SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
Wakiwa ndani ya gari wakiwa wanne wakikamata highway kuelekea kwa tausi, huku dereva akiwa ni Jose akiendesha gari kwa umakini huku akipiga stori kadhaa na mama yake mdogo Tausi ambaye alikaa siti za nyuma pamoja na Rahma,huku mbele wakiwa ni dereva Jose pamoja na Samson.
Dah hili gari liko vizuri sana, yaani bi mkubwa hapa alicheza vizuri sana, maana nilikuwa Kila nikimshauri anunue gari ananiambia bado kwanza , hata nilipomwambia nimuagizie gari, aliniambia nisubiri kwakuwa ana hitaji gari la ndoto zake, nakumbuka jinsi wanawake wenzie walivyokuwa wanamcheka kuwa eti anayaishi maisha ya kizamani, ni kweli hata sisi watoto wake tuliumia kwani tuliona uwezo wa kumiliki chombo anao Sasa kwanini iwe hivyo. alizungumza Jose huku akionekana analifurahia lile gari.
Dah hongera zake kwa kweli yaani sikujua kama kanunua gari dada yangu kiukweli , yaani ni msiri ajabu,
Mambo yake huwa hawezi hadharani, hivi na mzee Mgaya atakuwa alijua kweli? alimalizia Tausi kwa mfumo wa swali.
Ni kweli baba hana taarifa na kachukia kiukweli, nafikiri baada ya kuweka sawa haya mambo ya Samson yatafuata haya, ila dah ni
Hatari sana kwanini mama naye amiliki chombo kikubwa kama hiki bila kumtaarifu Mzee?
Hata kama ni kwa hela zake, Kuna vitu vidogovidogo unaweza kununua ukaweka ndani na usiulizwe, lakini kwa hili hapana, hata sijui nitaanzia wapi kuliweka sawa hili suala. aliongea Jose huku akitoa kicheko fulani cha kujihurumia.
Huu ni muda muafaka wa kurudisha maelewano, huruma, Upendo na kuijenga amani kwa misingi imara huku wakimrudia MUNGU zaidi, lakini wao Wana visa urafikiri watu wa wapi sijui, nashukuru wazazi wangu wote wamejaliwa uwezo na upeo fulani kiasi chake na ndiyo maana si haba , kwani wametuandalia angalau urithi wa Elimu, na ndiyo maana nilifurahi sana kusikia Father ameamua kumsaidia huyu mdogo wangu Samson, kwahiyo licha ya kuwa hatuna Elimu ya viwango vya juu kama wengine, lakini angalau mambo si mabaya.
Jambo pekee linaloniumiza ni hili la wao kutokuelewana, Tena Kwa umri waliokuwa nao yaani nasikitika mno, nimekuja kujipumzisha angalau nifurahi na wazazi wangu lakini hali imekuwa tofauti, ukikaa na mama unapokea malalamiko haya,
Ukikaa na mzee naye ana malalamiko yake,basi hali ya hewa imechafuka, ila nitajitahidi kuhakikisha Kila kitu kinakuwa sawa, alizungumza Jose kwa hisia sana akionesha hapendezwi na yanayoendelea.
Usijali baba yangu wakati mwingine sisi tulioingilia ndoa za watu huwa tunajikuta labda ndiyo chanzo cha ugomvi kwa familia za watu. aliongea Tausi huku akitoa kicheko Cha kishangingi na kumfanya Samson ageuke na kumwangalia mama yake mdogo Tausi huku akitabasamu.
Hivi mwanangu Jose huyu Samson ni ndugu yenu kweli, maana kwa kiasi fulani ni kama hafanani na nyinyi.aliuliza Tausi.
Ingawaje wazazi wake siwafahamu ila yeye Samson kafanana na mama yake mzazi, kwani familia ya marehemu Babu yetu Mzee Mgaya ambaye namfahamu kwani aliwahi kukaa kwetu zaidi ya mwaka, yeye ni mweusi na wanae karibu wote wamefanana naye, yaani alivyo baba yangu ndivyo alivyo baba yake Samson. alijibu Jose kwa kifupi.
Najua mamdogo huwa unanishangaa sana, ni kweli anavyosema kaka Mimi nimefanana na mama yangu kwakuwa alizaliwa Sehemu moja inaitwa Kalenga, na hiyo sehemu kwenye historia Karne ya kumi na nane huko, waliishi waarabu wakifanya biashara ya watumwa, hivyo wameacha masalia ya watu kadhaa wenye rangi kama mama yangu. alizungumza Samson akiwa serious na kuwafanya watu wote wacheke.
Wee dogo haya mambo umeambiwa na nani na sina uhakika kama historia ipo hivyo. aliuliza Jose kiutani.
Ni kweli kabla hata sijaanza shule niliambiwa hivyo na hata tulipoenda kwa Babu mzaa mama niligundua familia nyingi wapo vile. alijibu Samson akiamini ana uhakika na alisemalo.
Yes kipindi nahitimu chuo kikuu ilifanyika sherehe , walialikwa watu wengi ikiwemo wa kutoka kijijini, hivyo nilitambulishwa mama yako Samson huku nilishangaa kumuona yule mama nikajiuliza Sasa kwanini huyu naye anakubali kukaa kijijini? aliongea kwa utani kwa Samson.
Ila tuache masikhara jamani, Samson ni handsome tuseme ukweli, tena ukichanganya na upole wake, ndiyo kabisa anazidi kuvutia jamani khaaah, aliweka kituo Tausi huku akimwelekeza dereva njia asipotee.
Samson alishangaa kuona mama yake mdogo akitoa sifa zile aliishia kutabasamu bila kuongea chochote japokuwa Tausi njia nzima ni Samson tu ndiye aliyekuwa mdomoni mwake, Samson alimwangalia kaka yake Jose, akagundua yupo busy na usukani tu.
Hatimaye walifika nyumbani kwa Tausi huku Tausi na Rahma wakiwa wa kwanza kushuka akafuata Samson akimwacha kaka yake, waliingia ndani huku Tausi akizidisha mbwembwe na uchangamfu sana.
Yaani sijui Nini kimetupeleka wote kule kwa mama kulwa, maana mgeni kama Jose anaondokaje bila hata kula, eti shoga yangu kama ningekuacha hapa si ungeandaa Chakula? Maana hii aibu ya Leo ni rekodi ya Karne, kwanza mgeni mwenyewe yuko wapi mbona simuoni? Hajaingia ndani bado? aliropoka Tausi huku akitoka nje na kumuita Jose,
Baba yangu mbona mnafikia nje tena, haiwezekani jamani njoo uache hata baraka tu mwananguuu.
Jose aliingia ndani huku akionesha Kuna kitu hakikumpendeza ila alijitahidi kuficha ile hali ,
Aiseee ni kitambo sana mama nilikuwa nasikia tu kuwa mama yako mdogo amehamia kwake baada ya kumalizia nyumba yake, hakika hatimaye nimefika kwanza hongera sana mama.aliongea Jose huku akizungusha macho kuangalia kuta za ile nyumba
Mmmmh mwanangu, hii nyumba au kibanda? Aliuliza Tausi huku akibinua midomo yake na kumkazia macho Jose
Kwako ni kwako tu mama, kwanza kunakuwa na heshima, unaweza fanya unachokitaka kwa uhuru, waweza kutamani maua fulani yapandwe kuizunguka nyumba yako, jambo ambazo kwenye nyumba za kupanga hizi za kiswahili haiwezekani.
Zipo faida nyingi sana, hivyo kikubwa hongera sana. Jose aliongea huku akitazama chini maana hakutaka kukutanisha macho na Tausi
Halafu na wewe Rahma mbona hauchangamki yaani umeganda tu huwezi hata kuleta juisi, hivi wageni huwaoni? Eeenh halafu leo nakuona kama umepooza Nini shida, unaumwa?
Tafadhali shoga yangu usije ukawa unaumwa, usijifiche ohooooh wewe Kaa kimya utaumia ujue. aliropoka Tausi
Hamna mama Wala hakuna shida hapa Mimi ni kwangu , muda na siku yoyote nitakula Wala msijali mama, na wewe dogo Sam, kama una vya kuchukua beba tuondoke.
Mwende wapi tena baba, Samson kwa Leo nakuomba alale hapahapa kama kuishi kwa dada mama Kulwa, Hilo linafahamika na hata hapa ni kwake anaweza kuishi tu. Au Kuna ubaya baba? alihoji Tausi.
Jose alishangaa utaratibu kubadilika wakati walikubaliana tangu mwanzo ila kwakuwa aliujua ule mcharuko wa Tausi, akaona isiwe tabu akainuka akaondoka huku akimtaka kesho Samson aje na vifaa vyake vyote.
Samson aliweza kushuhudia vituko fulani Kati ya Tausi na Rahma,
Baadhi ya vitu vingi wakawa wanatofautiana,
Tausi hakujua mapema Nini kinasababisha Rahma kuwa na hasira vile na kakataa kuwa haumwi?
Halafu wewe nakuona sana leo, umebadilika sana, hicho kiburi Mimi sikihitaji, kama unajiona ushakuwa rudi nyumbani au tafuta sehemu ukaishi, hapa kwangu sikuhitaji, kwanza umenikera sana kuonyesha jeuri mbele ya mgeni.
alilalamika Tausi.
Mamdogo unapenda sana kunionea
Sasa Mimi Nina kosa gani, Mimi hapa Nina mawazo yangu tu, samahani kwa hilo ila kwa Leo sijisikii vizuri, alijibu Rahma huku akiinuka na kuelekea chumbani kwake.
Ni Samson pekee aliyetambua shida ya Rahma, kuwa alibadilika baada ya Tausi kumsifia Samson, wakati wakiwa kwenye gari, ndiyo, walikuwa wanaongea na kupiga stori vizuri tu ila baada ya Tausi kumsifia Samson mambo yakabadilika ghafla.
Enheee naona kesho Sam unaenda kuishi kwa mama Kulwa unatuacha , hakika tutakumiss maana tumekuzoea, tafadhali mwanangu usiwe unakaa sana uwe unakuja kunisalimia sawa baba, Tausi aliongea huku akimpigapiga Samson mgongoni, huku Sam jasho jembamba la uwoga likimtoka kwani hajawahi kukaa karibu na mama yake mdogo kiasi kile.
Halafu Samson usiwe unaniogopa sana, kwani mi kukaa karibu na wewe Kuna ubaya gani, hebu sogea baaasi.
aliongea Tausi kwa kudeka, huku kwa upande wa Samson moyo ukimuenda mbio kwa hofu.
Itaendelea.................