Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

Baada ya mzee Mgaya kumvutavuta mama Kulwa na kumlaza sakafuni, alimwangalia kwa kitambo kidogo, huku akiwa amekasirika sana kumuona mke wake akiwa vile hakika alichukua sana.

Alitamani kuongea jambo lakini mke wake alikuwa kalewa chakari, akatoka nje na kuelekea kwenye gari lake.

Boss samahani , vipi mama anaendeleaje huko ndani maana hali yake ilinitisha sana.
Aliuliza dada wa kazi akitaka kujua.

Hana tatizo lolote, yupo sawa tu ila kumbuka kwenda kumuangalia Kila wakati.
alijibu mzee Mgaya Kisha akaingia kwenye gari lake na kwenda kwa Tausi.

Eti Samson, unavyohisi mama atakuwa kapatwa na nini maana sijazoea kumuona akiwa vile.
aliuliza dada wa kazi akiwa hakuridhishwa na majibu ya mzee Mgaya akaona samson huenda akawa anajua.

Hata Mimi sijui, kwanza wewe ndiye tuliyekukuta naye Sasa Mimi nitajuaje dada ila huenda shida siyo kubwa kwani baba asingeondoka na kumuacha.
alijibu Samson huku akiwa anabahatisha majibu yake.

Samson na housegirl waliingia jikoni wakisaidiana kazi mbalimbali, huku Samson akitekeleza Kila anachotumwa na housegirl yule hatimaye Chakula kikawa mezani,

Dada wa kazi akaelekea usawa wa chumba Cha mama yake, licha ya kugonga mlango Mara kadhaa lakini hakuna ishara yeyote ambayo ilionesha muhusika anakuja,
Akaamua kurudi sebuleni na kupakua Chakula wakaendelea kula huku akiwa na wasiwasi,

Uje Samson hapa tunakula lakini Sina uhakika na Kila nikigonga mlango mama haitiki.
Aliongea dada wa kazi na kumfanya Samson akagonge mlango kwa nguvu sana.

Hatimaye mama Kulwa aliinuka na kuja kufungua mlango sehemu ndogo sana iliyotosha kuona nani yupo nje,

Vipi unasemaje wewe,
aliuliza mama Kulwa kwa sauti ya kilevi.

Tumekuja kukuamsha maana Chakula tayari.
Samson na Dada yake walijibu kwa pamoja.

Mxieeeeew, hebu tokeni hapa, kuja kunifuata fuata ndiyo ionekane mnanijali sana au?
alijibu mama Kulwa huku akibamiza mlango na kujifungia ndani.
Samson na housemaid walitoka huku wakiwa na amani sasa, hawakujali kuhusu ukali aliowatolea ila ile hofu yao ilitoka maana walihisi labda anaumwa ugonjwa mkubwa sana.

************"*********************""*
Samson na Dada yake waligawana vyumba tayari kwenda kulala, Samson alichukua daftari fulani wenyewe wanaita Summary, akapekua pekua kama muda wa saa moja na nusu, Kisha akalala.

Hakuwa na usingizi, alianza kufikiria nyumbani kwao jinsi kulivyo, alimuwaza baba yake Mzee Elias Mgaya,alimfananisha na ndugu yake James Mgaya ambaye ndiye anayemlea kwa kipindi hicho, aligundua ELIMU ndiyo kitu pekee kinachowatofautisha James Mgaya na mdogo wake.

Hivyo akajikuta anahamasika kusoma na kuwa busy zaidi na masomo. wakati akiwaza hayo aligongewa na dada wa kazi.

Samson, samsoooon, hebu fungua kwanza huku nje Kuna tatizo kidogo.

Samson alifungua, mlango haraka Kisha wakaongozana hadi sebuleni, ambapo alimkuta mama Kulwa ametapika ovyo ovyo kutokana na pombe alizokunywa.

Kwani wewe mtoto bado upo hapa, Mimi nikajua utaondoka ukakae sehemu ambapo wewe, utakuwa mtu wa kula, kulala ikiwezekana uogeshwe na maji kabisa, yaani hapa nilipo Sina hamu kabisa na wewe , sikia nakuomba ifikapo asubuhi mapema nisikuone hapa huwezi kuniua kwa presha, Mzee Mgaya ni mume wangu tumeanza kugombana tangu miaka hiyo,lakini hakuwahi kuonesha dharau kama alizoonesha pindi akikutetea wewe.
aliongea Mama Kulwa baada ya kuwa pombe zimepungua.

Kaka samson samahani nilikuta baada ya mama kumuona anatapika nikataka nikushirikishe kama anaumwa tumpeleke kwenye private dispensary hapo karibu ila kwa maneno haya wewe nenda kalale , Mimi najua hajakufukuza pengine ni hasira zake tu usijali Samson
aliongea dada wa kazi akimuhurumia Samson kwani alimuona alivyobadilika sura ghafla.

Samson alianza kulia kwa kwikwi huku akielekea chumbani kwake,
alikuwa bado mtoto, hakustahili kuambiwa Kila neno lenye kuumiza hakuwa na kifua Cha kiume Cha kuhandle na kuhimili mambo haswa kwa mtoto aliyekulia kijijini.

Alianza kukumbuka nyumbani picha ya kitanda cha miti huku juu kikiwa na mkeka alichokuwa akikalia kijijini kwake ilimjia vyema sana, alijikuta ni afadhali maisha yale kuliko kitanda na godoro zuri lililopo pale, alilia kwa sauti lakini hakuna aliyesikia ikafikia hatua akapitiwa na usingizi bila kujijua.

***************************************
Asubuhi ile alfajiri na mapema si kawaida kwa mzee Mgaya kujihimu namna ile, aliingia huku akimkuta housemaid akifanya usafi kama ilivyo ada kwake.

Walisalimiana Kisha Mzee Mgaya akapitiliza hadi chumbani kwake,

Wewe mama Kulwa, mke wangu,
Hivi usingizi gani huo mtu unalala Ina maana hata kama nyumba imeshika moto, inaungua kwa maana hiyo wewe ni wakufa tu.usingizi wako huo wa kilevi ipo siku utanielewa tu.
aliongea Mzee Mgaya huku akifungua droo ya kabati akiangalia makablasha yake.

Ahaaaaah kwahiyo mume wangu kwakuwa upo na Malaya wako Tausi Sasa , una wazo la kuichoma nyumba yangu si ndiyo, Sasa ulipofikia ni pabaya nikiamka naenda polisi, nataka vyombo vya Dola vipime haya ni maneno gani,
Unaninyanyasa unanitesa na kunitesa, na nimeongea na mwanao Jose, nimemwambia Kila kitu Jana kasema anaahirisha shughuli zake zote anakuja muongee kwani umri wako na mambo unayoyafanya ni tofauti, na kasema hiyo takataka yako uliyoileta hataki hata kuiona na unamjua vizuri mwanao sasa tutapima unga na maji kipi kitazama.
aliongea kwa kujiamini na kwa ukali mama Kulwa huku Mzee Mgaya akipoa baada ya kutajiwa ujio wa mwanae.

Josefu James Mgaya ni mtoto wa kwanza wa mzee Mgaya, alikuwa na Elimu nzuri sana huku degree zake mbili akizipata huko uingereza, mbali na Elimu yake, akili na uwezo binafsi vilimbeba kijana yule kiasi Cha kuaminiwa na watu wengi sana, hata Mzee Mgaya mwenyewe alitamba sana na kujivunia kijana wake ambaye ni moja ya wanasheria wazuri sana.

Licha ya kijana kushawishiwa ba baba yake kuwa ajiunge na jeshi la wananchi kama alivyokuwa yeye bado dogo alikataa akiwa na kazi ya ndoto zake LAWYER.
Na kwa kipindi alikuwa anaishi Marekani anakofanyia shughuli zake.

Sasa mama Kulwa kwanini unakuwa na haraka ya kupeleka mambo madogo hayo kwa watoto, mbona yanazungumzika haya, aliongea Mzee Mgaya kwa sauti ya chini yenye upole.

Wewe, Tena unikome watoto wangu wote nimewaambia mateso unayonipa kwanza Hawa walioko karibu Leo Leo utawaona. Huwezi kunidharau kwaajili ya huyo mwanao Mimi Sina ajabu ya watoto kama watu wengine (akimlenga Tausi)
Mwenyezi MUNGU kanijalia ndiyo hao na wameshangazwa na kukudharau kwa kiwango kikubwa sana wewe unanifanyiaje hivyo. aliongea huku akitoka nje akawakuta Samson na Dada wa kazi wapo karibu na mlango,kifupi walisikia Kila kilichoongelewa huku Samson akikariri neno la kuitwa takataka.

Mzee Mgaya aliwafikiria mabinti zake wawili akajua wale huwa hawana neno, kuhusu wale mapacha wa mwisho alijua wale ni watoto mno hawana Cha kumwambia, ila Kila akimfikiria his first born Jose, alijikuta ananyongea sana huku akiishi kujipa Imani kuwa endapo akimletea za kuleta atatumia cheo Cha ubaba.

Samson alikuwa kwenye kikaango, shule aliipenda ila mambo yalikuwa magumu sana, je atafanikiwa na shule, maana mama Kulwa hakutaka hata kumuona Samson.

Itaendelea...................
 
maskini samson,ila mzee mgaya nae hana sauti kama mwanaume bwana
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

Siku ilianza vibaya ndani ya nyumba ya mzee Mgaya, Kila mtu alikuwa busy kutafakari lake, Mzee Mgaya alitoka nje akaingia kwenye gari akajiinamia kwenye usukani wa gari akiwaza na kuwazua, ni mbabe, ni mkali, ana mikwara mingi, lakini si kwa mama Kulwa, hapa palimshinda.

Au niingie ndani nikamuangushie kipigo, maana huyu huenda ataenda kweli polisi, Sasa ni vyema aende kushtaki jambo la kweli, huyu nataka Leo aniheshimu ajue Mimi ni nani
Eti, polisi, halafu ili iweje, polisi ni nani kwangu.

Yaani aondoke kwa dharau, aende huko akalewe, bila adabu bado anazidi kubishana na Mimi, eti kisa namsomesha Samson, mbona yeye ana ndugu kibao nimewasaidia, hapana hakuna namna naweza ifanya zaidi ya kumuonesha kuwa Mimi ni mume wake. aliwaza mzee Mgaya

Kwa upande wa Samson hakuweza kuisikia njaa, hata hamu ya kula ilimuisha, ila msaada pekee ambao ulibaki ni baba yake Mzee Mgaya ikabidi atoke nje ili aongee naye jambo, alijaribu kuita Mara kadhaa ila hakumpata, alijaribu kuangaza macho huku na huko hakumuona baba yake mkubwa.

Wakati akiwa kwenye movements zile kumbe Mzee Mgaya yupo kwenye gari anamwangalia tu, akishangaa kwani Samson anatafuta Nini, ikabidi amuite.

Vipi wewe mbona hutulii, naona unazunguuuuka, Nini? Hebu katulizane basi.
aliongea Mzee Mgaya kwa ukali.

Baba Mimi nilikuwa nakutafuta wewe, tena naona ni afadhali umeniita , mimi nilikuwa naona ni afadhali niende kwa mamdogo kule Temeke kwasababu naona hapa kama mama mkubwa namkera, maneno aliyoongea leo,hali kadhalika jana,naona Bora niondoke tu,nilikuwa naomba kama Kuna uwezekano unipeleke. aliweka kituo Samson.

Wewe ni mpumbavu, tena acha upumbavu wako, Tena wote msinichanganye wewe nani aliyekuleta hapa, nauliza hapa umekuja na nani? na ni kwa nani?
aliuliza Mzee Mgaya safari hii akishuka kwenye gari na kufunga mlango.

Nilikuja na wewe na hapa ni kwako.
alijibu Kwa uoga Samson.

Sasa kwanini kuniletea dharau zako, ushaanza zile habari zako za kijijini siyo, kujifanya unatoroka mara unaenda wapi, ukasababisha watu kuingiwa na wasiwasi wakihisi umekufa, ukataka kuwatia hasara wazazi wako walivyotaka kutapeliwa na mganga wa kienyeji yote ukisababisha wewe. Sasa nikwambie jambo moja kwamba wewe utaishi hapa na utakaa hapa, Mimi najijua kuwa nina wake wawili, kwanini nisingekwambia ukakae kule?

Sam, wewee, usinione mjinga Tena naomba uniheshimu na uwe na adabu kwenye nyumba hii.
aliwaka Mzee Mgaya huku akiwa hatanii na samsoni alijikuta anaogopa huku haja kubwa ikilazimisha kutoka kabla ya wakati wake.

Wakati mzee Mgaya akipiga mkwara pale nje, alisikia geti likigongwa, akaenda kufungua, huku akiingia mama fulani mtu mzima, akionekana anafahamiana na mzee Mgaya.

Haaa shemeji, kumbe shemeji bwanaa karibu sana, karibu.
Nadhani mama J yupo ndani. Karibu sana. alijichangamsha Mzee Mgaya huku akiongozana hadi sebuleni na kumkuta mama J au mama Kulwa anapata chai huku akionesha bado ana hangover maana macho yalikuwa mazito.

Karibu sana shoga yangu, mwenzangu hapa nilipo kichwa kimekuwa kiziiito, yaani sikumbuki kama jana nilikula aliongea mama Kulwa huku akicheka kivivu,

Mzee Mgaya akataka kutoka ili wale wanawake waongee wenyewe, lakini akazuiliwa na yule mama mgeni,

Shemeji tafadhali Kaa tu, Nina maongezi yanayomuhusu huyu shoga yangu, hata hivyo nimefurahi kukuona sana tu.aliongea yule mama mgeni Kisha akaendelea,

Jana rafiki na shoga yangu mama Kulwa, alikuja kwangu Mimi kama mwenyekiti wenu wa mtaa huu, lengo likiwa kukushitaki wewe, kulingana na dharau ambazo anadai unamletea, lakini Mimi kutokana na kufahamiana kwetu siku nyingi, nikaona siyo kesi, Mimi siwezi kuanza kuandaa wajumbe kwaajili ya tofauti zenu badala yake nitakuja niongee na nyinyi ndugu zanguni kirafiki kuliko mambo yenu kuyaanika Kila mahali.

Na ugomvi wenu anadai Kuna kijana mpo naye hapa lakini wewe unamkingia kifua asifanye kazi zozote, hivyo yeye kama mama mlezi
anaona hiyo haifai, ni kumlemaza mtoto, kumbuka anapaswa kujifunza uwezo wa kujitegemea, maana hata wanafunzi waliopo boarding school wanafanya kazi nyingi tu ili kuwajengea utimamu wa mwili na akili. aliongea yule mama huku akimwangalia Mzee Mgaya kwa kitendo cha kumtetea mtoto asifanye kazi,.

Lakini Mzee Mgaya hakuwa na pupa kwa kile anachokisikia badala yake alikaa kimya huku akitoa kicheko chenye hasira ndani yake.

Shoga, wewe acha tu Dunia ya leo hii huwezi kumlea mtoto kimayai mayaj kwani hujui atakuja kuangukia wapi eeh,Mimi samson simchukii nampenda sana, sitaki wazazi wake waje waone nilimharibu mtoto wao kwa kumdekeza hapana. Lazima kijana afanye kazi. aliongea mama Kulwa huku akijifanya mwema sana mbele ya shoga yake.

Lakini pia shemeji na Mimi Nina malalamiko kuhusu huyu mke wako, maana haya ya kijana wako umekaa kimya hata sijui unawaza Nini.
aliongea yule mama.

Malalamiko juu ya mke wangu, yapi hayo? aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua.

Mkeo jana kaenda kwenye Cafe yangu, bila hata kuniambia, kufika hapo kaanza kuagiza pombe mfululizo, na kulewa sana huku akiwaagizia na watu wengine, wahudumu wangu walipompelekea bili alidai yeye anaongea na Mimi na si wao, hivyo ikabidi utokee ugomvi mkubwa kutokana na kwamba wahudumu wangu nilishawaambia Cafe yangu haina nani Wala nani hivyo Kila mmoja apewe huduma sawa na watu wengine.

Kilichotokea ni ugomvi mkubwa uliosababisha uharibifu mkubwa pale, tena uharibifu mkubwa mno kanitia hasara huyu mkeo, maana baada ya kunishitakia matatizo yenu aliniambia kuwa anatafuta sehemu ya kujiliwaza ili apunguze mawazo Lakini kumbe anaenda kunitia hasara Mimi. Kalipa hela nusu, na nyingine ikabaki kwake jumlisha na kuniharibia vitu vyangu , Sasa shemeji sisi wote tumezeeka na tayari tuna wajukuu, ni sahihi kwa haya aliyoyafanya shoga yangu.aliweka kituo yule mama

Mzee Mgaya hakujibu neno, badala yake alimwambia kuwa baadae waonane huko kwenye Cafe yake na atamlipa. Kisha wakaagana na yule mgeni akaondoka.

Mama Kulwa alijifanya ana hasira akakimbilia chumbani, Mzee Mgaya akaingia na kuufunga mlango huku akitafuta mkanda fulani, akiwa hahitaji maelezo yoyote kutoka kwa mkewe. Mama Kulwa kuona macho ya mzee Mgaya akagundua hakuna usalama, pengine angekimbia lakini alishachelewa.

Samson anaivuruga familia ya mzee Mgaya huku naye akitukanwa kwa Mara ya kwanza na mtu anayemtegemea, Sasa utakuwaje kwa Tausi hawezi kwenda kwani kapigwa marufuku.

Itaendelea.......................
 
Mambo yanazdi kunoga aseeee beb njoo moneytalk
 
Piga baba akili imkae sawa mama kulwa
 
Yaani mtandike hadi amkumbuke mwalimu wake wa darasa la kwanza, naona anataka kukupanda kichwani huyo
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

Baaada ya mzee Mgaya kutembeza kichapo barabara kwa Mama Kulwa aliwasha gari yake na kutokomea kusikojulikana kwani hakumuaga yoyote.

Samson na Dada wa kazi waliingiwa ubaridi, wakiwa na hofu kwani makelele waliyasikia muda mrefu na hata walipojaribu, kumzuia baba yao aache anachokifanya hakukuwa na majibu badala yake hadi pale Mzee Mgaya aliporidhika mwenyewe na kutoka nje.

Mama, mama, mamaaaa pole mama yangu tafadhali amka nikusaidie.
aliongea kwa uchungu dada wa kazi.

Hapana mwanangu niacheni nife, hapa Duniani tunapita tu, tunaishi hakuna anayeijua siku ya kufa, na kila nafsi itaonja umauti bila kujali utakufa kifo Cha aina gani,
Nimeishi na baba yako kwa zaidi ya miaka thelathini, hajawahi kunifanyia unyama kama huu, lakini Leo kwenye uzee huu mzee wenu ameamua kuniua kwa makusudi.
Naomba nisaidie niinuke mwanangu.
aliongea kwa sauti ya chini, huku akijitahidi kujizoazoa pale chini.

Samson na dada yake waliangaliana baada ya kuona uvimbe mkubwa usoni kwa mama yao, lakini pia mkono wake wa kulia ulikuwa umevimba huku bangili zake zikiwa zimemkata, huku ikionekana fujo zilikuwa ni nyingi baada ya mrundikano wa shanga pale chini zikiwa zimekatika. Kilikuwa ni kitendo cha aibu, ikabidi asitiri urembo wake usionekane vibaya.

Alijizoazoa huku akimtuma dada wa mahali ambapo Samson hakujua, ikabidi wabaki wawili yaani Samson na mama yake huyo huku wakiwa hawaongei chochote baada ya dakika kadhaa dada wa kazi alikuja akiwa kaongozana na dada mmoja ambaye anaonekana yupo vizuri kimaisha. Wakaingia hadi chumbani kwa mama Kulwa.

***************************************
Niambie mume wangu naona umefika ukionesha umefadhaika sana vipi kwani Kuna nini? baba sijakuzoea hivyo, vipi Kuna taarifa gani mbaya umeisikia.
aliuliza Tausi Mara baada ya kumpokea mumewe huku akigundua hayupo sawa.

Na vipi kuhusu ile Safari yako ya kwenda China, maana nadhani bado siku chache tu, au umeahirisha?
aliendelea kuuliza maswali huku akiwa hajibiwi.

Tausi eeeh, hebu niache kwanza nipumzike, nyinyi wanawake mtaniua yaani hata sijajua mnataka nini, huu umri wangu nahitaji faraja nahitaji kufanya shughuli zangu bila wasiwasi lakini inafika muda nyinyi mnataka kuniongoza, kunitawala na kunipelekesha mnavyotaka.
aliongea Mzee Mgaya kwa sauti ya chini yenye upole.

Mmmmh mwenzangu hata sijui unaongea nini, ila jipumzishe kwanza mume wangu Mimi nipo nje Kuna kazi nafanya,ila narudi ndani sasahivi
aliongea kijanja Tausi baada ya kugundua kuwa ni kweli Mzee Mgaya hayupo sawa.

*************************************
Mama pole sana, jikaze tuingie kwenye gari, huu si uuaji kabisa, yaani kweli my Daddy Mzee Mgaya anaweza kufanya unyama na uuwaji kama huu, jamani ni baba mshauri, ni mwenye Elimu na hekima zake, nyinyi ni Kati ya wazazi Bora na mfano wa kuigwa kwenye mtaa wetu, kwanza unajua mama bado siamini kama ni yeye aliyekufanyia hivi.
alilalamika dada aliyeitwa muda si mrefu ili aje amsaidie jirani yake alijulikana kwa jina la Catherine au Cathy kama walivyomuita mtaani kwao.

Ni Binti mwenye maisha mazuri sana ikiwemo kumiliki usafiri binafsi wa gharama, japokuwa hakujulikana ana kazi gani au biashara gani ila alikuwa rafiki mkubwa wa mama Kulwa kutokana na uchangamfu wake.

Hapa mwanangu Nina maumivu sana hasa huu mkono wa kulia, yaani sina uhakika kama upo salama nahisi umevunjika, naomba niwahishwe hospital. alilalamika mama Kulwa

Hapana mama ni hospital gani watakupokea wewe uliyeumizwa kwa makusudi kama hivi, hapa ni kwenda kwanza polisi ukatoe maelezo yaliyonyooka Kisha watakupa PF3 ni Hilo tu Kisha nitakuwahisha hospital, aliongea Cathy huku akiendesha gari kwa speed.

**************************************
Mzee Mgaya alikaa kwa Tausi, akiwa ana mawazo kiasi japo Kila saa aliongea peke yake huku akitukana lakini bado haikusaidia ukweli unabaki palepale alikuwa na hofu.

Mficha maradhi..... Mficha maradhi
Mimi nahisi kuna kitu kinakusumbua mume wangu, Sasa sidhani kama itasaidia wewe kukaa kimya ni vyema ukaweka wazi tatizo lako, Tena unanipa tabu kukaa natabiri tabiri Nini kinakusumbua kama vile naongea na mtoto mdogo.
Usinifanyie hivyo unanitesa hata Mimi bwana. alilalamika Tausi.

Wewe niache kwanza ni matatizo yangu nimekwazana na vijana huko barabarani Wala usijali najaribu kutuliza hasira zangu tu,
alidanganya Mzee Mgaya.

Heeeee haya baba ila kuwa makini na Hawa vijana wa kisasa waliokosa heshima, yaani watoto wa siku hizi hawajui huyu ni mkubwa wala ni nani wanawaza mashindano na ligi na kila mtu.
wakati Tausi akiendelea kuongea Mara walisikia mlango ukigongwa, walipoangalia waligundua ni samson.

***************************************
Sasa hapa mama yetu inatakiwa ufungue kesi huyu mtu ni muuwaji mkubwa, kwani hasa chanzo Cha ugomvi ni nini?
Waliuliza maafande kwa mshangao mkubwa.

Jamani wanangu naomba taratibu za Hilo karatasi ili nikatibiwe kwanza hayo mengine tutajua mbele kwa mbele, alijibu Kwa mikato mama Kulwa.

Unajua Mimi ni jirani mkubwa wa huyu mama Tena ni washauri wangu wakubwa tu, yeye na yule mzee ila kwa hili nitasimama na huyu mama,
Habari Iko hivi Kuna kijana ameletwa na mzee Mgaya tangu mwezi wa kwanza akiwa na lengo la kumsomesha lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nazisikia ni kuwa Mzee Mgaya hataki yule kijana afanye kazi hata ya kuosha kijiko alichokitumia yeye mwenyewe Sasa ni binadamu gani ambaye anaweza kuvumilia huo upuuuzi.sasa huyu mama hakukubali ndipo alipoanza kukorofishana na mume wake.
alifafanua Cathy akijifanya anaijua familia ya mzee Mgaya vizuri.

Uuuwii jamani msinichekeshe Ina maana wewe mama watoto wako wote huwa hawafanyi , aliuliza afande mmoja.maana inavyookana huyo mtoto labda ni wa huyo Mzee wewe hujui tu, pengine alimzaa na kukuletea hapo akijifanya ni mtoto wa ndugu yake, yaani Mimi akili yangu inaonaga mbali sana huyo ni mtoto wa huyo Mzee, waliongea maaskari huku wakicheka.

Na Dunia mtu kukuletea mtoto from nowhere nayo ni shida, tena si tatizo dogo Mimi binafsi siwezi kuishi na mtoto wa mtu tena mume wangu nilishamwambia siku nyingi sitaki nije kuvuma ubaya kwa kuniletea watu wasionihusu. aliongea afande mmoja wa kike ambaye alikuwa anaongea huku akitafuta muhuri ambao alitafuta bila mafanikio.

Kwani mama huyo kijana bado yupo kwako na anajisikiaje unavyoumizwa namna hii jamaniiiiii, aliuliza afande mwingine ambaye anaifahamu vizuri familia ya mzee Mgaya.

Jamani maafande nawaombeni mnifanyie haraka Hilo karatasi niwahi hospital. Mama Kulwa hakutaka kuwajibu chochote maaskari wale vijana badala yake alihimiza kwenda hospital.

Sawa mama ni Sasa hivi tu, alijibu afande mmoja huku akichovyachovya muhuri kwenye kidude Cha wino ambao nao ulishaisha akapewa karatasi yake.

Tafadhali mama kwenye sehemu ambazo atajaza daktari kwenye Hilo karatasi rudi nalo hapa, ili tuje tukamilishe zoezi, na si utafungua kesi eeeh. aliuliza afande akionekana anapenda Mzee Mgaya aingie matatani.

Mama Kulwa hakujibu aliingia kwenye gari la Cathy wakatokomea kuelekea wanakohitaji kwenda

***************************************
Wewe vipi umekuja na nani,
Umekuja mwenyewe, umewezaje kufika, halafu hebu njoo kwanza huku nje tuongee .
Ni maneno yaliyomtoka mfululizo Mzee Mgaya kutokana na ujio wa Samson.

Mimi nimekuja mwenyewe, nimeshaanza kujua baadhi ya maeneo, alijibu Samson.

Sawa hakuna shida ila sitaki usimulie jambo lolote hapa ya kule yaache kule sawa?
aliongea kwa kuamrisha mzee Mgaya huku wakirudi ndani.

Itaendelea..................................
 
beb njoo umsaidie mzee mgaya huku
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom