Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,042
- 16,872
- Thread starter
- #341
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
Mida ya saa kumi jioni, Samson alimuaga mama yake kuwa anaenda kwenye group discussion ambapo hakukuwa mbali na nyumbani kwao.
Sasa Sam mwananguuuu, kwanini Kila siku wewe uwe unaenda kusoma huko na kumbuka umekuwa ukirudi usiku, kwanini hao wenzio na siku moja moja wasije hapa kwako?
aliuliza mama Kulwa.
Sawa mama nimekuelewa sana, ila sisi kwenye group letu tumependekeza kukutania kwa mwl {akitaja jina} pale Kuna wanafunzi wa madarasa ya juu nao huwa wanafanya discussion zao pale, hivyo tumeamua na sisi kukutana pale ili pindi kama Kuna mada inatushinda basi tunaomba msaada kwa wenzetu.alijibu Samson.
Sawa ila kumbuka kuzingatia muda,maana huu mji tunaujua wenyewe, alitahadharisha mama Kulwa.
Wakati Samson anatoka nje ya geti,
Hamadi, alikutana na Tausi au mama yake mdogo akiwa anashuka kwenye Taxi, wakasalimiana,
Enheee vipi mwenzetu na mabegi wapi tena, aliuliza Tausi.
Naenda nyuma tu hapo huwa tunajisomea na marafiki zangu,alijibu Samson akitaka kupiga hatua kwenda atakapo.
Lakini akashikwa mkono na Tausi.
Vipi Baba yako Mzee Mgaya yupo? Maana ana siku kadhaa nyumbani hajaja? Tausi aliuliza.
Hapana baba yupo nje ya Dar, kaenda sehemu ambako amesema anataka kwenda kufanya mahesabu kwani kapata tenda ya kutengeneza milango ya shule. alijibu Kwa kifupi Samson.
Vizuri sana,hebu nambie huyu mpumbavu Rahma bado yupo hapa, maana mtoto mjinga sijapata kuona, yaani siku ya tano kang'ang'ania kukaa hapa anadhani Hawa nao ni ndugu zake? Hebu kwanza niingie ndani. aliongea Tausi huku akisukuma mlango wa geti dogo kwa nguvu Samson kuona vile ikabidi naye aingie ndani maana alijua hali huenda isiwe shwari.
Haya niambie wewe mtoto Malaya usiye na mipaka, usiye kuwa na adabu, umekaa hapa siku zote hata aibu huna mtoto wa kike, haya tufanye anatokea mtu anakuuliza huyu mama upoje nae, utamjibu nini?
Maana si ndugu yako, Wala wewe si mfanyakazi wake, halafu unawezaje kuwaamini watu baki kiasi hicho? Kipindi nakuleta mjini nilikuasa kuhusu, mazoea au kumwamini mtu haraka, lakini wewe msungo usiyefundwa husikii Wala huelewi.
Tausi alizidi kuropoka huku akiwa hajasalimia mtu yoyote mle ndani.
Wakati huo mama Kulwa alikaa kwa kutulia akiwa anamtazama Tausi kwa umakini namna anavyofoka, huku Rahma akiwa kasimamisha zoezi lake la kufua akiwa nusu nusu ,asimame, au akae,
Amjibu Tausi au asimjibu,
Uso wake ulionesha hasira za wazi huku akionesha anataka kulia.
Najua, tena najua kilichokuleta huku, na nikwambie tu kuwa wakijua lengo lako, watakufukuza kama mbwa Malaya wewe, mtoto mdogo unaendekeza ukahaba, najaribu kukuonya unanikimbia,
Tena unakimbilia kwa watu tu ambao si ndugu zako, kwanza ngoja nikuoneshe, Tausi alimrukia Rahma na kutaka kumpiga, bahati nzuri mwanaume mmoja mwenye nguvu aliwatenganisha huku naye akiwa na malalamiko kadhaa, si mwingine ni dereva Taxi aliyemleta Tausi.
Wewe dada mimi unanichukuliaje?
Hebu nipe hela yangu, Mimi niondoke hela tena nimekufanyia msaada tu kutoka kule hadi huku mbali hivi ningejua nisingekuja, alicomplain yule dereva.
Kwani Kuna nini baba, tena nashangaa unaingia ndani kwangu bila hata hodi, aliuliza mama Kulwa.
Samahani sana mama, Mimi ni dereva nimemleta huyu aunt, Sasa nashangaa ananisubirisha hapo nje, halafu alivyopanic nikaona atanichelewesha, Mimi natafuta hesabu mama. aliongea kwa uchungu dereva.
Acha ujinga na wewe uliambiwa hela yako sikupi, kwanza pale kituoni hata sikukuita wewe, ulijipendekeza tu,umri huo bado unagombania abiria na vijana,Mimi dereva wangu huwa ananivumilia, aliongea Tausi huku akimrushia hela yule jamaa,Kisha dereva wa watu akaiokota ile hela na kutokomea
Hebu watu wote njooni ndani kwanza na Samson funga geti na kufuli maana naona watu wanaingia tu humu kama choo cha umma.
Kwanza mdogo wangu Tausi nikusalimie, eeh nianze Mimi maana mtoto wa kike umefika tu na kuanza kutiririka maneno bila kujali hii ni nyumba ya mtu mwenzangu
Aliongea kwa utulivu mama Kulwa.
Kwanza dada nisamehe tu, kwakweli Nina jazba sana, huyu Binti alichofanya mpaka Sasa simuelewi nashindwa nikulaumu wewe au yeye,
Wewe dada umewezaje kukaa na mtoto wa mtu sikuzote,
Na yeye anawezaje kukaa kwa mtu muda wote huo? Tausi alianza kumlaumu mama Kulwa.
Tausi, nakuita kwa jina lako, Kuna vitu vingi unakosea na vinakushinda, kwanza unakosea kuniuliza hivyo,
Umekuja hapa umeanza kupiga kelele kwenye nyumba yangu sijakuuliza. nimekuita kwa upole tuongee ndani tuweke sawa haya mambo, umetukana weweee lakini nimekuacha tu, hii ni nyumba yangu inaheshimika na watu wengi, unadhani watu waliosikia neno Malaya na matusi kibao uliyotukana watatuchukuliaje wakazi wa humu,
Sasa naelewa kwanini Mzee Mgaya kasema Samson arudi hapa, labda ni nidhamu mbovu uliyokuwa nayo.
Unasema Rahma siyo ndugu yangu ni kweli, lakini huwa Kuna sababu zinazofanya watu wajenge undugu, wote hapa watatu nyinyi Mimi kikawaida siwajui.
Wewe ni mke wa mume wangu, hivyo tayari una undugu na Mimi.
Samson ni mtoto wa shemeji yangu hivyo ni mwanangu pia,
Huyu Rahma kakimbilia hapa pindi mmekwaruzana, najua alijua ni wapi anaenda asingekuja hapa kama hatufahamu sisi, huo ukurasa naufunga haya naomba shoga yangu uniambie Nini kinasababisha ugombane na Binti mdogo kama huyu, yaani kwanza inashangaza ujue,
aliweka kituo mama Kulwa.
Dada nisikufiche huyu mtoto, ana tabia mbaya sana na ndugu zake wanamtafuta wanasema nimsafirishe aende nyumbani kwao Tanga, Mimi sitaweza kukaa naye kwasababu tutakuja kufikishana pabaya, alileta sababu za uongo Tausi.
Mnajua wawili nyinyi mna ugomvi mkubwa sana halafu mkiulizwa mna majibu mepesi sana, yasiyoingia akilini, sasa niseme tu wazi kuwa, Mzee Mgaya anarudi leo hii na yeye ndiye atakuja kumleta rahma kwako , maana kwa hali hii nawaona kabisa mlivyo kama paka na panya hivyo sitaruhusu huyu aondoke.
Mama Kulwa samahani Mimi Kwa mamdogo siendi na kama narudi Tanga nitatokea hapa, ananiita Malaya wakati umalaya kaanza yeye, au anafikiri sijui tunachogombania, Mimi kwanza sitaki kwenda Tanga Wala wapi Mimi kama mtataka niwe mfanyakazi wa humu ndani, nitakubali ila si kwenda kwa mamdogo. aliongea Rahma akionesha kukerwa na akimaanisha liwalo na liwe.
Mama Kulwa alizidi kushangaa tu kwani hakujua chochote,
Kwa upande wa Samson alianza kuona hata njaa inapotea ghafla,
Na hofu kubwa ilitanda moyoni mwake, aliona jinsi Rahma na Tausi walivyo na hasira, na kwenye hasira mtu anaweza kuropoka chochote kile bila kujali itakuwaje na majuto huja baadaye.
Eti Sam wewe umeishi na Hawa watu kipindi kirefu, vipi huwa wapo hivi hivi maana siwaelewi?
aliuliza Mama Kulwa.
Sijawahi kuiona hii hali, ndiyo kwanza naona, siku zote tuliishi kama ndugu tukiwa na furaha sana tu Sasa hata sijui ni kwanini inakuwa hivi, watu hawaeleweki. alijibu Samson.
Halafu wewe mpuuzi wewe ndiyo chanzo cha matatizo yote, Sasa nitakukomesha mchawi mkubwa wewe, kila sehemu ukikaa wewe lazima kutokee matatizo na Dada nikwambie tu kuwa huyu mwanga kurudi hapa lazima kutatokea matatizo utakuja kuniambia.
aliongea Tausi huku akibana mkoba wake na kutoka nje kwa hasira.
Samson nenda kafungue mlango maana Mimi hata siwaelewi ngoja arudi mzee Mgaya atajua cha kufanya, yanini Mimi niumize kichwa kwa watoto wasio wangu. aliongea kwa dharau mama Kulwa.
Wakati Samson anafungua mlango ili Tausi atoke, Tausi akavunja ukimya.
Samson naomba haya masuala yasikuumize kichwa ila sharti langu ni Moja naomba uage si bado mapema! Jifanye unaenda kwa marafiki zako, halafu twende kwangu, na usipofanya hivi, nitamwambia Mzee Mgaya ulitaka kunibaka na Nina ushahidi maana Kuna bukta yako ya blue ninayo. aliongea Tausi akiwa hatanii.
Moyo ulimuenda mbio Samson ni kweli nguo yake ilipotea na aliitafuta bila mafanikio ila alipuuza tu kuwa huenda ilipotea, hakuwaza kuwa imechukuliwa na mtu, na kutokana na alivyotishwa ilibidi atii amri ya Tausi.
Sasa mamdogo inabidi utangulie si vizuri kuongozana, alijitetea Samson
Hilo mimi silijui, uje usije utajua mwenyewe. alijibu Kwa kujiamini Tausi hasa baada ya kuusoma uso wa Samson na kukiri kuwa ana uoga fulani akajiona kasukuma kete ya ushindi akaondoka zake.
Muda wa saa mbili usiku, Samson alifika kwa Tausi akimkuta yupo na kanga tu huku akionesha hajavaa kitu chochote ndani.
Habari za muda huu mamdogo, alisalimia Samson.
Huko kijijini kwenu ulikotoka mama yako mzazi hana wadogo zake ambao utawaita mama zako wadogo? au mama yako alikwambia na Tausi naye umuite mama yako eeeh. aliongea Tausi huku akitabasamu kimahaba.
Sasa nikuiteje? Samson aliuliza huku ujio wa huku akiwa hajaupenda ni kwasababu alilazimishwa tu.
Wakati Tausi akijiandaa kuja mahali alipo Samson, mlango ulisukumwa , do mwingine alikuwa ni Mzee Mgaya akiwa na mfuko mdogo, Tausi alimrukia na kumkumbatia Mzee Mgaya akijifanya alim miss sana.
Habari za siku my husband mbona ghafla halafu nilienda kumfuata Rahma kule kwa Dada mama Kulwa nikaambiwa umesafiri my mbona hukuniaga ? aliongea kwa kujibebisha Tausi.
Subiri nitakwambia, ndiyo maana nimekuja, halafu mbona mnaacha geti wazi vile halafu, mmekaa tu ndani bila wasiwasi, mmesahau timeshaibiwa Mara ngapi humu ndani ohooooh haya nyie jisahaulisheni tu.
aliongea Mzee Mgaya huku Samson akijikuta ni yeye alisahau kufunga.
Mke wangu kwanza samahani niliondoka ghafla nilienda huko njia za kusini lakini ni vijiji vya katikati tu ndani ya Mkoa wa Pwani. Kunaitwa Ikwiriri, huko nimegundua upatikanaji wa miti ya furniture kiurahisi, ingawaje nimekaa siku chache ila nimefanikiwa kupata data kadhaa ambazo nimezipenda na uzuri hapo ni jirani yaani kwa gari binafsi ni masaa mawili na nusu tu kutoka hapa mjini. alifafanua mzee Mgaya
Sasa my hujaja na gari umeacha wapi,maana ujio wako sikuzote huwa ni honi ya gari nashangaa leo umekuja kimyakimya.
aliongea kwa kuzuga Tausi.
Wala sijaja kimyakimya, ni kwamba lazima ningegonga geti, lakini lilikuwa wazi eti. Nikajikuta naingia kwa tahadhari nikijua labda ni wezi.
Kuhusu gari nimeliacha huko huko, kwasababu limeharibika yaani gari linanisumbua acha tu hata hivyo Kuna fundi nimewasiliana naye ataenda kulivuta ataleta mjini na pia najipanga ninunue lingine maana ipo siku lile gari litanilaza porini.
aliongea Mzee Mgaya huku wote wakicheka kasoro Samson aliyekuwa na hofu.
Halafu mke wangu, huu uvaaji gani mbele ya mwanao, na kila siku nakwambia mbona huelewi wewe.
Halafu huyu Sam naye hapa kafuata nini,? Eti Sam ulisahau Nini hapa. aliuliza
Kuna vitabu vyangu , kule nyumbani sivioni Sasa nikimuuliza mamdogo kama aliviona akadai yeye hajui, nikasema basi nitakuja kuangalia mwenyewe. aliongopa Samson huku Tausi akitoa tano ya hewani jinsi Samson alivyojitetea .
Mzee Mgaya aliwaangalia Tausi na Samson kwa zamu Kisha akainuka na kuingia chumbani bila kusema chochote.huku ikionekana hajaridhishwa na majibu ya Samson
Itaendelea...................