Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Yes! Inawezakana Ni Kama unao huambiwi. Kuna mshkaji tulikuwa tunasapua naye sapu Sasa bana si akashindwa kusapua na kusoma Ile gpa ili aendelee na mwana Sasa kiongozi akawa anagwaya kumwambia mtu Yuko udsm CoET ndoto zake zinatimia ghafula unaachishwa chuo,unadata na kuzimia ama kufa Kama unayo BP ,ilibidi niuvae ujasiri nimwambie Mana muda wa cafeteria tulikuwa pamoja. Tukinunua tikiti tunakata pasu tunalipiga na kijiko kwa pamoja, baadaye inabakia Kama sahani
Mzee wa COET....full kupiga RB!! Hahaaa umenikumbusha kitambo sana bro
 
Jamani Kuna michepuko una faida mno mjue yaani mno. Ila sio Hawa hàwaeleweki hawajasoma,mpaka vocha ya buku wanaomba. Kutana na mtu ambaye anakuomba milioni kwenda juu jamani.
Mapovu ruksa
Nakazia hapo..hata ukikwama anaweza kukubusti kwa pesa ndefu.Date na mwanamke mwenye akili na kazi yake. Utafurahi maisha
 
Nakazia hapo..hata ukikwama anaweza kukubusti kwa pesa ndefu.Date na mwanamke mwenye akili na kazi yake. Utafurahi maisha
Sure mkuu sio Hawa hata buku ama nauli tu ya Kuja kukufuata ama kulana utamu anataka atumiwe ,yaani yeye anachomiliki Ni mbususu na huku hata mbuzi mbususu anayo
 
Ahsante sana kwa maoni na mtazamo wako, wazo la kutoa movie hata baadhi ya member wengine wameshauri hivyo.

Ila si jambo jepesi, gharama zake ni kubwa hasa kama unataka tamthilia ifike kwa walaji ikiwa na viwango vya 2022, kama stori ilivyo Kunatakiwa Shots na scenes zote ziwe kali, kwa mfano boss awe boss kweli kweli, magari makali, vituo vya polisi kama ni police post iwe hivyo kama ni central, iwe hivyo, lakini pia wahusika nao ni wengi sana,

Yaani movement zote, from 2011 to 2013 ,huku locations zisiwe za kujibana , kumbuka Kuna riwaya na visa vipo humu jamiiforums ni Kali na zenye kuvutia, lakini baada ya wahusika kutoa movie au tamthilia hazikuwa na mvuto kama ilivyo simulizi.

Nikiri wazi hapa Tanzania,kunako bongo movie Kuna vipaji haswa, vya watunzi na waandishi lakini kazi zao Mara nyingi zinakosa .bajeti, bajeti, bajeti,.

Waigizaji mahiri,
Locations nzuri,

Mfano Mimi na madam tulikuwa tunakutana kwenye migahawa tofauti tofauti hivyo inatakiwa hata kwenye tamthilia iwe hivyo hivyo jambo ambalo kivitendo ni ngumu.

Hii inataka mzigo wa kutosha kuiandaa.

Yote kwa yote niwape pongezi wanaoguswa Kila mtu kwa namna yake , tuenjoy simulizi maana ipo hatua za mwisho

Uzuri simulizi inajisimulia yenyewe kwenye vitu vilivyonitokea, nipo tayari kujibu maswali yenu.
Tumtafute JB au Lamata producer wa Jua Kali
 
SEHEMU YA MWISHO......(FINAL)

Kwa wenye kuamini Dini na madhehebu yao, au hata wanaoamini sehemu wanazozijua, wote kwa pamoja tuweke IMANI kwa MUNGU mmoja maana yupo na anatenda.

Maisha yaliendelea, familia zilifurahi huku Kila kitu kikiwa kwenye mpango sahihi kabisa

Mume wangu, unajua kama tarehe 17 mwezi huu, ndiyo siku yako muhimu wewe kuripoti kazini?
(akimaanisha tarehe 17 ya mwezi wa kwanza mwaka 2013).

Usijali mke wangu, najua sana, najua hilo, ila bado wiki nzima ujue. nilimjibu.

Sawa, ningekuwa na uwezo ningekufungia ndani usitoke kabisa, maana najua huko kuzurura kwako unaweza kuyazua huko ukaja kukatisha ndoto zako, nimechoka masuala yasiyokuwa na maana.
alilalamika.

(Nikicheka)
Ajali haina kinga mke wangu, hata nikikaa hapahapa lolote linaweza kutokea bado nikakatisha ndoto zangu, kikubwa ni kumuomba MUNGU ili atufatufanyie wepesi na kunyoosha mapito yetu. Nilimjibu.

Amina, basi piga magoti nikuombee maana hiyo kazi ni ya muhimu kwangu kuliko hata wewe,. aliniomba nifanye hivyo.

Kwa kumridhisha kutokana na Imani yake niliweza kufanya hivyo ili tu nisilete mgongano Kati yetu.
Baada ya kumaliza yale maombi mafupi , nilimpigia Rose ili tukutane maana alikuwa ananyanyasa sana moyo wangu.

Ndugu msomaji, kazi niliyopata kwa sasa hakujua mtu yeyote zaidi ya mke wangu na Rose.
Rose anajua kwakuwa ni mmoja wa wahusika walionipigania kule, ila yeye hakuwa na Imani juu ya Mimi kufanya kazi pale, maana Mara nyingi alikuwa akiniuliza akitaka kuhakikisha, kama taratibu zimekamilika.

Na Mimi sikutaka kumwambia na kutapika yote, kuhusu ile kazi kwani, licha ya kuwa nilishakamilisha vitu vingi lakini bado niliamini kwa asilimia tisini tu, hivyo kumwambia mtu na kujimaliza Kisha mpango wako ukakwama, sijui utaeleza nini.

Lakini nilichogundua ni kwamba penzi letu na Rose, Lilianza kufifia yaani lile penzi moto moto sikuliona tena yote haya yalisababishwa na Mimi kutokuwa na uhakika na kazi.

Nakumbuka tulikutana kwenye mgahawa mmoja Mimi na yeye nikaagiza Chakula ili wakati maongezi yakiendelea tupate kuburudika naye.

Hivi my, kwanini unapenda kuharibu pesa hivyo, Mimi naona Bora hata uagize soft drinks tu inatosha, hakuna haja ya sisi kutumia gharama kubwa, alisema huku akimaanisha.

Nilimtazama nikimshangaa maana hawezi sema yale na hajawahi kusema jambo lile, hela hatoi mfukoni mwake kwanini zimuume?

Kwani baby Kuna tatizo, sioni kama ni vitu vya gharama kiasi hicho. niliuliza.

Ujue lazima tu nikwambie ukweli, Daniel (akinitaja kwa jina mithili ya shambaboy)
Wewe huna uhakika wa kazi, na kama ujuavyo hii ni January huwa Kuna ugumu fulani ambao unasumbua hivyo kuheshimu pesa ni suala muhimu sana,. aliweka kituo.

Kwanini unasema sina uhakika wa kazi, Ina maana huwa huniamini ninayokwambia? nishakwambia nimeambiwa niliripoti tarehe fulani, Cha ajabu nini my, au kama Kuna jambo unalijua nambie maana hata wakati naachishwa kazi kule, wewe na mdogo wako mlikuwa mnajua na msiniambie, Sasa basi hamna kuficha nambie Nini umekisikia. niliongea kiume huku nikikaza uso mtoto wa kike hawezi niletea dharau.

Akuuuh, sijasikia lolote toka kwa mtu yeyote, hata Yale ya tetesi za wewe kufukuzwa kazi, aliniambia mdogo wangu, ila zilisikika kama tetesi hatukuwa na uhakika Hadi pale ilipotokea kweli. kama nimekukwaza nisamehe, aliongea huku akiwa anavuta mkoba wake uliokuwa mezani na kuuweka mapajani ili kama ikitokea lolote iwe rahisi kuondoka.

Vyakula vililetwa muda mwingi sana nikaanza kula kwa kujilazimisha huku hasira nazo hazikuwa nyuma kutokana na demu anavyonichukulia poa.

Alipoona nakula naye akaanza kula nadhani alikuwa ananisindikiza tu ila hakuwa tayari kula na mimi,

Rose alibadilika sana.

Siyo Rose yule ambaye huwa haoni aibu kufanya chochote akiwa na Mimi, tulikuwa tukilishana mithili ya mapenzi ya under 23 age. alikuwa anafumua nywele zake Kisha ananiambia nimsuke basi kwakuwa siwezi tunajikuta tunafurahishana huku akinirudisha kwenye utoto,
Lodge zingekuwa zinaongea zina mengi zinashuhudia huku vyumba vikikosa ya kuongea kama samaki
Ndani ya maji.

Leo hii Rose hataki nimsogelee wala kumgusa, nikiuliza kwanini, anasema lazima tujiheshimu. Kweli hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho, lakini mbona huu mwisho kwangu umekuja mapema? nilijiuliza huku Chakula nacho kikipungua ladha sababu ya mawazo.

My tumekaa hapa, naona husemi umeniitia nini, maana nina haraka ujue sisi madaktari shughuli zetu huwa zina mabadiliko hivyo usishangae nikapigiwa simu muda wowote. aliongea huku akiwa busy na simu.

Nachojua Mimi na yeye tukiitana huwa hakuna sababu, yaani ukimwita njoo atakuja wala haulizi ulichomwitia, lakini Leo hii anataja niseme shida yangu! Ama kweli kanichoka.

Sina sababu maalum, ila furaha yangu nikukuona tu , we mwenyewe unatambua hilo. nilijibu huku nikimtazama kwa makini nikiusoma uso wake,.

Ahaaa ok, kama ni hivyo sawa, bila shaka umeshaniona, unaweza kuniruhusu niende? aliuliza

Mbona mapema hivyo my, kwanini tusikaekae kidogo, na tukitoka twende (nikitaja jina la lodge fulani)

Samahani yaani leo wala sijisikii vizuri sana, nashangaa mwenzangu mawazo hayo unayapata wapi, mwaka mpya umeingia huu, kule kwenye duka langu la dawa mkataba mpya wa kulipia lile eneo unatakiwa .

Hela zinazotakiwa pale, si haba pia hapa sijaja na gari kwasababu nimeliacha kwa fundi ili afanye marekebisho hela aliyonitajia ni MUNGU tu anajua yaani Sina msaada wowote ule, aliongea kwa kulalamika .

Akaendelea.....
Hivyo usione kama nakudharau ni kwamba navurugwa na vitu hivyo hapo. akaweka kituo.

Nilimwangalia Kisha nikacheka kidogo, maana mtu ambaye hakupendi ana Kila sababu ya kutaka muachane.huku nikijiuliza Kodi anayodaiwa huko dukani kwanini imsumbue, kwani duka au biashara yake haina faida, kusema huwa hapigi hesabu kuhusu TRA, Mtaji aliowekeza, faida zinazopatika, gharama za pango na makorokoro kibao kwani huwa hajui. Nilijiwazia moyoni.

Basi kwa maana hiyo , Mimi nimeridhika nashukuru kwa kutenga muda na nafasi ya kuonana na wewe, MUNGU akupe moyo huo huo. niliongea kimtego.

Usijali, nakupenda sana my, usinifikirie vibaya. alijibu shortcut huku akiondoka.

Si kawaida kuagana ndani ya mgahawa huwa ni lazima tusindikizane kidogo Kisha tunaachania mbele ila kwa siku hiyo ikawa tofauti.

Nilitoka nikichanja mbuga , huku moyo uliniuma kwani nilikuwa najua Rose anataka tuachane na Mimi sikuwa tayari kwani nilimpenda ile kumpenda sana, beautiful girl, English figure, na nywele nyingi Peruvian hair, ningemwachaje,

Achilia hayo kubwa zaidi ni Binti msomi, mwenye Elimu yake, mwenye kazi yake, nani anamrubuni my love Rose, mtu anayeongea kisomi huwa anapangilia maneno, kapata malezi Bora ya pande mbili, namuachaje jamaniiii.

Ni mshauri mzuri, ananiheshimu na kuiheshimu familia yangu. ana moyo wa huruma Kila unachomweleza huwa anakipokea na kutoa ushauri usioumiza, Sasa namwachaje Rose .

Ni Ms***e gani anataka kuniovertake achukue hii Mali. Aaaaaa weweee sitakubali.

Au ni masuala ya Kodi na gari lake yanamuumiza, ukute ni vitu hivyo kweli vitafanya nimkose Kisha akachukuliwa na mafioso wa hapa mjini.

Ngoja nitafanya kitu nauza shamba langu la huko kisemvule ili najua sikosi hela ndefu, nitahakikisha Rose hachomoki mikononi mwangu.

Ila shamba hapana, ekari kumi na kitu nauzaje kizembe? Ule ni urithi wa wanangu.

Au nikamsaundishe wife nimwambie nahitaji kama milioni moja Kuna jambo nakamilisha halafu, si nitarudisha ? halafu nimpe Rose naamini atalipa kupunguza matatizo yake. Kisha penzi litarudi upya .

Mmmh ila usawa huu kutoa jiwe moja uongo, wanawake huwa hawaridhiki hawa.

Nilijiuliza na kujijibu mwenyewe.

Nilifika nyumbani huku nikipokelewa na wife vikorokoro nilivyonunua na Mimi nikimpokea mtoto huku nikicheka cheka naye.

Mke wangu ujue siku zinavyosogea huyu mtoto anazidi kuchukua sura yangu, yaani huyu simuiti mwanangu Bali pacha wangu. sipati picha miaka hiyo tukikwaruzana Mimi na wewe , atavyokuja kunikoromea huku akinitisha.nilitania

Unapenda sana kusema mmefanana ila namuomba MUNGU mfanane sura siyo akili na maamuzi yako. Maana mume wangu kama ingekuwa siyo Elimu yako, napata picha ya maisha ambayo tungeishi. aliongea kwa kumaanisha.

Kila kitu hupangwa na MUNGU ukute ningekuwa Sina Elimu ningekuwa na good life zaidi , yaani circle of life ione hivyo hivyo mke wangu.nilijibu huku tukitaniana mambo mbalimbali, nilifurahi kwani ilinipunguzia machungu ya Rose.

Siku zilikimbia na kukatika huku tarehe husika ya Mimi kuripoti kazini ikifika, nakumbuka siku hiyo ya jumatatu nilifika kazini na kukabidhiwa ofisi yangu huku taratibu zingine zikiendelea kukamilika. hatimaye nikawa mfanyakazi rasmi wa taasisi yenye heshima nchini. Huku nikipewa na gari kwaajili ya kurahisisha mizunguko yangu maana kazi niliyopata huku neno kwenda mkoani lilikuwa ni jambo la kujiandaa kwani ni muda wowote na saa yeyote.

Penzi la kulazimisha Kati yangu Mimi lilirudi japo siyo kama zamani , maana penzi hili watu kukaa wiki nzima bila kutafutana ilikuwa kawaida tu.

Tuliachana vipi na Rose......

Nakumbuka Kuna siku moja , Rose Rose nilimpigia simu kuwa kesho ijumaa weekend inavyoingia tuonane, alikubali kuwa hakuna shida.
Kweli baada ya kesho kufika nilitegemea kuwa hii leo tutaonana ili tukamwagilie moyo, mimi na yeye, chaajabu Kuna muda kama saa kumi na moja alinipigia simu akidai tuahirishe tu lile zoezi, maana Kuna dharula mama yake anaumwa sana.

Nikamwambia kama ni hivyo basi nifike tu nije nimuone mama, alikataa kwa kusema si jambo jema , maana haitaleta picha nzuri.

(Na hili nililileta humu Kuna Uzi unasema hivi

"UJINGA NILIOWAHI KUUFANYA KULILIA PENZI LA MCHEPUKO "

Sasa endelea.....

Basi baada ya kunikatalia nisifike, niliamua kumrushia kiasi cha laki moja na nusu kama mwanaume uliyepokea taarifa ya ugonjwa lazima ujiongeze, alishukuru huku, Mimi Ahadi yangu ya kwenda viwanja ikiwa pale pale.

nilimchukua jamaa mmoja ambaye huwa tunaongoza sehemu nyingi tukachagua kiwanja kizuri tukaenda kufika pale, nilichokiona kilinishangaza sana kwani nilimuona Rose akiwa kimahaba na kijamaa fulani huku wakiwa kwenye mahaba mazito sana.

Aisee baada ya macho kugongana nilipata hasira sana, tena mno nikataka kuanzisha ugomvi lakini mchizi wangu alinisihi.

Dani braza, utaharibu ujue kwanza wewe una mke , vipi shemeji akija kusikia umeanzisha ugomvi sababu ya mchepuko utajidharaulisha bro acha, aliongea yule jamaa yangu huku akinishika mkono na kuondoka eneo lile.

Tulibadilisha kiwanja, huku tayari nikiwa nimevurugwa maana nilimpenda kupitiliza hivyo niliumia sana kwa aliyonifanyia.

Naam baada ya hapo hakuna aliyemtafuta mwenzake , na penzi likafika mwisho.

Nikarudisha UPENDO kwa familia yangu huku matukio ya mikosi kwa upande wangu yakipungua , nikizidi kupiga kazi huku wigo wa kujuana na watu wakubwa, wazito na kujua mambo mengi vikizidi kupanuka.
Kweli watu ni mtaji.

Hii ni tamati kwenye simulizi hii, nimeamua kushare na wanajamvi simulizi hii ili ,
Tuburudike na tujifunze mambo mbalimbali, kwa waliokata TAMAA wakae wakijua siku yao ipo kwani hakuna maisha magumu.

Bali Kuna mapito magumu.

Jack Daniel member wa jamiiforum.
Hongera Daniel Jack,,,nimejifunza mengi kupitia story ,,,,nimesoma hii story kuanzia saa 9.00 Am, hadi muda huu saa 11:36ndo namaliza,,,Asante sana
 
Yaani nimejikuta nataka kutoa chozi as if ni mhusika mwenyewe. If it's a true story I can't imagine how the situation became after receiving a letter from mtu mbaya manager wake.
Hii story nilianza kuisoma few days ago!! Sasa hapo alipoandika kuhusu kufukuzwa kazi huwezi amini niliweka simu chini butwaa imetamalaki as if mimi ndiye niliyekutwa na huo msala.

Kingine huyu aliyempa taarifa ya kufukuzwa ni GM sio yule manager aliyepigana nae.
 
Nilicheka kivivu, huku nikijiona Kuna kitu nimepoteza, why mpaka housemaid naye anataka pesa zibaki ili zitusaidie, si dharau hii.

Halafu mbona mke wangu, hakumwambia kuwa hatuna hela ya kumlipa, bali alimwambia sababu zingine tu.

HAPANA nilimwambia dada wa kazi kwamba Kama anatuma atume hela zake zote huko kwao Kisha yeye abaki tutaishi na mke wangu akakubali kuwa abaki si kasema anaweza kukaa bila kupewa posho yake, sawa tutaishi kuwa na amani mdogo wangu hatukuwa na lengo la kukufukuza, alimalizia mke wangu.

Lakini Mimi niliwaza tofauti, maana si kwa kupigika kule nakosa hata hela ya kumlipa huyu dada, hapana lazima nifight nihakikishe huyu hakai hapa bure kama alivyodai hata kama kwao inaonesha kuna maisha magumu zaidi lakini hatofanya kazi bure hapa kwangu.

Hela yake ya miezi minne nikiwa na kazi, si nilikuwa nikipita kwenye baa ya mshikaji wangu Shedrack nilikuwa naikata masaa mawili tu.

Lazima nitamlipa, nilijisemea.

Kama kawaida Sina kazi ya maana, nilikotuma maombi siitwi hata kwenye usaili, nikaona kweli shetani akiamua anaweza.

Mbona nikiwa na kazi yangu ndiyo kwanza mabosi wakawa wananitafuta, Leo hii jiji Zima hili sionekani wakati nikijiwazia hayo simu yangu ikaita kucheki jina ni mshikaji wangu shedy,

Nikaipokea,

Oy babuu mbona unalala tena, we Jana tuliongea Nini?

Unajua wewe, lazima ukubali kuwa kwasasa ile kazi yako huna Tena na ukikubali hutopata taabu kuliko kukaa ukijiliza kwa mkeo.

Alibwata sana,

Hiyo ndiyo salamu mwanangu, niliuliza.

Salaam kitu gani kaka kama ukitaka kusalimiwa pita maeneo ya shule za kayumba utachoka wewe tu.

Wahi bwana, akakata simu.

Nilihisi kudharauliwa, Shedy ni mshikaji wangu hakusoma kabisa yeye ni form four failure lakini yupo vizuri kimaisha, shughuli zake kubwa ni udalali na anapata hela kiasi Cha kumiliki vimiradi vidogo vidogo vingi huko pembeni ya mji.

Lakini pia ana bonge la baa hapa mjini, ndiyo sehemu yangu kubwa kipindi hicho kabla sijajivika ulokole kwa muda.

Lakini pia, Mimi naheshimika pale kwake, hata akiongea na Mimi jambo huwa mstaarabu, Leo hii ananikoromea?

Kama ni pata pesa tujue tabia yako,

Kwangu ikawa,

Kosa pesa ujue tabia zao.

Nilichukua mkoba wangu, huku kichwani Nina bonge la kapelo ili kuzuia watu wasinijuejue.

Hatimaye nikatimba ile sehemu nikamkuta Shedy yupo na washikaji kibao ambao ndiyo wenye Mali, ilikuwa ni gari ya mizigo aina ya Scania pulling 113.

Almaarufu one one three.

Nikawa nipo nipo tu, sijui biashara zinaendaje, basi nikavuta kiti nikakaa nikisubiri nipewe maelekezo,

Maana gari si yangu, kwamba nauza. Mimi Sina hela kwamba nanunua, nikawa nafikiria kila siku tunafanya udalali, lakini ya Leo kali.

Oyaa bro, unawaza Nini hapo, njioy huku basi yule jamaa kashafika, changamka basi au unafikiri unagonga mihuri kuidhinisha wakandarasi hapa.

Yule dogo akanikejeli.

Basi Shedy akanifuata na kusema,

Unajua ndugu yangu wee huna kazi ila nimekuita ili na wewe uwe sehemu ya huu mgao lakini kifupi huna majukumu makubwa kwenye hii ishu.

Nikamshukuru tu maana hata hivyo bado alikuwa na utu

Nikaingia ndani, nikakuta kuna watu wanne sura ngeni, kumbe ndiyo mabosi wenyewe wakiwa na fundi wao wa kujiridhisha kama chombo kizima ili biashara ifanyike.

Nilichogundua kwenye zile biashara usimwamini mtu, wale jamaa wakamwambia Shedy kwa gari iwashwe ili wasikie muungurumo lakini aingie yule fundi wao aendeshe waangalie namna ya uingiaji wa gia
Kama zinaingia zote.

Basi mshikaji wangu Shedy akaniambia Sasa hiyo ndiyo kazi yako na wewe muongozane na huyo fundi wao ili uwe ni sehemu ya wataoleta mrejesho

Basi wanaume bila kuzubaa tukaingia kwenye gari kule mbele kukiwa kuchafu maana inaonekana waliipaki tu huko yard

Aisee yule fundi alichangamka kichizi huku akionekana muongeaji sana,

Sikia mwanangu hii gari ni majanga ni hamna kitu hamna mipira, anaongea huku anaendesha ujue,

Sikia, sikia hii clutch haimalizi ujue, yaani gia zinaingia kiugumu.

Lakini gia namba nne ndiyo haiingii kabisaa, lakini mwanangu lazima tutengeneze pesa, tukitoka hapa tukawaambie gari ni nzima haina tatizo, dili likitiki nitakupa laki mbili.

Nikaona mbona freshi Haina shida nikamkubalia lakini nikawaza isije ukasifia kitu usichokijua, halafu wakakwambia uwaoneshe kinafanyeje kazi si ishu hiyo.

Tukarudi kuleta mrejesho,

Bahati nzuri wale mabosi wanunuzi walimwamini sana fundi wao, ambaye Mimi niliye Kaa naye dakika kumi tu nilijua huyu ni jipu.

Tukaisifia gari biashara ikafanyika, Tena bila longolongo.

Mambo ya documents na taka taka zote zihusuyo hiyo gari wakapewa.

Macho yangu yapo kwa yule mchizi, maana Shedy hawezi kunidhulumu si aliniita mwenyewe lakini huyu fundi aliyekosa uaminifu.

Bahati nzuri akaniita pembeni hakuna watu akanipa laki mbili cash huku akionekana ana burungutu ...jamani maisha haya, nilimshukuru sana yaani ilikuwa Kama mchezo wa kuigiza.

Watu tukasambaratika huku hata mshikaji wangu shedy akiwa hajui kama Nini mia mbili pembeni,

Angejuaje, na kwa nini ajue.

Itaendelea.........

Ntaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom