three phase
JF-Expert Member
- Mar 31, 2021
- 343
- 507
Duhh kama nishapata picha hivi

Mbona Tena watu mnampangia jamani Kama unammiliki. Mbona alitoa tambihi.iweke asubuhi masta
tulia wewe ona sasa amekuaibisha kwa kunisikiliza mm. hya sasa soma ufurahiMbona Tena watu mnampangia jamani Kama unammiliki. Mbona alitoa tambihi.
Yaani Kama anaenda job saa 11 asubuhi ahairishe ili akuwekee.
Akam anat00mbana ahairishe akupe wewe haja zake.
Kama vipi mlipe laki Sasa ili akuandikie.
Wewe tulia hata Kama akiweka mwaka kesho kwani utakufa
Shusha vitu broSEHEMU INAYOFUATA....
Usiku wa siku hiyo, nilikuwa na mawazo kiasi,
Huyu Madam, anataka nini kwangu, ana watu maarufu wakubwa wakubwa anafahamiana nao, amekosa wasiri wake kuwaeleza juu ya shida yake.
Kwanini Mimi,
Anadhani Mimi mtoto wakiume nitamsaidia Nini.
Halafu kumbe namheshimu bure tu hata Elimu hana ya kutosha yaani ndumba na uchawi vilimbeba,
Ila huyu stori zake zinatisha, yaani kile mwanaume anaye mpata rafiki yake alimpora, na kumroga kabisa, dah mdada ana roho mbaya sana huyu, Tena Sasa hivi sipaswi kujenga naye mazoea kuonekana naye kwa jinsi alivyo anaweza kukuchoma na kukuachisha kazi.
Ila anaonekana kakitembeza sana, maana Kuna Mwajuma wa uwanja wa fisi huwa wanamsifu kuwa aliitendea haki kazi yake ya kujiuza kiasi Cha kupata kibanda Cha vyumba vinne, lakini huyu Madam kiboko, kutoka huko mkoani Hadi kuwateka mtu na baba yake mbaya zaidi bado akapata utajiri wa kutosha. Kweli uchawi upo, na kama anatoka kweli huo mkoa alionitajia, Sina pingamizi kuhusu uchawi,niliwaza sana.
Mke wangu,
Akaitika.
Hivi yule kijana mnaye sali naye ambaye ni fundi ujenzi ana jicho chongo hivi bado yupo? Niliuliza
Ndiyo yupo, huwa anapiga kinanda kanisani? Alijibu
Sawa nataka namba zake au kesho ukimuona mwambie aje hapa nyumbani, nataka aje anipe ramani fulani jinsi fence yangu itakavyokaa,
Heeee mume wangu hivi naye yule ni fundi, mbona kama ni kilema?
Hapana, ni bonge moja la architecture kama hujui, nikamtajia baadhi ya majengo aliyosimamia na yakawa poa,
Na hata lile jicho aliumia kazini hajazaliwa nalo vile. Niliongeza
Haya, naona safari hii hutaki masihara baba, aliongea huku alitoa kicheko flani Cha sanifu.
Mke wangu , hata Kama huku ni uswahilini lakini, lazima nyumba yangu iheshimike hebu fikiria kesho unasema Kuna wageni watakuja naamini tutalazimika kukaa hapo nje kwenye mti huku wapita njia wakiona kila kinachoendelea. Yaani siyo sawa.
Ila nikweli, alijibu.
Halafu mke wangu, hivi umeniambia na ESTA anakuja hapa,?
Ndiyo atakuja, kwanini umeuliza hivyo mume wangu.
Ni kwasababu yeye ana sali kwenye makanisa mengine, kumbuka wanaokuja hapa ni sehemu ya jumuiya yetu.
Nilimjibu hivyo kwa kumpoteza ila nilitaka kuhakikisha ujio wake kwakuwa nilitamani kujua historia fulani ya maisha yake.
Ujue Nini mume wangu, yule ESTA anapenda sana kuwa karibu na Mimi na pia namfariji kwa namna moja au nyingine, unakumbuka siku ambayo ulitoka mkoani Kisha nikakwambia nitampeleka sehemu?
Ndiyo nakumbuka,
Nilimjibu
Basi kibao kilibadilika, baada ya Mimi kumpeleka, akanipeleka Mimi, kama unavyojua nilikuwa nimeishiwa nguvu kwahiyo akataka kunisaidia, Cha kushangaza baada ya kugundua kuwa ofisini kwako ni pale , nilimuona akinyongea sana yule shoga yangu,
Hata baada ya kutoka eneo lile bado hakuwa na amani kama mwanzo alivyokuwa akinifariji kuwa wewe utatoka tu, badala yake akawa yeye ndiyo mwenye mawazo zaidi, huku akiwa anaongea peke yake, siku zingatia mambo yake kwa kuwa nilikuwa nakuwaza wewe. Aliweka kituo
Nilimwelewa sana mke wangu Tena sana kwakuwa tayari nilijua kitu,.
Halafu mume wangu nasikia kumbe ESTA alikuwa malaya balaa, na kachezea maisha sana.
Wewe umemsikia nani? Niliuliza
Dunia Ina Siri baba, eheeeeh kila kitu kipo wazi mbona, wamechezea maisha huko halafu wanakuja kuishi maisha mabaya kiasi hiki, yaani ana maisha magumu yule dada wewe acha , Tena mzuri masikini, kweli uzuri siyo ndiyo kila kitu, Tena pale alipo Hana hata mtoto, sijui atapata lini maskini, wameharibu mimba weeeee Sasa hivi wanahaha,
Aliongea kwa kulaumu
Dunia Ina mapito mengi mke wangu huwezi jua, niliongea kwa utulivu huku huruma ikiniingia kulingana na nikichosikia mchana wa siku ile .
Sikutaka kumsimulia mke wangu, maana nawajua wanawake zetu hawa.
Lakini nikafikiria kama ESTA atakuja nitatumia nafasi hiyo kuongea naye mambo fulani ili nipate kuwianisha vitu, japo sikutaka kumwambia Yale aliyonituma Madam,
Kwanza ningeanzaje, mwanaume nakuwaje hivyo, niliwaza kumsaidia ESTA
Mume wangu ni saa sita hii tayari jumapili ishaingia tulale bwana tupunguze usingizi naona unawaza, unamuwaza huyo ESTA au,
Weweeee Mimi Nina mawazo yangu mke wangu kama tumeishiwa stori tulale, nilimjibu.
Asubuhi ilifika maandalizi ya kanisani yalipamba moto, Mama mzazi akanifuata,
Dani mwanangu Leo unaenda kanisani, kumbuka tangu nifike hapa sijawahi kuona ukijishughulisha na mambo ya kanisani vipi, na kesho kutwa jumanne nasafiri sitaki niondoke bila kuona ukienda kanisani, Sasa Leo lazima utaenda.
Nikaona ishakuwa kesi hii nikajiandaa nikaenda na Mimi ,
Huku nikijifichaficha baada ya Misa kuisha nikawa wa kwanza kutoka na kurudi nyumbani huku nikiwaza sana
MUNGU atusamehe sana , hivi Leo kifuani Nina chale,Tena mbichi kabisa Leo nimeenda kanisani, Yesu mwenye alikataa mtu kuwa wa vuguvugu , leo hii sijulikani wamoto au wa baridi, MUNGU nahitaji huruma yako, nafika nyumbani nilimkuta ESTA kajaa tele anatusubiri,
Shemu huyoooo, alinikaribisha ESTA
Najua kama nimewahi sana ila kwakuwa Sina simu nikaona ni vyema kuwahi, aliongea.
Ina maana huna simu ya mkononi . Niliuliza kwa mshangao.
Ndiyo Nini Cha ajabu nimeamua kuiuza kwakuwa maisha ni magumu Tena na maisha magumu we Daniel acha tu, sijui kwanini MUNGU hanichukui nikapumzike Mimi.
Aliongea kwa uchungu sana.
Hayo siyo maneno Dada yangu,kikubwa ni kuendelea kumuomba MUNGU mbona kila kitu kitakuwa sawa tu,nilimfariji.
Hapana Dani siyo kwangu,Sina makazi maalum Sina familia,kama nyie wenzangu ama kweli ujanja mwingi mbele kiza,naishije mjini Daniel, aliongeza.
Dah,kwani kwa Sasa una kazi gani ya kujiongezea kipato? Nikiuliza
Niwe na kazi gani mwenzangu,Mimi naishi kama omba omba tu.
Nikaingia ndani nikawaza sana
Yule madam anaonekana anajuta kwa kile alichomfanyia mwenzake miaka hiyo na yupo tayari kumsaidia kama kumlipa kwa mabaya aliyomfanyia.
Mmmmh hili ni balaa,na Mimi sitaki kujiingiza kwenye huu upumbavu,kwanini asitafute wanawake wenzie wawaunganishe ,halafu hivi anashindwa kabisa kumsaka huyu akamface mwenyewe,
Natamanj nimwambie kuwa Kuna mtu Ana shida na wewe lakini siwezi,au nimuunganishe yule madam na mke wangu ili ujumbe umfikie ESTA?
Haaaa siwezi kwanza nitamtesa mke wangu na tumbo lake siwezi.
Japo kuwa lazima nitakaa na ESTA ili anipe background ya maisha yake ili lazima nitakaa naye.
Nikachukua kiasi fulani Cha pesa nikampatia huku nikimuahidi kumsaidia na pia nikisisitiza ananunue simu,
Alifurahi na kunishukuru sana.
ESTA mwanamke wa mjini kipindi hicho niliwahigi kumfuatilia sana lakini alinifungia vioo,sikuwa saizi yake
Lakini siku si nyingi nilimtongoza huyu, Kabla hatujakutana tayari nikapata taarifa juu ya shida yake.
Ni mzuri,mrefu kaenda hewani mweupe umbo ni kama madamu yaani wanafanana vitu vingi tofauti yao ni kwamba Madam ana weusi kidogo,wanaita chocolate colour.
Ila madam ana ngozi ya hela, huyu ESTA ukute anaogea mpaka sabuni ya magadi,wakati nafikiria haya nilisikia sauti za watu wengi wakija nyumbani kwangu.
Huku wakiwa wameongoza na mke wangu,
Mke wangu naye yaani kawatoa watu kanisani anawaleta huku wamekula kweli Hawa,haya si mambo ya kuharibu bajeti haya.niliwaza
Mume wangu wakati ibada fupi ikiendelea hapa itabidi ,itabidi tuandae Chakula kwaajili ya ugeni,
Haaaa uandae saizi kwanini usingewahi? niliuliza
Sikujua kuwa tukitoka tu kanisani watakuja moja kwa moja na huu siyo muda wa kubishana, najua ulitoa hela ya vinywaji,ila Leo bajeti zimeongezeka, aliongeza
sikuwa na jinsi ikabidi nifanye nilichoambiwa si wanasema wageni ni BARAKA,
Halafu njoo huku nje haiwezekani watu wanakuja wewe upo ndani tabia yako sijapenda mtu naangaza macho kule kanisani kumbe wewe umetangulia huku
Itaendelea............
Mdgo mdgo tutafika tuSEHEMU INAYOFUATA......
Nilitoka nje nikaungane na wale wageni wetu, huku nikiilazimisha furaha ambayo hata sikuwa nayo.
Tuliendelea na ibada huku wale ambao ni viongozi wakiwa wakitoa vijembe vya chini chini,
Jamani ndugu washirika na waamini wa mahali hapa, hebu tuseme kwa pamoja , hii ni jumuiya gani,?
Wote kwa pamoja wakajibu,
Ni ya mtakatifu DANIEL, huku wakishangilia kwa sauti na nguvu sana,
Nikajisemea hapa nasemwa Mimi, lakini nilikuwa Mpole na mtulivu huku nikijikita zaidi kwa wachambuzi mahiri wa biblia, jinsi ambavyo Tunapaswa kumrejesha kondoo aliyepotea.
Baada ya kumaliza ile ibada fupi, huku nikiwa na furaha kuliko mwanzo, kilifuata kikao Cha kutaka nijieleze ni Nini hasa kunanifanya nisipende kwenda kanisani ni takribani miaka miwili Sasa.
Sikuwa na majibu ya kueleweka dhidi ya blah blah tu, ikabidi ESTA atoe tu ushauri kwamba licha ya kuwa yeye alikuwa kwenye dhehebu tufauti ila amependa jinsi waumini wenzangu walivyokuja kwaajili ya kunikumbusha jambo muhimu na la maana kabisa.
Akashauri nipige magoti niombewe ,
Nikafuata Kila nililoambiwa nifanye, kila Jambo likapita wa kuagana tuliagana huku watu wengi wakiwa wanaelekea makwao, kasoro mtu mmoja ESTA aliyekuwa nusu kuondoka nusu kubaki yaani kama ile ibada tungesema tukeshe pengine angefuraji sana.
Haya maisha hayaaaaaahh, yamejaa UNAFIKI sana, Leo hii Hawa waliokuja kutaka nirudi kanisani nikiwachambua mmoja mmoja hakuna aliye msafi, wote wamejaa uchafu Kila kona.
Huyu ESTA mwenyewe Leo hii naye eti yupo kanisa la kiroho, kwa msimamo gani aliokuwa nao , mbona nilimtongoza huyu akakubali, angekuwa mwema, angewaza kutembea na mume wa mtu, Tena mume wa rafiki yake kabisa.halafu historia yake si nimesikia huko makanisani huwa wanawatega wanaume
Hakuna lolote,*********nilitukana kimoyomoyo.
Lakiniiiii,
Sipaswi kumhukumu mtoto wa watu, Huyu ni mwanamke, mtu ambaye Hana kazi mjini, Hana hata biashara yenye mtaji wa elfu kumi, kwanini nimlaumu kwa maamuzi yake, aliamini kuwa akilala na Mimi atapata pesa walau ya kujikimu,Ikamsukuma siku mbili tatu.
Kwanza biblia yenyewe imeweka wazi juu ya udhaifu wa wanawake, sipaswi kumhukumu kwakuwa hakuna binadamu aliyekamilika Mimi mwenyewe Nina chale mbichi kabisa hapa nilipo, MUNGU anisamehe tu.
Nilijiwazia moyoni.
Sasa shemu mi naona niwaache maana naona umejiinamia hata sijui unawaza Nini, alisema ESTA
Hapana shemu ni kawaida tu mbona.
Nilimjibu.
Hapana mume wangu,wewe Leo neno limekuingia vizuri na jumapili ijayo ukumbuke kwenda kanisani,
Alijibu mke wangu Huku wote tukicheka.
Halafu mume wangu huyu ESTA ana shida na wewe ,maana Mimi ameshanielekeza shida yake lakini nikamwambia siwezi kumpa jibu lolote Hadi niongee na wewe.
Ana shida gani,niliuliza.
Mimi naona ni vyema basi nikawapisha muongee halafu utaniambia,mke wangu alionesha kuniamini sana yaani anaingia ndani ananiacha na mwanamke.
Shemu una shida gani,hebu njoo tukae hapa ,nilivunja ukimya.
Shemu,we acha tu maisha nayoishi Mimi ni Sasa na chokoraa maana nimegeuka mbwa koko, ambaye Hana mmiliki kwahiyo Kila anapopita ni kurushiwa mawe ,
Kitu pekee kinachonipa faraja ni kwenda kanisani sehemu pekee ambapo nahisi nasikilizwa,lakini Nako utajikuta unasikilizwa mkiwa hekaluni au ibadani lakini kwenye maisha ya kawaida ni kama Sina rafiki,nikiomba msaada huu nanyimwa nikimtangazia mtu shida Kuna kuwa na uzito wa kupata huo msaada,miezi michache tu hapa nilimpata mchumba pale kanisani ambaye alikuwa tayari kabisa tuoane,
Lakini nilirushiwa maneno,nikatangaziwa vibaya sana mpaka ikafikia hatua nikaambiwa Nina ukimwi yaani wale naosali nao ndiyo waliomshawishi yule mwanaume kuwa haoni nilivyokonda,haoni kuwa nina dalili zote za ukimwi.
Ikabidi yule mwanaume aachane na mpango wetu huku akiniasa nisiwe na mazoea na yeye.
Anaendelea ESTA..........
Nakumbuka Kuna siku nilikutana na yule mwanaume sehemu tu ambayo tulikuwa wawili ikabidi nimuulize kwanini ana sikiliza maneno ya watu kama Hana Imani na Mimi tukapime afya zetu, lakini alinikatalia katakata na kunionya kuwa hawezi kujiaibisha huko mahospital eti sijui anaenda kupima, alinitukana matusi mazito sana Hadi pale alipokuja kutuamlia mwanamke mmoja ambaye sikuwa namfahamu akaniambia twende nyumbani kwangu huku akinibembeleza nisilie wala nisijali na huyo mwanamke ni huyu mkeo.
Aliweka kituo.
Sawa, wewe ESTA nakujua kitambo sana, baadaye ulikuja kupotea ulikuwa wapi? Niliuliza
Mimi bwana nilikuwa na maisha mazuri sana, yule mfanyabiashara wa mbao ambaye nilizaa naye watoto wawili ambao walikufa wakiwa na miezi miwili tu, baada ya hapo upendo Kati yangu na yule mwanaume ukapungua nikaja kugundua kuwa ana uhusiano na rafiki yangu mmoja, ila hayo tuyaache. Alisema kwa sauti ya chini sana na kwa hofu
Nikanote kitu.
Baada ya hapo, nikatoka kuelekea mkoani kwangu(akiutaja huo mkoa)
Nikaifungua biashara fulani ambapo niliishia kufilisika tu, lakini ikatokea bahati ambapo Kuna wakandarasi wa barabara walikuja kutengeneza barabara mkoani kwetu, kwahiyo kukawa na kijana mmoja ambaye alikuwa na hela nyingi sana , akatokea kunipenda sana kiasi Cha kunisaidia mambo mengi kwa kipindi hicho niliweza hata kujenga kibanda kwa wazazi wangu.
Lakini baada ya kazi yao kumalizika alinichukua nije Dar es salaam tuanze maisha ila chaajabu alinibadilikia akanifukuza kwake nikawa natangatanga tu hapa mjini kabla ya ya yule rafiki yangu ambaye alinichukulia bwana wangu wa mwanzo kusikia eti anaye Tena na huyo, nilifikiria sana kwamba kwanini hili jambo la kuporwa wanaume linajirudia sana, ikabidi nirudi mkoani niuze kibanda changu ili nipate pesa ya kujitengeneza na kusafisha nyota.
Kweli nilizunguka kwa waganga wa kienyeji wa kila aina lakini toka hapo na huu uzuri wangu sikufanikiwa kupata bwana mwenye hela kama wale hata baada ya kumgeukia nimroge yule aliyeniibia watu wangu niliambiwa kwa pale nitagonga mwamba hasa kulingana na asili ya kabila na mkoa anaotoka jinsi wanavyosifika kwa ushirikina.
Aliweka kituo.
Pole sana shemu, je ulishawahi kupima afya yako ili ujijue? Niliuliza
Ndiyo, nilipima, Iko hivi baada ya mkeo kunichukua ile siku, alinishauri kuwa kama nimeambukizwa VVU ni vyema nikapime ili nianze dozi mapema,
Binafsi sikuwa na Imani kama nimeathirika , Cha ajabu mkeo akawa analazimisha kuwa ni lazima nipime akidai ananiona nikiwa na dalili zote, hata siku ile ambayo nilitaka kuja kutafakari neno halafu wewe ukawa bize sana, mke wako alisema kuwa lazima nikapime kwakuwa yeye anaziona dalili zote, sikumbishia kwakuwa wengi wape ujue neno likikolezwa na wengi hata Kama la uongo hugeuka kuwa la ukweli..
Tukapanga Mimi na mkeo anisindikize ili tukapime japo nilimwomba twende sehemu isiyokuwa na watu wengi kuogopa macho ya watu.
Tulipendekeza twende kituo Cha afya ambacho ni maarufu sana japo ilikuwa kupima na hela, Mimi sikuwa na chochote hata kumuomba mkeo hela nikaona aibu ,
Nikawa nategemea mpango wa Mimi na wewe ulionambia upo safarini ukishuka tutakutana lodge kabla ya kuona hupatikani, nikaamua kurudi nyumbani,
Kesho yake ilikuwa ni siku ya Mimi na mkeo kwenda hospital lakini nilimkuta akiwa na majonzi kuwa kapata taarifa kuwa wewe una matatizo. Ikabidi nimsindikize mpaka ofisi ulizokuwa unafanyia kazi, nilishtuka kuona kumbe ulikuwa unafanya kazi sehemu nayo ijua vizuri sana, nilishindwa hata kuingia ndani ya geti naamini hata mkeo alishangaa ila sikuwa na namna wala sikumwambia chochote.
Tulirudi huku nikimuaga mkeo njiani nielekee kwangu, baada ya kuwa nimekutana na mbaya wangu ambaye alipata mafanikio ambayo pengine yalikuwa ni yangu
NAMCHUKIA SANA BOSS WAKO
Aliweka kituo
Mara nikamuona house maid yupo mbele yetu,
Shemu unaitwa, nikiangaza macho nani ananiita , nikamuona mama yangu mzazi, akiniita kwa kuashiria vidole akiwa pembeni kabisa,
Eeenhee vipi mama Kuna tatizo, naona si kawaida kuniita ukiwa huku, niliuliza
Hivi we Daniel una akili kweli, hebu angalia saa ni saangapi, yaani ni tabia gani ya kuongea na mwanamke mwingine, kwenye nyumba ya wewe na mkeo, huoni hata aibu,
Aliongea mama kwa sauti ya chini kiukali.
Hapana Mama, kaniruhusu mwenyewe niongee naye,
Hata Kama mwanangu, anaweza kukuruhusu mwenyewe lakini akaja kukubadilikia , sisi wanawake tunajijua wenyewe hebu mruhusu aondoke na wewe ingia ndani, kama masuala yenyewe ndiyo haya Mimi sitakaa hapa sitaki masuala yasiyo ya kinidhamu aliwaka sana MAMA,
Nijaingia ndani, nikagundua kweli mke wangu kanuna.
Nimesikia ukweli wa madam yaani boss wangu wa kike,
Madam anadai anaomba akutane na ESTA amuombe radhi na amsaidie,
Nasikia Leo ukweli wa ESTA
ESTA hataki kusikia Wala kuonana na madam anadai ni mtu aliyemuharibia maisha yake yaani kwake haiwezekani kabisa,
Itaendelea..........
Interesting..... Shusha vitu mkuuSEHEMU INAYOFUATA......