Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Nilitulia, nikapata chakula fresh huku nikiwa na shauku nini kipo kwenye ile barua

Nikaifungua nikaisoma nikawa nimeelewa, ni moja ya kampuni mpya ambazo nilituma maombi miezi miwili iliyopita, kwahiyo ni barua ya wito ikiwa inanitaka nifike kwenye kampuni zao ili taratibu zingine ziendelee.

Nikapumzika, Kisha nikamwita mke wangu,

Enhee habari za hapa,

Ni nzuri sisi tumeshinda salama kabisa mume wangu ila nina mazungumzo kidogo na wewe maana hapa nilipo hali yangu nishakueleza tangu jana, kwahiyo nafikiri ni muda muafaka wa Mimi kuanza kuhudhuria kliniki mapema.

Lakini mume wangu mbona hii taarifa tangu jana hata leo ,naona upo mbali sana, kwanini?

Nipo mbali kivipi, umeniambia upo hivyo ile Jana nimekubali, umeniambia kuhusu habari za kliniki, Mimi sijakupinga!!!!

Ulitaka nifanyeje labda, ulitaka niruke ruke kama wanandoa waliokaa miaka ishirini bila kupata mtoto.

Kwamba pindi nisikiapo hii kauli nishituke? Sisi siyo wagumba mke wangu tumshukuru MUNGU kwakuwa wazima kwahiyo taarifa hiyo haijanishtua, kifupi nimefurahi sana, mahari yangu naona inalipa haikupotea bure, nilitania wote tukacheka.

Basi sawa mume wangu, mimi nimekuambia ili ujue kuwa humu ñdani una mgonjwa tayari, huku akiinuka kuelekea nje.

Nilikaa kitambo pale ndani nikichezea chezea simu huku sijui hata nabonyeza button kwa malengo gani maana nilishachoka, huku nikijiwazia.

Dunia ya Sasa, inahangaika kutengeneza uzazi wa mpango wa kila namna ikiwa ni njia ya ku decrease population ya watu.

Maana tupo wengi mno lakini kumekuwa na milipuko kadha wa kadha ikiwemo Ebola inayowapukutisha watu huko Afrika magharibi, wajuaji wanasema pengine ni mpango wa wazungu katika kupunguza watu.

Lakini pia Nina marafiki wengi ambao wapo vizuri kimaisha lakini ndoa zao zinayumba sababu zikiwa kutopata watoto, na ni kweli, mbona hata rafiki yangu Shedy haelewani na mkewe japo yeye ndiye mtuhumiwa kwamba mimba zinaharibika, watoto wanakufa Mara tu baada ya kuzaliwa, huku lawama zikikaa kishirikina zaidi kwamba jamaa anaua watoto ili nyota ing'ae na kupush biashara zake.

Walimwengu bwana.

Pengine hata haiko hivyo, nilijisemea

Yote kwa yote acha mke wangu azae hata akizaa watoto kumi nipo tayari. Nikainuka nikatoka nje nikawakuta mke wangu na dada wa kazi wanacheka huku wakionesha wanafuraha sana.

Nikawapita, nikaona ngoja hata niende sehemu nikapige stori, huyoo mpaka kwa fundi TV mmoja hivi ambaye vitu vyangu vingi hurekebisha yeye pindi vikisumbua.

Aaaa karibu kaka, karibu sana, ilibaki kidogo nikupigie yaani ni kama MUNGU kasaidia wewe ufike hapa,

Aliongea yule fundi,

Yule jamaa aliyekuwa anataka TV kubwa ananisumbua bwana maana yule bwana ana Banda la kuonesha mipira, kwahiyo alikuwa anahitaji screen kubwa ili kuleta ushindani, maana wateja wamekuwa wakimtukana kwa kwamba TV zake ni ndogo kama side mirror, kwahiyo inamuwia vigumu sana.

Na hela kaka ipo ana mia tano Cash, halafu kaka ile TV yako kubwa mno, yaani kuuuuuuubwa kama nani za projector ni Bora uuze halafu utafute TV fulani ndogo ndogo na Kuna mama mmoja wa kipemba anayo TV anauza yaani ni nchi 21 ila kizuri balaa anauza laki tatu tu.

Kwahiyo ungeuza yako, bado ungebakiwa na hela nyingi tu ha hahaaa akajichekesha.

Baada ya kimya Cha muda mrefu nikamjibu siuzi.

Aaaaa kaka huuzi vipi wakati ulisema mwenyewe na Mimi tayari Kila kitu kipo sawa na hela kaniachia laki tano hizi hapa, sawaa hata Kama kakuachia hela Mimi siuzi TV, tubadilishe hizo stori.

Mara Kuna pikipiki kubwa likatia timu. Oyaaa fundi vipi bwana hadi saizi TV bado au hiyo laki nane umeenda kumuonesha kwanza mkeo ili ajue una hela teh teh yalicheka majamaa, huku nikiwaza kumbe angepata chajuu laki tatu nzima, siyo mbaya mjini hapa lazima ujiongeze.

Fundi akawa anajiumauma maana hata kuwatajia kwamba, ni huyu hapa mwenye TV asingesema, maana dili litabuma. Wanaweza kuongea na mimi yeye asipate chochote.

Nikamuaga fundi huyo nikaelekea sehemu nyingine bado akawa anapiga simu kunishawishi, isingekuwa hivyo niuze TV yangu mwenye nilivurugwa tu na maisha Hadi nikaropoka kuiuza lakini siyo siwezi kuuza.

TV toka Australia niliyopewa zawadi na wazungu sababu ya kuwasaidia wasipelekwe jela baada ya kujikanyaga kwenye serikali ya JK.

Wakakosa hela ya kunilipa ikabidi waniachie vitu vyao ikiwemo tv, ni kama tuzo, kwenye ushindi wa super star, nani auze tuzo?

Njaa tu hizi kuziendekeza,

Jioni nikarudi nyumbani huku nikiwa na hamu ile tarehe ya wito iwe hata kesho, wakati sijaingia hata ndani wale jamaa waliokuwa wanataka TV nilioonana nao pale kwa fundi japo sikufahamiana nao, wakatia timu wakiwa na yule fundi.

Itaendelea............
Nzuri
 
Jack Daniel nimerud kusoma hapa tena yangu 2023 Ila nilicho notice hakuna mtu anayekuwa karibu yako kama huna kitu iwe muda pesa, ushauri, kuamini wewe ni sehemu salama la kukimbilia, n.k

Hii ya urafiki sijui mwanangu sana hamna kitu we are mutualism if not parasitism or symbolism
 
Jack Daniel nimerud kusoma hapa tena yangu 2023 Ila nilicho notice hakuna mtu anayekuwa karibu yako kama huna kitu iwe muda pesa, ushauri, kuamini wewe ni sehemu salama la kukimbilia, n.k

Hii ya urafiki sijui mwanangu sana hamna kitu we are mutualism if not parasitism or symbolism
16D96B09-269B-4B1E-B0F3-EEF2FB41B35C.jpeg
 
Hata ndugu wa exclude kabisa! Tena marafiki wana unafuu watakuvumilia bila manung’uniko!
Upo sahihi

Ingawa kwangu mpk sasa ndugu are the best ni kama marafiki aaani, hatuweki zile hisia za kindugu ety kwamba ndugu hakosei sjui nn kila kitu ni mipaka aseeh japo binadamu kubadilika ni any time
 
Upo sahihi

Ingawa kwangu mpk sasa ndugu are the best ni kama marafiki aaani, hatuweki zile hisia za kindugu ety kwamba ndugu hakosei sjui nn kila kitu ni mipaka aseeh japo binadamu kubadilika ni any time
Bado unakuwa, ila bora uendelee kuona hivyo itakupa amani zaidi.
 
Baada ya wale jamaa kutia timu nyumbani kwangu,kijihasira kikaanza kuninyemelea,kwakuwa nilishajua lengo lao.

Hivi huyu fundi ni mtu wa aina gani,mtu gani asiyeelewa? Ndiyo,?! Lazima mtu akikataa Chake ujue kakataa kuendelea kubembeleza inakuwa kero itakayosababisha ukahisiwa vingine. niliwaza sana.

Kaka,kamkubwa samahani bwana kwa usumbufu,tumerudi tena.aliongea yule fundi huku akijichekesha chekesha.

Kwani wanataka nini hawa?
Kuna usalama kweli hapa mume wangu? Nikamjibu,

Hakuna shida ngoja tuwasikilize,

Oy, bro eeh unajua nini babu mwanaume ukiamua kunyoosha jambo lako fanya kweli, wee umemwambia mwanetu kuwa una chombo unataka kusukuma,mkakubaliana ile fresh yaani, Sasa tumesikia unarusha yaani ile sitaki nataka,

Mchizi hapa alikuambia anatembea kilomita miatano au vipi,wee ukaona ni karibu,ni vyema ukafu....ukafunguka unataka kilomita ngapi ziongezeke,usikae kinyonge tiririka mwamba.

Aliongea kijana mmoja ambaye, haya majani mabaya yanayokatazwa na serikali,ni kama yanalimwa nyumbani kwake.

Kwa kifupi nilishakasirika,

Sikia wewe fundi,kuzoeana na wewe isiwe sababu ya wewe kuja kila unapojisikia hapa nyumbani kwangu,halafu unaleta watu design tofauti tofauti Mimi siwajui, heshima na Imani ninakupa wewe ndiyo maana huwa unafika kwangu Kila unapohitajika,kwahiyo nakuomba uondoke hapa hakuna biashara Mimi na wewe,

Halafu hivi,mbona hujiheshimu huyooooo mpaka uwanjani kwa watu kwahiyo hi fence kutomalizika ndiyo kigezo Cha nyinyi kujikuta mnaweza kufika muda wowote ule .nilibwata.

Baada ya kuona hapa maelewano hakuna wakaondoka bila kuaga wale wengine huku huyu fundi,akiniomba msamaha ambapo kwa muda huu sikuwa nakamatika,Kila mtu akawa ananiogopa,ikabidi yule fundi naye aondoke maana hali ya hewa ilishakuwa mbaya.

Twende ndani mume wangu,aliongea mke wangu Huku akiwa akinitazama kwa woga,maana tangu anijue sijawahi kuwa wa moto hivyo mbele yake,akawa ananiangalia sana , nikamwita kwa ishara ya kufumba na kufumbua kiganja, taratibu akaja mpaka pale kwenye kiti nilipokaa.

Usiogope mke wangu ni lazima kuweka mipaka,kwa baadhi ya watu ili kulinda heshima na hadhi yetu ,si Kila mtu lazima kuzoeana naye,

Au nimekosea mke wangu,?

Siwezi sema umekosea, au umepatia kwakuwa sijui chanzo Cha ugomvi wenu mume wangu.ni vyema ukanieleza Nini kilitokea.....

Nikamueleza Kila kitu tangu mwanzo mpaka nawapiga mkwara siku hiyo.

Lakini mume wangu,wewe uliwatamanisha sana, kwamba unauza Mali yako wakawa na Imani kuwa muda si mrefu watapata bidhaa,kifupi umewachanganya ndiyo maana wakafika hapa,

Ila kiukweli sijapenda,stahili waliyokuja nayo Mimi nikajua unadaiwa ,maana maisha tunayoishi tunayajua wenyewe.

Alisisitiza.

Mke wanguuuuu,yaani hata Kama nadaiwaaaa,ndiyo nidaiwe na wale wavuta bangi ,

Haaaaaa Dani my husband usiseme hivyo,hapa unajiona una maisha magumu lakini unaweza kushuka zaidi ya hapa ukajikuta wale ndiyo kampani yako.

Ila ni kweli mke wangu, tuachane na hizo stori naona kama unanitisha.niliongeza.

Siyo tuachane na hii stori,kwanza kwanini ulitaka kuiuza hii TV bila kushauriana ma mimi,najua Mimi hapa kwako Sina nachomiliki.mwenzangu ulisoma kwa kiasi fulani Mimi sikusoma.

Uliuza pikipiki bila kunitaarifu au kushauriana na Mimi,nilisikitika moyoni lakini sikuwa na namna ni vitu vyako kwanini nihoji,

Umeuza vitu vidogo vidogo vingi tu,sikuulizi,siyo kwamba siwezi Bali naepusha maneno madogo madogo

Najivunia kuwa na wewe mume wangu,Kila unachokileta ama kukitafuta huwa nafurahi na kukuombea uzidi kupata zaidi huku nikiringa na kutamba kuwa na mume Bora,ulinioa miaka nane nikiwa kwenye uyatima wa kukosa wazazi wote wawili,lakini baada ya kuolewa na wewe nikajikuta, nimepata mfariji,mlezi,baba wa watoto wangu na la mwisho nimepata mume mwema,

Leo hii,unauza vitu vidogo sana bila kuniambia,unadhani utaniambia kwenye mambo makubwa!

Una Mashamba lakini una hii nyumba
Na siku zote najivunia kuwa na wewe ni mpambanaji,naamini Sina Cha kukulipa zaidi ya kukuzalia watoto.

Najua kuwa hata hiki kiumbe kingine kilichoko tumboni mume wangu hujapenda lakini nikwambie tu kuwa najua ni wajibu wangu,kukuzawadia watoto ili ukuze jina lako mume wangu.

Mmmmmmmh mume wangu ipo siku utauza hii nyumba,Tena baada ya kuwa ushaanza udalali baada yakuwa huna kazi,na sifa za madalali nazijua wakikosa vya kuuza, huuza hata vitu vyao,

Hamna mke wangu, kamwe siwezi kuuza nyumba,.niliropoka,

Na nikiuza,au ukisikia tu tetesi za kuuza nipeleke mahakamani.

Nani akupeleke mahakamani,Daniel Mimi Sina huo muda,wa kugombania Mali sizizo kuwa zangu,we ukiuza utakuwa umeuza Mali zako.aliongea huku akilengwa na machozi,nilimuhurumia nikamkumbatia,muda huo hata sikuwa na Cha kumwambia zaidi ya kuona aibu tu,tulikumbatiana kitambo mpaka tuliposhituliwa na sauti ya dada wa kazi,

Akiita DADAA,!!!!!!.....

Itaendelea.........

Usichoke huu ni utangulizi tu mambo mazuri yanakuja.
Nimecheka kama mazuri,Kuna jirani Yangu,nilipopitia kama HAya,yeye akaona fursa nimuuzie nyumba
 
Nipo
Vyema ila nachosema ni kuwa mpk nilipo ndg zangu are the best..... Na tuna mfuko wa familia, ambao ndiyo unaotumika kusolve ishu za nyumbani muhimu, na kwetu muhimu tuu.

kwa mengi hasa niliyopitia walisimama nami bila kuchoka marafiki siku moja napost status sjui kitu gani ndo mtu anauliza upo

Kingn sipendlei kukimbilia marafiki hasa nikiwa na shda na wa face bros en sis kwanza tuone!! Na ndivyo tulivyo jizoesha home kwetu aseeh....

We come from different home, different màlezi na makuzi so hivyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom