Simu Janja (Smartphone) 19 bora zinazokaa na chaji muda mrefu

Simu Janja (Smartphone) 19 bora zinazokaa na chaji muda mrefu

Sio soko la magharibi soko la kimataifa,HUAWEI na Xiaomi washaingia labda kwa Infinix ndo sina hakika mana ni project ya Android kwa watu wa chini kumiliki simu janja
kwani Tecno haipo soko la kimataifa? ikiuzwa Tanzania na kenya tayari ni soko la kimataifa.
 
jinsi battery linavyokuwa kubwa ndio linavyochukua nafasi kubwa na kuzalisha joto jingi.

hivyo unapolibananisha battery na vifaa vyengine bila kuacha nafasi ya kutosha unahatarisha simu hata kulipuka. ie note 7.

Asante sana kwa maelezo murua ndugu.......

Je kipi kinachofanya simu kama iPhone chaji iishe haraka....!!?

Je kuna setting yoyote ninayoweza kuifanya kupunguza tatizo hilo.....!!!??
 
Hhahaha nenda kafanye utafiti tatizo mmejaza akilini mwenu neno "tecno"
Mh nilichukia kampuni ya Samsung kwa ajili ya Galaxy S III... nikasema jina linaitwa Samsung.. Marufuku..

Nikataka kwenda Huwaei.. Budget ikabana.. Niliitaka kama ya Messi hiyo Mate 8..
Niko zangu Tecno, japo siifagilii brand, lakini nafanyia shughuli zangu fresh tu..
 
Tecno ndio mbabe wa Betri kwa smartphone nilishasahau habari ya kubeba power bank
Huo ni utafiti wa kimataifa ndugu.. Siyo wa kwetu huku huu wa Twaweza.. Hapana..

Umeona S 8 hapo..simu inayotangazwa kwa sasa au Mate 10.. Lionel anatumia brand hiyo..

So usibishe sana.. Mi mwenyewe natumia Tecno K 9 plus.. Lakini nasubiri Twaweza wakifanya utafiti wao, wasipoiweka Tecno, niandamane!
 
Hizi habari naonaga kama ni fictions tuu, nimemiliki simu kadhaa sijawahi fanikiwa kuhusu ishu ya chaji hata wanazotumia wadau hazikai na chai.

Labda tecno p3 enzi hizo kuna mdau nilikua naona anakesha nayo mda sana akicheza game.
 
Kuna uwezekano tecno inakaa na chaji ila kumiliki simu zenyewe mmmmh ni ngumu sana bora ni baki na nokia tochi.
Tecno sio simu nazidharau mno sitakua comfortable kwa kweli kubeba hiyo michina.
 
Ka
Asante sana kwa maelezo murua ndugu.......

Je kipi kinachofanya simu kama iPhone chaji iishe haraka....!!?

Je kuna setting yoyote ninayoweza kuifanya kupunguza tatizo hilo.....!!!??
kinachofanya simu ile chaji haraka ni optimisation ya OS husika. Kama simu haijawa optimized ili iwe inasave battery kwa kufungia unneccessary programs ama hardware ambazo hutumii kwa wakati huo basi itazingua sana kwa kuisha charge mapema.
 
Wewe huo utafiti wako umeufanyia mtandaoni ila haujakaa na kutafiti sim zenyewe kabisa.

Umeshawahi kutumia Infinix?! Me nilishawahi kutumia infinix hot 4, hii sim huwa inakaa na chaji na alarm ya low battery inapiga baada ya masaa 48 kwa maana ya siku mbili kama ukiwa unawasha dadta kusoma text tu za whatsapp kisha unazima.

Ukipiga sim kuongea mfululizo mimi huwa naongea sim muda mwingine hata masaa manne mfululizo, ila ukija kutazama asilimia zimeganda pale pale.

Sitaki kusifia sana. Hii ni miongoni mwa sim smartphone nafuu sana ila kiukweli inaridhisha na kurejesha thamani ya pesa uliyotumia kuinunulia.

Kama unahisi ni porojo nakuruhusu agizia sim yako ya infinix now halafu uje kutoa ushuhuda. Hizo umetaja hapo nyingi hazina uwezo wa kukaa na battery muda mrefu sababu vitendea kazi vyake vina consume umeme mwingi sana wakati inatumika.
 
Back
Top Bottom