Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Moja ya story bora nlizowahi kusoma humu JF mwanzo mwisho..Hongera Kaka Daniel
 
mkuu uwa sijawah comment chochote lakini awamu hii kuna kitu umenigusa umenikumbusha kitu kilichonikuta kati yangu na shemeji yangu ambaye tulidumu kwa miaka 12, ambaye nilikuwa natoka na dada yake huku mahusiano yetu yakiwafanya ndugu hao kuwa chui na paka mpaka sasa. Ni story ndefu.
Mkuu tupe na hii yako inaonekana Ni tamu
 
Mkuu hakika historian yako inafundisha sana!
Vipi bado unaendaga kwa waganga?
 
SEHEMU INAYOFUATA....

Usiku wa siku hiyo, nilikuwa na mawazo kiasi,

Huyu Madam, anataka nini kwangu, ana watu maarufu wakubwa wakubwa anafahamiana nao, amekosa wasiri wake kuwaeleza juu ya shida yake.

Kwanini Mimi,
Anadhani Mimi mtoto wakiume nitamsaidia Nini.
Halafu kumbe namheshimu bure tu hata Elimu hana ya kutosha yaani ndumba na uchawi vilimbeba,

Ila huyu stori zake zinatisha, yaani kile mwanaume anaye mpata rafiki yake alimpora, na kumroga kabisa, dah mdada ana roho mbaya sana huyu, Tena Sasa hivi sipaswi kujenga naye mazoea kuonekana naye kwa jinsi alivyo anaweza kukuchoma na kukuachisha kazi.

Ila anaonekana kakitembeza sana, maana Kuna Mwajuma wa uwanja wa fisi huwa wanamsifu kuwa aliitendea haki kazi yake ya kujiuza kiasi Cha kupata kibanda Cha vyumba vinne, lakini huyu Madam kiboko, kutoka huko mkoani Hadi kuwateka mtu na baba yake mbaya zaidi bado akapata utajiri wa kutosha. Kweli uchawi upo, na kama anatoka kweli huo mkoa alionitajia, Sina pingamizi kuhusu uchawi,niliwaza sana.

Mke wangu,
Akaitika.

Hivi yule kijana mnaye sali naye ambaye ni fundi ujenzi ana jicho chongo hivi bado yupo? Niliuliza

Ndiyo yupo, huwa anapiga kinanda kanisani? Alijibu

Sawa nataka namba zake au kesho ukimuona mwambie aje hapa nyumbani, nataka aje anipe ramani fulani jinsi fence yangu itakavyokaa,

Heeee mume wangu hivi naye yule ni fundi, mbona kama ni kilema?

Hapana, ni bonge moja la architecture kama hujui, nikamtajia baadhi ya majengo aliyosimamia na yakawa poa,
Na hata lile jicho aliumia kazini hajazaliwa nalo vile. Niliongeza

Haya, naona safari hii hutaki masihara baba, aliongea huku alitoa kicheko flani Cha sanifu.

Mke wangu , hata Kama huku ni uswahilini lakini, lazima nyumba yangu iheshimike hebu fikiria kesho unasema Kuna wageni watakuja naamini tutalazimika kukaa hapo nje kwenye mti huku wapita njia wakiona kila kinachoendelea. Yaani siyo sawa.

Ila nikweli, alijibu.

Halafu mke wangu, hivi umeniambia na ESTA anakuja hapa,?

Ndiyo atakuja, kwanini umeuliza hivyo mume wangu.

Ni kwasababu yeye ana sali kwenye makanisa mengine, kumbuka wanaokuja hapa ni sehemu ya jumuiya yetu.

Nilimjibu hivyo kwa kumpoteza ila nilitaka kuhakikisha ujio wake kwakuwa nilitamani kujua historia fulani ya maisha yake.

Ujue Nini mume wangu, yule ESTA anapenda sana kuwa karibu na Mimi na pia namfariji kwa namna moja au nyingine, unakumbuka siku ambayo ulitoka mkoani Kisha nikakwambia nitampeleka sehemu?

Ndiyo nakumbuka,
Nilimjibu

Basi kibao kilibadilika, baada ya Mimi kumpeleka, akanipeleka Mimi, kama unavyojua nilikuwa nimeishiwa nguvu kwahiyo akataka kunisaidia, Cha kushangaza baada ya kugundua kuwa ofisini kwako ni pale , nilimuona akinyongea sana yule shoga yangu,

Hata baada ya kutoka eneo lile bado hakuwa na amani kama mwanzo alivyokuwa akinifariji kuwa wewe utatoka tu, badala yake akawa yeye ndiyo mwenye mawazo zaidi, huku akiwa anaongea peke yake, siku zingatia mambo yake kwa kuwa nilikuwa nakuwaza wewe. Aliweka kituo

Nilimwelewa sana mke wangu Tena sana kwakuwa tayari nilijua kitu,.

Halafu mume wangu nasikia kumbe ESTA alikuwa malaya balaa, na kachezea maisha sana.

Wewe umemsikia nani? Niliuliza

Dunia Ina Siri baba, eheeeeh kila kitu kipo wazi mbona, wamechezea maisha huko halafu wanakuja kuishi maisha mabaya kiasi hiki, yaani ana maisha magumu yule dada wewe acha , Tena mzuri masikini, kweli uzuri siyo ndiyo kila kitu, Tena pale alipo Hana hata mtoto, sijui atapata lini maskini, wameharibu mimba weeeee Sasa hivi wanahaha,
Aliongea kwa kulaumu

Dunia Ina mapito mengi mke wangu huwezi jua, niliongea kwa utulivu huku huruma ikiniingia kulingana na nikichosikia mchana wa siku ile .
Sikutaka kumsimulia mke wangu, maana nawajua wanawake zetu hawa.

Lakini nikafikiria kama ESTA atakuja nitatumia nafasi hiyo kuongea naye mambo fulani ili nipate kuwianisha vitu, japo sikutaka kumwambia Yale aliyonituma Madam,

Kwanza ningeanzaje, mwanaume nakuwaje hivyo, niliwaza kumsaidia ESTA

Mume wangu ni saa sita hii tayari jumapili ishaingia tulale bwana tupunguze usingizi naona unawaza, unamuwaza huyo ESTA au,

Weweeee Mimi Nina mawazo yangu mke wangu kama tumeishiwa stori tulale, nilimjibu.

Asubuhi ilifika maandalizi ya kanisani yalipamba moto, Mama mzazi akanifuata,

Dani mwanangu Leo unaenda kanisani, kumbuka tangu nifike hapa sijawahi kuona ukijishughulisha na mambo ya kanisani vipi, na kesho kutwa jumanne nasafiri sitaki niondoke bila kuona ukienda kanisani, Sasa Leo lazima utaenda.

Nikaona ishakuwa kesi hii nikajiandaa nikaenda na Mimi ,
Huku nikijifichaficha baada ya Misa kuisha nikawa wa kwanza kutoka na kurudi nyumbani huku nikiwaza sana

MUNGU atusamehe sana , hivi Leo kifuani Nina chale,Tena mbichi kabisa Leo nimeenda kanisani, Yesu mwenye alikataa mtu kuwa wa vuguvugu , leo hii sijulikani wamoto au wa baridi, MUNGU nahitaji huruma yako, nafika nyumbani nilimkuta ESTA kajaa tele anatusubiri,

Shemu huyoooo, alinikaribisha ESTA
Najua kama nimewahi sana ila kwakuwa Sina simu nikaona ni vyema kuwahi, aliongea.

Ina maana huna simu ya mkononi . Niliuliza kwa mshangao.

Ndiyo Nini Cha ajabu nimeamua kuiuza kwakuwa maisha ni magumu Tena na maisha magumu we Daniel acha tu, sijui kwanini MUNGU hanichukui nikapumzike Mimi.
Aliongea kwa uchungu sana.

Hayo siyo maneno Dada yangu,kikubwa ni kuendelea kumuomba MUNGU mbona kila kitu kitakuwa sawa tu,nilimfariji.

Hapana Dani siyo kwangu,Sina makazi maalum Sina familia,kama nyie wenzangu ama kweli ujanja mwingi mbele kiza,naishije mjini Daniel, aliongeza.

Dah,kwani kwa Sasa una kazi gani ya kujiongezea kipato? Nikiuliza

Niwe na kazi gani mwenzangu,Mimi naishi kama omba omba tu.

Nikaingia ndani nikawaza sana
Yule madam anaonekana anajuta kwa kile alichomfanyia mwenzake miaka hiyo na yupo tayari kumsaidia kama kumlipa kwa mabaya aliyomfanyia.

Mmmmh hili ni balaa,na Mimi sitaki kujiingiza kwenye huu upumbavu,kwanini asitafute wanawake wenzie wawaunganishe ,halafu hivi anashindwa kabisa kumsaka huyu akamface mwenyewe,

Natamanj nimwambie kuwa Kuna mtu Ana shida na wewe lakini siwezi,au nimuunganishe yule madam na mke wangu ili ujumbe umfikie ESTA?
Haaaa siwezi kwanza nitamtesa mke wangu na tumbo lake siwezi.

Japo kuwa lazima nitakaa na ESTA ili anipe background ya maisha yake ili lazima nitakaa naye.

Nikachukua kiasi fulani Cha pesa nikampatia huku nikimuahidi kumsaidia na pia nikisisitiza ananunue simu,

Alifurahi na kunishukuru sana.

ESTA mwanamke wa mjini kipindi hicho niliwahigi kumfuatilia sana lakini alinifungia vioo,sikuwa saizi yake

Lakini siku si nyingi nilimtongoza huyu, Kabla hatujakutana tayari nikapata taarifa juu ya shida yake.

Ni mzuri,mrefu kaenda hewani mweupe umbo ni kama madamu yaani wanafanana vitu vingi tofauti yao ni kwamba Madam ana weusi kidogo,wanaita chocolate colour.

Ila madam ana ngozi ya hela, huyu ESTA ukute anaogea mpaka sabuni ya magadi,wakati nafikiria haya nilisikia sauti za watu wengi wakija nyumbani kwangu.

Huku wakiwa wameongoza na mke wangu,

Mke wangu naye yaani kawatoa watu kanisani anawaleta huku wamekula kweli Hawa,haya si mambo ya kuharibu bajeti haya.niliwaza

Mume wangu wakati ibada fupi ikiendelea hapa itabidi ,itabidi tuandae Chakula kwaajili ya ugeni,

Haaaa uandae saizi kwanini usingewahi? niliuliza

Sikujua kuwa tukitoka tu kanisani watakuja moja kwa moja na huu siyo muda wa kubishana, najua ulitoa hela ya vinywaji,ila Leo bajeti zimeongezeka, aliongeza

sikuwa na jinsi ikabidi nifanye nilichoambiwa si wanasema wageni ni BARAKA,

Halafu njoo huku nje haiwezekani watu wanakuja wewe upo ndani tabia yako sijapenda mtu naangaza macho kule kanisani kumbe wewe umetangulia huku

Itaendelea............
Stori nzuri
 
Letaga story ingine basi,vipi esta hamuonani Tena siku hizi na madamu je yupo ,,ila sijui Kwa nini hukumla esta hapo uliniudhi sana
 
SEHEMU INAYOFUATA.........

Nilirudi nyumbani kuungana na familia huku nikitambua hakuna amani ya moja kwa moja,

Ile furaha ya kupokea kiumbe kipya ilitoweka watu walikuwa kimya sana nilisalimia huku mtu pekee aliyekuwa na furaha japo ya kulazimisha ni ESTA, ambaye tayari nilimchukia kwa kiasi fulani.

Daniel mwanangu kabla ya kufanya chochote Nina mazungumzo na wewe,

ni maneno toka kwa mama yangu mzazi

Kwanza mwanangu pole kwa misukosuko na mengi yanayokukabili, watu wote hapa tumeungana kwenye hii familia si kwa kuja kula Raha Bali ni visa na mikasa vimetuunganisha.

Kila mmoja anatambua Nini kimetutoa mkoani kuja hapa, labda nikukumbushe tu kuwa kwenye maisha Kuna mikosi, na mwanangu mikosi ilikutembelea, ukawekwa mahabusu, naamini ulihitaji dhamana kutoka kwa watu wenye uchungu na wewe , hebu kumbuka una marafiki na maswahiba wangapi hapa mjini,hawakukusaidia

Na je, unawezaje kutofautisha nyakati mwanangu au unaishi tu, mwanangu hii ni Dunia,

Nimekuja kutoka mkoani Mimi na dada yako siyo kwamba tulikuwa na uwezo wa kukutoa mahabusu sisi kwenye hii Dunia ya kisasa iliyojaa rushwa , hapana,.ni upendo tu

Unadhani Mimi au dada yako hata mkeo nani angeweza kukunasua kwenye ule mtego wa matajiri wenye pesa wanaoweza kukufanya chochote kile,

Sisi kazi yetu ilikuwa ni moja tu kukuonesha UPENDO tu, mwanangu unatambua kuwa sisi wazazi wako ni maskini si matajiri, tunakutegemea kwenye mambo mengi, unadhani tungekusaidia Nini kwenye kesi yako.

Naomba utambue nafasi aliyocheza mke wako kipindi una matatizo ni sehemu pekee ya kutambua thamani yake kwako, sisemi kuwa hakukosei, najua anakukwaza kwa mambo mengi lakini Mimi kama mama yenu na mama yako mzazi nakuombea na kukukumbusha kuwa makini.usipende kuweka msimamo Kila sehemu mengine yapuuze

Nachoweza kushukuru ni kwamba mkeo kajifungua salama na maendeleo yake yanaridhisha sana tu kwahiyo hatuna Cha kutuweka hapa kwako ni kwamba tuna masaa machache ya kurudi nyumbani mkoani maana ulituomba tukae kwaajili ya mgonjwa hatimaye MUNGU kajalia na kutia wepesi.

Lakini mwanangu nikuulize swali moja ulikuwa na maana gani kumkoromea mkeo?

Mtu ambaye anahitaji UPENDO wa dhati toka kwa mumewe hasa kipindi kama hiki alichojifungua,? Alimalizia Mama kwa mfumo wa swali.

Nikamjibu,

Kiukweli Mama wewe mwenyewe kwa siku ulizokaa hapa , umegundua ni jinsi gani huyu ESTA anavyokuwa karibu na mke wangu, Sasa iweje ujio wake uwe msala kwangu Mimi, kifupi mke wangu kanikera sana.nilimalizia

Sawa mwanangu, naomba utambue kuwa humu ñdani watu wote ni wanawake, hebu jitofautishe basi Dani, hebu jaribu kudharau baadhi ya vitu visivyokuwa na umuhimu , ni aibu kubwa Mimi nianze kuwasuluhisha nyinyi katika kipindi ambacho mkeo katoka kuponea kwenye tundu la sindano,

Yaani ilikuwa ni wakati wa wewe na mkeo kukaa na kuanza kupendekeza jina la mtoto ataitwa nani na siyo kutengeneza malumbano.
Aliweka kituo.

Nilimwelewa sana mama nikaingia chumba fulani ambacho huwa hakitumiki nikamkuta mke wangu akiwa na furaha tu anachezacheza na mtoto tofauti na nilivyofikiri baada yakuona watu wengine kule nje wamenuna nuna yeye alikuwa poa kabisa tulisalimiana nikampa pole huku tukitaniana baadhi ya vitu.

Oooh hiki kipindi kigumu, Mara ooh umeshikaje ujauzito Mimi Sina kazi, Sasa nimemleta huyo hapo mkatae Sasa, alitania mke wangu.

Weee nimkatae, kwanza hii jinsia nilikuwa naisubiri kwa hamu, yaani nataka siku moja kama nitakuwa hai niende pale airport nimuone akishuka kwenye ile midege ya Emirates huku akiwa nadhifu na Yale mavazi yao,
Halafu kwa makusudi nimwambie mbona simu yako haikuwa hewani,nilitania

Wewe mwanangu sitaki awe rubani , huyu atakuwa daktari bingwa nikwambie, alisema mke wangu Huku tukitaniana mambo mengi, ambapo nilifurahi sana,

Maana timbwili nililokuwa nimepanga kufanya nilijikuta nasutwa tu moyoni mwangu ila nikashukuru kama mambo yamekuwa sawa , najua atakuwa kamshitakia mama,
Na bimkubwa navyomjua atakuwa kaniponda weee ili ampe ushindi huyu , bimkubwa hajawahi niangusha kwenye kumbembeleza mtu

Baada ya kupata ile amani ya moyo sikutaka kuzungumzia habari za ESTA muda huo ili kuepusha Shari.

Nilitoka nje kucheki mazingira nikamuona ESTA akiwa anajituma anafua nguo za mke wangu akisaidiana na dada yangu, nilimuhurumia sana , Kuna wakati baada ya kukwazana na mke wangu kwenye simu nilimuona huyu ndiyo chanzo , nikapanga nije nimtimue lakini maisha acha yaitwe maisha

Kama tu Mimi mwanaume nilipigika Hadi nikawa nauza vitu vyangu kipindi fulani itakuwa kwa huyu mwanamke?

Kumbe atafanyaje, ajiuze, Bora kaja kuomba msaada sishindwi kuishi naye tatizo lipo kwa mke wangu lakini pia si madam karidhia tumfungulie biashara?

Kwanza ngoja, Kila kitu kitakaa sawa.

Kaka vipi mbona unaizunguka nyumba kama unaizindika vipi, alitania dada yangu,

Hapana nilikuwa huko nyuma naangalia mahali pa kumwaga tofali nahitaji kuijenga fence.

Ahaaa safi my brother, tunakuombea kwa MUNGU Kila kitu kiwe poa,naona nyumba itapendeza sana
Alijibu
Wakati tunaongea hayo nilipokea simu namba ngeni,nikaiweka sikioni

Habari kaka,za siku nyingi Mimi ni Shedy,

Kwanza nilibadilika, maana sikupenda mazoea Tena na huyu mshikaji,

Unasemaje, niliuliza

Aisee kaka jaribu kusahau yaliyopita Mimi na wewe ni ndugu kabisa unajua tulipotoka, nina mazungumzo na wewe kaka, aliongea kwa tahadhari.

Ongea nakusikiliza,

Sawa ni hivi ,mwenzio baada ya kukuta biashara inayumba na zile shughuli zangu zimekuwa ngumu nilikopa hela kwenye benki ya(akiitaja hii benki maarufu nchini)

Ni kutokana na shughuli zetu kuwa ngumu yaani udalali kwangu umenikataa kabisa, nikaona nikope hela ili niiboost biashara yangu, lakini mambo yamekuwa tofauti sana
Kwanza Kuna mtu hapa kafungua bar ya kisasa ni Mara tatu ya hii yangu kama ujuavyo kipya kinyemi yaani mwezi wa tatu Sasa wateja wangu maarufu anao yeye.

Hebu fikiria Kuna muda nauza kreti moja tu la bia huku vile vikali huuzi kabisa na wahudumu niliokuwa nao wanaihitaji pesa yao kama kawaida yaani ni hasara juu ya hasara , huku wafanyakazi Mara biashara haiendi jumlisha riba, nitatoka kweli kaka.
Aliongea kwa uchungu wa kujipendekeza.

Sasa hayo ni maisha yako, Mimi nahusika vipi, nilijibu

Hapana kaka, Mimi shida yangu ni moja nataka unisaidie, ni kwamba Kuna mwanamke anaitwa ESTA naamini unamfahamu vyema sana yule Mimi namtafuta sana, ni kwamba yule Kuna kipindi alikuwa mpenzi wangu wa Siri, Sasa wakati wa mapenzi yetu alikuwa na kiasi fulani Cha hela , nikamzuga kwamba aniazime niingize kwenye biashara yangu alikubali, baadaye niwe mkweli baada ya kuwa nishamchoka sihitaji kuendelea naye,

Nilimwambia aangalie ustaarabu mwingine , ndipo alipoamua nimpe hela yake kwanza ndipo tuachane lakini nilimtishia kuwa Hana hela kwangu na nitamshitaki, hakuwa na la kufanya ukizingatia pesa zaidi ya milioni tatu tulipeana bila ushahidi wowote,
Aliweka kituo.

Sikia Shedy unanidharau sana kwamba nikutafutue ESTA hapohapo unanipa mkasa wako wa kimalaya,kumbe ndio tabia yako kutembea na wanawake na kuwadhulumu,kwa mfano ukimpata unataka umfanye Nini,niliuliza safari hii ni kwa ukali,

Ni hivi kaka lengo nimuombe msamaha na naahidi kuwa nitamlipa mbele ya ushahidi kwasababu, kila nikizunguka kwa wataalamu Wananiambia Kuna mtu Ana masikitiko juu yangu,ndiyo maana biashara yangu inayumba.alimalizia

Cha kukwambia ni kuwa Sina mahali ambapo nitampata huyu ESTA kwahiyo wewe fanya mambo yako Mimi Hilo lipo nje ya uwezo wangu,nikakata simu.

Mapya haya kwangu,yaani Shedy mjinga sana,na habari zake za kishirikina,

Eti ananiambia kuwa biashara haiendi kwasababu ya masikitiko ya mtu,wakati anajua wazi Kuna biashara mpya kama yake Tena imekuja kisasa halafu bado unatafuta mchawi,

Ni sawa na bus jipya na la zamani route ile ile na nauli ni moja nani atachagua la zamani,?

Kweli nimeamini ushirikina ukizidi na akili inapungua ,

Lakini huyu ESTA naye kumbe mjinga eeh kweli alirogwa akarogeka na kukorogeka , unawezaje kutoa zaidi ya milioni tatu kumpa mwanaume Tena Ukiwa ni maskini,akijifanya Ana mapenzi ya kizungu huu si ulofa huu

Ndiyo maana Kila nikimuuliza baada ya kuuza kibanda chako mkoani kwenu hela ulifanyia Nini haeleweki huyu , niliwaza sana jinsi binadamu tulivyo tofautiana .

Nikarudi ndani huku nikisearch kampuni fulani ya uuzaji wa magari used wakidai bidhaa zao ni Bora sana licha ya kuwa zimetumika nikawa napoteza muda pale,

Mke wangu akavunja ukimya,
Samahani sana mume wangu, kwa Yale tuliyoongea mchana ila tufanye yamepita,

Hivi mume wangu ukimwangalia ESTA kwa ukaribu unadhani ana akili timamu?

Kwanini umeuliza hivyo, mke wangu,ni kwasababu kaja kukaa hapa?

Hapana,
Nahisi Kuna jambo linamsumbua tujaribu kusaidia.

Mke wangu aligundua Nini kwa ESTA?

Nani kampa huo ufahamu kiasi Cha yeye kuwa Mpole na mwenye huruma ?

Itaendelea.....................
Hatar faya
 
SEHEMU INAYOFUATA..............

Nilifikiria sana kauli ya mke wangu, kwanini ahisi ESTA ana mapungufu fulani, lakini nilikuwa na majibu kuwa sababu inayomfanya aonekane hivi ni kwasababu kapigika

Ukiwa na maisha fulani ya mazuri yaani hela ya kubadilisha mboga haikosekani, unaweza kuapa kutofanya kazi zozote za kijinga, yaani unakuwa mithili ya mhitimu wa chuo ambaye kulingana na alichosomea huwa wanajipangia hata mishahara,

Yaani anachagua kazi na kutaka kulipwa anachotaka anasahau kuwa mitaa haihitaji Elimu ya kwenye makaratasi Bali watu, wanapeana connection na marefa ambao bila kuwa na takrima fulani basi utatembea na bahasha miaka yote huku ukijenga urafiki na kazi ambazo ulikuwa ukizikataa mwanzo.

Hivyo kwa upande wa ESTA ni msongo wa mawazo tu unamsumbua huyu akipewa mtaji afanye biashara mbona atatulia huyu?

Lakini Kuna jambo inabidi asaidiwe huyu, ngoja nitamshirikisha mke wangu, nikainuka kuelekea alipo bimkubwa kwakuwa alikuwa akiniita .

Daniel mwanangu kama nilivyokuambia, mkeo kajifungua bila matatizo yoyote, hivyo ni wakati mzuri wa sisi kurejea nyumbani, alisisitiza Mama.

Haaaaa mamaaaa mbona bado?
Mimi nakutegemeeni nyinyi kwa Kila kitu huyu bado hajawa sawa pili huyu dada wa kazi naamini hawezi kummudu mzazi akiwa peke yake,

Naomba ukae kidogo mama, niliongea kwa kumaanisha maana niliona sitakuwa free kabisa nikiwa kazini,

Hapana mwanangu, tumekaa sana pili Mimi najua mkeo Hana tatizo lolote Kuna mambo ambayo sisi huwa tunaangalia yanayotupa tumaini kwa mgonjwa, Mimi niliwahi fanya kazi ya unesi japo Mimi ni darasa la Saba umesahau miaka ile ?

Hivyo nazifahamu hizi kazi sana tu,
Lakini mwanangu huu ni msimu wa kuandaa Mashamba hata baba yako ameshaanza kulaumu, hivyo niache niende nitamwacha dada yako kwa muda mpaka atapotengamaa mkeo japo hapaswi kuchelewa, aliweka kituo.

Sawa mama Mimi nimekuelewa vizuri sana mama.

Nilimaliza mambo yangu huku nikiwa na furaha fulani siku hiyo hasa nikimwangalia ESTA,nikikumbuka ule mchongo wa madam nikaona safi kabisa lazima nipige hela

Kesho asubuhi nilitoa maagizo fulani kwa mke wangu kuwa kwakuwa mama anahitaji kuondoka ningeomba basi baade mida ya saa tisa tuonane mjini .

Nikakubaliana na mke wangu kuwa ESTA kwakuwa ni mzoefu wa mjini atampeleka mama yangu duka lenye nguo za kike hasa watu wazima halafu Mimi nitawafuata baada ya kutoka kazini,

Nilipiga kazi ofisini mida ya saa nane mchana nikapokea simu ya mama kuwa wapo na ESTA kwenye duka fulani maarufu mjini,

Nikafunga vitu vyangu licha ya kuwa ule muda halisi wa kufunga ilikuwa bado nikamuaga meneja kuwa Nina dharula jambo ambalo hakukuwa na tabu,

Nilifika dukani pale , nikatulia zangu nje ya lile duka huku nikimwambia mama Kila kitu kizuri akikiona achague, kweli ikawa hivyo nikaletewa hesabu nikalipa,
Ni mama yangu mzazi ni lazima nimfanyie Kila chema na chenye kumpa faraja.

Wakati nikiwa pale nje hata sijaondoka lilikuja gari fulani la bei ghali sana , nalikumbuka si geni machoni mwangu , akashuka Madam ambaye alikuwa ni Boss wangu wa mwanzo lakini bado alikuwa ni Boss wangu kwakuwa nafanya kazi kwenye ofisi zao.

Tulisalimiana Kisha akazama dukani , kule ambako ESTA na mama mzazi bado wapo wakiwa wanachagua nguo fulani ya ESTA maana mama alinishauri kuwa hatupaswi kumtenga ni mtu kafanya kazi kubwa sana hivyo lazima naye apate zawadi na si yeye tu watu wote wapate yaani familia nzima hasa ukizingatia nyumbani kwangu karibu wote ni wanawake

Nilihisi bajeti itaongezeka lakini acha akina mama waitwe mama, Kila mtu alipata nguo kwa ushauri wa mama huku bajeti ikiwa hata haikufika niliyokuwa nimejiwekea.

Muda kama dakika kumi alitoka Madam akiwa amefurahi sana,

Jamani tolu kumbe huyu ndiye MAMA yetu jamani, nimefurahi sana kumuona MUNGU amlinde jamani,
Aliongea kwa hisia sana ,

Huku kimoyomoyo nikisema siulisema wasikanyage ofisini kwako kipindi nipo mahabusu licha ya kufika hukutaka kuonana nao,

Waliongea wakicheka na kufurahi sana huku nikiwa pembeni natabasamu nikiwaza unafiki wa wanawake hususani kule kukumbatiana Kati ya madam na ESTA.

Eeenhee naona mmekuja kufanya shopping ya nguvu tolu? Aliuliza madam

Ndiyo, ni bimkubwa anasafiri kuelekea mkoani nikaamua nimlete angalau aangalie vitambaa hapa, nilijibu

Sawa Sasa mwambie mama achague nguo anazotaka, wakaingia dukani kwa Mara ya pili huku ESTA akibaki ,akiwa kama hajapendezwa na ujio wa madam pale, just imagine mtu ambaye alikukosea,halafu ana maisha ambayo pengine yangekuwa ni yako, but kila binadamu ana riziki yake pengine isingekuwa hivyo.

Huku mama alitoka na begi jipya kabisa ambalo kanunuliwa na madam mule ndani huku zile pockets za pale dukani zikiwa kama hazina kazi.

Baada ya sisi tumshukuru yeye madam

Akawa anatushukuru sisi akidai ni kama MUNGU tu kamleta pale, tuliagana nikatafuta usafiri binafsi tukaondoka huku nikitambua mama hajafurahishwa na mambo aliyofanyiwa na madam.

Hivi Dani huyu ndiyo boss wako ambaye alikusumbua mwanangu, yaani nimeshindwa hata kukataa hivi vitu lakini ningefanyaje, pia kanipa hii hela mule ndani dukani ni hii shilling laki moja, nimepokea tu maana huyu Binti namuona kama ana wadhifa mkubwa sana, alimalizia Mama.

Mama yanguuu, Mimi natambua Kila kitu ni jinsi gani mmeumia kitendo walichonifanyia Hawa lakini tambueni kuwa nipo kwenye kampuni zao bado, hivi kama Kila kampuni ambayo itatokea migogoro nikaapa kutokufanya kazi nitazisusia kampuni ngapi?

Kikubwa mama mniombee tu , kazi hazipatikani kirahisi lakini pia, matatizo hutokea na lazima nikabiliane nayo,

Wewe hizo zawadi ulizopewa kuwa nazo na amani yaliyotokea tusahau,

Hebu fikiria mke wangu kajifungua na familia ni kubwa ningekuwa Sina kazi ingekuwaje?

Mama alikubaliana na Mimi kwa shingo upande.

Tena Mimi kanipa namba zake za simu eti nimtafute muda wowote, sitaki mazoea naye na hii namba naifuta, alizungumza ESTA tukiwa tunakaribia kushuka.

Kitendo Cha kuonekana wamepeana na namba kilinishtua sana,

Je, ESTA anafuta namba za madam ni kweli, kama ni hivyo sawa, na je kama madam naye anazo za huyu wakaongea wakabembelezana itakuwa sawa lakini mbona kama mpango wangu utavurugika?

Wakisameheana Hawa nitapata hela kweli si watapeana wenyewe, kwanza najuta hata sana kuwakutanisha,

Itakuwaje sehemu ijayo Ina majibu usikose.

Itaendelea.................
Ntqsoma tena kesho in alaaah
 
Asante sana kwa kushare hii stori tumejifunza vingi binafsi nimuombee ESTER najua kuna siku mtakutana tena.
 
MIMI NA BOSS WANGU
moja ya simulizi nzuri sana na yenye kuelimisha...

Much Respect Tolu 🙌🙌🙌
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom