Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

mkuu uwa sijawah comment chochote lakini awamu hii kuna kitu umenigusa umenikumbusha kitu kilichonikuta kati yangu na shemeji yangu ambaye tulidumu kwa miaka 12, ambaye nilikuwa natoka na dada yake huku mahusiano yetu yakiwafanya ndugu hao kuwa chui na paka mpaka sasa. Ni story ndefu.
 
mkuu uwa sijawah comment chochote lakini awamu hii kuna kitu umenigusa umenikumbusha kitu kilichonikuta kati yangu na shemeji yangu ambaye tulidumu kwa miaka 12, ambaye nilikuwa natoka na dada yake huku mahusiano yetu yakiwafanya ndugu hao kuwa chui na paka mpaka sasa. Ni story ndefu.
Fungua uzi
 
sio anataka bali anatakiwa kugongwa hata kwa kubakwa kabisa ili atunze siri.
 
Asee Dunia Iko kadi sana Yani mara hii broth kasahau ukimwi wa ESTA
 
SEHEMU INAYOFUATA............

Maisha yaliendelea huku Kila kitu kikienda sawa kadri kilivyooangwa , nakumbuka weekend moja kama kawaida yangu ilikuwa lazima nimpigie Rose japokuwa kwa Siri ili nisije kuharibu kwa mke wangu.

Dah kwa leo nisingependa kutumia kilevi Mr kwa kweli siku ile nilipata shida sana, aliongea Rose akionesha uoga fulani.

Hapana vipo vinywaji laini mbona ? Lakini yote kwa yote kama wewe hutumii kilevi hata Mimi siwezi kutumia kwanza siyo lazima. Nilimjibu huku nikifurahi maana nimejipunguzia gharama lakini hata hivyo kulewa Kila Mara si dalili nzuri.

Enheee nipe michakato ya maisha, life linaendaje , aliuliza huku akiwa ananitazama usoni, kitu pekee ambacho niligundua toka kwa Rose ni kwamba yupo tofauti sana na wanawake wengine baadhi, yaani anajiamini sana, kumbuka siku ile ilikuwa pekee ya kuweza kumwambia ukweli kutoka moyoni mwangu Sasa nikaona kama mzani umeinama yaani anataka kunishinda.

Hivi Mr Daniel una Elimu ya level gani, samahani lakini, akionesha shauku ya kutaka kujua,

Bila samahani unapaswa kujua tu kiufupi Mimi nina Degree ya uhandisi,,huku nikimpa analyse ya shule mpaka vyuo nilivyosoma .

Safi sana Mr, vipi kuhusu kazi umeanza lini kufanya kazi pale kwenye ile kampuni ? aliuliza .

Pale hata mwaka bado sijamaliza ila nimetokea sehemu tofauti tofauti kama unavyojua kupata kazi kwenye nchi hii kunahitaji marefa, au labda uwe na mtu maarufu au mtu mzito , kwahiyo nilianza chini kabisa kwani kabla sijaanza kufanya kazi inayohusu taaluma yangu, Ila nashukuru MUNGU maisha yanaendelea. Nilimjibu

Samahani lakini, unadhani umeshatimiza ndoto zako kulingana na taaluma yako? Alizidisha maswali

Hapana , kwanza niwe muwazi hakuna anayeridhika na kipato Chake hata iweje Leo utaona mshahara ni mdogo, utapata kazi yenye mshahara fulani wa kuridhisha lakini bado utakuwa kwenye kundi la wanaolaumu kuwa bado maslahi madogo, kwakuwa Kila kiwango Cha pesa kinavyoongezeka na matumizi huongezeka. nilijibu huku nikiwa nishachoka na maswali yake

Yote kwa yote nini kinapelekea uwe unaajiriwa kwenye Private sector, maana kwenye mlolongo wa sehemu ambazo uliwahi kufanya kazi kote ni sekta binafsi, na Elimu yako inaonesha unaweza ukawa kwenye chain ya wanaofanya Kazi serikalini. aliongeza huku nikishindwa kujua kwanini anapenda sana maswali.

Kama nilivyokueleza tangu mwanzo labda sijapata watu wakuniunganisha huko, nilijibu kwa mkato.

Je, una mpango gani kupitia Elimu yako kubuni kitu ambacho kitakuwa Cha tofauti huku kikileta matokeo chanya kwenye jamii ? She's asked

Kwanza sijawahi kufikiria jambo hilo lakini pia nashukuru ni kama nimepata mwanga fulani , nikipata muda nitalifanyia kazi suala hili.

Hahaha (akicheka) tatizo bado unaamini kwenye kuajiriwa ila bado una nafasi ya kufanya chochote maana unaonekana bado kijana kama Mimi, aliongea akafanya tukacheka kwa pamoja.

Kiukweli nafurahi sana kuongea na wewe umefanya hisia zangu kuwa kwenye level za juu kabisa, Rose we ni mwanamke ambaye tayari unanikosesha amani ya moyo, hasa Kila tukikutana kama hivi nafikiri ni MUNGU tu alituunganisha , Napenda sana mwanamke bright kama wewe nashukuru kadri tunavyokutana nanoti kitu kwako , yote kwa yote Sina lolote zaidi ya kusema NAKUPENDA, nakupenda sana Rose. Niliongea kwa kumaanisha huku nikikaza uso kumtizama.

Halafu wanaume mlio kwenye ndoa sijui mpoje? Hivi Mr Mimi na wewe hatuwezi kuwa marafiki bila kuwa wapenzi, aliongea huku aiinama chini na kunifanya nizidishe mashambulizi .

Najivunia kuwa na wewe Rose najihisi mwenyewe faraja ya moyo ninapokuwa na wewe , nafurahi nikikutaja kwa jina lako, hata kama hupendi kuitwa kwa jina lako lakini nitakuita kwa jina lako ili walau kuulisha au kupoza kiu ya moyo wangu.

Mr Daniel bwana , moyo huohuo unampenda mkeo , unawezaje kupenda watu wengine? aliongea huku safari hii akibonyezabonyeza simu ambayo niligundua ilishazima chaji kabisa, hivyo alikuwa anazuga zuga tu.

Moyo ni kama taa inayowaka ndani ya sebule yako , haijalishi mtu awe mwema, muovu au jambazi , taa itamumulikia Kila mmoja kusudi atimize hitaji lake, kwahiyo huo moyo wako ni wa namna Gani? aliuliza

Kwa jinsi ulivyotoa mfano wako , unahisi Mimi ni mtu muovu au mwema? Niliuliza.

Hakujibu zaidi ya kucheka tu,.

Nikaendelea , mfano uliotoa ni mzuri ila jua moyo huongozwa na ubongo au akili timamu za kiumbehai hasa kwa sisi binadamu, hivyo ni vyema nikajua jibu langu mapema. niliongea safari hii nikionesha liwalo na liwe.

Ila Mr Daniel samahani nimeshindwa kuja na gari yangu maana niliiacha vizuri tu Jana Cha ajabu napiga start asubuhi imegoma kuwaka hivi tatizo linaweza kuwa ni Nini? aliuliza huku nikitambua ananitoa kwenye maada

Kwani inafanyaje au betri ipo down, niliuliza

Hapana nimejaribu Hadi betri ya gari la baba haijakubali kwenye gari langu wakati kwake linawasha na la kwangu kwake linawasha pia yaani hata sijui tatizo ni nini maskini sijui jumatatu itakuwaje na Sasa hivi nilivyochacha alijisemea.

Ndugu msomaji, ukisikia yaani striker yupo yeye na goli ndiyo siku ile.

Ningekuwa karibu ningeicheki , nilisema huku nikisubiri atajibu nini.

Hamna shida tunaweza kwenda kuliona maana nikiwaza jumatatu bila gari naendaje kazini napata shida sana, tulitafuta bajaji , huku nikijitahidi nisije kuonekana na mtu anayenifahamu kuna vitu mtu hupaswi kuonekana.

Naam, tulifika kwenye geti la nyumba yao akafungua geti, karibu mwaya hapa hatuna hata mlinzi ujue

Hofu yangu ilikuwa namna nitatambulishwaje kwa wazazi wake nakua Haina tabu lakini bado ilinipa ukakasi

Karibu ndani mgeni, huku akiitwa kijana wa kiume ambaye nilimkuta
Akiwa anatupatupa ngumi mithili ya wacheza boxer akiwa kwenye singilendi Cha ajabu anaonekana ni mwenye heshima sana,

Tunaomba tuangalizie juisi kwenye friji, kijana akaleta huku nikijikaza maana sikupenda kuwa maeneo yale hasa Mimi mwenye heshima zangu.

Uliniambia unakaa na wazazi wako vipi wako wapi. niliuliza

Ah samahani sikukwambia, wazazi wamesafiri wameenda Morogoro watarudi jumatatu,hata hivyo usingekuja hapa si unajua tena. Aliongea huku akicheka cheka.

Nillikunywa ile juisi kama maji Kisha nikatoka nje kuelekea kwenye gari ya Rose. akaja mpaka pale nilipo .

Kama unavyoona hili ndo gari huku nikimsaidia kufungua Bonet,nilitumia njia ya kienyeji kwa kugusisha chanya na hasi huku betri ikionesha Ina moto wa kutosha,hii si njia nzuri lakini

Hebu piga starter kwanza, nilitoa maelekezo.akawasha.
Gari ilionesha starter haina shida maana inapiga kelele ila pump haipokei,nikaomba spana ili nivagae ile kazi huku nikihofia kama haitaleta matokeo nipo mbioni kuaibika.

Nikafungua valve zote nne kwenye pump ya gari baada ya kugundua Kuna moja ni kavu hata ukipiga free pump haileti kabisa mafuta , nilifungua huku nikikuta kiraba fulani kimelika huku kikiziba kabisa njia ya kupitisha mafuta, nikamuonesha zile raba zilizolika huku nikimuuliza kuwa aliwahi kubadilisha pump maana inaonekana siyo yake , akajibu ndiyo ni mwezi uliopita alibadilisha .

Tukaangalia kwenye toolbox yake nikavikuta viraba vingi vipya vikiwa kwenye special nylon. Nikaweka na Nikafunga vile vipya

Licha ya uwepo wake lakini hakujua kinachoendelea, nikazidisha utundu kwa kufungua plugs zote na kusafisha, huku zikiwa mbwembwe tu tatizo Wala halikuwa kubwa.ili anione wa maana

Nikafunga Kila kitu, nikwambia awashe , gari hiyoo ikawaka , tulibaki tunatizamana tu huku Kila mmoja akitabasamu , hakuna aliyesema neno alitamani anikumbatie lakini akaishia kuziba USO kwa viganja vyake, niliziona movements zake alionesha kufurahi sana, tuliingia kwenye gari huku akiwa akizima na kuwasha sijui alijua tatizo litakirudia .

Akaanza kutest kwa kulitoa nje ya geti lao , majaribio ya gari la Rose yaliishia kwenye lodge moja matata, huku akiniuliza ,

Sasa huku tumekuja kufanya Nini Tena , aliuliza kwa mshangao ila nilimuamrisha apaki gari huku nikiangalia ni saa kumi kamili hata adhana iliashiria hivyo,

Nikamshika mkono tukaingia mpaka lodge tukipokelewa na mdada fulani, nikaulizia chumba , nikalipa huku akiwa kama hataki fulani hivi hata wale wahudumu waliokuwa reception walishangaa kuona ni kama watu ambao hatukuwa tumekubaliana .

Rose aliwagundua mawazo yao, kwa kuniondolea aibu akanipiga busu moja takatifu mdomoni hata sikutarajia, Kisha akatangulia mwenyewe kwenye chumba tulichoelekezwa huku akiwakata ngebe wale waliodhani labda nalazimisha mapenzi.

Rose akiwa na kaaibu fulani, huku nikigundua wote tulikutana tukiwa tumekaa muda mrefu, yaani mithili ya mchezaji ambaye kasugua benchi muda mrefu Sasa anamshawishi kocha ili awe anamuweka first eleven.

Kiufupi Rose aliupiga mwingi sana , ni fundi sana wa mipira ya pembeni, iwe kushoto au kulia halafu na dimba la Kati ndiyo kabisa anakuja juu juu huku anakukaba ukienda kwa pupa ana chenga zake za kufinya. Jamani acheni tu.magoli ya mapema sana yalipatikana kwa Kila mmoja , huku timu zikishambuliana kwa zamu mechi iliisha kwa sare ya bao tatu kwa tatu huku wachezaji tukilowa tapatapa kwenye ile derby isiyo rasmi.

Rose alikuwa daktari haswa tena anatibu maeneo mengi sana,hakuwa tu daktari wa kusomea chuoni Bali alikuwa na kipaji .

Saa mbili kasoro, tulitoka huku , jina la Mr Daniel likifa mithili ya puto lililogusa kitu chenye ncha Kali.

Na Mimi ningemwitaje Rose Sasa?

Majina wanayoitana vijana ndiyo yaliyotawala. Tukatoka huku tumekumbatiana , tukiwa wapenzi rasmi, kufika pale mapokezi uso kwa uso na ESTA akiwa na mdada mmoja ambaye anaonekana anafahamiana naye wakiwa wanakabidhiana mawigi fulani na nywele bandia pale mapokezi.

ESTA ni mtu mzima Kila kitu alikijua , akavunga kiasi Cha Rose kutojua chochote, tulitoka huku nikigeuka nyuma nikamuona ESTA akitabasamu kwa muhaho.

Nilijiona nishaharibu , nikajisemea huyu lazima atarudisha uhusiano kwa mke wangu ili amsimulie Sasa dawa yake ni kumuwahi lazima nilale , Kesho jumapili nitahakikisha namgonga huyu, kinyume na hapo ataenda kusema kwa mke wangu.

Nini kitajiri usikose sehemu ijayo
burudika.

Itaendelea......
Esta nae anaenda chezea rungu
 
SEHEMU INAYOFUATA...............

Mimi na Rose ambaye ni sweet mpya, sijui honey mnaita, tuliingia kwenye gari lake huku tukiwa tunatazamana kwa kuibiana Kila mmoja akitabasamu.

Rose hakuongea lolote zaidi ya kuwa makini na usukani wake tu.

Sasa naomba uniache hapo mbele maana nataka uniache huku nyuma kabisa nichukue taxi inipeleke nyumbani. Nilimwambia Rose.

Huku nikitoa kiasi fulani Cha pesa na kumkabidhi kabla sijashuka kwenye gari ,

Sasa hii ni yanini my, aliuliza.

Chukua tu ni wajibu wangu kukupa Wala usihofu. nilimwambia.

Sikia my Mimi na wewe tumekubaliana tumeridhishana, naamini Kila mtu kaenjoy na kuburudika kwa namna yake, Sasa kunipa pesa, hii Ina maana nimekuuzia si ndiyo? aliongea akionesha mshangao.

Sikia mpenzi wangu, hujaniuzia Wala hukuniomba pesa , hii ni kawaida tu mbona? tena ni kiasi kidogo sana hicho nikiwa sawa mbona utafurahi asali wangu? niliongea kwa tambo kana kwamba nina hela kihivyo.

Sawa ila kwa Leo nipe nusu ya hii hela , nyingine we chukua tu, lakini pia nikwambie jambo moja , sipendi kuisambaratisha familia yako, sipendi uje uitelekeze familia yako kisa Mimi hapana, kama huna pesa usijikakamue kutaka kuniridhisha Mimi kwa kuipunja familia yako, samahani sitapendezwa na hilo. aliongea kwa kumaanisha huku nikimshangaa ni mwanamke wa aina gani huyu, akaendelea...

Nina kazi yangu, pia Nina duka langu la madawa muhimu nashukuru MUNGU nipo kwenye hatua nzuri hivyo hata hii pesa yako nimechukua tu ili usijisikie vibaya. alimalizia

Nilimwangalia jinsi nywele zake zilivyotimka na kukaa vibaya kutokana na ile mechi nilibaki kutabasamu tu. Tukaagana akaondoka huku akikamata barabara ya nyumbani kwake , hakika nilifurahi sana jambo lililonipa taabu na kuninyima amani ni ESTA.
Maana kaniona huyu na hizi taarifa nikifanya uzembe mke wangu zitamfikia, ila nitajua Cha kufanya, au nimfuate kesho ESTA nikamtishie kuwa najua uliona kitu Sasa ole wako nije kusikia, najua hapa nitazua msala maana ESTA ni jeuri .

Na hasa hiki kipindi na yeye anashika visenti basi hatonjelewa, au nikamtongoze, je atanikubalia haraka wakati katoka kuniona na mtu mwingine, ila ngoja nitakua Cha kufanya mwanaume haishiwi mbinu.

Nikatafuta daladala ili kubalance pesa nilimwambia Rose nitapanda taxi ili asinidharau ila ni kwamba usafiri wangu mkubwa ni DALADALA

Nilifika home mishale yaa saa nne kasoro usiku nikamkuta mke wangu anaangalia TV huku akiwa kawaida tu, mke wangu nayemjua hakuniuliza Wala hakuongea tulisalimiana huku nikimchumu chum mwanangu ambaye mpaka muda huu alikuwa macho.

Jamani huyu kamanda vipi mpaka muda huu hajalala, niliuliza

Kaamka siyo muda mrefu kalialia hapa nikawa nambembeleza, vipi Kuna usalama unakotoka . Aliuliza mke wangu

Salama tu , vipi mbona unauliza hivyo, Kuna tatizo? niliuliza huku nikiwa namsoma mke wangu yupo kwenye hali gani.

Ulinitisha ndiyo maana, wewe tangu umeondoka saa tatu asubuhi unarudi muda huu hata siku za kazi haiwahi hivyo mume wangu,. Ila kuwa makini sana na taarifa iliyopo ni kwamba dada yako ambaye aliaga kuwa anaenda nyumbani inaonekana hajafika na namba zake hazipatikani.
Kumbuka tulishauri tumsindikize stendi aligoma na vipi simu nyumbani ulipiga lini. aliuliza mke wangu

Nina muda mrefu sijawasiliana nao, (huku nikichukua simu nijaribu kuwatafuta wazazi wangu )

Sasa unataka kumpigia nani usiku huu, wewe lala tu utawasiliana nao kesho bwanaaaa, alishauri mke wangu

Halafu wewe sijui upoje yaani unaambiwa mtu kapotea, na simu yake haipatikani , bado unashauri nispige simu,? (Niliongea huku nikijaribu namba za baba na mama kuulizia taarifa nazozisikia Ila zote hazikupatikana, nikajua kijijini masuala ya network mtihani Mara nyingi huwa mpaka wakutafute wao

Hahaha (akicheka)nicheke mie maana wakati mwingine unasikia jambo unawaza Kisha unaamua kukaa kimya tu. aliongea mke wangu Huku nikigundua kuwa Kuna ukweli anaujua.

Sasa mke wanguuu kuliko kuzungushaaaaana kama Kuna taarifa unayojua di uniambie tu unaficha nini? nilimwambia

Wewe baba Mimi sijui kitu nachofahamu wazazi wako wamenipigia simu kuwa Binti yao hajafika wakati hapa ana wiki nzima tangu aondoke na wewe hukupatikana kwenye simu zako zote , wazazi walijua labda wifi bado yupo hapa , tena sijui malaika gani alisema hebu mpigie simu mama mkwe umsalimie ,

Hapo ndipo alipotaka nimpe Binti yake aongee naye, nikamwambia mbona hapa kaondoka Leo siku ya Saba, na nikajua labda mume wangu ulipiga simu kuhakikisha Dada yako/mdogo wako kafika nyumbani kumbe haikuwa hivyo masikini. aliongea kwa kujiamini sana .

Sasa mke wangu mbona unacheka,
Huwezi kusikia taarifa mbaya kama hii halafu badala ya kuhuzunika wewe unacheka , kama kavamiwa na majambazi je, yaani huna hata huruma?niliuliza kimtego

Heheheee usinivunje mbavu yaani majambazi gani kama ingekuwa hivyo Mimi nishakufa siku nyingi au hata wewe hao majambazi wameshakuua kitambo , nikalale mie nisije kuonekana mwanga kukesha mpaka usiku wa manane. aliongea mke wangu Huku akiinuka na kuingia kwenye chumba Chake anacholala na mtoto.

Aliniacha njiapanda sana nikaona Kuna kitu anakijua, mbona anachekacheka kwenye hii taarifa ambayo watu huko watakuwa roho juu, Tena naiona lawama kubwa sana toka kwa wazazi wangu sijui hata nitawaambia nini. nilijisemea huku nikirudia kupiga simu bila mafanikio.

Kesho alfajiri nilipokea simu toka kwa mzee wangu yaani baba yangu akishindwa hata kusalimia , huku akiniangushia lawama mfululizo.

Mwanangu nilikuwa nakutegemea na kukuamini hasa kwakuwa ni mtoto wangu pekee wa kiume haiba mwonekano wako ulitosha kukuamini na kujivunia kuwa kweli nilipata mtoto wa kiume , Sasa ni ulimbukeni gani unakufanya uwe kama mtu mgeni wa jiji , maana nasikia siku hizi hushindi kabisa nyumbani,

Kibaya zaidi dada yako naye yupo maeneo hayo hayo kafungiwa ndani na mwanaume yaani mnatuabisha sana wazazi wenu, mnadhani jamii inatutafsiri vipi juu ya malezi tuliyowapatia?

Mmetia aibu sana wanangu, hasa wewe ambaye mpaka mama yako anamuacha huko dada yako ni kwamba alikuamini sana wewe, lakini sitaki kukwambia Leo hii mama yako anakuchukuliaje, Sina mengi naomba fanya mpango tuletee Binti yetu, unadhani kama si mkeo kutupa hii taarifa tungejuaje aliongea baba kwa uchungu huku akikata simu .

Kwanza hasira zilinishika haswa, nikaingia chumbani kwa mke wangu, nimuulize kwanini kagundua dada yangu yupo kwa bwana akashindwa kuniambia Mimi kwanza , akaona aniaibishe kwa wazazi, haoni kuwa kawapa Presha huko nikataka nimnase vibao .

Wee weeee thubutu uone, nipige , nasema nipige ulitaka nikwambie saa ngapi, Mimi nimeletewa taarifa na wasamaria wema nikasema mume wangu atarudi nijue tunalijadili vipi hili suala, lakini Kila nikisubiri mtu hurudi ulitaka nisemeje, mi nikasema pengine hizi ndiyo tabia zao , dada yupo huku kaingilia huku kwa raha zenu wenyewe, aliongea kwa kichambo fulani.

Nilijikuta Kofi limenitoka huku nikiwahi kumzuia asiangukie kitandani alipolala mtoto.
Ujue wewe ume kuwa jeuri sana wewe kwanini huchagui majibu ya kumwambia mumeo , nilimuacha akilia huku nikimfuata dada wa kazi aliyekuwa akifagia nje,

Wewe naomba kujua , dada yangu alipo maana nachojua unafahamu, hebu niambie, ukweli Mimi sijui alipo ila Kuna gari fulani huwa inakuja hapa, nafikiri yupo na yule mtu, alijibu kwa uoga
Kila nikijikumbusha ile gari ilikuwa ngeni kwangu nikaona kwanini nihangaike siyo muda nitapata tu ukweli.

Nikaingia chumbani huku nikitafakari kauli aliyoitoa mke wangu, ni kweli Jana nilikuwa na Rose na dada yangu yupo kwa bwana, niliumia sana huku nikishikwa na hasira sana, nilichukua buti zangu fulani huwa sivai sana nakumbuka nikinunua kwenye mtumba maeneo ya mjini huku marafiki zangu wakinicheka kwamba ni Cha gharama sana, lakini pia nimekipendea Nini,

Lakini siku ile kilinifaa nikavaa suruali ambayo nitakuwa huru nikafunga mkanda kiunoni nikavaa viatu ambavyo havikufuliwa nikatoka nje, mke wangu akaja, baada ya kuniona natoka kuelekea asipopajua, hisia zangu ilikuwa nyumba fulani mbili tu nikijua mojawapo nitampata dada yangu.

Nikifikiria maneno ya mke wangu, nikifikiria maneno ya wazazi wangu nilibaki namuhurumia aliyemchukua dada yangu, ama kweli

Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Mume wangu unaenda wapi , umenipiga, umeniumiza, unajua wazi kuwa umenionea, najua unajua fika Sasa kwa hali nayokuona nayo najua unaenda kuharibu, nakusihi Daniel
Uliyonifanyia Mimi yanayotosha siyo kwamba najipendekeza kwako Bali nawaza ukiharibu familia yangu itaishije, Mimi ni mwanamke, ni rahisi tu kuachana na wewe na nikaolewa sehemu nyingine.

Vipi kuhusu watoto wetu, wanaokua bado vipi kuhusu hatima yako? Daniel (akiniita kwa jina kabisa)kuwa makini sana Dunia hadaa ulimwengu shujaa . alimalizia.

Kwanza nambie dada yangu yupo nyumba gani, sihitaji ushauri wako mwingine . Niliuliza

Wakati tunabishana kuhusu haya , dada wa kazi alikuja na karatasi fulani
Fulani alidai aliagizwa na jamaa mmoja ili ampe dada yangu.

Nilichukua ile karatasi yenye namba za simu, huku nikizihifadhi kwenye simu kifupi nilishajua pa kuanzia

Nilipiga simu huku ikiwa haipokelewi Mara nyingi sana, nikaamua kurudi ndani huku amani ikiwa hamna kabisa mle ndani,

Baadaye ile namba ilinipigia ikiniuliza Mimi ni nani,

Naongea na nani nilitoka kidogo, maana naona umepiiiiiiga kama mtoto yatima nambie, aliongea mtu ambaye kwa uzoefu wangu pale mtaani sauti naijua ni bishoo Fulani ambaye ana studio uchwara ya kurecord mziki kule town.

Kwani wewe ni nani maana ni kama nimekosea namba, nilidanganya ili asinijue fasta.

Oyaa jombaa ushajua umekosea namba unataka unijue ili iweje, kausha basi, alijibu kijeuri yule Dogo anayemiliki Brevis na kujiona kayapatia maisha.

Sikutaka kupoteza muda kwakuwa nilikuwa nafahamu alipo nilitoka na kuanza kumsaka,

Nilichukua round kadhaa, nikamkuta Dogo ka chill na washikaji zake huku akiwa anaongea yeye tu wengine wakimsikiliza . Nilifika pale bila kusalimia nikamkwida kwa roba moja matata nikaanza kumuuliza maswali licha ya washikaji zake kutaka kuniletea noma lakini Hawakuthubutu mwili wangu na walivyo tofauti.

Oyaa washkaji huyu Ms**ge anatakaje mbona mnamwangalia tu, ataniumiza wanangu.

Dada yangu yuko wapi , we k**a
Leo nakuchinja Sina masikhara na wewe .

Alikubali huku tukiongozana Hadi kwake alikopanga huku akiwa kwenye himaya yangu, nilimkuta Dada yangu Hana hata habari anafua nguo za kile kijamaa, kichapo nilichowaangushia hawatokaa wasahau (japo kwa Sasa ni shemeji yangu maana walikuja kuoana kabisa)

Kesho jumatatu asubuhi ilinikuta stendi ya ubungo nikiwa nahakikisha dada yangu kapanda gari huku nikiwa Sina Imani maana angeweza kushuka njiani nikawaambia wahudumu wa lile basi kuwa wahakikishe anashuka stendi fulani maarufu iliyo wilayani kwetu. Licha ya yeye kukiri kuwa hatofanya ujinga wa kushuka njiani lakini sikumuamini.

Niliwahi kazini, huku simu ya madam ikiingia , sikujua anataka Nini asubuhi asubuhi nikapokea simu.
Tukasalimiana.

Naomba kuuliza tolu, nasikia Jana Kuna kijana wangu umempiga nakumuumiza, alikukosea Nini?, na kama alikuwa na makosa kwanini ujichukulie Sheria mkononi?

Maana Jana alinitumia namba ili nijue nani kaniumizia kijana wangu?
Nikashangaa namba imekuja ya kwako, sikuamini nikataka arudie kutuma labda kakosea lakini, bado alituma namba hii hii,ni kijana wangu nimeishi naye kwa kipindi kirefu nimemsomesha mwenyewe kuanzia advance level Hadi chuo.

Sasa naomba kujua mlikosana Nini, na una bahati nakujua , pengine ungeozea jela, nambie naweza kuwaita wote niwasuluhishe, japo utalipa maana gari yake Kuna vifaa vimeibiwa baada ya wewe kumlazimisha akupeleke kwake , huku nyuma gari yake watu wakaiharibu, kwanza mchana tukutane hospital ya (jina kapuni) alipolazwa.. akakata simu

Huu Sasa msala, jamani huyu Madam Bora nisingejuana naye mbona ni matatizo.nilijisemea

MIMI NA BOSS WANGU

Endelea mpaka mwisho.

Itaendelea.......
 
mkuu uwa sijawah comment chochote lakini awamu hii kuna kitu umenigusa umenikumbusha kitu kilichonikuta kati yangu na shemeji yangu ambaye tulidumu kwa miaka 12, ambaye nilikuwa natoka na dada yake huku mahusiano yetu yakiwafanya ndugu hao kuwa chui na paka mpaka sasa. Ni story ndefu.
Let Uzi mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom