Simulizi: Miss Tanzania

Simulizi: Miss Tanzania

duh hii story ilikuepo humu toka 2018 hatari sana!?

nipo sehemu ya 31 ngoja niendee japokua ni story tu lakn inaumiza aisee......
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 8
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“I have to do something” Patrick akawaza.ghafla akatoka mbio kuelekea kijijini.Hakuna mtu yeyote aliyejua Patrick anakwenda wapi.Dakika kama kumi baadaye gari moja aina ya Toyota pick up ikaja kwa kasi kubwa maeneo hayo ya hospitali huku ikiwa imewasha taa.Watu waliokuwepo hapo nje wakaanza kuingiwa na wasi wasi labda kuna maafa mengine yametokea.Gari ikafunga breki kali na mara bila kutegemea Patrick akashuka.
Mpaka muda huo bado Happy alikuwa ndani ya gari akiwa hana fahamu huku mwalimu na yule muuguzi wakizuai damu kuendela kuvuja huku wakijadiliana jinsi ya kumpata daktari ambaye kwa wakati huo hawakujua alikuwa wapi.
“Haraka haraka,nisaidieni kumbeba.”Akasema Patrick akiwaambia watu wawili aliokuja nao katika ile gari.Huku mwalimu na muuguzi wakishangaa Happy akashushwa toka katika gari ya shule na kupakiwa katika ile gari ndogo aliyokuja nayo Patrick.
“Patrick unafanya nini??.................Alipaaza sauti mwalimu akiwa haelewi nini Patrick alikusudia kufanya.
“Dereva ondoa gari achana na huyo mwalimu”Patrick alisema huku akifunga mlango .
gari ikaondolewa kwa kasi ya ajabu kila mtu akibaki ameduwaa.

ENDELEA……………………

“ahsanteni sana ndugu zanguni nashukuru mmenisaidia”Patrick akawaambia dereva na yule msaidizi wake baada ya kufika katika hospitali ya Makambako na Happy kuanza kupatiwa matibabu.
“Usjali dogo siku yoyote ukiwa na tatizo unasema.sisi sote binadamu lazima tusaidiane.”akasema dereva.
Baada ya kuwalipa pesa zao wakaondoka kurudi malangali na kumwacha Patrick hapo hospitali.Giza tayari lilikwisha ingia.Happy alikuwa katika chumba cha upasuaji akishonwa jeraha lake la kichwa.Lilikuwa ni jereha kubwa lililompelekea apoteze damu nyingi .Bado alikuwa hajarejewa na fahamu.Patrick bado alikuwa nje ya chumba hicho akisubiri kujua hali ya Happy itakuwaje .Moyoni bado alikuwa na fundo kubwa lililomkaa juu ya kilichokuwa kimetokea.Alianza kuvuta picha ya jinsi tukio lile lilivyotokea .Alikumbuka wakati vurugu imeanza na mawe kuanza kurushwa.hadi jiwe lile kumpata Happy kichwani, ni wazi tukio lile lilikuwa limedhamiriwa.
“Naanza kupata picha kuwa mrushaji wa jiwe lile alikuwa amedhamiria kabisa kumjeruhi Happy au mimi.”akawaza Patrick.akiwa katika lindi la mawazo mara mlango wa chumba cha upasuaji ukafunguliwa na machela ikatoka.
“Kijana hali ya mwenzio inaendelea vizuri .Tumeshona jeraha lake na sasa tunampeleka wodini .Tutamuongezea damu kwa sababu amepoteza damu nyingi sana.wewe unaweza kwenda kupumzika .Uje asubuhi”Alisema daktari mama wa makamo ambaye alionekana kuwa na roho ya huruma.
“Ahsante daktari kwa kazi kubwa mliyoifanya.Lakini nitabaki hapa hapa mpaka asubuhi kwa sababu tayari imeshakuwa usiku na mimi hapa Makambako ni mgeni”
“Nyie mmetokea wapi” Akauliza yule daktari
“sisi ni wanafunzi wa shule ya sekondari malangali” patrick akajibu.Baada ya mahojoano mafupi na yule mama akamwangalia Patrick kwa sekunde kadhaa kisha akasema.
“Umefanya kitendo cha kijasiri sana ..kama ungeendelea kukaa pale shuleni hali ya mwenzio ingekuwa mbaya zaidi na hata kupoteza maisha.Nitamwambia dereva wetu akupeleke nyumbani kwangu ukapumzike hadi kesho.Umeonyesha moyo wa ujasiri sana wa kumsaidia mwenzako..Nisubiri hapo hapo” Alisema yule mama na kuingia ndani.
Patrick aliendelea kumwomba Mungu kimoyo moyo hali ya Happy iwe nzuri.
“Twende” akasema yule daktari wakaondoka na kisha Patrick akapanda gari la hospitalina kupelekwa nyumbani kwa yule daktari
.

* * * *

Saa kumi na mbili asubihi ilimkuta Patrick tayari amekwisha fika hospitali.Hakuweza kupata usingizi usiku huo licha ya kuhakikishiwa kuwa hali ya Happy ilikuwa nzuri.Moyo ulikuwa ukimwenda mbio.Aliingia katika wodi aliyolazwa Happy kwa wasi wasi mwingi.Lakini ghafla akakutana na sura angavu yenye matumaini ya Happy .tayari alikwisha pata fahamu toka usiku.Patrick akafumba mdomo kwa kiganja cha mkono wake akionyesha mshangao.kwa haraka akakimbia na kumkumbatia Happy pale kitandani.
”Pole sana Happy ”
‘ahsante Patrick.nashukuru sana kwa msaada wako”
“Usijali Happy ulikuwa ni wajibu wangu kufanya hivyo”akajibu Patrick.
“ nilikuwa na wasi wasi mwingi wakati fahamu zimenirudia nikiwaza nilifikaje fikaje hapa..Muuguzi mmoja aliyekuwapo zamu ya usiku akaniambia kuwa kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Patrick pamoja na watu wengine wawili ndio waliokuleta hapa.Nilifurahi sana kusikia hivyo.nashukuru sana Patrick.Kwa sasa naamini kuwa upendo wako kwangu ni wa kweli.”
Patrick hakujibu kitu akatabasamu.
“sasa Patrick nina imani nitazidi kuwepo hapa hospitali kwa siku kadhaa hivyo nitakupa namba hizi za simu umpigie mama yangu na umweleze mkasa mzima jinsi ulivyokuwa ili aje anihudumie kwa kipindi hiki chote nitakachokuwa hapa hospitali. Kwa sababu wewe unatakiwa kwa sasa uanze kujiandaa na mitihani ambayo haiko mbali sana.”
Patrick akakubaliana na ushauri ule na kuzichukua zile namba.
“ Happy ungependa kula ni ni asubuhi hii”Patrick akauliza
“Mimi nimeshashiba kwa kukuona wewe tu.Patrick wewe ni chakula tosha kabisa.Usisumbuke Patrick sintakula kitu .Jitahidi ukawasiliane na mama najua atanihamisha hapa na kwenda kutibiwa Mbeya.”
Waliongea mambo mengi asubuhi hiyo hadi muda wa kuwaona wagonjwa ulipoisha kisha Patrick akamuaga Happy kuwa anaenda kupiga simu.

****************************

Saa tano na dakika ishirini na saba gari moja ndogo yenye vioo vyeusi lilifunga breki katika hospitali ya Makambako .Mama mmoja akiongozana na binti mmoja ambaye ni wazi alionekana kuwa ni mwanae walishuka ndani ya gari lile na kuelekea mapokezi.Waliongea na wauguzi waliokuwapo pale mapokezi kisha wakapelekwa kwa mganga mkuu.Baada ya muda wakatoka wakiwa wameongozana na mganga mkuu na kuelekea maeneo ya wodi za wagonjwa.
Patrick alikuwa nje ya wodi aliyokuwa amelazwa Happy .Hali ya hewa ilikuwa ya kiubaridi baridi kama ilivyo ada ya hali ya hewa ya Makambako.Kijua kilichomoza na kuzima.Hii haikumsumbua sana kwa sababu alikuwa bado amevaa suti aliyokuwa ameivaa jana yake.Mara akawaona mama mmoja na mwanae wakiwa wameongozana na daktari mkuu.
“Mhhhh!!” Patrick akaguna.Akazidi kuwaangalia kwa makini watu wale wakija .
“Yule msichana mbona kafanana sana na Happy ? anaweza akawa ndiye yule ndugu yake ? hata yule mama amefanana sana na Happy” Patrick akaendelea kuwaza huku akiwatazama yule mama na yule binti wakielekea katika wodi aliyokuwa amelazwa Happy..
Mama yule ,binti yake pamoja na daktari mkuu wakampita Patrick pale nje na kuelekea moja kwa moja katika wodi ile aliyokuwa amelazwa Happy wakaingia ndani.
“Nahisi ni wenyewe hawa.nahisi huyu ndiye mama yake Happy .”Akawaza Patrick huku akijiweka sawa kwani alitegemea ni lazima wangeonana..Dakika kama tano hivi toka yule mama aingie mle wodini alikuja muuguzi na kumwita Patrick ndani.
“mama huyu ndiye Patrick ni rafiki yangu na ndiye aliyeyaokoa maisha yangu kwa kunileta hapa hospitali haraka.”
Akasema Happy baada ya Patrick kuingia
“ooh ! Ndiye huyu ! Ndiye huyu aliyenipigia simu asubuhi?”
“Ndiye mimi mama.Shikamoo” Patrick akasema kwa adabu
“Marahaba mwanangu.nashukuru sana kwa msaada wako.”
“Ahsante mama”Patick akajibu.
Mama yake Happy alikuwa ni mtu mchangamfu na mcheshi sana.
“Patrick huyu ni mdogo wangu anaitwa Margareth.” Happy akasema
“Nafurahi sana kukufahamu margareth.”Akasema Patrick huku akishikana mikono na Margareth.Mama yao alikuwa akitabasamu akasema
“Patrick tunashukuru sana kwa msaada wako lakini itabidi Happy tumuhamishe hospitali.Tutaenda naye Mbeya akatibiwe kule.Kwa hiyo wewe unaweza ukarejea shuleni.Utapewa barua na mganga mkuu wa hapa ili uipeleke shuleni ya kuthibitisha ugonjwa wa mwenzio.”
“sawa mama” akajibu Patrick
Saa saba na nusu za mchana Patrick akawasili shuleni na moja kwa moja akaelekea katika ofisi ya mkuu wa shule msaidizi.
“Patrick !!.. akasema mkuu wa shule msaidizi baada ya Patrick kuingia ofisini kwake.
“Naam mwalimu”
“Umefanya nini tena? Hata wiki mbili hazijaisha toka utoke kwenye adhabu leo tena unarudia mambo yale yale? Akasema mwalimu kwa ukali
“Sikiliza mwalim…………………..”
“noo !! sitaki kusikiliza upuuzi wako.kwa nini ukamchukua mgonjwa na kukimbia naye mahala kusikojulikana?Sisi kama walimu ndio walezi wenu ninyi mkiwa hapa shuleni . tutajibu nini kwa wazazi wake pindi tatizo kubwa likimpata? Akaendelea kufoka mwalimu mkuu msaidizi
‘.Mwalimu,siku ile ya mashindano baada ya kutokea vurugu Happy alijeruhiwa na jiwe kichwani akapoteza fahamu.damu nyingi ikawa ikimvuja.Mimi na mwalimu Steve pamoja na dereva wa shule tukampakia garini na kumpeleka zahanati .pale hakukuwa na daktari na muuguzi tuliyemkuta pale alikuwa akisita hata kumuhudumia Happy .Mimi sikuridhika na hali ile ikanibidi nikodi gari kwa pesa zangu na kumuwahisha Happy hospitali ya Makambako ambako alipatiwa matibabu,akashonwa jeraha lake ,akaongezewa damu pia.na hii hapa ni barua toka kwa mganga mkuu wa hospitali ya Makambako.”
Mkuu wa shule msaidizi akaichukua barua ile na kuisoma kisha akamwangalia Patrick kwa sekunde kadhaa.
“Ulifanya jambo jema Patrick .Uliokoa maisha ya mwenzio lakini siku nyingine unatakiwa ushauriane kwanza na sisi na siyo kuchukua maamuzi yako binafsi .Mashitaka yaliyoletwa hapa kwangu ni kwamba ulifanya vurugu na kumchukua Happy .Hivi sasa tulikuwa katika maandalizi ya kuripoti suala hili katika vyombo vya usalama vitusaidie kukutafuta na kukuchukulia hatua.Haya nenda ukapumzike ila kuwa mwangalifu sana kwa sasa unafuatiliwa kwa kila unachokifanya” akasema mwalimu
“Ahsante sana mwalimu nitakuwa mwangalifu”
Patrick akatoka ofisini kwa mkuu wa shule msaidizi na kuelekea bwenini.Akaoga na kujilaza kitandani.

* * * *

Mwezi wa kwanza mwaka uliofuata shule zikafunguliwa na ikawa ni awamu mpya kwa Patrick na Happy .Kwa sasa walikuwa kidato cha nne na walifahamu nini walichokuwa wakihitajika kukifanya hivyo hawakuwa na mzaha katika kusoma.Walisoma kwa bidii kubwa kwa lengo moja tu la kutimiza ndoto zao.Wawili hawa kwa ghafla waka ni mfano wa kuigwa na wengine.Tofauti na mwaka uliotangulia kwa sasa wakaanza kuwa na marafiki wengi wa madarasa ya chini yao ambao mara nyingi walipewa msaada mkubwa katika masomo.Kitendo cha kuheshimiwa na wanafunzi wa vidato vya chini kilizidi kuwapa wakati mgumu wale wanafunzi adui zao ambao walikuwa hawawatakii mema.
Ilikuwa ni tarehe 14/03 siku ya jumamosi ambapo wanafunzi walikuwa wametangaziwa kuwa siku hiyo kungekuwa na burudani ya muziki.Burudani kama hizi huja mara chache sana hapa shuleni,hivyo wanafunzi walikuwa wamejiandaa vilivyo.Patrick na Happy nao walishauriana na kukubaliana kuwa wangeingia ukumbini japo kwa muda mchache tu halafu waendelee na ratiba yao za kujisomea.
Baada ya mlo wa jioni milango ya ukumbi ikafunguliwa na wanafunzi wakaanza kujitoma ndani.Disko likafunguliwa rasmi na wanafunzi wakaanza kuserebuka.Patrick na Happy wakaingia ndani ya ukumbi lakini hawakukaa sana kutokana na joto ,wakatoka na kwenda kupunga upepo nje.Wakiwa nyuma ya bwalo la chakula wakipunga upepo huku mbalamwezi ikumulika mara ghafla likatokea kundi la vijana waliokuwa wamefunika nyuso zao wakiwa na mapanga matatu wakawazingira.Happy akaogopa na kumkumbatia Patrick
“Mama yangu !!!!,”Happy akasema kwa mstuko
“ kaa kimya na usijaribu kupiga kelele kwani tutawaua sasa hivi.”Akasema jamaa mmoja aliyekuwa na sauti nzito .Happy alikuwa akitetemeka.Patrick naye mikono ilikuwa ikimtetemeka.
Kundi lile lilikuwa na vijana zaidi ya kumi na wote walikuwa wamefunika nyuso zao.
Mmoja ambaye ndiye aliyeonekana kuwa kiongozi wao aliwasogelea na kumshika mkono Happy .
“Tuna shida na huyu binti” Akasema yule jamaa huku akimvuta Happy kwake.
Patrick akainua mkono lakini kabla hajafanya lolote akapigwa na chuma kizito shingoni akaanguka chini na kuona giza, yule jamaa akamshika Happy kisha kwa haraka wakamjaza vitambaa mdomoni ili asiweze kupiga kelele.
“Haya jamani haraka haraka tumalize kazi.Leo ni leo.Keo nenda kaangalie kama kuna mtu yoyote anakuja maeneo haya .Ukiona kuna mtu anakuja tufahamishe haraka.”
Akaamrisha yule jamaa ambaye alionekana kuwa ndiye kiongozi wa genge lile
Happy alikuwa ameshikwa bara bara kiasi cha kutoweza kufurukuta akabebwa juu juu na kupelekwa katika kichaka cha karibu.Kwa kasi ya aina yaka yule jamaa kiongozi akaichana blauzi nyepesi aliyokuwa ameivaa Happy na kuyashuhudia matiti machanga ya kimwana huyu.Udenda ukamtoka.Happy alikuwa akilia lakini sauti yake ilikuwa haisikiki kutokana na vitambaa walivyomuweka mdomoni.
Fedhuli yule akaishusha suruali yake hadi magotini na kuanza kumsogelea Happy huku uume wake ukiwa umesimama wima.Akaivuta suruali ya Happy na kuishusha chini kisha akaivuta nguo ndogo ya ndani aliyokuwa ameivaa na kuichana Akaitupa pembeni akawaamuru wale watu waliokuwa wamemshika Happy wampanue miguu.
“Hii niyo dawa yake mshenzi huyu.Halafu anaonekana bado bikira.Hii ndiyo dawa ya wasichana kama wewe wenye maringo”
Akasema yule jamaa huku akiuchezea uume wake tayari kumwingilia Happy kwa nguvu
Taratibu Patrick akapata fahamu na kuhisi maumivu makali sana maeneo ya shingoni na mara kumbu kumbu zote zikarudi.Akakumbuka kuwa walikuwa wamevamiwa na yeye akapigwa na kitu kizito shingoni.
“Happy yuko wapi?” Akajiuliza na mara akakumbuka kwamba wale wahuni waliowavamia walimchukua kwa lengo la kumtenda vibaya.Akajikaza na kuamka pale alipokuwa amelala huku akihisi maumivu makali mno.Happy hakuwapo na wala wale jamaa waliowavamia hawakuwapo.Hasira ikampanda .
“ I must do something immediately kabla hawa jamaa hawajatekeleza mpango wao” AkawazaPatrick.Pale chini akakiona kile chuma alichopigwa nacho akainama na kukiokota kisha akaanza kunyata kuelekea mahala aliposikia minong’ono ya watu.Alinyata taratibu akiwa amefura kwa hasira.
Ndani ya kichaka Happy alikuwa ameshikwa barabara kiasi kwamba hakuweza kufurukuta wala kupiga kelele kutokana na matambara yaliyojazwa mdomoni.Kiongozi wa genge lile alikuwa akijiandaa tayari kabisa kutekeleza kitendo cha kumbaka Happy .Ni machozi pekee ndiyo yaliyokuwa yakimtoka binti huyu mrembo .Roho ilimuuma sana kwa kushuhudia kitendo kile alichotaka kufanyiwa.Vile vile aliumia sana roho baada ya kumfikiria Patrick.Hakuwa na uhakika kama atakuwa salama kwani alishuhudia yeye mwenyewe kwa macho yake Patrick akipigwa na chuma kizito akaanguka chini.Ni uchungu ambao hauwezi kuelezeka aliokuwa nao binti huyu.Hakuwa na tumaini la kupata msaada wa aina yoyote kwa wakati ule.Msaada pekee alikuwa ni Patrick na ambaye aliamini kuwa kwa pigo lile lazima atakuwa katika hali mbaya ya kutokujitambua kama sio kufa kabisa
Wakati jamaa yule akiuchezea uume wake mkubwa ,Happy huku machozi yakimtoka akafumba macho na kuomba
“Ee Mungu najua sina ubaya wowote na mtu yeyote yule hadi kufanyiwa kitendo hiki.Ee baba kama sistahili kufanyiwa hivi basi na isiwe lakini kama …….
Hakumaliza maombi yake mara ghafla yule jamaa aliyekuwa tayari kumwingilia akapiga ukelele mkubwa na kuanguka chini.Kilichofuata hapo ni kusikia vishindo vya watu wakikimbia.Ulikuwa ni muujiza ambao Happy hakuutegemea katu.Kijana mmoja ambaye hakuweza kumtambua kwa haraka kutokana na giza alikuwa amesimama mbele yake na kisha akamwinamia.
“Happy are you ok?” Ilikuwa ni sauti ya Patrick ambaye aliongea akiwa katika maumivu makali sana.
Happy hakusema kitu ni machozi tu ndiyo yaliyokuwa yakimtoka .Hakuamini kabisa kwa alichokuwa akikiona.
Patrick akamtoa yale matambara aliyokuwa amewekewa mdomoni kisha akambusu.
“Patrick you are my Hero.” Ni neno hilo tu ambalo Happy aliweza kulisema kwa wakati huu.Mwili wote ulikuwa ukimtetemeka.
“Hawajakufanya kitu chochote washenzi hawa? Akauliza Patrick
“Hwakuwahi, ulifika kwa wakati muafaka kabisa bado walikuwa hawajatimiza azma yao.Ahsante Patrick”Akasema Happy huku machozi yakimtoka
Pale chini alikuwa amelala yule kiongozi wa genge lile la wahuni akivuja damu kichwani mahala alipopigwa na chuma .Patrick akamwangalia kwa hasira sana.
“Patrick huyu jamaa ni mzima kweli? Happy akauliza
“I don t know Happy .Sijui kama atakuwa mzima.Nilimpiga kwa nguvu zangu zote nilizokuwa nazo..Hiyo ni adhabu yake” akajibu Patrick
Ghafla wakasikia makelele ya watu wakija kwa kasi kule mahala walikokuwa.
“Happy lets get out of here.wasije wakatukuta hapa hawa watu.tayari wamekwisha ambizana.” Akasema Patrick na kumshika Happy mkono wakaanza kukimbia kushuka katika korongo.Hawakufika mbali wakamulikwa na tochi usoni.
“Hey ! simameni hapo hapo,mkikimbia ninaachia mshale huu”Ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume.Patrick na Happy wakasimama.Walikuwa ni watu wanne waliokuwa na mbwa .Watu hawa walikuwa ni wawindaji waliokuwa wakifuatilia mitego yao porini.
“Tafadhali jamani naomba mtuache tuondoke tuna matatizo makubwa” Akasema Patrick
“Hapana kwanza ninyi mnaonekana ni wanafunzi.Usiku huu mnafanya nini porini?Haya anzeni kuongoza tunawarudisha mpaka shuleni” Akaamuru jamaa mmoja ambaye alionekana kuwa ndiye kiongozi wa wale wawindaji.
Jitihada za Patrick an Happy kuomba waachiwe hazikuweza kuzaa matunda,jamaa wakaanza kuwaongoza kuwarudisha shuleni.
Hawakuwa na ujanja tena zaidi ya kufanya vile walivyoamriwa.

* * * *

“wameuaaaaaa !!!....wauajiiiiiiiiii!!!!!!......wauaweeeee!!!!!!!!!!” Hizo ni kelele zilizoufunika mji wa Malangali kwa muda huu wa usiku.Patrick na Happy walikuwa katika mikono ya polisi kwa ajili ya usalama wao.Yule jamaa aliyepigwa na chuma kichwani na Patrick alikuwa amekufa.
Karibu kijiji chote kilikuwa kimeamka kutokana na makelele ya wanafunzi na kukusanyika shuleni.Wote walitaka washuhudie ni wanafunzi gani waliofanya mauaji.Baada ya kuingizwa katika kituo kidogo cha polisi kilicho pembezoni mwa shule ikawabidi polisi kupiga risasi za moto juu ili kuwatawanya wanafuzi ambao walikuwa wameanza kurusha mawe wakitaka watuhumiwa waachiwe ili wauawe pia.Ilikuwa ni kazi kubwa kuwatawanya lakini hatimaye walifanikiwa baada ya kupiga risasi kadhaa hewani.
Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Hakutegemea kama siku moja angeweza kuingia katika dhahama ile.Hakuwahi kuota kama siku moja angeitwa muuaji.
“Nyamaza Happy ,usilie mambo yameshatokea..Jipe moyo Mungu yupo na yeye ndiye anayeufahamu ukweli.” Patrick akambembeleza Happy
“Patrick nina uchungu mwingi sana .Ni bora ningekuwa mwenyewe lakini sasa nimekuingiza na wewe katika matatizo makubwa namna hii.tayari nimekwisha kuharibia mwelekeo mzima wa maisha yako……….”
“Shhhhhhhh..!!!....Usiseme hivyo Happy .I did the right thing.Hata nikinyongwa nitakuwa na amani kwamba niliua kwa ajili ya kukulindia heshima yako.Hakuna mwanaume yeyote anayeweza kukubali kuona mpenzi wake akifanyiwa kitendo cha kinyama kama walichotaka kukufanyia hawa jamaa.nadhani nilifanya kitu sahihi.Sijutii kosa langu kwa sababu nimefanya kwa ajili ya mtu nimpendaye”
Happy akamkumbatia Patrick kwa nguvu huku akilia .
Kwa ajili ya usalama wao usiku huo huo wakapakiwa katika gari la polisi na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Iringa mjini

* * * *

Karibu kijiji chote kilikuwa kimeamka kutokana na makelele ya wanafunzi na kukusanyika shuleni.Wote walitaka washuhudie ni wanafunzi gani waliofanya mauaji.Baada ya kuingizwa katika kituo kidogo cha polisi kilicho pembezoni mwa shule ikawabidi polisi kupiga risasi za moto juu ili kuwatawanya wanafuzi ambao walikuwa wameanza kurusha mawe wakitaka watuhumiwa waachiwe ili wauawe pia.Ilikuwa ni kazi kubwa kuwatawanya lakini hatimaye walifanikiwa baada ya kupiga risasi kadhaa hewani.
Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Hakutegemea kama siku moja angeweza kuingia katika dhahama ile.Hakuwahi kuota kama siku moja angeitwa muuaji.
“Nyamaza Happy ,usilie mambo yameshatokea..Jipe moyo Mungu yupo na yeye ndiye anayeufahamu ukweli.” Patrick akambembeleza Happy
“Patrick nina uchungu mwingi sana .Ni bora ningekuwa mwenyewe lakini sasa nimekuingiza na wewe katika matatizo makubwa namna hii.tayari nimekwisha kuharibia mwelekeo mzima wa maisha yako……….”
“Shhhhhhhh..!!!....Usiseme hivyo Happy .I did the right thing.Hata nikinyongwa nitakuwa na amani kwamba niliua kwa ajili ya kukulindia heshima yako.Hakuna mwanaume yeyote anayeweza kukubali kuona mpenzi wake akifanyiwa kitendo cha kinyama kama walichotaka kukufanyia hawa jamaa.nadhani nilifanya kitu sahihi.Sijutii kosa langu kwa sababu nimefanya kwa ajili ya mtu nimpendaye”
Happy akamkumbatia Patrick kwa nguvu huku akilia .
Kwa ajili ya usalama wao usiku huo huo wakapakiwa katika gari la polisi na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Iringa mjini .

* * * *

Uchunguzi wa kesi ya mauaji inayowakabili wanafunzi wawili wa kidato cha nne Patrick na Happy ulianza kwa kasi .Wazazi wa happy wakishirikiana na wale wa Patrick waliweka mawakili sita wa kuwatetea watoto wao.Pamoja na jitihada hizo zote za kuhakikisha kuwa watoto wao wanaachiwa huru na mahakama bado kesi ikaonekana kuwa ngumu kutokana na ushahidi mkubwa wa wanafunzi kuwakandamiza Patrick na happy.Wanafunzi zaidi ya kumi walikubali kusimama mbele ya mahakama na kutoa ushahidi kuwa Patrick na Happy kwa pamoja walishirikiana katika mauaji ya Angatile mmoja kati ya wanafunzi watukutu hapo shuleni.
Baada ya miezi miwili Happy akaachiwa huru na mahakama alipoonekana hakuwa na kesi ya kujibu.Patrick ambaye alionekana kuwa ana shataka la kujibu akabaki gerezani huku kesi yake ikiendelea kusikilizwa.Huo ukawa ni ukurasa mpya wa maisha yake gerezani.
Miezi ilizidi kukatika Patrick akiwa bado gerezani akiendelea kushikiliwa kwa shitaka la mauaji.Happy ambaye alikubaliwa na uongozi wa shule yao kuwa ataruhusiwa kurudi kufanya mtihani wake wa kidato cha nne aliendelea na masomo jijini Mbeya..Alidhoofu kwa mawazo na ukiwa aliokuwa nao.Furaha yote aliyoipata kwa muda mfupi ilikuwa imetoweka.Hakuwa tena na rafiki Rafiki yake mkuu alikuwa ni Patrick ambaye kwa sasa alikuwa gerezani.Kila siku alikuwa akilia na kumuomba Mungu amsaidie Patrick aweze kutoka gerezani .Moyoni alijua ni yeye ndiye aliyesababisha Patrick kuwapo gerezani .Patrick aliua wakati akijaribu kumtetea yeye asibakwe.Aliumia sana kila alipolifikiria suala hili.
Kila mwishoni mwa wiki alikwenda kumtazama Patrick na kumpelekea vitu mbali mbali.Wazazi wa Happy halikadhalika walikwenda mara kwa mara kufuatilia maendeleo ya kesi ya Patrick na kumjulia hali.Happy alikwisha waeleza kwa kina juu ya kilichosababisha Patrick kuwepo gerezani.Wazazi wa Patrick walijitahidi kwa kila walivyoweza ikiwa ni pamoja na kuongeza mawakili maarufu wa kujitegemea katika jopo la mawakili wanaomtetea Patrick.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa familia zote mbili .
Hatimaye kikafika kipindi cha kufanya mitihani ya Taifa ya kumaliza kidato cha nne Patrick akiwa bado gerezani.Siku tatu kabla ya mtihani huo kuanza Happy akamtembelea gerezani ambako waliongea mambo mengi.
“Patrick mpenzi nasikia uchungu sana kwa hali hii.Tulikuwa na malengo mengi sana ya maisha yetu kwa siku za usoni lakini yote yameyeyuka.Sijui lini utatoka gerezani mpenzi wangu…………” Happy akashindwa kujizuia akaanza kulia ,Patrick akamkumbatia na kumbembeleza.
“ Nyamaza Happy .Hutakiwi kulia.Be strong.Haya ni mambo ya kawaida.Kila kitu hutokea kwa sababu maalum Huwezi kujua kwa nini sisi yametutokea haya.Maandiko matakatifu yanatuasa tushukuru katika kila jambo linalotufika.Sijutii kuwapo hapa kwa sababu niko hapa kwa ajili ya mwanamke nimpendaye.Kitu kimoja tu ninachokuomba jiandae vyema na mitihani yako na Mungu akujalie ufanye vizuri.Mimi nipo na Mungu atanisaidia siku moja nitatoka.Nitakuwa nimepoteza muda mwingi na mwelekeo mzima wa maisha yangu lakini nitakuwa na furaha kuwa nilipigana kiume kulinda heshima ya mtu nimpendaye duniani.Ila nakuomba kitu kimoja Happy ………”Patrick akanyamaza akavuta pumzi ndefu ,akamwangalia Happy kwa sekunde kadhaa ,akamfuta machozi .
“Happy naomba kabla muda wetu wa maongezi haujakwisha unihakikishie kitu kimoja kwamba pamoja na kuwa sijui lini nitatoka gerezani,pengine nitanyongwa lakini naomba kusikia kutoka kwako leo hii kuwa hautakuwa na mwanaume mwingine zaidi yangu pamoja na hali yangu hii kwa sasa.Naomba haya yote yaliyotokea yasipotee bure,naomba uendelee kuheshimu ahadi zetu tulizowekeana,naomba ue……………..”Patrick akashindwa kujizuia kutokwa na machozi.
“Patrick mpenzi wangu ,nyamaza kulia.Najua inauma sana na ni ngumu kuibeba adhabu hii kubwa lakini naomba nikuhakikishie kuwa kwa namna yoyote ile sintadiriki kuwa na mwanaume yeyote zaidi yako.Nitakusubiri kwa muda wote mpaka utakapotoka ili tuweze kutimiza ndoto zetu pamoja.I promise.”
Akasema Happy kisha wakakumbatiana kwa hisia kubwa huku kila mmoja machozi yakimdondoka.Muda ukaisha Happy akaombwa aondoke.

* * * *

Muda ulikwenda kwa kasi .Na hatimaye matokeo ya kidato cha nne yakatoka na Happy akachaguliwa kuendelea na kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa.Alifurahi sana kwa kuchaguliwa kwenda pale kwani atakuwa bado karibu na Patrick ambaye kwa sasa alikuwa ni sehemu ya maisha yake .Ingawa bado hakukuwa na matumaini yoyote ya Patrick kutoka gerezani kutokana na mwenendo wa kesi kuwa mgumu,lakini bado Happy alizidi kumpenda na kumpa moyo.Kila wiki alikuwa akienda kumtazama gerezani na kumpa faraja..
“Patrick matokeo yametoka “Alisema Happy alipokwenda kumtembelea Patrick gerezani mara baada ya matokeo kutoka.
“Hizo ni habari njema sana.Unakwenda shule gani ? Patrick akauliza
“nimechaguliwa kuendelea na masomo hapa hapa Iringa.Nitasoma Iringa girls.Nilikuwa nikiomba Mungu nisipangwe shule yoyote ya mbali ili isiwe vigumu kuja kukutembelea.Patrick wewe ni sehemu ya maisha yangu na kamwe siwezi kuvumilia kuwa mbali nawe.Nashukuru Mungu amesikia kilio changu .” Happy alisema huku amemkumbatia Patrick .
“Happy nimefurahi sana kusikia hivyo.Mungu bado anatupenda.Pamoja na misuko suko yote iliyotukumba lakini bado umeweza kufanya vizuri na kufaulu mtihani wako.Hongera sana Happy.Kumbuka kama imeandikwa kuwa mimi na wewe tutakuwa pamoja maishani hakuna ambaye anaweza kututenganisha.” Patrick akasema
Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwao.
Mpaka Happy anamaliza kidato cha sita bado Patrick alikuwa akisota katika mahabusu ya gereza kuu la Iringa.Kesi yake ilikuwa ikisomwa na kuahirishwa mara kwa mara.Tayari Patrick alikwishazoea maisha ya kukaa mahabusu.Afya yake ilikuwa imedhoofu kutokana na maisha magumu ya gerezani.Faraja pekee aliyokuwa nayo ni Happy aliyekuwa akienda kumtazama kila jumamosi pamoja na wazazi wake.Upendo wa Happy haukupungua hata kidogo.Kila siku upendo wake kwa Patrick ulikuwa ukiongezeka.
Jumamosi moja Happy alienda kumtembelea Patrick kama ilivyo kawaida yake.Kwa sasa tayari alikwisha maliza shule na alikuwa akisubiri matokeo ya kidato cha sita.Wakati wakiongea Patrick akamtazama Happy usoni kwa makini na kusema.
“Happy mpenzi naomba nikufahamishe kuwa Jumatatu ndo ile siku yangu ya Hukumu .Nashukuru Mungu kwani baada ya kusota gerezani kwa muda mrefu hatimaye nitaenda kusomewa hukumu yangu.Sijui nini kitatokea.Mwenendo mzima wa kesi yangu unaonesha kuwa nina hatia japokuwa kesi ilibadilishwa na ikawa ni kuua bila kukusudia...Siyo siri ninaogopa.Sijui kama nitafungwa maisha au nitahukumiwa miaka mingapi gerezani.Mungu anajua kuwa sikukusudia kufanya vile lakini nilifanya kwa sababu ya kumlinda mtu nimpendaye asidharirishwe na wahuni wale.Happy naomba usiwepo mahakamani siku hiyo ya hukumu.Sitaki uumie.Ni wewe tu ndiye unayeufahamu ukweli hivyo kusikia hukumu nitakayoipata najua itakuumiza mno.Ila kumbuka vyovyote vile itakavyokuwa naomba ujue kuwa nakupenda sana.I love you so much Happy .Wewe ni mtu pekee ambaye ninayatoa maisha yangu kwake.Sintapenda mtu mwingine kama ninavyokupenda wewe…………….”Patrick akasema kwa hisia kali
Huku akitokwa na machozi Happy akasema
“Patrick nashindwa hata niseme nini.Siku zote tumekuwa tukiomba siku hii ifike haraka ili tujue hatma yako lakini kwa sasa naona kama vile siku hii isije.lakini siwezi kuizuia isifike.I’ll be strong.Nitajitahidi kuwa jasiri na kuwepo siku hiyo ya hukumu.I must be there Patrick.I mus………………” Happy akaangua kilio.
Ilichukua muda kumbembeleza Happy .Huzuni kuu ilitanda kwa vijana hawa.Hawakuongea sana walikuwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiwa kimya.Kila mmoja akiwaza lake.

* * * *

Ni siku ya Jumatatu mahakama ilifurika watu.Wote walikuja kushuhudia hukumu ya Patrick,kijana mwanafunzi aliyemuua mwanafunzi mwenzake.
Ndugu za Patrick wote walikuwa wamewasili mapema sana hapa mahakamani.Si wao tu hata familia nzima ya akina Happy ilikuwa imewasili kusikiliza hukumu hii.Familia ya Happy na ile ya Patrick kwa sasa zilikuwa zimekwisha fahamiana na wote walikuwa kitu kimoja katika kumsaidia Patrick.
Saa mbili kamili juu ya alama gari lililowabeba washtakiwa wa kesi za mauaji ambao walikuwa wakisomewa hukumu zao liliwasili eneo la mahakama.Simanzi kuu ikatanda eneo hilo baada ya watuhumiwa wale kuwasili.Happy alishindwa kujizuia kudondokwa na machozi pale aliposhuhudia Patrick akishushwa toka katika gari maalum la kubebea mahabusu maarufu kwa jina la karandinga..Margreth na mama yake walijitahidi kumbembeleza na kumtaka ajikaze.Happy akanyamaza.
Hatimaye ule muda uliokuwa mgumu sana katika historia ya Patrick ukawadia.Muda wa hukumu.Patrick akapandishwa kizimbani akiwa ni mwenye majonzi makubwa .Macho yake yalikuwa hayaoni vizuri kutokana na machozi yaliyokuwa yanamtoka.Baadhi ya watu ambao hawakumuona kwa muda mrefu walikuwa wakimsikitikia kijana huyu kwa jinsi alivyodhoofu.Akiwa kizimbani mara akagonganisha macho yake na mama yake akajikaza na kutabasamu.Si mbali sana na alipokaa mama yake akakutanisha macho na Happy .Happy akatoa tabasamu la kulazimisha lenye kuonyesha kukata tamaa.Macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia.
Akapata faraja kubwa baada ya kugundua kuwa ndugu zake wote walikuwa wamekuja kusikiliza hukumu yake.
Jaji kutoka mahakama kuu akaanza kusoma historia ya kesi na baada ya masaa matatu ukafika ule wakati mgumu kupita wote ,wakati wa jaji kuisoma hukumu..Happy moyo ulikuwa ukimwenda mbio.Mwili wote ulikuwa ukimtetemeka.Jasho lilikuwa likimtiririka.mama yake Patrik midomo ilikuwa ikimcheza kwa uoga .Kila mtu alikuwa akiuogopa sana wakati huu.Patrick yeye alikuwa ameinama akisali kimoyo moyo akimwomba Mungu ampe ujasiri wa kuweza kuipokea adhabu yoyote atakayopewa.
Mahakama iliridhika na ushahidi wa pande zote yaani upande wa mashtaka na upande wa utetezi.Kutokana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili mahakama ikaridhia kuwa Patrick alikutwa na hatia ya kuua bila kukusudia hivyo akahukumiwa kwenda jela miaka mitano.
Mara tu baada ya hukumu kusomwa Happy akazimia na kutolewa nje kwa ajili ya huduma ya kwanza.Mama yake naye alishindwa kujizuia na kuangua kilio baada ya kumwona mwanae akipakiwa katika gari tayari kwenda kuanza kukitumikia kifungo chake cha miaka mitano.Patrick akajikaza kiume asilie ingawa alikuwa amepatwa na mstuko mkubwa .
Gari lililowabeba mahabusu likaondoka mahakamani hapo na kuacha vilio vikiendelea.mama yake Patrick naye alikuwa amezirai.Ni tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi. Hatimaye Patrick akayaanza maisha mapya ya gerezani katika gereza kuu Iringa.
Very touching ❤
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Back
Top Bottom