Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI 3

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA SITA

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Nilichoka, nilichoka, nilichoka. Nikajikuta natamka tu jina la huyu mwanamke hivyo, nikiwa siamini kama kweli ni yeye ndiye aliyekuwa amesimama mbele yangu. Maumivu yoyote niliyokuwa nahisi mwilini yakawa kama yametoweka, yaani hali yote ikabadilika. Ah! Sijui hata nisemeje. Bertha alikuwa hai! Alionekana kupendeza sana zaidi ya jinsi nilivyokumbuka kumwona mara ya mwisho kule mahakamani kabla ya taarifa za "ajali" iliyomuua kunipata. Alivaa gauni pana na zuri jekundu, mwonekano mzuri yaani kama malkia aliyejipa wadhifa wa kuwa sikuzote, na kwa kiasi fulani mwili wake ulikuwa umenawiri zaidi kuelekea kunenepa kiasi. Ilikuwa kama namwangalia Rose Ndauka mwenye mwili wa Kajala Masanja!

Kiukweli sikuamini. Fikira zote za mkazo nilizokuwa nazo kuelekea usalama wa Miryam zikaongezeka maradufu, kwa sababu hapa nilielewa sasa kwamba hatari iliyokuwa imetukumba haikupimika. Yaani ilikuwa kubwa vibaya mno. Huyu hapa Bertha, madam Bertha, alikuwa amerudi. Alikuwa amerudi na kisasi. Nilikuwa nimekwisha! Yaani kumtazama tu kulitetemesha, mpaka ningewaza bora ikiwa ni Festo ndiye ambaye angekuwa ametuteka. Ah!

Bertha sasa, alikuwa mbele yangu, akiniangalia usoni kwa utulivu, nami nikimtazama kama vile sijamjua bado ama ni mzimu ndiyo uliokuwa umesimama hapo. Hakushika chochote kile, vidole vyake akiviunganisha kwa mbele kama ilivyokuwaga kawaida yake, ndipo akatabasamu kiasi na kunishusha kwa macho yake taratibu. Nilijihisi vibaya mno, nikamtazama Miryam pembeni na kuona namna ambavyo aliniangalia kimkazo na kutoelewa, nami nikamtazama tena Bertha, presha ikiwa ishaanza kupanda.

Bertha akanitazama usoni, naye akasema, "HB."

Sauti yake ilisikika kuwa ya utulivu wa hali ya juu, nami nikajikuta napiga hatua mbili nyuma kama mtu aliyechoka sana. Bertha akatazama upande wa mwanaume mweupe aliyenielekezea bastola, na jamaa akaishusha, kuendana na mwenziye pia, kisha mwanamke huyu akanitazama na kutabasamu kiasi.

Bado nilikuwa kwenye bumbuazi zito, nami nikasema, "Hii inawezekanaje..."

Bertha akacheka kimguno na kusema, "Kinachowezekana hujawahi kukijua baby."

Nikaangalia chini na kutikisa kichwa kwa masikitiko. Yaani, sikuliona kabisa hili likija.

"Hii party isingenoga namna hii kama usingekuwa hapa uncle. Thanks," Bertha akasema hivyo.

Alikuwa amesema "uncle" kumwelekea mwanaume huyo pembeni yake, na hiyo ikanifanya nielewe sasa aina ya ukaribu waliokuwa nao.

Mwanaume huyo akasema, "Always."

Bertha akashusha pumzi na kuniambia, "Ni siku nyingi. Siyo sana, lakini... ni nyingi. Ulini-miss?"

Nikabaki kimya na kuendelea kumtazama tu usoni.

"Oh yeah, ulikuwa bize na huyu mwanamke, so... sidhani kama nimemisiwa. Sikujua hii ndiyo ingekuwa bebé yako siku ile tumekutana, oh what a twist... nilimpa manzi wako huyu offer ya kunifanyia kazi nakumbuka... halafu akasonya eh?" Bertha akasema hivyo na kumgeukia Miryam.

Miryam sasa alikuwa akimtazama Bertha kimkazo, nami nikamwangalia Bertha kwa wasiwasi mwingi na kusema, "Bertha... Miryam hakujua lolote kuhusu me na wewe.... najua una hasira na mimi, najua unataka kulipa ki... lipa kwangu mimi. Niko tayari kwa lolote, ila nakuomba umwachie.... please. Hajakufanyia baya lolote, ni mimi ndiyo mbaya wako, tafadhali..."

Bertha, akiwa ananiangalia kwa utulivu sasa, akatikisa kichwa, sijui kuonyesha uelewa, naye akasema, "Umebadilika. Umekuwa... soft zaidi. Inatia kinyaa."

Nikamwangalia Miryam pale nyuma, naye akawa ananitazama kwa njia iliyoonyesha huzuni, hofu, na hisia za maumivu kuelekea haya yote.

"Naona ni kwa sababu ya huyu mwanamke," Bertha akasema hivyo.

Nikamwangalia machoni kwa kiumakini.

"Unataka aachiwe, si ndiyo? Sawa. Mwachie," Bertha akasema hivyo.

Alielekeza neno hilo kwa watu wake nadhani, na kweli mwanamke aliyemshika Miryam akamwachia na kufanya kama kumsukuma mbele. Miryam akajitoa hapo na kunikimbilia upesi, akanikumbatia kwa nguvu huku akishusha pumzi za vilio, nami nikarudi nyuma zaidi pamoja naye huku nikimfungulia kitambaa kilichoifunika midomo yake. Najua Bertha hakuwa amefanya hivi kwa kumaanisha, nilielewa vizuri kwamba alitaka sana kuniumiza, na hii ya kumwachia Miryam ingeelekea kwenye maumivu makali sana ambayo sikutaka kuyawazia hata kidogo.

Nikaendelea kumkumbatia Miryam kwa upendo, huku nikimwangalia Bertha usoni kutokea mgongoni kwake, nami nikambembeleza kwa kumwambia, "Usijali Miryam. Kila kitu kitakuwa sawa. Usijali."

Baada ya mimi kusema hivyo, watu wa Bertha wakacheka kidogo, isipokuwa yeye na huyo mjomba wake, na mwanamke aliyekuwa amemkaza Miryam akaonekana akivuta bastola kutoka kiunoni kwake pia. Aisee! Nikamgeuza Miryam aje kwa nyuma yangu, akisimama kwa ukaribu nami huku akining'ang'ania, kiunoni, nami nikaweka kiganja changu mbele kumwelekea Bertha nikitaka kumwomba asifanye lolote baya kwa mpenzi wangu.

"Bertha tafadhali... nakuomba umwachie Mir...."

"Anachosha sana na hizi kelele zake, tuzinyamazishe tu," huyo mjomba wake Bertha akanikatisha kwa kusema hivyo.

"Mnakuwa hamna kazi, au? Kufanya haya inawapa faida gani?" Miryam akaongea hivyo kwa ujasiri.

"Mimi..." nikamwita kama kumzuia.

"Oh, kumbe na malaya wake ana mdomo..." mjomba akasema.

"Nyie wote ni wapumbavu!" Miryam akasema.

Huyo mjomba akapiga hatua kutaka kutufata, bila shaka ajaribu kumuumiza Miryam, nami nikarudi nyuma zaidi pamoja naye mpaka kugusa ukuta, lakini Bertha akanyanyua kiganja chake hewani kilichokatisha hatua za jamaa kutuelekea kilipogusa usawa wa kifua chake.

"Tumalize hii haraka, tuondoke. We're wasting time, na wameshanikera kuliko," mjomba akamwambia hivyo Bertha.

Bertha akaendelea tu kuniangalia kwa hisia makini.

Nikiwa nimemkinga Miryam bado, nikasema, "Bertha, najua hakuna kingine kitakupa furaha zaidi ya kuniumiza kama nilivyokuumiza... na nimekwambia niko tayari kwa hilo. Lakini usimuumize Miryam, hana kosa, na... ikiwa utamuumiza yeye unakuwa unaondoa na uhai ulio ndani yake pia... nakuomba... niko chini ya miguu yako..."

"Jayden..." Miryam akaniita kwa sauti ya chini.

Nikiwa namaanisha nilichosema, nikashuka chini na kupiga magoti, nikimwangalia Bertha kwa hisia, nami nikamwambia, "Unaelewa maumivu ya kupoteza mtoto Bertha... najua unaelewa. Sitaomba kingine zaidi. Nifanye lolote unalotaka Bertha... ila Miryam... mwache aende tafadhali..."

Mjomba akacheka kidogo kwa dharau, naye Miryam akashuka pia karibu yangu na kunishika usoni akijaribu kunitazamisha kwake.

"Jayden, unafanya nini?" Miryam akaniuliza kwa mkazo.

Nikaendelea tu kutazamana usoni na Bertha kutokea hapo chini.

"Jayd... kama ni kufa, nitakufa pamoja nawe. Siwezi kukuacha," Miryam akasema hivyo.

Nikafumba macho na kutikisa kichwa kwa huzuni.

"Umenisikia Bertha?" Miryam akasema hivyo.

Nikafumbua macho na kumwangalia.

"Lolote unalotaka kumfanya Jayden, nifanye na mimi pia," Miryam akamwambia hivyo.

Nikamwangalia kwa wasiwasi na kusema, "Mimi..."

"No. Hata useme nini Jayden... siwezi kukuacha. Ukiishi naishi nawe, ukifa nakufa nawe," akaniambia hivyo.

"Mi... usi... hhh... Bertha, please... nisikilize tafadhali. Kile ambacho..."

Miryam akanikatisha kwa kumwambia Bertha, "Hukuweza kuwa mama bora kwa mwanao, na ukawa mtu mbaya zaidi alipokufa. Hayo siyo makosa ya mtu yeyote isipokuwa wewe pekee. Unahamishia hatia unayohisi juu yako mwenyewe kwa kuwaumiza wengine, unafikiri hiyo itakupa furaha? Never. Chukua uhai wangu, wa Jayden, au wa yeyote unayetaka lakini mwisho wako pia utafika tu. Hautabaki na lolote la zaida, utakuwa mtu wa kujionea huruma mwenyewe ukifikiri utaridhika kwa kufanya unyama..."

"This bi***! Bertha..."

Mjomba mtu akaongea hivyo kwa hasira kuonyesha chuki kuelekea maneno ya Miryam, na akitaka Bertha amruhusu kumfanya mwanamke wangu jambo baya. Nilihofia zaidi sasa, nami nikamkaza Miryam kiganja huku nikiona jinsi alivyokuwa anamwangalia Bertha kwa hisia kali, asiogope lolote lile kabisa. Nikamwangalia Bertha, ambaye mpaka sasa bado alikuwa akinitazama tu, kisha akashusha pumzi kama kujipa utulivu na kuangalia juu.

"Naelewa maumivu ya kupoteza mtoto... sitabaki na lolote la ziada... mhm," Bertha akasema hivyo.

Nikabaki nikimwangalia kwa umakini.

Akanitazama, kisha akasema, "Nafikiri tabasamu la kuridhika lilikuponyoka siku uliyosikia nimekufa, eh? Ulifurahi..."

Nikawa natikisa kichwa kukanusha hilo huku nikimwangalia kwa hisia.

"Uliridhika kabisa ulipodhani umenimaliza, na kujua kwamba nisingekuwepo maishani mwako tena kukakupa bichwa... ukajiona ume-win," akasema.

"Bertha..." nikaishia kuita tu jina lake.

"Muda mwingine unajua nilikuwa nakaa nawaza... hivi kweli... hakukuwa na kitu fulani unanificha? Ahh... nikapuuzia ishara zote kabisa kuona rangi zako, yaani... ukanipumbaza. Nakiri hilo uncle, yaani hata Charles hakuwahi kufikia hicho kiwango cha kunifanya mpumbavu kama huyu kijana, na hakutumia dawa wala nini. Ilikuwa ni yeye tu. Yeye tu... ndiyo uliokuwa ujanja wake huo kwangu, akanitia udhaifu mpaka nikajisahau... nikaanguka..."

Mjomba mtu akatikisa kichwa kihuzuni huku akitutazama kwa chuki, nami nikaendelea kumwangalia Bertha machoni.

"Na tena uliponiangusha bado nikaendelea kuwa chini kwa sababu ya huo huo ujanja wako ulionikamatia... ukaendelea kunikandamiza ili niwe dhaifu zaidi. Nilidhani ndiyo umenimaliza, kwamba nisingeweza kunyanyuka kabisa, lakini ni wewe tena ndiyo ukanitia nguvu ili nisimame upya... na nimeweza kusimama tena... kwa sababu yako," akasema hivyo.

Kauli yake mwishoni nilishindwa kuielewa kabisa, na kwa kuona hilo, Bertha akaamua kunielewesha vizuri. Akashika sehemu ya mbele ya nguo yake pana na kuiachanisha, kama kusogeza pazia yaani, nami nikatazama hapo na kukaza macho kwa umakini baada ya kuona namna ambavyo tumbo lake lilionekana kutuna. Eh! Alikuwa na ujauzito! Nikamwangalia usoni tena, yeye akinitazama kwa utulivu wake tu, na maana ya maneno yake ikawa wazi kwangu. Miryam akanitazama usoni, mimi pia nikamwangalia, ikiwa kaa njia ya maswali mengi sana ambayo nisingeweza kumpatia majibu ambayo yangetosha kwa wakati huu, nami nikamtazama Bertha tena.

Akamwangalia Miryam, naye akamwambia, "Ukiongea kuhusu furaha kwa mtu kama mimi, judge unavyojua kwa chochote unachohisi unajua, lakini never say never. Siyo wewe pekee ndiyo unacho kinachokupa kiburi kwamba unaijua furaha zaidi ya wanawake wengine honey... hata mie ninacho, na ni HB wetu ndiyo amenipatia."

Aisee!

Miryam akashusha macho yake, kihuzuni yaani, nikiona namna alivyovunjwa sana moyo na jambo hilo. Nikakosa hata cha kusema, yaani mapya kwa mapya yalizidi kuibuka hapa.

Nikasema, "Bertha...."

"Baada ya kunifanyia ulivyonifanyia JC... ukafikiri nimekufa... ukajipatia mwanamke mwingine... unaenda kuzaa naye... sasa hivi umejua niko hai, na nimebeba mtoto wako... unafikiri natakiwa kufanya nini?" Bertha akaniuliza hivyo.

Nikatikisa kichwa kwa kusihi asifanye ubaya.

"Ningeshauri umuue tu, lakini hiyo itakuwa adhabu ndogo sana," mjomba mtu akasema hivyo.

"Right. Natakiwa nikufanye uhisi maumivu niliyopitia," Bertha akaniambia hivyo.

Nikamwambia, "Bertha najua huwezi kuamini hata nikisema sikufurahishwa na yote yaliyotokea. Sikuridhishwa kukuona vile, lakini kwa sehemu kubwa nilifanya yale ili kukuzuia usiendelee kufanya mabaya. Na sikujua kuhusu hili... sikufikiri ungekuwa ume...."

"Ulitaka niache mabaya? Baby... hukuwahi kuona ubaya wangu, sasa hivi ndiyo utaujua," Bertha akasema hivyo.

"Bertha...."

Akamwangalia Miryam na kusema, "Hujakosea dear. Sikuwa mama bora, na mimi ni mbaya kuliko unavyoweza kufikiria. Utaliona hilo now."

Nilihisi hofu kubwa kusikia maneno hayo kutoka kwa Bertha. Sikuwa na muda wa kusema lolote tena, kwani Bertha akaonyesha ishara kwa kichwa kuwaelekea wanaume wake hapo hapo, nao wakatusogelea mimi na Miryam, wakitushika kwa nguvu mikononi. Miryam akazidi kuning'ang'ania, huku nami nikimkaza zaidi kwangu, na baunsa mweusi akanipiga ngumi usawa wa ubavu ili kunilegeza kiasi, vilevile na yule mweupe ambaye akashika nywele za Miryam na kuzivuta kwa nguvu, mwanamke wangu akianza kulia kwa sauti ya juu.

"Bertha, please!"

Nikasema hivyo nikiwa nimeghafilika mno, na wanaume hao wakatutenganisha mimi na Miryam kwa kutuburuza pande tofauti za chumba hicho. Jamaa akaniachia na kuninyooshea bastola kichwani, huku Miryam akianza kufungwa mikono yake kwa nyuma na kuzibwa mdomoni tena kwa kitambaa, akilia kwa uchungu huku ananiangalia usoni. Mwanamke yule pembeni ya Bertha akamsogelea Miryam pia huku akielekeza bastola yake kichwani kwa mpenzi wangu, nami nikajinyanyua na kupiga magoti, nikijishika tumboni kwa mkono mmoja na kunyoosha mwingine kumwelekea Bertha kuomba asifanye ubaya kwa Miryam.

"Bertha... nakuomba... nitafanya lolote kwa ajili yako... niue ikiwa itakufaa... nakuomba... mwachie Miryam... tafadhali..." nikaongea kwa hisia.

Bertha akawa akinitazama kwa mkazo sana, huku mjomba wake na wengine wakimwangalia yeye pia kama kusubiri aseme jambo fulani, naye akageuza shingo yake kumwelekea mjomba wake huyo na kutikisa kichwa mara moja kutoa ishara. Nisingeelewa maana ya hilo, lakini mwanaume huyo akachomoa bastola kutoka kiunoni kwake na kuanza kumfata Miryam. Niliogopa mno.

Nikaanza kutembelea magoti upesi kumwelekea Bertha huku nikisema, "Usifanye hivi Bertha... please..."

Baunsa wa upande wangu akanikanyaga miguuni kwa nguvu na kunisukuma nianguke, na ni hapo ndiyo mjomba mtu akamfikia Miryam na kuiinua bastola yake hewani, mimi nikihisi kama nakaribia kupasuka kwa hofu iliyokuwa ndani yangu, naye akaishusha bastola hiyo na kumpiga nayo Miryam nyuma ya shingo yake kwa nguvu!

Nilishtuka sana, mshtuko ambao uliendana na kishindo cha mwili wake Miryam alipodondoka kwa kupoteza fahamu. Kisha, yule mwanamke mwingine akafungua kinguo cheusi chenye muundo kama mfuko, naye akakitumia kukivalisha kichwa chake Miryam na kusaidiana na jamaa mweupe kumnyanyua. Nilibaki hapo chini nikiwa nimelala na kuangalia hayo yote yakifanyika, nisijue la kufanya yaani, nami nikamwona mjomba wake Bertha akituma ishara kwa kichwa kumwelekea baunsa wa upande wangu, na hapo hapo nikahisi kitu kizito kikipiga kichwa changu kutokea nyuma, na yote yaliyokuwa mbele ya macho yangu yakageuka kuwa giza zito.

★★★

Giza zito liliofunika fahamu zangu likaanza kupenyeza kitu kama mwanga hafifu uliokuwa ukiyataka macho yafunguke, lakini bado ikawa ngumu kiasi kufanikisha hilo. Kilichozidi kuonekana mbele ya macho yangu yaliyofunikwa na giza hilo kikawa vitu kama mawaya-waya mengi, yaani maruerue, na ndipo maumivu yakahisika zaidi kichwani kwangu. Nikajitahidi kulazimisha mambo na kufanikiwa kufumbua macho, lakini mbele yangu hakukuonekana taswira yoyote yenye kueleweka. Na hata zaidi, nikaanza kusikia sauti za mvumo wa gari, mimi mwenyewe nikihisi kuwa mwendoni kutokana na mwili wangu kutikiswa huku na huku, na ndipo nikatambua sasa kihalisi ni hali gani nilikuwa ndani ya.

JC hapa nilitekwa. Mtekaji alikuwa ni Bertha, madam Bertha. Mikono yangu ilifungwa kwa nyuma, kichwa kikifunikwa kwa nguo-mfuko nyeusi, na nadhani nilibananizwa kwenye kona ya gari lililohisika kuwa na uwazi kwa upande wa nyuma; labda muundo wa hiace. Kichwa kiliuma, hilo likiwa ni athari ya kupigwa na "mjomba" wake Bertha mpaka kupoteza fahamu, na sasa tulikuwa mwendoni kuelekea mahali pasipojulikana kwangu. Na Miryam... oh Mungu wangu! Miryam angekuwa wapi?

Kumwaza tu kukafanya nikumbukie namna ambavyo yeye pia alipigwa na kupoteza fahamu mbele ya macho yangu, na jambo hilo likafanya nitahamaki sana moyoni. Ningetakiwa hata nijaribu kunyanyuka na kufanya ujanja fulani, lakini hilo lisingekuwa na faida hapa. Bertha alikuwa hai, kwisha nilikuwa nimekwisha. Sijui alikuwa akipanga kunifanya nini, lakini macho yake yalionyesha hasira ambayo ingeniachia maumivu mengi, najua, na ndiyo alikuwa akinipeleka huko alikojua yeye ili niyapitie. Kiukweli ningeweza kumwacha anifanye lolote lile, lakini kumwacha amuumize na Miryam siyo jambo ambalo ningesimama kutulia na kuona likifanywa. Lakini ningefanya nini? Ujanja wote ulikuwa umenitoka!

Nilihisi kuishiwa nguvu kiakili. Nilijilaumu kwa kupuuzia alama zote za tahadhari zilizoonekana mapema ingawa zilikuwa ndogo sana. Mtikisiko wa gari na mwendo usio wa kasi sana ulinifanya nitambue kwamba tupo kwenye njia isiyo rasmi, hivyo nadhani watu hawa walinileta maeneo yaliyo mbali sana na jijini. Sikujua ni muda kiasi gani ulipita toka nipoteze fahamu, ila najua masaa yalikatika. Sikusikia sauti ya mtu hata mmoja akiongea ndani ya gari hili, na kiukweli, kichwa kiliuma mpaka kizunguzungu cha kunirudisha kwenye kupoteza fahamu nikakihisi. Nilijisikia vibaya mwilini, hasa kwa sababu siku iliyopita sikuwa nimelala, lakini nikajitahidi kujikaza hivyo hivyo tu na kutulia mpaka ilipokuwa wazi kwamba gari limesimama.

Kilichofuata, sauti za hatua ndani ya gari kunielekea zikasikika, nami nikashtukia navulishwa kilichonifunika kichwa upesi. Nikafumba macho, na nadhani aliyenifunua uso akafikiri bado nimepoteza fahamu, hivyo akaanza kuniamsha kwa kunipiga-piga makofi yasiyo mazito sana shavuni. Akawa anakigeuza na kichwa changu kwa nguvu, nami nikamwangalia hatimaye na kutambua ilikuwa yule baunsa mweusi wa Bertha. Alipoona nimemwangalia, akafungua mlango wa nyuma wa gari hili, tena miwili, kisha akashuka na kunishika mikono kwa nyuma. Akanivuta nje kwa nguvu mpaka nikadondoka ardhini, kukiwa na hali laini kiasi kutokana na uoto wa nyasi nyingi ingawa zilichoma-choma. Ilionekana kuwa jioni, jua likiwa linaelekea kutua.

Nikiwa nimelala chini hapo, nikajaribu kulitathmini eneo hilo kidogo, lakini halikufahamika kabisa kwangu. Ilikuwa ni kama vile tuko porini, lakini miamba mikubwa ikionekana pande na pande kulizunguka, nami nikajigeuza kimwili na kumwangalia mwanaume huyo.

"Miryam yuko wapi?"

Nikatamka maneno hayo huku nikikaza maumivu kichwani, lakini hakunijibu chochote na kuangalia upande mwingine wa eneo hilo. Mwenzake, yule baunsa mweupe, akatokea upande wa mbele wa gari nililokuwemo, naye akajiunga na mwenzake hapo kisha kwa pamoja wakaninyanyua mpaka nikasimama. Nikiwa napumua kwa uzito, nikaangaza huko mbele na kuona gari lingine jeusi lenye kufanana na Escalade (la gharama), na ndiyo watu hawa wakaanza kuniongoza kulielekea. Nikawaza kuwa bila shaka humo angekuwepo bosi wao, na ni hasira ndiyo zikaanza kujaa ndani yangu kwa kuwa sasa nilitaka zaidi kujua wamemweka Miryam wapi. Nisingejali kingine ila mwanamke wangu awe salama, na kama Bertha angewaza kumuumiza, yaani ingekuwa ni bora aniue mimi kwanza.

Kufika karibu na gari hilo, nikatambua kwamba eneo tulilokuwepo lilikuwa ni mwamba wa mwishoni, yaani, hatua kadhaa kuelekea mbele na hiyo ardhi ya mwamba huu ingekwisha, hivyo kungekuwa na bonde refu sana kuelekea chini kama tu namna ambavyo miamba ya maporomoko ya maji huwa. Aisee! Sijui walikuwa wanapanga kuniua na kunitupa huko? Mimi na Mimi wangu pia? Wazo hilo likanitia hofu kubwa kwa ajili ya Miryam, nami nikabaki kulitazama gari hilo kwa umakini. Najua kulikuwa na watu kwa ndani wakiniangalia, na walipenda sana kufanya hivi vioja vyote kama kwenye filamu, lakini niliuona kuwa upumbavu.

Nilichotaka ilikuwa kujua Miryam yuko wapi, hata kama wangeniua, ningemwomba Bertha kwa vyovyote vile amwache mwanamke wangu. Ikiwa asingeweza hilo, basi kile alichoomba Miryam ndiyo ningemtaka akifanye pia. Aniue mimi pamoja na Miryam pamoja. Uwe mwisho wa mapenzi yetu pamoja. Basi. Dakika moja hivi ya kusimama hapo na mlango wa mbele wa gari hilo ukafunguka, akitoka yule "mjomba" wa madam Bertha. Sura yake ya kigaidi fulani hivi ilinifanya nihisi hasira kali sana nilipokumbukia namna alivyompiga Miryam. Nikataka kumfata kwa hasira lakini wanaume hawa wakanikaza zaidi, na huyo mjomba akasimama usawa wa hilo gari huku akinitazama kwa ujeuri.

"Miryam yuko wapi? Yuko wapi?!"

Nikauliza hivyo kwa sauti ya juu, na mmoja wa mabaunsa hawa akanitandika ngumi nzito tumboni. Ah, iliuma! Nikapiga magoti chini nikihisi maumivu makali, mpaka nikatambua kuna sehemu kwa ndani ilikuwa imeanza kuvuja damu. Jamaa akakishika kichwa changu na kunitazamisha kwa huyo mjomba, naye mjomba akafungua mlango wa siti ya nyuma kwenye gari hilo. Nilitarajia kwamba alikuwa akimfungulia Bertha bila shaka, lakini tarajio hilo likabadilika baada ya kumwona Miryam akiwa ndani ya gari hilo. Yaani, nilichoka kwa nilichokitazama mbele yangu!

Akiwa ameketishwa nyuma ya gari hilo la kifahari, Miryam alionekana kuwa kama mtu aliyepigwa vibaya sana mwilini kwa ukatili wa hali ya juu. Ilikuwa ni kama vile amepondwa-pondwa kwa matofali mwilini! Nguo zake zilichanika-chanika, kichwa chake kikiegamia siti aliyokalia kwa njia iliyoonyesha hakuwa akijitambua, uso wake ukifunikwa na nywele zake zilizovurugika na damu zikionekana kuitawala ngozi yake nyeupe ya uso. Nilibaki nimepiga magoti hapo chini nikiangalia jambo hilo kwa mshtuko wa hali ya juu. Sikuweza kuongea, sikuweza kujongea!

Mjomba mtu alikuwa amesimama hapo hapo akiniangalia kwa njia ya kuridhika, na kutokea upande wa pili wa gari hilo kwa mbele akaonekana madam Bertha, akija taratibu sehemu hii tuliyokuwepo huku mwanamke yule ambaye alimshikilia Miryam wakati ule tupo kule deluxe room akifuata nyuma yake. Mwonekano wake Bertha ulikuwa tofauti Kwa wakati huu, lakini sikujali lolote tena lililoendelea pembeni yangu zaidi ya kile nilichokiona mbele yangu. Niliishiwa nguvu kabisa. Kumwangalia Miryam namna hiyo, yaani nilihisi ni kama vile naota. Sikuelewa kilichompata, na sikujua ikiwa bado alipumua, lakini tamaa yote ndani yangu ilikuwa imekatishwa hapo hapo. Bertha alinimaliza.

Rundo la machozi likafurika machoni mwangu, nikihisi maumivu makali sana moyoni. Bertha aliendelea kusimama sehemu hiyo pamoja na wengine huku wakiniangalia tu, kisha bila hata kumtazama nikaona akitoa ishara Kwa kichwa kumwelekea mwanamke yule pembeni yake, naye akatoka alipokuwa na kwenda hadi walipomkalisha Miryam nyuma ya gari hilo. Akaushika mwili wa Miryam na kuuvuta kwa nguvu, akitaka kumtoa nadhani, nami nikaingiwa na hasira kali sana iliyonipa nguvu ya kunyanyuka upesi na kumfata mwanamke huyo kwa kasi.

"Usimshike, mpumbavu wewe!"

Nikapiga kelele namna hiyo huku nikiwa karibu kabisa kumgusa, na wale wanaume wawili wakafanikiwa kunikamata kabla sijamfikia kabisa. Bertha alishtuka kiasi na kupiga hatua chache nyuma, huku mjomba akija mbele yake, na mimi nikawa nafurukuta kwa nguvu nikitaka nimshike yeyote kati yao ili nifanye lolote juu yao.

Mjomba wa Bertha akanifata, mabaunsa wakinishikilia bado, naye akanipiga ngumi usoni na ubavuni mara sita mfululizo, kitu kilichofanya nirudi chini kwa kupiga magoti, na hatimaye nikadondokea ubavu mmoja kwa kuulalia ardhini. Nilianza kutokwa na machozi ya hasira kali sana, nikimwangalia mwanamke yule ambaye alifanikiwa kumtoa Miryam kwenye gari hilo na kuuporomosha mwili wake ardhini hapo. Yaani Miryam alikuwa amepondeka sana, asiweze kujongea hata kidogo, nami nikawa nahofia huenda tayari alikuwa mbali na uhai wake. Sikuamini kabisa!

Nikajitahidi kujiburuza hivyo hivyo kumwelekea mpenzi wangu, maumivu yangu na kizunguzungu kikinipa wenge zito kichwani, lakini nikakomaa tu mpaka nikakaribia kumgusa kichwani. Miguu yangu ikakanyagwa kwa nguvu sana kutokea nyuma, nami nikatoa sauti kuonyesha maumivu huku nikikaza meno kuyasitiri kwa kulazimisha. Nilichohitaji kilikuwa hata kumgusa tu mpenzi wangu, lakini watu hawa wakatili hawakutaka hata hilo nifanikishe.

Nikawa najaribu kuzishika hata nywele za Miryam, lakini nikashindwa. Niliumia sana. Na sehemu hiyo ya maumivu yangu haikuonekana kumtosha Bertha bado, kwa kuwa alipata alichokitaka kwa kuutesa kwanza moyo wangu, kisha naelewa angetaka kunimaliza na mimi pia. Lakini kufikia hapa nilipoteza matumaini mengine yote ya kuendelea kuishi. Ikiwa Miryam na mwanangu wangekuwa wamekufa, mimi ningebaki kufanya nini? Sikutaka kuishi tena.

Nikafumba macho kwa nguvu, nikikaza meno na pumzi zikitetemeka kwa msisimko mbovu mwilini, nami nikasema, "Bertha... hh sss... nakuomba uniue sasa hivi..."

Niliongea kwa mkazo, huzuni, na hisia zilizovurugika kwelikweli, nami nikamsikia mjomba mtu akicheka kidogo na kusema, "Bold."

Nikanyanyua uso wangu kumwelekea Bertha, nikikuta ananiangalia kutokea hapo aliposimama kwa umakini tu, nami nikamwambia, "Kama imekupa furaha.. hhh... na umeridhika... niue tafadhali..."

Mjomba wake akamtazama Bertha kwa umakini, mwanamke huyo akiniangalia tu, naye mjomba mtu akachomoa bastola kutoka kiunoni kwake na kuiweka mkononi kwa njia iliyoonyesha anataka Bertha aichukue.

Nikasema, "Yeah... kill me. Kwa sababu ninaapa Bertha... usiponiua... mimi nitakuua."

Papo hapo Bertha akaikwapua bastola aliyoshika mjomba wake kwa hasira na kuielekezea ardhini hapo nilipokuwa, naye akafyatua risasi moja iliyopasua sauti kali sana!

Nilikuwa tayari kuipokea, yaani kifo sikukihofia tena wakati huu, lakini kilichofuata ilikuwa ni kukatishwa tamaa juu ya hilo. Risasi aliyofyatua haikuwa kwa ajili yangu, bali ikatua juu ya kichwa cha mpenzi wangu na kurusha damu zilizonirukia mpaka usoni! Yaani, ah! Alikuwa ndiyo ananionyesha kwa mara nyingine kwamba mpenzi wangu asingekuwa wangu tena, na kuliona hilo waziwazi kulinitia maumivu zaidi ya niliyokuwa nikihisi mwanzoni.

Nikabaki nimeganda tu kuangalia kile ambacho kwa sasa ningeita ni maiti ya Miryam, nami nikaanza kulia Kwa uchungu zaidi na kuinamisha uso kugusa nyasi. Iliuma sana. Nikazishika nyasi kwa kuzivuta kwa nguvu sana na kupiga kelele kwa sauti ya juu, lakini huzuni yangu haikusaidia chochote tena. Machozi kama ya mtoto ndiyo yakabaki kunitiririka tu, nikingoja risasi nyingine ifuate kwa ajili yangu ili hatimaye injini yangu JC izime, lakini ombi langu halikutimia.

Walionikanyaga miguu wakaiacha hatimaye, nami nikanyanyua uso kuona namna walivyokwenda kuishika miguu ya Miryam na kuanza kuuburuza mwili wake kuelekea mwishoni mwa mwamba huo pale mbele. Kisha, wakanyanyua mikono na miguu na kuanza kuubembesha kimakusudi huku wakinitazama, halafu wakautupa kwa nguvu huko chini... mbali sana! Aisee! Yaani sijui hata nisemeje.

Nikiwa nimebaki kupatazama huko tu, Bertha akachuchumaa baada ya kunisogelea karibu, na hata sikumwangalia, lakini ikiwa wazi kwamba yuko karibu na sikio langu, akaniambia kwa sauti ya chini, "Bado."

Nikaanza kushusha pumzi kwa kujituliza zaidi, nami nikamwangalia usoni taratibu, na kwa umakini.

Akaiweka bastola yake usawa wa kidevu changu kukinyanyua juu kidogo, naye akaniambia, "Sijaridhika. Ndiyo nimeanza."

Aisee!

Akakisukuma kidevu changu na kusimama, kisha akaanza kulielekea lile gari huku akifuatwa na bodyguard wake mwanamke, akiniacha chini hapo na maumivu yangu tele. Alikuwa ndiyo ameanza tu. Yaani, hili lilikuwa ni trela, sinema yenyewe ndiyo ingefuata. Sijui alikuwa akipanga nini, lakini ni wazi alihitaji nibaki hai Ili nijionee mwenyewe. Mawazo yote ya mambo ambayo angefanya yalifunikwa zaidi wakati huu kwa jambo alilokuwa ametoka kunifanyia, yaani sikuweza kuamini kama kweli Mimi wangu aliondolewa maishani mwangu namna hiyo. Nguvu zilinikimbia kabisa. Nisingeweza kufanya lolote tena, ni kama vile Bertha alikuwa ameiua nafsi yangu pia.

Mabaunsa wake wakaja mpaka hapo nilipokuwa, wakisemeshana mambo fulani na mjomba wa Bertha, kisha jamaa akaenda kwenye gari aliloingia Bertha na mngurumo ukasikika. Nikiwa kama vile sijitambui, mabaunsa wakaninyanyua kwa nguvu na kunirudisha kwenye gari walilonitoa muda mfupi nyuma. Nadhani waliona namna ambavyo nilimaliza nguvu kihisia na kimwili kiasi kwamba hawakuhitaji kunifunga kamba wala kuufunika uso wangu tena, na gari likawekwa mwendoni kutuondoa sehemu hiyo. Hakukuwa na kingine kilichopita akilini mwangu isipokuwa taswira ya mwanamke wangu ambaye aliondolewa uhai mbele ya macho yangu, kwa sababu ya makosa yangu mwenyewe. Ningefanya nini bila Miryam sasa? Ningekuwa nani tena mimi?

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Whatsapp +255 678 017 280
 
Dah🥲
Mpaka nimeipata huzuni
Mimi, Binti wa watu anakufa kwa kulipia dhambi za JC!?
Mapenzi 💔🤔
Ila moto wa mjomba wake Bertha....😔😔
 
Daah this is more than a story 🥹
 
Dah! RIP Mimi...nimeumia aisee, Maryiam amekufa kwa makosa ambayo hayamuhusu kabisa
 
NA MIMI 3

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA SABA

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Sikuwahi kudhani maisha yangu yangekuja kugeuka kuwa mabaya kwa ughafla namna hii. Mimi Jayden, sasa nilikuwa nimetekwa na mwanamke mwenye kisasi dhidi yangu, na alitoka kufanya jambo zito mno lililoniondolea hamu ya kutaka kuendelea kuishi kabisa. Kila nilipofumba na kufumbua macho, ni taswira moja pekee iliyokuwa mbele yangu, taswira ya jambo baya alilofanya mwanamke huyo kwa mwanamke niliyempenda sana. Bado sikuamini kama yale yaliyotokea yalikuwa yametokea kweli, lakini kumbukumbu zote zilirejea pale pale na kuendelea kuichoma nafsi yangu kila nilipolazimika kuliona tukio lile akilini mwangu.

Iliendelea kujirudia na kujirudia kichwani kwangu, jinsi ambavyo Miryam alikuwa amefanywa. Kutokea ndani ya lile gari, mpaka alipotupwa mbali kwenye lile bonde. Hakukuwa na hisia mbaya zaidi kwangu kuliko kujua yote hayo yaliyompata yalisababishwa na mimi, na hata kutamani muda urudi nyuma ili mambo yabadilike ilionekana kuwa unafiki wa hali ya juu kutoka kwangu. Hakukuwa na mwingine wa kulaumu isipokuwa mimi mwenyewe. Kama ni jambo la kustahili ambalo nilitakiwa kupata sasa, basi ni adhabu kubwa kuwa chanzo cha mateso na kifo cha mpenzi wangu niliyempenda sana, na nilichohitaji kinipate kilikuwa ni kile kile kilichompata yeye ili hatia yote niliyohisi iambatane naye kwa njia iliyostahili.

Sikujua mahali nilikokuwa, lakini najua ilikuwa imepita siku moja kuelekea ya pili tokea Bertha anifanyie kisa kile mpaka sasa. Nilikuwa ndani ya chumba kilichoonekana kuwa kwenye nyumba moja nzuri, kukiwa na mandhari safi, kitanda, sofa, kabati, na vifaa bora vya chumbani kana kwamba iliikuwa chumba cha hoteli za kupangisha. Mikono yangu na miguu ilifungwa huku nikiwa nimeketishwa sofani, na nakumbuka, kwa masaa kadhaa yaliyopita, mmoja wa vikaragosi wake Bertha alikuja kujaribu kunipa chakula eti, lakini sikutaka kula chochote. Sikuwa nimekula wala kunywa chochote kile kutokea usiku niliokuwa hospitalini na mwanangu.

Alijaribu kunilazimisha kwa kuupiga mwili wangu, nile, lakini sikufungua mdomo na kumwacha akinitukana na kuondoka zake. Yaani niliendelea kubaki nimekaa hapo hapo nikifungwa kama mbuzi anayengojea kuchinjwa, mkojo nilioruhusu unitoke ukiwa umeshakaukia kwenye suruali, nikiwa sina hali. Mwili ulihisika kwa namna ovyo sana, lakini ndiyo jambo nililoona linafaa kwa wakati huu na kusonga mbele. Nilitaka kufa, kwa hiyo kama kunifunga kwao ilikuwa ni ili nisitoroke ama nisijiumize wangejua wao, ningeiruhusu njaa hii iniue taratibu tu ikiwa wangechelewesha kuyaleta mauti kwangu. Ndiyo kilichokuwa kimebaki.

Nimeendelea kukaa hapo hapo tu kwa dakika na masaa na masaa, pumzi zikinitoka kwa uchovu mwingi, na likiwa ni jira nisilotambua hata kidogo, mlango wa chumba hicho ukafunguka na viumbe fulani kusikika wakiingia. Hata kwa hali yangu mbaya ningeweza kuelewa hakuwa mtu mmoja, lakini sikujali. Macho yangu yalielekea chini, nikiwa nimeegamia sofa kama vile nguvu zote zimeniisha, ndipo sauti zikaanza kusikika hapo.

"... yuko hivi hivi tokea jana usiku...."

"Nilikaa kumwangalia, yaani ametulia hivyo hivyo..."

"Na hataki kula. Nikamlazimisha, lakini wapi. Nikakiacha hicho hapo mpaka sasa hivi hajakigusa..."

"Angekigusa vipi wakati amefungwa?"

Sauti iliyouliza swali hilo ikatambulika kwangu, na haikuwa ya mwingine isipokuwa Bertha mwenyewe. Leo ndiyo alikuwa amekuja. Ukimya ukafuata baada ya yeye kuuliza hivyo, nami niliendelea kutulia tu nisijali lolote tena. Kisha nikasikia sauti kama ya kiti kuvutwa, kikiletwa karibu nami hapo nilipokaa, halafu nikaona mjongeo mbele yangu ulioonyesha kwamba mtu alikaa hapo. Harufu nzuri iliyoingia puani mwangu ilinijulisha kwamba alikuwa ni Bertha, lakini ilinikera sana. Nikazidi kujihisi vibaya mwilini, nami nikapeleka macho yangu pembeni zaidi kwa kutotaka kumtazama mwanamke huyo.

"Nimefika HB. Pole nimekawia, kuna vitu nilikuwa naweka sawa kwanza. Hope hujani-miss sana," Bertha akaongea hivyo.

Nilimsikia vyema, lakini sikuwa na hisia yoyote ile yenye kunilazimu nijali chochote hapo.

"What is this, nasikia unagoma kula wakati kinatengenezwa chakula poa kabisa? Umeanza lini tabia mbaya?"

Kicheko laini kilisikika kutoka kwa watu wake hapo, akiwa ameniuliza kwa kejeli nyingi.

"Kwa hiyo nini... unataka kujiua HB?" Bertha akauliza hivyo.

Nikaendelea kunyamaza zangu.

"Look at you... hivi wewe... daktari eti, unakataa kula kisa nini? Halafu unajikojolea? Unataka nini, attention?" Bertha akasema hivyo.

Nikabaki kama nilivyokuwa.

"Oooh... hii yote kwa sababu baby mama wako mtarajiwa ameenda kuionja kuzimu eh? Ndiyo maana umesusa? Na uneninunia?"

Kauli yake ikanifanya nifumbe macho baada ya kumbukumbu ya Miryam kunirudi kichwani.

Bertha akabana kicheko laini na kusema, "Usiwe hivyo bwana. Ona... usinune kwa sababu ya hilo, haina maana tena HB. Mimi niko hapa, na ninamleta mtoto wetu ndani ya miezi michache tu. Kwa nini unahuzunika sasa? Unapaswa kuwa na furaha jamani."

Ikiwa ningetaka, ningeweza hata kumtemea mate usoni, na nasema hivyo huku nikijua mate yalikuwa yamekauka, lakini kejeli zake hazikunipa maumivu zaidi ya yale aliyokuwa ameshanipa. Alikuwa akijisumbua tu.

"Ona baby, nimekuletea chakula kizuri. Tena... nimepika mwenyewe, si mmeona nimekipika jamani... nimempikia baby wangu?"

Bertha alisema hivyo kama kuwaambia na wengine waliokuwemo, na nadhani wangempa kichwa kwa kukubali. Njia yake ya kuongea ilionyesha alikuwa anafurahia sana kuanza kunitesa namna hii, na naona hali yangu mbaya ilikuwa inampa mridhiko wa hali ya juu. Ila najua pia hakuwa amemaliza, lakini nilikuwa mbali mno kujali tena alichotaka kunifanyia kwa zamu hii.

"JC..." akaniita.

Nikabaki kimya tu.

"Niangalie," akasema hivyo.

Ni kama alikuwa akiongea na mfu tu hapa.

"Kwa hiyo hutaki kuniangalia?" akauliza.

Kimya.

"Niangalie!" akafoka kwa sauti ya juu.

Sijui nini kilifuata baada ya hapo, lakini sikumwangalia, ila nikahisi hatua zikija karibu nami lakini zikakatishwa.

"No, it's okay. I got this..." Bertha akasema hivyo.

Ni kama alikuwa anamzuia kikaragosi wake mmoja asije kunigusa, labda kunilazimisha nimwangalie madam wake.

"Well... hutaki kuniangalia nikikubembeleza, basi sawa. Ngoja nitumie fimbo," Bertha akasema hivyo.

Kama alitaka kunichapa, basi ningepokea hizo fimbo zote, lakini nisingemwangalia.

"Sihitaji kukupa motivation kubwa sana ili unipe nachotaka, but with you nimeshagundua huwa hautembei mpaka usukumwe. Hope this will do the trick..." akasema kwa sauti tulivu.

Alikuwa na maana ya kutaka kuniumiza ili nimpe alichotaka, lakini mimi hapo ndiyo nilihitaji aniumize alivyotaka na nisingejali. Sema, maumivu aliyotaka kuyaleta kwangu yangekuja kwa njia ambayo nisingetarajia kabisa, kwa sababu sikujua aliwaza nini. Nikiwa nimekaa namna hiyo hiyo, Bertha akaanza kuweka vitu fulani vilivyoonekana kuwa karatasi kwenye mapaja yangu, akiwa kama anavibandika kwa nguvu, mara nne, na macho yangu yalipofanikiwa kuona kilichokuwepo hapo, yakatanuka kiasi. Zilikuwa ni picha, na ni picha ambazo nilipoelewa zilimaanisha nini, nikajikuta nameza mate ndani ya koo langu kavu kwa hisia mpya ya msisimko iliyoniingia. Msisimko mbaya.

Picha ya kwanza ilionyesha kichwa cha mtu kilichokatwa, mwanaume, na huyo alikuwa ni Bobo! Picha ya pili ilionyesha mwanamke mmoja asiyekuwa na nguo mwilini, akiwa ameshikiliwa na wanaume watano walio uchi pia, na picha ya tatu ilionyesha wanaume hao wakiendelea kumshikilia mikono na miguu, mmoja akimwingilia kimwili kupitia kitoweo chake, mwingine nyuma yake, na mwingine mdomoni mwake, halafu ya nne ikaonyesha mwanamke huyo akiwa ametundikwa kwa kunyongwa huku mwili wake ukionekana kutapakaa damu, ndani kwake, na huyo alikuwa ni Adelina!

Nilihisi pigo zito sana moyoni. Nilishtuka! Macho yangu yakakaza hapo zaidi, nikiwa nimeganda tu kutazama picha iliyomwonyesha Adelina akiwa amenyongwa, na aisee! Nguvu zikaniishia. Sikuwa hata na muda wa kufikiria nini wala nini, yaani kile nilichokiona kilipita unyama wowote ambao nilidhani Bertha angenifanyia. Nilichoka mno. Eh Mungu wangu!

Nikasikia Bertha anasafisha pua yake, kisha akasema, "Niangalie."

Macho yangu hayakuwa na budi sasa kupanda na kumwangalia mwanamke huyu, na nilikutana na uso wake usiokuwa na aina yoyote ya hisia za majuto, wala hofu, wala huruma, bali ni kuridhika kabisa na kile alichotoka kunionyesha.

"Sasa je? Kama mtoto mzuri," akasema hivyo.

Niliingiwa na huzuni zaidi sasa, nikibaki kumtazama kwa mkazo huku midomo yangu ikitetema. Kulikuwa na watu kama wawili waliosimama nyuma yake.

"Umeonaje chakula nilichokuletea?" Bertha akauliza hivyo.

Nikaendelea kumtazama kwa hisia za maumivu.

"Oh, lazima umeona ni kitamu, maana mwanzoni ulikuwa hutaki kuniangalia, ila nilipokusogezea ndo' motivation ikakuingia hahahah..." akaongea hivyo kwa sifa na kucheka.

Wenzake wakacheka pia, na mimi nikiwa nimekabwa na huzuni, nikafumba macho na kufumbua, machozi yakianza kunijaa.

Bertha akaweka uso makini, naye akasema, "Najua unawaza 'kwa nini unafanya hivi Bertha?' 'Kwa nini umeamua kufanya hivi?' 'Why?' 'ohohooouu...' Ahahahah... ni kwa sababu yako, JC! COME ON!!"

Aliiongea kwa kejeli na mkazo mwingi, nami nikaendelea kumtazama kwa umakini.

Akanyanyua kidole na kuonekana kutaka kusema kitu fulani, lakini akaishia kushusha pumzi na kufumba macho yake, kisha ndiyo akasema, "Sitaongea sana. Najua una njaa, so nimekuja kukupa option mbili leo."

Alizungumza kwa njia yake makini wakati huu, na mimi hapo kusema kweli nilikuwa nimeshauelewa mchezo wake wote aliotaka kuufanya, hata ingawa sikuyajua makali yake. Akafanya kuelekeza kiganja chake kwa mmoja wa watu wake hapo, na ikiwa ni mwanaume, akampatia vitu vilivyoonekana kuwa picha zingine. Sikuweza kuzuia hisia zangu kupandisha hofu zaidi kwa kuwa najua angenionyesha vitu vibovu zaidi, na kweli ikawa hivyo, lakini kwa njia tofauti.

Bertha akanionyesha picha ya kwanza, nami nikaiangalia na kutambua mtu aliyekuwepo hapo kuwa mama yangu. Akaitupa na kunionyesha ya pili, nayo ilimbeba Jasmine. Ya tatu, ikawa ni Mariam, ya nne ikawa ni Tesha, ya tano ikawa ni Nuru, na ya mwisho, ikawa ni Evelyn. Zote zilikuwa picha safi, yaani, hakukuwa na mambo yoyote mabaya yaliyoonekana hapo kama kwenye picha za Bobo na Adelina, nami nikajikuta nadondosha machozi nikiwa naiangalia picha ya mwanangu iliyoendelea kushikiliwa vidoleni kwa mwanamke huyu mkatili.

Bertha akasema, "Two things. Moja, ufate KILA kitu nitakachokwambia ufanye kuanzia sasa, au mbili, kataa kufanya hivyo, na hawa wote uliowaona wanakenua hapa nitawageuza kuwa vyakula vya mbwa kama hao machangudoa wako wawili, na... sijui kama Bobo alikuwa ni swahiba wako kabisa, ila... you get it. Nitawaua wote."

Nikafumba macho na kuinamisha uso kwa kuhisi maumivu mengi moyoni. Nilichokuwa najitakia mwenyewe kutokea hapa killionekana kutonitaka mimi, yaani Bertha aliamua kuninyima hata haki ya kutaka kufa. Alitaka niendelee kuishi ili kila siku anifanye nihisi ni namna gani aliniweka kuwa mwanasesere wake chini ya kiganja chake.

"Kwa hiyo utachagua nini... handsome?" Bertha akauliza hivyo.

Nilihisi unyonge wa hali ya juu, na hisia za kustahili haya yote zilinilemea, lakini siyo kwa namna aliyoileta Bertha kwangu. Ilikuwa na ulazima gani kumuua mtu ambaye hakumkosea lolote, kumfanyia unyama mwanamke ambaye hata hakumjua ili tu anilipizie kisasi mimi, na kisha kumuua pia? Kwa nini isiwe mimi ndiye ambaye angenifanyia mambo hayo? Iliniuma sana.

Vifo vya watu hao niliowapenda na kuwajali vilikuwa ni makosa yangu, na sasa kama sikutaka vingine viongezeke kwa wengine, ingenibidi nikubali kufanya aliyotaka mnyama huyu ili kuwaokoa wasiokuwa na hatia. Najua hakutaka nikatize uhai wangu upesi ili aendelee kufurahia kuona nilivyoteseka, na kutokea hapa sikuwa na njia nyingine ya kukataa alichokitaka kutoka kwangu. Kama kuwa mtumwa kwa mateso, ningekuwa mtumwa wake tu. Hakukuwa na namna.

Alikuwa bado ameishikilia picha ya Evelyn, mimi nikiwa sijatoa jibu kwa swali lake, naye akasema, "Okay. Kama unahitaji muda zaidi wa kufikiria, nitakuacha ufikirie. Labda... hao wawili hawajatosha..."

Nikamwangalia machoni baada ya yeye kusema hivyo.

Akawa anaiangalia picha ya Evelyn kiufikirio, kisha akasema, "Niongeze mmoja, au wawili hivi ili nikupe motivation zaidi ya kutoa jibu. Nitaanza na huyu."

Aliongea hivyo huku akinionyeshea picha hiyo ya Evelyn, nami nikajipa nguvu kiasi na kujivuta, nikiuweka mwili wangu sawa ili nimtazame kwa namna makini zaidi. Alibaki akiniangalia kwa namna ya kutojali kabisa, mimi hapo machozi bado yakinitoka kama mtoto bila sauti ya kilio.

Nikafumbia mdomo, Bertha akionyesha subira ya kunisikia naongea, nami nikasema, "Unataka nini?"

Sauti yangu ilikuwa ya chini sana, na sasa nilikuwa nimejipa nguvu kidogo tu ya kumwonyesha kwamba nilichagua jambo la kwanza alilonipa nichague kati ya yale mawili. Sikupatwa na hisia yoyote zaidi ya maumivu kwa kila kitu nilichowazia kimetendeka na ambacho kingefanyika baada ya hapo lakini nilikuwa tayari kwa mengine yote isipokuwa watu niliowapenda kuumizwa kwa sababu yangu.

Bertha akatabasamu kiasi, kisha akaanza kucheka kwa namna iliyoonyesha furaha tele. Akaiangalia picha ya Evelyn tena na kusema, "Men are so weak. Uko tayari nikuue wewe, lakini paka wako akinyooshewa panga unanywea. That's so f***** gross."

Nikaangalia chini na kusema, "Niambie. Unataka nini? Nitafanya..."

Bertha akauliza, "Sure?"

Nikajitahidi kutikisa kichwa na kusema, "Ndiyo."

Akatulia kwanza akiniangalia kwa hisia makini, kisha akatikisa kichwa kukataa na kusema, "Naah. Haujanishawishi. Ahah... bado nahisi kama napaswa kukuongezea moti...."

Nikajivuta zaidi kujitoa sofani hapo, nikiwa na nia ya kutaka kupiga magoti ili nimwombe nikiwa chini yake, nami nikaangukia sakafuni nikiwa sijiwezi vizuri kutokana na uchovu na maumivu ya mwili. Nilianguka chini hapo na kuzilalia picha alizokuwa ametupa, mikono na miguu ikiwa imefungwa bado, na katika hali yangu mbovu nikaanza kujitahidi kuunyanyua mwili ili hayo magoti yapigwe. Najua ilimpa raha sana Bertha kuniona nilivyosumbuka hapo chini kujigeuza na kujigeuza hadi nilipoweza kupiga magoti kwa upande, nikiegamia mikono kwa chini na kumtazama kwa njia iliyoonyesha kweli nilitaka kumfanya ahisi ninamshawishi.

Hapa hakukuwa na nafasi ya kuweka ujeuri wa aina yoyote. Nilikuwa sitaki kumwacha aendelee kujipa kichwa zaidi maana tayari nilielewa alichokuwa akikitaka, kwa sababu nilimjua vizuri sana. Yote aliyokuwa amefanya, yalikuwa kuniumiza si kwa sababu tu ya niliyomtendea kipindi kile, ila kwa sababu alikuwa ananipenda. Upendo uliochochea chuki kubwa kunielekea. Kwa hiyo, ningefanya kila alichotaka kuhakikisha anawaacha kabisa wapendwa wangu. Na sijui kihalisi alitaka nini, ila JC nilikuwa tayari kumpa. Sikuwa na namna tena. Miryam alitoweka, Adelina dada wa watu alitendewa vibaya sana na kuuliwa pia, Bobo... yaani! Ilitosha.

Nikafungua kinywa changu tena na kusema, "Fanya lolote unalotak... hh.. hhh... juu yangu... mimi. Usiumize mtu m-mwingine... hh.. zaidi. Nakuomba... hhh... nitafanya yote unayotaka."

Bertha akabaki kunitazama kwa hisia makini, kisha akasema, "Natamani ingekuwa rahisi."

"Bertha..." nikaishia kutaja jina lake.

Akaangalia pembeni.

"Nachagua kufanya kila kitu... utakachotaka. Kila kitu. Nitafanya. Tafadhali... usiwaumize wengine... hhh... nakuomba..." nikaongea kwa hisia sana, machozi yakinitoka.

Bertha akarudi kuniangalia na kunikazia macho yake, akionyesha aina fulani hivi ya hasira kali, na kwa sauti ya chini akasema, "Tusingefikishana huku JC, kama tu ungekuwa halisi na mimi. Nilikuwa tayari kukupa kila kitu. Everything. Why? Kwa nini ulinifanyia vile? Huh?"

Nikaendelea kumtazama kwa hisia za huzuni.

Akatikisa kichwa kwa njia iliyoonyesha kukerwa sana, naye akasema, "Sawa. Unachagua kufata kila nitakachokwambia ufanye, si ndiyo?"

Nikatikisa kichwa kukubali.

Akasema, "Okay. Kuanzia sasa... wewe utakuwa mbwa wangu. Unanisikia? Nani?"

Nikaangalia chini na kusema, "Mbwa wako."

"Sikusikii..." akasisitiza.

Nikamwangalia machoni na kusema, "M-mbwa wako."

"Yeah. Wewe ukiwa mbwa wangu, utapaswa ufanye nini?" akaniuliza.

Nikasema, "Nitafanya kila kitu unachotaka."

"Ahahaha... 'nitafanya kilo kitu unachotakoh' huna hata aibu?" Bertha akaongea kwa kejeli.

Nikaangalia chini kwa kufadhaika.

"Well, kama utafanya kila kitu ninachotaka... anza kuthibitisha hilo. Sasa hivi," akaniambia hivyo.

Nikamtazama machoni tena, nikiwa naelewa angetaka nifanye jambo fulani lenye kumpendeza, lakini sikujua la kumfanyia. Ila yeye tayari alikuwa na wazo. Hapo hapo akamtikisia kichwa mmoja wa watu wake pembeni, na ndiyo kumwangalia mwanaume huyo nikaona alikuwa ameshika kitu kama hotpot ndogo mikononi mwake. Akasogea upande wangu na chombo hicho, kisha akakiweka chini karibu nami na kutoa kisu kidogo kutoka kwenye mkanda nyuma ya kiuno chake. Akaivuta mikono yangu na kuzikata kamba ngumu nilizofungwa, akiipa mikono uhuru sasa, kisha akasimama na kurudi nyuma yake Bertha. Nikamtazama mwanamke huyo usoni na kumwona amenikazia macho tu, na eti hilo ndiyo likawa jambo la kwanza alilotaka nifanye. Nile.

Hisia mbaya zaidi ziliniingia, kwa kuwa chombo hicho hakikufunuliwa, hivyo najua Bertha alitaka mimi mwenyewe nifunue ili nikutane na ishu fulani mbovu sana ambayo ingepima kama kweli nilimaanisha kile nilichomwambia. Kama hakikuwa chakula cha kawaida basi ni lazima niliwekewa uchafu wa aina fulani humo kabisa, lakini kwa jinsi mambo yalivyokuwa, nisingeacha kufanya alichotaka hata kama ingenigharimu vipi. Yote yangekuwa kwa yote. Huku mwanzo wa viganja kukiwa na maumivu ya kamba zilizoondolewa, nikanyoosha mkono kuushika mfuniko wa hotpot hiyo, kisha nikauondoa hapo na kubaki nimekitazama chakula kilichokuwepo humo. Wali, nyama, na hata ndizi mbivu.

Nikamwangalia Bertha usoni, naye ndiyo akasema, "Kula. Ama vipi? Unafikiri kuna sumu? Au ulidhani ni nyoka?"

Nikaendelea kumtazama tu.

"Ule. Umalize. Ndiyo tutaanza kuongea kuhusu nini nataka," akasema hivyo.

Hapo alionekana kuweka kituo kikubwa kabisa, na bila kungoja lolote, akasimama mbele yangu na kutumia sekunde chache akiniangalia kwa umakini. Nikashindwa kuacha kumtazama yeye alipoendelea kusimama tu namna hiyo, na ile ameangalia pembeni kwa namna iliyoonyesha kukosa subira, nikakivuta chombo karibu nami na kuanza kujilazimisha kula chakula alichokuwa amenipatia, viganja vikitetemeka haswa. Nilikula upesi, nikijaza mdomo na kutafuna huku narudisha macho yangu kumtazama yeye, kumwonyesha kwamba nilikuwa nimeanza kufanya aliyoyataka, naye Bertha akaniangalia kwa njia iliyoonyesha dharau sana na kisha kuanza kuondoka sehemu hiyo; akifuatwa na wanaume waliompa ulinzi.

Ni baada tu ya wote kutokomea ndiyo hisia zikanilemea zaidi, nami nikaanza kulia kwa kuhisi hatia nyingi moyoni. Picha ambazo Bertha alinionyesha zilikuwa hapo chini sasa, na nilipoangalia zile zilizoonyesha ukatili aliokuwa ameufanya, nikashindwa kuendelea kula na kubaki nalia kwa maumivu tu. Nikahisi mtetemo mwilini uliofanya nilegee zaidi na kujilaza chini hapo, nikiishika picha ya Adelina na kuikaza karibu sana na moyo wangu. Mwanaume mtu mzima lakini nililia haswa. Kwa nini maisha yangu yalikuja kuwa hivi? Mbona ni kama nilikuwa ndani ya sinema? Na haya yote yangekuja kuisha namna gani? Nilikata tamaa kabisa.

★★★★★★★★★★★

Daah sio poa 😢
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom