Simu ya Hawa Ghasia yatumia Sh. 25 milioni

Simu ya Hawa Ghasia yatumia Sh. 25 milioni

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
KUNA mchwa ndani ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Abdulrahman Ghasia (49), ni miongoni mwa wanaotafuna fedha za umma serikalini, mithili ya mchwa.

Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).
Katika kipindi kisichozidi siku 52, Ghasia ametumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi yake ya simu ya mkononi, tena kupitia kampuni moja ya Airtel.
​

Taarifa hizi za waziri kutumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi ya simu moja ya mkononi, ndani ya muda usiofikia miezi miwili, zinafichuka katika kipindi ambacho serikali imekuwa ikitumia nguvu kukusanya michango kutoka kwa wananchi.

Michango mingi ambayo serikali imekuwa ikikusanya, ni ile ya maabara kwenye shule za kata, madawati, ununuzi wa vitabu, madaftari na ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa.

Taarifa zinasema, katika maeneo mengi, maagizo ya serikali, yaliambatana na vitisho, huku baadhi ya walioshindwa kutoa michango hiyo wakifikishwa mahakamani na kufungwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya serikali na kampuni ya Aitel Tanzania Limited, waziri Ghasia ametumia mamilioni hayo ya shilingi kwa mawasiliano kati ya tarehe 1 Februari na 21 Machi mwaka huu.

"Kuna mambo ya ajabu sana ndani ya serikali hii. Taifa masikini kama hili, kuna viongozi wanaotumia kiasi cha Sh. 25 milioni kwa simu. Kwa kweli, umasikini tulionao ni wa kujitakia," ameeleza Juma Said, mkaazi wa Kinondoni na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii.

Nyaraka (Invoice) kutoka Aitel inamuonyesha Ghasia alipewa ankara ya malipo ya tarehe 1 Februri 2015, yenye Na. 29906000001374, ikielekeza serikali – Tamisemi – kulipa kwa kampuni hiyo, jumla ya Sh. 25,878,335.86.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, Ghasia amejitambulisha kuwa ni waziri wa Tamisemi. Anatumia anuani ya S.L.P 23, jijini Dar es Salaam; huku namba ya mteja – Customer Id – ikitajwa kuwa 1219937034.

Ghasia anatumia namba ya mlipa kodi (TIN) TIN: 100-961.520.

-----------Online linaweza kuripoti kuwa kila mwaka serikali inatumia mabilioni ya shilingi kwa njia za anasa, ikiwamo malipo ya simu, usafiri, nguo na fenicha za ndani, badala ya fedha hizo kuwekezwa kwenye maendeleo.
 
Yule mama bana,,alitetea kinoma wezi wa escrow.

Ccm katika Ubora wake waufisadi

Hivi hana undugu na mather house mbona wamefanana na wametoka kijiji kimoja na yule ccm bana pale juu kuna mzunguko wa ndugu balaa wengine wakwe, wajomba, binamu, mme mwenza , shemeji ndio maana mambo vululuvululu.
 
Shemeji wa profesa wa kilimo
 
Jee, zimelipwa au ni Invoice iliyoletwa kimakosa? maana haiingii akilini.

Sitoshutumu mpaka nisikie 2nd and 3rd party (Airtel na Hawa Ghasia) wakitoa ufafanuzi.

Kweli Dada yangu hata Mimi ilishakujaga report kuwa nimetumia simu ya ofisi makadirio yake yalikuwa zaidi malaki sikumbuki na wakat sikuwah piga hats senti makosa huwa yapo
 
Hivi hana undugu na mather house mbona wamefanana na wametoka kijiji kimoja na yule ccm bana pale juu kuna mzunguko wa ndugu balaa wengine wakwe, wajomba, binamu, mme mwenza , shemeji ndio maana mambo vululuvululu.

Katika utawala wa Mkapa, mwinyi sikuwahigi kusikia ushikaji wa kupeana nyadhifa kiasi hiki,
hata watoto wao hawakuwahi kujulikana tena kwa mabaya kama hawa wa sasa!
 
huyu mama si ndiyo wizara yake inahusika na Ajira za walimu huuyu? Hiyo pesa kama ni kweli si ingekua posho ya walimu wapya hata 20 hapo? Ndio maana ajira hakuna kama mawaziri wa wizara tu wana matumizi mabaya hivooo.
 
Anakusanya pesa akapambane na wababe wake kule Mtwara akina Murji na Kweka... Huyo Kweka wa Mtwara ndo kiboko ya huyu mama maana kanunua karibia mashamba yote ya ukoo wa Ghasia wamebakia na viplot plot vya kuunga tu. Zikusanye mama maana nasikia mission yako ni kukimbilia Ubunge Mtwara Mjini kule vijijini hawakutaki tena
 
Jee, zimelipwa au ni Invoice iliyoletwa kimakosa? maana haiingii akilini.

Sitoshutumu mpaka nisikie 2nd and 3rd party (Airtel na Hawa Ghasia) wakitoa ufafanuzi.
Muislamu mwenzio au sio? Napenda double standards zako. Vipi Mohammed Said leo ana historia gani za wazee wa kariakoo walioleta uhuru?
 
Muislamu mwenzio au sio? Napenda double standards zako. Vipi Mohammed Said leo ana historia gani za wazee wa kariakoo walioleta uhuru?

Ohhhoooo, hapo nimekupa usomi. Haiingii akilini 25m kwa mwezi mmoja kwa line moja, hata awe si Muislam, bado sitoshutumu wala kuhukumu mpaka nisikie upande wa pili na wa tatu.
 
Back
Top Bottom