muyakb24
JF-Expert Member
- Jul 31, 2018
- 412
- 296
SEHEMU YA 07:
“Eti?”
“Anambemenda na mwisho wake atamuua.”
“Mmh! Una maana gani?”
“Mkeo si muaminifu, watu wote mtaani wanajua, ukitoka na yeye nyuma anatoka, anarudi jioni wakati wewe umekaribia kurudi.”
“Sasa mama kutoka kwa mke wangu kunaingiliana vipi na mwanangu kuchelewa kutembea?”
“Baba jasho la janaba ni baya kwa mtoto hasa ikiwa mliokutana si wazazi wa mtoto, mmoja wenu akikosa uaminifu na akamshika na uchafu wake lazima mtoto atadhurika.”
“Sasa mama mke wangu mbona ni muaminifu?” kauli ile ilinishtua.
“Baba acha kusema hivyo, sisi ndiyo tunaojua, isingekuwa huyu mtoto wala nisingenyanyua mdomo wangu, ningekuacha ili siku moja ujionee mwenyewe uchafu wa mkeo.”
“Kwa hiyo chanzo cha matatizo ya mtoto ni mke wangu?” nilijikuta nikikosa amani moyoni.
“Baba usiandikie mate, kwa vile mkeo hata aibu hana, siku moja rudi nyumbani mchana utajionea mwenyewe. Kabla ya kufanya lolote fanyia kazi haya niliyokueleza. Ukipata majibu ndiyo utajua mkeo ni muaminifu au siyo muaminifu na kupata kiini cha matatizo ya mkeo. “Ila nakuomba kabla ya yote mtoto wako mpeleke kwa bibi yake kisha fanya uchunguzi wako.”
“Asante mama kwa maelezo yako.”
“Ila nakuomba ukienda kwako usioneshe mabadiliko yoyote, kuanzia Jumatatu siku yoyote rudi nyumbani ghafla mchana utaniambia niliyokueleza ni kweli na maendeleo ya mwanao utayaona kwa muda mfupi akiwa mbali na mama yake.”
“Asante mama.”
Niliagana na yule mama ambaye alikuwa mtu wa heshima na nilimheshimu sana pale mtaani. Nikiwa narudi nyumbani, njia nzima nilikuwa na mawazo mazito juu ya maneno niliyoelezwa na sababu ya matatizo yanayomfanya mwanangu ashindwe kutembea.
Kingine ambacho sikutaka kukikubali mara moja ni kuhusu kutoka kwa mke wangu nje ya ndoa. Kwa kweli sikuamini mke wangu kama angeweza kutoka nje ya ndoa hasa kutokana na ukimya pia kuonesha mapenzi mazito kwangu.
SEHEMU YA 18
Baada ya kutafakari niligundua lile gari ndilo lililomshusha mke wangu siku niliporudi nyumbani ghafla, nilishtuka kulikuta nyumbani na kujiuliza limefuata nini pale. Niliingia ndani na kukuta sebuleni kuna pombe kali juu ya meza na glasi mbili.
Sikujishughulisha navyo nilielekea chumbani, nilipofika kwenye mlango wa chumbani nilikuta umefungwa na ndani nilisikia sauti mbili, ya mwanamke na mwanaume. Sauti ya mwanamke ilikuwa ya mke wangu na ya kiume sikujua ni ya nani. Kwa haraka nilitoka mpaka nje na kuzunguka dirishani na kuchungulia ndani.
Niliyoyaona ndani nusura mapigo ya moyo wangu yasimame ghafla. Kitandani kwangu alikuwepo mke wangu na mwanaume mmoja ambaye hakuwa mgeni sana machoni mwangu japo sikukumbuka niliwahi kumuona wapi, wote wakiwa kama walivyozaliwa.
Ilionesha walikuwa wamemaliza kufanya uchafu wao muda si mrefu kwa jinsi walivyokuwa wamejilaza. Nilihisi miguu haina nguvu na kurudi chini bila kujieleza na kukaa kama mzigo. Nikiwa nimekaa chini huku nimeegemea ukutani nilisikia homa ikipanda mara mbili na jasho likinitoka kama maji, nikajiona kama nakufa muda si mrefu.
Nikiwa nimekaa chini niliyasikia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ndani.
“Sasa kwa nini uliitoa ile mimba, si uliniahidi utanizalia mtoto,” sauti ya kiume ilisema.
“Ni kweli, lakini damu yako ni kali sana ningeiacha ingeniletea matatizo katika ndoa yangu.”
“Matatizo gani?”
“Nilikuwa na wazo hilo, lakini siku niliyowaona watoto wako wanafanana kama mayai niliogopa. Nilikueleza niwe mke wako wa pili hutaki, ningejifungua humu ndani japo mume wangu asingejua kitu lakini walimwengu wangemweleza. Hata kutoka kwangu kuna watu wenye roho mbaya walimueleza.
“Bila kuhama kule mambo bado yangekuwa mabaya, japo inabidi kutokana na kukupenda lakini wakati mwingine namuonea huruma mume wangu. Toka tuhamie huku pamekuwa kama kwako, unakuja muda wowote unakula na kuvaa tofauti na kwako.
“Ukitaka nikuzalie mtoto nitoe kwa bwana huyu haichukui hata mwezi nitakubebea mimba.”
“Nimekuelewa mpenzi wangu, lakini japo tunamfanya yule jamaa fala huwa sijiamini sana kuja hapa, unafikiri akitufumania tutafanyaje?”
“Hawezi kutufumania.”
SEHEMU YA 25
ILIPOISHIA
“Mbona siri ipo wazi, taarifa hizi zilinifikia muda mrefu tangu matatizo ya mwanao kuchelewa kutembea. Pale mtaani kwenu kila nilipokuja kukutembelea nilielezwa tabia chafu za mkeo lakini nilishindwa nianzie wapi kukueleza kutokana na wewe jinsi unavyompenda mkeo.
“Kwa kweli nilihofia kuitenganisha nyumba yako kutokana na wewe kumuamini sana mkeo. Huwezi kuamini kuna mtu mmoja wa nyumba mliyokuwa mnakaa zamani, kila nilipokuja na kuondoka alinifuata njiani na kunieleza unavyopelekwa na mkeo kwa tabia zake chafu na kuniomba nikueleze ili uweze kumdhibiti mkeo.
SASA ENDELEA...
“Lakini bado ningeanzia wapi kukueleza unielewe? Bado kwangu ulikuwa mtihani mkubwa. Baada ya ninyi kuhama nilikutana naye tena yule aliyekuwa akinipa taarifa za mkeo, akaniambia kuwa nyumba uliyohamia umepangiwa na mwanaume mwenzio, bwana wa mkeo.
“Kwa kweli habari zile ziliniumiza sana lakini vilevile sikuweza kukueleza chochote baada ya mkeo kukukataza usitembelewe na rafiki zako nikiwemo mimi mtu wako wa karibu. La kunikataza nisije kwako halikuniumiza kwa vile hata nilipoacha kuja kwako hakuna kilichopungua kwangu.
“Hali yako ya sasa iliwachanganya sana watu wengi, najua uliulizwa na kila mtu akiwemo bosi, hakuna hata mmoja uliyemueleza tatizo lako. Juzi kuna kitu nilisikia sijui mkeo katoa mimba ya mwanaume wa nje na watu kusema huenda imekuchanganya sana.
“Japokuwa nilikuwa najua kila kitu lakini nilitaka kauli toka kwako kwa kujitahidi kukubembeleza lakini umekuwa ukificha ukweli wakati unazidi kuteketea.
“Lakini hali yako kila kukicha imekuwa ikizorota huku ukiwa mtu wa kuhama kimawazo kila dakika, unajisahau kama upo kazini. “Wengi wanakuonea huruma japokuwa matatizo yako wewe unajua ni siri yako, kutokana na kufanya siri wenzako waliamua kukuacha waone mwisho wako, wengi wanakuona mjinga kuendeshwa na mwanamke.
“Hebu naomba unieleze kila kitu usinifiche mimi rafiki yako. Kwa nini umefikia hatua hii ikiwa kila kitu cha mke wako unakijua?” alisema Simon kwa uchungu.
Samahani dada shunie baada ya muda gani story itaendepea...?Siwezii naendana na mwandishi anavyopost
SEHEMU YA 31
“Mume wangu mwenyewe nani, mwenyewe si sisi?”
“Mke wangu, hebu nyanyuka tuondoke.”
“Mume wangu mbona toka jana sikuelewi kuna nini?”
“Hebu kwanza tuhame kwanza muda si mrefu utanielewa.”
Tulikubaliana kuhama japo kwa shingo upande, tulipakia mizigo nikisaidiana na Simon, baada ya kupakia tuliondoka na kuhamia sehemu nyingine kwenye nyumba yenye wapangaji watatu na sisi kuwa wa nne. Baada ya kupanga vitu huku mke wangu akionekana kulazimishwa sikuiangalia ile hali.
Kwa vile siku ile nilikuwa na ruhusa, nilipumzika na Simon aliondoka kwenda kwake. Tukiwa tumebaki wawili mke wangu aliniuliza:
“Sasa ndiyo unafanya nini? Tumetoka kwenye nyumba kubwa tunakuja kwenye vyumba viwili?”
“Ndiyo uwezo wetu.”
“Sasa kwa nini tumehama kule?”
“Ile siyo nyumba yetu.”
“Si tulikuwa tumepanga?”
“Na hapa tumepanga.”
“Kama tumepanga huoni tunapoteza fedha bure, si heri tungerudi kwenye nyumba yetu kuliko kuja huku?”
“Hatujapoteza ila yeye ndiye kapoteza.”
“Mume wangu mbona sikuelewi nani kapoteza?”
“Mke wangu, we mkubwa si kila kitu nizungumze unatakiwa kutumia akili.”
“Una maana ile nyumba nilipangiwa na mwanaume?” mke wangu aliuliza macho yamemtoka pima.
“Wewe ndiyo unasema,” nilijifanya sijui kitu. “Lakini mume wangu kwa nini unapenda kusikiliza maneno ya watu?”
“Mke wangu tumia akili, utajua sababu gani imetufanya tuhame kule na tusirudi kwenye nyumba yako.”
“Najua tu watu wameshaanza kupenyeza umbea, nina imani nyumba hii muda si mrefu itanishinda.”
“Haiwezi kukushinda kama utanisikiliza.”
“Nikusikilize nini, kila siku unasikiliza maneno ya nje.”
“Kwani uongo?”
“Uongo nini?” mke wangu alishtuka.
“Yote yaliyotokea siku za nyuma?” nilimueleza ya nyuma sikutaka kumueleza niliyoyashuhudia mwenyewe yaliyosababisha nitake kutoka roho.
“Basi mume wangu, lakini kumbuka kusikiliza maneno ya watu tutaachana tunapendana.”
“Unanipenda?” nilimuuliza swali ambalo naamini hata wewe utaona la kijinga. Nilimuuliza kwa makusudi pamoja na kunifanyia yote bado mke wangu niliamini bado ananipenda, nilikuwa nina imani hata yeye ananipenda.
“Nakupenda sana mume wangu.”
“Kweli?”
“Tena sana, hebu nieleze toka tuhame Uswahilini nimekukosea kitu gani kibaya.”
Ukweli huu mchungu sana bora umeandika weye bibie ila ndio ukweli huo mnajijua wenyeweHahaha wanawake sisi ni kama embe ukisubiri liive wenzio wanalila na masala