SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
Huyu vipi mbona hadi muda huu yupo yupo tu, haendi shule.
Eti vipi Kuna tatizo gani mwanangu,
aliuliza Mzee Mgaya akiwa hajasalimia mtu yeyote.
Samson akaeleza mwanzo mwisho yaliyompata hadi kufikia kuwepo pale huku akiwaonesha shati ambalo lilibakiwa na kifungo kimoja tu,.
Ujue mume wangu hao waliomvamia wanajulikana si kasema rafiki yake Dullah anaonekana anajuana nao ni vyema tukamtafuta Dullah ili atusaidie namna ya kuwapata Hawa mabaradhuli, na Tena Hilo ni kundi la Kassim yaani huyu amekuwa mwizi Temeke hii, tena yule anajihusisha na ule wizi wa kutumia silaha kabisa taarifa zake tunazo sana, mwenyewe ana jina lake maarufu anajiita Bad K, yaani anatishia usalama si kidogo.
alifafanua Tausi.
Kwahiyo hajachukuliwa hatua yeyote yaani ni anaogopwa ama tusemeje,
Maana kama mtu ni hatari kwenye jamii halafu aangaliwe tu ujue inaleta maswali mengi sana.
aliuliza Mzee Mgaya.
Kwani hakamatwi, anakamatwa vizuri tu ila huwa anamtoa mama yake maana ndiye mtu anayetegemewa na familia, ameweza kusimamisha kibanda na mama yake huko Ubungo pembeni ya mji, lakini pia ndiye anayemsomesha mdogo wake Abdallah huku kazi yake kubwa ikiwa uporaji na unyang'anyi.
alizidi kupigilia misumari Tausi
Sawa Sasa nimeelewa, isipokuwa hatuwezi kuwasaka watu kwaajili ya tukio lililompata Samson, Bali ni Samson ndiye anayepaswa kuwa makini, baba (huku akimgeukia Samson) najua ulikuwa hujakaribishwa mjini, Sasa nadhani utaelewa wapi ni wapi na wapi ni wapi. isipokuwa nimesikia kumbe huyo rafiki yako Abdallah sijui Dullah ndiye mwenye huyo kaka yake jambazi Sasa Mimi nikwambie tu kuwa naomba punguza mazoea ya kwenda kwa akina Dullah Wala na yeye asikanyage hapa, maana unaweza kuja kuhusishwa na mambo ambayo Wala huyajui ukajikuta lazima uisaidie polisi, usikute huyo Dullah naye ni mwizi tu hivyo naomba upunguze mazoea naye ikiwezekana mwambie hutaki ukaribu naye tena.
Kwa Leo andaa mazingira yako Mimi nitaenda shuleni kwako nitaongea na walimu najua kukosa kwenda siku moja si mbaya,
Halafu mke wangu naomba yale makaratasi ya usajili wa Karakana yangu maana Kuna mashine mpya nimezileta pale, hivyo ni lazima nipeleke hizi Documents zikaangaliwe upya,
aliweka kituo mzee Mgaya
Mmh kwani lazima uende huko Tena huoni kama utajiongezea gharama zaidi, alihoji Tausi.
Weeeee mke wangu usiseme hivyo, yaani serikali hii ya Mkapa, ipo makini kuliko awamu zilizopita hivi unatambua zimeanzishwa taasisi chungu mzima zote zikiwa na lengo la kuhakikisha makusanyo ya Kodi yanaingia serikali ipasavyo Sasa wewe jiroge anzisha biashara yako isiyokuwa kwenye ramani ya serikali utaishia kufilisiwa.
alifafanua mzee Mgaya.
Siyo vibaya mume wangu hata hivyo kulipa Kodi ni uzalendo tu, aliongea Tausi akiwa anamkabidhi mume wake makaratasi fulani.
Kisha Mzee Mgaya akaondoka.
Samson aliingia ndani kwake, akihisi baridi baada ya kusikia stori zinazohusu familia ya rafiki yake Dullah mtu anayeitwa Kassim alimjua lakini jina la Bad K, ndiyo alilijua siku hiyo, alijikuta anapata wakati mgumu kuachana na Dullah, yaani swahiba wako, rafiki yako mliyeshibana, Classmate wako, halafu unaambiwa uachane naye , lilikuwa jambo gumu hasa Kwa umri wake, hata hivyo kwaasilimia nyingi alijikuta, ni lazima awasikilize wazazi/walezi wake kwani ndiyo wanaoendesha mambo yake yote.
Huku akiapa kutokutembea kwa miguu au kupita njia asiyoijua.
Kaka Samson vipi umejifungia ndani umelala mchana wote huu ,amka bwana njoo tusaidiane kazi huku nje.
Samson aliitwa na Rahma.
Mama katoka kaelekea dukani kwake kasema tusaidiane kazi,Mimi nafua nguo wewe, osha vyombo.
Samson aliangalia vile vyombo akaona kweli kazi ipo hakuna unafuu wowote wote ndiyo wale wale akikumbuka maneno ya Mzee Mgaya kuwa asione kama Tausi anampenda sana ni hadi akae naye ndiyo atamjua
Bila kinyongo akaanza kazi huku akijipigisha mluzi .
Kila akimwangalia Rahma aliye pembeni yake aliona anamvutia ajabu na tamaa za ngono zilikuwa karibu sana ikabidi aanze uchokozi.
Hivi dada Rahma, huwa huoni joto Kila muda umejifunika mwili mzima kuanzia kichwani hadi miguuni?
Eeh hii ni sharia ya dini, tunaamrishwa kuvaa hivi, na hatupaswi kuonesha maungo yetu ovyo ovyo hadi pale ambapo tutaolewa na anayepaswa kuona ni mume pekee. alijibu Rahma kwa uelewa wake
Wewe mbona mamdogo, kichwa kipo wazi muda wote, Leo utamuona kasuka kawaida , kesho yupo hivi , Mara Rasta lakini wewe sijawahi kuona hata kichwa chako. alizidisha maswali Samson.
Unavyomuona mamdogo alikuwa anavaa kama Mimi hivi, Sasa sijui ilikuwaje akabadilika ila kwangu haitotokea kamwe nikaacha amri na maagizo ya mwenyezi MUNGU.
alijibu Kwa hisia kali Rahma.
Basi Mimi naomba nikuone tu kichwani vile ulivyo, kwanza wewe ni mkubwa kwangu, pili tupo wawili tu sidhani kama kuna shida yeyote,
aliongea Samson akiwa ana tabasamu pana kiasi cha Rahma naye kutabasamu baada ya macho yao kugongana.
Sema nini kichwa changu kinawasha kweli sijui ile sabuni hainipendi , sijui kwakuwa sijawahi kufumua na kusuka upya nywele zangu? alijiuliza maswali yale Rahma, huku akitoa Hijab yake na kuiweka pembeni, hatimaye samson akaona kichwa Cha Rahma kwa Mara ya kwanza,
Nywele nyeusi laini zilizochanguka changuka zikiwa zinafumuka zenyewe huku kichwa cheupe Cha Binti wa kimanga, kikiwa kinang'aa kutokana na kuwa huwa kinafunikwa muda wote, kilimsisimua sana Samson,akajikuta Samson mwenye jina lake anaamka kunako Usingizini, na kuwa standby kwa lolote.
Bastola ya Samson ambayo haijawahi kutumika popote ilikuwa tayari huku ikiwa na risasi tayari kwa matumizi.
Mwangalie kwanza kumbe kanionaaaaa, yaani wewe ni mkorofi sana wale vibaka waliokupiga Jana Bora wangekubonda wakukomeshe.
aliongea Rahma huku akifunika hijab yake haraka na kuendelea na habari za kufua.
Waliendelea kufanya kazi huku wakiangaliana kwa kuibiana na Kila walipokutanisha macho yao Kila mmoja alitabasamu,ile hali ilimuathiri Samson kwani joto la mapenzi lilioverspeed kwa kiwango kikubwa.
Mwanzo Rahma hakuwa akimpenda Samson, haikujulikana ni kwasababu gani , hata Samson alijijua kuwa hakuwa na chemistry nzuri Rahma, lakini kwa siku hiyo alishangaa Rahma kuwa mwepesi vile na mchangamfu.
Hivi Samson kwenu mmezaliwa wangapi ? aliuliza Rahma
Tumezaliwa wanne, dada zangu watatu, wakiume Mimi na nikiwa wa mwisho kuzaliwa. alijibu Kwa pupa Samson ili kujiweka karibu zaidi.
Haaaaah kwahiyo wewe ni wa mwisho siyo, vipi hujapakumbuka nyumbani? Rahma aliuliza.
Nakumbuka sana, tena sana tu, hata hivyo nakomaa na shule najua ipo siku nitakutana na ndugu zangu pamoja na wazazi wangu. aliongea kwa hisia Samson.
Inshallah mwaya , omba uzima tu, Kila kitu kitakuwa sawa, kwani Samson una umri gani?
Samson {akitaja miaka yake Kwa pupa}huku akimwangalia Rahma kuona atasemaje,
Kumbe wewe ni mdogo wangu sana tu, nimekupita miaka nane ujue. inatakiwa Kila siku uwe unaniamkia, maana Mimi ni dada yako sawa, aliongea akitania Rahma.
Sawa, nitafanya hivyo, ila na wewe naomba ninapokuamkia uwe unatoa hiyo nguo kichwani Kisha nakuwekea mkono , naona itapendeza sana. alijibu Samson na kumfanya Rahma acheke kiasi Cha kuonesha meno yake mazuri na meupe na kuzidi kumchanganya Samson wa watu.
Haya bwana kama ni hivyo na usiniamkie tena maana naona una lako jambo, aliinuka Rahma akiwa anatandaza nguo kwenye kamba, huku Samson akigundua kabisa kuwa anategwa maana juba lilikunjwa kiasi Cha kuonesha miguu mizuri minene yenye vinyweleo vyeusi, hakika Rahma alimvutia Samson.
**************************************
Siku ya pili Samson alikuwa darasani huku akipewa lawama fulani na Dullah kwamba kwanini yupo mbali naye na Kila anachouliza anamjibu Kwa mikato, kwani Kuna ugomvi gani? aliuliza Dullah
Nishakwambia humu darasani, hapafai kujadili hayo, nitakwambia tukiwa nje ya darasa, mbona unakuwa si mwelewa? Hata mwalimu akitukuta tunajadili mambo yasiyohusiana na masomo, huoni itaeleweka vibaya mwanangu.
alilaumu Samson.
Ikabidi Dullah akubali shingo upande akiona Kuna kitu hakipo sawa kwa Samson.
Muda fulani Samson, alikuwa anamuwaza sana Rahma, na baadhi ya mambo aliyofundisha mwalimu wake wa physics yalimpita, maana tayari Pepo la mapenzi lilikuwa ndani yake, Kila akijitahidi kumsahau Rahma sura ilimjia tu, miguu mizuri, sura nzuri, nywele zake Sasa, Samson alijikuta hajiwezi, hali hiyo mwalimu aliijua akawa na mashaka na Samson kama kweli anamwelewa , ikabidi amsogelee,
Enhee, Samson umeelewa kilichofundishwa hapa?
Samson akaitikia kwa kichwa kwamba kaelewa.
Naomba definition ya nilichofundisha saizi yaani
Work, Energy and Power.
Samson, alijibu huku akichanganya zile maana kiasi cha wanafunzi wenzake kumcheka.
Mnaona, Samson si mtu wa kushindwa hizi definitions fupi niligundua tangu mwanzo kuwa huyu hanisikilizi , haya nifuate ofisini nataka ukaniekeze unasumbuliwa na nini, Samson akaongozana na mwl hadi ofisini.
Lakini kwakuwa ni muongo mzuri alijitetea huku akijifanya anaumwa akikazia zaidi kwamba hata Jana hakuja kwakuwa hakuwa sawa.
Walimu wakamdmshauri kuwa ni vyema akaweka wazi kuliko kujificha maana mwalimu mwingine anaweza kukuchapa akihisi unamdharau.
Wakati wakitoka pale assemble kwaajili ya kurudi nyumbani alijikuta anamtoroka Dullah, huyoo nyumbani kwake huku akiona gari linachelewa ili akamuwahi Rahma.
Samson anachanganya mapenzi na masomo tena akiwa na umri mdogo na yupo kidato cha kwanza bado,na hata Rahma kama anavutiwa hivi na Samson kwa kiasi fulani, itakuwaje tukutane sehemu inayofuata.
Itaendelea...........................