Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

Sam anatafunwa na penzi, Tunaendelea kufuatili Mkuu ukipata muda tuwekee wasomaji tupo Jack Daniel
 
Siku anaweka nukta ndo siku nitaanza kusoma nisije kufa kwa kihoro bure.
 
SEHEMU YA AROBAINI NA TISA

Sasa kwanini uliniacha? Ina maana uliniita ili ukanitelekeze kule, kwasababu gani ulifanya hivyo? Mimi sijapenda kwakweli, unajua fika mtaa huu ni mgeni hata njia na vichochoro sijavijua vizuri, nikipotea je?
alilaumu Rahma baada ya kuachwa na Samson.

Samson alitamani kusema kitu kwa Rahma lakini alijizuia, wivu ulimkamata vilivyo,alimuona Rahma kama msaliti kwake, lakini akili nyingine ilikataa kwani alitambua vyema kuwa yule ticha bishoo alikuwa anamlazimisha tu Rahma lakini huenda Rahma hakuwa tayari. alijiwazia Samson.
Hata hivyo alijikuta anashusha Presha na hasira zake kwani kosa la Rahma hakuliona.
akaingia zake ndani asijue anaenda kufanya nini.

Samahani Sam, nakuomba uje kwanza huku jikoni maana kazi zimenielemea sana hivyo inatakiwa tusaidiane . alishauri Rahma.

Samson aliingia usawa wa jikoni huku akiwa very hurry up, kwa Kila anachotumwa na Rahma , huku stori zao zikiendelea ............

Unajua nini Sam, mimi kule shuleni kwako nitakuwa siji tena, kwasababu nimepata usumbufu mwingi sana, Kuna mkaka , sijui nani vile, ananukia mafuta mazuriiiih, eti kang'ang'ana mwenyewe kesho tuonane,
sijui anataka kuniambia nini yule, halafu kule shuleni kwenu sijui kupoje, mtu Mara akushike , Mara Hawa wakupigie mluzi, yaani fujo tupu. aliweka kituo Rahma asijue namna alivyoutesa moyo wa Samson.

Kijasho chembamba cha wivu wa mapenzi kilianza kumtesa Samson, akajikuta anapata hasira sana kwanini yule mwalimu aombe kukutana na Rahma, kwanini?
Akijua wazi hata akiwafuma kwenye stori zao,hatofanya chochote kwani yule ni mwalimu wake , na yeye ni mwanafunzi, walezi Wake Kila siku wanamsisitiza juu ya kuzingatia masomo Ili atimize ndoto zake hivyo suala hili kusikika ni kujitafutia matatizo kwa wanaomlipia ada.

Waliendelea na kazi za hapa na pale huku Samson akili zikiwa siyo zake, alitamani Yale aliyoyaona angekuwa anasikia tu, akajikaza kiume japo suala la kuibiwa demu wake likimuuma alijua fika muda wowote Rahma atakuwa na mtu.
Waliendelea kupiga stori za hapa na pale huku Rahma akiongea kwa uchangamfu kwani hakujua kuwa samson anapitia kwenye maumivu muda huo

Kwahiyo kesho ndiyo mnaenda kuonana na yule mwalimu eeeh?
Samson alijikuta aliropoka kuuliza lile swali.

Akuuuuh,! Nani aende? yaani Mimi nitoke hapa niende sijui wapi huko, namfuata mtu, hapana Hilo haliwezekani, kwanza najuta hata muda ule kwenda huko, watu hawana aibu Wala adabu yaani mtu anakulazimisha umkubali wakati ndiyo kwanza mnaonana, loooh ama kweli, tena nimegundua watu wa huku Wana tabia ya kuona Kila kitu kwao kinawezekana , wanajiona
Kama wanastahili kukubaliwa na Kila mtu wajinga hawa.

Halafu sikia Samson,
Nahitaji kuishi hapa kwa heshima na adabu, kwanza siyo kwetu, Mimi Sina undugu na nyie, umesahau baba Mzee Mgaya aliniambia ukweli kuwa nisijione nyie ni ndugu zangu?
aliongea Rahma huku akimkazia uso Samson kuonesha anamaanisha ayasemayo.

Tambua kuwa nitakapo onesha tabia yeyote mbaya hapa, ni rahisi tu kuambiwa niondoke,
Haya nikiondoka naenda wapi kwa Tausi? Hapana huko siwezi kurudi nitatafuta popote pa kuishi lakini siyo kwa mamdogo Tausi. aliweka kituo Rahma.

Sasa Rahma, kwanini uhangaike pa kukaa kwani si urudi kwenu Tanga, siyo kwamba nasema hapa utafukuzwa, ila najaribu kuvuta picha kama ikitokea hivyo. aliuliza Samson.

Rahma alimwangalia Samson huku uso ukionesha umesawajika kwani ulikosa nuru Kisha akacheka,
Ni kicheko ambacho hakikuwa cha furaha bali ni chakujihurumia.

Samson naomba ujue kuwa mimi ni yatima,kwanza sijawahi kumuona baba yangu mzazi hata siku moja, hata mama yangu mzazi alikufa nikiwa mtoto mdogo sana , japo namkumbuka sana mama yangu.
(aliongea Rahma kwa sauti ya chini huku akitaja maneno fulani ya kiarabu ambayo Samson hakuyaelewa)
Kisha akaendelea....

Asili yetu sisi ni wakimbizi na nimezaliwa kwenye kambi za wakimbizi huko Handeni, Tanga .
ambapo walionilea wanasema mama yangu hakuwahi hata kuwaonesha baba yangu ni nani, wapo wanaosema yupo Lamu, nchini Kenya, wengine wanasema alizamia kwenda Italia. lakini yote kwa yote mimi sijui, kwani naambiwa pia nina asili ya kisomali, lakini somalia yenyewe naisikia tu wala sijui inafananaje, alizidi kufafanua Rahma.

Nasikia nikiwa na umri wa miaka mitano, mama yangu alitoroka kwenye zile kambi na kuja Handeni kwa wenyeji au wazaliwa wa pale, chanzo cha kutoroka inasemekana alikuwa anamkimbia mwanaume mmoja aliyekuwa anamsumbua wakati mama yangu hamtaki.

Basi alipokelewa na bibi mmoja ambaye aliishi na mama kama mtu na mwanaye, tuliishi kwa upendo wa hali ya juu, huku baadhi ya watoto wake wakiwa tayari Wana familia zao japo walikuwa wanaishi na vibanda {nyumba} vyao vikiwa karibu na pale pale, siku moja nikiwa natoka madrasa , fulani ambayo ilikuwa si rasmi sana ila ilianzisha na wanakijiji wa pale ili watoto wao wasiende mbali sana, huku sheikh mmoja akijitolea nyumba yake kama sehemu ya kusomea. alifafanua Rahma.

Samson alikuwa makini sana akimsikiliza Rahma, ilikuwa ni stori tamu kwake maana tangu afahamiane naye hajawahi kupiga stori kama ile,
Rahma akaendelea.......

Sikuweza kusoma hizi shule zenu kwasababu, mama yangu alinikataza hasa ukizingatia hakuwa na uraia kamili kwenye nchi hii, hivyo ikapelekea kutokusoma huku pia misimamo ya Dini ya mama yangu ikichangia akidai Elimu hii ni ya upotoshaji.

Basi siku moja mama aliniita akaniambia kuwa anaumwa sana, na hata mwili wake ulionesha akiwa amekonda sana, na miguu ikiwa imevimba sana, alijikongoja akaniandalia chai ili niwahi kwenda chuo, licha ya kuwa anaumwa sana ila hakutaka niteseke, nilipomaliza kuinywa ile chai mama aliniita kwenye chumba kidogo tulichokuwa tumelala huku kukiwa na giza kwani hakikuwa na dirisha kubwa,
Alianza kunitamkia kuwa ananipenda sana na kunikumbatia kwa nguvu huku akilia, kwa wakati huo sikujua ana maana gani.

Alinisihi kuwa niwe mcha Mungu sana , na nisiwe na tamaa wala kuwa mwenye kibri chini ya jua, badala yake niwe mwenye Heshima na Taadhima, na haya yote hutoka kwa yule mchamungu pekee hivyo akasisitiza nimche na kumtegemea ALLA'H kwani yeye ndiye muweza wa yote . safari hii Rahma aliongea kwa uchungu sana.

Nilienda chuo , nikarudi na kukuta watu wengi pale tulipokuwa tumeishi huku, wanawake wakiwa wanachota maji, na baadhi ya wanaume wakiwa wanasogeza kuni na baadhi ya wazee wakiwa wamekaa vikundi vikundi , nilitaka kuingia ndani lakini nikazuiwa huku nikishikwa mkono na yule bibi akinizungusha nyuma ya nyumba na kuniambia nicheze na watoto wenzangu.

Lakini nilimuuliza nikacheze vipi wakati sijamuona mama yangu? Yuko wapi, yule bibi alinijibu kuwa mama kaenda hospital hivyo wanajiandaa kwenda huko, lakini kabla hajamalizia alikuja Mzee mmoja akamwambia bibi kuwa vipi mpango wa sanda unapatikanaje?
Hapa ndipo nilipogundua kuwa mama yangu sipo naye tena. aliweka kituo Rahma.

Samson alishusha pumzi kwa nguvu huku , akijaribu kuvaa uhusika na kuhisi maumivu makali sana, akauliza, baada ya hapo ilikuwaje?

Niliendelea kuishi na yule bibi maisha yote huku akiwa kama mzazi wangu kwani aliendeleza pale alipoishia mama , huku akinilea kwa maadili sahihi kabisa, huku akiniambia kuwa wenye familia yake ana mtoto wa mwisho anayeitwa Salma, hata hivyo ameamua kuwasaliti na kubadili Dini nakuwa mkiristo kitendo ambacho kiliwaudhi sana familia na baadhi wakimtenga kabisa, kwa wakati huo sikuwa namfahamu hadi alipofariki yule bibi ndipo akaja kijijini nikamtambua.

Baada ya kufariki yule bibi mlezi nikaenda kwa mamdogo mtoto wa kwanza wa bibi ndipo nilipokulia, ndipo mwaka Jana alipokuja Tausi nakuniomba kuwa anataka nije niishi naye Sasa nashangaa kwanini yupo hivyo ilhali ndugu zake Wana roho nzuri? aliweka kituo Rahma kwa mfumo wa swali.

Ndipo Samson alipogundua mambo mengi sana, kuwa kumbe Tausi na Rahma hawana undugu wa damu kumbe ni kusaidiana tu, akiwa anawaza vile alisikia honi ya gari mfululizo huku akikurupuka kwenda kufungua geti , akamuona Mzee Mgaya akihangaika kutaka kupanda ukuta ili aje afungue,
Akawafungulia huku akijua kazi ipo maana alikutana na sura zenye hasira huku mama Kulwa akionesha kukasirika zaidi.

Itaendelea............... ...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom