SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
Mzee Mgaya alikaa kwa kutulia kwenye kiti huku akijaribu kujizuia hasira zake.
Vipi tena wewe upo huku unajua unaweza kuwapa watu wasiwasi, Mimi hata sikujua kama upo huku , ulichofanya siyo kizuri kwani unaweza kutuweka roho juu tukawaza vingine. aliongea Mzee Mgaya kwa sauti ya kivivu kisha akainuka na kuelekea usawa wa chumbani, ambapo na mkewe mama Kulwa alimfuata muda huohuo
Enhee niambie dogo kitabu kinase make, aliuliza Jose kwa sauti ya kirafiki huku akichukua begi la Samson na kuanza kupitia madaftari yake.
Nashukuru MUNGU mambo si mabaya sana, japo changamoto hazikosekani kaka. alijibu Samson
Mama Kulwa alitoka akamuita Samson watoke wakaongelee nje, huku wakimuacha Jose akipekuapekua Papers za Samson.
Samson niambie mwanangu maana nimegundua ujio wako hapa si wa kawaida, lakini pia baba yako naona kama hampo sawa naye Kuna nini hebu tafadhali niambie Kila kitu usinifiche, aliongea kwa shauku ya kimbea mama Kulwa.
Samson akaanza kueleza kuanzia baba yake na Tausi walivyosafiri kuelekea Tanga, lakini pia walivyorudi huku wakiwa wamebadilika na kumchukia ghafla bila sababu,
Lakini pia maneno aliyoongea Tausi asubuhi ya siku hiyo akimtuhumu Samson kuwa mchawi , yalimpa majibu ya wapi walikokuwa wameenda. aliweka kituo Samson.
Kwahiyo, hata huyu baba Kulwa anakosa busara za moja kwa moja na kusikiliza upuuzi wa Tausi, yaani heshima aliyojijengea halafu jamii isikie haya aliyokufanyia kifaranga kama wewe nani atamuelewa? au Mr anachanganyikiwa? hebu mwanangu turudi ndani nikaongee naye, aliongea mama Kulwa huku wakiingia ndani na kumkuta Mzee Mgaya akiwa karibu na mwanaye Jose wakiangalia baadhi ya matokeo ya Samson ambapo muda wote Jose alitikisa kichwa akionesha anakubali uwezo wa Samson.
Aiseeeh yaani kichwa hiki kama kingekuwa high school ingependeza sana, nahitaji kuona anavyofika mbali huyu dogo, aliongea Jose kwa furaha sana.
Baba Kulwa, na wote tuliopo hapa ndani hebu naombeni tusikilizane,
Naomba kujua baba Jose una tatizo gani na huyu mtoto. aliuliza mama Kulwa
Tatizo, tatizo gani? Mimi Sina matatizo na nwanangu kwani kakuambia nini, maana hata ulivyoingia hapa Mimi nimeshtuka Kuna jambo nimeliona halipo sawa, Sasa ni vyema wote tutajua ili kama mtoto kakukwaza aonywe, huyu siyo wa kumnunia, kwanza unachekesha sana mtoto huyu si kama mjukuu tu kwako? Jambo gani limekuudhi kiasi cha kumkalia kimya? aliuliza Mama Kulwa.
(Huku akicheka)Yaani wewe leo hii wakumuonea huruma Samson, huruma hiyo imeanza lini, au unataka uonekane mwema sana, Samson nimemtoa mkoani huku shule tukimtaka asome iliyokaribu na hapa , na kuishi aishi hapa ambapo ndiyo nyumba yangu kubwa watu wote wanajua wewe ndiye malkia wa mzee Mgaya na wageni wangu wote huwa wanafikia hapa, je nani amesababisha Samson ahame hapa siyo wewe? Ni Mara ngapi ulionesha humpendi lakini nikawa nazuia nikijua leo kesho mtakaa sawa lakini mambo yalizidi kuharibika nikaamua kumuhamisha Samson.
aliongea kwa hasira na dharau Mzee Mgaya.
Nimehangaika naye huyu toka kijijini hadi kufika naye hapa, matokeo yake yalichakachuliwa huku wajanja wakitaka kupora haki yake lakini nilipambana mpaka kufikia kufanikisha suala hili iweje leo nimchukie Samson, hajafikia hata Moja ya nane ya malengo yangu namuachaje? tatizo ni wewe ulishindwa kuishi na huyu mtoto nani asiyejua? Hivyo usianze kujiona mwema sana mbele ya mwanao Jose, wewe ni mke wangu nakujua vizuri sana tu. aliongea Mzee Mgaya
Weeeeeeee tena ishia hapohapo Mimi ni mama najua mtoto analelewa vipi, malezi ambayo ulitaka kumpa huyu mtoto siyo kabisa, unadhani huko kwao alikotoka alikuwa hafanyi kazi, Sasa ilifikia hatua unamkataza asinisaidie kazi ulikuwa na maana gani? kwakuwa na Mimi Nina misimamo yangu, nikaona mpeleke sehemu ambayo hatofanya kazi, huyu mtoto Mimi simchukii Wala si kama simpendi na akiamua kurudi hapa tutampokea kwa mikono miwili lakini lazima afanye kazi,
Eti wewe kwa Tausi huwa kazi yako ni kula tu na kutulia? aliulizwa Samson.
Akaitikia kwa kutikisa kichwa kuwa huwa anafanya kazi.
Mama Kulwa akaendelea............
Sasa wenzangu mmekuja na jambo kubwa zaidi mkimuita huyu mtoto mchawi, kweli jamani mbona mna dhambi hivyo?
Yaani Tausi aseme nini asikilizwe, atakuja kukufanya ukose heshima na Imani kwenye jamii kwa kuendelea kusikiliza Kila upuuzi wake.
Mama Kulwa aliongea bila uoga wowote akionesha kujiamini sana.
Mzee Mgaya alifura kwa hasira sana huku akitamani aseme neno lakini uwepo wa mwanaye Jose ulifanya adhibiti hali yake.
Kwa upande wa Jose yeye alikuwa kimya sana hakujibu neno lolote huku akiwaomba wazazi wake wakapumzike kisha na yeye akiingia kwenye chumba chake, hali kadhalika Samson akaingia kwenye chumba chake huku moyo Ukiwa unamuuma sana kwani kitendo Cha watu kuwa wanapishana kwa sababu yake, alijikuta anakata tamaa, sasa sehemu ambayo aliitegemea kuwa anaweza kuishi vyema kwa Tausi, nako kuligeuka kwa moto mbaya zaidi hata Mzee Mgaya naye alikuwa yupo upande wa Tausi hivyo ilimuwia vigumu mno.
Asubuhi aliamka akamkuta mama Kulwa nje wakasalimiana.
Mwanangu pole sana, hata hivyo usijali yule Malaya Tausi alileta fitina hadi kufikia wewe kuhama hapa lakini , unajisikiaje kuambiwa wewe ni mchawi?
Ina maana umetukanwa wewe na familia yako , yaani wazazi wako wote wanaonekana wachawi, sasa unawezaje kuishi hiyo sehemu,
Mwanangu ipo siku utapewa sumu kwani tayari mpo kwenye mashindano na familia ya Tausi,
Na asili ya mashindano lazima apatikane mshindi.
Sasa baba yangu Samson unadhani unaweza kushinda? aliongea mama Kulwa huku akimtisha sana Samson.
Samson alifungua geti kwa nguvu huku maneno yale yakimtisha sana , alifika shule huku ile hali ya yeye kuishi kama digidigi ikimuumiza sana mbaya zaidi alishindwa kujua hatma ya Nini kitatokea, akahisi kuwa hana muda anaweza kuacha shule , hakuwaza kuhusu kuhama shule,
Nani atamuhamisha?
Mtu ambaye alimfanyia mipango yote kuanzia kijijini kwao Hadi mjini lakini Sasa aliona kabisa hakuna tumaini la kuendelea kusoma.
Itaendelea.......................