Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Tunapitia mengi sana kwenye familia na hata maisha pia kama wanaume. Ninajifunza hakuna lisilokosa mwisho. Hakuna kukata tamaa, kujiamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu ndio ngao kuu.
 
Samahani wakuu,
Kwa wale wafuatiliaji wa mkasa wangu ni kwamba.

1.Sijalazimishwa na mtu kuleta hiki kisa hapa

2.Sitaongozwa Wala kuamrishwa na mtu namna na muda wa kupost.

3.Sitalazimika kufupisha stori kisa Kuna mtu inamchosha.pia Sina muda maalumu wa kuileta hapa

4.kuna simulizi chungu mzima humu jamiiforum zimeandikwa na waandishi mahiri,waweza kujikita zaidi huko

5.hiki siyo kisa cha kufikirika,ni kisa cha kweli hivyo stori italetwa kama ilivyo.

6Mimi si mwandishi mzuri,tusameheane pale yanapojitokeza makosa, typing error n.k
Wewe ni mwandishi mzuri saaaaana.Usikatae hilo.
 
Tarehe 17 mwezi wa kumi mwaka 2011, mimi, bosi na mke wake tulikuwa kwenye eneo fulani tukipata Chakula Cha mchana.

Si kawaida mimi kuandamana nao ila ni kwasababu, ilikuwa ni kwaajili ya mpango maalumu yaani Mimi kutumwa kufuata mzigo fulani mkoani.

Nirudi nyuma kidogo,

Mwaka 2011, nilikuwa na wakati mgumu sana kimaisha ni baada ya mwaajiri wetu kubadili kazi kutoka kazi uinjinia na tenda za kutengeneza barabara na kuhamishia nguvu kwenye biashara hoteli ikiwa ni hatua kubwa kwake

Huku wengine tukiachwa solemba maana ikabaki tu ile

Unajua nini Dani, Mimi nitakufanyia mpango palepale mi siwezi kukuacha tumetoka mbali bwana.

Huku nikiwaza, atanifanyiaje mpango Mimi kwenye biashara hiyo mpya ikiwa Sina utaalamu kwenye eneo lolote lile, anataka kunipa kazi gani?

Ulinzi? Au niwe naelekeza watu wapi pa kupaki magari au nikawe Gardner kwenye bustani zake, hahahaha siwezi kufanya hizo kazi na haya ni maneno ananipa ili kunifariji Hana kazi ya kunipa kwa Sasa.

Basi kadri maisha yanavyoenda ndivyo ugumu wa maisha ukawa unaongezeka, kila nikihangaika kutafuta kazi ikawa ni ngumu kupita maelezo, ikafikia wakati nikamnyang'anya pikipiki kijana fulani ambaye ni mtoto wa kaka yangu binamu.

Nikachukua pikipiki yangu kwakuwa haikuwa na mkataba ikawa rahisi tu, lengo siyo niendeshe Mimi ila ilikuwa iuzwe ili inisaidie kunyoosha mambo fulani ambayo pale nyumbani yalishaanza kukaa shaghala baghala.

Ikafikia hatua, nikiangalia baadhi ya vitu mule ndani naona kama vingi halafu vimebanana, basi friji la jokoni likawa muhanga, ni sawa na mchezaji ambaye kashindwa kuonesha kiwango bora kwenye timu,

Ni kipindi ambacho mke wangu alikuwa anahuzunika sana, kwanini kuuzauza vitu, akinisihi zaidi kupambana nipate kazi maana yake nilikokuwa naelekea si kuzuri.

Mambo yalienda hivyohivyo huku nikijitahidi kujikakamua kulipa ada ya mwanangu ambaye nilimpeleka nursery ya bei kubwa, ambapo nadhani ilikuwa ni kuiga ama kufuata mkumbo maana hata kazi yangu ya mwanzo sikuwa na mshahara wa kihivyo.

Basi huku tukiishi maisha fulani ya unga nusu na robo, siku moja tukiwa kwenye Chakula Cha usiku mke wangu alivunja ukimya.

Mume wangu, mume wangu, baba Jackiiiiiii, si nakuita wewe au?

Aliuliza,

Si kwamba nilikuwa simsikii hapana Bali macho yangu yalikuwa kwenye TV ambapo yeyote angedhani labda naangalia kwa makini kinachoonesha kile, kumbe Mimi naitathmini TV yangu ilivyo kubwa yaani naona hii nikiuza sikosi laki nane Hadi milioni.

Ni TV flani za mtumba hakika kama ni TV niliipata.

Naam mke wangu, teh teh nikijichekesha.

Mke wangu aliniangalia huku akionesha kukasirishwa ila hakusema chochote kibaya

Mume wangu Mimi hapa Nina mambo mawili nataka tuzungumze,

Nikamwashiria kwa kichwa kwamba aendelee,

Akasema, jambo la kwanza hapa ni kuhusu huyu dada wa kazi, ni mtu mzuri, ana tabia nzuri na ni mchapakazi lakini tuna miezi minne Sasa hatujampa haki yake, mbaya zaidi hatuna matarajio atapewa posho yake lini, alisisitiza mke wangu.

Nikawa nimekaa kimya.

Akaendelea jambo la pili, mimi ni mjamzito..

Enheeeeeeeeeeeeeeeeeeehh

Unasemaje?

Itaendelea.....
Asante

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
 
Mbona Tena watu mnampangia jamani Kama unammiliki. Mbona alitoa tambihi.
Yaani Kama anaenda job saa 11 asubuhi ahairishe ili akuwekee.
Akam anat00mbana ahairishe akupe wewe haja zake.
Kama vipi mlipe laki Sasa ili akuandikie.
Wewe tulia hata Kama akiweka mwaka kesho kwani utakufa
Nimecheka sana mkuu
 
Kiufupi Rose aliupiga mwingi sana , ni fundi sana wa mipira ya pembeni, iwe kushoto au kulia halafu na dimba la Kati ndiyo kabisa anakuja juu juu huku anakukaba ukienda kwa pupa ana chenga zake za kufinya. Jamani acheni tu.magoli ya mapema sana yalipatikana kwa Kila mmoja , huku timu zikishambuliana kwa zamu mechi iliisha kwa sare ya bao tatu kwa tatu huku wachezaji tukilowa tapatapa kwenye ile derby isiyo rasmi.
Sehemu kama hizi kuna maswahiba zangu wawili humu wanazipenda sana,yan stori ikiwa haina hiki kipengele hawasomi kbs😂,nasikitika sitaweza kuwataja hapa ila Antonnia na moneytalk mungu anawaona hakyanani
 
Sehemu kama hizi kuna maswahiba zangu wawili humu wanazipenda sana,yan stori ikiwa haina hiki kipengele hawasomi kbs😂,nasikitika sitaweza kuwataja hapa ila Antonnia na moneytalk mungu anawaona hakyanani
Hahahaaa!!! Nimefika ngoja nikitulia nisome vizuri!
Asante sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom