Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA AROBAINI NA TATU

Tumbo lilianza kumvuruga Samson, hata miguu ilimuishia nguvu alimwangalia Tausi kuona labda ana uamuzi gani, lakini akamuona kama mtu aliyekata tamaa.

Lakini huyu mamdogo nilimkatalia Mimi, kwanini kaniponza, ina maana ndoto zangu zinaishia hapa, aliwaza Samson huku akinyonga ufunguo wa mlango, alishtuka kumuona Rahma akiwa mlangoni akiwa kajifunga kanga tu.

Hivi wewe unalala usingizi wa aina gani , mtu nagonga mlango hadi nachoka. aliongea Rahma huku akilazimisha kuingia ndani, Samson akamzuia.

Wee vipi, mbona unanizuia? sikia nikwambie Mimi bwana nashindwa kulala peke yangu, siwezi kabisa tafadhali naomba niruhusu niingie. aliongea Rahma kwa sauti ya chini.

Sawa nimekuelewa ila kwa leo, siko sawa naomba uje siku nyingine, sawa? alijibu Samson huku ile presha ya uoga ikishuka taratibu

Halafu unajua Samson sikuelewi kabisa, kwani umepatwa na nini mbona upo mbali na Mimi kwa kiasi hicho? Sawa hakuna shida wewe nidanganye tu, unajua wazi kuwa kuanzia kesho hutakuwa tena hapa, sasa kwanini tusimalizane kabisa bwanaa. alilalamika Rahma huku akiondoka kwa hasira na kukimbilia chumbani kwake.

Samson alishusha pumzi kwa nguvu sana huku akirudi ndani alishangaa kumuona Tausi yupo karibu kabisa na mlangoni akiwa katulia tuli.

Sasa nimejua Kila kitu kuhusu wewe na Rahma na hata hicho kiburi alichokianza nilikuwa sijui kitu, Sasa Kila kitu kipo hadharani,nimesikia Kila kitu.aliongea kwa sauti ndogo ila yenye ukali.

Samson alijaribu kumsogelea Tausi lakini alisukumwa kwa nguvu akajikuta anaangukia kitandani, akabaki kushangaa tu, japo alijua kuwa mambo yameshakuwa magumu.

Lakini kwanza kwanini nijitese wakati huyu mama kaja mwenyewe? tena kwanza kesho nahama hapa Nini kinanitia hofu, au nimfuate tena Rahma nije nimalizane naye maana naye anaonekana anataka, ila Rahma kanikosesha raha mjinga huyu maana mamdogo ana mapaja mazuri kuliko yeye, ila ngoja nikamgongee Rahma.
aliwaza mawazo Yale ya kijinga huku akipiga ngumi hewani kuashiria ushindi.

Akainuka , akaanza kunyata hadi karibu na mlango wa chumba cha Rahma, ila kabla hajagonga mlango alisikia sauti ya Tausi chumbani kwa Rahma ikionekana wanagombana, ikabidi arudi kwa kasi chumbani kwake ili asijulikane kama alikuwa pale.

Alijifunika shuka gubigubi huku alifurahi kwa kujiona kidume baada ya kuona tupu za wale wanawake wote.
Kesho asubuhi na mapema alikuwa nyumbani kwa mama Kulwa huku akimkuta Mzee Mgaya akiwa nje anafungua tairi za gari.

Sasa na wewe jana tuliongea nini na umefanya nini, eeeh wewe unatakiwa uwe na msimamo wa kiume, yaani mtu anakuhadaa anakuambia ulale na wewe unakubali tu, hata kaka yako Jose aliishiwa nguvu baadaya kuona umeshakubali. alilaumu mzee Mgaya bila hata salamu.

Sawa Mzee , wewe unamjua mamdogo akilazimisha jambo kwahiyo nikajikuta nipo njiapanda kwakweli, alijitetea Samson.

Acha habari zako wewe hebu kaweke vifaa vyako uwahi shule, mwanaume mzima eti umezuiwa na wanawake, acha upumbavu wewe, kwanza baadaye ukirudi tuna maongezi na wewe, lazima upewe taratibu za kuishi hapa. aliongea kwa ukali Mzee Mgaya.

***************************************
Samson akiwa darasani mtu fulani alianza kumfikiria Mzee Mgaya, alijiuliza kwanini kawa mkali vile kwani Kuna nini kakosea, alikumbuka kitendo alichokifanya yeye na mama yake mdogo Tausi, aliangalia muonekano na haiba ya mzee Mgaya, heshima aliyonayo kwenye jamii, ushawishi, namna anavyoheshimiwa na vijana wake wa kule kwenye Karakana namna watu kadhaa kuja kujiuliza mambo mengi kwa yule mzee, akajikuta moyo unamsuta sana, kidogo akaanza kuliona kosa kubwa kabisa alilomfanyia yule mzee.

Mtu pekee ambaye alimpambania toka kwao kijijini, huku matokeo yake akipewa mtu mwingine, lakini Mzee Mgaya ndiye aliyepambana na kuhakikisha Samson anapata haki yake ya msingi ya kupata Elimu,
Gharama zote Chakula, mavazi, matibabu na dharula zote ni juu ya mzee Mgaya. Sasa iweje nije kulala na mke wake? Samson alijikuta anajuta sana kwa kilichofanyika alihisi ana dhambi isiyosameheka.
aliendelea kuwaza mambo mengi huku akiwa kajiinamia kwenye meza.

alishtuliwa na mwanafunzi mwenzie akiambiwa mwalimu wa nidhamu ambaye alikuwa anafundisha somo la Jiografia, akiwa anaingia kwenye kipindi chake. Hata wanafunzi waliposimama ili wamsalimie aliwaashiria wakae, akaanza kuandikaandika vitu ubaoni, Mara baada ya kumaliza alikuja kwenye meza ya Samson,

Unajua wewe nimechungulia dirishani, takribani dakika tano naona hujishughulishi kama wenzako, husomi yaani umelala tu, kwanini? Hapa shuleni hujaja kulala sawa, jitahidi sana kuwa active na kilichokuleta, na hili ni kwa wanafunzi wote siyo mnakuja halafu mnazidisha michezo na utani, wazazi na walezi wenu wanahangaika huku wakijinyima baadhi ya vitu ili mpate kusoma. muwe na huruma na ada za walezi wenu.

Maneno yale yalimgusa sana Samson huku akijikuta anajaribu kujichangamsha lakini bado hali ilikuwa mbaya sana kwa upande wake, mawazo yalimelemea sana.

Mida ya saa tisa alasiri alikuwa ameshafika nyumbani huku akikaribishwa vizuri na mama Kulwa pamoja na Jose,

Aisee dogo mambo vipi nasikia asubuhi ulipita hapa tulishindwa kusalimiana kwasababu nilikuwa nimelala, ila naomba tuongee wawili jambo fulani,
Wakatoka nje ya geti wakawa wanapiga stori huku wanatembea huku wakiizunguka fence ya nyumba yao.

Unajua dogo nakuomba sana pambana na masomo, komaa na masomo ndiyo urithi pekee na wa kudumu maishani mwako,
Najua tabia ya mama yangu mzazi, najua tabia ya mzee wangu, lakini nakuomba uishi kwa kujifanya mjinga ili utimize malengo na ndoto zako , nilipanga kukufanyia mpango ili ukasome pamoja na akina Kulwa lakini wazee wangu nao.......
Ila tuache tu bado shule uliyopo siyo mbaya ukikaza buti mbona unatoboa vizuri tu mdogo wangu,

Pia lingine ni kuhusu mamdogo Tausi, naomba nisikufiche wala kupepesa ni kwamba punguza mazoea ya kwenda kule, yule nilivyomuona hafai kuishi na kijana mdogo kama wewe, yaani lazima uishie njiani, nakwambia hutofika popote pale, safari ya kuisaka elimu inahitaji ukatae baadhi ya mambo ukae nayo mbali kabisa.

Lakini kama ilikaa kwa mamdogo Tausi basi huwezi fanikiwa yule ana tabia mbaya, hana heshima wala adabu, hebu fikiria jana alivyokusifia Mara sijui wewe ni handsome, kulikuwa na ulazima gani wa kuzungumza vile kama siyo ukahaba wake tu yule.

Na miaka yote nitamlaumu Mzee Mgaya, yaani kitendo cha kuwa na yule mwanamke kilimshushia hadhi na thamani vibaya mno, yeye mwenyewe anajua namna alivyodharaulika na kupoteza baadhi ya marafiki kwa kuwa karibu na yule mwanamke.
Masikini Jose alijikuta anafungua mwavuli wakati ameshalowa, kama maji yalishamwagika.

Samson alijikuta anachomwa vilivyo na maneno Yale hakika alikuwa mithili ya aliyechomwa na mwiba mchungu, alijikuta anawaza mbali sana.

Mdogo wangu, siyo Kila mwenye pesa au mafanikio amesoma hapana, ila nakwambia kuwa njia rahisi ya kuweza kufungua milango ya mafanikio ni Elimu, Elimu, Elimu alisisitiza Jose huku wakirudi ndani baada ya kupiga stori kadhaa.

Itaendelea.............................
 
hakika Jack Daniel, upo vzuri ktk Simulizi ya Mikasa..

Samson ndio Jack Daniel Mwenyewe kutoka Mufindi, Tarafa ya Sadani code yangu ndio inaninukia ivoo
 
Tunaendelea kufuatilia mkuu kongole sana kwako
 
Usijali Mkuu apo ndipo utakapo pata fursa ya kuona kivutio cha utalii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom