Simu ya Hawa Ghasia yatumia Sh. 25 milioni

Simu ya Hawa Ghasia yatumia Sh. 25 milioni

Kuna gharama za data roaming watu wengi wanazipuuzia na ndizo aghali zaidi kuliko voice roaming
sasa hawa wakubwa wana postpaid roaming contracts kwenye simu zao na akienda nchi anajiachia mahuduma yote huku simu inajiupdate aaplication nk akirudi home anakuta bill ndeeefu na kwa kuwa halipi yeye basi tabu tupu
Roaming bora iwe voice tu mambo mengine anunue local line ya huko aliko inapunguza gharama
 
Mimi pia nilifikira hivyo ikabidi nicheki gharama za kupiga simu nje ya nchi kwenye tovuti ya airtel. Nimekuta kuna nchi kupiga simu ni zaidi ya sh 12000 kwa dakika. Kwa nchi kama hizo ukiwa na kidumu huko ukapiga simu kwa masaa 2 kwa siku kwa siku 50 hesabu ya jumla ni 12000 x 60 x 2 x 50 = 72,000,000/-. Kwahiyo hiyo 25+ Milioni isikutishe inawezekana kabisa.[/

Issue iko Kwenye mobile data ikiwa on maana 1 Meg ni 12$ , ukikaa week tu Kila Kitu on Unatumia data kama Uko Tz 20 mil inafika Ndani Ya siku 5 tu!!
Sasa hapo ongezea na call time. Pointi ni kwamba hiyo inawezekana kabisa japokuwa inaonekana kama ni hela nyingi sana kwa kuwa wengi wetu hatuwezi hata kufikiria kutumia hela kama hiyo kwenye matumizi kama hayo.
 
Kumbe inawezekana kulipa wafanyakazi wa nchi hii kima cha chini milion moja tsh kwamwezi! pesa ipo...wanaitumia mafisadi wachache!
 
Jee, zimelipwa au ni Invoice iliyoletwa kimakosa? maana haiingii akilini.

Sitoshutumu mpaka nisikie 2nd and 3rd party (Airtel na Hawa Ghasia) wakitoa ufafanuzi.

Nilitegemea hilo jibu kwa nyie viruses wa lumumba!!
 
Fedha hizo ni zaidi ya mshahara waje kwa mwezi,huo ni ufujaji usioweza kufumbiwa macho
 
Ikiwa mwizi atamuona polisi na huyo mwizi hawi terrorized basi huyo polisi atakuwa na walakin.

Unaonesha hata maana ya terror huijui. Hujui nini kuwa terrified? Pole sana.

Hivi shule mlienda kusomea ujinga?

Huyo ni yule polisi wa Pinda. Piga tuuuu!!
 
We ni kawaida yako kubishana

Mkuu wala hajakosea, mara ngapi kampuni hizi za simu uwabambikia wateja bill ambazo niza kubuni tu - we mtu/Waziri anawezaje kutumia kiasi hicho ndani ya muda tajwa, au tuseme alikuwa ana-download 3D movies kutoka Hollywood!!
 
Kama ni kweli huyu atakuwa analipa pesa hiyo ya serikali Airtel halafu wanamrudishia kwa mlango mwingine
 
"kama ilivyo vigumu kuku kupona nyakati za sikukuu, ndivyo itavyokuwa kwa wadhulumaji kuiona kesho" kuenea kwa taarifa kwa kasi mithili ya upepo kutokana na maendeleo ya mawasiliano ni dhairi siri za wadhulumaji hazipo tena salama.

ikiwa waziri wa tamisemi anatumia milioni 25 katika kipindi cha miezi miwili kwa ajili ya mawasiliano sitaki kujua Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe atatumia milioni ngapi katika kipindi kama hicho?

wajinga ndio waliwao, na faida ya mjinga ni kuumia. migomo, mashinikizo, maandamano, ni ishara waongozi wamezidisha ubadhirifu na kutojali wananchi au taarifa ya madudu yao zinavuja kwa kasi kutokana na mapinduzi ya mawasiliano.
 
Huyu mama inaelekea hajui kujiunga kifurushi chochote. Ana surf freely bila kujali, sms kama kawaida anaongea masaa kwa masaa
 
Unajuwa Kiingereza gaidi ni terrorist, sasa kama kuna polisi halafu awe hawezi kum terrorize mwizi huyo atakuwa si Polisi.

Waislam ni makhalifa hapa duniani, mkituona mnatuogopa "we terrorize you", hivyo ndivyo anatakiwa khalifa awe. Lazima umuogope.

Khalifa wa nani? Mohd? Al lah? Hatuogopi mtu auaye mwili kisha hawezi kufanya zaidi. Yesu Yuu Hai hata uislam unajua Yesu yu hai.
 
Ndo maana yule mama Tibaijuka alisema milion 10 ni pesa ya mboga kumbe ukishakuwa waziri pesa zipo nje nje kabisa huu ndo mwaka wa mwisho kwa utawala wa ccm
 
Dah kama taarifa hii ni ya kweli basi viongozi wetu wana dhambi kubwa mno! hv unajua huku barabarani kuna kina mama wanafiwa na watoto zao kwa kutokumudu gharama za matibabu! kwa magonjwa ya kawaida kabisa ikiwemo malaria. Ila najua kuna siku ya mabadiriko makubwa sana inakuja.

Hakika neno zuli la KIIMANI KUNA baadhi ya viongozi wetu wana dhambi SANA yani MPAKA MUNGU APENDEZWI na matendo yao ila kwa sababu ni waja wake uwastahi na kuwapa muda watubu....wakichelewe kufanya hivyo kwa wakati sahihi ushusha aibu kwao binafsi na aibu hiyo uishi nao mpaka vizazi na vizazi.

Hebu fikiria milioni 25 zingefanya mangapi kwa vijiji kadha wa kadha kuwasaidia wakina mama vifaa vya kujifungulia uzazi salama.

Siwezi amini waziri anashinda JAMII FORUM, kutoa matusi, kutetea hoja dhaifu, kutoa kashifa dhidi ya watu wengine, kumbe inawezekana ni kwa PESA yetu wenyewe Watanzania ambayo ilipaswa ifanye kazi ya maendeleo ya Taifa zima kupitia wizara anayo iongoza yeye.

Kwa kuwa hatuna wa kumuumbua kwa sasa, lakini MUNGU kwa matendo yake UTENDA KWA NAMNA YA KUSHANGAZA [MYSTERIOUS WAY]. Bila kutegemea mzaa mzaa kwa kuwa wanamkasilisha MUNGU wasivyojitambua anaweka upofu, matokeo yake kwa kuwa MATUMIZI ya mtandao huo si HAKI kwa Watanzania watu wanajikuta bill maradufu pasipo kutarajia.Japo kwa kuanzia aina hizi kama ni kweli basi MUNGU NI MUNGU na ATABAKI KUWA MUNGU, inachukua muda lakini inajibu.

Tunao humu na wanachangia thread kama hii, na uwezi kuwadhania kabisa...
 
Jee, zimelipwa au ni Invoice iliyoletwa kimakosa? maana haiingii akilini.

Sitoshutumu mpaka nisikie 2nd and 3rd party (Airtel na Hawa Ghasia) wakitoa ufafanuzi.

Wezi tangu lini wakakubali kuwa wao ni wezi?
 
Back
Top Bottom