Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

Tuongezee kidogo basiiii jamani
Do something jisahaulishe kama haipo. Soma kitabu Cha novel hamishia huko akili utasahau huku. Ama fanya Kama imeisha. Jiulize umeshasoma story ngapi na je ukipata ngapi
 
SEHEMU YA THELATHINI NA SITA

Mida ya jioni kama saa kumi na mbili hivi, Mzee Mgaya alitoka akiliacha gari lake akaingia mtaani kwa miguu, ni kawaida yake kufanya hivyo, akifahamika kwa kupenda sana mchezo wa bao, hivyo familia haikuwa na wasiwasi juu uondokaji wake.

Samson alivunja ukimya Mara baada ya kuwa wote kama familia wametulia pale sebuleni,

Mamdogo pole sana kwa matatizo yaliyokutokea hakika ni tukio limetusikitisha sana kama familia, lakini tunashukuru zaidi kukuona Ukiwa bado mzima, hakika mwenyezi MUNGU ni mkubwa. Samson aliweka kituo.

Mmmmh ahsante sana mwanangu, kwanza siamini kama maneno haya yanatoka kwenye kinywa chako, nikupongeze tu kuwa kweli umekua Sasa, kwa maneno haya Sasa tunakutegemea kama mmoja wa wanaume humu ndani. aliongea Tausi na kumfanya Samson atabasamu kwa sifa anazopewa.

Tausi akaendelea,
Hata hivyo wanangu, hapa kuna vita tena vita kubwa sana kwa haraka haraka wale wezi/majambazi hawajaja kwa bahati mbaya ila inaonekana wametumwa, kwasababu wangekuwa wanahitaji kuiba bidhaa dukani pale, wangevunja usiku,lakini hili tukio akili zangu zinacheza kwa mtu fulani ambaye naona hafurahii mafanikio yangu. aliongea Tausi kwa uchungu.

Lakini mama, si tuliambiwa huyo mwizi anafahamika kiasi cha Mimi kuambiwa nisijihusishe urafiki na familia ya akina......................
Samson kabla hajamalizia, sentensi yake , alimuona mama yake mdogo Tausi akiweka kidole mdomoni, kama ishara ya kumtaka anyamaze.

Samson mwanangu haya mambo muyaache kama yalivyo, tena msiyaweke sana vifuani mwenu badala yake Mimi nitayafanyia uchunguzi, na nikijiridhisha nitajua nichukue hatua gani. Tausi aliweka kituo.

Muda huo Mzee Mgaya alirudi, akiwa kachangamka kidogo, kwakuwa wanafamilia wanamjua hawakupata taabu kugundua kuwa amelewa,
Lakini pia alikuwa anacheka Mara kwa Mara huku akiongea peke yake, na akionesha hacheki kwa furaha bali ana masikitiko,

Unajua nini mke wangu, Kuna jambo hapa halipo sawa, nimepokea taarifa si muda mrefu sana, nimeambiwa kule kwenye Karakana yangu Kuna mashine haionekani, tena hiyo mashine ndiyo yenye umuhimu kuliko zote mke wangu, Tena ndiyo iliyonifilisi pesa nyingi mno,
Kwanza ni kama ilikuwa na mkosi, maana siku naenda kuichukua bandarini, kila kitu nilikuta kipo sawa kasoro ile mashine haikuwepo, ikaja kupatikana baada ya wiki nzima,
Unafikiria nini mke wangu,huoni kama yupo mratibu wa kukwamisha mipango yangu?aliuliza Mzee Mgaya

Hapo kiukweli siwezi kujua chochote mume wangu, maana Mimi mwenyewe nimevamiwa juzikati tu hapa na sijui kama Kuna usalama, najikuta mwenye hofu kubwa sana,halafu kwenye Karakana yako si Kuna mlinzi kwanini usianze naye yeye kwanza? Maana sioni sababu ya kuwa kwenye mawazo wakati vitu ulimkabidhi mtu, Anza naye yeye, mbane hadi aseme kaficha wapi.
aliongea kwa uchungu Tausi.

Mke wangu, tunapenda kupanda miti ya kivuli karibu kabisa na nyumba zetu, lakini Kuna miti ina mizizi mibaya, yaani mzizi huanza kutembea chini kwa chini, hadi kufikia nyumba kuweka nyufa, je hapo mke wangu utakata matawi ya mti kutatua shida husika au utadeal na mizizi au shina? aliuliza Mzee Mgaya huku akicheka.

Nimekuelewa sana Mr, nadhani unaweza kumfunga mlinzi wako lakini tatizo likaendelea tu hivyo tutadili na mizizi my husband. alijibu Tausi huku naye akicheka.
Wakati huo maongezi yakiendelea, Samson na Rahma hawakuweza kujua mafumbo ya wakubwa wao waliona labda ni stori za kawaida tu.

**************************************

Asubuhi na mapema siku inayofuata Samson aliamshwa na baba yake Mzee Mgaya,

Hey weee kijana, amka nataka twende mahali , leo ni jumamosi hivyo lazima ujifunze kazi za kiume siyo kukaakaa tu hapa nyumbani haitokusaidia chochote,
Samson licha ya kutafuta maji angalau anawe uso lakini aliambiwa aingie kwenye gari haraka.

Wakiwa kwenye gari alishangaa kutokusemeshwa chochote na mzee Mgaya, si kawaida kutokumuongelesha lakini siku hiyo ikawa tofauti, wakiwa wanaelekea asipopajua, Samson aliendelea kuwa mtulivu.

Walifika sehemu ambayo Samson hajawahi kupaona, ila kwa mujibu wa stori za kuhusu Karakana ambazo huwa anaziongelea Mzee Mgaya, alipata picha kuwa pale ndiyo kwenye Karakana ya mzee Mgaya huku akishangaa watu walivyochafuka na vumbi kutokana na shughuli za pale zinazohusu masuala ya mbao

Yaani vifaa vyangu vinapotea, halafu nyinyi mnaendelea tu na kazi si ndiyo? najua hamuwezi kuumia kwakuwa si mali zenu, hebu simamisheni kwanza kazi, na mlinzi yuko wapi asogee hapa,.
Alifoka Mzee Mgaya huku Samson akishangaa kuwa mkali namna ile.

Mzee mmoja umri wa mzee Mgaya, alisogea akiwa anatetemeka, na pia uso wake haukuwa sawa, alianza kupiga magoti mbele ya mzee Mgaya, huku akijitetea kuwa pindi anakabidhiwa hivyo vifaa yeye hakuzingatia vizuri, hivyo anaomba asamehewe.

Mzee Mgaya au boss kwenye ile Karakana hakumjibu yule mzee Wala kuonesha kumsikiliza badala yake aliendelea kuongea na wafanyakazi au vibarua wake mambo mengine huku akimwacha yule mzee (mlinzi) akiwa kapiga magoti vilevile,

Alizunguka zunguka, huku akiangalia baadhi ya milango fulani ambayo alipata oda kubwa kutoka kwenye kituo fulani Cha afya, aliona jinsi ilivyopendeza huku akitajiwa baadhi ya vifaa vinavyohitajika pamoja na upungufu wa mbao ili kutimiza mahitaji ya pale.

Unajua nyinyi mmemzunguka huyu mlinzi , mmeamua kunipiga mashine yangu, Sasa kabla sijaita polisi waje wawazoe wote, nahitaji kujua mashine yangu iko wapi. aliongea Mzee Mgaya akiwa hatanii,

Wale vijana waliangaliana kisha wakawa kama wamechukia fulani hivi,walitamani kusema neno lakini ile hofu kwa Boss wao ilifanya warudi nyuma, ndipo kijana mmoja anayejiamini akaanza kujitetea,

Boss, wewe umeweka utaratibu wa Kila mfanyakazi kukaguliwa Kila anapotoka, kwenye hii Karakana yaani yule mlinzi wa mchana anatupekua kiasi kwamba huwezi kuiba hata kitu chenye uzito wa gramu tano, Sasa sisi tunahusika vipi kwenye huu msala? aliongea kwa kujiamini yule kijana, Samson akagundua kuwa Mzee Mgaya ni mtu anayeogopwa sana pale,

Mzee Mgaya hakujibu neno akarudi kwa mlinzi akimkuta Mzee wa watu akiwa kapiga magoti vilevile,

Wewe Mzee ulikuja kwangu kuomba kazi ya ulinzi baada ya kusikia Mimi natafuta mtu wa aina hiyo, nikakukatalia nikakueleza kuwa nahitaji mtu mwenye mafunzo maalum na awe na uzoefu wa siku nyingi pamoja na cheti kinachoonesha amepita kampuni gani ya ulinzi, lakini ulinidanganya ukaniletea nyaraka fulani za uongo, ili tu nikupe kazi, na ni kweli ulifanikiwa , si kazi nilikupa?
Lakini tambua kuwa niliujua uongo wako ila kutokana na kutambua hali ya maisha na jinsi ulivyonilalamikia nikaamua kukupa hiki kibarua, Sasa je mashine yangu naipataje na wewe ndiye mwangalizi, aliongea Mzee Mgaya akionesha hasira za juu.

Mzee wa watu hakujua mashine iliibiwa muda gani, au ilipitia wapi na hakujua chochote akabaki kuomba msamaha tu, Mzee Mgaya hakutaka stori na mtu tena, akaingia zake kwenye gari Samson akiwa kushoto akaingia barabarani,

Kama kawaida, hakuna aliyemuongelesha mwenzie, ikawa Samson anawaza namna Mzee mtu mzima alivyopiga magoti, akajikuta anapata hasira sana, aliwaza kuhusu umasikini wa nyumbani kwao, akaona una nafuu, alivuta picha baba yake mzazi Mzee Elias ndiye angekuwa anampigia mtu magoti, alijikuta anahuzunika sana, aliwaza mbali mno,

Kwanini hawa wazee wasirudi tu kijijini wakalime kuliko kuaibika hapa mjini maana naona kabisa anaenda kufungwa huyu mzee Sasa sijui itakuwaje, ikabidi amuulize swali Mzee Mgaya,

Sasa baba,ujue yule mzee (mlinzi) anatia huruma sana
ina maana mashine yako isipopatikana, yule mzee unamfunga au?

Kwanza Mzee Mgaya alicheka sana Kisha akamjibu,
Hapana sitamfanya chochote, taarifa ya upotevu wa kifaa changu niliipata tangu jana, kama ningetaka kumfunga ningemuweka chini ya ulinzi tangu Jana.
Hata hivyo najaribu kumtia mikwara ili awe makini na pia jumatatu nikienda kule Nampa stahiki zake Kisha tunaachana akatafute kazi sehemu nyingine Mzee kama yule uanze kuhangaika kumfunga si utapata laana bure. aliongea kivivu Mzee Mgaya.

Hapa Samson angalau alijisikia ahueni kusikia kumbe Mzee Mgaya Hana mpango wa kumsweka ndani mtu, ikabidi aulize tena.
Na vipi kuhusu hiyo mashine yako Ina maana ndiyo imepotea si ndiyo?

Hapana mwanangu, na ndiyo Maana yule mlinzi nimemuacha kwakuwa nimejua mchezo niliofanyiwa, hata hivyo ngoja maana tumeshafika nyumbani.

Samson alishangaa wamefikaje kwa mama Kulwa, ikabidi apige kimya tu,akashuka akasukuma geti dogo ambalo halikufungwa wakaingia huku gari likiachwa nje kabisa ya fence,
Waliingia ndani, Samson akalikuta lile gari aliloliona juzikati likiwa kwenye parking, hakustaajabu kwani aliwaza huenda ni gari la mama yake.

Mzee Mgaya yeye alishika kiuno kuona gari mpya na geni machoni pake, alishangaa kuona lipo kwenye parking, maana lingekuwa pembeni tu angejua labda ni gari la mgeni, lakini kuwa pale lilimshangaza,
Wakati akiendelea kuangaza macho alikaribishwa na mkewe,

Haaaa my husband baba Jose vipi, mbona hamuingii ndani?
Njooni basi, kwanza nani kawafungulia geti au nilisahau kufunga mlango mdogo,aliongea mama Kulwa.

Hili gari la nani? aliuliza Mzee Mgaya

Hiyo ndiyo salaam, kwanza salimia Kisha ingia ndani Kaa, tulia, Kisha uliza chochote utajibiwa, alijibu Kwa kujiamini mama Kulwa.

Mzee Mgaya akiwa kachoka kabisa kwani Kuna vitu vilimshangaza, akaingia ndani kufika sebuleni, akashangaa mashine yake mpya anayoitafuta ipo tu sebuleni, kitu chenye uzito wa kilo miatano (nusu Tani) nani alikiingiza hapa , akapata majibu kuwa Kuna mchezo anafanyiwa.

Mke wangu hii mashine yangu, imefikaje hapa mbona sielewi na Hilo gari la nani?
aliuliza kwa ukali Mzee Mgaya.

Weweeeee Tena ukome, umenunua vifaa vikubwa vya mamilioni hujanishirikisha, unasomesha watoto wa ndugu zako, miye sisemi, nasikia pia umemfungulia biashara Tausi Mimi unaniona zoba tu, kwanini? aliwaka mama Kulwa.

Lakini mke wanguuu wewe ni daktari mstaafu, na una miradi yako mingi tu, wewe ni kuwaonea wivu watu wa kijijini, nimewasaidia kujenga kibanda Cha bati chache tu , wenyewe wanaita mgongo wa tembo, yaani bati kumi na mbili huku na upande mwingine kumi na mbili, si nyumba ya maana mke wangu, alijitetea mzee Mgaya.

Sawa hakuna shida, na Mimi nikwambie kuwa hiyo mashine nimechukua Mimi, na Hilo gari ni langu Mimi, kwanza nishazeeka na miradi yangu inaenda vizuri kwanini nijitese, na wewe upo bize na Tausi, juzi unaingia unatoka nikikuuliza hunijibu, matatizo yako ni yangu, yule Tausi si kama mwanangu tu, uliwezaje kunificha habari zake, au ulisikia Mimi ndiye niliyemsababishia matatizo yake. alilaumu mama Kulwa.

Mke wangu wewe si wa kunifanyia fujo kwenye ofisi yangu, kwa kuchukua vifaa vyangu je, ningefanya maamuzi magumu kwa wafanyakazi wangu huoni ungesababisha shida? na hata hivyo waliohusika kuileta hii mashine hapa , hawana kazi tena.
aliongea kwa uchungu Mzee Mgaya.

Samson aliwaza sana namna mama Kulwa na mzee Mgaya wanavyolumbana Kila mara, akijiona yeye ni msababishaji, hakika aliumia sana.

Itaendelea............................
 
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA

Baada ya mzee Mgaya kupishana na mama Kulwa, aliamua kuepusha Shari, akatoka nje, wakaingia ndani ya gari na kutokomea safari hii ikiwa wanarudi kwa Tausi, wakiwa njiani Mzee Mgaya alikuwa akiongea mambo mengi ambayo Samson hakuyaelewa.

Hatimaye wakafika nyumbani kwao na kukuta wametembelewa na wageni ambao sura na nyadhifa zao alizitambua,

Karibuni sana ndugu zanguni, nilitoka kidogo weekend hii kwaajili ya kukagua miradi fulani,hivyo samahani kwa usumbufu ambao utakuwa umejitokeza, aliongea kwa tahadhari Mzee Mgaya huku akijichekesha kirafiki.

Usijali hatuna muda mrefu toka tuingie hapa, hivyo ondoa shaka, lakini bila kupoteza muda, tunakuhitaji kituoni kwa mahojiano.
Aliongea mmoja wa wale jamaa wawili huku wakimtaka ainuke.

Jamani ndugu zanguni Kuna jambo gani tena, nakuombeni kama Kuna lolote ambalo nimefanya mniambie, mimi nitaongea na nyinyi Kila kitu kitakaa sawa, siwezi kwenda kituoni bila kujua naitiwa na nini au Nina kosa gani. alihoji mzee Mgaya

Wale maaskari waliovaa kiraia waliangaliana kisha wakatabasamu, na kumwambia Mzee Mgaya awafuate waongelee ndani ya gari lake, lakini baada ya kama dakika tatu walitoka ndani ya gari na kuanza kumsukuma Mzee Mgaya huku wakitukana matusi makubwa sana, waliingia naye kwenye gari lao na kuondoka naye.

Tausi, Samson pamoja na Rahma walilisindikiza gari kwa macho huku Kila mmoja moyo ukimuenda mbio, hakuna aliyejua Mzee Mgaya anakosa gani, Tausi alingia ndani akachukua mkoba wake akaingia kwenye gari la mzee Mgaya huku macho yakiwa yamebadilika.

Jamani wanangu hii familia imeshaingiwa na mkosi fulani,haiwezekani matatizo yawe hayaishi tu, kila siku sisi tu, likitoka hili linaingia hili, Sasa mimi natoka ili nibahatishe kituo gani kapelekwa mr, na nyie kuweni makini sana.
aliongea Tausi huku akiliondoa gari kwa spidi.

Samson alirudi ndani akaingia chumbani kwake huku akiwa mnyonge sana, alijaribu kuhesabu baadhi ya mitihani anayokumbana nayo baba yake akajikuta anaogopa maana hakufahamu Nini kinasababisha yote yale.

Wakati akiwaza yale aliisikia sauti ya Mzee Mgaya ikizungumza sebuleni, akakurupuka pale kitandani na kutoka nje.

Pole sana baba, kwani ilikuwaje na wale wanataka nini, maana yanayoendelea hakika tumehuzunika sana, aliongea kwa hisia Samson.

Wala usijali mwanangu wale ni wahuni tu, njaa ndogo ndogo zinawasumbua , vipi mama yenu yuko wapi. Aliuliza Mzee Mgaya

Ulivyotoka naye alitoka akawa anakufuatilia, alijibu Kwa kifupi Rahma.

Huyu naye hata hajapona sawasawa namuona kabisa tukio la kuibiwa lilivyomtesa kisaikolojia, Sasa kuanza kuendesha gari kwenye barabara zenye harakati nyingi, anaweza kuleta maafa mengine. alilaumu mzee Mgaya.

Mida ya jioni sana Tausi alirudi huku akishangaa kumkuta Mzee Mgaya alimkimbilia na kumkumbatia huku akitoa machozi ambayo hayakujulikana ni ya furaha kumuona mumewe au ni ya huzuni,

My husband hii hapana, nasema si kweli Kuna shida kwenye upande wako, tunajua ndiyo matatizo ni sehemu ya maisha, lakini kwanini kwenye familia yako mambo yaongozane? Kwanini yafuatane baba? lazima tufanye kitu, lazima tufanye jambo mume wangu, najaribu kuvuta picha nakuta mambo yanaenda kuharibika.

Kwanza niambie imekuaje huko walikokupeleka, wamekwambia una kosa gani? maana kwa udhalilishaji waliokufanyia ama kweli Dunia haina utu mume wangu . aliuliza Tausi huku safari hii akiwa analia kabisa.

Wale wameniambia kuwa Kuna vitisho nimetoa, hivyo nahatarisha maisha ya watu, wakidai Kuna familia inaishi kwa hofu kwasababu yangu, lakini Kila nikiwauliza ni nani ambaye, nilimtishia hawaniambii, hivyo wakaniambia kuwa ili wasinipeleke kituoni niwape hela, nikawakatalia ndiyo maana mmeona wamenitoa mkukumkuku , hata hivyo hatukufika mbali, wakaniacha wakinambia wakinihitaji watanitafuta.
Aliongea mzee Mgaya huku akicheka kivivu.

Una uhakika ni maaskari kweli, kirahisi hivyo wakuachie my husband pengine ni matapeli tu,. alihoji Tausi

Mmoja namfahamu vyema sana wamesoma pamoja na mwanangu Jose ila yeye akafeli akaangukia huku, na nimeshangaa kunikosea adabu kiasi kile, lakini usijali mke wangu wale nitajua cha kufanya hawawezi kunidhalilisha kiasi hicho mimi.aliongea kwa masikitiko Mzee Mgaya.

Hapana mume wangu kabla hujafanya chochote lazima twende kwanza nyumbani Tanga, nadhani kile Kijiji unakikumbuka vizuri, kwanini tusiende kujiuliza? alishauri Tausi

Ahaaa yes, siyo mbaya nakumbuka, kwanini yule kijana bado yupo, maana kitu alichonifanyia hakika niliamini hii Dunia Ina watu wa kweli, mtoto anajua sana anachokifanya , wakati nafungua Karakana yangu nilikutana na upinzani mkubwa sana hadi nilifikia kutaka kuuza tu zile mashine lakini baada ya wewe kunipeleka, kila kitu kilifunguka mapema mno , wateja walijazana hadi ikawa kero.
alijibu mzee Mgaya akimsapoti Tausi.

Ndiyo hapo sasa, kama ni hatua tuchukue hakuna kujiuliza tena, vinginevyo tunaweza kukaribisha msiba mkubwa ndani ohooo, Sasa tupange ni lini twende. aliuliza Tausi

Hakuna cha lini, hapa naipeleka gari service wakacheki mifumo yote, na safari ni kesho, kwanza nikushukuru kwa kunizindua hili wala sikufikiria kabisa, wewe mke wangu jiandae tu, aliongea mzee Mgaya huku akiinuka na kuelekea kwenye gari lake.

Samson alibaki akiwaangalia na kusikiliza maoni na mashauriano yao akagundua kuwa wanaenda kwa mganga wa kienyeji, laiti angejua angeanza kumuomba MUNGU mapema.

Alfajiri wakati adhana yenye kuwakumbusha waislamu kwenda kuswali ikilia tayari Mzee Mgaya na Tausi walikuwa wanafunguliwa geti na Samson tayari kwa safari.

Kwakuwa siku hiyo ilikuwa ni jumapili Samson aliandaa vifaa vyake, pamoja na kunyoosha nguo zake kwa maandalizi ya kesho, huku akiwaza kutumia ile nafasi ambayo huwa anakosa kumshawishi Rahma afanye naye mapenzi.

Wakati akiwa kwenye hayo mawazo ya hovyo, aliitwa na Rahma,

Vipi mbona upo bize sana huko ndani, unafanya nini, au umemfungia mrembo nini mwenzangu, aliongea Rahma huku akicheka kiasi Cha kuonesha meno yake mazuri,

Nimekuita ili twende wote sokoni sawa, aliongea Rahma kwa sauti tamu ya kudeka.

Hapa Samson alijikuta anasisimka kushinda maelezo wakatoka huku, wakipiga stori za hapa na pale,
Wakiwa njiani Samson alishangaa kuona Rahma akipigiwa miluzi Kila saa na wengine kumfuata na kutaka awasikilize shida zao, watu wazima kwa vijana walimsumbua sana.

Kitendo kile kilimkera sana Samson,
Wivu ulimjaa huku hisia fulani za hasira zikija lakini hakuwa na uwezo wa kuwaambia chochote wahuni wa mtaani, walirudi nyumbani wakaanza kusaidiana kuandaa Chakula Cha mchana.

Hivi Rahma mbona watu wengi wanakusumbua vile, kwanini usiwe unawatukana uwakomeshe, yaani huoni kama wanakusumbua sana weee njia nzima, si wakati wa kwenda si kurudi usumbufu tu vipi?
aliuliza Samson huku wivu ukimsumbua.

Wewe acha tu, tena si afadhali leo walikuwa na heshima, Kuna siku nyingine Kuna watu wananisindikizaga hadi getini hapo ujue, tena kuna muuza nyama yule mbaba wa pale buchani, kila siku ananisumbua, nimemuhama kwaajili ya kero zake, ni zaidi ya Mara tatu ananipa nyama bure Tena yule huwa hatanii ananitaka kweli. aliongea Rahma asijue anazidi kumuumiza zaidi Samson.

Samson alikasirika sana kusikia Kuna watu huwa wanafika Hadi getini, alitamani amuone mtu akisogea Kisha amtukane maana alimpenda sana Rahma.

***************************************
Kama kawaida kwakuwa wazazi wao walisema hawatorudi, Rahma alitaka Samson alale kwake,
Samson akakubali huku akipanga kutofanya makosa tena kama mwanzo,
Samson alikaa sebuleni akiwa anatizama TV, lakini hakuwa anaona Wala kuelewa chochote mawazo yake yote yalikuwa kwa Rahma mwanamke anayemtesa sana moyo wake, baadaye Rahma alitoka bafuni akiwa kajifunga kijitaulo kifupi huku umbo lake zuri likionekana vyema zaidi, Samson alijikuta anamfuata Rahma kwa tamaa.

Vipi wewe Mimi nataka nibadilishe nguo zangu kwanza kisha nitakuita , aliongea Rahma kwa ukali. Samson hakujali azima yake ilikuwa pale pale alijipa matumaini kuwa lazima afanikishe hata kwa kutumia nguvu.

Baada ya dakika fulani aliitwa akaingia akakuta leo Kuna mashuka mengine mazuri na yenye kuvutia zaidi akajilaza kitandani akimwangalia Rahma kwa wizi ambapo alikuwa anafunga kitambaa kichwani.

Sasa vipi tena unafunga kitambaa kichwani, aliuliza Samson.

Mwenzangu mi nalinda nywele zangu lakini pia ni kawaida yangu kulala nikiwa hivi, alijibu Rahma huku akiwa kavaa suruali na kupanda kitandani akiwa analala kimchongoma yaani miguu ya samson ilipo yeye akaweka kichwa.

Sasa unalalaje hivyo, njoo uku basi, Samson alilaumu huku akishangaa mambo yenyewe yanavyozidi kuwa magumu

Wee unatakaje, si ndiyo tunalala au, sipendi ukorofi kama unanipangia basi kalale kwako bwana , aliongea kwa kudeka Rahma kiasi Cha Samson kushindwa kujua, huyu hataki au anataka?

Muda fulani Rahma alionekana kupitiwa na usingizi, wakati huo Samson akiwa macho na Kila kiungo chake cha mwili kilifanya kazi kwa kiwango kikubwa, aligeukia upande alipo Rahma akaanza kumpunguza nguo huku akifanya kwa umakini mkubwa ili asije kumshtua na zoezi likawa gumu.

Hatimaye Rahma akawa kama alivyozaliwa huku, alijigeuza geuza kama mtu anayeota ndoto mbaya,
Samson akiwa na joto la mwili ambalo lilivuka kiwango, huku moyo ukimdunda dunda na pia ugeni nao ulichangia akose kujiamini, akaanza taratibu kuchanua mapaja ya Rahma huku akiwa na tahadhari kama mwizi aliye juu ya fence ili asitue chini kwa nguvu.

Hatimaye akafanikiwa huku Rahma akiwa anaonesha ana usingizi mzito, na miguu ikiwa imechanuka kama nyuzi tisini hivi Samson akaona panatosha kabisa kufanya vitu vyake,
Alihangaika sana kuweza kutumbukiza mpira kunako wavuni, alikumbuka zile picha ambazo huwa anaangalia akaona mbona mambo huwa ni marahisi Sasa yeye anakwama wapi,? Aliwaza kuforce kwa nguvu, lakini akaogopa asimwamshe muhusika na zoezi likaishia hapo.

Zaidi ya saa nzima alikuwa hajafanikisha akaanza kupata hasira fulani, huku akigundua yale mambo si mepesi kama alivyotarajia, wakati akiendelea na mashambulizi ili mradi bastola iue mnyama licha ya shabaha zake mbovu, Rahma aliamka huku akijishangaa,

Wee Sam kwanini umenivua nguo zangu, aliuliza kwa sauti yenye usingizi, Sam akaona nikifanya masikhara nitakosa ikabidi amkandamize kwa kumlaza tena chali kwa nguvu, Rahma alijaribu kufurukuta lakini alizidiwa nguvu, akijaribu kubana miguu ilishindikana kwa Samson alikuwa yupo Kati ya miguu iliyochanuliwa, Rahma akaanza kulia akiwa kakata tamaa Samson akaanza kuforce kwa nguvu maana hakukuwa na sababu ya kuvizia tena kama muhusika kashaamka.

Utaniumiza Sam hebu tulia kwanza, akaishika maiki ya Samson huku akiielekeza sehemu husika Samson alifurahi kuona vile maana anavyoshikwa alidhani labda anataka kuumizwa, alishangaa kuona Rahma akizungusha kiuno , huku yeye akiwa kaganda tu, Rahma msichana mkubwa zaidi kiumri kwa Samson alianza kumnyanyua Sam na kumrudisha chini baada ya kugundua Sam ni mgeni wa kutumia pistol,
Sam naye akaanza kupumb huku akisikia raha zisizoelezeka lakini alishangaa zile raha zikizidi zaidi ya mwanzo tena huku akihisi mwili si wake baadaye akagundua ile hamu imepotea ghafla, na hata pistol yake kama inalegea. Hakujua Cha kufanya

Akasukumwa na Rahma huku akisonywa, loh fujo tu kumbe mtu mwenyewe mgeni wa Jiji nimekuona tangu mwanzo ukihangaika mwenye ulijua nimelala, hebu inuka usichafue mashuka bwana na pia nipeleke chooni Samson akiwa na aibu huku akishangaa kwani ule utamu uishie karibu akainuka wakaingia maliwato kwa zamu, kisha wakarudi kulala, Sam akashangaa pistol yake hiyo tena inataka kuua , safari hii hakupata tabu alivyomgeuza tu Rahma alipewa ushirikiano akaanza tena huku safari akiwa mchezaji underdog maana Rahma alikuwa mwalimu, lecture wa nguvu na safari Sam alidumu hata ule utamu na spidi kuongezeka alijua Nini kinatokea alijaribu kujizuia lakini ilishindikana risasi zikatika bila trigger kufyatuliwa na yeye.

Alienjoy akajikuta kujiamini kumeongezeka wakalala kawaida wakiwa wamekumbatiana, usingizi mzito ulimpitia Sam kiasi cha kujikuta anaamka jua limechomoza na Rahma hayupo, alitoka nje na kumkuta Rahma yupo anafanya usafi .

Mbona hujaniamsha hujui Leo ni jumatatu natakiwa kwenda shule, aliuliza Samson.

Weeeee acha ujinga, sikuzote nakuamshaga Mimi, alijibu Rahma huku akiwa hataki ukaribu Wala mazoea na Samson,

Dah muda huu nianze kuoga, nianze kutafuta Daladala na foleni ya jumatatu, shule siendi, alijisemea samson kwa sauti.

Rahma aligeuka akimwangalia Sam Kisha macho yaligongana wote wakatabasamu, siku hiyo walishinda wote huku Rahma akiwa anamkwepa kwepa Sam hakutaka mazoea naye, labda ni aibu fulani. Sam hakujali yeye alifurahi kuona katimiza lengo lake.

***************************************
Mida ya saa nane mchana mzee Mgaya na Tausi walingiia, huku wakipokelewa vizuri,

Wewe vipi mbona si kawaida muda huu kuwa hapa, hujaenda shule? aliuliza Mzee Mgaya

Samson akaitikia kwa kutikisa kichwa.

Mzee Mgaya alianza kumporomoshea matusi Samson, na hata Tausi ambaye huwa anakuwa mtetezi kwa Samson akawa mbogo na yeye,

Samson aliwatazama kwa zamu akagundua wa nyuso zinazoonesha wanamchukia sana, na walionesha hawamuhitaji

Yaani matatizo yoooote kumbe wewe ndo..............alishindwa kumalizia sentensi yake baada ya kuzuiliwa na mzee Mgaya huku wakiingia ndani. Hakika walimchukia Samson kwa kiwango kikubwa.

Sam Kila akikumbuka kafanya kosa gani hakupata jibu, akabaki akiwa Hana amani, Mzee Mgaya, Tausi na Rahma waliongea wakicheka ila Sam akijaribu kutia neno anashangaa anadharauliwa Mara aambiwe anyamaze, akaingia chumbani kwake akiwa na mawazo sana.

Mzee Mgaya mtetezi wake mkubwa anageuka na kumchukia ghafla Samson, je Samson ataishije?
Endelea kufuatilia simulizi hii ili kujua ni wakati gani Samson alifanikiwa

Itaendelea............ ......
 
Kitu kinazidi kunoga
Umeona hujatolewa hela kweli mpaka hapa ulipo. Hawa jamaa inabidi wawe wanabustiwa hela ya bando kidogo Mana tutazoea vibaya. We've to know we're living in capitalism na sio ujamaa. Itatufanya hata kuzoea maisha Mana tunapenda mno fair,Mara kuonewa huruma. We've to think and we're grown-up we know anything consume his energy and time and money and even his phone anayotumia.
 
Umeona hujatolewa hela kweli mpaka hapa ulipo. Hawa jamaa inabidi wawe wanabustiwa hela ya bando kidogo Mana tutazoea vibaya. We've to know we're living in capitalism na sio ujamaa. Itatufanya hata kuzoea maisha Mana tunapenda mno fair,Mara kuonewa huruma. We've to think and we're grown-up we know anything consume his energy and time and money and even his phone anayotumia.
Ni kweli mkuu keisangora ila mimi binafsi sitomtoza mtu yeyote hela, hata ikitokea anataka kunipa kwa hiyari, basi atafute mtu wa karibu naye anayehisi ana uhitaji ampe kwaniaba yangu.

Nashare simulizi na wanabodi kwaajili ya kujifunza na kuburudika.
Pongezi kwa jamiiforum
Pongezi kwa wanachama wa jamiiforum
Ahsante.
 
Ni kweli mkuu keisangora ila mimi binafsi sitomtoza mtu yeyote hela, hata ikitokea anataka kunipa kwa hiyari, basi atafute mtu wa karibu naye anayehisi ana uhitaji ampe kwaniaba yangu.

Nashare simulizi na wanabodi kwaajili ya kujifunza na kuburudika.
Pongezi kwa jamiiforum
Pongezi kwa wanachama wa jamiiforum
Ahsante.
Pamoja. Wengi hawajui kuwa una exert force/power/energy na energy inayo various forms and that forms can exchanged to each other. Sasa mwingine amekaa hapa Ni kukumbusha kuwa utaleta muda gani Mara tunakufa. People can't handle their emotions/brains. Na ndio Mana saivi Kuna dopamine inapatikana kwa social networks yaani ishakuwa uraibu Kama uraibu mwingine. Baadaye huko mbele itabidi tuanzishe sober house for social networks addicted/affected.
 
Pamoja. Wengi hawajui kuwa una exert force/power/energy na energy inayo various forms and that forms can exchanged to each other. Sasa mwingine amekaa hapa Ni kukumbusha kuwa utaleta muda gani Mara tunakufa. People can't handle their emotions/brains. Na ndio Mana saivi Kuna dopamine inapatikana kwa social networks yaani ishakuwa uraibu Kama uraibu mwingine. Baadaye huko mbele itabidi tuanzishe sober house for social networks addicted/affected.
"Sober house for social networks addicted/affected"

Hii sentence imefanya siku yangu iwe nzuri sana, yaani imebeba ukweli mtupu, tena tulioathirika ni wengi mno.
 
"Sober house for social networks addicted/affected"

Hii sentence imefanya siku yangu iwe nzuri sana, yaani imebeba ukweli mtupu, tena tulioathirika ni wengi mno.
Na ndio Mana ukiwa seriously na kazi yako. Zima simu Mana inaleta distractions zisizo na msingi ujue. Kuna ofisi hauingii na simu. Bando zinapanda Ni kusaidia watu sometimes.
 
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE

Asubuhi na mapema sana ikiwa bado giza tofauti na siku zote Samson alikuwa ameshajiandaa tayari kwaajili ya kwenda shule, ile anatoka tu akakutana na Tausi getini akiwa ameshikilia vitu fulani mkononi mithili ya hirizi.

Wewe ni asubuhi asubuhi, umbea tu sikuzote huwa unawahi hivi, sasa nimeamini maneno ya mtaalam, wewe mtoto ni mchawi kweli, wewe haiwezekani Mimi nije kufanya mambo yangu na wewe uje ili iweje? na tayari umeshaniharibia dawa zangu.sasa huo uchawi wako Mimi nikwambie tu kuwa hutopambana na mimi bali utapambana na wenzio.

Wewe ni mtu gani tangu ufike hapa matatizo hayatuishi, likitoka hili linaingia hili, kumbe chanzo ni wewe sasa nikwambie tu kuwa umejulikana na anza kutafuta pa kwenda. aliongea Tausi akiwa anamaanisha.

Baada ya kusikia makelele ya mkewe, Mzee Mgaya alitoka haraka akiwa kavaa taulo tu,

Vipi kuna nini my wife, asubuhi tu makelele, aliuliza kwa pupa Mzee Mgaya.

Si huyu mwanao, sijui mwanga mwako nashindwa hata nielezee vipi, hata sijui kajuaje, nashangaa mtu yupo nyuma yangu eti anaenda shule, tangu lini huwa anawahi hivi? Huyu kataka kuniharibia tu, hana lolote na tayari dawa ishaharibika si unajua mtaalam alisema sitakiwi kuonekana na yeyote. alilalamika Tausi.

Mzee Mgaya alimwangalia Samson kwa jicho baya na kali sana, huku akirudi ndani bila kusema chochote, wakaachana Samson akashika njia ya kwenda kituo cha daladala.

Samson alipata siti ya nyuma kabisa akajiinamia huku akiwaza,

Kwani mimi nina mkosi gani, mbona matatizo yananiandama kila siku, sasa Mimi nawezaje kuwa mchawi?
Kwani uchawi ni nini?
Ni kitu gani kinakufanya mtu uitwe mchawi?
Au Mimi ni mchawi kweli, halafu sijijui tu, Sasa nitafanyaje kuiondoa hali ambayo hata Mimi mwenyewe siijui, au niache tu shule nimwambie baba mkubwa kuwa nataka tu kurudi nyumbani? alijiuliza maswali kadhaa asipate majibu

Alifika shule huku baadhi ya wanafunzi wenzake wakimchangamkia kwani, kukosekana siku moja tu kufika shule kulifanya washkaji zake wajisikie vibaya, lakini Samson alijitahidi kuficha ile hali bila mafanikio, kwani Kila alipolazimisha kuchangamka ilishindikana.

Hayahaya kwanza sitaki salamu zenu kaeni tu, kuanzia asubuhi, muda wa mapumziko tunasalimiana tu, hivyo mimi sitaki salamu zenu labda kama mnataka kutimiza kaulimbiu ya serikali yetu, maana hizi salamu huwa zina malengo tofautitofauti.
Aliongea mwalimu wa darasa wa Samson ambaye alijulikana kwa jina la utani la "Miwani" shule nzima ilimuita hivyo kutokana na muda wote kupenda kuvaa Miwani Hadi watu wakahisi pengine huwa analala nayo, kwa upande wa wanafunzi wa form one walimpachika jina lingine walimuita "Potential" hili ilitokana na kuwa anakazia sana anapofundisha somo lake.

Mwalimu mchangamfu, mjanja na smart akiwa ndiye anayetegemewa kwa kufundisha masomo ya Sayansi, huku akiwa na kasoro moja tu, hakujua kuvaa, hakuwa msafi sana, kuwa rafu tu mithili ya mpiga debe,
Alianza kuangalia kitabu cha mahudhurio huku akiwataka wale ambao hawakufika shule wapite mbele, ni wanafunzi wanne tu ndiyo walikuwa hawakufika shule siku ya jumatatu, huku mwalimu kushangaa Samson naye kuwa kwenye lists ya wale wengine ambao wao walijulikana kabisa kuwa ni watoro.

Licha ya kujitetea sana akitaja sababu za uongo lakini mwalimu hakumsikiliza akajikuta anapewa adhabu ya viboko.

Samson alirudi kwenye kiti chake akajiinamia akiwa mwenye mawazo sana, baadhi ya wanafunzi walidhani labda kwasababu ni maumivu vile alivyochapwa lakini haikuwa hivyo, yeye aliwaza sana kuhusu hatma ya kusoma.

Aliwaza sana vile ambavyo Mzee Mgaya kabadilika, akajikuta anakata tamaa kabisa,
Ni mlezi wake,
Ni mtu anayemsomesha na mahitaji yote muhimu, Sasa tayari anaonekana kama hanitaki tena, na kwanini Mimi waniite mchawi? Ina maana safari yao ya Tanga ndiyo wameenda kuambiwa kuwa Mimi ndiye msababishaji wa matatizo yao, MUNGU naomba nisaidie nipate kuendelea na masomo yangu.
alijiwazia kwa uchungu Samson.

**************************************
Muda wa wanafunzi kutawanyika tayari kuelekea majumbani mwao uliwadia, Samson akajikuta anazidi kuingiwa na wasiwasi, kwani sehemu ambayo huwa anaifurahia na huwa anaona muda hauendi lengo likiwa tu ni kumuwahi Rahma, msichana aliyetokea kumpenda na kumkubali vibaya mno, lakini kwa siku ile alijikuta anarudi darasani na kuendelea kujisomea kama ambavyo huwa wanafanya baadhi ya wanafunzi wenzake wanaokaa karibu.

Saa kumi na mbili alitoka na kuelekea kwenye kituo cha daladala na kuanza kuangalia magari ya kumfikisha kule, hata hivyo magari yalionekana kujaa mno, huku makonda wakionesha dharau kwa anayeonekana ni mwanafunzi.

Alikaa takribani saa nzima huku giza likiingia , akapata wazo kwanini asiende kwa mama Kulwa, kwani aliamini mama Kulwa angempokea tu kwakuwa siku za hivi karibuni alionesha hata tatizo naye, akashika uchochoro fulani, akichanja hadi upande wa pili dakika kadhaa akafika kwenye geti la nyumbani kwa mama Kulwa, akagonga geti likafunguliwa na mwanaume mmoja ambaye Samson hakumtambua ila alionesha ni mwenye maisha mazuri sana.

Unaitwa nani na una shida gani, yule jamaa alimuuliza Samson Mara baada ya kusalimiana,
Naitwa Samson Mgaya nimekuja hapa ni kwa baba yangu. alijibu Samson.

Ahaaa karibu sana mdogo wangu, karibu sana, mama yupo ndani, alijibu yule jamaa mrefu na mweusi mwenye nywele ndefu zenye kupendeza.

Karibu mwanangu Samson naona leo umeamua kuja kunisalimia, yaani hadi upende ndiyo uje hapa kweli, usifanye hivyo bwana, aliongea kwa utani mama Kulwa.

Samson huyu unayemuona hapa ni kaka yako, ni mwanangu wa kwanza anaitwa Joseph, kama huwa unasikia mama J, Jay mwenyewe ndiye huyu, watu wengi wananiita mama Kulwa kwasababu wale ni wa mwisho na wamezaliwa watu wengi wakiwaona tukiwa tupo kwenye nyumba yetu hii hii. alifafanua mama Kulwa akiwa na furaha.

Mdogo wangu, kama mama alivyoeleza nadhani Haina haja ya kurudia, ila taarifa za uwepo wako nilizisikia na nimefurahi kukuona, lakini pia nahitaji kujua maendeleo yako ya shule, pia nilishangaa kwanini wakupeleke shule ile kwanini wasingekujumlisha na akina Kulwa?

Hamna Jose, mbona hiyo shule ni nzuri tu tena inafaulisha vizuri sana, alidakia mama Kulwa kwasababu ambazo alizijua.

Jose akaendelea......

Na pia nishukuru umekuja kwani nilikuwa na mpango wa kuja, kwanini nahitaji kuongea mambo fulani na mzee kuhusu msimamo wa wewe why ukae hapa halafu uhame, kwahiyo kilichokufanya uhame hapa ndicho kitakachokuhamisha hata kule. Kwahiyo ili uwe busy ba masomo hupaswi kukaa kwa mtu unatakiwa kukaa shule ya bweni
Jose aliendelea kushauri kuwa Samson ahame ile shule.

Samson alijikuta moyo wake ukilipuka kwa furaha, tayari furaha ikaanza kurudi alimuona Jose ni mtu mwenye hekima na busara za hali ya juu hata hivyo wajihi wake ulimtambulisha hivyo, kwani Jose alikuwa kijana msomi mwenye Elimu yake anayejihusisha na masuala ya sheria.

Furaha zikaongezeka nyumbani kwa mama Kulwa, huku wakipata Chakula Cha usiku kwa pamoja, wakati furaha zikiendelea mzee Mgaya aliingia huku wakikumbatiana na mwanaye Jose kwa furaha.

Lakini hali ya Mzee Mgaya ilibadilika baada ya kumuona Samson, na hata mama Kulwa na mwanaye Jose walishangaa why amtazame yule mtoto Samson kwa jicho baya.

Itaendelea........... . .........
 
Kiukweli kupitia hii stori imenikumbusha magumu niliyowahi kupitia maishani hasa kwa ndugu pale nilipokiishi majumbani kwao,hakika walininyanyasa sana ila nashukuru nilikomaa mpaka nikavuka salama ila leo nimekuwa juu kuliko wao na watoto wao,kuna muda huwa nakaa nasema hivi kweli nikifa hawa wanangu nani atawapenda na kuwajali ?
 
Kiukweli kupitia hii stori imenikumbusha magumu niliyowahi kupitia maishani hasa kwa ndugu pale nilipokiishi majumbani kwao,hakika walininyanyasa sana ila nashukuru nilikomaa mpaka nikavuka salama ila leo nimekuwa juu kuliko wao na watoto wao,kuna muda huwa nakaa nasema hivi kweli nikifa hawa wanangu nani atawapenda na kuwajali ?
Ni kweli kabisa kwenye kusaka mafanikio Kuna hitaji uvumilivu na Imani ya kiwango kikubwa
 
Kiukweli kupitia hii stori imenikumbusha magumu niliyowahi kupitia maishani hasa kwa ndugu pale nilipokiishi majumbani kwao,hakika walininyanyasa sana ila nashukuru nilikomaa mpaka nikavuka salama ila leo nimekuwa juu kuliko wao na watoto wao,kuna muda huwa nakaa nasema hivi kweli nikifa hawa wanangu nani atawapenda na kuwajali ?
Daaah mim kila nkiwaza mama wa kambo alichonfanyia nabaki kulia nawaza tu mlango wa mafanikio kwangu utafunguka lin kwani shule nmesoma ila bado sielewi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom