Wewe ni taga au?Muwe mnakunywa supu kabla ya kusoma
Wewe ni taga au?Muwe mnakunywa supu kabla ya kusoma
Pamoja mkuu labda nimechanganya mamboCopy hiyo sehemu niliyosema hivyo iweke hapa
Inawezekana aisee, ile kujimwambafai kuwa yeye si mtu wa kutaka pesa kisa ana kazi yake ilikuwa kumuingiza jamaa king tu. Ili aweze kumpiga pakubwa, na mahesabu yake yalikuwa million.😄😄😄Mkuu inawezekana Rose alijilipa mapema baada ya kudokezewa na mdogo mtu.
Mademu achana nao kabisa yaani.
Hapo amefanya kosa kubwa sna ambalo si mabaharia lazima tumlaumu, na ndio sababu akaanza kumletea maringo.Kosa ulilofanya hujachakata mbususu ya ESTA hata kimasihara
Mkuu ninkweli unampata huyo jmaaaHuyu sande nampata
Mkuu toa connectionMoyo wa shukrani big up mkuu
Sijakuelewa badoMkuu toa connection
Si hapo tanroad boss😂😂😂😂😂Sijakuelewa bado
Ohooo takucheki buda I need your CVSi hapo tanroad boss
All in all wewe ni mtunzi mzuri mkuu. I salute
Ahsante mkuuUzi mzuri. Nimejifunza sana kiukweli kumbe jf kuna big writers. Sijui ni mtazamo au ni fact niliyoiderive... Ni kwamba I think your destiny lies with your family. Umerudisha upendo kwa familia ukaachana na "kelele" za nje I bet Mungu alikua anataka hivyo.
Wengi hawajui tu lakini wake wana nafasi kubwa sana katika.maendeleo. unapombariki na.kumsupport mke na ukampenda na kumuheshimu.kuna your heaven hapo. Weng hawajui hili wanajikuta mishe zinafeli ukija kuchunguza kuna nuksi aliichota somewhere.
Unless uwe mshirikina haswa sio.wa kubipu. Men should respect their families.ili Mungu abariki na alete maendeleo katika generation.
SEHEMU YA MWISHO......(FINAL)
Kwa wenye kuamini Dini na madhehebu yao, au hata wanaoamini sehemu wanazozijua, wote kwa pamoja tuweke IMANI kwa MUNGU mmoja maana yupo na anatenda.
Maisha yaliendelea, familia zilifurahi huku Kila kitu kikiwa kwenye mpango sahihi kabisa
Mume wangu, unajua kama tarehe 17 mwezi huu, ndiyo siku yako muhimu wewe kuripoti kazini?
(akimaanisha tarehe 17 ya mwezi wa kwanza mwaka 2013).
Usijali mke wangu, najua sana, najua hilo, ila bado wiki nzima ujue. nilimjibu.
Sawa, ningekuwa na uwezo ningekufungia ndani usitoke kabisa, maana najua huko kuzurura kwako unaweza kuyazua huko ukaja kukatisha ndoto zako, nimechoka masuala yasiyokuwa na maana.
alilalamika.
(Nikicheka)
Ajali haina kinga mke wangu, hata nikikaa hapahapa lolote linaweza kutokea bado nikakatisha ndoto zangu, kikubwa ni kumuomba MUNGU ili atufatufanyie wepesi na kunyoosha mapito yetu. Nilimjibu.
Amina, basi piga magoti nikuombee maana hiyo kazi ni ya muhimu kwangu kuliko hata wewe,. aliniomba nifanye hivyo.
Kwa kumridhisha kutokana na Imani yake niliweza kufanya hivyo ili tu nisilete mgongano Kati yetu.
Baada ya kumaliza yale maombi mafupi , nilimpigia Rose ili tukutane maana alikuwa ananyanyasa sana moyo wangu.
Ndugu msomaji, kazi niliyopata kwa sasa hakujua mtu yeyote zaidi ya mke wangu na Rose.
Rose anajua kwakuwa ni mmoja wa wahusika walionipigania kule, ila yeye hakuwa na Imani juu ya Mimi kufanya kazi pale, maana Mara nyingi alikuwa akiniuliza akitaka kuhakikisha, kama taratibu zimekamilika.
Na Mimi sikutaka kumwambia na kutapika yote, kuhusu ile kazi kwani, licha ya kuwa nilishakamilisha vitu vingi lakini bado niliamini kwa asilimia tisini tu, hivyo kumwambia mtu na kujimaliza Kisha mpango wako ukakwama, sijui utaeleza nini.
Lakini nilichogundua ni kwamba penzi letu na Rose, Lilianza kufifia yaani lile penzi moto moto sikuliona tena yote haya yalisababishwa na Mimi kutokuwa na uhakika na kazi.
Nakumbuka tulikutana kwenye mgahawa mmoja Mimi na yeye nikaagiza Chakula ili wakati maongezi yakiendelea tupate kuburudika naye.
Hivi my, kwanini unapenda kuharibu pesa hivyo, Mimi naona Bora hata uagize soft drinks tu inatosha, hakuna haja ya sisi kutumia gharama kubwa, alisema huku akimaanisha.
Nilimtazama nikimshangaa maana hawezi sema yale na hajawahi kusema jambo lile, hela hatoi mfukoni mwake kwanini zimuume?
Kwani baby Kuna tatizo, sioni kama ni vitu vya gharama kiasi hicho. niliuliza.
Ujue lazima tu nikwambie ukweli, Daniel (akinitaja kwa jina mithili ya shambaboy)
Wewe huna uhakika wa kazi, na kama ujuavyo hii ni January huwa Kuna ugumu fulani ambao unasumbua hivyo kuheshimu pesa ni suala muhimu sana,. aliweka kituo.
Kwanini unasema sina uhakika wa kazi, Ina maana huwa huniamini ninayokwambia? nishakwambia nimeambiwa niliripoti tarehe fulani, Cha ajabu nini my, au kama Kuna jambo unalijua nambie maana hata wakati naachishwa kazi kule, wewe na mdogo wako mlikuwa mnajua na msiniambie, Sasa basi hamna kuficha nambie Nini umekisikia. niliongea kiume huku nikikaza uso mtoto wa kike hawezi niletea dharau.
Akuuuh, sijasikia lolote toka kwa mtu yeyote, hata Yale ya tetesi za wewe kufukuzwa kazi, aliniambia mdogo wangu, ila zilisikika kama tetesi hatukuwa na uhakika Hadi pale ilipotokea kweli. kama nimekukwaza nisamehe, aliongea huku akiwa anavuta mkoba wake uliokuwa mezani na kuuweka mapajani ili kama ikitokea lolote iwe rahisi kuondoka.
Vyakula vililetwa muda mwingi sana nikaanza kula kwa kujilazimisha huku hasira nazo hazikuwa nyuma kutokana na demu anavyonichukulia poa.
Alipoona nakula naye akaanza kula nadhani alikuwa ananisindikiza tu ila hakuwa tayari kula na mimi,
Rose alibadilika sana.
Siyo Rose yule ambaye huwa haoni aibu kufanya chochote akiwa na Mimi, tulikuwa tukilishana mithili ya mapenzi ya under 23 age. alikuwa anafumua nywele zake Kisha ananiambia nimsuke basi kwakuwa siwezi tunajikuta tunafurahishana huku akinirudisha kwenye utoto,
Lodge zingekuwa zinaongea zina mengi zinashuhudia huku vyumba vikikosa ya kuongea kama samaki
Ndani ya maji.
Leo hii Rose hataki nimsogelee wala kumgusa, nikiuliza kwanini, anasema lazima tujiheshimu. Kweli hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho, lakini mbona huu mwisho kwangu umekuja mapema? nilijiuliza huku Chakula nacho kikipungua ladha sababu ya mawazo.
My tumekaa hapa, naona husemi umeniitia nini, maana nina haraka ujue sisi madaktari shughuli zetu huwa zina mabadiliko hivyo usishangae nikapigiwa simu muda wowote. aliongea huku akiwa busy na simu.
Nachojua Mimi na yeye tukiitana huwa hakuna sababu, yaani ukimwita njoo atakuja wala haulizi ulichomwitia, lakini Leo hii anataja niseme shida yangu! Ama kweli kanichoka.
Sina sababu maalum, ila furaha yangu nikukuona tu , we mwenyewe unatambua hilo. nilijibu huku nikimtazama kwa makini nikiusoma uso wake,.
Ahaaa ok, kama ni hivyo sawa, bila shaka umeshaniona, unaweza kuniruhusu niende? aliuliza
Mbona mapema hivyo my, kwanini tusikaekae kidogo, na tukitoka twende (nikitaja jina la lodge fulani)
Samahani yaani leo wala sijisikii vizuri sana, nashangaa mwenzangu mawazo hayo unayapata wapi, mwaka mpya umeingia huu, kule kwenye duka langu la dawa mkataba mpya wa kulipia lile eneo unatakiwa .
Hela zinazotakiwa pale, si haba pia hapa sijaja na gari kwasababu nimeliacha kwa fundi ili afanye marekebisho hela aliyonitajia ni MUNGU tu anajua yaani Sina msaada wowote ule, aliongea kwa kulalamika .
Akaendelea.....
Hivyo usione kama nakudharau ni kwamba navurugwa na vitu hivyo hapo. akaweka kituo.
Nilimwangalia Kisha nikacheka kidogo, maana mtu ambaye hakupendi ana Kila sababu ya kutaka muachane.huku nikijiuliza Kodi anayodaiwa huko dukani kwanini imsumbue, kwani duka au biashara yake haina faida, kusema huwa hapigi hesabu kuhusu TRA, Mtaji aliowekeza, faida zinazopatika, gharama za pango na makorokoro kibao kwani huwa hajui. Nilijiwazia moyoni.
Basi kwa maana hiyo , Mimi nimeridhika nashukuru kwa kutenga muda na nafasi ya kuonana na wewe, MUNGU akupe moyo huo huo. niliongea kimtego.
Usijali, nakupenda sana my, usinifikirie vibaya. alijibu shortcut huku akiondoka.
Si kawaida kuagana ndani ya mgahawa huwa ni lazima tusindikizane kidogo Kisha tunaachania mbele ila kwa siku hiyo ikawa tofauti.
Nilitoka nikichanja mbuga , huku moyo uliniuma kwani nilikuwa najua Rose anataka tuachane na Mimi sikuwa tayari kwani nilimpenda ile kumpenda sana, beautiful girl, English figure, na nywele nyingi Peruvian hair, ningemwachaje,
Achilia hayo kubwa zaidi ni Binti msomi, mwenye Elimu yake, mwenye kazi yake, nani anamrubuni my love Rose, mtu anayeongea kisomi huwa anapangilia maneno, kapata malezi Bora ya pande mbili, namuachaje jamaniiii.
Ni mshauri mzuri, ananiheshimu na kuiheshimu familia yangu. ana moyo wa huruma Kila unachomweleza huwa anakipokea na kutoa ushauri usioumiza, Sasa namwachaje Rose .
Ni Ms***e gani anataka kuniovertake achukue hii Mali. Aaaaaa weweee sitakubali.
Au ni masuala ya Kodi na gari lake yanamuumiza, ukute ni vitu hivyo kweli vitafanya nimkose Kisha akachukuliwa na mafioso wa hapa mjini.
Ngoja nitafanya kitu nauza shamba langu la huko kisemvule ili najua sikosi hela ndefu, nitahakikisha Rose hachomoki mikononi mwangu.
Ila shamba hapana, ekari kumi na kitu nauzaje kizembe? Ule ni urithi wa wanangu.
Au nikamsaundishe wife nimwambie nahitaji kama milioni moja Kuna jambo nakamilisha halafu, si nitarudisha ? halafu nimpe Rose naamini atalipa kupunguza matatizo yake. Kisha penzi litarudi upya .
Mmmh ila usawa huu kutoa jiwe moja uongo, wanawake huwa hawaridhiki hawa.
Nilijiuliza na kujijibu mwenyewe.
Nilifika nyumbani huku nikipokelewa na wife vikorokoro nilivyonunua na Mimi nikimpokea mtoto huku nikicheka cheka naye.
Mke wangu ujue siku zinavyosogea huyu mtoto anazidi kuchukua sura yangu, yaani huyu simuiti mwanangu Bali pacha wangu. sipati picha miaka hiyo tukikwaruzana Mimi na wewe , atavyokuja kunikoromea huku akinitisha.nilitania
Unapenda sana kusema mmefanana ila namuomba MUNGU mfanane sura siyo akili na maamuzi yako. Maana mume wangu kama ingekuwa siyo Elimu yako, napata picha ya maisha ambayo tungeishi. aliongea kwa kumaanisha.
Kila kitu hupangwa na MUNGU ukute ningekuwa Sina Elimu ningekuwa na good life zaidi , yaani circle of life ione hivyo hivyo mke wangu.nilijibu huku tukitaniana mambo mbalimbali, nilifurahi kwani ilinipunguzia machungu ya Rose.
Siku zilikimbia na kukatika huku tarehe husika ya Mimi kuripoti kazini ikifika, nakumbuka siku hiyo ya jumatatu nilifika kazini na kukabidhiwa ofisi yangu huku taratibu zingine zikiendelea kukamilika. hatimaye nikawa mfanyakazi rasmi wa taasisi yenye heshima nchini. Huku nikipewa na gari kwaajili ya kurahisisha mizunguko yangu maana kazi niliyopata huku neno kwenda mkoani lilikuwa ni jambo la kujiandaa kwani ni muda wowote na saa yeyote.
Penzi la kulazimisha Kati yangu Mimi lilirudi japo siyo kama zamani , maana penzi hili watu kukaa wiki nzima bila kutafutana ilikuwa kawaida tu.
Tuliachana vipi na Rose......
Nakumbuka Kuna siku moja , Rose Rose nilimpigia simu kuwa kesho ijumaa weekend inavyoingia tuonane, alikubali kuwa hakuna shida.
Kweli baada ya kesho kufika nilitegemea kuwa hii leo tutaonana ili tukamwagilie moyo, mimi na yeye, chaajabu Kuna muda kama saa kumi na moja alinipigia simu akidai tuahirishe tu lile zoezi, maana Kuna dharula mama yake anaumwa sana.
Nikamwambia kama ni hivyo basi nifike tu nije nimuone mama, alikataa kwa kusema si jambo jema , maana haitaleta picha nzuri.
(Na hili nililileta humu Kuna Uzi unasema hivi
"UJINGA NILIOWAHI KUUFANYA KULILIA PENZI LA MCHEPUKO "
Sasa endelea.....
Basi baada ya kunikatalia nisifike, niliamua kumrushia kiasi cha laki moja na nusu kama mwanaume uliyepokea taarifa ya ugonjwa lazima ujiongeze, alishukuru huku, Mimi Ahadi yangu ya kwenda viwanja ikiwa pale pale.
nilimchukua jamaa mmoja ambaye huwa tunaongoza sehemu nyingi tukachagua kiwanja kizuri tukaenda kufika pale, nilichokiona kilinishangaza sana kwani nilimuona Rose akiwa kimahaba na kijamaa fulani huku wakiwa kwenye mahaba mazito sana.
Aisee baada ya macho kugongana nilipata hasira sana, tena mno nikataka kuanzisha ugomvi lakini mchizi wangu alinisihi.
Dani braza, utaharibu ujue kwanza wewe una mke , vipi shemeji akija kusikia umeanzisha ugomvi sababu ya mchepuko utajidharaulisha bro acha, aliongea yule jamaa yangu huku akinishika mkono na kuondoka eneo lile.
Tulibadilisha kiwanja, huku tayari nikiwa nimevurugwa maana nilimpenda kupitiliza hivyo niliumia sana kwa aliyonifanyia.
Naam baada ya hapo hakuna aliyemtafuta mwenzake , na penzi likafika mwisho.
Nikarudisha UPENDO kwa familia yangu huku matukio ya mikosi kwa upande wangu yakipungua , nikizidi kupiga kazi huku wigo wa kujuana na watu wakubwa, wazito na kujua mambo mengi vikizidi kupanuka.
Kweli watu ni mtaji.
Hii ni tamati kwenye simulizi hii, nimeamua kushare na wanajamvi simulizi hii ili ,
Tuburudike na tujifunze mambo mbalimbali, kwa waliokata TAMAA wakae wakijua siku yao ipo kwani hakuna maisha magumu.
Bali Kuna mapito magumu.
Jack Daniel member wa jamiiforum.
SEHEMU INAYOFUATA,...................
Baada ya kutoka kukwazana na ESTA nilitulia huku msaada wangu pekee, au mtu aliyebaki ni Rose, licha ya kuwa alikuwa na umri wa mdogo sana kwangu, lakini bado alikuwa na busara za hali ya juu.
Hebu fikiria mchepuko kukupeleka hadi kwa wazazi wake si jambo jepesi mjue, niliendelea na michakato mingine huku kwa upande wa mahabusu yaani Shedy nilikuwa napokea simu na wale ndugu zake huku tukishauriana mambo tofauti tofauti.
Nakumbuka jumatatu Moja nilikuwa kwenye taasisi Moja ambayo baba yake Rose alinifanyia mpango, huku nikiwa nadhifu na mavazi safi, tofauti na kote nilikopita huku kulikuwa na watu wengi sana maarufu, wanasiasa wanaojulikana nchi nzima lakini , hata magari yaliyopark pale plate number za serikali ziliongoza.
Niliambiwa nikae sehemu nitulie, nisubiri wahusika waje, nakumbuka nilikaa kuanzia saa tatu asubuhi Hadi saa kumi huyo mlengwa hakutokea, nikaanza kuona utofauti Kati ya Sekta binafsi na serikalini, huku kulihitaji uvumilivu na subira haswa, baadaye muda ukikaribia kuisha alikuja mama fulani mtu mzima, sura haikuwa ngeni kwani namuonaga kwenye magazeti. hakika sehemu hii nilipaona pazito kila niliyemuona aliniona kama Sina hadhi ya kuongea na wewe.
How are you? alinisalimia kwa kimombo huku akiwa ananitazama usoni.
Nikaitikia salamu yake.
Unajua tangu saa tano nimekuona hapa kwani una shida gani kijana, au unataka kuchukua contract ya madaraja nini maana wengi wanachukua ili kufanya maboresho ya madaraja huko vijijini.
Akiongea kwa kejeli akitambua kabisa, sifanani na maboss wa aina hiyo.
Hapana boss Mimi hapa nimekuja kuwasilisha, maombi ya kazi hata hivyo Kuna mtu namsubiri hapa niliambiwa atakuja.nilimjibu.
Akawageukia wenzie huku wakicheka atakuwa anamsubiri (akitaja jina).
Huyo boss kaenda mkoani, na hii sikukuu hii hayo mambo sidhani kama yatatekelezwa Kirahisi aliongea
yule mama huku nikivunjika moyo .
Niliwasindikiza kwa macho, huku wakipanda kila mtu kwenye gari lake haoooo wakafunguliwa geti wakaishia, nilishindwa nifanyaje, ni kweli hata Mimi nilijua wazi kuanza kupeleka maombi ya kazi msimu ule wa sikukuu ikikuwa kama vitu vya kubahatisha tu.
Nilirudi hadi pale mapokezi nikamweleza yule mzee aliyenipokea kuwa naona muda umeisha na hakuna uhakika wa huyo mtu kutokea .
Yule mzee alinihurumia na kunisikitikia sana,
Umesema unaitwa nani,?
Ni kawaida mtu kujifanya kakusahau jina, iwe kwa bahati mbaya au makusudi, ila hupaswi kuchoka kumuelekeza jina lako, nikataja full name.
Akachukua simu yake akampigia huyo boss niliyemsubiri kutwa nzima, waliongea huku nikisikia vizuri
Maongezi yao,.
Aisee Kuna jamaa amekuja hapa anaitwa (akitaja jina langu)Sasa kwakuwa boss ulituahidi utafika leo, ikabidi nimwambie akusubiri. aliongea yule mzee huku akionesha hakuwa na uhakika wa huyo jamaa kurudi.
alikata simu Kisha akanieleza kuwa huyo ninayemsubiri yupo mkoani yaani alikozaliwa akiwa anaikaribisha sikukuu hata hivyo harudi leo wala kesho.
Tuliagana nikaondoka huku tayari mawazo yakirudi pale pale maana Kila nikichopanga kikawa hakiendi, nikiwa njiani nikamtafuta Rose maana ndiye mtu pekee aliyekuwa ananisikiliza lakini pia,
Eh niambie mpenzi wangu, vipi umefikia wapi, aliuza kwa pupa.
Mpenzi wangu wewe acha tu, huwezi amini masaa zaidi ya nane nimekaa pale lakini sijaongea na mtu jambo la maana, hivi my kwani yule mzee wako(nikimaanisha baba yake) alisema Kuna mtu anajuana naye lakini mbona kila nikipiga simu hapokei , na nikupe tu ukweli sioni dalili ya mafanikio pale.nilimwambia ukweli,.
Mmmh baby basi jaribu namba fulani ni za simu ya mezani, huenda atakupokelea kwakuwa ni simu ya kiofisi. Akanitumia zile namba,.
Nilisevu huku nikifika nyumbani nikiwa nimechoka najua si kwasababu ya kuzurura bali, kwakuwa sijafanikisha lengo langu. nilimsimulia Mke wangu akahuzunika sana,. nilifikiria Mara mbili huku nikitambua Kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo wa maisha yangu. Huku nikiwa naangaliana na Mke wangu hakuna aliyekuwa anajua mwenzake anawaza nini, maana najua hata yeye alikuwa kwenye lindi la mawazo.
Alifahamu fika jitihada zangu katika utafutaji wa maisha,. alifahamu fika juu ya balaa linalokuja mbele yetu ikiwa sina kazi, akavunja ukimya,
Mume wangu, naona huu si wakati wa kibweteka kumbuka Kuna kiakiba chetu kile ukiniambia niweke, unaonaje tukafungua hata kiduka fulani cha vyakula yaani mahitaji muhimu ya nyumbani, mume wangu lazima tuanze kwenye msingi tatizo wewe unaamini sana kwenye kuajiriwa, lakini kwenye ajira hizohizo naona huna bahati Nako kabisa. aliongea kwa sauti ya chini Sana iliyoonesha imekata matumaini.
Ni kweli maana najua hali itakayokuja mbele yetu si nzuri sana,. nilijibu huku nikimuonea huruma kwani sikupenda aumie Wala, apate shida.
Kila mwanaume hufurahi na kufarijika pale anapoiona familia yake ina furaha ila kinyume na hapo maumivu yake hayaelezeki.
Niliamka asubuhi, huku nikiwa sijakata tamaa bado nilikuwa na Imani, nikapanga ngoja niende Tena kule kwa Jana. Kabla ya yote nilipokea simu toka kwa jamaa mmoja akiwa ni sehemu ya wadhamini wa Shedy. Nilipokea simu tukasalimiana.
Akaanza kunikoromea
Ujue wewe Dani una dharau sana tulitegemea utatupigia simu lakini hukufanya hivyo, sisi ni majirani tu ujue lakini wewe ni ndugu yako kabisa mmetoka mkoa mmoja, lakini unajiweka nyuma wakati nyie ndiyo kila kitu. Na hapa tunapoongea nimeweka loud speaker Kila mtu anakusikia. aliongea kwa jazba yule jamaa.
Ikabidi nimwite Mke wangu kwa ishara ili asikie huku na Mimi nikiweka loud speaker.
Jamaa akaendelea kubwata.
Haya mshindi ni wewe maana uliamua kukaa kimya lengo tukutafute na ni kweli umeshinda maana, sisi ndiyo tumeshindwa ila Kaa ukijua kuwa ndugu yako anafungwa maana tumeenda jana tukaambiwa dhamana ni Hadi sikukuu ipite Sasa Kuna Nini Tena , aliongea kwa kujiamini sana.
Si kwamba sikuwa na uwezo wa kumjibu vibaya ila baada ya kuona watu wengi wananisikiliza nikakaa kimya huku nikimzuia Mke wangu ambaye alikuwa ameshakasirika mpaka namba ya mwisho.
Jamaa akakata simu.
Matusi ya nguoni aliyoyatukana mke wangu sikuwahi kumsikia tangu nimfahamu, ni kwamba siwezi kuyaandika hapa.
Sasa hapo unanitukana Mimi na wote tulioko kwenye hii nyumba. Maana hao hawakusikii. Nilimuonya
Mume wangu kwanini hawa wakugeuze kama choo cha stendi Ina maana wewe ndiye uliyemshawishi yule ms****aibe. tena kuanzia leo sitaki kusikia ukijihusisha na mambo ya watu, unajua ni mangapi umejihusisha nayo, na yakaleta matokeo mabaya, hizo huruma zako hizooo?
Ona Sasa yaani wewe miaka yote utakuwa mtu wa kutafuta kazi, badala ya kuiheshimu kazi uliyoipata ili ikuletee maendeleo unakuwa mtu wa kutembea na vihandbag Kila siku .
aliwaka mke wangu.
Nikaona kuendelea kukaa hapa nikujiletea matatizo nikaaga na kuondoka kuelekea kule kwa jana huku nikipanga kutokupiga simu.
Nikaona ni bora nikawaface moja kwa moja.
Kama kawaida niliingia kwenye ile yard huku nikitetemeshwa na Yale mandhari mazuri huku watu wakiwa wengi kila mtu akiwa busy na mambo yake.
Niliingia mapokezi, nikamkuta yule mzee na wafanyakazi wengi, akanikaribisha, chaajabu alinitoa nje nikashangaa, tunaongelea nje tena.
Bwana mdogo naona umerudi tena, bila shaka ni wewe uliyeambiwa uje na mzee(akitaja jina)ni baba yake Rose.
Akaendelea....
Samahani sana kijana wangu kwa usumbufu, ni kwamba Mimi na yule mzee tuliwahi kukutana kwenye baa moja, si unajua tena mambo ya pombe? (huku akicheka cheka)
Basi katika harakati za kufahamiana nikajikuta naropoka , nikimwambia Mimi ni afisa mwajiri hapa jambo ambalo si kweli. (Huku akitaja nafasi yake pale)
Hivyo Yule mzee mwenzangu aliniamini tukabadilishana namba,Sasa juzikati tu hapa alinipigia simu kuwa ana kijana wake, anataka nimfanyie mpango lakini tayari aliniweka kwenye wakati mgumu, hata Jana nilishindwa nifanyaje, lakini lazima nikwambie ukweli,
Mimi Sina cheo hicho lakini pia hapa ajira zikitoka huwa zinatangazwa kwenye vyombo vya habari na magazeti, hivyo wewe nenda mwaka wowote ukisikia tangazo la ajira usisite kuja kujaribu bahati yako,
Aliongea yule mzee huku nikigundua anaona aibu,.
Sasa dogo tafadhali naomba usimwambie yule mzee kuwa nilimdanganya wewe mwambie tu kuwa nafasi hakuna si unajua tena, huku akijichekesha.
Kwanza miguu ilikufa ganzi na tumbo likaanza kukata maana nilishakosa tumaini.
Sasa mzee wangu yaani hakuna namna yeyote Mimi kupata kazi. niliuliza nikiwa mnyonge.
Wewe kijana vipi bwana uambiweje huo ndiyo ukweli wenyewe mwanangu, alinijibu huku akirudi ofisini kwake.
Kweli pombe siyo chai, yaani baba yake Rose alipangwa akapangika.
niliwaza kisha nikielekea usawa wa getini, kabla sijatoka, Kuna Prado liliingia ni la kisasa ila linaonekana
Linapata suruba sana kutokana na kazi zao.
Mtu aliyekuwa upande wa kushoto kwa dereva alishusha kioo huku akiniangalia kwa muda , nilipigwa na butwaa kwani mhandisi mkubwa kabisa serikalini alikuwa akitazamana na Mimi.
Habari yako kijana ujue nimekufananisha na mfanyakazi fulani anaitwa Kelvini, Sasa nikashangaa yule tulimuacha Jana site ya mkoa huku kafikaje. aliongea yule injinia,
Aisee Boss ni kweli huyu jamaa kafanana kweli na kelvin alidakia yule dereva.
Kwahiyo wewe unaitwa nani na unataka Nini, aliuliza yule Injinia.
Naitwa(nikitaja full name)natafuta kazi.nilisema nikiwa nimenyooka kama nipo kwenye gwaride huku mkuu wa nchi akipita.
Hakujibu kitu alinishiria nisubiri huku akimwarisha dereva wake akamshushe karibu na mlango mkuu , nilichogundua ni kwamba siti za nyuma kulikuwa na njemba hata sikuziona zilipiga Jeans na fulana pamoja na buti ngumu, akaniashiria nimfuate ofisini, huku wale majamaa wakiniamuru nisiwe namkaribia boss wao,
Nilikaribishwa kwenye kiti huku, akiomba vyeti vyangu nikampatia.
Vipi mbona unahema boss vipi, aliniuliza huku wote wakicheka, ukweli ni kwamba nilimuona mtu mzito nadhani hakustahili kabisa kuongea na Mimi.
Cha ajabu hakuangalia vile vyeti ila alidili na vitambulisho vya makampuni binafsi nilikotoka.
Akaitwa afisa mwajiri ambaye alikuwa anaongea na yule mkuu huku kakusanya mikono, kwa heshima.
Huyu jamaa nimemkuta hapo nje eti anatafuta kazi, watu kama Hawa sijawahi kubahatika kuwaona huwa wanaishia kwenu tu, hivyo naomba kaangalie kama ana shahada kweli.
yule afisa akachukua akatoka, na Mimi nikaambiwa nitoke nikasubiri kule mapokezi,
Yule mzee ambaye kumbe ni tapeli tu alishtuka sana aliponiona,
Yaani wewe umepata nafasi ya kuitwa na Boss yule, huwa hadili na watu kabisa yule, sema,acha ALLAH aitwe ALLAH, kijana wewe mwenyezi MUNGU amekuona, hivyo ni vyema ukamtolea zaka na sadaka ALLAH maana Leo nimeona ukuu wa MUNGU.
Aliongea kwa kushangaza yule mzee anayedhani kila mtu ni muislamu.
Mara nikaitwa tena kule juu,
Vipi Ofisa anatufaa huyu, anatufaa tumpeleke mkoani maana kule huu mwaka ujao Kuna uhaba wakemia kule. aliuliza yule Injinia.
Anatufaa boss, ila ni vyema akabaki hapa hapa maana Kuna kitu nimegundua , huku akimsogelea na kusearch vitu kwenye desktop iliyokuwa pembeni ya boss , wakawa wanawianisha makaratasi yangu na vitu vilivyoko katika computer, wakacheka Kisha Injinia akakubali kwa kutingisha kichwa. basi utampa taratibu zote.
Huku yule mwajiri akiniambia nimfuate ofisini kwake, alikuwa ni mzee fulani wa makamo ila anajiweka kijana, kuanzia mavazi Hadi ongea yake ,
Bwana Danieliiiii we jamaa mganga wako ni yupi utuoneshe na sisi maana sikutegemea yule Boss akubali kuongea na wewe. aliongea kwa utani yule jamaa. Nikapewa taratibu zote huku baadhi ya vitu vikichelewa huku nikiambiwa kazi ni mwezi wa kwanza 2013.
hakuna Cha madam,
hakuna Cha ESTA
Hakuna Cha Shedy, nikiwa blacklist kwenye maisha yangu.
Niko na Rose sasa mtu aliyehusika nipate ajira ya heshima serikalini japo kwa ngekewa.
Itaendelea.......................
Nilikuwa mpya kama dhahabu.
Vipi


