SEHEMU INAYOFUATA................
Nilijua tu lazima urudi muda huu, tena umelewa mwenyewe kwa raha zako, kweli maskini akipata......... (Kabla hajamalizia )
Mke wangu naomba tuheshimiane, kuna njia nyingi za kuweza kumkosoa mtu ila si kumtukana , sisi binadamu tuna majina mengi Duniani. Kuna sehemu ukipita watu watakuita genius kwa sababu wanazozijua wao , wengine watakuita fala au mpumbavu, si kwamba labda Kuna kibaya umewafanyia bali Kila mmoja ana haki ya kukuchukukia anavyoona yeye .
Lakini wewe kwangu unalazimika kuniheshimu kwa asilimia nyingi, siyo kwamba siwezi kukuudhi, maudhi si ndiyo kama haya? Lakini Kuna namna ya kumkosoa mumeo. Naitwa mume Mimi ni rafiki yako, mshikaji wako lakini Nina nafasi kubwa zaidi watu wote wananiita mume wa..........
Tuheshimiane mke wangu.
nilimsema.
Sawa mume wangu, swali liko pale pale ulikuwa wapi, aliuliza.
Nilikuwa baa na marafiki zangu tukipanga na kupangia vipi Kuna Sheria nimeivunja,Nini hakipo hapa nyumbani, kila kitu kipo kwanza sioni haja ya kuendelea na maswali Hadi sasa. Nilimjibu kwa uonevu hali iliyopelekea akashindwa kuendelea kuniuliza huku akikasirika kwa kiwango Cha juu, nakumbuka alichukua kigogo fulani akanirushia kikanipata sawa sawa, ikabidi nikimbilie chumbani nikijifanya nimeumia sana .
Namjua mke wangu akikasirika, hachelewi. Kitendo Cha yeye kuniumiza kikawa ni mtego kwake., nilingia chumbani nikafikia kuoga huku nikijifanya Nina maumivu sana, ila haikuwa kweli ila niliigiza ili nimkomeshe asiwe ananiuliza uliza.
Shemeji, shemeji, ilikuwa ni sauti ya dada wa kazi akiniita kwaajili ya Chakula Cha usiku .
Hapana nyie kuleni , Mimi! Najisikia vibaya. Nilimjibu huku nikisikia akipiga hatua na kuondoka.
Dakika chache mke wangu alikuja akasukuma mlango huku akiwa kaweka mikono kiunoni,
Mume wangu Chakula tayari amka basiiiiii,
Siwezi Nina maumivu sana huku mgongoni nikiwa sawa nitakuja , tayari nilishapata pointi,aliondoka huku aliongea maneno ambayo sikumsikia vizuri ila alionesha kujuta sana, kesho asubuhi na mapema alikuja kwangu.
My husband umeamkaje, vipi unaendeleaje? Maumivu je?
Nimeamka salama japokuwa Nina maumivu sana nadhani nikiamka nitaenda hospital na Leo jumapili sidhani kama nitapata huduma kirahisi . niliongea kwa mtego.
Mmmmh mume wanguu naomba unisamehe Mimi ujue hata sijapata usingizi mwenzio, Jana hujala vile vile bado unaumwa, nisamehe baba Jack sitarudia tena,aliongea alionesha kujuta.
Mke wangu Mimi nilishakusamehe tangu jana, mpaka Sasa sijui kosa langu Nini maana umenihukumu kisa umetambua kuwa nimelewa , Sasa nikuulize, ni wapi nimevunja nikivunja Sheria, niliongea huku nikizidi kujifunika shuka .
Mimi Sina maumivu ya kwenda hospital ila nakuonya kwa Mara ya mwisho, kurushiana vitu siyo vizuri , muda wowote unaweza kupata murder case wewe, tena nikukumbushe unakumbuka ulivyomfanyia Shedy?
Kidogo umtoe jicho Sasa vipi kama angeanguka hapo nje akapoteza uhai huoni kama tungeungana mahabusu huku wewe ukikakabiliwa na kosa lisilo na dhamana, mke wangu unanitisha sana kwa naamuzi yako naomba jitahidi kujizuia na kudhibiti hasira zako vinginevyo wewe ni mfungwa mtarajiwa.
Usiseme hivyo mume wanguu (huku akitoa machozi) naomba nisamehe sirudii tena Mimi .aliongea kwa uoga.
Hapa shida siyo msamaha, tatizo ni tabia yako, Mimi nitakusamehe lakini jua wengine hawana msamaha kabisa, kwahiyo punguza hasira my wife, nilimtuliza ni wanawake tu Hawa kuharibu kitu na kukimbilia kujiliza , yaliisha.
Mume wangu naomba niende kanisani, maana tangu nijifungue sijawahi kwenda, aliongea hivyo baada ya kugundua kuwa sina maumivu kihivyo.
Usijali we nenda tu, nilimruhusu.
Walijiandaa huku Mimi nikiombea watoke nipate kuongea na simu zangu, baada ya mke wangu na dada wa kazi kwenda kanisani nilitoka ili nikapate mchemsho maeneo jirani na nyumbani kwangu maana njaa + hangover za pombe nadhani nilihitaji kuupatia mwili chochote kitu.
Aaah Daniiii afadhali nimekuona bosi wangu maana mwenzetu maisha safi kabisa naomba japo nichukue chapati mbili na chai na mimi maana hali si hali, aliongea kijana mmoja.
Sina kitu jamani hamuoni jua ni kali wanangu,?
Haaaaaa Dani, acha hizo juzi tu tumepita kwako tumeiona fence hiyooo inakaribia kuisha halafu unajifananisha na sisi acha hizo jombaa , walizidisha maneno wale vijana wahuni, ikabidi niwanunulie wanachotaka, walishukuru sana,
Dah mwanetu Dani tunashukuru sana we ndo homeboy wetu unajua Nini hunaga baya yaani, waliongea huku natamani waondoke, nikiwa naendelea kula wao walishamaliza tayari, ni vijana fulani wa mtaani pale , hawana tabia nzuri sana ila Ukiwa mjanja jitahidi kuishi nao vizuri usipende kuwakazia mlioishi uswahilini hapa nadhani mmenipata.
Oyaa braza Dani nimewasikia vijana kuwa una ujenzi huko kwako, vipi Kuna maisha. Aliuliza jamaa mmoja anayeonekana kunifahamu sana,.
Hapana Sina kazi kwasababu Kuna mtu keshachukua tenda hiyo hivyo ana vijana wake tayari anaofanya nao kazi, nilimjibu
Poa pia bro kama una mishe naomba nikuachie namba zangu za simu (huku akitaja) .
Nilimaliza kula pale Kisha nikaishika njia taratibu nikirudi nyumbani huku natafuta jina la Rose nililo sevu navyojua Mimi, simu ikionesha inaita upande wa pili.
Hello habari (niliisikia sauti yake nzuri huku mapigo ya moyo yakiongezeka)
Salama my friend umeamkaje? niliulizia hali.
Weeeeh (huku akicheka) yaani ile wine huwezi amini ilinichanganya hata vile nilivyokimbilia kwenye gari kifupi nilikuwa sijisikii poa, hivi hukunigundua? aliuliza
Hapana, Mimi nilijua labda kwakuwa muda umefika ndiyo maana ukaondoka. ila pole sana unaonekana si mtumiaji wa vitu vile, niliuliza.
Aisee umejuaje kiufupi Nina muda mrefu sijawahi kutumia kilevi, halafu kichwa changu nakijua mwenyewe, mnaitaje vile mtu asiyeziweza pombe?...
Kabla sijamjibu, niliona Kuna ugomvi mbele yangu watu wawili mwanamke na mwanaume Tena mwanamke namtambua, ikabidj niisubirishe simu ya Rose ili nione kinachoendelea hapa, alikuwa ni ESTA na jamaa mmoja wakiwa wanavutana huku ESTA akiburuzwa, huku baadhi ya wapita njia na majirani wakiwa wanaangalia ile action bila kutoa msaada.
Jamani, jamanii Kuna nini hebu tulienk kwanza mbona mnatiana aibu mtaani jua lote hili Kuna Nini kaka hebu nambie, nilimshika mkono yule jamaa mgeni machoni mwangu huku nikimbembeleza apunguze jazba .
Unajua kaka Hawa wanawake was...e sana , huyu alikuwa ni mchumba wangu muda mrefu sana ila nilisafiri , Sasa kwakuwa huko nilikokuwa nilikaa muda mrefu nimerudi na kukuta amebadilika na pia ana saloon kubwa sana maeneo ya mjini (akitaja eneo ambalo hata Mimi nilishangaa maana navyojua Mimi saloon ya ESTA haiko mbali na maeneo yale)
Muongo huyo shemeji, hakuwa mchumba wangu, Bali ni mtu nilikuwa nasali naye kanisa moja hivyo mchungaji akawa anashauri tuoane, ni ushauri tu ila hatukufikia hata level za uchumba. Kwanza Mimi hata sikumpenda huyu ni kwasababu mchungaji alikuwa ananilazimisha. aliongea kwa jeuri huku nikitambua kashaanza kujivunia uwepo wangu.
Usijali bro, we usigombane naye tumia njia tu za kistaarabu atakuelewa tu huyu , pia hapa wote mmeshakuwa na presha hivyo hakuna jibu litapatikana zaidi ya kuharibu, utajikuta unaishia pabaya.
Si wanawake, si wanaume walimtukana sana jamaa kuwa kwanza haendani na ESTA na kwanza wanawake walivyojaa kwanini amng'ang'anie mtu mmoja? nilimuhurumia mshikaji maana mtu pekee nilikuwa namtetea ni Mimi tu wengine wakimuona jamaa ni mshamba na limbukeni wa mapenzi.
Sasa na wewe ulikuwa unaenda wapi. Nilimuuliza ESTA,
Mimi nilikuwa nafuata gari ili ikanihamishe nahamia sehemu nyingine pale naona pamekaa kiswahili sana. alijibu kwa nyodo,
Nikacheka huku nikijisemea moyoni kweli pesa sabuni ya roho.
Kuepusha Shari niliondoka na yule mshikaji ambaye alionesha kuchanganyikiwa sana yaani alinasa kwa ESTA.
Kwani ESTA ana nini au hata Mimi ningetembea naye ningepagawa maana wanawake wengine ukinasa hutoki, ila siyo Mimi labda Hawa walugaluga. Nilijisemea kimoyomoyo
Bro unaonekana unafahamiana na yule ESTA. aliniuliza yule mshikaji.
Ndiyo, namfahamu ni rafiki wa mke wangu. Nilimjibu .
ila usiwaze Mimi kwakuwa namfahamu vizuri na nishajua shida yako hili niachie Mimi litakaa sawa tu nitaongea naye. Jamaa alifurahi sana
Halafu nikushauri jambo moja jitahidi sana kutumia njia ya kujishusha maana pale mlipokuwa
Mnaburuzana wenzio walisubiri tu uharibu ili wakupige au upelekwe polisi au hujui furaha ya binadamu wengi ni kuona mwenzao akiingia kwenye matatizo.
Jamaa alinielewa sana, huku tukiagana,.
Siyo kwamba nilitaka kumsaidia kweli, ila ilikuwa ni njia ya kumuweka sawa maana alikuwa kama kachanganyikiwa, hivyo mwanaume mwenzio akiwa kwenye hali ile lazima umuoneshe matumaini ni maisha tu haya.
Baada ya upepo ule kupita nikarejea kwenye calls nikipiga simu kwa Rose ila haikupatikana, nililaumu nikajilaumu, piga Mara kadhaa lakini majibu yakiwa ni sifuri.
Nilirudi nyumbani nikawasha PC yangu nikakaa nayo kitandani huku nikitafuta vitu ambavyo sikuvielewa Mara niangalie video hii Mara hii ili mradi napoteza muda
Delivery report ya sms niliyomtumia Rose ilirudi , nikajua simu yake ipo hewani, nilitoka chumbani mbio huku nikiweka simu sikioni ili nikaongelee nje simu ilipokelewa bila kusikia sauti yeyote upande wa pili,
Hadi pale nilipoongea Mimi baada ya kuigundua sauti,
Hello Mr, vipi Kuna usalama kweli, sauti Rose iliyo kwaruza kwa hofu ilisikika
Ni salama tu my friend, vipi mbona sauti ya chini hivyo.niliuliza
Unajua haya mambo ya waume za watu ndiyo maana sijawahi kutamani , yaani baada ya wewe kukata simu ghafla nikajua pengine mkeo kakustukia hivyo nilizima simu kwa muda , Sasa yote haya yanini , yaani hapa nilipo moyo wangu unaenda mbio kwa hofu . alilalamika
Ondoa Shaka kwanza ukiona nimekupigia simu jua kuwa nipo sehemu salama tu. nilimtoa hofu.
Sawaa bado, nahisi Kuna matatizo nayatafuta huwezi amini umenitisha sana tu , aliongeza.
Kwanza uko wapi my friend maana uliniambia huwa unaenda kanisani, imekuwaje unaniambia upo nyumbani tu, niliuliza
Wewe nimeamka nimechoka sana nikashindwa hata kuamka mapema nilitamani Jana unisaidie hata kuendesha gari lakini nikiogopa waume za watu, kweli walioshauri usiendeshe Ukiwa umelewa waliongea point sana Jana ndiyo nimejua maana nilikuwa kama learner. (Huku akicheka)
Ennhee na mwenzangu ilikuwaje au wenzetu mmeshazoea ?
Aliuliza akidhani na Mimi Nina gari, ndiyo asingeelewa , maana nilikuwa wa kwanza kufika hotelini huku yeye akifuata pia akawa wa kwanza kuondoka, hivyo kwenye zile parking alidhani na Mimi Nina usafiri wangu,
Sikutaka kumwambia kuwa Sina gari japo tayari kutokumiliki usafiri kulianza kuninyima Raha.
Aaaahaaa hakukuwa na shida Mimi nilifika salama tu, nilimuongopea.
Sawa kwakuwa sipo bize sana Leo ningependa tuonane nimemiss stori zako , yaani hunichoshi kukusikiliza, aliongea kwa kudeka.
Sasa tuonane wapi, nilihoji kwa pupa maana mrembo nayemuwaza Leo anaanza yeye kutaka tuonane.
ESTA Kawa matawi ya juu kwanza anahamia maeneo ya mjini, pia Kuna taarifa kuwa hata saloon kafungua nyingine tena yenye hadhi ya juu.suala la kukosa gari lishaanza kuninyima amani huenda nikawakosa watoto wakali wa mjini
ESTA ni character mkubwa kwenye hii simulizi hivyo atapotea atarudi. Nini kita jiri usikose sehemu inayofuata.
Inaendeleaa very soon............