Kumbe tupo wengTupo wengi kusubiri
pamoja bossSEHEMU INAYOFUATA. ...........
Niliingia chumbani huku nikitambua kuwa mke wangu kakasirika, nilitulia tu , nilitamani nimwambie kitu lakini kutokana na hali yake ya tumbo kuwa kubwa nikaona nitaamsha mengine.
Dah , mke wangu hakuna jambo zuri kama kuamka unaelekea ofisini kwako, yaani Nina FURAHA sana hata hii jumatatu ya kesho naiona inachelewa, nilivunja ukimya.
Ni kweli mume wangu, ila hata hivyo nashauri ni vyema ukajipanga vyema utafute mtaji ili tuwe na biashara, kumbuka kuwa hata uwe na hela nyingi kiasi gani, Kama pesa haizunguki si chochote si lolote.
Lakini baby Jack, nimekwambia umsikilize ESTA shida yake, Cha kushangaza umekaa naye muda mreeefu kana kwamba anasimulia vitu vya maana, kumbe ni mambo ya kimalaya tu, aliongea kwa hasira.
Sasa mke wangu wewe ndiye uliyeniambia nimsikilize, imekuwaje unanigeuka. Nilihoji.
Baba weeee naamini kakueleza Kila kitu kuhusu umalaya ulivyomfanya akapoteza dira ya maisha, kwanza kabla hajanisimulia haya mapito yake nilikuwa namuonea huruma sana, nikashangaa kwanini hata kanisani kwake wanamtenga, hasa ukizingatia pindi nafahamiana naye , nilimkuta anatukanwa na baba mmoja ambaye alikuwa anamuonya apunguze mazoea naye.
Lakini tangu anisimulie mambo yake aliyopitia nimemdharau mpaka basi huyu mbwa. Hivi mume wanguuuu mtu anakusimulia kuwa alikuwa anashiriki kanisani kwa lengo la kutega wanaume, huyo mtu utamchukuliaje?
Halafu ninayeambiwa Nina mume unadhani nitakuwa na amani kweli?
Kuanzia Leo sitaki mazoea naye nishamuona si mtu mzuri, mtu gani yeye stori zake ni za kimalaya, yaani wenzake tunaenda kanisani kufuata tiba na msaada wa kiroho yeye amepafanya kama night club akivizia mapedeshee. aliongea mke wangu kwa hasira.
Hivi mke wangu uliniambia huyu mtu ni muathirika eeeh . Niliuliza
Eeeenheee, yule ni muathirika ndiyo mbona watu wengi wanasema mbaya zaidi, halafu kila nikimshauri akapime anakuwa mziiito, we unadhani Kuna Nini mwili wake tu unaonesha kaumia. Aliongea kana kwamba ana uhakika
Kutokana na alivyokuwa wa moto sikutaka kuendelea na stori zile, huku nikishangaa unafiki wa wanawake, yaani kama wanapendana ukiwakuta.
Asubuhi ya jumatatu, saa kumi na moja alfajiri ilinikuta kwenye daladala tayari kuelekea kazini kwangu,
Ni kazi mpya, na Mimi ni mgeni kwenye ile kampuni, hivyo nidhamu ya kwanza ni kuwahi kazini . Niliripoti kama kawaida huku nikiifurahia ile ofisi ambayo kiukweli ilinipa heshima, nilikaa kwenye kile kiti Cha kuzunguka huku nikitafakari jambo ni jinsi gani napaswa kuwa makini kuliko umakini wenyewe,
Nikaiwasha desktop iliyokuwa mbele yangu, huku nikibofyabofya vitu Fulani, mlango uligongwa, sikuwa na Shaka sana juu ya ujio wa mtu yoyote yoyote kwakuwa ukaguzi unaofanyika pale mpaka mtu anaruhusiwa kuja kwako ni mkali sana japo huwezi kuwa na Imani kwa asilimia mia moja.
Ingia, nikimkaribisha yule mtu.
Oooh Mr Daniel waaaooooh, habari za asubuhi,
Alikuwa ni yule dada ambaye nilimzingua baada ya kuniletea dharau eti kwanini Sina gari, nikampoza kwa kumtia lunch. Ni kadada Fulani kana nyodo sana .
Akaendelea....
Vipi wifi hajambo na wanangu,
Wazima wa afya, nikamuitikia
Sawa, ila Mr umejihimu kweli Mimi nakuwaga wa kwanza hasa siku kama ya Leo ya jumatatu.
Aaah unajua Mimi nakaa mbali kidogo hivyo ni vyema kujihami ili kujipa ahueni , nilimjibu.
Sawa, vipi bosi alikuambia kuwa kasafiri? Aliuliza
Hapana, Sina taarifa hiyo?
Sawa hata Mimi siyo kwamba kaniaga ila nimeona taarifa sasahivi kwenye PC ofisini kwangu na wewe ifungue hiyo laptop unaweza kuiona hiyo taarifa, basi sawa nilikuwa nakusalimia tu Mr Mimi nipo ofisini kwangu.
Nilifungua PC iliyokuwa pembeni kabisa huku ikiwa inafanana sana na ya kwangu ya nyumbani zote ni
LENOVO nikaikuta taarifa ya bosi kuondoka.
Ila nikaona maelezo ambayo nilishangaa sana yalisomeka hivi
Bwana Daniel, karibu sana kwenye kampuni yetu, Ukiwa ni mfanyakazi mpya, taratibu utakazoelekezwa ndizo unapaswa uzifuate.
Lakini pia , ni vyema ukajitambua kuwa Kila unachokifanya ni kwaajili ya wewe na familia yako, majungu na fitina ni sehemu ya kazi kwa Kila mtu , naamini ipo namna unayojua kuyakabili na kuyaepuka kwa ustawi wa kazi na maisha yako.
Nakutakia utendaji kazi mwema.
Kwangu yalikuwa ni maneno ya kawaida tu japo nilishangaa yeye yanamuhusu Nini ila si mbaya ndivyo tulivyo binadamu,
Nikaendelea na kazi zangu , ndogo ndogo nikaona ni muda wa kwenda kutafuta chai, kutoka nje niliona parking zilivyochafuka kwa magari nikagundua kuwa hii kampuni Ina wafanyakazi wengi kuliko ninavyodhani.
Niwe mkweli niliumia sana nikiyaona yale magari nikajikuta Kuna wakati nawaza niibomoe akaunti yangu Nini, ili nivute mkoko, shetani alikuwa kwenye kazi yake.
Nikapata chai yangu kwenye mgahawa Fulani pale nje nikarudi zangu ñdani huku walinzi wakinizongazonga eti niwape hela ya sigara,
Najua ni tabia zipo kila mahali hasa wakikuona ni mgeni.
Wakati wa mchana nilipata kutambuana na watu wengi sana pale wengine wanahudumia kampuni zote yaani ikiwemo ile ya zamani kwangu Mimi.
Nikagundua mambo mengi sana kadri siku zinavyokwenda , ni jinsi gani mtu kapanga vyumba viwili lakini ana gari,
Mtu mwingine hajaoa anaishi kwa wazazi wake lakini ana gari ya gharama, mtu mwingine, pia wakati Mimi naiogopa mikopo kwa vitu ambavyo ni liability wengi wetu kwenye kampuni wana magari ya mikopo, nikajikuta napata faraja ya kinafiki japo bado naumia
Wasiokuwa na magari kwenye kampuni walikuwa wengi kulingana na nafasi zao, ila kwangu Mimi Kila mtu alilaumu eti.
Nilipiga kazi kwa uaminifu sana huku nikifuata ushauri wa boss wangu kutokuwa na mazoea sana na watu wengine huku yule madam akiwa ni mtu ambaye nilikuwa makini naye licha ya vitisho vya hapa na pale kwakuwa alitaka nimsaidie shida zake za kiwaki bado Mimi niliendelea na kazi yangu huku miezi wiki zikikatika,
Siku moja nipo ofisini nilipokea taarifa kuwa mke wangu ni mgonjwa yupo moja ya hospital binafsi city centre, sikushtuka sana nikajua ni ile hali yake hasa ukizingatia siku zilikaribia, sikuwa na presha nilitoa maelekezo huku niliendelea na kazi nikiwa na maana lisaa tu baadaye nitaenda kuwaona.
Nilienda pale hospitali nikakutana na shangwe tu , watu wakiita kapata jina kapata jina, nikataka kuingia nikazuiliwa, huku niking'atwa sikio kuwa mke wangu kajifungua mtoto wa kiume , nilifurahi sana, sana, sana, sanaaaaa, nikaambiwa kuwa kutokana na kuwa mjamzito alijitunza vizuri kesho ataruhusiwa , nikakubali huku nikiwa na furaha njia nzima.
Kufika nyumbani nilimkuta ESTA, akiwa anapiga stori na dada yangu pamoja na housemaid wetu, maana mama mzazi alikuwa na mgonjwa hospital.
Huyu si Hana uhusiano mzuri na mke wangu huyu? Kafuata nini?
Kwanza mke wangu hayupo na Mimi mwenyewe sitaki mazoea naye, Leo hii namchana, kama ni matatizo yake apambane nayo tu.
Kabla sijasema kitu , dada yangu aliniwahi akaniita ñdani
Kaka pole na kazi, na pia hongera sana ndugu yangu tumepata simu kuwa wifi amenifungua salama.
Nikweli hata hivyo nimepita hospital japo mgonjwa sijafanikiwa kumuona.
Nilimjibu.
Sawa, ila Kuna huyo mgeni hapo nje katueleza kuwa alikokuwa amepanga kafukuzwa kutokana na kudaiwa Kodi kwa muda mrefu hivyo kaja kuomba hifadhi kwa muda.
Muhurumie kaka , yaani ni Kama kachanganyikiwa.
Aliongea Dada yangu.
Mmmmmmmh, hapa familia imeshakuwa kubwa wengine ndiyo haoo wako hospitali ni wageni wapya wanaonihusu Kila kitu, huyu ESTA naye anataka msaada wa kukaa hapa.
Huyu tayari haelewani na mke wangu,Sasa itakuwaje.
Wanaume tumeumbwa mateso.
Itaendelea.......................................
Bado ya moto hii
Nakazia hapo😛Kama hii story ni kweli wewe ni mwanaume kama story ya kutungwa basi wewe ni mtunzi bora
True story mkuu huwezi amini,Kama hii story ni kweli wewe ni mwanaume kama story ya kutungwa basi wewe ni mtunzi bora
Pamoja mkuu. Hela Ina nguvu mno pia Ni emotional commodity none can escape itSEHEMU INAYOFUATA......
ESTA mwanamke ambaye alikimbiza sana mjini, ambaye wanaume wengi tulimtamani lakini hatukuwa na uwezo wa kumpata , huku aliwapanga mabosi wa mjini.
Hatimaye mambo yaliharibika na kuishia pabaya huku akiwa Hana tumaini jipya,kadri siku zinavyokwenda ESTA anakataliwa na Kila mtu, katika maisha ya mjini hakuna aliye tayari kuishi na mtu asiye ndugu yoyote na hivi vipato vyetu mbona mtihani?
Mbali na kipato ESTA hajaweka wazi kuwa ana ndugu hapa mjini, mtu mwenyewe ana msongo wa mawazo akijiua je?
Nilifikiria kwa kitambo kidogo, ikabidi nimfuate,
Habari shemeji pole na kazi na karibu sana, maana sisi wageni tumetangulia kuliko nyinyi wenyeji,
Aliongea bila breki,.
Kiukweli nilishakasirika ila nilijizuia asijue niliona si vyema kumnunia mtoto wa kike, tuliongea kiufupi Kisha nikaingia chumbani nakumbuka licha ya dada wa kazi kuniita muda wa dinner nilikataa, nilikuwa na mawazo sana.
Hivi yule madam si alisema yupo tayari kumsaidia huyu ESTA,
Sema huyu ESTA kama hataki vile kusikia lolote kumuhusu mbaya wake,
Ila nitamlazimisha akubali, maana kaja hapa kuomba hifadhi ambayo sijui ni ya muda gani, na Mimi nahitaji kuijenga familia yangu na kama msaada nitatoa inapohitajika na kwenye ulazima.
Halafu sijui nimpeleke kwa mganga, maana huyu ni kama kachanganyikiwa ninavyomjua ESTA ni mwanamke mjanja sana lakini awamu hii namuona kazubaa sana, Tena Hana hata chembe ya aibu mbaya zaidi hata haeleweki,
Masikini kumbe unaweza kupewa uzuri ukanyimwa vingine, ana umbo matata ana shepu lakini anashindwa hata kuomba kazi ya mamantilie?
Niliwaza mengi usiku huo, asubuhi kama kawaida nikawahi kazini, nakumbuka siku hiyo nilifanya kazi huku mawazo yakiwa kwa ESTA , baada ya Chakula Cha mchana nikatafuta sehemu isiyokuwa na watu wengi nikampigia madam,
Hello tolu naona umenikumbuka mwenzangu, aliongea baada ya kupokea simu,
Ni kweli madam nipo bize wewe mwenyewe unatambua, moja kwa moja madam nikwambie kuwa nilimtafuta ESTA nilimpata, ila Kila nikimgusia stori kuhusu wewe hataki kabisa na mbaya zaidi Hana msaada Wala Hana pakuishi tunamsaidiaje?
Niliuliza.
Usijali najua kuwa ananichukia, lakini nenda naye taratibu atakuelewa tu.
Hapana madam Mimi naomba tufanye kitu kwasababu hapa napoongea yupo kwangu na pia naona kama mke wangu hamkubali kivile, kwahiyo nahitaji tufanye kitu madam,
Tumfungulie biashara kupitia Mimi huku huo msaada ulioamua kumpa nijifanye nimempa Mimi.
Ooh aisee nashukuru sana Dani umewaza vema, Mimi hapa Nina milioni tano za haraka haraka unadhani unaweza kumshauri afanye biashara Gani? aliuliza madam
Naomba nipe muda nifikirie, nilimjibu huku nikikata simu, niliuona mchongo wa pesa ambao sipaswi kukurupuka kujibu, tamaa ikaniingia
Kwanza nitahakikisha huyu madam na ESTA hawakutani Wala hawawasiliani hata kwa njia ya simu ili nipige hela .
Wakati nikiwaza hayo simu kutoka kwa mke wangu iliita ,
Nikaiweka sikioni,
Sisi hapa tumekodi usafiri tayari tunaelekea nyumbani,
Aliongea mke wangu.
Sawa nitawakuta nikirudi, nilimjibu huku nikiwaza jinsi ambavyo nitajitetea kuhusu uwepo wa ESTA nikapanga uongo wote wa kumwambia ili nisije kuharibu mishe niliyoambiwa na madam.
Kama madamu katamka M5
Haraka haraka vile unadhani hawezi kutoa kumi halafu nikapiga tano na ESTA nikampa tano nikijidai nimemkopesha afanye biashara ,
Niliwaza huku nikiwa nishapata hata wazo la kutembelea wapi wanafyatua tofali nzuri zilizokolea saruji tayari kuweka kwangu ili shughuli ya ujenzi ianze ,
Halafu nikitoka hapo naenda mission Fulani pale Kuna wanafunzi wa seminary huwa wanauza mijibwa ya kizungu, nitachukua mbwa mdogo huku nikimpa mafunzo, yaani kwangu sidhani kama atakanyaga mtu ovyo ovyo, niliwaza Yale mambo ya kijinga Kisha nikaanza kuzima vifaa vyangu vya kieletronic tayari kwa kujiandaa kutoka.
Nikapokea simu ya wife kwa Mara nyingine,
Tumefika salama tunashukuru MUNGU ila mume wanguuuu huyu ESTA Mimi simuelewi, kabisa naona kagundua kuwa nimejifungua Sasa kaamua kuja kuziba nafasi yangu,
Ndiyo, sasahivi Mimi ni mzazi, ni mgonjwa ninalea ni kipindi ambacho atakufaa wewe kama mke mwenzangu,
Aliongea kwa maudhi sana.
Wewe acha upumbavu, nakuita mpumbavu kwakuwa sioni kama unaniheshimu siku hizi , acha kudeka kipumbavu.
Kwa Mara ya kwanza ESTA alipajua kwangu, si ulimleta wewe?
Mmekuwa na ratiba za maombi hapo nyumbani, hao watu huwa nawaita Mimi?
Kuna kipindi ulikuja naye, ukadai nimsikilize madai yake, lakini ulinigeuzia kibao na kunichukia bila sababu ni kwanini?
Nilikukalia kimya kwa sababu ambazo hata wewe unazijua lakini una fahamu kama ulikera sana?
Hakujibu neno akakata simu, nilikasirika niliona nikiwa kama mwanaume sipaswi kudekeza haya mambo atanipanda kichwani.Na nikifika sitajali mama yangu mzazi Wala nani nitamkoromea mbele ya huyo ESTA wake,
Tena kama ESTA atachukia na kuondoka na aondoke mjinga mkubwa yule Tena ni mchonganishi nikachukua mkoba wangu nikafunga mlango nikapiga hatua kuelekea nje.
Safari hii nilijiapiza mke wangu naenda kumsema hata Kama bado mbichi hawezi kuwa na dharau kiasi Cha kutaka na kunisingizia, nikatafuta daladala za moja kwa moja huku nikiwa mtaratibu nisiharibu suti yangu, kwa kugombea kuingia ndani
Nilingia huku nikikosa siti kwenye ile Eicher chakavu,
Hivi hii tabu Hadi lini hivi million kumi mtu huwezi kupata gari kweli ?
Wewe zipo gari Kali kabisa Tena zingine chini ya hiyo hela ,
Sema Kuna Lexus mahali japo ni old modeli lakini Iko vyema sana sema mwenyewe anataka kuminambili
Ingenisaidia sana kuliko hii adha ya kuchafua nguo.
Sasa ilifika kipindi natamani gari, je nitaamsha ugomvi kwangu ili ESTA aondoke?
Na akiondoka, si nitakosa ule mchongo kwa madam?
Lakini ni rahisi kuila hiyo hela kizembe hivyo? Au nitajitafutia matatizo.
Usichoke inakuja very soon.
Itaendelea...................
PAMOJA SANASEHEMU INAYOFUATA......

Ina mafunzo mengi sanaTrue story mkuu huwezi amini,
Ila imeandikwa kiufundi ikiwemo kuacha baadhi ya visa ambavyo ni vya wazi mno, enjoy story
DuuSEHEMU INAYOFUATA.........
Nilirudi nyumbani kuungana na familia huku nikitambua hakuna amani ya moja kwa moja,
Ile furaha ya kupokea kiumbe kipya ilitoweka watu walikuwa kimya sana nilisalimia huku mtu pekee aliyekuwa na furaha japo ya kulazimisha ni ESTA, ambaye tayari nilimchukia kwa kiasi fulani.
Daniel mwanangu kabla ya kufanya chochote Nina mazungumzo na wewe,
ni maneno toka kwa mama yangu mzazi
Kwanza mwanangu pole kwa misukosuko na mengi yanayokukabili, watu wote hapa tumeungana kwenye hii familia si kwa kuja kula Raha Bali ni visa na mikasa vimetuunganisha.
Kila mmoja anatambua Nini kimetutoa mkoani kuja hapa, labda nikukumbushe tu kuwa kwenye maisha Kuna mikosi, na mwanangu mikosi ilikutembelea, ukawekwa mahabusu, naamini ulihitaji dhamana kutoka kwa watu wenye uchungu na wewe , hebu kumbuka una marafiki na maswahiba wangapi hapa mjini,hawakukusaidia
Na je, unawezaje kutofautisha nyakati mwanangu au unaishi tu, mwanangu hii ni Dunia,
Nimekuja kutoka mkoani Mimi na dada yako siyo kwamba tulikuwa na uwezo wa kukutoa mahabusu sisi kwenye hii Dunia ya kisasa iliyojaa rushwa , hapana,.ni upendo tu
Unadhani Mimi au dada yako hata mkeo nani angeweza kukunasua kwenye ule mtego wa matajiri wenye pesa wanaoweza kukufanya chochote kile,
Sisi kazi yetu ilikuwa ni moja tu kukuonesha UPENDO tu, mwanangu unatambua kuwa sisi wazazi wako ni maskini si matajiri, tunakutegemea kwenye mambo mengi, unadhani tungekusaidia Nini kwenye kesi yako.
Naomba utambue nafasi aliyocheza mke wako kipindi una matatizo ni sehemu pekee ya kutambua thamani yake kwako, sisemi kuwa hakukosei, najua anakukwaza kwa mambo mengi lakini Mimi kama mama yenu na mama yako mzazi nakuombea na kukukumbusha kuwa makini.usipende kuweka msimamo Kila sehemu mengine yapuuze
Nachoweza kushukuru ni kwamba mkeo kajifungua salama na maendeleo yake yanaridhisha sana tu kwahiyo hatuna Cha kutuweka hapa kwako ni kwamba tuna masaa machache ya kurudi nyumbani mkoani maana ulituomba tukae kwaajili ya mgonjwa hatimaye MUNGU kajalia na kutia wepesi.
Lakini mwanangu nikuulize swali moja ulikuwa na maana gani kumkoromea mkeo?
Mtu ambaye anahitaji UPENDO wa dhati toka kwa mumewe hasa kipindi kama hiki alichojifungua,? Alimalizia Mama kwa mfumo wa swali.
Nikamjibu,
Kiukweli Mama wewe mwenyewe kwa siku ulizokaa hapa , umegundua ni jinsi gani huyu ESTA anavyokuwa karibu na mke wangu, Sasa iweje ujio wake uwe msala kwangu Mimi, kifupi mke wangu kanikera sana.nilimalizia
Sawa mwanangu, naomba utambue kuwa humu ñdani watu wote ni wanawake, hebu jitofautishe basi Dani, hebu jaribu kudharau baadhi ya vitu visivyokuwa na umuhimu , ni aibu kubwa Mimi nianze kuwasuluhisha nyinyi katika kipindi ambacho mkeo katoka kuponea kwenye tundu la sindano,
Yaani ilikuwa ni wakati wa wewe na mkeo kukaa na kuanza kupendekeza jina la mtoto ataitwa nani na siyo kutengeneza malumbano.
Aliweka kituo.
Nilimwelewa sana mama nikaingia chumba fulani ambacho huwa hakitumiki nikamkuta mke wangu akiwa na furaha tu anachezacheza na mtoto tofauti na nilivyofikiri baada yakuona watu wengine kule nje wamenuna nuna yeye alikuwa poa kabisa tulisalimiana nikampa pole huku tukitaniana baadhi ya vitu.
Oooh hiki kipindi kigumu, Mara ooh umeshikaje ujauzito Mimi Sina kazi, Sasa nimemleta huyo hapo mkatae Sasa, alitania mke wangu.
Weee nimkatae, kwanza hii jinsia nilikuwa naisubiri kwa hamu, yaani nataka siku moja kama nitakuwa hai niende pale airport nimuone akishuka kwenye ile midege ya Emirates huku akiwa nadhifu na Yale mavazi yao,
Halafu kwa makusudi nimwambie mbona simu yako haikuwa hewani,nilitania
Wewe mwanangu sitaki awe rubani , huyu atakuwa daktari bingwa nikwambie, alisema mke wangu Huku tukitaniana mambo mengi, ambapo nilifurahi sana,
Maana timbwili nililokuwa nimepanga kufanya nilijikuta nasutwa tu moyoni mwangu ila nikashukuru kama mambo yamekuwa sawa , najua atakuwa kamshitakia mama,
Na bimkubwa navyomjua atakuwa kaniponda weee ili ampe ushindi huyu , bimkubwa hajawahi niangusha kwenye kumbembeleza mtu
Baada ya kupata ile amani ya moyo sikutaka kuzungumzia habari za ESTA muda huo ili kuepusha Shari.
Nilitoka nje kucheki mazingira nikamuona ESTA akiwa anajituma anafua nguo za mke wangu akisaidiana na dada yangu, nilimuhurumia sana , Kuna wakati baada ya kukwazana na mke wangu kwenye simu nilimuona huyu ndiyo chanzo , nikapanga nije nimtimue lakini maisha acha yaitwe maisha
Kama tu Mimi mwanaume nilipigika Hadi nikawa nauza vitu vyangu kipindi fulani itakuwa kwa huyu mwanamke?
Kumbe atafanyaje, ajiuze, Bora kaja kuomba msaada sishindwi kuishi naye tatizo lipo kwa mke wangu lakini pia si madam karidhia tumfungulie biashara?
Kwanza ngoja, Kila kitu kitakaa sawa.
Kaka vipi mbona unaizunguka nyumba kama unaizindika vipi, alitania dada yangu,
Hapana nilikuwa huko nyuma naangalia mahali pa kumwaga tofali nahitaji kuijenga fence.
Ahaaa safi my brother, tunakuombea kwa MUNGU Kila kitu kiwe poa,naona nyumba itapendeza sana
Alijibu
Wakati tunaongea hayo nilipokea simu namba ngeni,nikaiweka sikioni
Habari kaka,za siku nyingi Mimi ni Shedy,
Kwanza nilibadilika, maana sikupenda mazoea Tena na huyu mshikaji,
Unasemaje, niliuliza
Aisee kaka jaribu kusahau yaliyopita Mimi na wewe ni ndugu kabisa unajua tulipotoka, nina mazungumzo na wewe kaka, aliongea kwa tahadhari.
Ongea nakusikiliza,
Sawa ni hivi ,mwenzio baada ya kukuta biashara inayumba na zile shughuli zangu zimekuwa ngumu nilikopa hela kwenye benki ya(akiitaja hii benki maarufu nchini)
Ni kutokana na shughuli zetu kuwa ngumu yaani udalali kwangu umenikataa kabisa, nikaona nikope hela ili niiboost biashara yangu, lakini mambo yamekuwa tofauti sana
Kwanza Kuna mtu hapa kafungua bar ya kisasa ni Mara tatu ya hii yangu kama ujuavyo kipya kinyemi yaani mwezi wa tatu Sasa wateja wangu maarufu anao yeye.
Hebu fikiria Kuna muda nauza kreti moja tu la bia huku vile vikali huuzi kabisa na wahudumu niliokuwa nao wanaihitaji pesa yao kama kawaida yaani ni hasara juu ya hasara , huku wafanyakazi Mara biashara haiendi jumlisha riba, nitatoka kweli kaka.
Aliongea kwa uchungu wa kujipendekeza.
Sasa hayo ni maisha yako, Mimi nahusika vipi, nilijibu
Hapana kaka, Mimi shida yangu ni moja nataka unisaidie, ni kwamba Kuna mwanamke anaitwa ESTA naamini unamfahamu vyema sana yule Mimi namtafuta sana, ni kwamba yule Kuna kipindi alikuwa mpenzi wangu wa Siri, Sasa wakati wa mapenzi yetu alikuwa na kiasi fulani Cha hela , nikamzuga kwamba aniazime niingize kwenye biashara yangu alikubali, baadaye niwe mkweli baada ya kuwa nishamchoka sihitaji kuendelea naye,
Nilimwambia aangalie ustaarabu mwingine , ndipo alipoamua nimpe hela yake kwanza ndipo tuachane lakini nilimtishia kuwa Hana hela kwangu na nitamshitaki, hakuwa na la kufanya ukizingatia pesa zaidi ya milioni tatu tulipeana bila ushahidi wowote,
Aliweka kituo.
Sikia Shedy unanidharau sana kwamba nikutafutue ESTA hapohapo unanipa mkasa wako wa kimalaya,kumbe ndio tabia yako kutembea na wanawake na kuwadhulumu,kwa mfano ukimpata unataka umfanye Nini,niliuliza safari hii ni kwa ukali,
Ni hivi kaka lengo nimuombe msamaha na naahidi kuwa nitamlipa mbele ya ushahidi kwasababu, kila nikizunguka kwa wataalamu Wananiambia Kuna mtu Ana masikitiko juu yangu,ndiyo maana biashara yangu inayumba.alimalizia
Cha kukwambia ni kuwa Sina mahali ambapo nitampata huyu ESTA kwahiyo wewe fanya mambo yako Mimi Hilo lipo nje ya uwezo wangu,nikakata simu.
Mapya haya kwangu,yaani Shedy mjinga sana,na habari zake za kishirikina,
Eti ananiambia kuwa biashara haiendi kwasababu ya masikitiko ya mtu,wakati anajua wazi Kuna biashara mpya kama yake Tena imekuja kisasa halafu bado unatafuta mchawi,
Ni sawa na bus jipya na la zamani route ile ile na nauli ni moja nani atachagua la zamani,?
Kweli nimeamini ushirikina ukizidi na akili inapungua ,
Lakini huyu ESTA naye kumbe mjinga eeh kweli alirogwa akarogeka na kukorogeka , unawezaje kutoa zaidi ya milioni tatu kumpa mwanaume Tena Ukiwa ni maskini,akijifanya Ana mapenzi ya kizungu huu si ulofa huu
Ndiyo maana Kila nikimuuliza baada ya kuuza kibanda chako mkoani kwenu hela ulifanyia Nini haeleweki huyu , niliwaza sana jinsi binadamu tulivyo tofautiana .
Nikarudi ndani huku nikisearch kampuni fulani ya uuzaji wa magari used wakidai bidhaa zao ni Bora sana licha ya kuwa zimetumika nikawa napoteza muda pale,
Mke wangu akavunja ukimya,
Samahani sana mume wangu, kwa Yale tuliyoongea mchana ila tufanye yamepita,
Hivi mume wangu ukimwangalia ESTA kwa ukaribu unadhani ana akili timamu?
Kwanini umeuliza hivyo, mke wangu,ni kwasababu kaja kukaa hapa?
Hapana,
Nahisi Kuna jambo linamsumbua tujaribu kusaidia.
Mke wangu aligundua Nini kwa ESTA?
Nani kampa huo ufahamu kiasi Cha yeye kuwa Mpole na mwenye huruma ?
Itaendelea.....................