.Safari hii macho yake yalionekana mekundu na yasiyo na masihara hata kidogo.Happy akaingiwa na woga.Mwili ukamtetemeka
Happy dakika kumi zimekwisha na ninadhani tayari umekwisha fanya maamuzi” Akasema Khumalo huku akimuangalia Happy kwa macho makali sana.
Happy mwili ulimtetemeka na hakujua aseme nini
“Inaoneka bado hujaamua lolote.I’m so sorry Happy.” Khumalo akasema kwa masikitiko halafu akatoa simu yake na akabonyeza namba na kupiga
“Hallow Josh,amekataa kutoa ushirikiano endelea na mpango wetu,mpe Patrick chakula” akasema Kumalo halafu akamuangalia Happy kwa masikitiko
“I’m so sorry Happy.Muda mfupi toka sasa Patrick hatakuwa nasi tena.”
“Stop it !!!!!..Please stop it !!!!...” akapiga kelele Happy
“Please stop it.Dont kill Patrick.Niko tayari kufanya mnavyotaka.” Akasema Happy.Khumalo akamtazama kwa makini machoni halafu akatoa simu yake na kupiga
“Hallow Josh,subiri kwanza.Sitisha kwanza hilo zoezi” akasema Khumalo na kukata simu
“Happy nadhani sasa umeamua kumuokoa Patrick”
“Niko tayari kufanya lolote ili msimdhuru Patrick”
“Vizuri sana” akasema Khumalo huku akitabasamu
“Please don’t hurt Patrick.Hastshili mateso yoyote.Kama ni mateso naomba mnitese mimi”
“Hatukutesi Happy.Fanya kama ulivyoamriwa na utakuwa huru na hakuna mtu atakayemgusa Patrick” akasema Khumalo
“Niko tayari kufanya mnavyotaka lakini kwa sharti moja tu.Mtu huyo ambaye mnataka afanye mapenzi na mimi lazima atumia kinga”
“Usihofu kuhusu hilo Happy.Tunazingatia sana usalama wa afya yako.Jiandae Happy,baada ya muda watakuja vijana wawili unachotakiwa ni kuonyesha ushirikiano na jitahidi kuwaridhisha vijana hao.Baada ya hapo tutakuruhusu uende zako” akasema Khumalo halafu akatoka mle chumbani akimuacha Happy ameinama akilia
“Mpango mzima umekamilika .Mtashuhudia kila kitu muda si mrefu.Ninawahakikishia kwamba hili ni pigo kubwa kwa Happy” akasema Khumalo baada ya kurejea katika chumba walichokuwamo akina Linah
Baada ya dakika zipatazo kumi hivi,Khumalo akiwa ameongozana na vijana wawili waliojazia miili yao na wenye vifua vipana,wakaingia katika chumba alichokuwamo Happy.Vijana wale walikuwa wamezificha nyuso zao ili wasitambulike. Happy alipowaona akaogopa na kuanza kulia.
“Naombeni mnihurumie jamani.Nimewakosea nini hadi mnifanyie hivyo? Akalia Happy lakini Khumalo wala vijana wake hawakumsikiliza
“Happy nyamaza kulia.Futa machozi yako na tukamilishe zoezi letu ili tukurejeshe nyumbani kwenu.Nina imani familia yako ina wasi wasi mwingi sana sasa hivi” akasema Khumalo huku akiwasha taa kubwa iliyokuwamo mle chumbani na kukifanya chumba kiwe na mwanga mkali
“Happy kumbuka makubaliano yetu kwamba unatakiwa uonyeshe ushirikiano na uwaridhishe vijana wangu .Tumeelewana Happy? akasema Khumalo
“Ndiyo “ akajibu Happy
“Vizuri sana” akasema Khumalo na kutoka mle chumbani .Jamaa mmoja kati ya wale vijana walioletwa na Khumalo akamfuata Happy akaketi karibu yake na kumfuta machozi
“Fanya kama alivyokuamuru mkuu wetu.Endapo utaenda kinyume na matakwa yake anaweza akabadilika na akibadilika huwa ni mtu mbaya sana” akasema yule jamaa huku akianza kumtomasa Happy
“Please don’t hurt me “ akasema Happy
“Hautaumia mrembo.You’ll feel like you are in heaven” akasema jamaa mwingine
“Ninafanya hivi kwa ajili ya Patrick, kwa ajili ya kumlinda yeye “akawaza Happy halafu kijana mmoja akaanza kufungua vifungo vya lile shati lake dogo alilokuwa amevaa
“Leave me alone…Nitafanya mwenyewe” akafoka Happy na kumsukuma Yule jamaa halafu akasimama na kuanza kufungua vifungo vya shati lake huku machozi yakimtoka
“Mtu anayenifanyia kitendo hiki ni nani? Nimemkosea kitugani? akawaza Happy
Khumalo,Linah na Loniki walikuwa wameyaelekeza macho yao katika runinga ile kubwa mbele yao wakiangalia namna zoezi linavyoendelea.Baada ya kama dakika tano za mabishano kati ya Happy na wale vijana hatimaye vijana wale wenye nguvu walifanikiwa kumuangusha Happy kitandani na kuanza kumuingilia kwa zamu.Happy alilia sana wakati vijana wale wakiendelea na udhalimu wao juu ya mwili wake.Zoezi liliendelea huku likiendelea kurekodiwa pamoja na kupigwa picha.
Zoezi lilichukua zaidi ya dakika ishirini .Vijana wale walimaliza kazi waliyopewa huku wakihema kwa nguvu sana.Taratibu waliondoka mle chumbani na kumuacha Happy akiwa analia.
“kazi tayari” akasema Khumalo huku akitabasamu
“Ina maana kazi ndo imeishia hapa? Akauliza Loniki kwa mshangao
“Pesa zote hizi nilizotoa ni kwa ajili ya kazi hii ?
“Ndiyo Loniki.Lengo lako ni kumuadhibu Happy,? Akasema Khumalo
“Ndiyo” akajibu Happy
“Kama lengo lilikuwa hilo basi kazi imekwisha kwa leo na subiri kwa hatua itakayofuata.Kesho asubuhi nchi nzima itatikisika kwa taarifa hii.Ni skendo ambayo haijawahi kutokea hapa nchini” akasema Khumalo
“Kwa hiyo nini kitafuata baada ya hapa? Akauliza Loniki
“Niachie mimi kila kitu.Kesho asubuhi usiache kufuatilia vyombo vya habari,magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii.Taarifa itakayokuwa inatawala ni ya picha za ngono za Happy” akajibu Khumalo.
Baada ya maongezi kadhaa na Khumalo Linah akamshika mkono rafiki yake Loniki wakaelekea katika gari ambalo liliwarudisha hadi ofisini kwa Linah ambako Loniki alichukua gari lake na kurejea nyumbani
Baada ya Loniki na Linah kuondoka ,Khumalo akaelekea katika chumba alimo Happy,akaufungua mlango na kuingia ndani.Happy alikuwa amelala kitandani akilia.Khumalo akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akapuliza dawa ya usingizi na kutoka mle chumbani
Baada ya dakika kumi na tano kupita toka Khumalo aipulize dawa ile katika chumba alichokuwamo Happy,Khumalo akarejea akiwa na vijana wake na kumkuta tayari Happy amelala fofofo hajitambui.Wakamuinua na kumpakia katika gari lake na kuondoka naye
“Kazi ya kwanza imekwisha.Kazi iliyobaki ni kuzisambaza picha na video.Naamini hadi kesho asubuhi zoezi hili litakuwa limekamilika na hatutakuwa na deni tena kwa Loniki“ akawaza Khumalo akiwa na vijana wake wakimrejesha Happy nyumbani kwao.Khumalo ndiye aliyekuwa ametangulia mbele na gari lake halafu gari la Happy lililokuwa linaendeshwa na kijana mwingine likafuata nyuma.Tayari Khumalo alikuwa anafahamu mahala anakoishi Happy kwani alikwisha mfanyia uchunguzi wa kutosha.
Saa saba kasoro za usiku waliwasili nyumbani kwa akina Happy.Kwa haraka haraka vijana wale wa Khumalo wakashuka katika gari la Happy.Kabla ya kushuka walimuwekea kitu fulani puani na kumzindua toka usingizini .Akapiga chafya mfululizo.Kwa haraka vijana wale wakaingia katika gari la Khumalo na kuondoka kwa kasi maeneo yale.
Mlio wa magari nje ya nyumba yake,ulimstua mzee Kibaho ambaye alikuwa macho mpaka mida hii akimsubiri mwanae arejee.Akatoka chumbani kwake na kwenda getini.Mbwa walikuwa wanabweka.Akachungulia nje kupitia uwazi mdogo na kuliona gari la Happy.Haraka haraka akafungua geti na kuliendea gari.Akachungulia ndani ya gari na kumuona Happy akiwa amelala kitini.Akapigwa na butwaa kwa hali aliyokuwa nayo .Happy alikuwa amelegea na mwili wake haukuwa na nguvu hata kidogo.Kwa haraka akamtoa mwanae garini na kumpeleka ndani na familia nzima ikaamka .Kila mtu alistushwa na hali aliyokuwa nayo Happy.Haraka haraka akaanza kupatiwa huduma ya kwanza.Hakuna aliyefahamu nini kimemsibu hata akawa katika hali ile.Ilikuwa ni hali ya kusikitisha sana.Daktari wa familia aliitwa akafika kwa haraka kuja kumuangalia Happy,akampima na kisha akampatia dawa na kumtaka akapumzike hadi asubuhi atakapopata majibu ya vipimo alivyochukua.

*******************

Kumekucha Tanzania.Ni saa moja za asubuhi, jijini Dar es salaam barabara zimesheheni watu na magari wote walikuwa wanaelekea katika shughuli mbalimbali za kila siku za uzalishaji mali.Katika vibanda na katika sehemu mbali mbali za kuuzia magazeti,kulikuwa na makundi ya watu waliokuwa wakihitaji magazeti ili kufahamu kulichoandikwamo asubuhi hii.Katika baadhi ya vituo vya kuuzia magazeti kulitokea ugomvi wa watu wakigombea magazeti kitu ambacho ni nadra sana kushuhudiwa.
Gazeti lililozusha mjadala asubuhi hii na kuwafanya watu wajazane katika vibanda vya kuuzia magazeti na wengine kufikia hata hatua ya kurushiana makonde ni gazeti la Mitikisiko,gazeti maarufu kwa kuandika habari za udaku na hasa zile zinazowahusu watu maarufu ndani na nje ya nchi.Siku hii ya leo gazeti hili lilipambwa na kichwa cha habari kilichobeba habari iliyozua gumzo nchini.
“HAIJAWAHI KUTOKEA” hiki kilikuwa ni kichwa cha habari kilichoandikwa kwa maandishi makubwa na chini yake kulikuwa na vichwa vingine vidogo vidogo.
“NI VIGUMU KUAMINI LAKINI KWELI”
“HUU NDIO UCHAFU WA MISS TANZANIA”
Vichwa hivi vya habari vilisindikizwa na picha kubwa ya Happy Kibaho,akiwa mtupu huku sehemu ya kifuani na chini ya kiuno zikiwa zimezibwa kwa rangi nyeusi.Picha nyingine ilimuonyesha Happy akiwa amelala kitandani akiwa na wanaume wawili waliozifunika nyuso zao ambao ilionyesha wazi walikuwa katika harakati za kufanya mapenzi.
“Mlimbwende aliyenyakua taji kubwa la urembo hapa nchini la miss Tanzania ambaye siku chache zilizopita amelivua taji hilo kutokana na kashfa ya kujihusisha katika ugomvi wa kumgombania mwanaume,na kusababisha kifo cha msichana aitwaye Veronika ,ameingia katika aibu kubwa baada ya picha na video yake ya ngono kuvuja” Haya yalikuwa ni maelezo ya utangulizi ya habari hii kubwa na kulifanya gazeti la Mitikisiko kuongoza katika mauzo kwa siku hii.Taarifa ile iliendelea katika ukurusa wa tatu huku ikipambwa na picha zinazomuonyesha Happy akiwa mtupu huku akifanya mapenzi na wanaume wawili waliozifunika nyuso zao katika mitindo tofauti tofauti..Ilikuwa ni aibu nzito isiyoelezeka .
Katika tovuti mbali mbali na mitandao ya kijamii,tayari video na picha za Happy vilianza kusambaa kwa kasi kubwa na kuwa gumzo mtandaoni.Watu walikuwa wanatumiana video na picha hizo za Happy akifanya ngono na wanaume wawili hadi katika simu za mikononi.Kutokana na kukua kwa teknolojia ya upashanaji habari ndani ya masaa machache tayari habari kuhusu Happy ilikwisha sambaa karibu nchi nzima.
Mlango mdogo katika geti la kuingilia nyumbani kwa akina Happy ulikuwa wazi,hivyo kumfanya mama Joseph jirani wa akina Happy,apite kama mshale na kuingia ndani huku akihema akiwa na gazeti mkononi
“Mama Happy ..!!! akaita mama Joseph .Alikuwa anahema huku jasho likimtoka.Mama yake Happy ambaye alikuwa katika kazi za usafi wa nyumba asubuhi hii,akaja kwa kasi baada ya kusikia sauti ya mama Joseph.
“Mama Joseph kuna tatizo gani? akauliza mama Happy kwa mshangao
“Mama Happy njoo huku” akasema mama Joseph huku akimvuta mama Happy kuelekea sebuleni.
“Mama Happy umeshapata taarifa?
“Taarifa gani mama Joseph? Mama yake Happy akazidi kushangaa
“Ina maana hakuna hata mtu mmoja aliyekupigia simu kukueleza nini kimetokea leo?
“mama Joseph mbona unanichanganya? Nini kimetokea?
“Soma gazeti hili” akasema mama Joseph huku akimpa mama Happy gazeti lile alilokuwa amelishika mkononi.Mara tu mama Happy alipolitupia macho akaanguka na kupoteza fahamu
Mama joseph akapiga ukulele mkubwa uliomstua mzee Kibaho aliyekuwa chumbani na kumfanya atoke haraka na kuelekea sebuleni kuangalia kumetokea nini.Alistuka baada ya kumkuta mkewe akiwa ameanguka chini akiwa hana fahamu
“Nini kimetokea? Akauliza mzee Kibaho huku akimuinamia mkewe.Mama Joseph hakuweza kujibu chochote alikuwa anatetemeka huku machozi yakimtoka.Haraka haraka mzee KIbaho akaanza kumpatia mke wake huduma ya kwanza.
Kelele zile za mama Joseph,zilimstua pia Happy .Alizisikia kelele zile akiwa usingizini na mwanzoni alidhani labda alikuwa ndotoni lakini alipofumbua macho aliendelea kuzisikia.Akaogopa pengine kuna jambo baya limetokea pale nyumbani kwao. Kichwa kilikuwa kizito na mwili wake ulimuuma sana.Alisikia maumivu makali sana sehemu za kinenani lakini akajikaza na kuinuka na kukaa kitandani.Akafikiri kidogo halafu akavaa nguo na kutoka mle chumbani na kuelekea sebuleni ambako ndiko kelele zilikokuwa zinatokea.Alistuka baada ya kumuona mama yake akiwa amelala chini hana fahamu.Baba yake alikuwa anahangaika kumsaidia ili aweze kurejewa na fahamu.
Mama Joseph na mfanyakzi wa ndani Pendo walikuwa wanalia kwa uchungu.Mara tu mama Joseph alipomuona Happy ameingia pale sebuleni akazidi kulia.Happy akatamani ajue kilichokuwa kimetokea na kumpelekea mama yake apoteze fahamu,akamfuata mama Joseph na kumuomba anyamaze ili aweze kumueleza nini kilichotokea
“Mama mdogo kuna nini? Nini kimetokea hapa? ..akauliza Happy kwa sauti dhaifu lakini mama Joseph hakujibu kitu na badala yake akamuonyeshea ishara alichukue lile gazeti lilikokuwa limeanguka chini.Taratibu Happy akainama na kuliokota ,akalikodolea macho.Mwili wote ukamtetemeka alipokuwa analisoma.Alikuwa ni kama mtu aliyeliona jitu la kutisha.Mara gazeti lile likaanguka chini na uso wa Happy ukajaa machozi .Taratibu bila kuongea na mtu yeyote akageuka na kutembea kwa kasi kuelekea chumbani kwake.
Mama Joseph aliyekuwa anamuangalia Happy kwa makini ,akaogopa sana kutokana na mstuko alioupata Happy.Akamfuata mzee Kibaho na kumuomba amfuate Happy
“Kuna nini? Happy amefanya nini? Akauliza mzee Kibaho huku akiendelea na jitihada zake za kumpatia huduma ya kwanza mke wake ili aweze kurejewa na fahamu
Mama joseph akaliokota gazeti lililoanguka chini na kumpatia mzee Kibaho
“Hili ndilo chanzo cha haya yote” akasema mama Joseph
Mzee Kibaho akaanza kulipitia lile gazeti na mara akahisi mikono yake ikimtetemeka.
“Ouh My God !!!” akasema mzee Kibaho na kwa haraka akainuka na akaelekea chumbani kwa Happy.Mlango wa Chumba cha Happy ulikuwa umefungwa.Akagonga lakini hakukuwa na dalili zozote za kuwepo mtu ndani.Akachungulia katika tundu la funguo na kuiona funguo ikiwa ndani.
“Happy fungua mlango..Fungua mlango mwanangu …” akasema mzee Kibaho lakini hakusikia dalili zozote za kuwepo mtu mle chumbani.Kwa kasi akakimbia kuelekea chumbani kwake akachukua ufunguo wa akiba na kuja kuufungua mlango akaingia ndani
“Ouh Mungu wangu ..!!!!!..Mzee Kibaho nusura aanguke kwa alichokiona mle ndani.Happy alikuwa amelala kitandani huku mapovu yakimtoka mdomoni.
“Happy..!! Happy.!!! Happy.!!!!!...akapiga ukelele mzee Kibaho huku akimtikisa Happy lakini hakuwa na fahamu hata kidogo,alikuwa anakoroma.
“Ouh Mungu wangu !!” akasema mzee Kibaho baada ya kuiona chupa ndogo yenye dawa ya kuulia panya ikiwa mezani.Haraka haraka akamuinua Happy na kukimbia naye hadi garini.Mama Joseph na Pendo wakapiga ukeleel mkubwa baada ya kuishuhudia hali ile ya Happy.Mzee Kibaho hakuwajali akawasha gari lake na kwa kasi ya aina yake akaondoka pale nyumbani huku akipishana na majirani waliokuwa wakiingia kwa kasi mle ndani baada ya kusikia kilio cha mama Joseph na Pendo.
“Please God.dont let my daughter die, Please save her” mzee Kibaho ambaye kwa mbali macho yake yalilengwa na machozi ,alikuwa akiyarudia maneno haya mara kwa mara wakati akiendesha gari kwa kasi kuelekea hospitali.Kila sekunde zilivyozidi kusonga mbele ndivyo hali ya Happy ilivyozidi kubadilika na kupoteza matumaini.Alikuwa anakoroma na povu jingi likiendelea kumtoka
Geti la hospitali ya Brahmaputra inayomilikiwa na daktari bingwa Makhresh Patel lilikuwa wazi .Gari la mzee Kibaho lilikuwa likija kwa kwendo wa kazi huku likiwa limewasha taa zote.Watu waliokuwa wamesimama karibu na geti walikimbia baada ya kuliona gari lile namba lilivyokuwa likija.
Namna gari lile lilivyoingia hospitali na sauti za matairi yakilalama kutokana na breki kali aliyofungwa,iliwafanya madaktari na wauguzi watoke nje na kushuhudia nini kilichotokea.Mzee Kibaho akashuka na kukimbia na kuwataarifu wauguzi kwamba kulikuwa na mgonjwa mahututi ndani ya gari.Kwa kasi ya aina yake,wauguzi wakampakia Happy katika kitanda na kumkimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mzee Kibaho akaombwa asubiri nje.Bado mwili wake ulikuwa unamtetemeka kupita kiasi.Aliogopa sana.
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 47
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Namna gari lile lilivyoingia hospitali na sauti za matairi yakilalama kutokana na breki kali aliyofungwa,iliwafanya madaktari na wauguzi watoke nje na kushuhudia nini kilichotokea.Mzee Kibaho akashuka na kukimbia na kuwataarifu wauguzi kwamba kulikuwa na mgonjwa mahututi ndani ya gari.Kwa kasi ya aina yake,wauguzi wakampakia Happy katika kitanda na kumkimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mzee Kibaho akaombwa asubiri nje.Bado mwili wake ulikuwa unamtetemeka kupita kiasi.Aliogopa sana.

ENDELEA…………

“Please my Lord,don’t let my daughter die” akazidi kuomba mzee Kibaho.na mara simu yake ikaita.Alikuwa ni Margreth.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu kabla ya kuipokea simu ile halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea.
“Hallo Margreth” akasema mzee Kibaho
“baba uko hospitali gani?
“ niko hapa Brahmaputra hospital.Uko wapi Margreth?
“Nimefika hapa nyumbani sasa hivi nikaambiwa kuhusu hali ya Happy.Dady tell me please how’s she? Akauliza Margreth
“Tayari amepokelewa hapa na ameingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Madaktari wamesimamisha shughuli zote na wanajitahidi kuokoa maisha yake.”
“Unaonaje hali yake? Akauliza Margreth
“Margreth siwezi kusema chochote kwa sasa”
“sawa baba,nakuja sasa hivi huko hospitali” akasema Margreth
“Maggie mama yako anaendeleaje?
“Mama hali yake naye si nzuri hata kidogo.Amezinduka na kuzirai tena.Dokta Salome Yule jirani yetu yuko hapa anaendelea kumuhudumia.” Akasema Margreth.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu na kukata simu
“Whats happening to my family? Ee Mungu naomba unipe nguvu ya kuweza kuyakabili matatizo haya makubwa yanayoikabili familia yangu kwa sasa.Naomba umsaidie mwanangu Happy aweze kupona” Mzee Kibaho alikuwa anaomba kimoyo moyo.Hakuweza kutulia sehemu moja.Alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa.
Margreth aliwasili Brahmaputra hospital na moja kwa moja akaelekea mahala alikokuwa baba yake.Macho yalikuwa mekundu kwa kulia
“baba kuna taarifa yoyote tayari umepata kuhusiana na Happy? akauliza Margreth
“Hakuna taarifa yoyote mpaka hivi sasa.Bado madaktari wanaendelea kumshughulikia.” Akasema mzee Kibaho.Jibu lile likazidi kumtoa machozi Margreth.Baba yake akamsogelea na kumkumbatia
“Please Margreth be strong.We need to be strong for Happy” akasema mzee Kibaho huku naye sauti yake ikionyesha kutetemeka
“Dady why could Happy do such a thing to us? Kwa nini aamue kunywa sumu? Akasema Margreth huku akilia
“I don’t know Maggie,I don’t know”
“Inauma sana baba.Sijawahi kuumia kama nilivyoumia leo.Hapa nilipo ninahisi moyo wangu unakatwa vipande vipande.Baba ninampenda sana Happy na sijui nitafanya nini kama hataweza kupona.Sijui kama nitaweza kuishi bila yeye” Margreth akaendelea kulia
“Tunatakiwa tujikite katika maombi tumuombee.Mungu atasikia vilio vyetu na atamponya Happy.I know Happy is strong and she’s going to fight this .She’ll fight for us and for all those who love her.” Akasema mzee Kibaho huku naye macho yake yakiwa na machozi.Margreth akatoa kijikaratasi toka katika mkoba wake na kumpatia baba yake
“Kikaratasi hiki kimekutwa chumbani kwa Happy.Ni ujumbe aliouacha”akasema Margreth.Mzee Kibaho akakunjua kikaratasi kile na kuanza kukisoma
“wakati mnausoma waraka huu tayari nitakuwa nimekwisha ondokewa na uhai.Nimechukua maamuzi haya magumu kutokana na kuchoshwa na aina ya maisha ninayoishi sasa.Mambo mengi yamenitokea ndani ya kipindi kifupi sana na nimeyavumilia yote lakini kwa hili lililotokea leo limenifadhaisha mno .Kwa ufupi tu ni kwamba jana nilitekwa na watu nisiowafahamu wakanipeleka mahala na wakanilazimisha kuyafanya haya mliyoyaona katika magazeti,kwa ajili ya kuokoa uhai wa Patrick.Sitaki kuliongeala sana suala hili lakini naomba mnifikishie ujumbe kwa Patrick kwamba nimekufa na yeye akiwa ni mwanaume pekee ninayempenda na sintaacha kumpenda hata huko niendako.Nilikubali kufanya haya kwa ajili ya kumuokoa yeye asiuawe.Nawapenda wote na ninawaomba mnisamehe kwa jambo hili ambalo najua litawaumiza sana lakini sina namna nyingine ya kuniondoa katika aibu hii kubwa zaidi ya kujitoa uhai…Kwa herini nyote”
Mzee Kibaho alishindwa kuyazuia machozi kumtoka baada ya kumaliza kuusoma ujumbe ule wa Happy
“Ee Mungu najua unaweza na haushindwi na lolote,nakuomba umponye binti yangu Happy.Mimi na familia yangu bado tunamuhitaji sana.Ni wewe tu ambaye unaweza kumuokoa toka kifoni kwa sasa.Naomba usikilize maombi ya familia yangu na Happy aweze kupona” Mzee Kibaho akaomba kimya kimya huku akijifuta machozi kwa kitambaa
Taarifa za Happy kutaka kukatisha uhai wake kwa kunywa sumu zilianza kusambaa kwa kasi baina ya ndugu na marafiki wa karibu wa familia.Wengi walianza kufika pale hospitali ili kujua kilichokuwa kinaendelea.
“Nilijua tu lazima kuna sababu iliyomfanya Happy afanye kitendo kile.Sikuamini kabisa kama Happy ambaye nimemlea na kumkuza katika maadili anaweza akatenda kitendo kama hiki cha kujidhalilisha kwa hiari yake.Ni nani huyo ambaye amemfanyia mwanangu unyama na udhalilishaji huu mkubwa? Huu ni udhalilishaji uliovuka mipaka.Happy ameshindwa kuvumilia na ndiyo maana akaamua kuchukua maamuzi haya aliyoyachukua.” Akawaza mzee Kibaho
“Aliyefanya jambo hili na kumdhalilisha mwanangu lazima atakuwa na lengo la kulipiza kisasi.Ninaanza kuhisi kwamba pengine jambo hili linahusiana na kifo cha Veronika kwa sababu kwa nini jambo hili litokee sasa? Lazima uchunguzi ufanyike na wale wote waliohusika na udhalilishaji huu walipe uovu wao.Lazima watu hawa wapatikane kwa namna yoyote ile.Nitahakikisha watu hawa wanakamatwa na hata kwa kuwatumia wapelelezi binafsi nitafanya hivyo.Niko tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili kuwasaka watu hawa waliomfanyia mwanangu jambo hili.” Akawaza mzee Kibaho.

* * * *

Mlio wa simu ukamstua Loniki toka usingizini.Akanyoosha mkono na kuichukua .Mpigaji alikuwa ni Linah
“Hallo Linah” akasema Loniki akiwa bado na usingizi
“Lonny bado umelala?
“Simu yako ndiyo iliyonistua.Jana niliporudi nilikunywa sana mvinyo na ndiyo ulionipelekea kulala namna hii” akasema Loniki
“Lonny umepata habari?
“Habari gani tena wakati wewe ndiyo mtu wa kwanza kuongea naye leo?
“Dah ! mambo tayari yameanza”
“mambo gani tena Linah?
“Leo jiji zima limeamshwa na habari moja tu.Habari ya Happy”
“Tayari habari yake imeshatoka? Akauliza Loniki na kuinuka akakaa
“Chezea Khumalo wewe .! akasema Linah huku akicheka.
“Khumalo amekwishamaliza kila kitu na hivi nikwambiavyo gazeti la Mitikisiko limekwisha na halipatikani tena mtaani.Katika mitandao ya kijami,taarifa inayozunguka hivi sasa ni hii ya Happy.Kila mtandao zimetapakaa picha na video ya Happy”
“Dah ! nashukuru sana kama kazi imekamilika.Nadhani hivi sasa kama Happy atakuwa amezipata taarifa hizi atakuwa katika maumivu makali sana kama niliyonayo mimi .Baada ya kummaliza Happy sasa tutahamia kwa Patrick” akasema Loniki.
“Lazima nihakikishe wale wote walioudhulumu uhai wa mdogo wangu wanalipa.They all must pay.This is just the beginning…” akasema Loniki
“Lonny nina imani ushauri huu alioutoa Khumalo ni wa busara sana kwani endapo Happy ataziona picha zile ni wazi ataumia mno .Ni picha zenye kudhalilisha sana.”
“Kweli kabisa Linah.Ninaanza kukubaliana na Khumalo kwamba unaweza usimuue mtu moja kwa moja lakini ukampa mateso makali ya moyo na akateseka katika maisha yake yote.Kwa mfano Happy,kwa sasa maisha yake hayatakuwa sawa tena.Tayari ameingia katika kashfa nzito na hii itamtesa katika maisha yake yote yaliyobaki.Pamoja na hayo Linah kuna jambo nataka kukuuliza”
“Uliza Lonny”
“Khumalo ni mtu wa namna gani? Anajishughulisha na nini? Na kile chumba alichowekwa Happy kina kazi gani hadi kikafungwa kamera za kisasa namna ile?
Linah akavuta pumzi ndefu halafu akasema
“Kwa kuwa wewe ni rafiki yangu nitakueleza lakini naomba mtu mwingine yeyote asifahamu.Khumalo anajishughulisha na biashara nyingi haramu ikiwamo ya madawa ya kulevya na hata shughuli kama hii uliyompa na wakati mwingine hata ujambazi wa silaha huwa anahusika pia.Kwa sasa ameamua kujikita zaidi katika biashara ya madawa ya kulevya ambayo ndiyo inayomuingizia fedha nyingi sana.Ukiacha biashara hiyo ya dawa za kulevya,hukitumia kile chumba alichowekwa Happy kwa ajili ya kurekodi filamu za ngono ambazo huziuza katika nchi za ulaya na Amerika na kujipatia fedha nyingi.Huwatafuta mabinti wazuri wa kiafrika na kuwalipa pesa nyingi halafu huwarekodi wakifanya ngono.Hii ndiyo kazi ya chumba kile.Lonny tutaongea zaidi baadae kwa sasa kuna mahala ninawahi” akasema Linah
“Ok Linah.Nitakuja ofisini kwako baadae.Ahsante kwa taarifa” akasema Lonny na kukata simu
“Ouh gosh !!Sasa moyo wangu unaanza kupata amani.I cant imagine how painfull Happy is right now.Picha ndo kwanza linaanza.Nitahakikisha wale wote waliohusika kusababisha kifo cha Vero wanalipa.Japokuwa ni gharama kubwa lakini nitajitahidi kufanya kila niwezavyo hadi nihakikishe nimemilipia kisasi mdogo wangu.” Akawaza Loniki huku akitoka mle chumbani

* * * *

Akiwa bado katika mapumziko huku akiendelea na shughuli zake za usafi asubuhi hii,Sarah hakuwa na habari juu ya kilichokuwa kinaendelea hadi pale jirani yake alipoingia akiwa na gazeti mkononi na kumstua.
“Shoga yangu huyu si miss Tanzania aliyevunja uchumba wa Vero? Akasema shoga yake Sarah huku akimpa Sarah lile gazeti.Sarah akafuta maji mkononi na kulichukua gazeti lile
“Ouh My God ..!!! “ akasema Sarah kwa mshangao.Taarifa ile ilimstua mno.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka.
“Hakika malipo ni hapa hapa duniani.Amemzuia mwenzake asiolewe halafu kumbe huu ndio uchafu anaoufanya.Dah ! ameumbuka sana” akasema Yule shoga yake Sarah
“Hapana..!!..Hii si sahihi.Sidhani kama Happy anaweza akafanya kitendo kama hiki.Lazima hapa kuna namna iliyofanyika ili kumzalilisha .Lazima kuna mkono wa mtu hapa na kama ndiyo hivyo mtu huyo si mwingine atakuwa ni Loniki.Ni yeye peke mwenye chuki na Happy na aliweka dhamira ya kulipiza kisasi na ninadhani hii ni moja ya mipango yake.” Akawaza Sarah.
“Mbona uko kimya Sarah? Akauliza Yule shoga yake
“Nimestushwa sana na taarifa hii.” Akasema Sarah na kuingia ndani akachukua funguo za gari lake na kuondoka kwa kasi
“Nina hakika mkubwa Loniki anahusika kwa kiasi kikubwa na jambo hili la udhalilishaji.Lazima leo hii niufahamu ukweli.Kwa nini anataka kuendeleza uhasama usiokuwa na faida yoyote kwetu? Hapana siwezi kukubali jambo hili liendelee” akawaza Linah
“Ninahisi hata zile fedha ambazo mama aliniomba jana na kisha akampatia Lonny,alikuwa anazihitaji kwa ajili ya kutekeleza mipango yake hii miovu.Ninahisi hata mama naye atakuwa anahusika kwa namna fulani na jambo hili.Kuna kitu atakuwa anafahamu kuhusiana na mipango ya Lonny ya kulipiza kisasi.Kama ni kweli Lonny atakuwa amehusika katika kumdhalilisha Happy namna hii ,kamwe sintaweza kumsamehe .” akawaza Sarah
Mama yake sarah alikuwa amekaa nje ya nyumba yake na pembeni yake kulikuwa na meza ndogo iliyokuwa na chupa kubwa ya chai.Alistuka alipomuona Sarah akiingia pale ndani akiwa na uso uliojaa hasira
“Mama shikamoo” akasema Sarah
“Marahaba Sarah.Mbona hivyo? Kwema huko utokako?
“Kwema mama” akajibu Sarah halafu akalitoa gazeti lile la mitikisiko na kumpatia mama yake
“mama hebu niambie unafahamu chochote kuhusiana na jambo hili?
Mama yake akalichukua gazeti lile akalitazama na kustuka sana
“Ouh Mungu wangu..!!
“Hii ni kashfa kubwa sana”
“kweli mama ni kashfa kubwa mno.Nina hakika Loniki anahusika na jambo hili” akasema Sarah
“Loniki .!! mama yake akashangaa
“Ndiyo mama .”akasema Sarah
“Hapana Sarah.Loniki hawezi kuhusika na jambo kama hili”
“Mama humjui vizuri Loniki.Nina hakika lazima atakuwa anahusika na jambo hili.Aliapa kwamba atalipiza kisasi kwa Happy na wale wote waliohusika na kifo cha Vero.”
“Hapana Sarah.Sikubaliani nawe kwa hilo .Ni kweli Lonny ameumizwa sana na kifo cha vero lakini sidhani kama atakuwa anahusika kwa namna yoyote na jambo hili.Hii ni tabia ya Happy mwenyewe .Amemdhulumu mwanangu na haya ndiyo yanayomkuta sasa.”
“mama pesa ulizoniomba jana zilikuwa za kazi gani?
“Sarah naomba usitake kuyafahamu mambo yangu binafsi.Kama umeifuata pesa yako nitakurejeshea baadae kama nilivyokwambia” akasema mama yake kwa ukali
“mama sijaja hapa kufuata fedha.Nimekuja kutak…………….” Sarah akastuka baada ya Loniki kutokea ghafla
“Mbona kuna mabishano hapa? Akauliza Loniki huku akiangaliana na Sarah kwa macho makali
“Niambie uhusiki katika jambo hili ?” akasema Sarah huku akimpa Loniki gazeti ambaye alilichukua akalipitia kisha akaangua kicheko kikubwa.
“Haya ndiyo malipo ya udhalimu wake.Yeye na yule mshenzi wake Patrick walimdhulumu Vero uhai wake.Ona sasa alivyoumbuliwa na magazeti..” Akasema Loniki huku akicheka.Sarah akamtazama kwa hasira
“Mbona unanitazama hivyo Sarah? Hufurahi kwa kilichompata mtu aliyemuua mdogo wako?
“Kwa nini nifurahi? Happy si adui yangu na wala sintajenga uadui naye hata mara moja.Hata kama alihusika na kifo cha vero ,lazima niuheshimu utu wake.Kitendo cha kumdhalilisha namna hii hakivumiliki hata kidogo.”
“ Nilijua tu.Huna uchungu wowote kwa kifo cha Vero na ndiyo maana kila mara umekuwa upande wa Patrick na Happy.naomba nikufahamishe kwamba Happy anastahili kudhalilika namna hii.Anastahili kuumia kama tulivyoumia sisi kwa kufiwa na mdogo wetu.Huu ni mwanzo tu na bado ataumia sana.Mengi bado yatamkuta yeye na huyo shetani mwenzake Patrick”
Sarah alishindwa kumvumilia dada yake akamsogelea karibu
“Loniki wewe ni ndugu yangu wa damu lakini ninakuonya kwamba nitafanya uchunguzi wangu na endapo nitagundua kwamba unahusika kwa namna yoyote ile na jambo hili .I swear in heaven and earth I will never forgive you.”
“Utanifanya nini? Akauliza Loniki kwa ukali
“Utafahamu wakati utakapofika.”
“Go to hell sarah.Tena nakuomba uuchunge sana mdomo wako usije ukakuponza.Mimi si mtu wa kunyooshewa kidole kama unavyofanya.Kama ni mapambano niko tayari kupambana nawe na siogopi hata kama wewe ni ndugu yangu.Ninaweza nikakufanyia kitu kibaya sana na usiamini Sarah.”
Ilimlazimu mama yao kuingilia kati na kuwaamua wanae wale ambao walikuwa wanatoleana maneno makali.Sarah hakutaka tena kukaa pale nyumbani akapanda gari na kuondoka zake kwa hasira

* * * *

Savanna hakuwa mpenzi sana wa kusoma magazeti.Hii ilitokana na kuwa na kazi nyingi kiasi cha kukosa muda wa kupitia habari magazetini.Akiwa ofisini kwake akikamilisha baadhi ya kazi zake za kila siku asubuhi kabla ya kuelekea gereza la Uwangwa kuonana na Patrick,mara mmoja wa watumishi wa ofisi yake akaingia akiwa na gazeti mkononi.
“Savanna ,najua hupendi kusoma magazeti lakini naomba uchukue dakika chache upitie gazeti hili” akasema Edson mmoja wa mawakili wanaomtetea Patrick
“Edson toka lini umeniona nikipata muda wa kusoma magazeti? Ninataka kuelekea gerezani kuonanana na Patrick halafu nije niendelee na shughuli zangu nyingine” akasema Savanna
“Naomba usome Savanna.” Akasisitiza Edson na kuliweka gazeti lile mezani.Savanna akavutiwa na kichwa cha habari akalichukua ili alisome na ghafla akalitupa mezani
“Ouh My Gosh !!!... akasema Savanna kwa mstuko
“Bado siamini.Happy anaweza akafanya uchafu wa namna hii kweli? Happy huyu ninayemfahamu mimi? No..!! thats not true..!!!” akasema Savanna
“Ni kweli Savanna.Ukiacha picha hizi kuna video yake pia ambayo imesambaa mitandaoni.” Akasema Edson huku akiisogelea kompyuta ya Savanna akaifungua video ile ya Happy .Savanna akaitazama video ile na kujikuta mdomo wazi.
“Ouh gosh !! ..Ni vigumu kuamini.Happy kweli anaweza akafanya mambo ya aibu namna hii? Akasema Savanna na kujikuta akiishiwa nguvu miguuni,akakaa kitini.
“Usishangae Savanna.Siku hizi umezuka mtindo wa mabinti hasa hawa maarufu kujirekodi wakifanya ngono au kupiga picha za utupu kisha huzihifadhi kwa ajili ya kumbu kumbu zao wenyewe lakini ikitokea zikashindwa kuhifadhiwa vizuri na zikaingia katika mikono ya watu wabaya ,huziuza kwa waandishi wa habari kwa fedha nyingi ambao hutengeneza mamilioni ya fedha katika magazeti yao kwa kuichapisha habari hiyo” akasema Edson.Savanna akainama akafikiri halafu akachukua simu yake na kumpigia Margreth.
“Hallow “ akasema Margreth baada ya kupokea simu.Savanna akastushwa kidogo na sauti ya Margreth
“Margreth,sauti yako inaonyesha kama unalia.Unaumwa? akauliza Savanna .Margreth akashindwa kukizuia kilio chake akalia kwa nguvu
“Margreth nini kimetokea? Please tell me”
“Its…..it’s….” Margregth akashindwa kuongea akaangua kilio tena
‘Margreth nini kimetokea? Tafadhali naomba unieleze”
“Its Happy….!!
“Happy kafanya nini?
“Amekunywa sumu” Margreth akajibu halafu kikapita kimya cha sekunde kadhaa.Savanna akabaki mdomo wazi akashindwa aseme nini.Akameza fundo la mate na kusema
“Margreth tafadhali naomba uniambie ukweli”
“Ni kweli Savanna.Happy amekunywa sumu “
“So how’s She? Where ae you now?
“Niko hapa Brahmaputra hospital.She’s in critical condition fighting for her life “
“Ouh gosh ! ,nakuja sasa hivi” akasema Savanna na kukata simu kisha akachukua mkoba wake na kutoka kwa kasi hadi katika gari lake na kuondoka kuelekea hospitali.
“haya mambo mbona yanazidi kuchanganya? Jana nimepigiwa simu Happy haonekani lakini leo hii amekunywa sumu.Kitu gani kinaendelea hapa? Akawaza Savanna akiwa katika mwendo mkali kueleka hospitali
“Masikini Patrick,sipati picha atakuwa katika hali gani mara atakapozipata taarifa hizi.Sifahamu atachukua maamuzi gani lakini nafahamu lazima ataumia sana.” Akawaza Savanna
Baada ya kuwasili Brahmaputra hospital Savanna akakutana na familia ya Happy
“Shikamoo baba”
“Marahaba Savanna hujambo?
“Sijambo baba. Poleni sana” akasema Savanna halafu akamuomba mzee Kibaho wakaongee pembeni
“Nini kimetokea ? Happy anaendeleaje? Akauliza Savanna.Mzee Kibaho akakohoa kidogo halafu akasema
“Unakumbuka nilikupigia simu jana usiku nikitaka kufahamu kama unaweza ukafahamu lolote kuhusu mahala aliko Happy kwani hadi wakati ule ninakupigia hakuwa amerejea na hata simu yake haikuwa inapatikana kitu ambacho si kawaida yake.” Akasema mzee Kibaho
“Nakumbuka baba.Happy nilikutana naye jana asubuhi gerezani akiwa na Patrick.Nilipoingia nikiwa nimeongozana na familia ya Patrick yeye akaondoka na hatukupata muda wa kuongea.Nini kilitokea? Alikuwa wapi? Akauliza Savanna
“Mida ya kama saa nane hivi za usiku nilisikia muungurumo wa gari nje ya nyuma.Nilipotoka nje ya nyumba nilikuta gari la Happy na yeye akiwa ndani yake lakini akiwa hoi hajitambui.Hatukujua nini kilimpata kwa sababu alionekana ni kama mtu aliyelewa.Tulimuita dokta wa familia akaja mara moja na kumpatia huduma na alipopata nafuu akatuomba tumuache akapumzike.Hakutueleza alikuwa wapi na wala nini kilimpata.Asubuhi ya leo nilisikia mtu akilia sebuleni nikaenda kutazama nini kimetokea nikamkuta mke wangu akiwa amezirai.Wakati tukimpatia huduma ili azinduke akatokea Happy na kuliokota gazeti lililokuwa limeanguka chini.Ghafla akalitupa na kuelekea chumbani kwake.Nililitazama gazeti lile nikastuka sana.Nilimfuata Happy chumbani kwake lakini mlango ulikuwa umefungwa,ikanilazimu kuchukua ufunguo wa akiba nikaufungua mlango na kumkuta Happy akiwa hana fahamu na povu jingi likimtoka mdomoni.Alikunywa sumu ya kuulia panya.Nimemkimbiza hapa hospitali na toka nilipomfikisha hapa madaktari wanaendelea kumshughulikia.Shughuli zote hapa hospitali zimesimama kwa muda madaktari wote wanaendelea kumuhudumia Happy.Vile vile Happy aliacha ujumbe huu” mzee Kibaho akampatia Savanna ujumbe ule aliouacha Happy.Savanna akaupitia ujumbe ule na kisha akatoa kitambaa mfukoni na kuyafuta machozi
“Nilijua tu ,Happy hawezi kufanya jambo kama lile kwa hiari yake mwenyewe.Nilijua tu lazima jambo hili lina mkono wa mtu.Ni nani huyo ambaye anaweza kuwa amefanya unyama wa namna hii? Akasema Savanna
“Hakuna ajuaye ni nani muhusika wa jambo hili.Anayefahamu ni Happy pekee.Tuombe Mungu apone na atufahamishe ni nani hawa waliomfanyia kitendo hiki.Lazima wafikishwe katika mkono wa sheria“ akasema mzee Kibaho
“Ni kweli baba watu hawa waliohusika na udhalilishaji huu lazima walipe uovu wao.lazima wafikishwe katika vyombo vya sheria.” Akasema Savanna halafu kikapita kimya kifupi
“Savanna wewe ni wakili”
“Ndiyo baba”
“Naomba ushauri wako wa kisheria kuhusu kitendo hiki cha Happy.Hiki kitendo alichokifanya Happy cha kutaka kujiua ni kosa kisheria?
“Ni kweli baba,hiki ni kitendo cha kijinai.Kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu sura ya ishirini na mbili kifungu cha 217 kinachosema mtu yeyote anayejaribu kujiua ana hatia ya kosa.Iwapo suala hili litafuatiliwa na vyombo husika Happy anaweza kukabiliwa na adhabu
“Ouh My Gosh ..!!! what am I going to do ? akasema kwa masikitiko mzee Kibaho.Savanna akamtazama mzee Yule kisha akasema
“Baba kuna jambo ambalo tunatakiwa kulifanya kwa sasa”
“Jambo gani hilo savan?
“Kwanza nataka kufahamu kama suala hili limekwisha ripotiwa katika vyombo vya usalama.”
“Hapana Savanna.Suala hili halijaripotiwa sehemu yoyote ile na tunaofahamu ni sisi familia yake pamoja na ndugu wachache pamoja na majirani”
“Vizuri sana.Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kulifanya suala hili kuwa siri kubwa na kuhakikisha hakuna mwandishi wa habari anayezipata taarifa hizi.Ongea na uongozi wa hospitali hii ili hata kama ikitokea watahojiwa na vyombo vya habari au usalama wasiweke wazi kwamba Happy alijaribu kujiua kwa kunywa sumu.Baada ya hapo itabidi tufanye jambo la haraka sana kwa Happy”
“Jambo gani hilo? Akauliza mzee KIbaho
“Najua hautalipenda lakini hakuna jinsi ninabidi lifanyike tu”
“Niambie Savanna.Niko tayari kufanya lolote hivi sasa kwa ajili ya Happy” akasema mzee KIbaho.Savanna akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“I wapo Mungu atamsaidia akapona We have to take her away from here as quick as possible”
Mzee Kibaho akastuka kwa maneno yale ya Savanna
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 48
MTRUNZI.PATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Jambo gani hilo? Akauliza mzee KIbaho
“Najua hautalipenda lakini hakuna jinsi ninabidi lifanyike tu”
“Niambie Savanna.Niko tayari kufanya lolote hivi sasa kwa ajili ya Happy” akasema mzee KIbaho.Savanna akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“I wapo Mungu atamsaidia akapona We have to take her away from here as quick as possible”
Mzee Kibaho akastuka kwa maneno yale ya Savanna

ENDELEA……………..

“Baba najua umestuka sana kwa maneno haya lakini naomba uniamini haya nikwambiayo kwamba endapo Mungu atamjalia Happy uzima,tunatakiwa kumuondoa Happy hapa nchini haraka sana”
“Kwa nini unashauri hivyo ? Akauliza mzee Kibaho
“Jambo hili lililotokea si jambo dogo kama unavyoliona na hadi hivi sasa tayari limemuathiri Happy kwa kiasi kikubwa.Taswira yake katika jamii imeharibiwa na habari hii ya leo.Kwa maana hiyo basi anatakiwa kupata sehemu tulivu yenye uangalizi makini ili aweze kupatiwa msaada wa kisaikolojia na akili yake iweze kutulia.Kuendelea kumweka hapa ni kumuongezea maumivu na kutaendelea kuhatarisha usalama wake.Vile vile kumuondoa hapa kutasaidia kumuepushia mashtaka ya kijinai.Najua hili si suala jepesi lakini inatubidi tushirikiane sote kwa faida ya Happy” akasema Savanna.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu .Alionekana kama amechanganyikiwa
“I don’t know what I’m going to do” akaongea peke yake.Baada ya dakika mbili za tafakari akamgeukia Savanna
“Savanna mawazo yako naona yana msingi sana.Nina mdogo wangu anaishi Mtwara.Nadhani itakuwa vyema kama nitampeleka kule akakae kwa muda”
“Hapana baba.Mtwara bado ni Tanzania.Happy anatakiwa aende mahala ambako hakuna mtu anayemfahamu mahala ambako atapata msaada wa kisaikolojia na kumsaidia kurejea katika hali yake ya kawaida.Hapa nchini Happy ana jina kubwa na anafahamika kila kona”
“Savanna suala hili linahitaji muda wa kutosha kulifanyia maandalizi.Inabidi nikae na familia yangu baada ya kujua maendeleo ya Happy na kwa pamoja tujadili suala hili ndipo tufikie maamuzi “ akasema mzee Kibaho huku akionekana ni mwenye mawazo mengi sana
“Mzee wangu nakubaliana na wazo la kukaa na kufanya maamuzi kama familia .Pamoja na hilo naomba na mimi nitoe mchango wangu.Iwapo mwenyezi Mungu atamjalia Happy uzima na iwapo mtakubaliana na mawazo yangu basi ninapendekeza Happy asafirishwe kwenda Kigali Rwanda.Mimi nitagharamia gharama zote za safari.Nitakodisha ndege binafsi hadi Kigali.Pale Kigali nina rafiki yangu aitwaye Christine umuhiza ambaye ndiye atakayemuhudumia Happy kwa kipindi chote atakachokuwa pale.Vile vile ninafahamiana na mmiliki wa hoteli moja iitwayo Reonald Hotel.Ni hoteli mpya na kubwa pale Kigali yenye hadhi ya nyota tano.Nitafanya mpango ili Happy aweze kukaa hotelini hapo kwa muda wote atakaouhitaji akiwa katika chumba chenye hadhi ya rais.Christine atamtafutia daktari ambaye atamsaidia kumtibu na vile vile tutamtafutia daktari wa masuala ya kisaikolojia “ akasema Savanna.Mzee Kibaho aliyekuwa anamsikiliza kwa makini akakohoa kidogo na kusema
“Savanna mimi binafsi nimeumizwa sana na jambo hili na kwa mantiki hiyo basi niko tayari kufanya jambo lolote lile ambalo litakuwa na msaada kwa Happy.Sipingani hata kidogo na wazo lako la kumpeleka Happy nje ya nchi.Ninachotaka kufahamu ni iwapo Happy ataondoka hapa nchini kwa ajili ya kumsaidia kwanza kumuepusha na aibu hii na pili kumuepusha na mkono wa sheria kwa kosa la kujaribu kujiua, nini itakuwa hatima ya watu waliomtenda hivi? Sitakuwa na amani hadi nihakikishe kwamba watu waliomfanyia mwanangu kitendo hiki cha kinyama wamekamatwa ,wamefikishwa katika mkono wa sheria na wameadhibiwa kutokana na kitendo walichokifanya.Lakini ninajiuliza maswali mengi hilo litawezekana vipi wakati Happy akiwa nje ya nchi? Nataka jina la mwanangu lisafishwe .Nataka umma wa watanzania wafahamu nini kilitokea na kwamba mwanangu hawezi kufanya kitendo kama kile kwa ridhaa yake.” Akasema mzee Kibaho
“Baba hayo yote unayoyasema ni ya msingi sana lakini tukumbuke kwamba ni Happy pekee ambaye anawafahamu watu hao na ambaye anaweza akatusaidia kuwatambua watu hao na anaweza akafanya hivyo pale ambapo akili yake itakuwa imetulia .Mimi binafsi nakuahidi ushirikiano wangu wa dhati katika suala hili na mara tu watakapogundulika watu hawa nakuahidi kwamba kesi hiyo nitaisimamia mimi mwenyewe na kuhakikisha kwamba wanapata adhabu kali sana”
Kabla mzee Kibaho hajasema chochote,akatokea Margreth na kumtaarifu baba yake kwamba anahitajika na daktari.Kwa haraka wote watatu wakaongozana kuelekea katika ofisi ya daktari

“karibuni sana” akasema daktari mkuu wa hospitali hii ambaye ana asili ya India lakini anakifahamu vizuri sana Kiswahili
“Poleni sana kwa matatizo” akasema daktari.Wote watatu nyoyo zao zilikuwa zinawadunda wakisubiri taarifa ya daktari
“Jamani nimewaiteni hapa ili kuwapeni taarifa kuhusiana na maendeleo ya mgonjwa wenu.Kwa ujumla ni kwamba Happy alikuwa amekunywa dawa ya kuulia wadudu ambayo ni sumu katika mwili wa binadamu.Ninakushukuru sana mzee wangu kwa jitihada zako za kumfikisha mapema hapa hospitaloi kabla sumu ile haijasababisha madhara makubwa mwilini.Tulimpokea Happy akiwa katika hali mbaya na tumefanya kila jitihada ili kumuondoa katika hali ya hatari ya kupoteza maisha.Tunapaswa kumshukuru sana Mungu kwani tumefanikiwa katika hilo.Kwetu sisi tunaona ni kama muujiza kutokana na hali aliyokuwa nayo Happy.Tumefanikiwa kuiondoa sumu iliyoko mwilini mwake kwa kutumia mtambo wetu maalum ambao ni mpya kabisa wa kuondoa sumu ya aina yoyote mwilini.Kwa sasa ninaweza kutamka kwamba Happy hayuko tena katika ile hatari ya kupoteza maisha na endapo litatokea jambo kama hilo basi itakuwa ni kwa mapenzi ya Mungu lakini napenda kuwahakikishia kwamba tumemuondoa katika hatari hiyo.” Akasema daktari na wote watatu wakashusha pumzi .Mzee Kibaho akajifuta jasho lililokuwa linamtiririka kwa wingi
“Zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuipitisha damu yake katika mtambo maalum wa kuchuja sumu ili kuweza kujiridhisha zaidi kwamba hakuna kiasi chochote cha sumu kitakachobaki mwilini mwake.Kwa hiyo nawasihi ndugu zangu,ondoeni wasi wasi mliokuwa nao.Happy yuko salama na anaendelea vizuri.Zoezi hili litakapomalizika tutamuondoa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kumpeleka katika sehemu ya uangalizi maalum ili kuangalia maendeleo yake.”
“Ouh Thanx God” akasema mzee Kibaho huku akiinua mikono yake juu kumshukuru Mungu
“Daktari zoezi hilo la uchujaji wa sumu litachukua muda gani? Akauliza Savanna
“Ni muda wa masaa manne”
“Mzee wangu nini hasa kilichopeleka binti mdogo kama huyu kutaka kukatisha uhai wake? Nini kimemsibu ili tuone namna ya kumpatia msaada wa kisaikolojia na asiweze kurudia tena kufanya kitendo cha hatari kama hiki? akauliza daktari.Mzee Kibaho akakohoa kidogo na kusema
“Happy ni binti yangu wa kwanza.Hivi karibuni alifanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania.Baada ya kulinyakua taji hilo ndipo matatizo yalipoanza.Yote haya yamesababishwa na mgogoro wa kimapenzi uliopekeka msichana aliyekuwa akizozana naye kufariki dunia.Leo asubuhi katika gazeti moja la udaku kumechanpishwa picha za Happy za faragha.Ni picha zenye kuumiza sana na zote hizi ni njama za wabaya wake za kutaka kumchafua.Jambo hilo ndilo lililopelekea aamue kujaribu kukatisha uhai wake kwa kunywa sumu.” Akasema mzee Kibaho
“Poleni sana.Hii inaonyesha ni jinsi gani dunia ilivyobadilika hivi sasa.watu wamekosa huruma na wako tayari kufanya jambo lolote lile kwa manufaa yao bila kupima athari zinazoweza kujitokeza.Poleni sana ,lakini kitu ninachoweza kuwaambia ni kwamba Happy anahitaji msaada wa kisaikolojia.Hapa tunao madaktari wazuri sana wa masuala haya ya akili.Tunacho kitengo hicho hapa cha kuasadia watu wenye matatizo kama ya Happy.Ninawashauri kwamba baadaya hali yake kuwa nzuri basi tuendelee kumpatia msaada wa kisaikolojia hapa hapa hospitalini kwetu” akasema daktari
“Nakubaliana nawe daktari kwani inaonyesha wazi kwamba binti yangu ameathirika kisaikolojia na anahitaji msaada .Lakini kuna jambo ninataka kukuomba.Kwa mujibu wa sheria ,kitendo hiki alichokifanya Happy ni kosa la kijinai kwa hiyo kuna uwezekano endapo vyombo vya kisheria vikazipata taarifa hizi vikamfungulia mashitaka,kwa hiyo tunakuomba daktari ,jambo hili libaki kuwa siri na asifahamu mtu mwingine yeyote yule awe ni mwandishi wa habari au afisa wa polisi.Unaweza ukaandika ugonjwa mwingine wowote lakini si sumu.Jambo la pili ambalo tumekusudia kulifanya kwa haraka ni kumuhamishi Happy nje ya nchi haraka iwezekanavyo.mahala ambako hakuna mtu yeyote anayemfahamu.Nadhani hii itakuwa ni njia nzuri sana ya kumsaidia kumuondoa katika mazingira haya na wakati huo huo tukiendelea kumpatia msaada wa kisaikolojia.” Akasema mzee Kibaho
“Kwanza kabisa kuhusiana na kutoa taarifa kuwa vyombo vya habari na vile vya usalama,msiwe na hofu.Nitawasaidia katika hilo.Pili kuhusiana na suala la kumpeleka Happy nje ya nchi ni suala zuri sana lakini nina wasi wasi kidogo.Happy anahitaji bado kuwa katika uangalizi wa madaktari.Kama ni kumuondoa hapa nchini basi itawabidi msubiri kidogo hadi hapo hali yake itakapoboreka kabisa.”
“Inaweza kuchukua muda gani daktari? Akauliza Savanna
“Inaweza kuchukua zaidi ya wiki moja”
“Daktari tunahitaji kumuondoa Happy nchini leo hii.”
“Kwa leo haitawezekana kumsafirisha Happy” akasema Daktari
“Daktari naomba ufanye kila linalowezekana ili tuweze kumuondoa Happy hapa nchini siku ya leo” akaendelea kusisitiza Savanna
Daktari akafikiri kidogo na kusema
“Kama mkihitaji hivyo basi ni lazima pawepo makubaliano maalum”
“makubaliano gani hayo? Akauliza Savanna
“Baada ya zoezi la kuchuja sumu kukamilika mgonjwa anatakiwa apumzike kabla ya zoezi lingine lolote kufanyika.Endapo mtahitaji kumsafirisha Happy kwa siku ya leo,itawalazimu kumsafirisha na mmoja wa madaktari wetu kitu ambacho kitawaongezea gharama zaidi kwa hiyo nawashauri mngesubiri hadi hapo Happy atakapokuwa amepata nafuu ndipo mumsafirishe”
“Daktari hilo ulilolisema si tatizo kwetu hata kidogo kwani tunatumia ndege ya kukodi.Tunaelekea jijini Kigali Rwanda.Usijali kuhusu gharama.Tutakulipa pesa zote zitakazotakiwa ikiwa ni pamoja na kumuhudumia daktari huyo hadi hapo Happy atakapopata nafuu.” Akasema Savanna
“Kama mko tayari kwa hilo mimi sina shida yoyote.Kwa sasa naombeni mnipe nafasi nikakutane na jopo la madkatari wangu ili kwa pamoja tuweze kushauriana namna bora ya kuweza kulifanikisha jambo hili” akasema daktari.
“Usijali daktari.Sisi pia ngoja tukajiandae kwa safari.Naomba hesabu ya gharama zote unitumie kwa kupitia namba hizi hapa” akasema Savanna huku akimpatia daktari kadi yake yenye namba za simu halafu wakatoka mle ofisini.
“Baba mpango huu wa kumpeleka Happy Kigali umetoka wapi? Mbona hakuna aliyekuwa anafahamu kama kuna mpango kama huu? Akauliza Margreth baada ya kutoka ofisini kwa daktari
“Margreth samahani kwa kulisikia jambo hili kabla ya kutaarifiwa.Ni kwamba Savanna alikuja na wazo hili la kutaka kumuhamisha Happy na kumpeleka nje ya nchi ili kumuweka mbali na mazingira haya.Endapo ataendelea kukaa hapa wakati tayari jina lake limekwisha chafuka ataendelea kuumia zaidi.Ni bora ikiwa atakwenda kukaa mbali na hapa,mhala ambako hafahamiki kabisa.Hii itamsaidia sana kumsahaulisha kilichotokea”
“Ni mpango mzuri baba lakini maandalizi yanakwendaje manake nimemsikia Savanna akisema kamba Happy atapelekwa Kigali.Imekuwa ghafla sana na nina wasi wasi kama kuna maandalizi yoyote yaliyofanyika”
“Margreth,usihofu chochote kuhusiana na jambo hilo.Pale Kigali kuna hoteli moja kubwa ya nyota tano ambayo mmiliki wake tunafahamiana vyema na ndipo Happy atakapofikia na kukaa yeye na watu atakaoambatana nao hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri.Kuhusu usafiri nitagharamia mimi ,nitakodisha ndege hadi Kigali “

* * * *

Saa tano na dakika ishirini za usiku familia ya Happy ikaruhusiwa kuingia katika chumba alichokuwa amelazwa Happy.Tayari alikwisha amka toka saa mbili za usiku lakini madaktari hawakuruhusu aonane na mtu yeyote hadi hapo atakapokuwa amerejewa na fahamu zake kamili
Mara tu alipoiona familia yake ikiingia mle chumbani wakiongozwa na baba yake mzee Kibaho Happy alishindwa kujizuia akaanza kulia.
“Ouh Happy mwanangu” akasema mama yake huku akiinama na kumkumbatia wote wawili wakilia.
“Mungu ahsante kwa kumponya mwanangu” akasema mama yake Happy. Happy akasalimiana na baba yake mzee Kibaho na halafu mdogo wake Margreth na ghafla akastuka baada ya kugonganisha macho na Savanna
“Pole sana Happy” akasema Savanna.Happy akashindwa ajibu nini,donge kubwa likamkaba kooni.Savanna alilitambua hilo akatoka nje ya kile chumba.
“what is she doing here? Baba kwa nini umemleta Savanna hapa? Akauliza Happy
“Usijali Happy,Savanna tuko naye kutwa nzima ya leo tukishughulikia suala hili.Amekuwa ni msaada mkubwa kwetu katika wakati huu mgumu tulionao.Ametupa ushirikiano mkubwa sana.” Akasema mzee Kibaho
“Dady I don’t want to see her here.That woman is a devil.She’s a monster” akasema Happy kwa hasira juku akiendelea kulia.
“Its ok Happy It’s ok.Nyamaza usiendelee kulia mwanangu” akasema mzee Kibaho huku akimfuta Happy machozi
“Dady why you saved me? Akauliza Happy
“Happy naomba usahau kilichotokea.Kitu pekee kwa sasa ni kumshukuru Mungu kwa kukuponya .Sisi kama familia ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba unakuwa salama.Tunakupenda sana na hakuna mtu yeyote anayeweza akakubali upoteze maisha” akasema mzee Kibaho halafu.Happy akainua mkono akafuta machozi.
“Baba ungeniacha nife.Nimechoka na maisha haya.I’m real tired with this kind of life.Nili……………….” kabla hajaendelea baba yake akamuwekea kidole mdomoni
“Shhhhhhhhh..!!!!..Happy usiseme hivyo.Sahau kilichotokea .Hii ni mitihani ya maisha na ambayo hatuna budi kuishinda.Happy tunakupenda sana zaidi ya unavyoweza kufikiri”
“Najua kwamba mnanipenda sana lakini kwa aibu hii niliyowapa najiona sistahili hata kuitwa mwanenu.Nime………………” Happy akashindwa kuendelea akaangua kilio
“Happy usilie mwanangu.Tunakupenda sana na siku zote tutakuwa pamoja nawe katika kila jambo.Tuko pamoja katika suala hili na ndiyo maana tumeamua kukuhamisha hapa nchini usiku huu na kukupeleka sehemu ambayo utaweza kupumzika na kusahau kilichotokea,sehemu ambayo hakuna mtu yeyote anayekufahamu”
“Mnataka kunipeleka wapi baba?
“Tumeamua kwanza uende ukapumzike Kigali Rwanda wakati tukiangalia sehemu nyingine ambayo itakufaa zaidi.Tayari kila kitu kimekwisha andaliwa kwa msaada mkubwa wa Savanna ambaye ndiye aliyefanikisha mipango yote ya safari ikiwa ni pamoja na kuandaa hoteli ambayo utafikia kule Kigali na hata kuwalipa madkatari wote watakaokuwa wakikuhudumia katika kipindi hiki chote utakachokuwa kIgali.Tumefikia uamuzi huu wa kukuondoa hapa nchini ili kukusaida usiweze kuumia zaidi kutokana na maneno ya watu na vyombo vya habari.Iwapo utaendelea kukaa hapa utakuwa ukiumia zaidi kila siku” akasema mzee Kibaho
“Please dady take me out of here right now” akasema Happy huku akitoa machozi.
“Usijali Happy.Kila kitu kimekwisha andaliwa na tuchosubiri ni taratibu za hapa hospitali .Lakini kabla hatujaondoka hapa kuna jambo ninataka kukuuliza” akasema mzee Kibaho halafu akamtazama mwanae na kusema
“Unawafahamu au kuwa na hisia ni nani aliyekufanyia hivi?
Happy akafumba macho kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“Its not important anymore dady.Just take me out of here”
“Happy waliofanya unyama huu wanatakiwa wafikishwe katika vyombo vya sheria.Huu ni ukatili mkubwa sana ambao hauvumiliki.Tafadhali tusaidie tuweze kuwafahamu watu hao.Mimi na Savanna tutashirikiana na kuhakikisha kwamba wale wote waliotenda hivi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria”
“Dady not now.Please take out of here” Happy akaendelea kuushikilia msimamo wake.Mzee Kibaho akatoka ndani ya kile chumba akakutana na Savanna.
“Savanna naomba usimjali Happy.Twende tukashughulikie masuala ya hapa hospitali ili tuweze kuruhusiwa kuondoka.” Akasema mzee Kibaho
“Kitu gani kinaendelea baina yako na Happy? Akauliza mzee Kibaho wakati wakishuka ngazi
“Its something stupid.Tulipishana maneno.Kuna mtu ambaye alimpelekea Happy maneno ambayo yalimfanya akasirike na kuja juu na mimi nikashindwa kudhibiti hasira zangu na tukajikuta tukitamkiana maneno makali.” Akasema Savanna
“Ninaweza kufahamu ni jambo gani hilo lililosababisha wewe na Happy mtupiane maneno? Akauliza mzee Kibaho
“Si jambo la msingi sana na sioni sababu ya kukwambia.Ni mambo ya wanawake tu na tutayamaliza” akasema savanna
Hatimaye ruhusa ya Happy kuondoka ikatolewa na akapatiwa daktari mmoja ambaye angeongozana naye kuelekea Kigali Rwanda ambaye angeendelea kumuhudumia hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri.Wote waliingia katika gari moja na safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza.Walikuwa makini sana kuhakikisha kwamba hawafuatiliwi na mwandishi yeyote wa habari kwani suala hili lilikuwa ni siri kubwa ya familia.Safari ilikuwa ya kimya kimya na hakuna aliyekuwa anaongea ndani ya gari.Waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ,mizigo ya Happy ikashushwa garini.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana hasa kwa mama yake Happy.Alimkumbatia mwanae huku wote machozi yakiwatoka.
“Mom I’m going to miss you” akasema Happy
“Happy sina cha kusema zaidi ya kukuombea kwa Mungu akutangulie huko uendako.Uwe salama kila siku “ akasema mama yake Happy huku machozi yakimtoka
“Nitakuwa salama mama” akasema Happy halafu akamuacha mama yake na kumfuata Margreth.
“Be safe there and get well soon” akasema Margreth
Happy hakusema kitu ,macho yake yalikuwa yamefunikwa na machozi
“Its time to go Happy” akasema mzee Kibaho kwa sauti ndogo
“Baba Happy” akaita mama yake Happy.Mzee Kibaho akageuka
“Tafadhali hakikisha Happy anakuwa salama”
Mzee Kibaho hakujibu kitu zaidi ya kutingisha kichwa ishara ya kukubaliana na kile alichokisema mke wake halafu akamshika mkono Happy na kumuomgoza kuelekea ndani ya uwanja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za hapo uwanjani kabla ya kuruhusiwa kuondoka

TUKUTANE SEHEMU IJAYO.....
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 49
MTUNZI : PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Its time to go Happy” akasema mzee Kibaho kwa sauti ndogo
“Baba Happy” akaita mama yake Happy.Mzee Kibaho akageuka
“Tafadhali hakikisha Happy anakuwa salama”
Mzee Kibaho hakujibu kitu zaidi ya kutingisha kichwa ishara ya kukubaliana na kile alichokisema mke wake halafu akamshika mkono Happy na kumuomgoza kuelekea ndani ya uwanja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za hapo uwanjani kabla ya kuruhusiwa kuondoka

ENDELEA…………………..

Waliwaisli salama katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Kigali.Christine Umuhiza alikuwepo uwanjani kuwapokea wageni wake na kisha wakaelekea moja kwa moja Reonaldo hotel,moja ya hoteli mpya na kubwa jijini Kigali
Tayari kila kitu kilikwisha andaliwa na Happy akapewa chumba chenye hadhi ya rais yaani presidential suit kama alivyokuwa ameahidi Savanna.Mzee Kibaho ambaye ambaye naye alikuwa ameambatana na mwanae naye alipewa chumba kizuri sana kwa ajili ya kupumzika kwa siku zote atakazokaa hapo Kigali,daktari aliyeambatana nao pia alipewa chumba cha hadhi ya juu kabisa.
“Happy,nilipendekeza ufikie katika hoteli hii kwa sababu ni nzuri na huduma zake ni nzuri na za kimataifa.Jitahidi kupumzika kwa kadiri utakavyoweza na kwa muda wowote utakaohitaji.Mmiliki wa hoteli hii ni rafiki yangu sana na anafahamu uwepo wako hapa na gharama zote ni juu yangu .Endapo kutakuwa na tatizo lolote wasiliana nami moja kwa moja.Christine atakusaidia kumpata daktari bingwa wa magonjwa ya akili ambaye atakuwa akifika hapa kila siku na atakusaidia kisaikolojia ili uweze kurejea katika hali yako ya kawaida.”Akasema Savanna halafu akamtazama Happy aliyekuwa amejilaza kitandani.
“Happy najua tulipisha kauli na kutoleana maneno makali.Tafadhali naomba tusahau yale yote yaliyopita na tuangalie mambo ya mbele.Binafsi nimeumizwa mno na jambo hili kama walivyoumia wale wote wanaokupenda na ndiyo maana nimejitolea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu ili kuhakikisha unarudi katika hali yako ya kawaida na kwa pamoja tuhakikishe wale wote waliohusika na kitendo hiki wanatafutwa kwa gharama zozote na kufikishwa mbele ya sheria” akasema Savanna.Bado Happy alikuwa anamuangalia kwa macho makali yaliyojaa machozi
“Happy mimi naenda kupumzika nyumbani kwa Christine.Nitakuja kukuaga asubuhi kabla ya kurejea Dar es salaam” akasema Savanna baada ya kugundua kwamba Happy hakuwa tayari kuongea naye kwa usiku ule .Akaufungua mlango na kutoka mle chumbani

* * * *

Kumekucha Kigali,kijua tayari kimechomoza na shughuli mbali mbali za uzalishaji mali zilikuwa zinaendelea kama ilivyo ada.Saa mbili za asubuhi Chistine na Savanna wakawasili hotelini.Wa kwanza kuonana naye alikuwa ni mzee Kibaho ambaye alikwisha amka na kufanya mazoezi ya viungo katika ukumbi mkubwa wa mazoezi uliopo katika hoteli ile.
“Happy ameamkaje? Akauliza Savanna
“Nimeongea naye kwa simu asubuhi ya leo ,amesema anaendelea vizuri ,lakini kwa mujibu wa daktari ni kwamba itamchukua siku kadhaa kurejea katika hali yake ya kawaida” akajibu mzee Kibaho
“usijali baba.Nina hakika baada ya muda hali yake itakuwa nzuri na maisha yataendelea kama kawaida.” Akasema Savanna halafu akaenda kuonana na daktari aliyemuhakikishia kwamba hali ya Happy ilikuwa inaendelea vizuri.Baada ya hapo akaelekea katika chumba cha Happy akabonyeza kengele ya mlangoni.Dakika kama mbili zilipita bila majibu yoyote .Akaanza kuingiwa na wasi wasi.Akabonyeza tena kengele na baada ya kama dakika mbili tena akasikia kitasa cha mlango kikinyongwa na mlango ukafunguliwa.Akagonganisha macho na Happy ambaye bado yalikuwa yamemvimba kutokana na kulia sana.Happy hakusema kitu akarejea kitandani kwake akaketi.Savanna naye akaingia mle chumbai na kusimama pembeni ya meza kubwa ya chakula.
“Happy unaendeleaje? Akauliza Savanna lakini Happy hakumjibu kitu.
“Happy nafahamu hukupenda kuniona hapa.Nafahamu ndani ya moyo wako mimi ni mmoja wa wale watu unaowachukia sana hivi sasa.Unapaswa kunichukia hasa baada ya maneno yale makali tuliyotoleana.Sote tulitoleana maneno makali kutokana na hasira tulizokuwa nazo.Sina mengi sana ya kusema lakini naomba utambue kwamba nimeguswa sana na jambo hili na kama rafiki na mwanamke mwenzako,niko pamoja nawe katika wakati huu mgumu” akasema Savanna halafu akanyamza kidogo akamtazama Happy na kuendelea
“Happy nimekuja kukuaga.Muda mfupi ujao ninarejea Dare s salaam.Ningependa kuwa nawe hapa kwa muda mrefu zaidi lakini bado ninakabiliwa na majukumu mengine mengi.Mzee Kibaho na daktari ,wataendelea kufuatilia hali yako kwa karibu na watatufahamisha kila hatua na endapo kutakuwa na tatizo lolote basi tutasaidiana namna ya kulitatua.Kitu pekee ambacho nitaka kukushauri ni kwamba ,japokuwa ni vigumu sana lakini naomba ujaribu kusahau kilichotokea na uruhusu maisha yaendelee.Happy nakufahamu wewe ni mwanamke jasiri sana naomba tafadhali usikubali kushindwa katika hili.Usimpe nafasi mtu,au kikundi cha watu kukufanya ukate tamaa na ushindwe kutimiza ndoto zako.” Savanna akanyamaza na kumtazama Happy ambaye macho yake yalikuwa yemejaa machozi
“Hapa hotelini utaishi kwa muda wowote utakaoutaka,utapatiwa kitu chochote utakachohitaji.Endapo kutakuwa na tatizo lolote naomba unipigie simu yangu moja kwa moja.Mwisho naomba ufahamu kwamba kuna maelfu ya watu wanaokupenda na mashabiki wako wanaokusubiri upone na siku moja urejee tena Tanzania.Get well soon Happy “ akasema Savanna huku naye akilengwa na machozi halafu akageuka na kuanza kupiga hatua kuondoka
“Savanna subiri kidogo” akasema Happy.Savanna ambaye alikuwa ameukaribia mlango akasimama na kugeuka.Happy akainuka pale kitandani akamfuata
“Savanna naomba unisamehe kwa yale yote niliyokutenda.Ni kweli siku ile tulipopishana maneno nilikuwa na hasira sana lakini naomba unisamehe.Kabla hujaondoka,naomba toka ndani ya moyo wangu niseme kwamba ahsante sana kwa yote.Wema huu ulionitendea ni mkubwa na sina hakika kama nitaweza kuurejesha.Pamoja na shukrani zangu kuna jambo moja nataka kukuweka wazi”akasema Happy akamtazama Savanna kwa makini halafu akasema
“Savanna sintarejea tena Tanzania.I’ve left Tanzania for good.Its my country but I hate Tanzania so much.Kwa sababu hiyo basi naomba nimkabidhi Patrick katika mikono yako.Ninamuacha mikononi mwako kwa sababu ninaamini unampenda na utahakikisha anakuwa mwenye furaha siku zote katika maisha yake.Please take good care of him .He’s all yours now.Kokote nitakakokuwa nitajua kwamba Patrick ana furaha kwa sababu yuko katika mikono salama.” Akasema Happy huku machozi yakimtoka
“Tafadhali Happy usiseme maneno hayo” akasema Savanna kwa mshangao
“Savanna naomba ufanye kama nilivyokuomba.Huu ni uamuzi wangu na nimeamua kuchukua maamuzi haya magumu kutokana na hali halisi ilivyo na ukweli ulio wazi kwamba mimi na Patrick hatutaweza kuwa pamoja japokuwa tunapendana kwa mioyo yetu yote.Pamoja na hayo naomba unihakikishie jambo moja.”
“Jambo gani Happy?
“Naomba unihakikishie kwamba Patrick atashinda kesi na atakuwa huru na kwamba hautamwambia mahala niliko.Can you promise me that?
Savanna akamwangalia Happy usoni na kusema
“Patrick will be free.I give you my word” akasema Savanna
“Thank you Savanna.Thank you so much.You can go now” akasema Happy huku uso wake ukiwa umeloa machozi
“Thank you so much Happy.” Akasema Savanna huku naye machozi yakimtoka na kumkumbatia Happy halafu akatoka mle chumbani

* * * *

“The war is over now.Patrick is mine and he’s mine alone.” Akawaza Savanna akiwa katika ndege akirejea Dar es salaam.Uso wake ulikuwa umepambwa kwa tabasamu pana
“Sijafurahia kilichomtokea Happy japokuwa sote tulikuwa katika vita ya kumgombania Patrick lakini kufa kufaana.Namuonea huruma sana Happy japokuwa kwa upande wa pili nimejawa na furaha kwa yeye kuamua kuachana na Patrick.” Akawaza Savanna
“Lakini ni nani hawa waliomfanya udhalilishaji huu mkubwa? Ninaanza kujenga picha kwamba waliofanya kitendo hiki walikuwa na lengo moja tu la kumdhalilisha Happy.Nashawishika kuamini kwamba yeyote aliyefanya jambo kama hili alikuwa na lengo la kulipiza kisasi.Ninalazimika kuamini pia kwamba lazima tukio hili litakua na uhusiano fulani na kifo cha vero.Nasikitika kwamba hatutaweza kuwapata watu hawa kwa sababu Happy hayupo tena Tanzania na hana mpango wa kurejea tena wala wa kuwatafuta watu hawa. ”
Savanna alikuwa na furaha sana kwani aliamini ile ndoto yake ya kuwa na Patrick sasa inakwenda kutimia

*****************

Saa tatu za asubuhi gari moja dogo jeupe likaingia katika gereza la Uwangwa.Kijana mmoja mfupi mnene aliyevaa suti ya kijivu iliyomkaa vyema akashuka toka ndani ya gari lile na kuelekea sehemu ya mapokezi ambako alijitambulisha kama mgeni wa Apolinary.Moja kwa moja akapelekwa katika ofisi ya Apolinary mmoja kati ya maafisa wa gereza hili
“karibu sana kijana” akasema Apolinary ,mzee mmoja mnene mweupe
“Ahsante sana mzee.” Akajibu Yule kijana huku akiketi kitini na bila kuchelewa akaitoa bahasha ya khaki toka mfukoni na kupatia mzee Apolinary ambaye aliifungua na kukutana na bunda kubwa la noti mpya kabisa nyekundu
“Sina haja ya kuhesabu,nadhani ni millioni tatu kamili.”
“Ndiyo mzee,ni tatu kamili”
“namuamini sana Khumalo.Ahadi zake huwa za kweli.” Akasema Apolinary huku akizifungia fedha zile katika kabati lake na kuchukua fimbo yake akamuomba Yule kijana amfuate.Apolinary alienda hadi katika ofisi moja inayohusiana na masuala ya mahabusu akaongea na askari mmoja aliyekuwamo mle ofisini kisha akainua simu akapiga na muda si mrefu wakatokea askari wawili ambao akaongea nao jambo fulani halafu wakaongozana na mzee Apolinary pamoja na yule kijana wake.Waliingia katika chumba kimoja kidogo kilichokuwa na viti viwili.
“Nickson, Patrick ataletwa hapa muda si mrefu na utaongea naye” akasema Apolinary halafu akawatuma wale askari wawili wakamlete Patrick.Baada ya kama dakika saba hivi Patrick akaletwa
“Patrick kuna mtu amekuja kukutembelea.” Akasema Apolinary halafu akawafanyia ishara askari wale watoke mle chumbani na kuwaacha Patrick na yule kijana Nickson
“Nickson una dakika kumi tu za kuongea na Patrick” akasema Apolinary naye akatoka nje
“Watatumia dakika kumi tu halafu mumrudishe Patrick mahabusu” Apolinary aliwaambia wale askari waliokuwa wamesimama nje ya kile chumba
“Patrick pole sana.Nadhani ni mara ya kwanza mimi na wewe tunaonana.Bila kupoteza muda naomba nijitambulishe “ akasema Nickson na kutulia kidogo halafu akaendelea
“Ninaitwa Nickson.Ni mfanyabiashara.Nimekuja hapa kukuletea taarifa ambazo si nzuri na nina imani hautazifurahia lakini kama mwanaume nakusihi ukaze moyo.” Akasema Nickson na kumfanya Patrick apatwe na wasi wasi
“Nickson sina hakika kama tumewahi kuonana mahali.Ni taarifa gani hizo ambazo si nzuri kwangu? Akauliza Patrick
“Patrick ninafahamu mahusiano yako na Happy Kibaho.Ninafahamu kwamba ulivunja mahusiano yako ya awali kwa ajili yake.Ninasikitika kukutaarifu kwamba pamoja na mapenzi yote uliyomuonyesha Happy lakini yeye ameshindwa kuwa mwaminifu kwako na hasa katika kipindi hiki ambacho uko gerezani” akasema Nickson na kumfanya Patrick azidi kuwa na wasi wasi
“Happy amefanya nini? Akauliza Patrick kwa wasi wasi.Nickson hakuongea kitu akaingiza mkono katika koti lake na kutoa bahasha akaisogeza karibu na Patrick
“Fungua uangalie” akasema Nickson.Patrick akaichukua bahasha ile na kuifungua.Ndani ya bahasha ile kulikuwa na picha akazitoa.Picha ya kwanza ikamstua na kuzifanya picha nyingine zote alizokuwa amezishika mkononi zianguke mezani.Akaitazama picha ile aliyokuwa ameishika mkononi.Mikono ilikuwa inamtetemeka huku kijasho kikianza kumchuruzika.Akaiweka picha ile chini na kuchukua picha nyingine akaiangalia.Macho yake yakaanza kutoa machozi.Akajikaza na kuanza kuzipitia picha zile moja baada ya nyingine.Kabla hajamaliza kuzitazama akamtazama Nickson kwa macho makali sana
“Nani amekutuma uniletee picha hizi? Akauliza Patrick huku machozi yakimtoka.Akainama tena akaziangalia picha zile.
“Ouh my gosh !! Happy !!!.Siamini .Siamini kama Happy anaweza akanifanyia hivi.” Akasema Patrick na kufuta machozi.Ghafla kwa nguvu akainuka ,akaisukuma ile meza na kumkaba Nickson
“Niambie nani amekutuma uniletee picha hizi?
Patashika kubwa likaibuka mle ndani na mara askari waliokuwa nje ya kile chumba wakaingia haraka na kumkamata Patrick kisha wakamuamuru Nickson aondoke haraka sana.Kwa haraka Nickson akazikusanya zile picha akaziweka mfukoni na kutoka mle chumbani huku Patrick akiwa ameshikiliwa na askari.Ghafla Patrick akamsukuma kwa nguvu askari aliyekuwa amemshikilia na kwa kasi ya aina yake akamvaa askari aliyekuwa amesimama pembeni ya mlango na kutaka kunyang’anya bunduki.Kuliibuka kizaazaa kikubwa .Patrick na Yule askari walikuwa wananyang’anyana silaha.Yule askari aliyekuwa amesukumwa na kuanguka chini akakiona kitendo kile na kuinuka haraka akamtandika teke kali la mbavuni na kumfanya Patrick aachie bunduki ile aliyokuwa akiing’ang’ania na kutoa yowe.Bila kujali maumivu aliyoyapata kwa teke lile akainuka tena kwa kasi na kutaka kumvamia askari tena yule mwenye silaha lakini askari Yule e alikiona kitendo kile na kwa nguvu akampiga na kitako cha bunduki akaanguka na kupoteza fahamu.Kwa kutumia simu ya upepo wakatoa taarifa kwa viongozi ambao walifika mara moja kushuhudia kilichotokea na kuamuru Patrick apelekwe katika hospitali ya gereza kwa matibabu wakati uchunguzi wa tukio lile ukiendelea.Patrick akatolewa mle chumbani na kukimbizwa katika hospitali ya gereza kwa ajili ya matibabu


* * * *

Savanna aliwasili salama jijini Dar es salaam,kutoka pale uwanjani alikodisha teksi iliyompeleka hadi nyumbani kwake.
“ Kitu cha kwanza ninachotakiwa kukifanya siku ya leo ni kwenda kuonana na Alois na kumuomba wasimueleze kitu chochote Patrick kuhusiana na tukio lile la Happy.Inatakiwa itafutwe namna nzuri ya kumfahamisha Patrick juu ya tukio hili kwani endapo tukikurupuka kumweleza tunaweza kusababisha mambo mengine.” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake
“Namuonea huruma sana Patrick.Matatizo aliyonayo ni makubwa sana.Amempoteza Vero,baba yake na sasa amejitumbukiza katika kesi kubwa ya mauaji na kabla haijajulikana hatima yake linaibuka tena suala hili la Happy.Ninatakiwa nifanye kila niwezalo ili kuhakikisha ninamtoa Patrick gerezani “akaendelea kuwaza Savanna
Alifika nyumbani kwake akaoga na kuvaa suruali nyeupe ya jeans na shati jekundu .Alipendeza vilivyo kama ilivyo kawaida yake.Kabla hajatoka akampigia simu Alois kaka yake Patrick na kumuomba waonane,kisha akaingia katika gari lake akaondoka .
“Nayaona maisha yangu kama yamejaa nuru na furaha hivi sasa na yote hii ni kwa sababu nina uhakika wa kuishi maisha yangu yote nikiwa na mwanaume nimpendaye kuliko wote duniani.” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Patrick kuonana na Alois kaka wa Patrick
Alipofika alipokelewa na Alois na baada ya maongezi machache akamkaribisha sebuleni
“Unaendeleaje Alois?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Tumekwishaizoea hali hii.Nashukuru Mungu hata mama naye anaendelea vizuri hivi sasa” Akasema Alois
“Nashukuru kusikia hivyo”
“Vipi kuhusu wewe Savanna unaendeleaje? Kesi inakwendaje?
“Mimi ninaendelea vizuri sana Alois na kuhusu kesi hakuna haja ya kuwa na wasi wasi kila kitu kinakwenda vizuri .Nawaomba muondoe shaka kabisa kuhusu kesi hii kwani ni lazima tushinde.” Akasema Savanna na kumfanya Alois atabasamu
“Ahsante sana Savanna kwa kuzidi kutupa matumaini.Umekuwa mfariji wetu na tegemeo letu katika suala hili la Patrick.Umemsaidia sana hata mama kutokuwa na wasi wasi na mwanae.Nikupe siri moja mama anampenda sana Patrick.”akasema Alois halafu kikapita kimya kifupi
“karibu sana Savanna” akasema Alois
“Alois mimi si mkaaji sana nimepita hapa mara moja ili tujadili kwa pamoja jambo hili lililotokea.” Akasema Savanna
“Jambo gani Savanna? Hili la Patrick?
“Ni kuhusu Happy.Nadhani umeisikia kashfa iliyompata”
“Ndiyo.Alinipigia simu Andrew jana na kunifahamisha.Niliitazama video yake katika mtandao sikuamini kama ni kweli Happy ameweza kufanya kitendo cha aibu kama kile.Nimefadhaika sana kwa sababu yule msichana ndiye chanzo cha Patrick kusota gerezani hivi sasa.Ni aibu kubwa mno na hata mama nimemficha sijamweleza chochote” akasema Alois
“Nakubaliana nawe Alois.Kitendo kile ni cha aibu sana na hakivumiliki.Kikubwa kilichonileta hapa ni kukuomba kwamba Patrick asifahamishwe kwa sasa.Endapo akifahamu alichokifanya Happy itamsababishia matatizo makubwa sana kwani kchwa chake kwa sasa kimebeba mambo mengi ”
“Savanna bila hata kuomba lakini naomba nikuhakikishie kwamba si mimi wala mtu yeyote katika familia yetu angeweza kumweleza Patrick kitu chochote kuhusiana na uchafu uliofanywa na Happy.Ni kitendo cha aibu sana na kisichovumilika.Moyo wangu umeumia hasa nikimuangalia mdogo wangu anavyoteseka gerezani kwa ajili ya huyu huyu msichana”
“Ahsante sana Alois kwa busara hiyo.Basi ni hilo pekee lililonileta hapa.Naomba uniruhusu niondoke nikaendelee na majukumu mengine.” Akasema Savanna
“Nashukuru sana Savanna kwa kuja kututembelea bahati mbaya mama amelala alikuwa na hamu sana ya kukuona”
“Mpe salamu zangu.Nitakuwa nikija hapa mara kwa mara kumsalimu” akasema Savanna kisha akainuka na kuondoka.
“Kwa sasa ni safari ya moja kwa moja kueleka Uwangwa .kabla sijafanya chochote lazima niaonane kwanza na Patrick.Sijamtia machoni kwa siku nzima ya jana” akawaza Savanna

* * * *

Ilimchukua dakika arobaini kuwasili katika gereza la Uwangwa.Kijua kilikuwa kikali sana siku hii.Kisha shuka garini akaelekea moja kwa moja mapokezi kama ilivyo kawaida yake na pale alipewa taarifa kwamba akaonane na mkuu wa gereza.Alistushwa sana na taarifa ile.Alijaribu kudadisi ili kufahamu nini kilichotokea hadi ikamlazimu akaonane na mkuu wa gereza kabla ya kuonana na Patrick lakini hakuna aliyekuwa tayari kumweleza chochote.
Huku akiwa na uso uliojaa wasi wasi Savanna akatembea kwa kasi kuelekea katika ofisi ya mkuu wa gereza.Alijitambulisha kwa katibu muhtasi wa mkuu wa gereza ambaye alimpigia simu mkuu wake na kisha akamruhusu Savanna aingie ofisini.
“karibu Savanna” akasema mkuu wa gereza.
“Nashukuru sana mkuu” akasema Savanna.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa
“Mkuu nimekuja kuonana na mteja wangu lakini nimestushwa kidogo kwa kuambiwa kwamba unahitaji kuniona kabla ya kuonana na mteja wangu” akasema Savanna
“Ni kweli Savanna.Nilitoa maagizo hayo.Kuna jambo limetokea leo kuhusiana na mteja wako” akasema mkuu wa gereza na kumfanya Savanna astuke
“jambo gani limetokea tena?
“Leo asubuhi kuna mtu ambaye alikuja kuonana na Patrick.Kwa mujibu wa askari waliokuwepo eneo la tukio,mtu huyo alikuwa na bahasha yenye picha ambazo alimpa Patrick azitazame.Hatujui picha hizo ni za nani na kwa nini mtu huyo alimpa Patrick lakini inasemekana baada tu ya Patrick kuziona picha hizo alibadilika na kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.Alimkaba mtu Yule aliyempeleka zile picha na akazua tafrani kubwa.Askari ambao walikuwa nje waliingilia kati ugomvi huo na kumdhibiti Patrick lakini alifanya kitu cha ajabu sana kwani alimvamia askari na kutaka kumnyang’anya silaha.Hatuelewi alikusudia kufanya nini na ile bunduki lakini nina hakika angefanikiwa kuipata silaha ile angeleta maafa makubwa.Askari walifanikiwa kumdhibiti na kumsababishia jereha kidogo kichwani na hivi sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika zahanati ya gereza”
“Ouh my gosh !! akasema Savanna huku ameshika kichwa kwa mikono.
“Kuna taarifa zozote za maendeleo yake?
“Kwa taarifa nilizozipata toka kwa madaktari muda si mrefu ni kwamba Patrick anaendelea vizuri.”
“Ouh Mungu wangu ..!!” akasema Savanna.Suala lile lilikuwa limestua sana.
“Savanna suala hili la Patrick ni suala zito sana na endapo litafika katika vyombo vya sheria litakuwa na athari kubwa sana kwa Patrick na hata kwa uongozi wa gereza.Kwa heshima yako suala hili litaishia hapa hapa na halitaenda sehemu yoyote lakini hata hivyo inabidi tuchukue hatua za kuzuia jambo kama hili lisijitokeze tena.Tumeamua kudhibiti watu wanaokuja kumtembelea Patrick.Kuanzia hivi sasa watakaoruhusiwa kuonana naye ni wewe pamoja na familia yake pekee.Hakuna mtu mwingine yeyote atakayeruhusiwa kumuona.Hii ni kwa ajili ya usalama wa Patrick vile vile kwani hatujui katika watu wanaokuja kumtazama ni yupi atakuwa adui yake”
“Nashukuru sana mkuu wa msaada wako huu mkubwa.Nitaongea na Patrick na kumsihi asithubutu kufanya kitendo cha hatari namna hiyo tena.Ninaweza kuruhusiwa kuonana naye?
“Twende tuongozane na mimi nikaangalie maendeleo yake.” Akasema mkuu wa gereza huku akiinuka akatoka mle ofisini
“Nahisi mwili wote ni kama umekufa ganzi.Ni nani huyu aliyemletea Patrick picha? Najua ni lazima zitakuwa ni picha za Happy.Ninaanza kujenga hisia kwamba jambo hili si la mtu mmoja bali linahusisha kikundi cha watu na wana ajenda yao ya siri kufanya hivi na ajenda yao kubwa ni kuuharibu uhusiano wa Patrick na Happy.Kwa mujibu wa barua ile aliyoindika Happy ni kwamba alitekwa na kundi la watu waliomlazimisha kufanya ngono na kisha kumpiga picha za utupu na kuzisambaza.Kuna ulazima wa kuwafahamu watu hawa wenye roho za kikatili namna hii” akawaza Savanna wakati wakielekea katika zahanati ya gereza kumuangalia Patrick
Mkuu wa gereza na Savanna waliingia katika ofisi ya mganga mkuu wa gereza ambaye aliwapa taarifa za maendeleo ya Patrick na kisha kuwapeleka katika chumba alichokuwa amelazwa Patrick
“Tumemchoma sindano ya usingizi nadhani baada ya masaa mawili au matatu ataamka.” Akasema daktari.Patrick alikuwa amelala usingizi mzito sana pale kitandani na sehemu ya juu ya jicho lake alikuwa na jeraha.Mkono wake wa kushoto ulikuwa umefungwa pingu.Savanna akashindwa kuvumilia kumuona Patrick katika hali ile akaangusha machozi
“Tafadhali mkuu naombeni mumfungue hiyo pingu.Hatakwenda sehemu yoyote.Hawezi kukimbia”
“Hii pingu amefungwa kwa ajili ya usalama.Alipoamka mara ya kwanza alionekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa.Alitaka kukimbia akazuiwa hivyo tumeona ni bora kama tukimfunga pingu ili asiweze kutoka hapa kitandani akasema daktari
“Savanna wewe unaweza kwenda kupumzika.Mteja wako yuko katika uangalizi makini .Endapo kutakuwa na tatizo lolote tutakutaarifu” akasema mkuu wa gereza.
“Ahsante sana mkuu ,lakini naomba niendelee kukaa hapa hadi hapo atakapoamka ili niweze kuongea naye hata maneno mawili na nimsihi atulie asifanye jambo lolote la hatari.tafadhali mkuu naomba uniruhusu kwa hilo” akaomba Savanna
Mkuu wa gereza akainama akafikiri kwa muda kisha akasema
“Sawa Savanna,kama unahitaji kujiridhisha zaidi na maendeleo ya mteja wako basi hakuna shaka.Kuna mgahawa wa gereza unaweza kwenda kukaa pale na pindi atakapoamka tutakutaarifu.” Akasema mkuu wa gereza halafu wakatoka .Savanna akakabidhiwa askari aliyempeleka hadi katika mgahawa wa maofisa wa gereza.
“Sintawataarifu familia yake kwa sasa hadi hapo nitakapohakikisha anaendelea vizuri.Nikiwaeleza sasa hivi kwamba mtoto wao amepatwa na matatizo tena ninaweza kuwasabishia matatizo mengine katika wakati huu mgumu walionao” akawaza Savanna
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 50
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mkuu wa gereza akainama akafikiri kwa muda kisha akasema
“Sawa Savanna,kama unahitaji kujiridhisha zaidi na maendeleo ya mteja wako basi hakuna shaka.Kuna mgahawa wa gereza unaweza kwenda kukaa pale na pindi atakapoamka tutakutaarifu.” Akasema mkuu wa gereza halafu wakatoka .Savanna akakabidhiwa askari aliyempeleka hadi katika mgahawa wa maofisa wa gereza.
“Sintawataarifu familia yake kwa sasa hadi hapo nitakapohakikisha anaendelea vizuri.Nikiwaeleza sasa hivi kwamba mtoto wao amepatwa na matatizo tena ninaweza kuwasabishia matatizo mengine katika wakati huu mgumu walionao” akawaza Savanna

ENDELEA……………….

Ni mtu mmoja tu aliyekuwa anasubiriwa atoke ndani ili safari ya kuelekea makaburini ianze.Siku hii ya leo familia ya Vero waliamua kwenda kulitembelea kaburi la Vero ambalo tayari lilikuwa limemalizwa kutengenezwa.Kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kuweka vigae pamoja na marembo mengine na kulifanya lipendeze mno
Familia yote ilikwisha kusanyika na aliyekuwa anasubiriwa ni mama yao.Wote walikuwa wamepanda katika gari moja.
“She’s taking too long” akasema Loniki
“Labda anasal…….” Shangazi yao akataka kusema kitu lakini kabla hajamaliza mtu waliyekuwa wanamsubiri akatokea na safari ikaanza
Kabla hawajafunga mlango simu ya Loniki ikaita.Akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji alikuwa ni Linah
“Hallow Linah
“Lonny umeamkaje dear?
“Nimeamka salama Linah.”
“Uko wapi mida hii? Bado umelala?
“Hapana Linah.Niko na familia tunajiandaa kwenda kutembelea kaburi la Vero.Mafundi tayari wamemaliza matengenezo”
“Lonny kama ningekuwa na muda ningekuja kuungana nanyi lakini nimebanwa sana leo”
“usijali sana Linah.Vipi kuna habari gani mpya?
“Khumalo kanipigia simu sasa hivi na kunitaarifu kwamba tayari Patrick ameziona zile picha”
“Ouh gosh ..!! what happened? Akauliza Loniki kwa furaha huku akishuka garini ili aweze kuongea vizuri na Linah bila ya mtu kusikia maongezi yao
“kwa mujibu wa taarifa ya kijana aliyezipeleka picha hizo ni kwamba mara tu Patrick alipozitama alibadilika na kuwa kama mtu aliyepandwa na uchizi.Alimvamia kijana huyo na kutaka kufahamu aliyemtuma ampelekee picha hizo kwa bahati nzuri kulikuwa na askari karibu hivyo hakuweza kumdhuru.Baada ya askari kumshikilia Patrick asiendelee kuleta fujo ,alimrukia askari aliyekuwa na bunduki na kutaka kumnyang’anya silaha jambo lililowalazimu askari kumtembezea kipigo kikali sana.Hivi sasa nasikia hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya gereza”
“Ouh gosh ! that’s great news to hear this morning.Sipati picha ingekuaje kama angefanikiwa kuinyakua hiyo bunduki.Nadhani lengo lake lilikuwa kujiua.Hahaha haaa I think the plan is working .Patrick and Happy are both in great pain right now” akasema Loniki huku akitabasamu kwa furaha
“Si hilo tu Lonny kuna taarifa nyingine pia imevuja kwamba Happy alitaka kujiua kwa kunywa sumu baada ya kuziona picha zile.Taarifa zinaseama kwamba baada ya kunywa sumu alikimbizwa katika hospitali ya Brahmaputra lakini uongozi wa hospitali ile umekanusha taarifa hizo.Taarifa mpya iliyopatikana toka vyanzo vya karibu vya Khumalo ni kwamba mpaka muda huu Happy hajulikani alipo.Waandishi wa wa habari wamekuwa wakimtafuta kwa mahojiano lakini hawajui yuko wapi na simu yake haipatikani tena na hata familia yake haiko tayari kusema mtoto wao yuko wapi” akasema Linah
“hahaaa aahahaa haaa!! Loniki akacheka kwa furaha na mara honi ya gari ikapigwa
“Linah wananipigia honi.Tutaongea baadae.Ahsante kwa taarifa” akasema Linah akakata simu na kukimbilia garini
“mambo ndo kwanza yanaanza Patrick.I’ll make your life a living hell.You and your girl must pay for what you did to Vero” akawaza Loniki
“Natumai kwa muda huu Patrick na Happy watakuwa katika mateso makubwa sana.Niliahidi kulipiza kisasi kwa kifo cha mdogo wangu na nitafanya hivyo.Huu ni mwanzo tu” akawaza Loniki
Safari ilikuwa ya kimya kimya hadi walipofika makaburini.Wakashuka garini na kuelekea katika kaburi la Vero.Lilikuwa kaburi linalopendeza na lililojengwa kwa ustadi mkubwa.Mama yake Vero akashindwa kuyazuia machozi kumtoka tena.Akakaa juu ya kaburi la binti yake aliyempenda sana na kuanza kulia
“Masikini binti yangu,wamekukatili uhai wako.Hukustahili kuondoka na kuniacha peke yangu mapema namna hii.Ninaomba usiku na mchana wale wote waliokukatili mwanangu na kunisababishia mateso haya makali wapate adhabu kali inayowastahili” akalia mama yake Vero.Loniki akamsogelea na kukaa pembeni yake
“Usilie mama,wote waliohusika na kifo cha Vero watapata adhabu inayowastahili na tayari yamekwisha anza kuwapata makubwa.Wataumia na kuteseka kama sisi tunavyoumia na kuteseka” akasema Loniki
Sarah ambaye anaye alikuwa amesimama karibu na kaburi akastuka baada ya kusikia maneno ya Loniki.
“mama ,kitu peke kinachoweza kukupa amani ya moyo ni kumuachia Mungu suala hili na si kuwaombea mabaya wahusika wa tukio hili.Kwa kuwaombea mabaya unakwenda kinyume na maandiko yanayotukumbusha kwamba tuwapende wabaya wetu na tuwaombee neema na Baraka .Ni Mungu pekee ndiye atakayewaadhibu” akasema Sarah
“Sarah najitahidi sana kufanya hivyo lakini ninashindwa.Kila nikifikiria namna mwanangu alivyokufa najikuta nikiwa na hasira na hamu ya kutaka kuwaona wale wote waliofanya kitendo kile wakipata adhabu kali.”
“Usiseme hivyo mama.Unat……” akasem Sarah lakini Loniki akaingilia kati
“Mama usimsikilize huyu.Siku zote yeye amekuwa upande wa Patrick.Hana uchungu wowote na kifo cha mdogo wake.Mama mimi ndio niko pamoja nawe.Wote waliosababisha kifo cha Vero lazima wapate adhabu kali”
Sarah na Loniki wakaangaliana kwa macho makali sana.Ikamlazmu mama yao kuingilia kati
“Haya inatosha sasa.Tuwekeni maua tuondoke” akasema mama yao halafu akachukua maua akayaweka juu ya kaburi na kupiga magoti,akasali kimya kimya na kusogea pembeni kuwapa nafasi wengine.Kila mmoja aliyekuja hapo aliweka shada la maua na kusali sala fupi
“Vero mdogo wangu,natumai huko uliko unaniona mida hii.Niliahidi kulipa kisasi kwa wale wote waliokufanyia unyama ule mkubwa na kukukatili maisha yako .Tayari nimeanza kuitekeleza ahadi yangu na wahusika wameanza kulipa.Si kazi rahisi lakini nakuahidi nitaifanya hadi nihakikishe Patrick na mwenzake wamelipa” akasema Loniki kwa sauti ndogo akiwa amepiga magoti katika kaburi la Vero.Zoezi lilipokamilika wakaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani

* * * *

Mlio wa simu ukamstua Savanna toka katika mawazo mengi.Ilikuwa ni simu toka kwa mkuu wa gereza
“hallo mkuu” akasema Savanna
“Savanna nimetaarifiwa kwamba tayari Patrick ameamka,unaweza kwenda kumuona sasa”
“Ahsante sana mkuu” akasema Savanna huku akiinuka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika zahanati ya gereza
“Mungu msaidie Patrick katika kipindi hiki kigumu alichonacho.” Akaomba Savanna wakati akipanda ngazi kuingia zahanati.Alionana na daktari ambaye alimpeleka moja kwa moja katika chumba alicholazwa Patrick
Mara tu Patrick alipomuona Savanna akainuka na kukaa kitandani.Savanna akamuendea na kumkumbatia
“Ouh Patrick,pole sana” akasema Savanna
“Savanna nashukuru umekuja” akasema Patrick kwa sauti ndogo yenye kukwama kwama.
“Patrick unajisikiaje sasa hivi?
“I’m dead Savanna.I feel dead” akasema Patrick
“Patrick usiseme hivyo”
“Savanna I want to die.namba uwaambie wanifungue hii pingu nife.I want to die.Sioni tena sababu ya kuendelea kuishi“
“Patrick tafadhali naomba unisikilize”
“Savanna believe me I’m dead.Ninahisi maumivu makali ya moyo.Nahisi kama kuna kitu kikali kinaukata moyo wangu vipande vipande..Ninasikia maumivu makali ambayo siwezi kuyaelezea” akasema Patrick
“Patrick nini kimetokea? Akauliza Savanna
“Savanna Happy yuko wapi? Happy ameniua.Ameniua bila kosa kama alivyomuua Vero.Nimemkosea nini mpaka anifanyie unyama wa namna hii? Upendo wote huu niliomuonyesha iweje leo hii anifanyie namna hii? It was all a lie.There was no us,there was no love ,it was all lies.Please let me die” akasema Patrick kwa uchungu
“Patrick tafad…………….” kabla Savanna hajamaliza alichotaka kukisema Patrick akapaaza sauti
“Waambie wanifungue.I want to die..!!!!!!!!!!!!!!!!”
Savanna akaogopa na kuwaita madaktari ambao walimkamata na kumchoma sindano ya usingizi
“Savanna unaweza kwenda nyumbani saas.Patrick bado akili yake haijatulia.Tutaendelea kumuangalia na kama kutakuwa na tatizo lolote tutakufahamisha” daktari akamshauri Savanna ambaye alikubali na kuondoka kuelekea nyumbani kwake.Hakutaka tena kufanya kazi yoyote kwa siku ile.kili yake yote ilikuwa inamuwaza Patrick.

* * * *

Ni siku ya pili sasa toka Parick alpolazwa katika hospitali ya gereza.Hali yake ilikuwa imeimarika tofauti na siku zilizotangulia
“Halloo Patrick “ akasema Savanna aliyekuja kumsalimu asubuhi hii
“Savanna.Karibu sana” akasema Patrick huku akijilazimisha kutabasamu
“Ahsante Patrick,unaendeleaje?
“Namshukuru Mungu leo sijambo.Naendelea vizuri sana.Madaktari wamenisaidia sana kunirejesha katika hali ya kawaida” Akajibu Patrick ambaye siku hii hakuwa amefungwa pingu kama siku zilizotangulia.
“Nashukuru sana kama unaendelea vizuri” akasema Savanna huku akiifungua chupa ya chai aliyokuja nayo na kummiminia Patrick chai katika kikombe
“mama na ndugu zangu wote hawajambo? Akauliza Patrick
“wote wazima na wanaendelea vizuri .Ninapita kila siku kuwasalimu na kumpa mama maneno ya matumaini.Mama anafarijika sana kila anionapo.Utanisamehe kwa kuwa sijawaambia chochote kuhusiana na wewe kulazwa hapa hospitali.Niliogopa kumuongezea mama matatizo hasa katika wakati huu ambao hali yake imeanza kuimarika.”
“Ulifanya vizuri sana Savanna kutokuwaeleza chochote.Wamekwisha umia vya kutoka kwa sababu yangu na sitaki waendelee kuumia zaidi.Nataka niendelee kuteseka mimi mwenyewe.” Akasema Patrick
“Savanna nakushukuru sana .Sipati nena la kuelezea shukrani zangu .You are my true friend.Umekuwa na mimi toka dakika ya kwanza na hadi leo hii haujaniacha hata siku moja.Savanna you have a special place in my heart.Sikujua kama siku moja wewe ndiye ungekuja kuwa mkombozi wangu.Watu niliowaamini na kuyatoa maisha yangu kwa ajili yao leo hii hawako tena na mimi,wamenisaliti na kuniacha peke yangu.Rafiki yangu Andrew,Happy…” Patrick akainama akazama katikam awazo halafu akainua kichwa na kusema
“Savanna naomba unisaidie ili niweze kutoka humu gerezani kwani sioni tena sababu ya mimi kuendelea kukaa humu gerezani.Nimempoteza Vero msichana aliyenipenda kwa moyo wake wote kwa ajili ya mtu ambaye haoni thamani yangu kwake.I was so wrong” Akasema Patrick kwa uchungu.
“Patrick usijilaumu sana kwani hukutegemea kama yangetokea haya yaliyotokea.Pamoja na kuondoka kwa Vero lakini kaa ukijua kwamba bado kuna watu wengi wanaokupenda na kukuombea usiku na mchana ili uweze kutoka salama gerezani na kuendelea na maisha yako.Familia yako,Happy na m………” kabla hajamaliza sentensi yake Patrick akasema kwa ukali
“Savanna tafadhali naomba usilitamke jina la huyo Malaya mbele yangu tena.Hilo ni jina ambalo sitaki kulisikia tena katika masikio yangu.Nilimpenda sana nikampa mwili na moyo wangu,nilikuwa tayari kuachana na kila kitu kwa ajili yake lakini kwa alichonifanyia sidhani kama nitakuja kumsamehe Happy.Savanna nimeumia sana.Sikuona sababu ya kuendelea tena kuishi siku ile niliponyeshwa picha za uchafu wake.” Akasema kwa uchungu Patrick
“Sijui nimweleze ukweli kuhusu suala hili? Lakini hapana,siwezi kufanya hivyo.Tayari amekwisha mtoa Happy akilini mwake na hii ni nafasi yangu sasa.Nataka Patrick awe wangu na inanibidi kuitumia vyema nafasi hii niliyoipata.Sintamweleza lolote kuhusiana na Happy” Akawaza Savanna
“Patrick pole sana.Hata mimi nilistuka sana nilipoziona picha za Happy katika gazeti na mitandao.Niliogopa sana hata kukwambia kwani nilijua ungeumia mno.” Akasema Savanna
“Usijali Savanna.Kuna watu walioguswa sana na kitendo kile na wakaniletea picha zile ili niangalie uchafu alioufanya mtu niliyemkabidhi moyo wangu.Siwafahamu watu hawa lakini nawashukuru sana kwa kunisaidia kutambua kwamba mtu niliyedhani ni kondoo ,alikuwa ni chui.Sikutegemea kama Happy angeweza kutenda kitendo kichafu na cha kujidhalilisha kama kile.Ninachoweza kukuomba kwa sasa ,nisaidie niweze kutoka humu gerezani na nianze upya maisha yangu.tafadhali Savanna usiniache nikafungwa kwa sababu ya mtu ambaye haioni thamani yangu kwake.”
“Patrick usijali kuhusu hilo.Kama nilivyokwisha kuahidi na ninavyoendelea kukuahidi ni kwamba nitafanya kila niwezalo ili uweze kushinda kesi hii.Bado hujachelewa kuyaanza upya ,maisha yako.Siku zote fahamu kwamba umezungukwa na watu wanaokupenda na kukujali kwa hiyo usijione mpweke.I’m right here for you any time you need a friend” akasema Savanna..

**********************


Dr Consolata bugama bingwa wa magonjwa ya akili,aliagana na mgonjwa wake akapanda gari lake na kuondoka pale Reonaldo hoteli.Happy alilitazama gari lile hadi lilipotoka kabisa katika lango la hoteli ile ya kifahari jijini Kigali.Akatabasamu na kuelekea katika sehemu ya kupumzikia
Ni siku ya tisa sasa toka alipokuja katika jiji hili la Kigali.Hali yake ilikuwa inaimarika siku hadi siku.Kwa msaada mkubwa anaoupata toka kwa daktari aliyeambatana naye toka Dar es salaam pamoja na Dr Consolata bingwa wa magonjwa ya akili katika hospitali kuu ya Kigali hali yake ilikuwa ya kuridhisha sana.
“Namshukuru sana Mungu kwa huruma yake hivi sasa ninaendelea vizuri.Sikutegema kama hali yangu ingekuwa namna hii.Mungu ni mwema sana na bado ananipenda na ndiyo maana hakuruhusu nife kwa sumu.Nawashukuru sana madkatari wangu kwa jitihada zao za kuhakikisha kwamba ninarejea katika hali yangu ya kawaida.Dr Consolata amejitahidi sana kuhakikisha kwamba akili yangu inarejea katika hali yake ya kawaida.Namshukuru sana pia Christine.Huyu dada amekuwa ni mtu wangu wa karibu na kila mara ninapohitaji mtu wa kuongea naye yeye amekuwa tayari kufanya hivyo.Siwezi kuusahau uongozi na wafanyakazi wa hoteli hii .They are all wonderfull people.Ni wakarimu na wote wananipenda sana.Ninahudumiwa kama mtoto wa rais.Ninapenda sana kuendelea kuishi hapa.Nimepapenda Kigali.I feel so Happy and safe around here” akawaza Happy huku akitabasamu
“Ouh gosh ! siwezi kumsahau Savanna.Japokuwa moyo wangu unastuka kila ninapoikumbuka sura yake lakini sina budi kumshukru kwa msaada mkubwa alionipatia.Najua hata wazo la kuondoka Tanzania na kuja Kigakli ni yeye ndiye aliyelitoa na kulisimamia kwa nguvu zote na likafanikiwa.Amenisaidia mno kuniondoa katika aibu na fedheha niliyoipata.Niko nje ya Tanzania sasa,ninashukru sana kwa sababu aibu niliyoipata ni kubwa na ambayo inanifanya nisitake tena kurudi Tanzania.Inaniuma sana kuiacha nchi yangu na kumuacha Patrick mwanaume wa maisha yangu niliyempigania kwa kila namna niliyoweza lakini kwa hili lililotokea nimeinua mikono.Sina namna nyingine zaidi ya kukubali kushindwa na kumuacha Patrick mikononi mwa Savanna.Najua atakuwa katika mikono salama.Mimi na Patrick hatuwezi kuwa pamoja tena.Huu ni ukweli ambao hatuwezi kuukwepa.” Akawaza Happy na sura yake ikaanza kubadilika na kuwa ya huzuni kidogo
“ Najaribu kumuhusisha Savanna na tukio lile la kutekwa kwangu lakini sioni kama ana uhusika wowote katika jambo lile.Kama si yeye nani basi anaweza kuwa nyuma ya tukio lile? Picha niliyoipata ni kwamba watu walionitenda vile lengo lao lilikuwa ni kunidhalilisha na kuhakikisha kwamba kwa namna yoyote ile ninaachana na Patrick.Laiti ningejua kwamba lengo lao ni hilo nisingekubali kufanyiwa udhalilishaji ule mkubwa.Anyway namuachia Mungu yeye ndiye atakayenilipia kwa mambo yote niliyofanyiwa.” Akaendelea kuwaza Happy
“Najua maisha yangu hayatakuwa na furaha tena na ninajua kwamba sintampata mwanaume kama Patrick katika maisha yangu yaliyobaki lakini ni vyema endapo nitakwenda kuishi mbali kabisa naye,mbali na Tanzania .Sitaki kukaa karibu naye kwani itanifanya niendelee kulipigania penzi letu na kadiri ninavyoendela kuupigania uhusiano wetu ndivyo mambo mabaya yanavyozidi kunitokea.Nimekwisha msababishia Patrick maumivu mengi ya moyo na sitaki aendelee kuumia zaidi.Nadhani uamuzi huu wa kutorejea tena Tanzania ni uamuzi wa busara sana ingawa najua Patrick ataumia mno na kunichukia.Ataniona kama ni msaliti na nilifanya kitendo kile kwa makusudi.Hakuna siri siku hizi hata kama yuko gerezani lazima atazipata taarifa zangu na nina hakika ataamini kwamba hii ndiyo tabia yangu.Ouh gosh ! ni mateso makali sana ya moyo atakayoyapata..” Akawaza Happy halafu akainuka na kuanza kuzunguka bustanini
“Dr Consolata amekuwa akijitahidi sana kuhakikisha ninasahau yaliyopita .Sipaswi kuendelea kuyafikiria yaliyopita.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kufikiri kuhusu maisha yangu ya mbele yatakuwaje.” akawaza Happy huku akiendelea kuzunguka zunguka mle bustanini
“Nimeipenda sana Rwanda .Ni nchi nzuri na ningefurahi mno kama ningeishi katika nchi hii kwa maisha yangu yote yaliyobakia.Lakini siwezi kufanya hivyo.Lazima niondoke Rwanda.Natakiwa kwenda kuishi mbali kabisa na Tanzania ikiwezekana nje kabisa ya Afrika.Nataka nikaishi mahala ambako nitaishi bila kuonana na mtu yeyote wa kutoka Tanzania.Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza akanisaidia katika hili. Ni Mike pekee.Najua niliutia moyo wake jeraha kubwa ambalo si rahisi kupona haraka ,niliuvunja vunja moyo wake pale nilipoamua kuachana naye na kurudiana na Patrick.Najutia nafsini kwangu kwa kitendo kile.It needs more than a man to forgive me for what I did.Japokuwa kabla hajaondoka Tanzania alinihakikishia kwamba amenisamehe lakini sina hakika kama ataweza kukisahau kitendo kile nilichomfanyia.”
Happy akasimama baada ya picha ya Mike akiondoka Tanzania chini ya ulinzi mkali kumjia kichwani.
“Ouh Gosh ! forgive me Mike” akasema Happy huku akisikia uchungu mwingi moyoni
“Sina hakika kama Mike anaweza kuwa tayari kunisaidia au hata kunisikiliza lakini sitakiwi kukata tamaa.Natakiwa kujaribu kumuomba anisaidie.Endapo atakataa kunipa msaada ninaoutaka nitatafuta namna nyingine ya kufanya.Nitamuomba hata Savanna anisaidie.Kitu pekee ninachokiami na kinachonipa msukumo wa kutaka kuwasiliana na Mike ni kwamba Mike ananipenda kwa moyo wake wote.” Akawaza Happy na kuupeleka mkono sehemu ulipo moyo wake ambao ulikuwa unadunda kwa kasi kubwa.
“lazima niwasiliane naye na nimuombe anisadie.Lazima niondoke hapa Kigali na kwenda mbali.Namuonea huruma sana baba yangu .Amekuwa nami kwa kipindi kirefu toka matatizo haya yalipoanza na yeye ndiye amekuwa msaada mkubwa kwangu.Ni wakati sasa wa yeye kupumzika na kuendelea kufanya shughuli zake za kimaendeleo.Ninajisikia furaha sana kuwa na baba kama huyu.He’s the best father in the world.” Akawaza Happy na kutabasamu
“Ngoja sasa nikampigie simu Mike.” Akawaza Happy na kuelekea chumbani kwake.Alipoingia chumbani kwake akasimama mbele ya meza iliyokuwa na simu akaitazama simu ile na kuvuta pumzi ndefu.
“I’m so scared” akasema kwa sauti ndogo.Kwa takribani dakika tatu alisimama akiitazama simu ile.Alihisi kama mikono yake ikimtetemeka kila alipojaribu kutaka kuichukua simu ile na kupiga
“Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie.Nahitaji kufanya hivi.Nahitaji kuongea na Mike” akasema Happy kwa sauti ndogo.Baada ya tafakari akaamua kupiga.Alizifahamu namba za simu ya mkononi ya Mike na akaziandika huku mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi kubwa.Akauweka mkono wa simu sikioni na simu ikaanza kuita.Baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ikimwambia
“Mike hayuko katika nafasi ya kupokea simu kwa sasa tafadhali acha ujumbe wako baada ya mlio.” Happy akavuta pumzi ndefu na mara baada ya mlio kusikika akasema
“Hallow Mike,ni mimi Happy.Naomba upatapo uumbe huu,unipigie simu.Kwa sasa niko Kigali Rwanda,Reonaldo hoteli presidential suit number two.Please call me back Mike.I real need to talk to you” Happy aliyasema maneno haya huku machozi yakimtoka.Akauweka mkono wa simu chini ,akapangusa machozi na kwenda kuketi sofani
“Please Help me Mike” akasema kwa sauti ndogo
Baada ya dakika tano kupita simu ikaita.Akainuka na kwenda mezani akasimama na kusita kuipokea.Simu ikaendela kuita na mwishowe akaamua kuipokea.
“hallo “ akasema Happy
“Hallow Happy.Mike hapa nongea” Ikajibu sauti ya upande wa pili.Mikono ya Happy ikaloa jasho.Kwa sekunde kadhaa alihisi kama sauti yake ikigoma kutoka
“Hallow Mike” akasema Happy kwa sauti yenye kitetemeshi
“Hallow Happy.Unaendeleaje? Nimeupata ujumbe wako muda si mrefu.Habari ya Tanzania?
“habari ya Tanzania nzuri ila kwa sasa niko Kigali Rwanda”
“Sawa Happy.Nashukuru sana kwa kunikumbuka .Patrick anaendeleaje?
Swali lile likamchoma sana Happy akahisi kama miguu inaisha nguvu
“ Anaendelea vizuri” akajibu kwa ufupi
“Happy una tatizo gani? Naisikia sauti yako kama haiko sawa.Ninakufahamu vyema wakati una tatizo”
Happy akakaa kimya akahisi kama midomo yake inashindwa kufunguka
“ Happy una tatizo gani? Akauliza tena Mike
Happy akakohoa kidogo na kusema
“Mike ni kweli nina tatizo na ninahitaji msaada wako” kimya kifupi kikapita Mike akasema
“Una tatizo gani Happy?
“Mike siwezi kukueleza katika simu ni tatizo kubwa.Najua kwa sasa mimi ni mtu ambaye hupendi kuniona na hata kuisikia sauti yangu kutok…………”
“No ! No ! Happy.Usifikiri hivyo” mike akamkatisha Happy
“Ni kweli Mike.Hata mimi mwenyewe nafsi yangu inanisuta sana kwa kitendo nilichokufanyia lakini pamoja na hayo yote yaliyotokea sina mtu mwingine ninayeweza kumkimbilia kuomba msaada kwa sasa.Mike najua ndani kabisa mwa moyo wako bado nina nafasi japokuwa ndogo sana.Ninakuomba kama rafiki unisaidie” akasema Happy huku machozi yakimtoka.Kupitia spika za simu Happy akamsikia Mike akivuta pumzi ndefu na kusema
“Happy,napenda niwe wazi kwako kwamba kilichotokea baina yetu kiliniumiza sana.Nilipata jeraha ambalo halitaweza kutibika.Ulipoamua kuniacha niliumia sana.hadi hivi sasa bado ninaamini kilichotokea ni kama ndoto na ndiyo maana nilipoupata ujumbe wako nimekupigia simu mara moja.” Akasema Mike na kunyamaza .Maneno yale yakamuumiza sana Happy na kuzidi kumtoa machozi.Mike akaendelea
“Happy kama nilivyosema siku ile nilipokuja kukuaga kwamba mimi tayari nimekusamehe na wala sina kinyogo chochote nawe.Kwangu mimi ,wewe bado ni mtu muhimu sana na rafiki wa pekee kabisa. Niko tayari kukupa msaada wowote na kwa wakati wowote.Naomba unieleze unahitaji msaada gani Happy? Akasema Mike .Happy ambaye kifua chake kilikuwa kimeloa machozi akasema
“Mike kwa sasa nimekwama hapa Kigali na lengo langu kubwa ni kuondoka hapa. Nataka kuja Marekani lakini sina namna ya kuondoka hapa.Naomba unisaidie ili niondoke hapa kuja Marekani.Nahitaji kuwa mbali na Tanzania.Tafadhali Mike nahitaji sana msaada wako sasa kuliko wakati wowote katika maisha yangu.Tafadhali naomba unisaidie Mike” Happy akaomba.Sauti yake ilitia huruma sana na ilionyesha dhahiri ni jinsi gani alivyokuwa akihitaji msaada wa Mike
Mike akavuta pumzi ndefu ,kikapita kimya cha dakika moja halafu akasema
“Nimekuelewa Happy.Nitakusaidia.Siwezi kukuacha wakati wa matatizo.Nitakusaidia Happy.Ninachohitaji kufahamu ni kama nyaraka zako zote za kusafiria unazo?
“Ndiyo Mike.Nyaraka zote ninazo hapa”
“Sawa Happy.Usijali nitakusaidia .Nitakupigia simu jioni ya leo kukufahamisha mchakato mzima ulivyo”
“Ouh Mike nakushukuru sana kwa kukubali kunisaidia” akasema Happy huku uso wake ukichanua kwa tabasamu
“Ni wajibu wangu kukusaidia Happy na nitafanya hivyo.Nitaongea nawe tena jioni ya leo kwa kirefu zaidi”
“Ahsante Mike” akasema Happy na kukata simu
“Ouh Gosh ! Siamini kabisa kama Mike amekubali knisaidia. Nasikia aibu sana kumuomba msaada Mike lakini kwa wakati huu nimekwama na ni yeye pekee anayeweza kunisaidia.Ninaamini Marekani nitaweza kuishi kwa amani bila bughudha.Ouh Mungu wangu naomba unisaidie ili Mike asiweze kubadili mawazo yake.” Akawaza Happy
Wakati Happy akiwa katika lindi la mawazo lililochanganyika na furaha mara kengele ya mlangoni ikalia. Haraka akajipangusa machozi na kuelekea mlangoni.Alikuwa ni baba yake mzee Kibaho aliyetoka kuvinjari mitaa ya jiji hili la Kigali
“Ouh Dady..!!” akasema Happy na kumkumbatia baba yake.
“I missed you dady” akasema Happy.Baba yake akamtazama kwa makini usoni
“Ulikuwa unalia? akauliza mzee Kibaho .Happy akakaa kimya
“Happy una tatizo gani? Siku zote nimekuwa nikikwambia kwamba kama una tatizo lolote usisite kuniambia”
“Ni kweli baba nilikuwa nalia lakini machozi ya furaha.
“Machozi ya furaha?
“Ndiyo baba”
“Umefurahi nini leo?
“Dady kwanza kabisa napenda sana nikushukuru kwa upendo wako mkubwa kwangu.Dady umekuwa nami katika matatizo yangu.Hujawahi kuniacha hata sekunde moja toka nilipoanza kuandamwa na matatizo.You are the best dady in the whole world.I’m proud to be your daughter.” Akasema Happy na kumfanya mzee Kibaho atabasamu
“dady umekuwa nami hata katika nyakati zile ambazo hakuna mwingine aliyethubutu.Kazi uliyoifanya ni kubwa na ninadhani ni wakati wako sasa wa kupumzika”
“Happy unazidi kunichanganya.Hata siku moja sijawahi kuchoka wala sintachoka kuwa nawe kwani ni jukumu langu kuhakikisha kwamba siku zote binti zangu wanakuwa na furaha.”
“Nafahamu hilo dady na ndiyo maana nasema kwamba wewe ni baba wa kutiliwa mfano duniani.Nimesema kwamba ni wakati wako wa kupumzika kwa sababu nimeamua kuondoka Kigali
“Unaondoka Kigali? Mzee Kibaho akashangaa
“Ndiyo dady.Kigali ni mji mzuri na ninapapenda sana na ningependa kama maisha yangu yote yaliyobaki ningeishi hapa lakini kuwepo kwangu hapa kutaendelea kunikumbusha tukio lile.Baada ya kufikiri sana nimeamua ili niweze kulisahau kabisa tukio lile basi niende kuishi mbali na nyumbani,mahala ambako sifahamiki na sintaweza kukutana na mtu yeyote anayenifahamu.Nataka niyaanze maisha yangu mapya.Nataka nisahau yale yote yaliyonipata japokuwa najua si kazi rahisi lakini nitajilazimisha kufanya hivyo .Maisha yangu mapya nataka kwenda kuyaanza mbali kabisa mahala ambako ni familia yangu pekee watapafahamu”
“Happy nashukuru sana kwa maamuzi hayo.Siku zote hilo limekuwa ni wazo langu kwamba ukaanze maisha mbali kabisa na nyumbani ikiwezekana nje ya afrika.Ni wapi umefikiria kwenda ili tuanze mchakato wa Safari.?
“Ouh dady.Huna haja ya kusumbuka.Tayari nimekwisha pata msaada .Nitakwenda kuishi Marekani”
“marekani?
“Ndiyo baba”
“marekani yuko Mike na ukumbuke bado atakuwa na hasira kwa mambo yaliyomtokea Tanzania.Nina wasi wasi anaweza akakufanyia kitu kibaya cha kulipiza kisasi”
“hapana baba.Huwezi kuamini kwamba Mike ndiye anayenisaidia mimi katika mchakato huu wa kurejea Marekani”
“Happy…!!!!” akastuka mzee Kibaho
“Usiogope baba.Tayari nimekwisha ongea naye na ameniahidi kunisaidia.”
Mzee Kibaho akamtazama mwanae kwa makini na kusema
“Do you trust him?
“Yes dady ! I trust him.Mike ananipenda sana na hawezi kukataa kunisaidia”
“Najua Mike bado anakupenda na anaweza kuwa amekubali kukusaidia kwa matumaini kwamba mtarejesha mahusiano yenu.Naomba nisikie toka kwako je bado unampenda Mike na uko tayari kurudana naye?Vipi kuhusu Patrick?..akauliza mzee Kibaho.Haoppy akafikiri kidogo na kusema
“I don’t know dady… I real don’t know what going to happen there.Kuhusu Patrick I think its right time now that I let him go.Matatizo niliyoyapata katika kipindi hiki kifupi nilichokutana naye yametosha na sintaweza kuvumilia zaidi.Dady nimekuwa ni mtu wa kulia kila siku kutokana na majanga yasiyokwisha.Inauma kusema lakini ni ukweli ulio wazi kwamba mimi na Patrick hatuwezi kuwa pamoja tena.NI vyema kama tutatengana kwa sasa.Ninaumia sana kwa kuamua kuondoka na kumuacha Patrick gerezani kwa kosa nililolisababisha mimi lakini sina namna ya kufanya siwezi tena kurejea Tanzania.Nina hakika Savanna atahakikisha kamba hafungwi gerezani.Savanna amenihakikishia kwamba Patrick atakuwa huru na ataendelea na maisha yake.Patrick told me to put a trust in her and I trust her. It hurt so much dady.All these years I’ve been dreaming that some day I’ll be married to Patrick but now I have to forget him.”” akasema Happy huku machozi yakimtoka.Kikapita kimya kirefu mzee Kibaho akasema
“Nakubaliana nawe Happy ni kweli yawezekana wewe na Patrick haikupangwa muwe pamoja.Ni vyema kama utakwenda kuishi mbali naye na kujitahidi kumsahau.Vipi kuhusu wale wanaharamu waliokufanyia udhalilishaji ule? Uko tayari kuliongelea suala hilo kwa sasa?
“No dady .I’m not ready.Thats the part of my life I’m trying to forget”
“Ok Happy usijali.Utaliongelea suala hilo pale utakapokuwa tayari”
Happy akainuka pale alipokuwa amekaa akaenda dirishani akatazama nje kisha akasema
“I’ll never be ok without Patrick.But then I have to live my life without him.It hurt so much dady……” Happy akashindwa kujizuia akazidi kulia
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 51
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“No dady .I’m not ready.Thats the part of my life I’m trying to forget”
“Ok Happy usijali.Utaliongelea suala hilo pale utakapokuwa tayari”
Happy akainuka pale alipokuwa amekaa akaenda dirishani akatazama nje kisha akasema
“I’ll never be ok without Patrick.But then I have to live my life without him.It hurt so much dady……” Happy akashindwa kujizuia akazidi kulia

ENDELEA………………..

Tayari kiza kimetanda jijini Dar es salaam,ndani ya mkahawa mmoja maarufu sana jijini Dar es salaam,watu watatu,wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa wameizunguka meza iliyokuwa imesheni vinywaji vikali
Mwanamke mmoja aliyekuwa na sigara mkononi akapuliza moshi mwingi hewani na kusema
“Khumalo tumekuja kama ulivyotutaka tuonane jioni ya leo” akasema Yule mwananmke na kuchukua glasi yake ya mvingo akapiga funda kubwa.Khumalo akawatazama wanawake wale kisha akasema
“Loniki na Linah ,nimewaiteni hapa ili kuwapeni taarifa ya maendeleo kuhusiana na kazi mliyonikabidhi.Kama mnavyokumbuka ,makubaliano yetu yalikuwa ni kuwashughulikia watu wawili waliohusika katika kifo cha ndugu yenu,.Watu hawa ni Patrick na Happy.Kwa mujibu wa Loniki ulitaka watu hawa wauawe lakini nilikushauri kwamba suala la kuua mmoja wao kati ya Hapy au Patrick kwa wakati huu lingeweza kuleta utata mkubwa na lingeonekana kabisa ni tukio la kulipiza kisasi.Nashukuru mlikubaliana na ushauri wangu na na kazi ya kwanza ikafanyika. Happy alishughulikiwa na nyote mkishuhudia.Ninathubutu kusema kwamba tulifanikiwa sana lengo letu kwa Happy kwani toka picha zile na video kutolewa Happy amepotea na hajulikani alipo.Vijana wangu wamekuwa wakimtafuta lakini hakuna anayefahamu mahala alipo.Kuna tetesi vile vile kwamba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu lakini hakuna aliyepatikana kulithibitisha hilo kwani hospitali ile aliyotibiwa wamegoma kata kata kuthibitisha taarifa hizo.Kuhusu Patrick tulifanikiwa kumpekekea picha za Happy na alipoziona nusura apandwe na uchizi.Nina hakika kwamba tumefanikiwa kuyavunja mahusiano ya watu hawa na hivi sasa watu hawa wote wawili watakuwa katika mateso makubwa sana.Happy akiteseka kwa picha zile na Patrick akiteseka kwa kumuona mpenzi wake akifanya jambo kama lile. Jana usiku nilipokea simu toka kwa Linah akiniambia kwamba Loniki bado hajaridhishwa na jambo tulilolifanya na anataka Patrick na Happy wauawe.” Khumalo akanyamaza kidogo akanywa mvinyo na kuendelea
“Loniki naomba niwe wazi kwako kwamba suala la kumuua Patrick kwa sasa limekuwa gumu kidogo kwa sababu ulinzi umeimarishwa sana pale gerezani toka alipopelekewa picha zile za Happy na akazua tafrani kubwa.Kwa sasa wanaoruhusiwa kuonana naye ni mawakili na familia yake tu.Ninashauri kwamba suala hili la kumuua Patrick au tulivutie subira kwanza ili tuweze kutafuta namna bora kabisa ya kuweza kuutekeleza mpango huu.Endapo tutataka kulazimisha jambo hili linaweza kutuletea matatizo”
Kauli ile ya Khumalo haikuonekena kumfurahisha Loniki
“Ouh gosh..!!” akasema Loniki na kukaa kimya
“Mbona umestuka Lonny? Akauliza Khumalo
“Damn you Khumalo ! laiti ungejua ni namna gani ninavyosubiri usiku na mchana kuona watu hawa wakifutika toka katika uso wa dunia usingetamka maneno hayo uliyoyatamka”
“Nahafahamu Loniki,lakini naomba ufahamu kwamba mimi ndiye uliyenikabidhi kazi na ndiye ninayefahamu ugumu wa kazi yenyewe.Hii si kazi ya kuiendea haraka.”
“Khumalo naomba usianze kuniletea hadithi zako.I’ve paid you a lot of money for this job ,so do your job..I want Patrick and Savanna dead !! ..” akasema Loniki kwa ukali.Khumalo akamtazama,akainua glasi na kupiga funda moja na kusema
“Lonny,naomba ufahamu kwamba nilikubali kuifanya kazi hii kwa heshima ya Linah.Naomba vile vile ufahamu kwamba kazi hii nimeifanya kama msaada tu kwa sababu kazi kama hii mimi huifanya kwa milioni mia mbili na zaidi.Nimekwambia haya yote ili ufahamu kwamba sijaifanya kazi hii kwa pesa. Na endapo ukihitaji fedha zako unaweza ukaniambia nikakurejeshea na ukatafuta watu wengine wa kukufanyia kazi yako” akasema Khumalo.
“Jamani naomba tusifike huko.Loniki naomba umsikilize Khumalo anavyosema.Ushauri wake mimi binafsi naona ni mzuri tu.Tujipe muda ili tuweze kujipanga vizuri zaidi kwani hata kazi iliyofanyika ni kubwa na inatia matumaini.Patrick na Happy wote kwa pamoja wameumia sana na nina hakika hawatakuwa pamoja tena “ akasema Linah
“ Linah hujui ni namna gani nilivyokuwa nahitaji kuona Patrick na Happy wameuawa kabla sijarejea London.Kamwe moyo wangu hautakuwa na amani kumuona Patrick akiendelea kuvuta hewa hii safi wakati mdogo wangu akioza kaburini”
“Usihofu Lonny.Hata kama hautakuwepo mimi nitakuwepo kuusimamia mpango huu.Unaweza ukawa Uingereza lakini tukafanya kila kitu sisi tuliobaki huku.Ninakuahidi mimi binafsi nitashirikiana na Khumalo kwamba nitahakikisha lazima Patrick na Happy wanauwa na tunalipa kisasi kwa kifo cha Vero “ akasema Linah na kauli ile ikampa moyo Loniki na kumfanya akubaliane naye japo kwa shingo upande.

MIEZI SITA

Ni siku iliyotawaliwa na kijua kikali kama ilivyo kawaida ya jiji la Dar.Pilika pilika katika jiji hili lenye shughuli nyingi ziliendelea kama kawaida.Katika mahakama ya kisutu kulikuwa na idadi kubwa ya watu tofauti na ilivyozoeleka.Ongezeko hili wa watu lilitokana na minong’ono iliyokuwa imeanza kusambaa kwamba huenda Patrick ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia,angepatiwa dhamana siku ya leo baada ya taratibu zote kukamilika.Kwa muda wa miezi sita sasa toka Patrick alipoanza kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha mauaji,kesi hii imekuwa ikipewa umuhimu mkubwa sana na vyombo vya habari na hasa kutokana na miss Tanzania Happy Kibaho kutajwa kuhusika katika ugomvi uliosababisha kifo cha Vero.Kutokana na kutangazwa sana na vyombo vya habari watu wengi walikuwa wanaifuatilia ili kujua nini hatima yake.
Wengi wa watu waliofika walitegemea kumuona miss Tanzania aliyevua taji lake Happy Kibaho akiwa mahakamani.Toka picha na video yake ya utupu kuchapishwa na kusambaa mtandaoni Happy alipotea ghafla na hakuna aliyefahamu mahala alipo hivyo wengi walitegemea pengine angeweza kuonekana mahakamani siku ya leo.
Hatimaye kama ilivyokuwa imetegemewa na wengi,saa saba za mchana Patrick alipatiwa dhamana baada ya masharti yote yanayohitajika kutimizwa.Kilikuwa ni kipindi cha furaha sana hasa kwa familia yake,ndugu jamaa na marafiki.Ilikuwa ni kama ndoto pale Patrick aliposhikwa mkono na Savanna na kuthibitishiwa kwamba yuko huru kuondoka.Hakuamini macho yake.
“Savanna thank you very much.” Hilo ndilo neno pekee aliloweza kulitamka Patrick kwa wakili huyu mahiri ambaye amekuwa akimtetea katika kesi hii.Patrick akasalimiana pia na mawakili wengine ambao kwa pamoja wanaunda jopo la mawakili wanaomtetea na kisha taratibu huku akiwa ameongozana na Savanna wakatoka nje ya jengo la mahakama ambako aliendelea kusalimiana na watu mbali mbali mbali waliofika mahakamani.Wakati akiendelea kusalimiana na watu mbali mbali ,ghafla akastuka baada ya kuiona sura yenye tabasamu ya mwanadada mrembo na kuufanya moyo wake kuanza kudunda kwa kasi.Alikuwa anatazamana na Sarah dada yake Vero.Kwa sura Sarah na Vero walikuwa wanafanana sana kiasi kwamba ungeweza kudhani ni mapacha
Sarah ambaye alikuwa anatabasamu na kumkumbusha Patrick lile tabasamu alilolizoea la Vero akamsogelea na kumkumbatia.
“Pole sana Patrick.Usijali Mungu atakusaidia na mambo haya yatakwisha.” Akasema Sarah na kumshangaza sana Patrick ambaye alikosa neno la kusema midomo yake ilikuwa inamtetemeka.Hakutegema kama Sarah angeweza kuongea naye kistaarabu namna ile hasa baada ya kusababisha kifo cha mdogo wake.
“Sarah nashukuru sana” Patrick akasema.Sarah akatabasamu na kusema
“Patrick tutaongea siku nyingine kwa sasa unahitaji mapumziko.” Akasema Sarah halafu wakaagana akaondoka zake.Baada ya Patrick kusalimiana na watu wengi waliokuja kumpa pole siku hii ya leo,Savanna akamshika mkono na kumuongoza hadi katika gari lake na ndugu wengine nao wakaingia katika magari yao na kuondoka pale mahakamani.Patrick alikuwa amegeuza shingo yake akiangalia nje na mara akavuta pumzi ndefu
“Ouh my gosh ..!!! “ akasema Patrick akionekana kustushwa na kitu Fulani
“Patrick whats wrong? Akauliza Savanna
“Bado naona ni kama muujiza vile leo nimerejea tena uraiani.Sipati neno la kukushukuru Savanna.Ni Mungu pekee ndiye atakayekulipa” akasema Patrick
“Ouh Patrick plase don’t say anything.Ni wajibu wangu kufanya hivi na huna sababu ya kunishukuru” akasema Savanna huku akitabasamu
“Unanipeleka wapi,nyumbani kwangu au kwa mama? Akauliza Parick
“Patrick ,haitakua vizuri kama ukienda nyumbani kwako kwa sasa.Nyumba ile ina kumbukumbu nyingi ambazo zitakukumbusha historia ya wewe na Vero ambayo unajitahidi kuisahau.Nyumbani kwa mama nako kuna kumbukumbu nyingi ambazo zitakukumbusha kuhusu baba.Unatakiwa kwanza kuwa tayari kukabiliana na hayo yote.Nashauri kwanza upate mapumziko halafu tutakwenda nyumbani kwa mama lakini kwa sasa utakwenda kuishi kwangu .Nimekuandalia chumba maalum.Pale utapata kila kitu unachokihitaji hadi hapo utakapojisikia kuwa tayari kurejea kwako” akasema Savanna.Patrick akatabasamu
“Nilipenda sana kufika nyumbani kwa mama siku ya leo.Najua hata yeye pia ana hamu kubwa ya kuniona”
“Nyumbani kwa mama utakwenda lakini kwanza unatakiwa ukaoge,upate chakula,upumzike kidogo halafu ndipo uwe tayari kuonana na mama”
“Ok Savanna.Wewe ndiye kiongozi wangu kwa sasa.Siwezi kukupinga kwa lolote” akasema Patrick huku akicheka na kumfanya Savanna naye acheke
“Simu hii hapa mpigie Alois na umtaarifu kwamba utakwenda nyumbani kwa mama jioni ya leo” akasema Savanna.Patrick akaichukua simu ile na kumpigia Alois akamtaarifu kwamba atakwenda kuonana nao jioni.

* * * *

Geti la rangi nyeupe likafunguliwa na gari aina ya Range rover vogue likaingia katika jumba la kifahari lenye rangi nyeupe.Milango ikafunguliwa akashuka Savanna na Patrick
“Karibu nyumbani Patrick” akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna.Una nyumba nzuri sana” akasema Patrick huku akitabasamu.Waliingia ndani ya sebule kubwa
“Jisikie nyumbani Patrick” akasema Savanna
“Nashukuru sana Savanna.Nyumba yako nzuri mno” akasema Patrick huku akitabasamu.Mtumishi wa ndani akafika na kuwahudumia vinywaji.
Baada ya maongezi kidogo,Savanna akampeleka Patrick katika chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajili yake
“Patrick, hiki ndicho chumba chako.Nimekiandaa maalum kwa ajili yako..Utaishi hapa hadi hapo utakapojisikia kurejea katika makazi yako.Nimejaribu kuweka karibu kila kitu unachokipenda.Katika kabati kuna nguo nilizokuandalia na sina hakika kama nimekosea vipimo” akasema Savanna na wote wakacheka halafu Savanna akamuacha Patrick na kwenda chumbani kwake .
Patrick aliingia bafuni na kabla ya kuoga akasimama kwanza na kuzama katika mawazo
“Hatimaye nimekuwa huru tena.Naona ni kama ndoto lakini huu ndio ukweli nimerudi tena nyumbani baada ya kusota gerezani kwa muda wa miezi sita.Ama kweli maisha yanaweza kubadilika ndani ya sekunde moja kama yalivyobadilika kwangu.Sikuwahi kuota kma maisha yangu yangebadilika namna hii” akawaza Patrick na mara sura ya Vero ikamjia kichwani
“Sura hii ya Vero itaendela kuniandama kwa muda mrefu sana na kuifuta sura hii kichwani kwangu itanichukau muda pia” akawaza Patrick
Baada ya kuoga akajumuika na Savanna wakapata chakula pamoja halafu akarejea chumbani kwake kupumzika.
“Ni muda mrefu sijalala katika sehemu nzuri kama hii.I missed this life a lot.Shukrani za pekee zimwendee Savanna ambaye amepambana na kuhakikisha ninapata dhamana.Savanna ni mwanamke wa shoka.Nina deni kubwa kwake.Amenionyesha kwamba yeye ni rafiki wa kweli kuliko hata wale niliowaamini kwa moyo wangu wote.Ni Mungu peke atakaye mlipa Savanna kwa wema wake huu mkubwa” akawaza Patrick
“Kwa sasa natakiwa kujipanga kwa ajili ya kuanza upya maisha yangu.Nimepoteza kila kitu.Nimepoteza kazi,nimewapoteza wapendwa wangu Vero na Happy , hata Andrew rafiki yangu mkubwa naye ameniacha na sina taarifa zake tena. Sijilaumu sana kwa kilichotokea bali napaswa kutuliza akili na kujipanga upya.Bado sijachelewa kuyapanga na kuyajenga upya maisha yangu bila ya wale niliowapenda .Tukio lililotokea limenifundisha mambo mengi sana na safari hii sitaki kurudia makosa.Nakiri nilifanya kosa kubwa kuachana na Vero.Sikupaswa kufanya vile.Vero alikuwa ni mwanamke aliyenipenda kwa moyo wake wote na siku zote alikuwa tayari kwa lolote kwa ajili yangu.Nilimpuuza,nikaupuuza upendo wake kwangu na kuamini kwamba Happy ndiye mwanamke ambaye nimepangiwa niwe naye katika maisha.Nilijidanganya sana.Mimi na Happy katu hatuwezi kuwa pamoja.Tumekwisha jaribu na imeshindikana na tayari nimemfahamu Happy ni nani.Nashukuru nimeweza kumuondoa moyoni mwangu na amebaki ni katika historia ya maisha yangu lakini moyo wangu haudundi tena kwa ajili yake.Alichokifanya kimenifanya nimvue thamani kabisa na hana nafasi tena moyoni mwangu” Akawaza Patrick halafu akafumba macho na kulala
Saa moja za jioni akiwa ameongozana na Savanna akawasili nyumbani kwa wazazi wake ambako baadhi ya ndugu walikuwa wamekusanyika ili kumpa pole kwa masahibu yaliyomkuta.Wote walijawa na furaha kubwa kwa Patrick kurejea tena nyumbani.Chakula kizuri kiliandaliwa,wakala na kunywa na ilipofika saa tano za usiku Patrick na Savanna wakaondoka kurejea nyumbani kwa Savanna ambako Patrick aliwekewa makazi yake ya muda

* * * *

Saa nne za asubuhi siku iliyofuata iliwakuta Patrick na familia yake katika kaburi la baba yao.Alois ndiye aliyeongoza sala fupi ya kumuombea marehemu baba yao halafu ukafuata wakati wa kuweka shada za maua.Patrick aliyekuwa amevalia suti nyeusi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuweka shada la maua juu ya kaburi la baba yake.Akaliweka karibu kabisa na msalaba halafu akapiga magoti na kuliinamia kaburi
“Baba kokote uliko hivi sasa naomba unisamehe sana kwa mambo niliyoyafanya na kusababisha kifo chako.Sikutegemea kama maamuzi yangu yangetufikisha hapa.Ninasikia uchungu mkubwa sana ambao si rahisi kuuelezea.Baba nahitaji msamaha wako ili niweze kuondokana na mateso haya makubwa niliyonayo na nianze maisha mapya.Siku zote nitakuombea kwa Mungu ili aipumzishe roho yako mahala pema peponi Amina”
Baada ya kumaliza maombi yale mafupi ya kimya kimya akainuka na kuwapa nafasi ndugu zake wengine nao waweke shada zao za maua.Zoezi lile lilipokamilika Patrick na Savanna wakaingia garini na kuondoka kuendelea na ratiba nyingine ya siku hiyo.
“Kinachofuata sasa hivi kwa mujibu ratiba yetu tunaelekea katika kaburi la Vero” akasema Savanna
Walifika makaburini na Savanna akamuongoza Patrick hadi katika kaburi la Vero.
Hapa ndipo alipozikwa Vero” akasema Savanna.Patrick akaweka shada lake la maua na kuliinamia kaburi na machozi mengi yakamtoka.Savanna akasogea mbali kidogo na kumpa Patrick nafasi ya kuwa peke yake katika kaburi la aliyewahi kuwa mchumba wake.
“Anatia huruma sana Parick lakini hii ndiyo hali halisi ambayo lazima akabiliane nayo.” Akawaza Savanna
Baada ya dakika kumi za Parick kuliinamia kaburi la Vero akainuka.Macho yake yalikuwa mekundu na uso wake ulijaa machozi.Savanna akamsogelea na kumpa kitambaa
“its ok Patrick,Don’t cry anymore” akasema Savanna Patrick akafuta machozi.Akaendelea kulitazama kaburi lile kwa uchungu
“rest in peace Vero.You’ll always be in my heart” akasema Patrick halafu wakaondoka .

Toka makaburini ,Patrck na Savanna wakaendelea na safari yao hadi nyumbani kwa Patrick.Walinzi toka katika kampuni binafsi ya ulinzi ya Chem Chem security waliendelea kuilinda nyumba ya Patrick kwa kipindi chote ambacho Patrick alikuwa gerezani
“Welcome home Patrick” akasema Savanna huku akitabasamu.Patrick alishindwa kuzuia furaha yake alipoishuhudia nyumba yake namna ilivyokuwa imependeza.Ilikuwa imepakwa rangi nzuri nyeupe na kupandwa maua mengi kuizunguka.
“wow !! its incredible…!!!” akasema Patrick kwa furaha
“Nyumba yote ni salama.Imeendelea kulindwa na kampuni hii ya ulinzi kwa kipindi chote ulichokuwa gerezani.Niliingia nao mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuilinda nyumba yako na tayari fedha zote nimekwisha zilipa.Vile vile nyumba yote imepakwa rangi kwa nje.It looks beautiful,isn’t it?
“Savanna sijui hata niseme nini.Sijui nikushukuruje.The house looks so beautiful.Sikutegemea kama ningeikuta nyumba yangu katika hali hii.Ahsante sana Savanna kwa kunitunzia nyumba yangu.” Akasema kwa furaha Patrick na kuufungua mlango mkubwa akaingia ndani.Patrick alionekana kama anaiogopa nyumba yake.Hakutaka kugusa kitu chochote mle sebuleni.Walitoka sebuleni wakazunguka katika baadhi ya vyumba na hatimaye wakaingia katika chumba cha kulala cha Patrick.Mara tu walipoingia Patrick akastuka sana baada ya kuziona picha mbili kubwa zilizowekwa ukutani.Ilikuwa ni picha yake na Veronika.Alisimama kwa sekunde kadhaa akizikodolea macho picha zile kubwa
Juu ya kitanda kulikuwa na nguo za vero ambazo alizivua na kuziweka kitandani mchana wa siku ile ya kufariki kwake.Patrick akakumbuka dakika za mwisho akiwa na Vero mle chumbani.Vero alikuwa akimkumbatia kwa mahaba mazito.Alikumbuka namna walivyofanya mapenzi kwa mara ya mwisho na walipanga kuendelea tena jioni yake lakini Vero hakurejea tena katika chumba kile
“That’s the day I’ll never forget in my life.It’s the day that I made the biggest mistake of my life.Niliipoteza dhahabu ya thamani kubwa kwa mng’ao wa jiwe” akawaza Patrick huku machozi yakimlenga
“Savanna I need to be alone for a while” akasema Patrick na Savanna akatoka mle chumbani,Patrick akaufunga mlango halafu akapanda kitandani na kuzikumbatia nguo za Vero huku akilia
“Please forgive me Vero,forgive me“ akasema Patrick huku machozi yakimtoka.Alilia sana kisha akainuka na kwenda katika meza ya vipodozi iliyokuwa imesheni vipodozi vya kila aina alivyokuwa anatumia Vero.Akalifungua kabati kubwa na kuzikuta nguo nyingi za Vero ,akaanza kuitoa nguo moja baada ya nyingine na kuziweka kitandani.Kila nguo aliyoishika ilimkumbusha nyakati zile za furaha alizokuwa nazo akiwa na Vero.Alivikusanya vitu vyote vya Vero na kuviweka katika masanduku mawili makubwa
“Natakiwa kuvirudisha vitu hivi kwa ndugu zake.Kuendelea kuviweka hapa vitanifanya nishindwe kumsahau Vero na kuendelea na maisha yangu.Nitamtafuta Sarah na kumpatia vitu hivi vya mdogo wake” akawaza Patrick
“Itanichukua muda mrefu kurejea tena katika nyumba hii.Kwa sasa itanilazimu kuendelea kuishi nyumbani kwa Savanna.Ninahisi furaha na amini nikiwa pale.Savanna ananijali sana na anajitahidi kwa kila namna niweze kurejea katika maisha yangu ya kawaida.She’s a wonderfull woman” Patrick akatabasamu halafu akatoka na kuelekea sebuleni aliko Savanna.
“Savanna itanichukua muda sana kuweza kumsahau Vero .Kuna kumbu kumbu nyingi humu ndani zinazonikumbusha mbali na hasa dakika za mwisho nilizokuwa na Vero.Laiti ningejua kama ile ilikuwa ni siku ya mwisho ya Vero basi nisingefanya vile nilivyofanya.” Akasema Patrick
“Pole Patrick.Mambo haya yote yatakwisha japokuwa ni ngumu na itachukua muda kumsahau Vero lakini naomba ujitahidi kwa kila namna kuizoea hali hii na kuiona ya kawaida”
“Nitajitahidi Savanna.I’ll be ok” akasema Patrick halafu wakazungukia nyumba yake yote na walipomaliza wakaingia garini na kuondoka kurejea katika makazi ya Savanna
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 52
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT : 0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Pole Patrick.Mambo haya yote yatakwisha japokuwa ni ngumu na itachukua muda kumsahau Vero lakini naomba ujitahidi kwa kila namna kuizoea hali hii na kuiona ya kawaida”
“Nitajitahidi Savanna.I’ll be ok” akasema Patrick halafu wakazungukia nyumba yake yote na walipomaliza wakaingia garini na kuondoka kurejea katika makazi ya Savanna

ENDELEA……………..

Siku zilizidi kusonga huku Patrick akijitahidi kujaribu kusahau mambo yote ya nyuma na kuanza maisha mapya.Bado aliendelea kuishi nyumbani kwa Savanna.Maisha ndani ya nyumba hii yalikuwa mazuri,aliishi yeye,Savanna pamoja na mtumishi wa ndani,.
Siku moja mwishoni mwa wiki Savanna alimuomba Patrick watoke kwa ajili ya matembezi.Walikwenda katika hoteli moja kubwa na tulivu iliyokuwa na ufukwe mzuri na msafi.Savanna alikuwa amejitahidi sana kwa kila namna alivyoweza ili kumsahaulisha Patrick yaliyopita na kumfanya awe na furaha lakini bado alionekana kuna jambo linamnyima raha.
“Patrick ni jambo gani hasa linalokunyima raha? Tafadhani naomba unieleze .Mimi ni rafiki yako na kama kuna jambo lolote ambalio linakufanya usie na furaha naomba unieleze mimi nitakusaidia.” Akasema Savanna wakiwa ufukweni.
“Savanna wewe ni zaidi ya rafiki yangu kwa hiyo siwezi kukuficha kitu.Kitu kinachoninyima raha ni pale ninapowaza kuhusu maisha yangu.Kama unavyojua nimepoteza kila kitu pamoja na mwelekeo mzima wa maisha yangu.Nimepoteza kazi yangu na mpaka sasa hakuna hata kampuni moja iliyoonyesha dalili za kuniajiri tena.Ninajiona kama nina laana vile lakini hata hivyo nahitaji kusahau kilichotokea na kuanza maisha mapya lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda najikuta nikishindwa namna ya kuweza kuanza tena maisha yangu na kujitegemea mimi mwenyewe.Sijisikii vizuri ninapokutegemea wewe katika kila jambo”
Savanna akatabasamu na kusema
“Pole Patrick lakini hukupaswa kuumiza kichwa chako namna hiyo.Ulipaswa kunieleza kuhusu jambo hilo kwani tayari ninalifahamu hilo na nina mipango mizuri kwa ajili yako ila sikuweza kukueleza mapema kwa sababu nilikuwa nataka nikwambie wakati kila kitu kimekamilika.Kwa ufupi tu ni kwamba nimeanzisha kiwanda cha kusindika nyama na muda wowote kuanzia sasa kitaanza kazi.Wewe ndiye utakayekuwa meneja wa kiwanda hicho.
.majukumu yote ya uendeshaji wa kiwanda hiki yako juu yako kwa hiyo usiumize kichwa chako kuhusiana na ajira,you are a manager now.” Akasema Savanna huku akicheka.Patrick akashindwa kujizuia akasimama akamkumbatia Savanna kwa furaha.
“Savanna ni kitu gani nimekufanyia hadi ukanifanyia mambo yote haya? Nitakulipa kitu gani? Patrick akasema huku akimtazama Savanna
“Ni wajibu wangu kufanya hivi nifanyavyo Patrick na hutakiwi kunilipa chochote .Nina imani hata mimi ningekuwa katika hali kama yako ungefanya kama nifanyavyo mimi.Isnt it Patrick?
“Ndiyo Savanna .Ningefanya kama ufanyavyo.Nisingethubutu kukuona ukiwa katika hali kama yangu.Naomba nikiri kwamba ni hali ngumu sana lakini nimeweza kuvumilia na kufika hapa kutokana na jitihada za watu wachache wanaonuipenda na kunijali wakiongozwa na wewe Savanna ,watu ambao wamesimama nami toka dakika ya kwanza ya matatizo yangu na hadi leo bado wako nami.Nina deni kubwa kwako Savanna na sijui nitalilipaje.” akasema Patrick halafu akainamisha kichwa chini akazama katika mawazo ghafla.
“Patrick unawaza nini? Akauliza Savanna baada ya kumuona Patrick amebadilika ghafla
“Savanna nimekumbuka kesi yangu.Kila mara niwazapo kuhusu kesi hii ninashindwa kujizuia kuogopa.Ninafikiria itakuwaje endapo nitahukumiwa kifungo gerezani na kushindwa kutimiza malengo yangu.Sitaki kufungwa jela kwa sababu ya mtu asiyekuwa na thamani kwangu hata kidogo.”
“Patrick siku zote nimekuwa nikikwambia kwamba usiwaze chochote kuhusiana na kesi hii. Mambo yote niachie mimi na nitalishughulikia suala hili na litakwisha.I give you my word Patrick” akasema Savanna huku akitabasamu .Kikapita kimya cha dakika mbili kila mmoja akiwaza lake
“Patrick ..!! akaita Savanna.Patrick akamtazama usoni
“Kuna jambo ambalo nataka kukueleza”
“Jambo gani Savanna?
“Patrick najua ni namna gani unavyoumia kila siku moyoni kwa haya yaliyotokea.Ninayaona maumivu yako na kuyahisi na kunifanya na mimi pia niumwe kwa kukuona ukiwa katika hali hii ya mateso makubwa ya moyo.Patrick nafahamu kwamba si rahisi kuyasahau yaliyotokea na kuanza maisha mapya kwa haraka.Itachukua muda kuwasahau wapendwa wako,vero,Happy na baba yako.Hawa ni watu uliowazoea na kuwapenda lakini leo hii hawako tena nawe.Pamoja na kwamba kumbu kumbu zao bado zinakujia ,lakini ni wakati sasa wa kuwaacha waende na wewe uuruhusu moyo wako uanze maisha mapya.Its time now to let them go.Kuondoka kwao si mwisho wa maisha yako wala ndoto zako .Bado unayo maisha marefu na yenye furaha lakini pale tu utakapoufungua moyo wako na kuuruhusu uanze maisha mapya.Ufungue moyo wako sasa kwa wale wanaokupenda na kukujali na kuwa tayari kusimama nawe katika nyakati zote za shida au raha.Pamoja na yaliyotokea lakini bado unahitaji kuwa na marafiki na hata mtu ambaye unaweza tena kumwamini na kumkabidhi moyo wako.” Akasema Savanna.Patrick akamuangalia kwa makini halafu akatabasamu na kusema
“Unamaanisha nini Savanna unaposema mtu ambaye ninaweza kumwamini na kumkabidhi moyo wangu?
“Ninamaanisha kwamba you have to learn to love again.Only love can help you forget the past” Akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu na kucheka kidogo
“Mbona unacheka Patrick? Ni kosa la jinai kupenda? Akauliza Savanna
“Si kosa la jinai lakini…………………………”
“ Lakini ……………? Akauliza Savanna
“Sina hakaika kama moyo wangu uko tayari kupenda tena Savanna.Kidonda nilichonacho moyoni kilichosababishwa na mapenzi kitachukua muda mrefu kupona..Nimeumizwa sana na pengine sintaweza kupenda tena.Pengine nitaishi maisha yangu yote yaliyobakia nikiwa mwenyewe.Sintavumilia tena maumivu yoyote ya kuumizwa.Kuna watu katika dunia hii hawajaumbwa ili kupenda na ninaamini mimi ni mmoja wao” akasema Patrick katika hali ya kukata tamaa kabisa
“Patrick nafahamu ni namna gani ulivyoumizwa. Sisi sote tunaumizwa na mapenzi .Lakini mimi bado nasisitiza kwamba kuuruhus moyo wako kupenda tena kutakusaidia sana katika kusahau mambo yaliyopita.Find yourself someone who truly loves you and I swear you’ll be Happy again” akasema Savanna
“Hata kama nikiamua kupenda tena ni nani nitakayempenda? Nani ambaye nitamuamini katika ulimwengu huu wa sasa na kumkabidhi moyo wangu tena? Savanna naomba niwe wazi kwako kwamba sioni sababu ya kupenda tena kwani kila mara nilipojaribu kupenda nimeishia kuumizwa moyo wangu tu.Nilimpenda mno Happy na nilikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake,niliwahi hadi kuua kwa ajili yake lakini ona jeraha alilonitia moyoni..I’m hurt Savanna..’m deeply hurt.”Akasema Patrick.Savanna akamshika mikono na kumuangalia usoni.
“Patrick si wanawake wote ni wabaya na wanaweza kukuumiza kama ulivyoumizwa.Usiuamini ule msemo usemao samaki mmoja akioza na wote wameoza.Bado kuna wnawake wazuri ,wenye kukupenda ,kukujali na kukuthamini,wanawake ambao kwao una maana kubwa sana.Tafadhali usiufunge moyo wako kwa mwanamke kama huyu”
“Savanna hata wale niliokuwa nao Happy na Vero walinipenda kwa mioyo yao yote.Walinijali na kunithamini.Kwa ufupi ni kwamba sina tatizo na wanawake hata kidogo lakini sina uhakika wa kupenda tena kwa sababu niliwapenda kwa moyo wangu wote.Kuna nyakati ninahisi kama dunia inaniadhibu.The world has been so cruel to me so even if I’ll start a new relationship it wont work out and I’ll get hurt again.Sitaki kuumia tena” akaendelea kusisitiza Patrick
“Patrick,Mungu ametuleta hapa duniani tuyafurahie maisha na ndiyo maana akaumba mwanamke na mwanaume kwa hiyo si sahihi kusema au kuamini kwamba kuna watu ambao wameshushwa katika hii dunia kwa ajili ya kuishi wao wenyewe bila kuwa na mahusiano.Kama kuna watu wa namna hiyo basi Mungu angewaumba bila kuwa na jinsia” akasema Savanna halafu wote wawili wakacheka sana.Savanna akaendelea
“Ninavyoamini mimi ni kwamba kila mtu ana haki ya kuwa katika mahusiano labda upende mwenyewe kutokujihusisha na mahusiano kama vile watawa na makasisi lakini hata hao watawa wanaishi chini ya uangalizi maalum tena mkali ili kuwasaida wasiweze kuingia katika vishawishi vya kimahusiano.Tukirudi katika swala lako lingine,si kweli kwamba dunia imekuwa katili sana kwako ,dunia si mbaya hata kidogo ,dunia inatupenda wote na ndiyo maana wote tunavuta hewa sawa,inatupa mazao na kila kitu.Binadamu waishio juu ya dunia ndiyo wabaya na kwa upande wako ni kwamba you fell I love with wrong people.People whom you’re not meant to be with” akasema Savanna,Patrick akatabasamu halafu akasema
“Maneno yako yanaweza kuwa na ukweli Savanna kwa sababu kuna usemi usemao kwamba kila jambo linafanyika kwa sababu maalum.Inawezekana ni kweli nilipenda watu ambao hawakuwa sahihi kwangu.Hata hivyo nahitaji kulifikiri tena suala hili kabla ya kuamua kuingia katika mahusiano mengine na nina hakika inaweza ikanichukua muda mrefu sana.Kwa sasa nataka nielekeze nguv na akili yangu katika kazi yangu mpya” akasema Patrick
“Hilo ni jambo la msingi sana Patrick.Hutakiwi kuidhulumu nafsi yako.You need to be Happy and to be be Happy you need to love and be loved ” Akasema Savanna .Patrick hakujibu kitu
“It’s getting late Patrick.Twende tuondoke .Leo nataka tukaandae pamoja chakula cha usiku.Unakumbuka ni muda mrefu sana umepita toka tulipoandaa kwa pamoja chakula cha usiku?” Akasema Savanna
“Wow ! That’s great Idea.Ni siku nyingi sana sijaingia jikoni kupika .Nakumbuka sana nyakati zile tulizokuwa tukiandaa chakula pamoja. “ akasema Patrick huku akicheka kidogo
“Unapenda tupike nini kwa ajili ya usiku wa leo? Akauliza Savanna
“Kitu chochote utakachopenda tupike Savanna mimi niko tayari.” Akajibu Patrick na kumfanya Savanna atabasamu
“Today we’re going to have a very special dinner just for two of us.Lets make this night a wonderful and memorable one.” Akasema Savanna kisha wakaondoka.
Kabla ya kuelekea nyumbani walipita kwanza kununua vitu mbali mbali ambavyo wangependa kuvitumia kwa ajili ya usku huo.Walipofika nyumbani,waliingia jikoni na kuanza maandalizi kwa pamoja.Kitendo cha kushirikiana kuandaa chakula kile kilimpa Patrick furaha ya ajabu sana na kumkumbusha nyakati zile wakati bado alikuwa katika mahusiano ya sirina Savanna
Mpaka kufika saa mbili za usiku,chakula kilikuwa tayari.Savanna akamuomba Patrick amuachie yeye kazi zilizobakia na yeye aende akajiandae kabla ya kupata mlo huo wa usiku wazo ambalo Patrick alilikubali na kwenda kujiandaa
“Tonight is the night .I’ve been waiting for this night for so long.Leo hii Patrick lazima awe wangu tena” akawaza Savanna huku akitabasamu baada ya Patrick kuondoka mle jikoni
“Baada ya usiku wa leo nitaamka nikiwa mikononi mwa mwanaume ninayempenda sana kuliko wote.After tonight I’ll be complete and no one than death can separate us again.Patrick will be mine forever” akawaza Savanna wakati akiandaa meza
Kwa upande wake Patrick baada ya kuingia chumbani kwake,moja kwa moja aliingia bafuni akajimwagia maji
“Namshukuru sana Savanna kwani kwa sasa najisikia vizuri na nina nguvu ya kuendelea na maisha yangu mapya. Bila yeye sijui ningekuwa katika hali gani hivi sasa” akawaza Patrick halafu akaendelea kujimwagia maji .Wakati akiendelea kuoga akakumbuka kitu halafu akatabasamu
“ Katika siku zote ambazo nimekuwa na Savanna ,siku ya leo nimejikuta nikiwa na furaha sana na hasa zoezi la kupika pamoja,zoezi ambalo limenikumbusha nyakati zile nilizokuwa naye katika mahusiano ya siri .Niliwahi kuwa katika mapenzi mazito na Savanna,nakumbuka wakati ule nilikuwa na furaha sana japokuwa nilikuwa tayari katika mahusiano na Vero.Savanna alinionyesha mapenzi ya dhati na moyo wangu ulifurahi .Nilikubali kuachana naye kwa shingo upande pale alipompata George.Kama nisingekuwa katika mahusiano na Vero kwa wakati ule basi tayari ningekuwa nimekwisha funga ndoa na Savanna kwani ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuwa mke bora .Zaidi ya yote bado ananipenda kwa dhati ya moyo wake na ndiyo maana amejitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha kwamba suala la kesi yangu linakwisha na ninakuwa huru tena.” Akawaza Patrick na kisha akaendelea kuoga
“Hata mimi toka ndani kabisa ya moyo wangu ninakiri kwamba bado ninampenda Savanna.Ninahisi yeye anaweza kuwa ndiye mwanamke anayenifaa,lakini kutokana na msaada mkubwa alionisaidia ninasita kuziamsha tena hisia za mapenzi kati yetu” akawaza Patrick halafu akaendelea kuoga.Sura ya Savanna wakiwa jikoni wakipika pamoja ikamjia kichwani akatabasamu
“She have a pretty face,macho mazuri,shepu nzuri na sauti kama malaika.Savanna ni mwanamke bora na mzuri kupita kiasi” akawaza Patrick kisha akatoka mle bafuni
Savanna aliendelea na zoezi la kuandaa meza kwa ajili ya chakula cha usiku.Alizima taa na kuwasha mishumaa na kupafanya mahala pale pawe pa kuvutia sana.Alipohakikisha kila kitu kiko sawa akaenda chumbani kwake kujiandaa kwa ajili ya usiku huo ambao aliupanga uwe maalum kwake

* * * *

“Huu ni usiku wangu wa pekee kabisa ni usiku ambao nimekuwa nikiuota kwa muda mrefu.Ni usiku ambao nitalala nikiwa kifuani kwa Patrick.” Mawazo hayakumkauka Savanna wakati akimalizia kujipaka rangi ya mdomo halafu akajitazama katika kioo na kutabasamu.Alikuwa amependeza sana.Alivaa gauni refu jepesi la rangi jeupe ambalo lilionyesha hadi nguo ya ndani.Akageuka akajitazama na kutabasamu halafu akachukua uturi wa gharama kubwa na kujipulizia kisha akatoka mle chumbani.Patrick alikuwa bado chumbani kwake wakati Savanna alipowasili sebuleni.Savanna akampigia simu na kumtaarifu kwamba muda wa kupata chakula cha usiku umewadia.
Patrick akatoka chumbani na kuelekea sebuleni.Mara tu alipoingia ,akapigwa na mshangao kwa alichokikuta.Sebule ilikuwa imebadilika na kuwa na mandhari ya kuvutia mno.Taa zote zilikuwa zimezimwa na kilichokuwa kinawaka ni mishumaa iliyopapendezesha mahala pale na kupafanya pa pekee kabisa.
“Wow ! amazing “ akasema Patrick huku akitabasamu
“karibu Patrick” akasema Savanna kwa sauti laini huku akiinuka pale sofani alipokuwa amekaa na kwenda kumshika Patrick mkono akaumuongoza kuelekea katika meza ya chakula.Japokuwa mwanga ulikuwa hafifu lakini Patrick aliweza kulishuhudia vyema vazi la Savanna na kusisimka mwili kwani aliweza kuiona hadi nguo ya ndani aliyokuwa amevaa .Mapigo ya moyo wake yakaanza kumuenda kasi.Ni muda mrefu sasa umepita hajawahi kusisimkwa mwili.Savanna na Patrick wakaangaliana kwa sekunde kadhaa Savanna akauliza
“Mbona unaniangalia hivyo Patrick?
“You are so amazing tonight” akajibu Patrick
“Thank you” akajibu Savanna kisha wakaelekea katika meza iliyokuwa imesheheni vyakula vya aina mbali mbali walivyoviandaa
“Karibu chakula Patrick,chakula ambacho ni maalum kwetu.Just for tonight let us forget the world and enjoy the night.Let us make our own world ” Akasema Savanna.
Waliendelea kula taratibu huku wakisindikizwa na muziki laini.Kila Patrick alipomtazama Savanna alisisimka mwili wake kutokana na kuzishuhuhudia chuchu za kuvutia za Savanna ambazo zilikuwa zinaonekana kwa urahisi kutokana na vazi lile alilokuwa amevaa lililoonyesha kila kitu.Taratibu akahisi mtafaruku katika sehemu za ikulu ambazo zilikuwa zimechachamaa kupita maelezo.
“Gosh ! haya ni majaribu makubwa sana.Savanna ananiweka katika wakati mgumu mn😵uh jamani nitafanya nini mimi? Akawaza Patrick huku akiendelea kumtazama Savanna ambaye alikuwa ameinamisha kichwa.Ghafla akainua kichwa na kugundua kwamba Patrick alikuwa anamuangalia akatabasamu
Baada ya kumaliza kula Savanna akamuomba Patrick waelekee katika sofa lililokuwa na meza ndogo pembeni iliyokuwa na chupa tatu za mvinyo pamoja na glasi mbili.
“Na tunywe kwa furaha huku tukitakiana maisha marefu” akasema Savanna huku akiisogelea glasi yake iliyokuwa na mvinyo karibu na Patrick wakagonganisha glasi.Waliendelea kunywa na kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo maongezi na vicheko vilivyozidi.Walikumbushana mambo mengi na hasa nyakati zile walizokuwa wapenzi,Ulikuwa ni wakati wa furaha mno kwa wote.Maongezi yalikolea na kulikuwa na kila dalili kwamba walianza kulemewa na kilevi.Savanna akainuka pale alipokuwa amekaa na kuelekea katika redio akaweka muziki laini sana halafu akamfuata Patrick
“Patrick can we dance?
Bila ubishi Patrick akainuka akakumbatiana na Savanna wakaanza kucheza.Patrick akahisi kama chaji za umeme zinapita mwilini mwake pale kifua cha Savanna kilichobeba chuchu laini kilipokigusana na kifua chake.Kadiri muziki ulivyokuwa ukienda ndivyo walivyojikuta wakikumbatiana kwa nguvu zaidi.Muziki ulimalizika lakini bado waliendelea kukumbatiana kwa nguvu .Taratibu Savanna akaupeleka mkono wake wa kulia chini kidogo ya kiuno cha Patrick na kukutana na kitu kigumu kilichotuna.Taratibu na kwa ufundi Savanna akakishika kitu kile kilichotuna na kumfanya Patrick atoe mguno na kuhema kwa nguvu kisha akampiga Savanna busu zito lililomfanya aweweseke.Taratibu Patrick akausogeza mdomo wake karibu na Savanna na kuutoa ulimi wake na zoezi la kunyonyana ndimi likaanza huku wakishikana na kutomasana sehemu mbali mbali za mwili.Wote wawili walikuwa wakihema kwa nguvu na kila mmoja akiongea maneno ambayo mwenzie hakuweza kuyaelewa.
“Ouh,Ouh,ouh Patrick take ..m.me..to ..parr….r..paradise” akasema Savanna kwa sauti yenye kukwama kwama.Alikuwa hajiwezi tena kwa raha alizozisikia.Patrick akamuinua na kwenda naye chumbani.Kilichoendelea huko ni miguno na vilio vya utamu uliopitiliza

* * * *


Mlio wa saa ya ukutani ndio uliomstua Patrick akafumbua macho na kutazama ukutani kulikokuwa na saa kubwa.Ilikuwa ni saa mbili za asubuhi.Pembeni yake alikuwa amelala Savanna akiwa katika usingizi mzito.Patrick akamtazama na kutabasamu
“Gosh ! Usiku wa jana kamwe sintausahau katika maisha yangu.Sijawahi kuwa na usiku wa kipekee kama ule.Nilijihisi kama nimetoka kabisa katika ulimwengu huu.Ouh Savanna I didn’t know how much I still love you.Umenirudishia tena furaha yangu iliyopotea.” akawaza Patrick halafu akainama na kumbusu Savanna shavuni na mara Savanna akafumbua macho.
“Ouh Patrick thank you so much.You are so sweet” akasema Savanna
“Thank you for the wonderfull night.Sijawahi kuwa na usiku mzuri kama wa jana.Nimekuwa nikiuota usiku kama ule kwa miaka mingi.Ahsante sana Patrick..Ahsante sana” akasema Savanna akamvuta tena Patrick kwake na kumpa busu zito.Patrick akatabasamu na kusema
“Savanna you are wonderfull,you are amazing.Baada ya usiku wa jana,najiona mtu mpya.Savanna naomba nitamke kwamba najiona ni kama mfalme mwenye nguvu mwenye uwezo wa kufanya chochote nikiwa nawe.Umenipa nguvu na matumaini.Siku zote nitaendelea kumshukuru Mungu kwa kunikutanisha nawe.Nina uhakika mkubwa kwamba kukutana kwetu haikuwa kwa bahati mbaya.Mungu alikuwa na makusudi yake na ndiyo maana leo hii ninathubutu kutamka kwamba pamoja na kwamba tuliachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake ,lakini bado moyoni mwangu una nafasi ya kipekee kabisa.Bado ninakupenda Savanna na hata siku moja upendo wangu kwako haujapungua.Sitaki kubishana na moyo wangu kwamba wewe ndiye mwanamke ambaye umeumbwa kwa ajili yangu.Savanna ninaombi moja kwako” Patrick akanyamaza akamtazama Savanna ambaye machozi yalikuwa yanamtoka
“Omba chochote Patrick nitakupatia” akasema Savanna huku akifuta machozi yale ya furaha
“Savanna pengine ombi langu kwako linaweza kuwa gumu hasa kutokana na matukio ambayo yamekuwa yananitokea lakini napenda kuwa wazi kwako kwamba ninaomba nafasi nyingine katika moyo wangu.Ninakubaliana na maneno uliyoniambia jana kwamba natakiwa kuufungua moyo wangu tena.Nimeufungua moyo wangu kwako na nina imani wewe ndiye pekee ambaye utaweza kunisahaulisha mambo yote yaliyopita na kunifanya niwe na maisha yenye furaha sana hapa duniani.Naomba uwe malkia wangu Savanna.” Patrick aliyasema maneno haya taratibu na kwa hisia kubwa.Mara tu alipomaliza kusema ya moyoni mwake,Savanna aliinuka kwa kasi na kulitupa shuka pembeni kisha akamkumbatia Patrick kwa nguvu.Alikuwa akiweweseka huku akimpiga Patrick mabusu mfululizo
“Patrick unataka kunipa uchizi.Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiota kuusikia mdomo wako ukitamka meneo haya mazito uliyonitamkia sasa hivi.Patrick nashukuru sana na sina cha kusema zaidi ya kukuhakikishia kwamba siku zote moyo wangu ulikuwa na nafasi kwa ajili yako pekee.Niliamini siku moja mimi na wewe tutakuwa pamoja hata kama si katika maisha haya basi katika maisha mengine baada ya kufa.Nimekuwa nikimuomba sana Mungu kwa jambo hili lakini hatimaye leo hii limekuwa kweli.Huu ni kama muujiza kwangu.Patrick nakukabidhi moyo wangu na kila kilicho changu.Naomba unitawale ee mfalme wangu.Niamuru chochote nitakutii” akasema Savanna kwa hisia kali huku akitokwa na machozi ya furaha.Ilikuwa ni kama ndoto.Hakuamini kama ile ndoto yake ya siku nyingi ya kuwa na Patrick leo hii imekuwa kweli.Walikumbatiana kwa furaha huku wakiepeana mabusu mfululizo na taratibu wakajikuta wakianza kuhama katika ulimwengu huu na kwenda katika ulimwengu uliojaa mahaba mazito.Migumo na mihemo ya kimahaba ndivyo vilitawala chumba hiki.Patrick akaufungua mpya wa mapenzi na Savanna.
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 53
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT : 0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Patrick nakukabidhi moyo wangu na kila kilicho changu.Naomba unitawale ee mfalme wangu.Niamuru chochote nitakutii” akasema Savanna kwa hisia kali huku akitokwa na machozi ya furaha.Ilikuwa ni kama ndoto.Hakuamini kama ile ndoto yake ya siku nyingi ya kuwa na Patrick leo hii imekuwa kweli.Walikumbatiana kwa furaha huku wakiepeana mabusu mfululizo na taratibu wakajikuta wakianza kuhama katika ulimwengu huu na kwenda katika ulimwengu uliojaa mahaba mazito.Migumo na mihemo ya kimahaba ndivyo vilitawala chumba hiki.Patrick akaufungua mpya wa mapenzi na Savanna.

ENDELEA………………

Ukurasa mpya wa maisha ya Patrick umefunguliwa na tayari ni meneja wa kiwanda cha kusindika nyama.Maisha yake yanakwenda vizuri kwa sasa.Alinawiri na kupendeza sana.Alikiongoza kiwanda hiki cha kusindika nyama kwa ufanisi mkubwa na ndani ya kipindi kifupi kiwanda hiki kilikuwa ni moja kati ya viwanda bora kabisa nchini
Mizizi ya penzi imara kati yake na Savanna ilichomoza kwa kasi na kwa sasa penzi lao halikuwa la siri tena.Lilikuwa kwa ndugu jamaa na marafiki.Alimtambulisha rasmi Savanna kama mpenzi wake na kwa pamoja walikuwa na mipango mingi na ndoto nyingi za kutimiza katika maisha yao yajayo na kubwa likiwa ni kufunga ndoa mara tu kesi ya Patrick itakapomalizika.Bado kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili Patrick iliendelea kuunguruma mahakamani.Tayari upande wa mashitaka ulikwisha funga funga ushahidi wao hivyo kutoa nafasi kwa upande wa utetezi nao kuwaleta mahakamni mashahidi wanaomtetea Patrick.Upande wa utetezi ukiongozwa na Savanna uliitaka Mahakama kumuachia huru mteja wao kwa sababu alisababisha kifo wakati akijaribu kunyang’anya silaha mtu aliyekuwa ameishika silaha hiyo na aliyekuwa na dhamira ya kufanya mauaji.Baada ya Patrick kutoa ushahidi wake mahakamani ilifuata nafasi ya mashahidi kuanza kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.
Siku moja jioni Savanna alichelewa kurudi nyumbani na kukuta tayari Patrick amekwisha rejea toka kazini.Siku hii Savanna alionekana mchovu na mwenye mawazo mengi.Patrick aliligundua hilo na kumuuliza ni jambo gani lililokuwa limemsibu.Savanna hakujbu kitu akainuka pale sofani akajimiminia mvinyo katika glasi akanywa funda kubwa halafu akamtazama Patrick
“Savanna una tatizo gani leo mpenzi wangu? Si kawaida yako kuwa katika hali hii.Tafadhali niambie kama una tatizo lolote.” Akasema Patrick.Savanna akainama akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema
“Patrick nina tatizo mpenzi wangu.Kuna jambo linaniumiza kichwa changu sana.Nimekuwa nikilifikiria suala hili kwa muda mrefu sasa lakini nimeshindwa kulipatia ufumbuzi”
“Jambo gani hilo linakusumbua Savanna? Tafadhali niambie.Hakuna jambo lolote linaloweza kutushinda kulipatia ufumbuzi” akasema Patrick.Savanna akainamisha kichwa akafikiri kidogo na kusema
“Kuna tatizo kidogo katika kesi”
“Katika kesi? Patrick akastuka
“Ndiyo Patrick kuna tatizo dogo”
“Tatizo gani” akauliza Patrick ambaye tayari moyo wake ulianza kumwenda mbio
“Patrick nilishindwa kukutaarifu mapema kuhusu jambo hili kwa kuwa naamini ni jambo ambalo hutapenda kulisikia lakini naomba nikutaarifu kwamba katika orodha ya watu wanaotakiwa kutoa ushahidi wao mahakamani lipo pia jina la Happy”
Patrick kijasho kikamtoka .Alistushwa sana kwa taarifa ile
“Ou my God “ akasema kwa sauti ndogo huku akimkazia macho Savanna
“Happy kibaho? Akauliza Patrick
“Ndiyo.Happy Kibaho”
“Ouh my Gosh.! How could you do that Savanna?Tulikubaliana kwamba Happy hatahusika na chochote katika kesi hii,aliniacha nikisota gerezani kwa kosa ambalo sikulifanya,hakuona umuhimu wangu,kwake yeye hata kama nikifungwa gerezani hatajali,kwa nini basi tumtumie mtu kama huyu? Savanna Happy kibaho ni jina ambalo sitaki kulisikia tena katika masikio yangu.” Patrick akasimama
“Patrick hii ndiyo sababu sikutaka kukueleza mapema.Nilijua lazima ungeshtushwa sana na taarifa hiyo”
“Savanna tafadhali niko chini ya miguu yako naomba kama kuna uwezekano liondoe jina la Happy katika orodha ya mashahidi.Tunao mashahidi wengi ambao tutawatumia katika kesi hii.” Akasema Patrick.Savanna akamshika mabegani na kusema
“Patrick mpenzi wangu ninafahamu ni namna gani Happy alivyokuumiza na jinsi gani unavyomchukia.Nafahamu pia uhusika wa Happy katika kesi hii unavyokuumiza kwani utairudisha tena taswira ya mtu ambaye hutaki tena kumuona au kumsikia katika maisha yako.Hata mimi suala hili ni gumu sana kwangu lakini naomba niwe wazi kwako kwamba Happy ni mtu muhimu sana katika hatua hii tuliyofikia.Ushahidi wake una nguvu sana”
“Savanna mashahidi hawa wote tulionao hawatoshi hadi Happy naye ashirikishwe katika kutoa ushahidi? To be honest I hate her.Sitaki kuiona tena sura yake kutokana na mambo aliyonifanyia.” Akasema Patrick
“Ushahidi mzito tuliouwasilisha mahakamani pamoja na ule unaoendelea kutolewa na mashahidi unajitosheleza sana lakini katika ushahidi wote huo Happy ametajwa sana kwani yeye ndiye aliyekoswa na risasi iliyotoka katika bastora aliyokuwa ameishika Vero.Happy anatakiwa aieleze mahakama kila kitu kilichotokea jioni ile.Ni ushahidi muhimu mno ambao ninaamini ndio utakaoisaidia mahakama kuamua hatima ya kesi hii.Patrick nakuomba mpenzi wangu tumtafute Happy na kumuomba atoe ushahidi wake .Nafahamu kwamba unamchukia na hutaki kumuona tena lakini kwa hatua hii Happy ni mtu muhimu sana kwetu.Patrick we’re almost to the end now so we need to do everything we can to win.Ninamuomba sana Mungu atusaidie ili tuweze kulimaliza suala hii haraka na tuitimize ndoto yetu ya kufunga ndoa.Naomba uniruhusu mpenzi wangu nimtafute Happy ili aweze kuja kutoa ushahidi wake “ akasema Savanna.
Patrick akashika kichwa kwa mikono yake akainama na kuzama katika mawazo.Akainuka pale alipokuwa amekaa akaenda dirishani,akasimama na kuelekeza macho yake nje kana kwamba kuna kitu alikuwa anakiangalia
“Happy Kibaho !” akasema taratibu halafu akainama tena
“Nilimpenda kiasi ambacho siwezi kuelezea.Nilimpa kila kitu na kuamini kwamba yeye ndiye mwanamke pekee ambaye nimepangiwa niwe naye katika maisha yangu.Pamoja na kumuonyesha kila aina ya upendo lakini Happy bado alidiriki kufanya kitendo kichafu ambacho sikuwahi kutegemea au hata kuota kama msichana kama Happy anaweza akafanya.Aligundua kosa alilolitenda na akapotea moja kwa moja akiniacha nikiozea gerezani kwa kosa ambalo alilisababisha yeye mwenyewe.Je mtu wa namna hii aliyenisababishia majeraha makubwa ya moyo ninastahili kuonana naye tena ana kwa ana? Moyo wangu hautaki kabisa na hauko tayari kuonana tena na Happy lakini kwa kuwa hili ni ombi la Savanna itanibidi nikaze moyo na kukubali aje atoe ushahidi wake.” Akawaza Patrick halafu akamgeukia Savanna
“Unafahamu mahala aliko Happy kwa sasa? Savanna akainuka na kumfuata Patrick pale alipokuwa amesimama.
“Patrick kuna jambo lingine ambalo naomba ulifahamu”
“Jambo gani hilo Savanna?
“Happy hayupo hapa nchini”
“Hayupo hapa nchini?.How do you know that she’s not here? Akauliza Patrick kwa wasi wasi
“Samahani Patrick kwa kutokufahamisha suala hili toka mwanzo lakini naomba nikufahamishe kwamba mimi ndiye niliyemsaidia Happy kuondoka hapa nchini” akasema Savanna.Patrick akazidi kuchanganyikiwa
“Savanna unazidi kunichanganya akili yangu.Ulimsaidia Happy kuondoka hapa nchini? Kwa nini hukuniambia muda wote huu? Do you know where she is now?
“Patrick ni hadithi ndefu sana na sikutaka kukwambia mapema kwa sababu nilijua utaumia na mimi sitaki kukuona ukiumia.”
“Ok niambie nini kilitokea? Happy yuko wapi? Akauliza Patrick.Savanna akainama akafikiri kidogo halafu akasema
“Nilipigiwa simu usiku na mzee Kibaho baba mzazi wa Happy akaniuliza kama nina taarifa zozote kuhusiana na Happy kwani hakuwa ameonekana nyumbani kwao toka alipoondoka asubuhi.Sikujua mahala alipokuwa Happy na mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni gerezani asubuhi.Hii ilikuwa ni siku ile nilipokuja gerezani na mama na tukamkuta Happy pale mama akamfokea sana.” Savanna akasema halafu akamtazama Patrick kisha akaendelea
“Asubuhi ya siku iliyofuata nikiwa najiandaa kuja gerezani ,alikuja mmoja wa wafanyakazi wangu akiwa na gazeti lililokuwa na picha chafu za Happy katika ukurasa wa mbele.Nilistuka sana baada ya kuziona picha zile na kama haitoshi mtumishi yule akainionyesha pia na video iliyokuwa mtandaoni.Ilinibidi nimpigie simu Margreth naye akanifahamisha kwamba Happy alikuwa amekunywa sumu kwa lengo la kujiua.Nilikwenda hadi katika hospitali ya Brahmaputra ambako Happy alikuwa amekimbizwa na kupatiwa huduma ya kuondolewa sumu mwilini.Nilishauriana na familia yake na tukakubaliana kwamba ili kumuepusha Happy na aibu kubwa aliyoipata itabidi kumpeleka mafichoni nje ya nchi sehemu ambako hakuna mtu anayemfahamu .Kama mchango wangu kwao nilijitolea usafiri wa kwenda Kigali Rwanda ambako tayari nilikwisha fanya mawasiliano na meneja wa hoteli moja kubwa mjini Kigali ambaye ni rafiki yangu na kumuomba Happy akae katika hoteli yake hadi hapo atakapopona kabisa .Mimi baba yake,mzee Kibaho pamoja na daktari mmoja tulielekea Kigali Rwanda na nilimuacha Happy kule akiwa na baba yake pamoja na daktari “ akasema Savanna.
“So she’s in Kigali now? Akauliza Patrick
“Alikuwa Kigali lakini kwa taarifa nilizozipata toka kwa rafiki yangu Christine ni kwamba Happy alitoweka pale hotelini na hakuna anayefahamu alikwenda wapi.” Akasema Savanna
“Ouh my God.Tumekwama tena” akasema Patrick
“Tukitaka kumpata Happy hatuna budi kuwasiliana na familia yake.Nina imani lazima watakuwa wanafahamu mahala alipo”
“Hilo nalo ni tatizo lingine.Sina hakika kama familia yake inaweza kutupa ushirikiano na kutuambia mahala aliko Happy” akasema Patrick
“Mimi ndiye nitakayekwenda kuonana nao.Nina imani msaada wangu hawataweza kuusahau kwa hiyo watanisaidia”
“Hata kama familia yake itakubali kushirikiana nasi ,vipi kuhusu Happy mwenyewe atakuwa tayari kurudi tena hapa Tanzania kutoa ushahidi wake baada ya mambo ya aibu kubwa aliyoyafanya? Sina hakika kama anaweza akakanyaga tena Tanzania hasa kutokana na aibu kubwa aliyoipata kutokana na uchafu mkubwa alioufanya.Sina hakika kama suala hili litafanikiwa Savanna,Naomba tusiumize vichwa vyetu kuhusu huyu mwanamke.Tutafute njia nyingine ya kutusaidia na si kumtegemea Happy” akasema Patrick akionyeaha kukata tamaa kabisa ya kumpata Happy
“Patrick mpenzi wangu laiti kama kungekuwa na njia nyingine ya kufanya nisingethubutu kukutajia jina la Happy lakini kwa hatua tuliyofikia ni lazima tumpate Happy.We’re almost to the end.Patrick naomba uniruhusu mimi nikaonane na familia ya Happy nitawalilia na kuwaomba wanisaidie.Mzee Kibaho ni mtu mwelewa sana na nina hakika atakuwa tayari kutusaidia”
Patrick akainama akafikiri kidogo na kusema
“Do what you have to do Savanna lakini moyo wangu haujapenda kuonana na Happy kabisa”
“Ahsante sana mpenzi wangu.Umefanya jambo la maana sana kwa kukubali.Najua si maamuzi mepesi lakini its for the best of us.I promise you that we’re going to finish this once and for all” akasema Savanna,Patrick hakujibu kitu

* * * *

Saa nne za asubuhi siku iliyofuata ilimkuta Savanna nje ya geti la nyumba ya akina Happy.Ni muda mrefu umepita toka alipokuja katika nyumba hii.Akiwa ndani ya gari lake ,alilitazama geti la nyumba ile na kuvuta pumzi ndefu
“Help me God.Laiti ningekuwa na namna nyingine ya kufanya katu nisingethubutu kuja tena katika nyumba hii.Sikutaka Happy aonane tena na Patrick hasa katika wakati ambao penzi letu limekwisha weka mizizi imara,lakini kwa hali halisi ilivyo ninalazimika kurejea tena katika nyumba hii kutafuta msaada” akawaza Savanna halafu akashuka na kwenda kubonyeza kengele ya getini
Baada ya dakika moja geti likafunguliwa.Alikuwa ni mama yake Happy.Savanna akaingiwa na woga kidogo lakini akakaza moyo akasalimiana na mama yake Happy na kukaribishwa ndani
“Savanna umepotea sana mwanangu.Habari za siku nyingi?
“Kazi zimekuwa nyingi mama na ndiyo maana sijafika hapa muda mrefu sijafika kuwatembelea.Habari za hapa?
“Habari za hapa nzuri Savanna.Karibu sana” akasema mama Happy kisha mtumishi wa ndani akawahudumia vinywaji
“Mama mna mawasiliano yoyote na Happy? Nilipigiwa simu na Christine yule rafiki yangu niliyemkabidhi amuhudumie kule Kigali kwamba Happy aliondoka katika hoteli ile aliyokuwa anakaa na mpaka sasa hajui alipo.Nimepata wasi wasi sana na nikaona ni bora nije kuuliza kama mnalifahamu jambo hili” akasema Savanna na mama yake Happy akaonyesha mstuko Fulani
“Savanna suala hili tumelisikia na hata sisi limetustua sana.Mpaka hivi sasa hatujui Happy yuko wapi na hatuna mawaliano naye yoyote.Tumeamua kumuachia Mungu na kumuomba amlinde na kumpa uzima kokote kule aliko.Tunaamini siku moja lazima atarejea nyumbani” akasema mama Happy
Savanna kijasho kikamtoka.Akavuta pumzi ndefu na kusema
“Ouh my gosh !
Kimya kikatanda mle sebuleni halafu Savanna akauliza
“Margreth naye yuko wapi?
“Margreth yuko kazini “
Savanna akainama na kufikiri kwa muda kisha akasema
“Mama mimi nakwenda.Tutaonana tena siku nyingine.Endapo mtapata mawasiliano yoyote ya Happy naomba mtanitaarifu “akasema Savanna huku akiinuka.Mama yake Happy akastuka
“Savanna kulikoni? Mbona ghafla hivyo?
“Utanisamehe mama nimekumbuka kwamba nina miadi na mtu wa muhimu sana muda mfupi ujao.Nitakuja tena kukusalimu siku nyingine” Akasema Savanna na kuonyesha kwamba hakutaka tena maongezi akaingia katika gari lake na kuondoka
“Kuna kitu nimekigundua toka kwa mama yake Happy. Alikuwa na wasi wasi mwingi.Inaonekana kuna jambo analifahamu kuhusu Happy na hakutaka kunieleza.Margreth au mzee Kibaho wanaweza wakanipa ukweli halisi.Ngoja kwanza nikaonane na Margreth” akawaza Savanna halafu akaegesha gari pembeni ya barabara akachukua simu yake na kumpigia Margreth
“Hallo Savanna.Habari za siku nyingi? Akasema Margreth baada ya kupokea simu
“Habari nzuri Margreth.Hatujaonana muda mrefu sana”
“Ni kweli Savanna.Mbona umekuwa kimya hivyo?
“Ni mihangaiko tu Margreth.Uko wapi sasa hivi?
“Sasa hivi niko kazini lakini niko mbioni kutoka nataka kwenda kuhudhuria mazishi ya rafiki yangu”
“Margreth,ninahitaji sana kuonana nawe.Kuna jambo muhimu nahitaji kuongea nawe.Tunaweza kuonana kabla hujaenda msibani?
“Hakuna tatizo Savanna.Tukutane wapi?
“Tuonane pale Lemina Café.Ninaelekea huko sasa hivi.Utanikuta pale”
“Sawa Savanna.Nakuja hapa muda si mrefu” akajibu Margreth na kukata simu.

* * * *

Habari za siku nyingi Margreth? Alianzisha mazungumzo Savanna baada ya kuonana na Margreth
“Habari nzuri Savanna.Umepotea sana dada yangu”
“Ni kweli Margreth ni muda mrefu sana hatujaonana.Hii inachangiwa na majukumu mengi ya kazi”
“Ni kweli kabisa Savanna” akajibu Margreth.
“ Patrick anaendeleaje? Kesi yake imefikia wapi?
“ Patrick anaendelea vizuri na kesi yake naendelea vizuri pia.Kwa hivi sasa kinachoendelea na kusikilizwa kwa mashahidi wa utetezi.Tutalimaliza suala hili” akasema Savanna
“ namuombea Mungu Patrick suala hili liishe na aendelee na maisha yake” akasema Margreth kisha kikapita kimya kifupi.Savanna akasema
“Margreth nimekuita hapa nina tatizo ambalo nahitaji sana msaada wako” akasema Savanna
“Usijali Savanna niko tayari kukusaidia kwa lolote”
“Ahsante sana.Tatizo langu ni kutaka kufahamu mahala aliko Happy.Nahitaji kuzungumza naye”
Margreth akastuka na kumuangalia Savanna
“Happy ..?!! akauliza Margreth.
“Ndiyo.Nina shida kubwa ya kuongea na Happy.”
“Happy yuko Kigali mahala ulikomuacha” akajibu Margreth na kumfanya Savanna acheke kidogo
“Happy hayuko Kigali.Aliondoka kule muda mrefu sana .Tafadhali naomba Margreth unisaidie nizungumze na Happy.” Akasema Savanna.Margreth akaona aibu kidogo na kutabasamu
“Samahani Savanna kwa kutaka kukudanganya lakini ukweli ni kwamba taarifa hiyo uliyonayo ndiyo hata sisi tunayo.Tulitaarifiwa kwamba Happy ameondoka katika hoteli aliyokuwa akikaa na haijulikani alielekea wapi.Tumejaribu sana kumtafuta bila mafanikio.Kwani kuna tatizo gani Savanna?
“Nina tatizo kubwa sana kumuona Happy.Tatizo ninalomtafutia Happy ni kwa sababu ya Patrick.”
“Patrick !!..” Margreth akashangaa
“Patrick anamtafutia nini Happy?
“Nadhani ulisikia kwamba Patrick alipata dhamana akatoka gerezani”
“Dada Savanna kwa kweli sihitaji kusikia au kufuatilia lolote linalohusiana na Patrick.Yeye ndiye chanzo cha dada yangu kuteseka na kupoteza mwelekeo mzima wa maisha yake.Kila anapokuwa karibu na Happy basi lazima kuna jambo baya linatokea.Kabla hajaonana na Patrick maisha ya Happy yalikuwa mazuri na yenye furaha lakini mara tu alipokutana na Patrick basi maisha yake yamebadilika ghafla na kupoteza kabisa mwelekeo mzima wa maisha yake.To be honest I hate that dude” akasema Margreth
“Nakuelewa sana Margreth lakini naomba nikukumbushe kwamba mara ya kwanza Patrick aliua bila kukusudia wakati akimuokoa dada yako asidhalilishwe na kundi la wahuni waliokuwa na lengo la kumbaka.Alifungwa gerezani na yakatokea yaliyotokea hadi walipokuja kukutana tena siku chache kabla ya kufunga ndoa.Kwa mapenzi makubwa waliyokuwa nayo na kwa ridhaa yao wenyewe waliamua kuachana na wapenzi wao ili waweze kutimiza ndoto yao ya kuwa pamoja.Katika ugomvi ule uliotokea na kupelekea kifo cha Vero na ni Happy ndiye aliyemsukuma Vero akajigonga ukutani na kufariki dunia.Kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo Patrick wa Happy aliamua kuubeba mzigo wote wa kesi hii.Na kwa taarifa yako ni kwamba mimi ndiye niliyepambana na kumtoa Happy katika kesi ile kwa ombi la Patrick.Kwa maana hiyo hakuna sababu ya kumlaumu Patrick” akasema Savanna.Margreth hakusema kitu na kwa mbali macho yake yalionyesha kulengwa na machozi
“Kesi ya Patrick inaendeleaje? Akauliza Margreth
“Mashahidi wanaendelea kutoa ushahidi wao na wiki hii shahidi aliyebaki atatoa ushahidi wake na baada ya hapo atabaki shahidi mmoja tu katika orodha ya mashahidi upande wa uetetezi.Ni Happy.Yeye ndiye mtu wa mwisho kutoa ushahidi wake .Ushahidi wake una nguvu sana kwa sababu yeye ndiye anayeifahamu vyema historia yake na Patrick na kila kitu kilichotokea usiku ule.Kwa hiyo namuhitaji sana Happy.Nakuomba kama unafahamu mahala alipo niambie tafadhali”akasema Savanna.
“Sifahamu aliko Happy” akajibu Margreth.Savanna akamtazama kwa macho makali na kusema
“Margreth nafahamu kuna kitu ambacho unanificha”
“I don’t know anything Savanna” akasema Margreth
“Margreth mimi ni rafiki wa familia yenu.Nilimsaidia Happy kama ndugu yangu wakati alipokutwa na matatizo.Na mimi nimepatwa na tatizo na ninaomba mnisaidie kama ndugu yenu.Sina maana ya kwamba nataka Patrick na Happy warudiane tena la hasha.Ninachotaka mimi ni ushahidi tu tena teknolojia imeimarika sana siku hizi anaweza akatoa ushahidi wake huko huko mahala aliko na si lazima aje Tanzania” akasema Savanna
“Savanna nimekwisha kwambia kwamba sifahamu mahala aliko Happy,mbona hutaki kunielewa? Akafoka Savanna
“Ok! Ok! nimekuelewa Margreth.Hakuna yeyote kati yenu anayeiona thamani ya Patrick tena.Natumai nyote mnatamani kusikia Patrick amefungwa gerezani.I cant let Patrick go to jail after all that has sacrificed.He’s my friend and I’ll do anything to set him free.Nitakwenda kumtafuta Happy mimi mwenyewe kwa gharama zangu na kwa njia ninayoijua mimi.Kama bado yuko hai nakuhakikishia kwamba nitampata tu.Kesho nitakwenda Kigali na nitaanza kumtafuta Happy tokea pale.Nina marafiki wengi pale na watanisaidia kujua Happy alipo.Ahsante kwa kuitika mwito wangu.Tutazidi kuonana” akasema Savanna halafu akainuka akachukua mkoba wake na kuanza kuondoka.
“Savanna wait…!! akasema Margreth.Savanna akageuka ,akamtazama Margreth na kurejea pale mezani
“Unasemaje Margreth? akauliza Savanna
“Naomba ukae chini Savanna” akasema Margreth
“Savanna umenipa wakati mgumu sana.Nashindwa nifanye nini lakini naomba nikufahamishe kwamba ninafahamu mahala alipo Happy” akasema Margreth.Uso wa Savanna ukaonyesha tabasamu .
“Ahsante sana Margreth kwa kuwa muwazi.Happy yuko wapi?
“Happy aliondoka Kigali na kuelekea Marekani .Kwa sasa anashi Los angeles .Yeye binafsi hataki mtu yeyote zaidi ya familia yake afahamu mahala aliko.Hivi sasa maisha yake ni mazuri na yenye amani.Nimeamua kukueleza ukweli wa mahala alipo Happy kutokana na uzito wa suala unalomtafutia japo najua kutakuwa na mtafaruku kwa sababu nimevunja makubaliano yetu ya kutomweleza mtu yeyote mahala aliko” akasema Margreth
“Usihofu Margreth.Hakuna mwingine zaidi yangu atakayejua kuhusu jambo hili.Sasa nieleze nitampata vipi? Unaweza kunipatia mawasiliano yake?
“Its not that simple Savanna.Nitakachofanya mimi ndiye nitakayeongea naye kwanza ili tuone atatoa jibu gani.Naomba niwe wazi kwako kwamba Happy hataki mawasiliano na mtu yeyote sasa na hasa hasa wewe.Sijui ulimfanya kitu gani kwani aliweka wazi kwamba katika watu anaowachukia basi wewe ni mmoja wao.Naomba uniachie mimi hiyo kazi nitaongea naye halafu nitakwambia jibu atakalonipa” akasema Margreth
“Ahsante sana Margreth.Nakuomba ujitahidi kwa kadiri utakavyoweza umshawishi akubali.Mkumbushe kwamba hatima ya Patrick iko mikononi mwake.”
“Ni kazi ngumu Savanna lakini nitajitahidi” akajibu Margreth.
“Jitahidi Margreth.Hata kama italazimika kumtumia tiketi ya ndege ya kuja na kurudi mimi niko tayari kugharamia.Kitu kingine ambacho unapaswa kumkumbusha ni kwamba hakuna mtu mwenye lengo la kumshawishi arejeshe uhusiano wake na Patrick kwani najua tayari ana maisha yake yenye furaha halikadhalika Patrick naye ana maisha yake yenye furaha pia.Tunachohitaji sisi ni ushahidi tu ambao utamuweka huru Patrick “ akasema Savanna halafu akafungua pochi lake na kutoa bunda la noti akahesabu noti kumi na tano za elfu kumi kumi na kumkabidhi Margreth.
“Hizi ni kwa ajili ya mawasiliano na Happy” akasema Savanna.Margreth akazichukua fedha zile na kumrudishia
“Nashukuru sana Savanna lakini naomba uziweke pesa hizo utazitumia kwa kitu kingine.Nitafanya mawasiliano kwa gharama zangu.” Akasema Margreth .Savanna akazichukua fedha zile na kuweka mkobani wakaagana akaondoka
Baada ya Savanna kuondoka,bado Margreth aliendelea kubaki pale mezani akiwa na mawazo mengi
“Nimefanya kosa kubwa sana kuvunja makubaliano yangu na Happy . Kwa mdomo wake mwenyewe alitamka kwamba hataki tena kurudi Tanzania.Nitaanzaje kumwelezea kuhusiana na suala hili? Ouh my gosh ! nimekoroga mambo.Happy atanilaumu sana kwa jambo hili lakini kwa upande mwingine ana haki ya kufahamu kinachoendelea huku nyumbani.Ana kila sababu ya kuja kutoa ushahidi mahakamani na kumuepusha Patrick na adhabu yoyote anayoweza kuipata kwa kosa ambalo hakulitenda.” Akawaza Margreth halafu akainuka akachukua mkoba wake na kuondoka
Margreth alifika nyumbani kwao lakini kabla hajaingia chumbani kwake mama yake akatokea
“Margreth mbona umewahi kurudi leo?
“Ninakwenda kuhudhuria mazishi ya yule rafiki yangu aliyefariki juzi” akasema Margreth
“Maggie ,Savanna alifika hapa “
“Alikuwa anataka nini? Akauliza Margreth
“Kikubwa alichoniuliza ni kama tuna mawasiliano na Happy au kama tufahamu mahala aliko hivi sasa.”
“Ulimjibu nini?
“Nilimjibu kwamba hata sisi hatufahamu mahala aliko Happy.Baada ya jibu hilo akaondoka zake.Nina wasi wasi sana kwa kuamua kumtafuta Happy hivi sasa.Sitaki kabisa wafahamu mahala Happy alipo” akasema mama yake
“Mama nimeonana na Savanna.Alinipigia simu wakati nikitoka kazini na nikaonana naye.Ni kweli ana tatizo na ndiyo maana anamtafuta Happy.” Akasema Margreth
“Ana tatizo gani? Sitaki wamuhusishe tena mwanangu katika masuala yao.”
“Mama Savanna ana matatizo makubwa na ni lazima aonane au awasiliane naye”
“Ana tatizo gani?
“Ni kuhusiana na ile kesi ya Patrick”
“Kesi ya Patrick ?!!..mama yake akashangaa
“Ndiyo mama.Happy anatakiwa atoe ushahidi wake.”
“Margreth ..!!!! akasema mama yake
“Hapana Margreth.Mwanangu Happy kamwe sintaruhusu aje tena huku na kuonana tena na Yule kijana.Mambo aliyokumbana nayo yanatosha sitaki tena mwanangu aumie.Maisha yake ni mazuri kwa sasa na tayari amekwisha msahau Patrick.Sitaki aonane tena na yule kijana aliyejaa mabalaa mwili mzima”
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 54
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACK:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Mama Savanna ana matatizo makubwa na ni lazima aonane au awasiliane naye”
“Ana tatizo gani?
“Ni kuhusiana na ile kesi ya Patrick”
“Kesi ya Patrick ?!!..mama yake akashangaa
“Ndiyo mama.Happy anatakiwa atoe ushahidi wake.”
“Margreth ..!!!! akasema mama yake
“Hapana Margreth.Mwanangu Happy kamwe sintaruhusu aje tena huku na kuonana tena na Yule kijana.Mambo aliyokumbana nayo yanatosha sitaki tena mwanangu aumie.Maisha yake ni mazuri kwa sasa na tayari amekwisha msahau Patrick.Sitaki aonane tena na yule kijana aliyejaa mabalaa mwili mzima”

ENDELEA………………….

“mama..!!! “ akasema Margreth
“Hapana Margreth.Siruhusu mwanangu kushiriki kwa namna yoyote katika kesi hii.Tayari maisha yake yametulia hivi sasa na sitaki apate tena matatizo mengine.”
“Mama kama Happy asipofanya hivyo kuna uwezekano Patrick akafungwa gerezani.”
“Itakuwa vyema kama akifungwa.Ninamchukia sana yule kijana na kama ningekuwa na uwezo ningemuondoa kabisa katika uso wa dunia” mama yake Happy akasema kwa ukali
“mama si sahihi kusema hivyo.Kumbuka Patrick alikubali kuubeba mzigo mzito wa kesi kwa kosa ambalo hakulitenda.Happy ndiye aliyeua na ndiye anayestahili kusimama mahakamani hivi sasa lakini Patrick ameliepusha hilo na amejitolea yeye mwenyewe kuubeba mzigo huu.Mama huoni kwamba Happy analazimika kuwa mstari wa mbele kumtetea Patrick? Ninajua kwa sasa amekwisha anza maisha mapya na hana mpango tena na Patrick wala kurejea nyumbani lakini pamoja na hayo bado ana wajibu wa kuja kumtolea ushahidi mwenzake.” Margreth akajitahidi kumuelewesha mama yake ambaye bado alionekana kutokubaliana kwa namna yoyote ile na hoja ile ya kumtaka Hapy atoe ushahidi kwa Patrick
“Pamoja na hayo,bado sitaki mwanangu arejee.Sitaki aumie tena.Margreth wewe mwenyewe unafahamu fika kwamba yule kijana sijui amempa nini Happy.Kitendo cha Happy kumuona tu basi huwa anasahu kila kitu na kumkimbilia yeye.Kwa sasa Happy amekwisha rudiana tena na Mike na maisha yake yana furaha sitaki aonane tena na yule kijana.“ mama Happy bado aliendelea kuushikilia msimamo wake
“Mama natambua Happy tayari ameamua kuendelea na maisha yake na hana tena mpango wa kuendelea na Patrick kwa hiyo usiogope hata kama wataonana hakuna kitakachotokea.Anachotakiwa kufanya yeye ni kutoa tu ushahidi wake halafu aondoke zake akaendelee na maisha yake.Isitoshe hata Patrick naye amekwisha endelea na maisha yake na hana tena mpango na Happy”
“Margreth nimekwisha kueleza kwamba hata unishawishi vipi Happy hatakuja tena na kuonana na Patrick.Neno langu mimi ni la mwisho na sitaki tena mjadala huu uendelee.” Akasema mama yake Happy huku akiondoka akiwa amekasirika sana.Margreth naye akaelekea chumbani kwake na kujitupa kitandani
“Sikubaliani na mama hata kidogo.Hatutatenda haki kama Happy hatatoa ushahidi wake mahakamani kumtetea Patrick mtu aliyeubeba mzigo wa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili yeye.Lazima niwasiliane na Happy nisikie naye ana maoni gani kuhusu suala hili.Tukifanya mchezo Patrick anaweza akafungwa” Akawaza Margreth halafu akaichukua simu yake na kuzitafuta namba za Happy akapiga huku moyo wake ukimwenda mbio.Simu iliita na kukata.Akaangalia saa ya ukutani ilionyesha ni saa sita za mchana
“Yawezekana yuko katika usingizi mzito kwani mida hii huko kwao bado ni usiku.Ngoja nimpigie tena” Margreth akapiga tena
“Hallow “ simu ikapokelewa na sauti nzito ya kiume.Margreth akastuka na kudhani labda amekosea namba
“Halow naitwa Margreth,napiga simu toka Tanz…..” kabla hajamaliza,yule mwanaume aliyepokea simu akasema
“Margreth,Mike hapa naongea.Habari za Tanzania?Umekwisha isahau sauti yangu mara hii?
Margreth akavuta pumzi ndefu na kusema
“Mike !! nafurahi kuongea nawe tena.Ni muda mrefu umepita.Samahani kwa kukusumbua na kukuamsha usingizini.Nilikuwa Nahitaji kuongea na Happy”
“Happy niko naye hapa.Subiri kidogo nimuamshe” akasema Mike na baada ya muda sauti yenye usingizi ya Happy ikasikika
“Hallow Margreth”
“Happy.!! Samahani nimekuamsha”
“Usijali Margreth hata hivyo nimelala muda si mrefu sana.Mike amekuja leo hivyo tukaenda club,Habari za huko?
“Huku kwema Happy,tunaendelea vizuri isipokuwa yule rafiki yangu Salama amefariki dunia wakati akijifungua na leo tunamzika”
“Salama yule aliyeolewa na mzungu?
“Ndiyo huyo”
“Dah ! poleni sana.Habari nyingine?
“Habari nzuri Happy.” Akasema Margreth
“Maggie nilikuahidi kukutumia ile hela ya kununua gari,sijasau nitakutumia wiki ijayo,wiki hii nilikuwa nimetingwa sana na kazi”
“Ahsante sana Happy lakini sijakupigia kwa ajili ya suala hilo.Kuna suala linguine”
“Suala gani Maggie?
“Happy kuna tatizo limejitokeza”:
“Tatizo gani? akauliza Happy.Margreth akashusha pumzi na kusema
“Its about Patrick”
“Patrick ..!!!! “ Happy akastuka
“Ndiyo Happy.Nimeoanana na Savanna muda si mrefu na amenifahamisha kwamba Patrick alifanikiwa kupata dhamana na yuko huru lakini kesi yake inaendelea kusikilizwa na kinachoendelea hivi sasa ni mashahidi wa upande wa utetezi kutoa ushahidi wao.Savanna alitaka kufahamu mahala ulipo” akasema Margreth
“Ananitafuta mimi? Kwa nini? Akauliza Happy kwa wasi wasi
“Jina lako liko katika orodha ya watu wanaotakiwa kutoa ushahidi wao mahakamani kumtetea Patrick”
“No ! No ! no !!!..Thats impossible.Margreth no body should know where I am.” Akasema Happy
“Its too late Happy.Nimelazimika kumweleza ukweli Savanna kutokana na uzito wa suala lenyewe.”
“Ouh Margreth how on earth could you do such a thing? Tulikubaliana kwamba asiambiwe mtu mwingine yeyote mahala nilipo.Kwa nini lakini umefanaya hivyo? How could you betray me? Akalalama Happy
“Naomba unisamehe sana Happy kwa kilichotokea.Najua yalikuwa ni makubalianao yetu kwamba asifahamu mtu mwingine yeyote mahala ulipo lakini nimelazimika kumweleza Savanna na hakuna mtu mwingine yeyote anayelifahamu hilo zaidi yake.”
“Margreth siwezi kukuamini tena.Umeyafanya maisha yangu yawe magumu tena.Umenifanya nirudi tena katika kile ambacho nimekuwa nikikimbia kwa muda huu wote” akasema Happy
“Happy naomba unisikilize kwa makini.Nililazimika kumweleza Savanna mahala ulipo baada ya kuniweka wazi kwamba ushahidi wako una nguvu sana ya kumsaidia Patrick asihukumiwe kifungo.Happy hata mimi inaniuma sana kukukumbusha mambo ambayo unajitahidi kuyasahau lakini naomba niwe muwazi kwako kwamba you have to save Patrick.He saved you from going to jail and its your turn now to save him” akasema Margreth.Baada ya ukimya mfupi Happy akasema
“Margerth nimekuelewa lakini sina hakika kama nitaweza kufanya hivyo.Ninapambana hivi sasa kumsahau Patrick na kuendelea na maisha yangu mapya yenye furaha na siko tayari kuonana tena na Patrick ana kwa ana.” Akasema Happy
“Happy sina maana ya kwamba ukitoa ushahidi utarudiana tena na Patrick na wala sikushauri ufanye hivyo lakini nakukumbusha tu kwamba Patrick ameubeba mzigo mkubwa sana na endapo atafungwa kwa sababu tu ya kukosekana ushahidi wenye nguvu,nakuapia Happy hautakuwa na furaha hata siku moja katika maisha yako.Patrick’s shadow will haunt you forever” Akasema Margreth
“What can I do Margreth? Let it be.Look Margreth ,there is nothing I can do now to help him.I’m trying to pick up the pieces and arrange my life again so I cant go back to square one.Nilimtenda vibaya Mike na kumsababisia maumivu makali ya moyo lakini hivi sasa ndiye amekuwa msaada wangu mkubwa na ndiye anayenisaidia kusahau mambo yote yaliyopita.Ninaishi hapa Marekani kwa sababu yake.Amenitafutia nyumba,kazi na kila kitu.He loves me and I’m learning to love him so how could I tell him that I’m going back to Tanzania? Please Margreth,this conversation is over.” Akasema Happy
“Happy kabla hujakata simu naomba nikukumbushe kitu kimoja.Ulinitamkia wewe mwenyewe kwa mdomo wako kwamba Patrick hakusababisha kifo cha Vero bali ni wewe uliyemsukuma akajigonga ukutani na kufariki.Patrick kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwako aliamua kujitwisha yeye mzigo wote .Ameteseka gerezani kwa kipindi kirefu na bado anaendelea na kesi.Nomba leo unitamkie neno moja tu kwa mdomo wako kwamba uko tayari Patrick afungwe gerezani kwa kosa ambalo hakulitenda? Nipe jibu moja tu na nitakuelewa” akasema Margreth.Happy machozi yakamtoka
“I don’t know Margreth.’ll call you later” akasema Happy na kukata simu.Machozi yalianza kumtoka na akaanza kulia kwa kwikwi.Mike aliyekuwa chumbani akatoka haraka aliposikia Happy akilia kwa kwikwi.
“Happy kuna nini? Mbona unalia? Kuna taarifa ambayo si nzuri? Akauliza Mike
Happy akamkumbatia Mike kwa nguvu huku akiendelea kulia
“Nyamaza kulia mpenzi wangu na uniambie nini kinakuliza.Kuna tatizo gani nyumbani? Akauliza Mike.Happy hakujibu kitu aliendelea kulia kwa kwikwi.Mike akamletea glasi ya maji akanywa
“Tafadhali niambie Happy una tatizo gani?
“Mike kuna tatizo limetokea”
“Niambie Happy ni tatizo gani ? Niko hapa kukusaidia”
“Si tatizo kubwa lakini linahusiana na kesi ya Patrick” akasema Happy na kumstua Mike
“Nini kimetokea katika hiyo kesi?
“Savanna wakili anayemtetea Patrick amefika nyumbani leo hii na kuulizia taarifa zangu na kuomba apatiwe mawasiliano yangu lakini kwa bahati mbaya amekutana na Margreth na akamueleza kila kitu kuhusu mimi”
“Ouh my gosh ! Kwa nini lakini amefanya hivyo wakati mlikwishakubaliana kwamba mtu yeyote asifahamu mahala ulipo?
“Kwa madai ya Margreth ni kwamba aliamua kumweleza ukweli Savanna kutokana na uzito wa suala hilo alilokuwa ananitafutia”
“Ni suala gani alilokuwa anakutafutia?
Happy akafikiri kidogo na kusema
“Natakiwa kutoa ushahidi wangu mahakamani kumtetea Patrick.”
Kimya kikatanda mle ndani.Kila mmoja alikuwa anawaza lake.Mike alionekana kuishiwa nguvu.
“Happy my angel tell me its not true and if true you wont do it” akasema Mike
“Its true Mike.Natakiwa mahakamani nikatoe ushahidi wangu.
“That’s impossible.You cant go back there” akasema Mike.Alistushwa sana na taarifa ile ya Happy
“Happy mpenzi naomba unihakikishie kwamba hutakwenda tena Tanzania.Hutakwenda kuonana tena na Patrick.Kama ingekuwa ni kesi inayomkabili mtu mwingine nisingekuwa na wasi wasi wowote lakini kukuacha ukaonane tena na Patrick hilo ni jambo ambalo siwezi kulifanya” akasema Mike huku amemshika Happy mabegani
“Mike kuna jambo ambalo ningependa ulifahamu” akasema Happy
“Jambo gani Happy ? Mbona unanipa wasi wasi mpenzi wangu? Akauliza Mike.Happy akavuta punzi ndefu na kusema
“Patrick hakumuua Vero”
Mike akastuka na kumtumbulia Happy macho.
“Sikuelewi unamaanisha nini Happy.Patrick anatuhumiwa kwa kusababisha kifo cha Vero.Kwa nini unasema kwamba si yeye aliyesababisha kifo cha Vero? Akauliza Mike.Happy akamtazama usoni na kusema
“Mimi ndiye nilisababisha kifo cha Vero.” Akasema Happy
Mike akastuka na kumuachia Happy mikono halafu akasimama na kumuangalia Happy kana kwamba ni mara ya kwanza anamuona
“That’s not true .Its not true…” akasema Mike
“Its true Mike.I killed her.Samahani kwa kutokwambia kuhusu suala hili kwa sababu hii ni sehemu moja ya maisha yangu ambayo ninapambana ili niisahau.”akasema Happy
“Sikuelewi mpenzi wangu.Kwa nini unifiche kitu kikubwa kama hiki?
“Nisamehe mpenzi wangu.Naomba unisamehe Mike na unielewe kwamba sikufanya makusudi kutokwambia kitu kama hiki.Naamini hata wewe ungekuwa katika nafasi yangu ungefanya kama nilivyofaya mimi yaani kuliweka jambo hili kuwa ni siri ya moyoni.Ni jambo ambalo kila nikilifikiria huwa linanipa wakati mgumu sana.I’ve been trying to forget that night but I cant..” akasema Happy huku akishindwa kujizuia na kutoa machozi.Mike akamsogelea na kumkumbatia
“Nyamaza mepnzi wangu.Nyamaza Happy.Naomba unieleze ni kitu gani kilitokea usiku huo na kwa nini Patrick ndiye anayetuhuiwa kwa kusababisha mauaji hayo? Akasema Mike.Happy akafuta machozi akafikri kidogio na kusema
“Tulikuwa hotelini mimi na wewe tukipata chakula nilipopigiwa simu na Patrick kwamba kuna matatizo yametokea na baba yake amelazwa katika hospitali kuu ya magonjwa ya moyo .Kama utakumbuka nilikuomba unirudishe nyumbani ambako nilichukua gari langu na kukimbia hospitali.Nilimkuta Patrick halafu tukapanda katika ghorofa ya juu ambayo bado ujenzi wake ulikuwa unaendelea na Patrick akaanza kunisimuilia kilichotokea.Ghafla akatokea Vero akiwa na bastora mkononi.Alikuwa amekasirika na sura yake ilionyesha kwamba alikuwa amedhamiria kufanya kitu kibaya.Nadhani nilikueleza kuhusiana na kitendo alichokifanya Patrick cha kuvunja uchumba na Vero kitendo ambacho kilimuumiza sana.Alituelekezea bastora ile huku akitoa vitisho vingi sana na kutishai kututoa uhai mimi na Patricki.Patrick alimsihi aache utani na silaha za moto na ndipo alipoonyesha kwamba hakuwa akitania pale alipoachia risasi iliyonikosa na kupiga nguzo.Nilihisi kama nimekufa nikaanguka chini.Kitendo kile kilimkasirisha Patrick ambaye bila kujali hatari iliyokuwepo akamfuata Vero na kuanza kumnyang’anya Vero ile silaha.Kitendo kile kiliniogopesha sana na nikajua Vero angeweza kumdhuru Patrick hivyo nikainuka na kwenda kumsukuma Vero ambaye alijigonga ukutani na kufariki dunia.Patrick hakutaka nihusishwe katika kesi ile kwa kuamua kuubeba mzigo wote wa kesi ya mauaji .Kila mtu anajua kwamba Patrick ndiye aliyesababisah kifo cha Vero.Alikubali kuubeba mzigo huu mzito wa kesi kubwa kama hii kwa ajili yangu kwa ajili yua kunikinga na kesi hii.”akasema Happy.Mike akamtazama kwa makini na kusema
“Ahsante Happy kwa kunieleza ukweli lakini pamoja na hayo ninataka kukuuliza jambo moja ”
“Uliza Mike”
“Do you still love him? Akauliza Mike
“Mike !! ..akasema Happy
“Just answer my question Happy.Do you have any feeling for him?
“Mike I’m with you now.Its you that I love now.Nimekuwa nikijitahidi kuifuta picha ya Patrick moyoni mwangu na hiyo inamaanisha kwamba sina hisia zozote kwake”
“Are you sure? Akauliza Mike
“Yes Mike I’m sure”
“Kama ni kweli hayo unayoniambia kwa nini ulikuwa unalia baada ya kuzipata taarifa hizi?
“Mike hata kama ungekuwa ni wewe lazima ungetoa machozi.Patrick naye ni binadamu na anakabiliwa na kesi kwa kosa ambalo hakulitenda .Nilishindwa namna ya kufanya hasa katika wakati huu ninaojitahidi kumsahau ndiyo maana nikashindwa kujizuia kulia” akasema Happy
“Its ok Happy.Forget about that.Umeshaamua kuyasahau yote ya nyuma kwa hiyo songa mbele.Mimi niko hapa na niko tayari kukusaida kwa kila namna nitakavyoweza ili uweze kusahau historia na matukio yote yaliyopita.Let him go”
“Mike ! How could you say that? Ingekuwa ni wewe uko katika nafasi yangu ungefanya nini? Ungemuacha mtu kama huyu afungwe gerezani? He saved me.He saved a woman you love.So that’s how you repay him? Akauliza Happy
“So what’s your decision? Akauliza Mike
“Nitakwenda Tanzania.Nitakwenda kutoa ushahidi wangu mahakamani.Siko tayari Patrick afungwe gerezani.Tafadhali Mike naomba uniruhusu niende Tanzania nikamtolee Patrick ushahidi.Lengo langu ni ili Patrick awe huru na aendelee na maisha yake.Najua unaogopa nini kitatokea endapo nitaonana naye lakini nakuhakikishia kwamba kitakachonipeleka huko ni kutoa tu huo ushahidi wangu na jambo lingine lolote.Me and him its over.” akasema Happy.Mike akazunguka zunguka mle ndani na kusema
“Laiti nisingekuwa na marufuku ya kukanyaga ardhi ya Tanzania nisingekubali uende peke yako.Ningekupeleka ukatoe ushahidi wako halafu turudi wote marekani.Sijui ni kwa nini ninakosa imani na Patrick.” Akasema Mike kwa masikitiko
“Kwa maana hiyo unaniruhusu niende Tanzania? Akaulza Happy
“Sina haja ya kukuruhusi kwani tayari umekwisha fanya maamuzi na siwezi kukukatalia.Ni kweli Patrick anastahili kutendewa wema kama alioutenda kwako.Lakini sijui kwa nini roho yangu bado inasita sana”
“Huniamni Mike?
“Nakuamini sana mpenzi wangu lakini nashindwa kujizuia kuwa na wasi wasi kuja kwamba unakwenda kuonana na Patrick tena.Patrick alifanya kitendo cha kijasiri sana ambacho hata mimi kimenigusa ,lakini naomba nikiri kwako mpenzi wangu kwamba siwezi kushindana na Patrick katika vita ya kukugombania .Nafahamu Patrick amekuwa moyoni mwako kwa miaka mingi sana .Nenda Tanzania mpenzi lakini ujue kwamba ninakuamini na kwamba hutafanya kitendo kama ulichonifanyia kipindi kile kwani sijui kama nitaweza kuyavumilia maumivu na mateso ya moyo kama niliyoyapata wakati ule.” Akasema Mike
“Mike naomba uniamini haya nikwambiayo kwamba kilichobaki kati yangu na Patrick ni historia tu.Kinachonisukuma kutaka kwenda kutoa ushahidi wangu ni kumsaidia ili kama ikiwezekana aweze kuachiwa huru.Alionyesha ubinadamu mkubwa kwangu kwa hiyo na mimi sina budi kumsaidia.After this I’m done with him.Patrick atakuwa huru na maisha yake na mimi nawe tutakuwa huru” akasema Happy

* * * *

Margreth akiwa msibani pamoja na waombolezaji wengine mara simu yake ikaita.Alikuwa ni Happy aliyempigia
“Hallo Happy” akasema Margreth baada ya kupokea simu
“Tayari umefika msibani?
“Ndiyo Happy.Tunajiandaa kwenda kuzika”
“Sawa Magreth,nimekupigia kukutaarifu kwamba ninakuja Tanzania kutoa ushahidi wangu halafu nitarejea tena marekani. Najua nitakabiliana na matatizo mengi lakini sina namna lazima nikabiliane na kila kitu.Naomba uongee na Savanna na akwambie ni lini ninahitajika mahakamani.”
“Ouh god thank you so much.Ahsante sana Happy kwa uamuzi huu.Nitamtaarifu Savanna halafu nitakufahamisha jibu atakalonipa” akasema Margreth na kukata simu halafu akamtafuta Savanna na kumtaarifu kuhusiana na jibu la Happy” .Hizi zilikuwa ni habari njema sana kwa Savanna japokuwa alishindwa kujizuia kuwa na wasi wasi nini kitatokea pale Patrick na Happy watakapokutana tena
“Sijui ni kwa nini ninakuwa na wasi wasi mwingi kuhusu Patrick kuonana na Happy.Labda ni kutokana na historia yao kwamba kila wakutanapo hushindwa kuzizuia furaha zao basi mapenzi yao huanza upya.Lakini sipaswi kuwa na wasi wasi wowote.Patrick ni wangu na hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumnasua toka katika mikono yangu.Ni Happy pekee ndiye mwenye kunipa wasi wasi “akawaza Savanna akiwa ofisini kwake
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 55
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Sijui ni kwa nini ninakuwa na wasi wasi mwingi kuhusu Patrick kuonana na Happy.Labda ni kutokana na historia yao kwamba kila wakutanapo hushindwa kuzizuia furaha zao basi mapenzi yao huanza upya.Lakini sipaswi kuwa na wasi wasi wowote.Patrick ni wangu na hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumnasua toka katika mikono yangu.Ni Happy pekee ndiye mwenye kunipa wasi wasi “akawaza Savanna akiwa ofisini kwake

ENDELEA………………….

Ndege ya shirika la ndege la afrika kusini iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam saa mbili za usiku.Miongoni mwa abiria waliokuwemo katika ndege hii ni Happy Kibaho ambaye monekano wake ulikuwa umebadilika sana na alionekana mrembo zaidi ya alivyokuwa alipoondoka Tanzania miezi zaidi ya kumi iliyopita.Kama ungekutana naye ghafla ingekuwia ugumu kidogo kumtambua.
Baada ya kukamilisha taratibu alitoka nje na kulakiwa na familia yake yote.Kilikuwa ni kipindi cha furaha kubwa kwa familia hii kukutana tena na mtoto wao ambaye hawakuwa wametegemea kama wangeonana naye tena hivi karibuni.Wote waliustaajabia uzuri wa Happy na namna alivyokuwa amebadilika.Hakukuwa na mwandishi yeyote wa habari aliyekuapo pale uwanjani kwani ujio wa Happy ulikuwa ni wa siri kubwa
“Wow Happy umebadilika sana” akasema mzee Kibaho na kumkumbatia mwanae kwa mara ya pili
“Ouh Dady ! nililazimika kufanya mabadiliko kidogo katika muonekano wangu wa zamani.Nilitaka nibadilike na kuwa Happy wa tofauti na zamani”
“You look so wonderfull and amazing as always.You look more than an angel” akasema mzee Kibaho kisha wote wakaelekea katika gari lao na kurejea nyumbani.Waliwasili nyumbani ambako kuliandaliwa tafrija ndogo ya kumkaribisha tena nyumbani Happy.Baada ya chakula na maongezi Happy akapelekwa chumbani kwake kulala.
“Margreth naomba nikalale chumbani kwako.Sitaki kulala katika chumba change cha zamani.Kuna kumbukumbu nyingi za nyuma ambazo nimekwisha anza kuzisahau.” Akasema Happy na kuelekea katika chumba cha Margreth.Kabla ya kulala,Happy akamkumbusha Margreth amtaarifu Savanna kwamba tayari amekwisha wasili na kama ana nafasi waonane kesho .Margreth akazitafuta namba za simu za Savanna akapiga.
Kwa muda wa dakika kadhaa sasa Savanna alikuwa anamkodolea macho Patrick bila kuongea lolote
“C’mon my angel ! Mbona unanitazama namna hiyo? Akauliza Patrick
“Sijui ni kwa nini nimejikuta nikiwa hivi siku ya leo.Natamani niendelee kukuangalia usiku kucha.Patrick nakupenda sana.Nakupenda zaidi ya unavyoweza kufikiri.Naomba niwe wazi kwako kwamba sintaweza kuishi maisha yangu bila ya kuwa nawe.” Akasema Savanna kwa sauti laini yenye mahaba mazito.Patrick akamvuta kwake na kumbusu kisha akasema
“Savanna wewe ni malaika wangu.Naomba ufahamu kwamba nakupenda na nitakupenda daima.Nakuahidi mara tu mambo haya yatakapokwisha basi tutafunga ndoa na tutaishi sote hadi kifo kitakapotutenganisha.” Akasema Patrck
“Patrick my love kwa nini tusifunge ndoa hata kabla ya kesi hii kumalizika? Binafsi sioni kipingamizi chochote cha kutuzuia tusifunge ndoa mapema” akasema Savanna
“Hakuna kipingamizi chochote Savanna cha kutufanya mimi nawe tushindwe kufunga ndoa.Kitu pekee kinachonisukuma na kunifanya niamni kwamba ni vyema kama tutafunga ndoa baada ya kesi kumalizika ni kuogopa kuchanganya mambo.Ninafikiria ni bora kama tukaelekeza nguvu katika jambo moja kwanza na baada ya kulimaliza basi tuelekeze nguvu katika jambo lingine ambalo ni ndoa yetu”
“Nakubaliana nawe Patrick japokuwa nilipenda sana jambo hili tulifanye mapema.Hata hivyo wazo lako zuri ni la msingi sana.Hatuna budi kuelekeza nguvu zetu zote kwa sasa katika kesi na baadae tushughulike na ndoa.” Savanna akastushwa na mlio wa simu yake.Akausogeza mkono na kuichukua
“Ni Margreth” akasema Savanna
“Anataka nini usiku huu? Akauliza Patrick
“sijui ngoja nimsikilize” akasema Savanna na kubonyeza kitufe cha kupokelea
“Hallo Margreth”
“Hallo Savanna.Samahani kwa kukusumbua usiku huu”
“Bila samahani Margreth.Jisikie huru kunipigia wakati wowote”
“Ahsante sana.Savanna nimekupigia kukutaarifu kwamba Happy amekwisha wasili.Amefika usiku huu.Ameomba kesho muonane hapa nyumbani”
“Ouh ok.Thats good news.Mwambie nashukuru sana kwa kufika kwake .Amefanya jambo kubwa na la maana sana na kesho nitakuja kuonana naye” akasema Savanna
“Kitu kingine Savanna,utakapokuja kuonana na Happy please don’t bring Patrick with you.Make sure Patrick and Happy they wont see each other.”
“Usijali Margreth.Siwezi kuambatana na Patrick. “
“Thank you Savanna.Good night”
“Good night Margreth” akajibu Savanna na kukata simu halafu akamgeukia Patrick
“Happy amekwisha wasili”
Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akasema
“Hizo ni habari njema sana.”
“Yah.Amefanya jambo la maana ” akasema Savanna kisha akamkazia macho Patrick
“Nini Savanna? Mbona unaniangalia hivyo?
“Kuna kitu ambacho nahitaji uhakika toka kwako”
“Kitu gani Savanna?
“Are you sure there will be no problem when you see Happy again?
Patrick akamtazama Savanna akavuta pumzi ndefu na kusema
“Usihofu Savanna,nakuhakikishia kwamba hakutakuwa na tatizo lolote.Siwezi kukuficha kwamba tayari nimekwisha mtoa Happy moyoni mwangu lakini bado nina donge kubwa limenikaa kooni la kutaka kufahamu ni kwa nini alitenda vile ? Kwa nini alifanya kitendo kile cha kupiga picha na video za utupu na kuzivujisha? Zaidi ya yote kwa nini aliamua kunitelekeza gerezani wakati akifahamu fika kwamba nilikuwa nimeubeba mzigo ambao ulimuhusu yeye? Ningefurahi sana kama ningepata nafasi ya kumuuliza na kupata majibu ya maswali yangu lakini sintaweza kufanya hivyo kwani sitaki kukumbuka mambo ya nyuma.Kitu cha msingi ninachoshukuru ni kwa kukubali kwake kuja kutoa ushahidi.Baada ya kumaliza kutoa ushahidi sintahitaji kumuona tena.Nataka niendelee na maisha yangu nikiwa na wewe mpenzi wangu ambaye unanipenda,unanijali na kunithamini.” Akasema Patrick na uso wa Savanna ukajenga tabasamu pana,akainama na kumbusu halafu wakakumbatiana.

* * * *

Ni Happy ndiye aliyemuamsha mdogo wake Margreth asubuhi ili ajiandae awahi kazini.Usiku wa kuamkia siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwa Happy na hakuweza kupata kabisa usingizi.Picha za matukio yaliyotokea miezi zaidi ya kumi iliyopita zilikuwa zkimjia kila alipojaribu kufumba macho.Alikumbuka toka kipindi alichokutana na Patrick shuleni Malangali Iringa hadi muda huu.
“Happy leo hujalala kabisa” akasema Margreth kwa sauti iliyojaa usingizi.Happy akatabasamu
“Mimi ni kawaida yangu.Huwa nina muda mchache sana wa kulala,muda mwingi ninafanya kazi.Amka ujiandae uende kazini” akasema Happy
Margreth akaamka akajindaa na kuondoa zake kuelekea kazini.Happy naye akatoka na kuanza kuizunguka nyumba yao.
Saa nne za asubuhi ilimkuta Savanna katika geti la akina Happy.Akapiga honi na Pendo mfanyakazi wa ndani akamfungulia geti na kumkaribisha ndani
Mtu wa kwanza kusalimiana naye alikuwa ni mzee Kibaho.Kwa kuwa mzee KIbaho alikuwa na haraka ya kuwahi katika shughuli zake hakuongea sana na Savanna akaondoka na kumuacha Savanna akiongea na mama yake Happy hadi pale Happy alipojitokeza.Savanna alishindwa kujizuia kutoa tabasamu pana sana baada kumuona tena Happy na namna alivyobadilika na kuwa mzuri
“My gosh ! huyu ni Happy au ni mzimu wake? Gosh ! she’s so pretty.She’s amazing.Dah ! binti huyu amejaaliwa uzuri wa aina yake” akawaza Savanna
“Hallow Savanna” akasalimu Happy
“Hallow Happy” akajibu Savanna na kuinuka kisha wakakumbatiana
“karibu tena nyumbani Happy” akasema Savanna
“Ahsante Savanna,nimefurahi sana kurejea tena nyumbani.Poleni na matatizo ya kila siku”
“Tumekwisha poa Happy.” Akasema Savanna halafu mama yake Happy akainuka na kuwaacha peke yao pale sebuleni ili kuwapa nafasi nzuri ya kuongea mambo yao kwa uhuru.
“Savanna twende bustanini ,naona hapa sebuleni hapatufai kwa maongezi yetu” akasema Happy kisha wakainuka na kuelekea bustanini
“Karibu sana Savanna.Habari za siku? Akaanzisha mazungumzo Happy baada ya kufika bustanini
“Habari nzuri Happy.Nimefurahi tena kukuona.Umebadilika sana.Ouh my gosh you are so beautiful.You are mazing” akasema Savanna na Happy akatabasamu
“Thank you Savanna” akajibu Happy
“Vipi maisha yako kwa ujumla? Akauliza Savanna
“Namshukuru Mungu .Kwa kweli Mungu anaweza.Ukimuomba kwa dhati Mungu anajibu.Nilikwisha kata tamaa kabisa na maisha yangu.Nilimuomba Mungu nikamlilia anisaidie na kweli amenisaidia na hali yangu imebadilika kama unavyoniona” akasema Happy na kucheka kidogo
“Nilipatwa na wasi wasi mkubwa Christine aliponipigia simu na kunitaarifu kwamba umetoweka pale hotelini Kigali na hawajui mahala ulipo.” Akasema Savanna na kumfanya Happy acheke kidogo
“Savanna kwanza kabisa napenda nikushukuru wewe binafsi kwani msaada wako ulikuwa mkubwa mno na ambao siwezi kuulipa.Ulinisaidia sana kujitambua na kunifanya niamue kuishi tena.Baada ya kukaa kwa muda pale Kigali nilipata wazo la kuondoka .Niliamua niende Marekani .Nilijua ile ndiyo sehemu salama kwa mimi kuishi tofauti na pale Rwanda ambako ni karibu sana na Tanzania.Vile vile tayari taarifa zangu zilikwisha fika kule na tayari nilianza kufahamika.Mtu pekee aliyenisaidia nikarejea tena Marekani ni Mike.Ninamshukuru sana kwa msaada wake mkubwa.Kwa sasa ninaishi na kufanya kazi Los Angeles na maisha yangu yanakwenda vizuri.” Akasema Happy
“So you are back together,you and Mike” akauliza Savanna
“I’m sorry to say this Savanna but yes ! we’re back together and deeply in love na tunategemea kufunga ndoa” akasema Happy huku akitabasamu kuona aibu kwa mbali
“Ouh ! Congraturations” akasema Savanna
“Thank you” akajibu Happy kisha kimya kifupi kikapita
“What a stupid woman..Yaani anadiriki kusema wazi wazi kwamba amerudiana na Mike na wanatarajia kufunga ndoa huku akisahau kwamba alimuacha Patrick akisota gerezani kwa kosa ambalo hakulitenda.” Akawaza Savanna.Happy akasema
“Savanna haikuwa rahisi kwangu kuamua kuja tena Tanzania.Niliapa kutokurudi tena Tanzania lakini kutokana na uzito wa suala lenyewe nimevunja kiapo changu ili na mimi niweze kutoa msaada wangu japo mdogo kwa Patrick ambaye alifanya jambo la kijasiri sana kuniokoa mimi nisikae gerezani kwa hiyo isingekuwa vyema kama ningekataa kuja kumtolea ushahidi .Nimekuita hapa ili unipe mwongozo wa kinachoendelea na ninachotakiwa kukisema mahakamani” akasema Happy
“Happy nimefurahi sana kusikia maendeleo yako na kukuona ukiwa ni mwenye furaha.Lakini kabla hatujaendelea na maongezi yetu aren’t you gonna ask?
“Ask what? Happy akashangaa
“How he’s doing”
“Savanna,Patrick ni mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote.Sijawahi kupenda mtu kama nilivyompenda yeye.Amenifanyia mambo mengi ambayo hakuna mtu yeyote anaweza akanifanyia.Patrick made me a woman.Kuna mengi ambayo naweza kueleza kwa siku nzima kuhusu Patrick lakini naweza kusema kwamba maisha ni kitu cha ajabu sana.Pamoja na upendo wote na kila kitu alichonifanyia Patrick lakini hivi sasa I’m fighting to forget him.Its difficult but I thank God I’m doing fine without him.Ninaamini mimi na Patrick hatukupangwa tuwe pamoja.” Akasema Happy akanyamaza akameza mate na kuendelea
“Sijataka kumuulizia kwa sababu ninajua mimi ni mtu ambaye hataki kuniona tena katika maisha yake na ana hasira kubwa na mimi kwanza kwa kuziona picha zile na pili kwa kuondoka na kumuacha gerezani.Savanna moyo wangu unaniuma sana japokuwa hakuna anayeweza kulifahamu hilo.Bado kitendo kile cha kudhalilishwa kwa zile picha chafu hakijapona na kurudi kwangu tena Tanzania kumekitonesha kidonda change.Sina hakika kama ulimueleza Patrick ukweli halisi wa kilichotokea.Japo kwa ufupi unaweza ukanieleza anaendeleaje?
“Patrick is fine.He’s doing ok.Tuliibadili kesi na kuwa kesi ya kuua bila kukusudia na akapatiwa dhamana.Anaendelea vizuri na maisha yake mapya na kwa sasa ni meneja wa kiwanda cha kusindika nyama.” akasema Savanna
“Ouh that’s great.Is he married ? akauliza Happy huku akitabasamu.Savanna naye akatabasamu
“Not yet”
“Ouh Gosh ! what he’s waiting for? Is he still waiting for me?
“Tunasubiri mambo haya yamalizike ndipo tuanze taratibu za ndoa yetu” akasema Savanna huku akitabasamu
“We? are you two together? Akauliza Happy kwa mshangao.
“Yes ! we’re together now.We live together though not yet married” akasema Savanna
Happy akavuta pumzi ndefu na kumeza fundo la mate.Akapatwa na kigugumizi akakohoa kidogo na kusema
“Congraturations guys” akasema Happy na sura yake ilionyesha mabadiliko kidogo.
“Thank you “ akasema Savanna.Ni wazi maneno yale ya Savanna yalimchoma Happy.Savanna aliligundua hilo na hakutaka kuendeleza maongezi kuhusu mahusiano yake na Patrick na badala yake akaendelea kumweleza Happy kuhusiana na mwenendo wa kesi na namna atakavyotoa ushahidi wake.Baada ya maongezi marefu Savanna akaondoka zake.

* * * *

Ni alhamisi siku ambayo Happy alitakiwa kusimama kizimbani na kutoa ushahidi wake.Siku hii aliamka mapema sana asubuhi akaanza kujiandaa.Alikuwa mkimya na mwenye wasi wasi.Mpaka ilipotimu saa tatu za asubuhi tayari alikwisha jiandaa tayari kabisa kuelekea mahakamani .Familia nzima ilikuwa imejiandaa kuandamana naye mahakamani.
“Are you ready Happy? akauliza mzee Kibaho
“I’m ready dady though I’m a bit nervous” akajibu Happy
“Be strong .You can do it” akasema mzee Kibaho
“Yes Dady.I’ll be strong.I need to finish this”
“Tuko pamoja Happy usiogope” akasema Margreth kisha kwa pamoja wakaingia garini na safari ya kuelekea mahakamani ikaanza.
Mahakama ilifurika watu tofauti na siku za kawaida.Tetesi za Happy kuwepo mahakamani siku hii zilisambaa na kuwafanya watu wafurike mahakamani ili kumuona mrembo huyu ambaye aliviteka vyombo vya habari miezi zaidi ya kumi iliyopita kutokana na skendo zake mbali mbali na hasa ile ya mwisho ambapo picha na video zake za utupu vilisambaa katika magazeti na mitandao na kisha akatoweka ghafla bila kujulikana alielekea wapi.Wengi walikuwa na hamu ya kumuona tena.
Saa tano na dakika ishirini,Happy aliwasili mahakamani akiwa ameongozana na familia yake.Pale mahakamani alipokewa na Savanna na kuongozwa kuelekea ndani ya jengo la mahakama.Wengi hawakuweza kumtambua kwa haraka kutokana na namna alivyokuwa amebadilika.
“Nashukuru sana umekuja Happy.Naomba ondoa wasi wasi” akasema Savanna
“Usijali Savanna.I’ll do my best” akajibu Happy huku uso wake ukijilazimisha kutabasamu
Savanna aliingia ndani ya mahakama na Happy akaufungua mlango wa chumba kimoja mle mahakamani akaingia ndani na kumuomba Happy naye aingie.Mara tu alipoingia ndani ya chumba kile Happy akapatwa na mstuko mkubwa.Alitumbua macho kana kwamba ameona mzuka au kitu cha kushangaza.Alibaki amesimama huku akihisi mwili wake kuingiwa na baridi.Alikuwa anatazamana na Patrick ambaye naye alipatwa na mstuko .Chumba kikagubikwa na ukimya mzito.Savanna ambaye alisimama katikati yao akawaangalia wote na kisha akasema
“I’ll be outside.I’ll leave you guys alone so that you can great each other” akasema Savanna na kutoka mle chumbani.Patrick na Happy waliendelea kutazamana huku wote wakiwa bado wamesimama.Baada ya kama dakika mbili Patrick akakohoa kidogo na kusema
“Hallow …Ha..Happy”
“Hallo Patrick” akajibu Happy kwa sauti ndogo yenye kutetemeka.Kimya kidogo kikapita Patrick akasema
“Nimefurahi kukuona tena Happy”
“Hata mimi nimefurahi kukuona tena Patrick” akajibu Happy.Baada ya maneno hayo machache ukatanda ukimya mzito mle chumbani.Hakuna aliyemsemesha mwenzake.Patrick akaketi kitini na kuinama chini.Happy akamtazama kwa makini na kutaka kusema neno akafumbua midomo yake lakini sauti ikakwama.
“ouh my gosh ! Hiki ndicho nilichokuwa nakikwepa.Sikutaka kuonana tena na Patrick ana kwa ana.Kwa nini Savanna amenikutanisha naye wakati tulikubaliana kwamba sitaki kuonana na Patrick? Ouh gosh ! Nitafanya nini sasa? .akawaza Happy ,akaufunika uso wake kwa viganja vya mikono.Machozi yalikuwa yanamtoka
“God please help me.Niko katika wakati mgumu sana.Kumbu kumbu zote za nyuma zimerejea ghafla baada ya kumuona tena Patrick.I feel so guilty.I don’t know what to do anymore.” Akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa Savanna akaingia
“Are you guys ok? Akauliza Savanna
“Yes ! we’re ok” akajibu Happy.Macho yake yalionekana kujaa machozi.Savanna akamuuliza
“Are you ready Happy?
“Yes ! Yes !.I’m ready” akajibu Happy huku akifuta machozi
“Patrick ni muda sasa wa kuingia mahakamani.” Akasema Savanna Patrick akainuka na kuelekea katika chumba cha mahakama.
“Savanna kwa nini umefanya hivi? Kwa nini umenikutanisha na Patrick? Akauliza Happy
“Happy ni vigumu kukwepa kuonana na Patrick lakini hata hivyo tutaongea baadae lakini kwa sasa hebu tuelekeze mawazo yetu katika jambo lililotuleta hapa” akasema Savanna huku akikusanya mafaili yake
“Usiogope Happy.Ondoa hofu.You can do it” akasema Savanna na kisha akaongozana na Hapyy kuelekea katika chumba cha mahakama.Happy alikuwa anamulikwa na mianga ya kamera za waandishi wa habari waliofika kwa wingi mahakamani

* * * *

Saa nane za mchana Happy alimaliza kutoa ushahidi wake.Toka mashahidi wa upande wa utetezi walipoanza kutoa ushahidi wao haikuwahi kutokea siku ambayo Mahakama ilikumbwa na simanzi kama siku hii ya leo.Watu wote walikuwa kimya kabisa wakimsikiliza Happy
Happy ambaye alikuwa anaongea kwa hisia kubwa na wakati mwingine kulazimika kusimama na kufuta machozi,alianza kwa kuielezea mahakama historia fupi ya mahusiano yake na Patrick toka walipokutana shuleni,wakajenga mahusiano hadi walivyopotezana baada ya yeye kuondoka na kwenda masomoni Marekani.Aliielezea mahakama namna Veronika alivyotunga uongo na kuwatenganisha yeye na Patrick hadi walipokuja kuonana tena siku aliyoshinda taji la miss Tanzania.Aliendelea pia kuielezea mahakama juu ya maamuzi waliyoamua kuyachukua kwa pamoja yeye na Patrick ya kuachana na wapenzi wao na kuurejesha tena uhusiano wao kwani bado walikuwa wanapendana.Alikiri kumpenda Patrick zaidi ya anavyoweza kueleza na ndiyo maana alikuwa tayari kuachana na mpenzi wake Mike na kuurejesha uhusiano wa kimapenzi na Patrick.
Happy aliieleza makahama kilichotokea jioni ile na kusababisha kifo cha Vero.Sehemu hii ilikuwa ni sehemu ambayo iliwatoa machozi watu wengi akiwamo Patrick ambaye alishindwa kuyazuia machozi kumchuruzika mashavuni pale Happy alipotamka kwamba Vero aliteleza na kujigonga ukutani wakati akinyang’anyana silaha na Patrick ,silaha ambayo alitaka kuitumia kufanya mauaji
Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake na mahakama kuahirishwa,Happy alitoka huku ameinamisha kichwa.Bado machozi yaliendelea kumtoka.Familia yake ilikuwa pamoja naye wakiongozana kutoka nje ya jengo la mahakama.Waandishi wa habari na wapiga picha waliendelea kumfuata Happy na kumpiga picha nyingi.Ili kuwakwepa waandishi wa habari waliokuwa wakimsonga Happy,familia yake ikamuwahisha katika gari na kufunga milango kabla gari halijaondoka Happy akaomba wasubiri alitaka kuongea na Savanna.Margreth akampigia simu Savanna na kumfahamisha kwamba Happy anahitaji kuonana naye.Baada ya kama dakika tano Savanna akafika
“Thank you Happy.You did great” akasema Savanna.Happy akafuta machozi na kusema
“Nini kitaendelea baada ya hapa?
“Tayari tumefunga ushahidi kwa upande wetu.Nitakufahamisha baadae nini kitakachoendelea” akasema Savanna ,kisha wakaagana na kuondoka
Baada ya kuachana na akina Happy,Savanna naye akaingia garini na Patrick wakaondoka .Hawakutaka kupita sehemu yoyote na moja kwa moja wakaelekea nyumbani.Ndani ya gari ,Patrick alikuwa kimya sana
“Say something my love” akasema Savanna baada ya kuona kimya kimezidi mle garini
“I have nothing to say my love” akasema Patrick
“Still thinking about her?
“No ! She’s not in my thoughts anymore.Ninachowaza ni nini kinakwenda kutokea baada ya hapa”
“Usihofu Patrick.Niamini ninachokwambia kwamba mpaka hapa tumefanya vizuri sana na nina hakika tutashinda kesi hii.Ushahidi uliotolewa ni dhahiri unaendana na hoja tuliyoijenga ya kuitaka mahakama ikuache huru.” Akasema Savanna
“Nilihitaji sana kuonana na Happy ana kwa ana.Nina maswali mengi ambayo nataka anijibu lakini mara tu nilipomuona sikuweza tena kuwa na ujasiri wa kumuuliza chochote.” Akawaza Patrick
“Happy amebadilika sana.Uzuri wake umeongezeka maradufu.Inaonekana ameridhika na maisha anayoishi sasa.She’s already forgoten about me.Kweli dunia ina maajabu sana.Happy msichana ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote na tuliwekeana ahadi lukuki kwamba hatutaachana hadi kifo kitutenganishe lakini leo hii tumetazamana kama hatujuani,kama hatujawahi kuwa katika mahusiano.Nilipoteza kila kitu kwa ajili yake lakini pamoja na mambo yote aliyonitendea hakuthubutu hata kusema samahani kwa mambo aliyoyafanya.Inaonekana hajutii kabisa kitu alichokifanya.” Akawaza Patrick
“I was so stupid kuamua kuacha kila kitu kwa sababu yake nikiamini kwamba ndiye mwanamke ambaye ananifaa maishani.Nilikuwa na upofu wa fikra nikiamini kwamba hakuna mwanamke mwingine ambaye anafanana naye.Nilifanya kosa kubwa sana.Kwa sababu yake nimempoteza Vero mwanamke aliyenipenda kwa moyo wake wote,nimempoteza baba yangu,marafiki na nilipoteza hata dira na mwelekeo mzima wa maisha yangu na mwishowe na yeye mwenyewe akanikimbia na kuniacha nikiteseka gerezani.Anyway sitakiwi kuwaza sana kuhusu mambo haya.Yaliyopita yamepita na kinachotakiwa kwa sasa ni mimi kuelekeza nguvu na akili yangu katika kuyajenga maisha yangu na Savanna.Hata hivyo Happy amenifundisha kitu kimoja kikubwa.Amenisaida kumjua binadamu ni kiumbe wa namna gani.” akawaza Patrick halafu akageuza shingo yake na kumtazama Savanna ambaye naye aligeuza shingo yake wakatazamana na kutabasamu
“Why you are looking at me like that?
“Its nothing Savanna.” Akasema Patrick na kutabasamu halafu akaegemeza kichwa chake kitini.
“Namshukuru sana Mungu kwani pamoja na yote yaliyotokea lakini bado ameendelea kuwa upande wangu na ameniletea tena mwanamke mwingine ambaye ninaamini ndiye aliyeumbwa kwa ajili yangu.Savanna ananipenda kwa moyo wake wote .Amekuwa nami toka matatizo haya yalipotokea .Amenipigania kwa nguvu zake zote.Ananijali na kuniheshimu.Ni yeye ndiye aliyeokota vipande vya moyo wangu uliovunjwa vunjwa na Vero akaviunga na kunifanya nirejee tena katika maisha yangu ya kawaida.Yeye ni sababu ya mimi kuamua kupenda tena.Hakika huyu ndiye mwanamke ambaye nitampenda kwa moyo wangu wote na kwa siku zote za uhai wangu.Hata siku moja sintathubutu kumtoa chozi.Wanawake kama yeye ni nadra sana kuonekana zama hizi zilizojaa ulaghai.Najiona ni mtu mwenye bahati kubwa sana kuwa na Savanna na nitamuomba Mungu atujalie maisha mazuri na yenye furaha” akawaza Patrick halafu akamgeukia Savanna na kumtazama
“I love you Savanna.I love you so much.I just want you to know that you mean a lot to me” akasema Patrick na kumfanya Savanna atabasamu.akauchukua mkono wa kulia wa Patrick na kuubusu.
“I love you too Patrick more than words can say” akasema Savanna na safari ikaendelea
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 56
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Wanawake kama yeye ni nadra sana kuonekana zama hizi zilizojaa ulaghai.Najiona ni mtu mwenye bahati kubwa sana kuwa na Savanna na nitamuomba Mungu atujalie maisha mazuri na yenye furaha” akawaza Patrick halafu akamgeukia Savanna na kumtazama
“I love you Savanna.I love you so much.I just want you to know that you mean a lot to me” akasema Patrick na kumfanya Savanna atabasamu.akauchukua mkono wa kulia wa Patrick na kuubusu.
“I love you too Patrick more than words can say” akasema Savanna na safari ikaendelea

ENDELEA…………………

“Happy jitahidi ule walau kidogo.Nyamaza kulia” Margreth alikuwa anambembeleza Happy ambaye toka wamerejea amekuwa akilia
“Margreth ninajuta ni kwa nini nimerudi Tanzania” akasema Happy huku akifuta machozi.
“Usiseme hivyo Happy.Umefanya jambo la maana sana kuja kutoa ushahidi wako kwa Patrick”
“Nilidhani nimekwisha msahau Patrick na hayupo tena moyoni mwangu lakini nilikuwa najidanganya”
“kwa nini unasema hivyo Happy?
“Margreh sikufichi mara tu nilipoonana na Patrick moyo wangu ulistuka .Nilihisi kama moyo wangu unataka kusimama.Nilikosa kitu cha kuongea,midomo ilikuwa inanitetemeka .Mwili wote ulikuwa wa baridi.Ouh gosh !!” akasema Happy
“Pale mahakamani nilikuwa natoa ushahidi wangu huku machozi yananitoka kutokana na uchungu niliokuwa nao moyoni baada ya kuonana tena na Patrick.Historia nzima ya maisha yangu ya nyuma ilirudi tena .Niliona aibu kubwa ,nilijisikua uchungu mkubwa na kuutambua ujinga nilioufanya wa kuamua kuondoka na kumuacha Patrick akiteseka gerezani” akasema Happy akainama na kukishika kichwa chake.Margreth akamtazama na kusema
“Sasa utafanya nini Happy?
“I don’t know what to do Margreth.Nahisi kuchanganyikiwa kabisa.Sijui nifanye nini” akasema Happy
“Kwa nini usifanye mpango wa kuonana na Patrick ili muongee na muyaweke sawa mambo haya? Nadhani mkikaa na kuyaongea mambo haya na mkaombana msamaha nyote mtabaki na amani.Nina hakika hata yeye mwenyewe ana hamu ya kuongea na wewe.Nadhani ni wakati muafaka sasa wa Patrick kufahamu kilichotokea.Hata wewe mwenyewe umekuwa mgumu sana kueleza kuhusu tukio lile na hata sisi ndugu zako mpaka leo hii hatufahamu nini kilitokea na ni akina nani waliokutenda kitendo kile.Naona ni wakati muafaka sasa wa kuliweka wazi jambo hili.Nina hakika hata Patrick angependa kusikia sababu iiliyokufanya ukaondoka ghafla na kumuacha peke yake gerezani.” Akasema Margreth
“Margreth kwa mara ya kwanza najilaumu sana kwa jambo nililolifanya.Nimetambua kosa langu.Nilipaswa kusimama imara na kueleza kilichotokea.Sikupaswa kuikimbia nchi.Sikupaswa kumuacha Patrick peke yake gerezani.Kwa hivi sasa nimechelewa sana na hakuna ambaye ataniamini hata nikisema ukweli.Natamani nipate walau dakika hata mbili za kuongea na Patrick na kumfahamisha juu ya kilichotokea na kumuomba anisamehe.lakini….” Happy akasita
“lakini nini Happy?
“Patrick has moved on.Tayari yuko katika mahusiano na Savanna na wana mipango ya kufunga ndoa mara tu baada ya kumalizika kwa kesi” akasema Happy
“Tell me you are jocking.!!!! Margreth akashangaa
“Si utani Maggie.Haya ni maneno toka katika kinywa cha Savanna mwenyewe”
“Gosh .! akasema Margreth
“Hiyo ndiyo hali halisi.Maisha yana maajabu sana” akasema Happy kwa huzuni
“I think there must be ana explanation to this.Hainiingii akilini kabisa.Ninachofahamu ni kwamba Parick anakupenda sana na yuko tayari hata kufanya jambo lolote kwa ajili yako.Mambo aliyoyafanya Patrick kwako ni makubwa sana na yananifanya nisiwe mwepesi kuamini kama ni kweli Patrick anaweza akahamisha penzi lake kwa Savanna katika kipindi kifupi namna hii”akasema Margreth.Happy akamtazama mdogo wake na kusema
“Margreth bado kuna mambo mengi ambayo hujayafahamu bado lakini kitu kimoja ambacho napenda ufahamu ni kwamba I’m no longer in Patrick’s heart”
“Kwa nini unasema hivyo Happy? Una hakika na unachokisema?
“Mbona umelin’ang’ania sana suala la kutaka kuonana na Patrick ? Akauliza Happy
“Naomba usinielewe vibaya Happy.Lengo langu si kutaka wewe na Patrick mrudiane kwani hilo ni jambo ambalo haliwezekani kwa sasa kwani kila mmoja tayari amekwisha anza maisha mapya.Ninachokitaka mimi ni wewe na Patrick mkutane muongee na mzimalize tofauti zenu ili muishi kwa amani.Kama hutafanikiwa kuonana na Patrick na ukamfahamisha kilichotokea ,nina hakika hautakuwa na amani kwa maisha yako yote yaliyobakia kwa sababu ni wewe ndiye uliyeondoka bila kumtaarifu chochote Patrick.Kama alifanikiwa kuziona picha zile na jinsi ulivyoondoka ghafla bila taarifa yoyote ni wazi Patrick ataelewa kwamba ulifanya kitendo kile .Suluhisho hapa ni wewe kuonana na Patrick mkaongea na ukamueleza kila kitu bila kumficha.I swear to god you’ll be free “
“Margreth sikatai ushauri wako kwani hata mimi ninahitaji sana kupata nafasi ya kuonana na Patrick lakini laiti ungeuona uso wa Patrick leo mara tu niliponana naye ungekubaliana na ninachokisema kwamba siko tena katika moyo na akili yake.He hates me.I deserve all that for what I did to him.It hurt so much” akasema Happy na kushindwa kuvumilia kutokwa na machozi
“Usilie Happy.Kama kweli una nia ya dhati ya kuonana na Patrick ili muongee na kuyaweka sawa mambo haya basi tunatakiwa tutafute njia.”
“Nahitaji sana kuonana na Patrick lakini sijui ni kwa namna gani nitafanikiwa kwa hilo” akasema Happy
“Happy I‘m your sister and a friend too so tell me the truth” akasema Margreth
“What truth?
“Do you still love Patrick?
“Baada ya kurejesha uhusiano wangu na Mike niliamini kwamba Patrick amekwisha toka moyoni mwangu lakini baada ya kuonana naye leo nimegundua kitu kimoja” Happy akasita na kutazama chini.
“Umegundua kitu gani Happy? Akauliza Margreth
“I was so wrong.Patrick ni mtu ambaye siwezi kumfuta kirahisi katika moyo wangu.To answer your question Yes I still love him.” Maneno yale yakamfanya Margerth akae kimya kwa muda akamuangalia dada yake.

* * * *

Ni saa nne za usiku,Linah rafiki mkubwa wa Loniki alikuwa amejilaza katika sofa kubwa lililokuwa sebuleni.Kama ilivyokuwa kwa watu wengine wenye ukaribu na familia ya Vero,Linah naye alikuwepo mahahakani kusikiliza ushahidi wa Happy.Baada ya kutoka mahakamani alirejea moja kwa moja nyumbani kwake.Toka amerudi alikuwa amejilaza katika sofa hili akitazama runinga huku katika meza ndogo iliyokuwa pembeni kulikuwa na chupa kubwa ya mvinyo
“Leo nilipomuona Happy mahakamani moyo wangu ulistuka sana.Niliumia mno hasa nikikumbuka kitendo tulichomfanyia.Kwa nini nilikubali kushirikiana na Loniki kumfanyia Happy mambo yale? Najilaumu sana kwa jambo lile.Happy hastahili hata kidogo kufanyiwa ukatili wa namna ile.” akawaza Linah halafu akachukua glasi yake ya mvinyo na kupiga funda kubwa
“Maelezo aliyoyatoa mahakamani yalinitoa machozi.Aliongea kwa uchungu sana na kwa hisia kubwa.Wote tuliokuwa hatufahamu historia yake na Patrick leo tumeufahamu ukweli.Sioni sababu ya kuwalaumu Patrick na Happy kwa sababu aliyeanzisha haya yote ni Vero pale alipodiriki kutunga uongo na kuwatenganisha.Uongo wake umekuja kumuumbua na badala yake akataka kufanya mauaji.Stupid girl” akawaza Linah na kuchukua glasi yake ya mvinyo akanywa
“Naungana na yule wakili anayeongoza jopo la mawakili wanaomtetea Patrick kuitaka mahakama imuachie huru Patrick.Hakuna kesi ya maana hapa.Nasikitika niliingia kichwa kichwa katika jambo hili kabla sijaufahamu ukweli halisi.Sitaki tena kushirikiana na Loniki” akawaza Linah lakini ghafla akastuka
“Mhh !! Inabidi nitumie akili nyingi ili kuanza kumkwepa Loniki na kumfanya asiendelee na mipango yake ya kulipiza kisasi.Mpaka sasa lengo lake bado halijabadilika. Bado anataka Patrick auawe.Amekuwa akinitumia fedha nyingi ili niweze kusuka mipango ya kumuua Patrick.,fedha ambazo nimekuwa nikigawana na Khumalo.Iwapo atagundua kwamba nilikuwa namdanganya na kwamba hakuna mpango wowote wa kumuua Patrick basi lazima kutazuka vita kubwa sana kati yangu naye.Ngoja kwanza nimpigie simu nimpe taarifa za kilichotokea leo mahakamani” akawaza Linah na kuinuka akachukua simu yake akampigia Loniki.
“hallow Loniki,habari za London?
“London kwenda,habari za huko nyumbani?
“Huku nako ni kwema kabisa” akasema Linah na kuvuta pumzi.Sauti ya Loniki ilionyesha ni kama mtu ambaye hakuwa na furaha kama ilivyozoeleka
“Mama kanipigia simu na kuniambia kwamba Happy alikuwepo mahakamani leo na ametoa ushahidi wake” akasema Loniki
“Ndiyo Lonny,Happy ametokea mahakamani leo na ametoa ushahidi wake “ akajibu Linah
“Vipi kuhusu mwenendo mzima wa kesi? Akauliza Loniki
“Lonny pamoja na jitihada zote tulizozifanya,naomba niwe wazi kwako kwamba kutokana na ushahidi uliotolea mahakamani na upande wa utetezi na hasa huu ambao umetolewa leo na Happy,tuna kazi ngumu ya kufanya kuhakikisha kwamba Patrick anafungwa.Niliongea na mwanasheria mmoja wa serikali na akaniweka wazi kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani ni mzito sana na unatosha kabisa kuishawishi mahakama kumuachia huru Patrick”
“Damn it !!..That wont happen..!! akaongea Loniki kwa ukali
“Linah nilikuachia kazi hii na ukanihakikishia kwamba utafanya kila uwezalo na kuhakikisha kwamba Patrick anauawa au anafungwa gerezani .Nimekuwa nakutumia fedha nyingi kwa ajili ya kufanikisha hayo sasa iweje leo unipe kauli yenye utata namna hiyo? Unataka kunihakikishia kwamba juhudi zote tulizofanya na mamilioni yote ambayo nimekuwa nakutumia wewe na Khumalo nimetwanga maji kwenye kinu? Akauliza Loniki
“Loniki wewe ni zaidi ya rafiki kwa hiyo naomba uniamini kile ninachokwambia.Ni kweli mipango ilifanyika na kama nilivyokueleza .Nimekwisha hakikishiwa na watu wazito mahakamani kwamba Patrick lazima afungwe hata kama kutatolewa ushahidi wa aina gani.Kwa hiyo usiwe na wasi wasi Loniki” Linah akamdanganya Loniki
“Sawa Linah.Naomba iwe hivyo lakini endapo itatokea vinginevyo sijui itakuaje kwa sababu tumepoteza fedha nyingi sana mpaka sasa na hakuna matunda yoyote.Lengo langu mimi lilikuwa kuwaua Patrick na Happy lakini ni wewe Na Khumalo ndio mliopinga jambo hilo kwa hiyo basi hakikisheni kwamba kwa vyovyote itakavyokuwa kama haitawezekana kumuua basi lazima Patrick afungwe gerezani.Endapo mtashindwa kulitekeleza hilo basi nitarudi mimi mwenyewe na safari hii sintakuwa na namna nyingine zaidi ya kutafuta watu wengine na kuwaua Patrick na Happy.Inaniuma sana kuwaona washenzi hawa wakiendelea kuvuta hewa hii safi wakati mdogo wangu waliyemkatili uhai wake anaoza kaburini.” Akasema Loniki kwa ukali
“Loniki naomba unisiklize vizuri.Suala hili si jepesi kama unavyolifikiri.Tulilipinga wazo lako la kutaka Patrick na Happy wauawe kutokana na athari ambazo zingeweza kujitokeza.Lakini kwa kuwa lengo lako lilikuwa ni kulipa kisasi ndiyo maana tukapendekeza kwamba badala ya kufanya mauaji basi tuyafanye maisha yako yawe magumu na Patrick afungwe kigerezani.Hicho ndicho nimekuwa na kifanya na Khumalo muda huu wote..” akasema Linah ambaye alikuwa ameukunja uso wake kwa hasira. Na mara simu ikakatwa
“Amekata simu Sitaki tena kujihusisha na mipango ya Loniki.Sitaki kutafuta mgogoro na vyombo vya dola kwa sababu ya hivi vimilioni alivyokuwa ananitumia.Ninayamudu maisha yangu mwenyewe.Biashara zangu zinaniingizia fedha nyingi na kunifanya niishi kama binti mfalme.Patrick na Happy hawana kosa lolote la kustahili kutendewa hivyo anavyotaka..Najua atakuwa amekasirika lakini simuogopi hata kidogo.Tena ngoja nimpigie simu Khumalo nimueleze kuhusiana na ujinga wa Lonny” akawaza Linah

* * * *

Saa nne za usiku Happy bado alikuwa amekaa kitandani.Alikuwa ameegemea kitanda macho yake yamemvimba
“Happy tafadhali usiendelee kulia.Toka umerudi umekuwa unalia.Tafadhali usilie tena.Inatosha sasa” akasema Margreh aliyekuwa pembeni ya dada yake
“let me cry Margreth.Nina uchungu mwingi sana na sijui nifanya nini.I’m confused” akasema Happy.Margreth akamtazama dada yake usoni akainuka na kuiendea meza ndogo akachukua simu
“Mpigie savanna sasa hivi na umwambie kwamba unahitaji kuonana na Patrick” akasema Margreth.Happy akamtazama na kusema
“Are you sure you want me to do this? Akauliza Happy
“Happy kama kweli una nia ya dhati ya kutaka akili yako itulie na maisha yako yawe na amani tafadhali ongea na Patrick”
“Nitamwambia kitu gani? Ninaogopa Margreth”
“Ukweli.Mweleze ukweli” akajibu Margreth na kuzitafuta namba za Savanna akapiga
“Hallow” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Hallow Margreth…!! Akasema tena Savanna.Happy akakohoa kidogo na kusema
“Savanna its me Happy”
“Ouh Happy.How are you my dear? Akasema Savanna
“I’m ok Savanna”
“Nafurahi kusikia kwamba unaendelea vizuri”
“Yah !..” akasema Happy
“Happy napenda nikushukuru sana kwa kitendo ulichokifanya leo.You did it so well” akasema Savanna
“Yah ! akajibu Happy na kumfanya Savanna astuke kidogo
“Happy are you ok? Akauliza Savanna.Happy hakujibu kitu
“Happy is there anything wrong? Akauliza tena Savanna
“Savanna I’m sorry to disturb you at this time” akasema Happy
“Usijali Happy.Hujanisumbua chochote.Muda wowote unaruhusiwa kunipigia simu.Una tatizo lolote Happy? Akauliza Savanna.Happy akasita kidogo kisha akasema
“Savanna unaweza kuniruhusu niongee na Patrick japo kwa dakika mbili? Akasema Happy.Savanna akasita kidogo na kusema
“Hakuna tatizo Happy.Patrick huyu hapa ongea naye” akasema Savanna na kumpatia Patrick simu
“Happy anahitaji kuongea nawe” akasema Savanna.Patrick akamtazama usoni
“Ongea naye”akasisitiza Savanna.Patrick akaiweka simu sikioni
“Hallow” akasema
“Hallow Patrick “ akajibu Happy
“Are you ok ? akauliza Happy
“I’m ok” akajibu Patrick kwa ufupi
“Savanna ameniambia kwamba unataka kuongea na mimi” akasema Patrick
“Ndiyo Patrick.Kwanza samahani sana kwa kukusumbua”
“Bila samahani Happy”
“Patrick sina hakika kama utakuwa tayari lakini nahitaji kukuona.Nina maongezi nawe ya maana sana”
“Maongezi na mimi?! Patrick akashangaa
“Ndiyo Patrick.Nina maongezi nawe kidogo”
“Unataka tuongee kuhusu nini Happy?
“Patrick kuna mambo ambayo nahitaji kukueleza.Kuna mambo ya maana sana ambayo unahitaji kuyafahamu”
“mambo hayo huwezi kunieleza simuni sasa hivi?
“hapana Patrick.hatuwezi kuongea simuni.Nahitaji sana kuonana nawe ana kwa ana” akasema Happy
“Sawa Happy niko tayari kuonana nawe ili unieleze hicho unachotaka kunieleza lakini nina sharti moja tu kwamba lazima na Savanna kipenzi cha roho yangu awepo.Yeye anastahili kufahamu kila kinachoendelea katika maisha yangu.Uko tayari kwa hilo? Akauliza Patrick lakini ghafla simu ikakatika ‘
“Amekata simu” akasema Patrick
“Mpigie pengine ni tatizo la kimawasiliano” akasema Savanna
“Hakuna sababu ya kumpigia.Isitoshe sina mpango na sihitaji kuonana naye sasa na katika maisha yangu yote yaliyobaki.Biashara ya mimi na yeye ilikwisha pale alipoamua kuondoka na kunitelekeza gerezani” akasema Patrick
“Pengine ana jambo la maana anataka kukwambia” akasema Savanna
“Hana tena jambo lolote la maana ambalo anaweza akanieleza.Ninachoshukuru ni yeye kukubali kuja kunitolea ushahidi na baada ya hapo mimi naye hatuna tena mahusiano.Mahusiano yangu naye yaliisha alipoondoka na kunitelekeza gerezani” akasema Patrick. Savanna akamuangalia na kuuliza
“Why are you avoiding her?
Patrick akamvuta Savanna karibu yake akambusu .
“It’s because I have you now.Sihitaji kuiumiza akili yangu kwa mambo yaliyokwisha pita.Ninachokiangalia hivi sasa ni maisha yangu na mbele nikiwa nawe malaika wangu.Nakupenda sana Savanna zaidi ya ninavyoweza kueleza” akasema Patrick na kumbusu tena Savanna mdomoni
Suala la Patrick kuweka sharti la kuongozana na Savanna lilimuumiza sana moyo Happy na kumfanya akate simu na kuitupa kitandani
“Damn you Patrick..How could you do that to me? Happy akahamaki
“Patrick kasemaje? Akauliza Margreth
“Amesema hawezi kuonana nami hadi aongozane na mpenzi wake Savanna.Margreth I’ve lost him..I’ve lost Patrick.” akasema Happy kwa uchungu
“Usiseme hivyo Happy.Kama kweli bado unampenda kwa dhati,tafuta namna utakayoweza kumtafuta mkakaa na kuliongea jambo hili.” Margreth akajaribu kumpa moyo dada yake
“No way Margreth.Nimeshampoteza Patrick.Tayari yuko katika mahusiano mengine na amekwisha nisahau.Sitaki tena kuingilia mahusiano yake kwani nimekwisha jifunza wakati ule wa Vero.Ni kosa langu na ninastahili kuteseka kwa maisha yangu yote.Sikupaswa kukimbia na kumuacha Patrick peke yake gerezani.Kitendo kile kimemfanya Patrick anichukie sana na hata nilipomtazama machoni niliona wazi kwamba ananichukia mno” akasema Happy
“Sasa utafanya nini Happy?
“Sina cha kufanya tena.Its my mistakes and I cant blame anybody”
“will you be ok?
“No ! I’ll never be ok in my life but I’m going to try living my life without him .Margreth my life will never be the same again.Patrick ndiye alikuwa ni kila kitu kwangu”
Margreth akamtazama dada yake kwa huruma na kusema
“Laiti ningekuwa na njia yoyote ya kuweza kufanya ili kuurejesha tena uhusiano wako na Patrick ningefanya hivyo lakini nasikitika sina namna yoyote ninayoweza kufanya kwa sasa.May be the best thing is to let him go for good” akasema Margreth
“May be that’s the best way for now. Its obvious me and Patric we’re finished.Patrick atabaki kuwa sehemu ya kumbu kumbu yangu .Pamoja na hayo sintaondoka Tanzania hadi hukumu yake itakapotolewa.Nataka niwepo siku hiyo ya hukumu.” Akasema Happy
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 57
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Laiti ningekuwa na njia yoyote ya kuweza kufanya ili kuurejesha tena uhusiano wako na Patrick ningefanya hivyo lakini nasikitika sina namna yoyote ninayoweza kufanya kwa sasa.May be the best thing is to let him go for good” akasema Margreth
“May be that’s the best way for now. Its obvious me and Patric we’re finished.Patrick atabaki kuwa sehemu ya kumbu kumbu yangu .Pamoja na hayo sintaondoka Tanzania hadi hukumu yake itakapotolewa.Nataka niwepo siku hiyo ya hukumu.” Akasema Happy

ENDELEA…………….

Abiria waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la British airways walianza kutoka nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.Miongoni mwao alikuwamo Loniki akitokea jijini London Uingereza anakoishi.Linah rafiki yake mkubwa alikuwepo uwanjani kumpokea.
“Karibu tena nyumbani Lonny” akasema Linah huku akikumbatiana na Loniki
“Ahsante sana Linah.Wow ! Unazidi kunawiri” akasema Loniki na wote wakacheka kisha wakaondoka pale uwanjani.
“Mambo yanakwendaje Linah? Akauliza Loniki wakiwa garini
“Mambo ni kama vile nilivyokwambia Lonny.Tunasubiri siku ya hukumu”
“Vizuri sana.Mambo yote umeyaweka sawa?
“Kwa mujibu wa mtu ambaye yuko ndani ya mahakama ambaye ndiye tunamtumia kurekebisha mambo ametuhakikihsia kwamba kila kitu kimewekwa sawa na kwamba Patrick lazima atafungwa.”
“Nafurahi kusikia hivyo.Khumalo ana taarifa kwamba ninakuja na tunakwenda kuonana naye usiku huu?
“Ndiyo.Nilimtaarifu mapema na amenielekeza mahala ambako tutamkuta”
“Ok thats good” akasema Lonny na safari ikaendelea
Ni siku tatu zimebaki kabla ya hukumu ya Patrick kutolewa.Hii ndiyo iliyomsukuma Loniki na kumlazimu aje mara moja ili kufanikisha mipango yake ya kuhakikisha kwamba Patrick anafungwa gerezani baada ya mipango ya kumuua kuonekana kugonga mwamba.
“Lonny ..!! akaita Linah.Loniki akageuka na kumtazama
“Itakuaje iwapo itatokea mahakama ikamuachia huru Patrick?
Loniki akatabasamu kidogo na kusema
“I will kill him myself.Hicho ndicho kitu ambacho kimenirejesha nyumbani.Kama mahakama itamuachia huru Patrick lazima afe.Sintakubali kumuona akiendelea kuishi kwa furaha wakati mdogo wangu ameoza kaburini.Lazima naye afe na ndiyo maana usiku huu nataka nikamtaarifu Khumalo ili alifahamu hilo.Kwa nini umeuliza?
“Never mind its nothing” akajibu Linah na safari ikaendelea kimya kimya hadi walipofika katika klabu moja ya usiku ambako ndiko Khumalo alikokuwa anastarehe.Waliingia pale klabuni na kuelekea moja kwa moja sehemu alipo Khumalo.Alikuwa amezungukwa na mabinti watatu wazuri waliovaa nusu utupu.Mara tu alipowaona Linah na Loniki akawaondoa wale mabinti na kuwakaribisha
“Pole na safari Lonny” akasema Khumalo
‘Nashukuru nimefika salama.Habari za huku?
“Habari za huku nzuri .maisha yanaendelea kama unavyoona” akasema Khumalo na kucheka kidogo halafu akatoa pakiti la sigara akatoa moja na kumrushia Lonny naye akatoa sigara moja akawasha na kuendela kuvuta
“Maisha ni mazuri na matamu.Sina sababu yoyote ya kulalamika” akasema Khumalo
“yah ! Hata mimi naona” akajibu Lonny huku akipuliza moshi mwingi hewani
“Linah alinitaarifu kwamba utafika jioni ya leo na kwamba ulihitaji kuonana nami.Nilistuka kidogo nikajua lazima una suala zito ambalo huwezi kulala bila kuniona”
“Ndiyo Khumalo.Nadhani unafahamu kilichonirejesha nyumbani”
“Nafahamu Loniki na hukuwa na sababu ya kuacha kupumzika na kuja kuniona.”
“Nisingeweza kupata usingizi bila kukuona.Kama unavyofahamu hukumu ni jumanne ijayo.Nataka Kujua mipango inaendaje.Mmejiandaa vipi?
“Kujiandaa kwa nini Lonny? Ninavyofahamu mimi ni kwamba tuliufuta mpango wa kumuua Patrick na tumekuwa tukifanya kila linalowezekana ili Patrick ahukumiwe kifungo kirefu gerezani.Hayo si ndiyo yalikuwa makubaliano yetu?
“Ndiyo Khumalo lakini kuna mambo mawili ambayo yanaweza yakatokea hapa.Patrick anaweza akafungwa au akachiwa huru.Endapo ikitokea akahukumiwa kifungo gerezani basi biashara na wewe itakuwa imekwisha lakini ikitokea kwamba ataachiwa huru na mahakama basi kazi bado itaendelea.Lazima Patrick auawe.Siko tayari kumuona Patrick akiendelea kutamba mtaani wakati alimuua mdogo wangu kwa makusudi kabisa” Loniki aliongea pasi na masihara
“Hilo ni suala ambalo halina tatizo.Kama ataachiwa huru na mahakama basi tutatekeleza huo mpango wako wa kumuua.Lakini naomba utambue kwamba kama ukitaka Patrick auawe itatulazimu tuongee biashara mpya”
Loniki akastuka sana baada ya kauli ile ya Khumalo
“Fedha !!...” akauliza Khumalo kwa mshangao.
“Ndiyo Lonny.Unatakiwa kuongeza fedha kwani itakuwa ni kazi nyingine.”
“You are kidding Khumalo.Nimekuwa nawatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kazi hii.Mnataka tena niongeze fedha nyingine?
“Loniki pesa ulizokuwa unatuma zote tumezitumia katika kusuka mipango ili Patrick aweze kufungwa.Na kama unavyofahamu hii ni kama bahati nasibu.Mnaweza mkatumia fedha na mkashindwa vile vile kwa hiyo endapo itatokea Patrick ataachiwa huru na ukataka auawe basi itakulazimu kuongeza fedha.Kitu kingine naomba ufahamu kwamba mimi huwa sipendi kuzungumzia mambo ya biashara au kazi katika sehemu za sterehe.Nimewaheshimu sana na ndiyo maana nimekubali kuonana nanyi kati kati ya starehe zangu.Kwa hiyo sitaki tuendele kubishana.Naomba jibu moja kama utaongeza fedha au utatafuta mtu mwingine wa kukufanyia kazi yako? Akasema Khumalo.Loniki akaingiwa na woga kwa namna Khumalo alivyokuwa amebadilika
“Manataka niongeze shilingi ngapi? Akauliza Loniki huku ameukunja uso wake
“millioni arobaini” akajibu Khumalo.Lonny akasimama na kushika kiuno chake akamtazama Khumalo kwa jicho la kali.
“Milioni arobaini?
“Ndiyo.Si fedha nyingi kwa kazi kama hiyo unayoitaka ya kutoa uhai wa mtu.Kama utaona ni nyingi naomba utafute mtu mwingine.”
Loniki akainama akafikiri na kusema
“Nitaangalia namna ya kufanya.Tusubiri kwanza hukumu itolewe” akasema Loniki akiwa na hasira akamshika mkono Linah wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa akina Loniki wakaagana na Linah akaanza safari ya kurejea kwake.
“Loniki ni mtu mwenye roho mbaya sana.Bado nia yake ya kumuua Patrick iko pale pale.Hapana siko tayari kumuacha afanikishe mipango yake hiyo.I have to do something to stop her.Ninachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuonana na Sarah.Kwa pamoja tunaweza kumzuia asifanye mpango wowote wa mauaji.Mimi peke yangu siwezi kumshauri aachane na mipango hiyo kwa sababu nimeshiriki kuanzia mwanzo na tayari nimekwisha tumia fedha zake nyingi nikimdanganya kwamba kuna mipango ninaisuka ili Patrick afungwe gerezani.Najua Sarah atataka kuufahamu ukweli wote lakini sina namna nyingine itabidi nimueleze kila kitu kuhusiana na uchafu wa Loniki” Akawaza Linah akapunguza mwendo wa gari na kuchukua simu yake akazitafuta namba za simu za Sarah na kumpigia.
“Hallow Sarah” akasema Linah baada ya Saraha kupokea simu
“Hallow Linah,habari yako? Nimestuka sana baada ya kuiona simu yako mida hii.Si kawaida yako kunipigia simu hasa kwa nyakati kama hizi’ akasema Sarah
“Samahani Sarah kwa kukusumbua.Ni kweli sijawahi kukupigia simu kwa muda kama huu lakini imenilazimu kufanya hivyo leo.Saraha nina shida na wewe ya muhimu sana.Nahitaji kuonana nawe usiku huu kuna jambo la muhimu mno nataka tuongee”
“Linah mbona unanipa wasi wasi? Kuna tatizo gani? akauliza Sarah kwa wasi wasi.
“Usihofu Sarah ni mambo ya kawaida tu ya kuelekezana.Uko wapi sasa hivi?
“Niko nyumbani kwangu.Wewe uko wapi?
“Niko barabarani,nimetoka kumpeleka Loniki nyumbani”
“Loniki !!!...Sarah akashangaa.
“Ndiyo .Ina maana huna taarifa kwamba Loniki anakuja leo?
“Hapana Linah.Sina taarifa yoyote ile kuhusu Lonny.Unajua mimi na dada yangu hatuna maelewano mazuri toka ulipotokea msiba wa Vero kwa hiyo mawasiliano kati yetu si mazuri”
“Yah ! nalifahamu hilo Sarah.Kwa hiyo tunaweza kuonana usiku huu?
“Unaweza ukaja nyumbani kwangu? Unajua siwezi kutoka usiku huu kwani mume wangu amerejea usiku huu kwa hiyo siwezi kuondoka na kumuacha peke yake”
“Nmekuelewa Sarah.Ninakuja hapo hapo nyumbani kwako.” Akajibu Linah na kukata simu
Ilimchukua zaidi ya dakika arobaini kufika nyumbani kwa Sarah.Akafunguliwa geti na kuingia ndani.
“Karibu sana Linah.” Akasema Sarah
“Ahsante sana Sarah.Ni muda mrefu hatujaonana”
“Kweli Linah.karibu sana”
“Nashukuru sana Sarah.Lakini nisingependa kukupotezea muda zaidi .Tunaweza tukaongea hapa nje?
“Hapana Linah.Twende tukaongelee ndani“ Sarah akamuongoza Linah hadi katika chumba cha maongezi
“Linah umenistua sana leo.Kuna tatizo gani? akauliza Sarah akiwa na shauku ya kutaka kufahamu kilichomleta Linah nyumbani kwake usiku ule
“Usiogope sarah.Nimelazimika kuja usiku huu kutokana na unyeti wa jambo lenyewe.Sarah kilichonileta hapa ni kuhusiana na Loniki”
“Loniki kafanya nini tena?! Saraha akashangaa
“Ni hadithi ndefu kidogo lakini nitajaribu kukuelezea kwa ufupi.Ni kwamba kwa muda mrefu sasa Loniki amekuwa katika mikakati ya kuhakikisha analipiza kisasi kwa wale waliosababisha kifo cha Vero,hapa anawalenga Patrick na Happy”
“Yah ! Nilijua toka mwanzo kwamba Lonny alikuwa na mpango wa kulipiza kisasi kwani aliwahi kunitamkia hata mimi kwamba ni lazima atalipiza kisasi kwa watu waliosababisha kifo cha Vero na hilo ndilo jambo ambalo limekuwa likituweka mbali mbali mimi nay eye kwani sioni mantiki ya kulipiza kisasi wakati tayari shauri hili liko katika vyombo vya maamuzi” akasema Sarah
“Kama aliwahi kukutamkia hivyo basi hakuwa anatania.Alimaanisha alichokuwa anakisema.Alinishirikisha mimi pia katika mipango yake kwa kuniomba nimsaidie kutafuta mtu au watu ambao watamsaidia kuifanya kazi hiyo.Nilimsaidia kumpata mtu mmoja ambaye alikuwa tayari kuifanya kazi hiyo.Niliwakutanisha wakaongea na kuelewana namna watakavyotekeleza mpango huo wa kulipa kisasi.Loniki alitaka Patrick na Happy wauawe.Khumalo alilipinga wazo hilo la kuwaua Patrick na Happy kwa haraka kama alivyokuwa anataka Lonny badala yake akashauri kwamba kwa kuwa wakati ule Patrick alikuwa gerezani basi nguvu ielekezwe kwa Happy lengo hapa likiwa ni kumfanyia udhalilishaji mkubwa ambao utapelekea uhusiano wake na Patrick kuvunjika.Khumalo na genge lake walifanikiwa kumteka Happy na kumpeleka mafichoni na huko alifanyiwa udhalilishaji mkubwa sana.Alifanyishwa ngono na vijana wawili huku akirekodiwa na kupigwa picha .Aliamriwa kufanya vile kwa kisingizio kwamba endapo angekataa basi Patrick angeuawa na kwa kuwa Happy anampenda sana Patrick alikubali kufanya vile ili kumuokoa Patrick” akasema Linah na kumtazama Sarah usoni ambaye alionyesha mstuko mkubwa
“My Gosh ! kumbe Lonny ndiye aliyemfanyia Happy kitendo kile?? Akauliza Sarah
“Ndiyo.Happy alifanyiwa udhalilishaji ule huku Loniki akishuhudia.Sarah kwa kweli lile lilikuwa ni tukio baya sana ambalo halitaweza kufutika moyoni mwangu.Ninalijutia sana kosa lile kwani hata mimi nilishiriki” akasema Linah kwa masikitiko halafu akaendelea
“Kilichofuata baada ya hapo ni kama tulivyoona katika magazeti na mitandao.” Linah akanyamaza,akamtazama Sarah na kuendelea
“Katika kipindi hiki ambacho amekuwa Uingereza bado ameendelea na mipango yake ya kuhakikisha kwamba Patrick anafungwa gerezani tena kifungo kirefu.Amekuja leo hii ili kufanikisha kile ambacho amekwisha kianza muda mrefu .Kikubwa zaidi kilichonifanya nikutafute usiku huu ni kwamba amedhamiria kumuua Patrick endapo mahakama itamuachia huru” akasema Linah.Sarah akasimama kwa hasira
“Why are you telling me all this now? Akauliza Sarah
“Because we have to stop her !! akasema Linah naye akasimama
“No Linah ! go away.Wewe na Happy lenu moja.Nyote mmeshiriki katika njama hizi.Linah how could you do that? How could you hurt Parick like that? .akauliza Sarah kwa uchungu
“Sarah please forgive me. Sikuwa nikiufahamu ukweli wa mambo na ndiyo maana nilikubali kushirikiana na Loniki.Kwa sasa baada ya kuufahamu ukweli ninajutia na tafadhali Sarah naomba tushirikiane sote tumuokoe Patrick “
“Go away Linah ! You and Lonny are both killers and tomorrow morning I’m going to report you ” akasema Sarah ambaye alikuwa amepandwa na hasira
“Tafadhali usifanye hivyo Sarah.Tunatakiwa tutafute namna ya kufanya ili kumzuia Lonny asitekeleze mipango yake bila kuwashirikisha polisi.Ukitoa taarifa hizi polisi Loniki anaweza akaenda gerezani.” Akasema Linah
Sarah akainama akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akainua kichwa akamuangalia Linah kwa macho makali.
“Bado siamini kama na wewe umekubali kuungana na Loniki.Nilikuheshimu sana kama dada yangu lakini kwa jambo hili ulilolifanya umenifanya nikutazame upya” akasema Sarah
“C’mon Sarah.Huu si wakati wa kuanzisha malumbano.Tunatakiwa kushirikiana katik…………….” Kabla hajamaliza sentensi yake Sarah akamzuia
“Hakuna njia nyingine zaidi ya kulifikisha suala hili katika vyombo vya dola.Wewe na rafiki yako mtakwenda kujieleza mbele ya vyombo vya sheria.” Akasema Sarah kwa ukali.Linah akamsogelea na kumshika bega
“Nisikilize vizuri Sarah.Najua wewe na Loniki hamna maelewano mazuri lakini yule ni dada yako,ni ndugu yako wa damu.Ukilifikisha suala hili polisi Loniki atakamatwa na anaweza akafungwa gerezani.So tell me are you sure you want to send your sister to jail?
Sarah akainama halafu akainua kichwa akamtazama Linah na kusema
“Unataka tufanye nini?
“Kwa sasa bado najaribu kuangalia namna tutakavyoweza kumzuia Lonny asitekeleze mpango wake.Leo nimeona nikufahamishe kinachoendelea.Nitakupugia simu kesho kukufahamisha mipango yake inavyoendelea na kwa pamoja tutaona namna ya kuweza kumzuia.Sitaki afahamu kama nina mawasiliano nawe kwa hiyo usinipigie simu mimi ndiye nitakayekupigia.Naomba vile vile unihakikishie kitu kimoja”
“kitu gani hicho Linah?
“Naomba haya tuliyoyaongea hapa yabaki kati yetu”
Sarah akamtazama Linah na kusema
“Sintamwambia mtu yeyote lakini naomba utafute haraka mpango wa kumzuia Loniki asiweze kutekeleza mpango huo wa kumuua Patrick” akasema Sarah
“Usihofu Sarah.Nitakufahamisha kila kitu namna tutakavyofanya” akasema Linah halafu akaagana na Sarah akaondoa zake.
“Kazi ya kwanza nimeimaliza.Japokuwa haikuwa rahisi lakini nashukuru Sarah amenielewa.Kinachofuata sasa ni kuongea na Khumalo.” Akawaza Linah akiwa garini akapunguza mwendo wa gari na kuliegesha pembeni ya bara bara akachukua simu yake na kumpigia Khumalo.
“hallo Linah´ akasema Khumalo
“Khumalo bado uko klabuni?
“Ndiyo Linah bado niko hapa klabuni na warembo wangu.Unasemaje?
“Ni kuhusu Lonny”
“Lonny kafanya nini tena? Si tumekwisha malizana naye?
“Nafahamu hilo Khumalo lakini kuna jambo ambalo nataka tulijadii.” Akasema Linah na kuliwasha gari akaliingiza barabarani.
“jambo gani hilo Linah?
“Ni kuhusu huu mpango wake wa kumuua Patrick”
“Kuna tatizo gani katika hilo?
“Are you real gonna do it? Akauliza Linah
“Do what ? khumalo naye akauliza
“Kill Patrick” akasema LInah.Khumalo akacheka kidogo na kusema
“Kwa nini unauliza hivyo Linah wakati unafahamu kabisa kwamba hakuna mpango wowote wa kumuua Patrick? Mimi na wewe tulikwishakubaliana kwamba tutakula fedha za Loniki lakini hatutakeleza mpango wake wowote.Tulichomfanyia Happy kinatosha sana.Siwezi kuendelea kuumiza tena watu wasio na hatia”
“Nimekeuelewa Khumalo lakini nina wazo moja”
“Wazo gani Linah?
“Ninaomba uondoke hapa Dar na usirudi hadi hapo nitakapokutaarifu.”
“Hata hivyo huo ndio ulikuwa mpango wangu.Kesho nilipanga niende Zanzibar kula raha na mpenzi wangu Sakina.Nasubiri milioni arobaini za mwisho toka kwa Lonny”
“Hilo ni jambo zuri sana Khumalo na nina imani endapo ikitokea mahakama ikamuachia huru Patrick Lonny atakutafuta na akikukosa basi hatakuwa na la kufanya tena zaidi ya kuahirisha mpango wake”
“usihofu Linah.Endapo kutakuwa na tatizo lolote na utahitaji msaada wangu utanitafuta na nitawatuma vijana wangu wakusaidie”
“Ahsante sana Khumalo” akasema Linah akaagana na Khumalo na kukata simu
“Sasa mambo yamekaa sawa.Nadhani huu ndio mwisho wa urafiki wangu na Loniki.Ni heri kuishi bila kuwa na rafiki kuliko kuishi na rafiki kama Lonny.” Akawaza Linah huku akielekea nyumbani kwake


* * * *

Siku mpya imeanza.Saa tatu za asubuhi ilimkuta Loniki mbele ya kaburi la Veronika. Kwa muda wa dakika kadhaa alikuwa amesimama akiliangalia kaburi hili huku michirizi ya machozi ikionekana mashavuni
“Vero mdogo wangu nilikuahidi kwamba lazima nikulipizie kisasi kwa wale wote waliokukatili na kusababisha kifo chako.Ule muda wa malipo umewadia.Kesho ni hukumu ya Patrick.Endapo mahakama itamuachia huru basi sintakuwa na njia nyingine zaidi ya kuhakikisha naye anauawa.Ni adhabu mbili tu anazostahili Patrick,kifungo gerezani au kifo.Yule mwanamke wake hali kadhalika naye anastahili adhabu ya kifo.Nitamsaka kokote aliko na kuhakikisha kwamba naye anakufa.Sintakuangusha mdogo wangu” akasema Loniki huku akitoa machozi.Akachukua maua aliyokuja nayo akayaweka juu ya kaburi na kuondoka


* * * *

Saa tatu za usiku,Patrick amejilaza kitandani.Pembeni yake alikuwepo mpenzi wake Savanna.Kutwa nzima ya leo Patrick alikuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana.
“Patrick mpenzi wangu,nimekwisha kuambia kwamba usiwe na mawazo wala wasiwasi.Kesi hii tumepambana nayo vya kutosha na nina uhakika mkubwa wa kushinda.I’ve done my best na ndiyo maana nina uhakika mkubwa wa kushinda kesi hii.Endapo itakuwa vnginevyo basi yatakuwa ni matakwa ya mahakama lakini hata kama ikiwa hivyo basi nitakata rufaa na kupambana tena.Kitu muhimu ni kuwa tayari kwa maamuzi yoyote yatakayotolewa na mahakama.” Akasema Savanna.Patrick ambaye alikuwa amejilalaza akainuka na kukaa halafu akamtazama Savanna kwa makini na kusema
“I’m scared.Sielewi kwa nini nina hofu kubwa.Sijawahi kuwa na hofu ya namna hii maishani mwangu.|” akasema Patrick huku akiupeleka mkono wake sehemu ya kifua unapokaa moyo
“Kitu gani kinakufanya uwe na hofu Patrick? Akauliza Savanna
“Nahofia iwapo nitahukumiwa kifungo maisha yangu ambayo kwa sasa tayari yameanza kwenda vizuri yataharibika na kila kitu kitapotea” Akasema Patrick
“Patrick,tumepambana vya kutosha na mimi kama wakili niliyeisimamia kesi hii ninauhakika mkubwa sana kwamba nimefanya kazi yangu ipasavyo kuishawishi mahakama ikuachie huru.Hoja tulizojenga na kuziwasilisha ni nzito na zina ushahidi wa kutosha.Lakini watoa hukumu nao ni binadamu na inawezekana wakaamua tofauti na tunavyotegemea sisi lakini hata kama ikitokea watakuhukumu kifungo tutakata rufaa.” Akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu na kumvuta Savanna karibu akambusu
“Kila mara namshukuru sana Mungu kwa kunipa mwanamke ambaye ni jasiri na ambaye yuko tayari kufanya kila linalowezekana kwa ajili yangu.Endapo mahakama itaniachia huru basi ndani ya kipindi kifupi sana lazima tufunge ndoa.”
Uso wa Savanna ukajenga tabasamu pana
“Patrick mpenzi wangu ,Mungu aliyetukutanisha anafahamu ni namna gani ninakupenda.Ni Mungu huyu huyu ambaye atatusaidia ili tuweze kuitimiza ndoto yetu hii kubwa.Siku zote tunatakiwa tumuamini na kumtegemea yeye pekee.Kwa imani niliyonayo kwa Mungu huyu mmoja muumba wa mbingu na nchi nina imani tutashinda kesi na tutafanikiwa kuwa pamoja milele “ akasema Savanna huku amemkumbatia Patrick kwa nguvu
“Savanna endapo nitapewa adhabu ya kifungo gerezani tafadhali naomba usinitelekeze kama walivyofanya wengine.Naomba unisubiri hadi hadi hapo nitakapomaliza kifungo changu ili tuweze kuitimiza ndoto yetu ya kuwa pamoja.Will you wait for me darling?
“Patrick kwanza naomba ufahamu kwamba hutakwenda gerezani.Hata kama ikitokea kwamba utahukumiwa kifungo basi itapambana hadi nihakikishe ninakutoa.Kuhusu kukusubiri usitie shaka kuhusu hilo.Niko tayari hata kutumia muda wangu wote uliobaki hapa duniani kukusubiri wewe tu kwa hiyo usiwe na hofu hata kidogo na hilo.” Akasema Savanna kwa sauti laini
Waliongea mambo mengi sana usiku huo .Savanna alijitahidi kwa kila alivyoweza kumpa moyo Patrick kuhusu hukumu yake siku itakayofuata.Huu ulikuwa ni usiku mgumu sana kwa Patrick.Alitumia muda mwingi kusali na kumuomba Mungu amuepushe na kifungo
 
Back
Top Bottom