Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,971
Mtunzi: Ally Katalambula
SEHEMU YA 01
Awali ya yote, namshukuru mwandishi wa mkasa huu, kaka Ally Katalambula, pamoja na mhariri wa gazeti la Champion ndugu John Joseph ambaye ameipa nafasi simulizi yangu hii ya kweli. Kusikilizwa, kuandikwa, na kisha kuichapwa kwenye gazeti la Champion toleo la kila ijumaa.
Katika maisha yangu, sikuwahi kuwaza kuua hata nzi. kutokana na huruma niliyokuwa nayo. Watu wengi walipenda kuniita mlokole japo historia yangu yote niliishi maisha ya kutokuwa na dini nikiamini Mungu wa Wakristo ndiye Mungu wa Waislamu kutokana na mafundisho ya dini zote niliyoyafuatilia.
Utashangaa kwa nini niliishi bila kuwa na dini ikiwa wazazi wangu wana dini, tena dini tofauti, baba Muislam na mama Mkristo. Katika maisha yao hakuna aliyekubali kumfuata mwenzake na kukubaliana kila mmoja aishi katika imani yake. Hivyo nikawa mtoto wa wazazi wa dini mbili. Pamoja na wazazi wangu kuishi kila mmoja na dini yake, waliishi katika upendo wa hali ya juu kwa kila mmoja kuheshimu imani ya mwenzake.
Nilipopata ufahamu nilijikuta nipo njia panda kwa vile sikutaka kumuudhi mmoja wa wazazi wangu kwa kumpendelea mmoja. Halafu kitu cha ajabu nilikuwa mtoto mmoja kama roho, hivyo niliamua kusimama katikati ya wazazi wangu kwa kutochagua dini yoyote. Lakini nilikuwa nafahamu kipi mwanadamu anatakiwa kukifanya ili asimuudhi Mungu.
Katika maisha yangu yote niliamini tofauti ya dini mbili ni ndogo sana lakini anayetakiwa kuabudiwa ni Mungu mmoja. Tangu hapo niliishi nikiwa sina dini na kuishi kama mpagani, tofauti yangu nilikuwa najua Mungu ni mmoja na ndiye anayetakiwa kuabudiwa, lakini sikwenda msikitini wala kanisani na malumbano ya dini hizi mbili mimi yalikuwa hayanihusu.
Wazazi wangu nao walikubaliana na mimi baada ya ushawishi wa kila mmoja kugonga mwamba. Huu ulikuwa muhtasali wa maisha yangu ya awali ya kunifanya nisiwe na dini kwa ajili ya mapenzi ya wazazi wangu. Kutokana na malezi mazuri ya wazazi wangu niliweza kuishi sehemu yoyote na mtu wa aina yeyote, siku zote heshima na ucheshi ndivyo vilifanya watu wanipende.